content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Meneja huyo alitoa kauli hiyo Dar es Salaam akizungumzia matokeo hayo ya Stars na Super Eagles ya sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.“Binafsi nimefurahishwa mno na kiwango kilichooneshwa na Taifa Stars kwani timu imeonesha mabadiliko makubwa mno ukilinganisha na siku za nyuma ambapo wengi wangetegemea kuwa tutafungwa tu kirahisi,” alisema Kikuli.Alisema wachezaji wote walionesha moyo wa kujituma na wa kizalendo na ndivyo inavyotakiwa katika kila mechi.“Lazima kuwepo na ule moyo wa kujituma na kujitoa kwa aliji ya nchi yako na hicho kilionekana wazi siku ya Jumamosi na mwisho wake wa Nigeria wakashindwa kutufunga. “Kocha amefanya kazi kubwa sana hasa ukizingatia bado ni kipindi cha mpito kwake ila dalili ni nzuri na akipewa muda zaidi na wachezaji hawa, ana uwezo wa kuleta matokeo mazuri ambayo sisi kama wadhamini tunayahitaji ili tuwe na kitu cha kujivunia katika udhamini wetu,” alisema.Meneja huyo aliyehudhuria mechi hiyo, aliwashukuru Watanzania waliokuwepo uwanjani kwa kuonesha uzalendo wa hali ya juu na kuwataka waiunge mkono timu yao kwa mechi zijazo ili wachezaji wapate morali ya kufanya vizuri zaidi.Aliwataka wachezaji wasibweteke na matokeo haya kwani bado kuna kazi kubwa ya kufanya na sio kazi ya kocha tu, bali wachezaji pia na mashabiki wana nafasi yao katika kusababisha matokeo mazuri.“Sisi kama wadhamini tunaahidi kuendelea kuwa karibu na timu ya Taifa na kwa kushirikiana na TFF kuhakikisha timu inawekewa mazingira ya kufanya vizuri kama ilivyofanyika kabla ya mechi hii dhidi ya Nigeria,” alisema.Stars inakabiliwa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malawi itakayochezwa Oktoba 7 Dar es Salaam.
michezo
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma ilipokea Sh milioni 68.5 kutoka Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Dodoma Mjini kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali jimboni humo.Akitoa taarifa hiyo mbele ya wabunge kutoka Kenya waliofika kujifunza kuhusu Uendeshaji wa Mfuko huo, Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini, Shaban Juma alisema fedha hizo ni za mwaka wa fedha 2018/19.Juma ambaye ni mchumi wa jiji alisema, fedha za mfuko huo unaoongozwa na Mwenyekiti wake, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde zilitolewa kwa vikundi mbalimbali ambavyo vilitangaziwa katika kila kata kupeleka mradi itakayotekelezwa kwa mwaka huo.Alisema kata 37 kati ya 41 zilizopeleka maombi na miradi inayopendekezwa ikiwemo ya ufugaji wa kuku na samaki kwa vikundi hivyo. Jumla ya vikundi 35 viliomba mradi wa ufugaji kuku na vikundi viwili viliomba mradi wa ufugaji samaki.Juma alisema Kamati ya Mfuko wa Jimbo ilichambua maombi yote na kuazimia kuwa vikundi 35 vilivyoomba mradi wa kuku vipatiwe vifaranga 540 vya kuku aina ya kroiler pamoja na vyombo 16 vya maji, vyombo 16 vya vyakula na chanjo aina tatu, dawa na mifuko tisa ya chakula.Kuhusu ufugaji wa samaki, vikundi viwili vilivyoomba mradi wa samaki, kamati iliridhia kuwa vipatiwe vifaranga vya samaki aina ya sato, matangi ya kuhifadhia maji na kufungwa mfumo wa maji kutoka kwenye samaki hadi kwenye mboga.Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe alisema fedha za mfuko wa jimbo zinachechemua miradi midogo lakini vinataka pia halmashauri kutumia fedha za ndani kuongeza fedha katika miradi.Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema pamoja na kwamba fedha hizo zinaletwa katika jimbo lakini zinakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) hata kama miradi inaibuliwa na wananchi wenyewe. Akizungumza kiongozi wa Wabunge kutoka Kenya, Fred Omondi alisema wamejifunza mengi kuhusu uendeshaji wa mfuko huo.
kitaifa
WAANDISHI WETU -DAR, SOGEA VIONGOZI wa dini katika makanisa mbalimbali nchini jana walitumia ibada ya Ijumaa Kuu kutoa ujumbe mzito, wakikemea utesaji, utumwa, matumizi yasiyofaa ya simu ambayo yameziweka ndoa nyingi shakani na kuhubiri amani, uhuru, upendo na kujitoa kwa ajili ya wengine. Akitoa salamu za Ijumaa Kuu katika Ibada ya Kitaifa iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Usharika wa Lukajange, Karagwe mkoani Kagera, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Karagwe, Dk. Benson Bagonza, alisema siku ya jana ni ya kukumbuka mateso na kifo cha Yesu, ambayo ndiyo msingi wa dini ya Kikristu. Alisema binadamu huwa hawapendi mateso kama ya Yesu, lakini wakilazimika sana huwa wanapenda kuwatesa wengine na si kuteswa. “Sisi binadamu hatupendi   mateso, kama tukilazimika sana tunapenda kuwatesa wengine, lakini si kuteswa, kukwepa mateso ni ishara ya ushupavu na ushujaa, usimtese mtu kwa sababu Bwana Yesu aliteswa, ukifanya hivyo unamgeuza mtu huyo kuwa Bwana Yesu, kwa hiyo si sawa, mara nyingi watesaji jambo hili hawalijui,” alisema Askofu Bagonza. Alisema utesaji ni kama bangi, ikishaingia mwilini unajenga mazoea ya kupenda kutesatesa  watu na usipowatesa unajisikia kuwashwa washwa na kwamba ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa Kiyahudi. Akitoa mafundisho ya upendo na upatanisho, aliwataka watu kuwa na tabia ya kujitoa kwa ajili ya wengine, kuanzia kanisani hadi  katika ngazi ya Taifa. “Tujitoe kwa ajili ya wengine, kujitoa na kujitolea ni mambo ambayo yanazidi kupotea katika kanisa letu na hata ndani ya Taifa letu, siku hizi kila kitu ni fedha, nawasihi ndugu zangu tujitoe, tujitoe muda wetu na mali zetu  katika kulitumikia kanisa na Taifa. “Kutoa na kujitoa ni ibada kamili, ikifanyika kwa usahihi na mwongozo kwa kufuata Biblia vinaongeza thamani yetu kwa Mungu, Bwana Yesu alitoa damu yake isiyo na hatia ili kutukomboa sisi. “Nakumbuka nikiwa kijana wakati nasoma shule ya msingi hapa Karagwe tulihamasishwa kutoa damu kwenda Msumbiji  tuliambiwa inaenda Msumbiji kumkomboa ndugu yangu, sijasahu hadi leo thamani ya damu katika uhusiano na upatanisho, ni kubwa sana kuliko unavyodhani,” alisema Askofu Bagonza. Mbali na hilo, Dk. Bagonza pia aliwataka waumini wa Kikristu kuonyesha tofauti ya watumwa waliokombolewa na waliopo utumwani. Alisema watumwa waliokombolewa huwa ni watu huru wenye shukurani, wana furaha, wanajiamini, wanachukia utumwa hata wakiwa huru hawafurahi kuwaona wengine wakiwa bado utumwani. “Kukombolewa halafu wewe ukawa mfuga watumwa ni jambo la aibu mno, kuna tabia moja ya kuzoea utumwa, tabia mojawapo ya mtu kuzoea utumwa ni kupenda kubaki utumwani, ya pili kupenda kumiliki watumwa, ndugu zangu nayasema haya kuwaeleza kuwa ukombozi unaotokana na kifo cha Bwana Yesu pale msalabani unatutaka sisi sote tuwe chachu ya kupenda uhuru sisi wenyewe na kwa wengine pia. “Hapa kwakuwa naongea na Watanzania wote niseme tu kwa ufahari tunu moja tuliyobarikiwa kuwa nayo katika Taifa hili chini ya uongozi wa Baba wa Taifa ni pale tulipotangaza kuwa uhuru wetu hauna maana kama bado kuna nchi nyingine zipo utumwani, tukaona uhuru si kamili, tukatumia rasilimali nyingi kuwasaidia jirani zetu waondokane na ukandamizaji, ukoloni na utumwa, sisi wa Mkoa wa Kagera,” alisema Askofu Bagonza. Alisema anakumbuka jinsi Taifa lilivyoingia gharama kubwa kuingia vita kupinga udikteta katika nchi ya jirani. “Ulituhusu nini ule udikteta, sisi hatukuwa na dikteta hapa, tulikuwa tunaishi vizuri, lakini kwa sababu tuliona jirani kuwa katika shida si sawa na sisi tukaingia katika gharama, hii ni sawa na kuteseka kwa Yesu, tumtii aliyetukomboa. “Anatuagiza tushike amri zake ambazo zinatuweka salama kwa kutokomboa sisi, si yeye, wapo watu wanaodhani kwa kukataa kukombolewa wanamkomoa anayemkomboa. “Katika somo la leo, cha kwanza tupendane kwa sababu ni watumwa tuliokombolewa, wewe na mimi wote ni watumwa waliokombolewa, tufurahie ukombozi, tuuchukie utumwa,  tusitamani kurudi huko, tuishi maisha ya shukurani kwa mkombozi wetu, ndugu zangu mfano wewe umeiba unakimbia na kupepea kakamatwa mtu mwingine ambaye hajaiba  anahukumiwa kuuawa, wewe unaangalia tu na kuchekelea unaona inakuja, unafikiri ni ujanja?” alisema Bagonza. Mbali na hilo, Askofu Bagonza pia alizungumzia kuhusu umwagaji damu, akisema damu ya mwenye haki haimwagiki bure  na kwamba isipokomboa itaangamiza. “Damu yenye haki kama ya Yesu ikishamwagika kwa sababu ni damu ya mwenye haki  isipokomboa inaangamiza, tuwe macho sana kwa sababu  kutukuza, kushabikia, kukalia kimya au kukumbatia umwagaji wa damu usio na hatia kuna madhara kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo, kazi ya damu ya mwenye hatia ni kukomboa na kutakasa, isipofanya hivyo inaangamiza, waweza usiangamie wewe uliyeshiriki, unayeshabikia, unayekaa kimya wakaja kuangamia uzao wako au Taifa lako na hao hawana hatia kwa sababu hawakuwepo wakati unashabikia umwagaji damu usio na hatia,” alisema Askofu Bagonza. Wakati Askofu Bagonza akisema hayo, kwa upande wake, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu, amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuilinda imani kwa kuyahubiri mema na si kufanya kama walivyofanya Petro na Yuda. Akihubiri kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, Askofu Dallu alisema kipindi cha miaka ya karibuni Wakristu walipita katika wakati mgumu wa kiimani, lakini waliyashinda majaribu kwa kuendelea kuhubiri amani na kumtangaza Kristo. “Katika kipindi hicho kigumu baadhi yao walimkumbuka Petro na kusema tuchomoe na sisi upanga uliorudishwa alani mwa Petro, lakini wengine walisema hapana, bali tusimame katika imani,” alisema Askofu Damian Dallu. Alifafanua kuwa baadhi ya wanafunzi wa Yesu, akiwamo Petro, hawakutambua kuwa Yesu Kristo hulindwa kwa imani na ndiyo maana alichomoa upanga alani mwake na kumkata sikio mmoja wa maadui, huku Yuda akipokea vipande vya fedha kutoka kwa makuhani kwa maslahi yake, jambo ambalo kiimani haikutakiwa.  “Ni mambo ya ajabu kwa Mkristo wa Kanisa la Katoliki kuwa waoga kuhubiri ukweli uliopo kwa kuogopa kufanyiwa vibaya na baadhi ya watu wenye nia mbaya, hali hiyo haitakiwi kwa kuwa mbaya yeyote akimzuru kiongozi wa dini siyo kwamba ameliuwa kanisa au Ukristo, bali Kanisa litazidi kusonga mbele,” alisema Askofu Dallu. Naye Mkurugenzi wa Utume na Familia, Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Padri Novatus Mbaula, ameishauri jamii kupunguza matumizi ya simu za mikononi ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia mafarakano kwa wanandoa na jamii kwa ujumla. Akitoa mahubiri ya Ijumaa Kuu katika ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Jijini jana iliyohudhuriwa pia na Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, Padri Mbaula alisema binadamu wamekuwa na kiburi na majivuno kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii na kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo, hali ambayo inamchukiza Mungu. “Wanadamu wamejaa viburi kiasi ambacho kimesababisha mifarakano kwa baadhi ya wanandoa, huku muda mwingi wakitumia kwenye mitandao ya jamii kupitia simu za mikononi bila kuwaza athari ambazo zinaweza kutokea, hali ambayo imesababisha kuongezeka kwa migongano na mifarakano baina yao,” alisema Padri Mbaula. Alisema kiburi na majivuno, hayawasaidii chochote katika maisha, zaidi ya kujitenganisha na upendo wa Mungu. Zaidi alionya vitendo vya imani za ushirikina, dhuluma kwa mazao ya wakulima, wastaafu na watu wanaotengwa na kukandamizwa katika jamii ya sasa, ambavyo kwa sasa alidai  vimeongezeka. Alisema kitendo cha kukumbatia mambo ya ulimwengu bila ya kuwa na hofu ya Mungu kunasababisha jamii nyingi kuporomoka. Zaidi alizungumzia hulka ya kujikweza na kujitukuza kuliko kujishusha na kujiona dhaifu mbele za watu, kunachangia kuongezeka kwa chuki. “Binadamu wameacha kumtolea Mungu sadaka, badala yake wanaishi maisha ya kujikweza na kujitukuza bila kuwa na hofu, wakati umefika wa kila mmoja kujifikiria na kutafakari yupo kwenye kundi gani ili aweze kurudi na kutubu, jambo ambalo linampendeza Mungu,” alisema. Alisema kutokana na hali hiyo, waamini wanapaswa kukumbatia haki na mapatano katika jamii wanazoishi ili waweze kuongeza wema na amani, huku wakiwa na upendo ambao utasaidia kuboresha amani kati yao. Katika mwelekeo huo huo, naye Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Chediel Luiza, alisisitiza upendo pamoja na kusamehe. Akitoa mahubiri hayo katika Kanisa la Azania Front, Jijini Dar es Salaam, Mchungaji Luiza mbali na hilo, alisisitiza kuwa kuna wakati viongozi wanachonganishwa, raia wanachonganishwa, lakini msamaha ndio unaotakiwa. “Viongozi wakichonganishwa wakashindwa kutenda haki wanakosea,” alisema Mchungaji Luiza. Pia Mchungaji Luiza alisema  thamani ya mtu inapaswa kutunzwa kama maandiko yanavyosisitiza, watu wasiteswe, wasiuliwe, bali utu utunzwe. “Unaangalia taarifa ya habari watu wanateswa huko nje ya nchi, wamechoshwa na viongozi,  lakini Yesu anatufundisha kusamehe,” alisema Mchungaji Luiza. Alisema mateso ya Yesu Msalabani yasitumike kama kigezo cha watu kuteswa, kwasababu ya imani zao na misimamo, ni ishara ya ukombozi. Alisema mateso hayo yanakumbusha pia kutimiza wajibu kama Yesu alivyomkabidhi mama yake kwa mwanafunzi aliyempenda ambaye naye alitii. Alisema haijalishi unazungumzwa vibaya, unasemwa, lakini ibada ya misa ya Ijumaa Kuu inakumbusha kuwa upendo hushinda hayo. Habari hii imeandaliwa na AZIZA MASOUD, PATRICIA KIMELEMETA Na AGATHA CHARLES (DAR), AMON MTEGA(SONGEA)
kitaifa
JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kukutwa na zana mbalimbali za kutengeneza noti bandia kwa lengo la kujipatia kipato kwa utapeli. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley alisema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 8, mwaka huu wakati askari wakiwa katika doria.Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Beatus Taita (28) mkazi wa Mwanza, Pasifili Masawe (33), mkazi wa Ipuli, Shaban Mrisho (26) mkazi wa Mwinyi na Anicet Joseph (27) mkazi wa Uzunguni. Wengine ni Hance Mkonongo (31) mkazi wa Block T Mbeya, Denis Simbee (39) mkazi wa Tunduma na Nickson Shitindi (38) mkazi wa Mbozi, Songwe. Alieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na makaratasi yanayotumika kutengeneza noti hizo bandia Alisema katika mahojiano, watuhumiwa hao walikiri kujihusisha na uhalifu huo.Katika msako mwingine uliofanyika saa 2.30 usiku siku hiyo polisi walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa 12 wa dawa za kulevya katika eneo la Vatican, Kata ya Gongoni Manispaa ya Tabora wakiwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni kokeni. Waliokamatwa ni Khadja Halfan (40), mkazi wa Isevya, Haji Abdallah (45), mkazi wa Isevya, Ally Sunga (23), mkazi wa mkoani, Elias Msuya (29) mkazi wa Ipuli na Yusuph Sijamini (33), mkazi wa Kalunde. Wengine ni Rashid Mrisho (35), mkazi wa Isevya, Rashid Lungwa (37), mkazi wa Isevya, Gumsan Kairo (28), mkazi wa Isevya, Kulwa Chambi (35), mkazi wa Isevya, Mashaka Akida (25), mkazi wa Isevya, Said Salum (25), mkazi wa Chemchem na Miraji Omar (22), mkazi wa Ipuli. Alieleza kuwa watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara moja baada ya upelelezi kukamilika.
kitaifa
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wadogo kulipia na kuchukua vitambulisho maalumu vilivyotolewa na serikali kwa ajili yao vinginevyo vitahesabika kuwa ni wafanyabiashara wakubwa wanaopaswa kulipia kodi.Hatua itasaidia kuwatambua na kuepusha usumbufu wakati wa kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo.Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa TASAF wilayani Sikonge ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora.Alisema mfanyabiashara ndogo ndogo asiyetaka kulipia Sh 20,000 za kitambulisho maalumu atahesabika kuwa yeye anapaswa kukata leseni na kulipa kodi kama walivyo wafanyabiashara wakubwa.Makamu wa Rais aliongeza kuwa kama Sh 20,000 zinaonekana ni nyingi kwa baadhi ya wafanyabiashara wadogo kulipa kwa mkupuo, uongozi wa mkoa, wilaya unaweza kuweka utaratibu ambao utawawezesha kulipa kwa awamu.Alisema mfanyabiashara huyo anaweza kulipa kwa awamu mbili au tatu na akishamaliza malipo anakabidhiwa kitambulisho chake.Aidha Makamu wa Rais alitoa angalizo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha hakuna mfanyabiashara atakayepewa kitambulisho kabla ya kumaliza malipo yote kuwa upo uwezekano wa kutoroka na kwenda mkoa mwingine na kuendesha shughuli zake kwa kutumia kitambulisho ambacho bado anadaiwa.
uchumi
    Na Christian Bwaya, MARA nyingi tumesikia watu wakilaumu mtalaa wetu kwamba unafunga fahamu za wanafunzi wetu. Wenye madai haya wanafikiri bila mtalaa kufanyiwa marekebisho makubwa, haiwezekani elimu yetu ikamnufaisha mwanafunzi. Hata hivyo, tulisema wiki iliyopita, kazi ya mtalaa ni kutoa dira ya jumla ya aina ya raia wanaotarajiwa kufundwa kupitia mtalaa husika. Mwalimu ndiye mwenye kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kile kinachokusudiwa kufikiwa na mtalaa. Katika makala haya ninalenga kuonesha namna gani mwalimu aliyefuzu anaweza kutumia mtalaa huu unaolalamikiwa kujenga tabia ya udadisi kwa wanafunzi wake. Ningependa nitumie mfano wa Shirika lisilo la Kiserikali liitwalo Opportunity Education. Shirika hili linaendesha mradi unaoitwa Next Generation Learning (NGL) ambao kimsingi unajaribu kutafsiri maudhui ya mtalaa katika mazingira halisi ya mwanafunzi. Kazi hii inafanywa na walimu wa shule zetu waliopata mafunzo maalum kuandaa mfululizo wa masomo yanayoandaliwa kutokana na mtalaa wetu. Sambamba na kutafsiri maudhui ya mtalaa wetu, NGL wametengeneza mfumo wa ufundishaji na ujifunzaji wanaousimamia wao wenyewe kwenye shule teule. Mradi huu ambao tayari umeshaonesha mafanikio, unatumia kanuni kuu tano ambazo naamini mwalimu yeyote anaweza kuzitumia. Kwanza, kuhakikisha kuwa mwanafunzi anaelewa kwa nini anahitaji kujifunza kile anachojifunza. Hili kwa hakika limekuwa changamoto ya ufundishaji wa kimazoea. Tumekuwa tukifundishwa maudhui ambayo kwa kweli hatuelewi tutayatumia wapi. Nakumbuka kwa mfano, nikiwa kidato cha V kwenye somo la Fizikia tulifundishwa hesabu ndefu za namna ya kutafuta muda utakaotumiwa na tone la mwisho kudondoka kwenye bomba la maji linalofungwa. Hatukuelewa kwa nini ilikuwa ni lazima kusumbua akili kufanya hesabu hizi ngumu zisizotatua tatizo lolote kwenye maisha yetu. Ufundishaji wa namna hii, kwa hakika, unamkatisha tamaa mwanafunzi. Mwanafunzi asiyeelewa kwa nini anasoma kitu hawezi kuwa na udadisi. NGL wameonesha mfano wa namna tunavyoweza kuondoa hitilafu hii. Kupitia mfumo wao wa ujifunzaji, NGL wanajaribu kufikiri namna gani kile kinachofundishwa kinagusa maisha ya kawaida ya mwanafunzi. Kujua uhusiano wa maudhui na maisha yake kunamwongezea mwanafunzi ari ya kujifunza kwa sababu anaelewa thamani ya kile anachotarajiwa kujifunza. walimu anapata somo muhimu hapa. Kwamba ni muhimu atafute namna ya kuhusianisha somo lake na maisha ya mwanafunzi. Kwa mfano, mwalimu wa Kemia anapofundisha somo la Mada (matter) anahitaji kufanya kazi ya ziada kumsisimua mwanafunzi kuona namna maarifa ya mada yanavyoweza kumsaidia katika maisha yake ya kila siku. Kazi hii haifanywi na mtalaa bali mwalimu. Kanuni ya pili inayotumiwa na NGL, ni kuhakikisha mwanafunzi anajenga uwezo wa kujiuliza maswali ya msingi kuhusu hicho anachojifunza badala ya kutegemea majibu yaliyopikwa na mwalimu anayeonekana kuwa mjuzi na mmiliki wa maarifa. Kwa hakika madarasa yetu yanafanya kinyume. Kazi ya walimu imekuwa ni ‘kuhubiri’ maarifa kwa mwanafunzi. Mwanafunzi anachukuliwa kama mtu anayesubiri kupikiwa kila kitu na kazi yake ni ‘kumeza’ kile anachoambiwa. Hana fursa ya kuuliza wala kuhoji. Shule zetu ‘zinazofaulisha sana’ kimsingi zinajitahidi kuhakikisha mwanafunzi anafahamu kwa hakika nini cha kukariri. Walimu wa shule hizi wanafanya bidii kubwa kuwaimbisha wanafunzi kile wanachojua kitaulizwa kwenye mtihani. Somo tunalopewa na Opportunity Education ni kwamba mwanafunzi anayewekewa mazingira ya kujiuliza maswali na kushiriki moja kwa moja katika kutafuta majibu, anakuwa na uwezo wa kudadisi kuliko mwenzake anayeshiriki ‘kumeza’ maarifa. Mwalimu lazima afanye kazi kubwa ya kuibua maswali yanayohusiana na kile anachokifundisha ili wanafunzi waweze kujifunza kwa mfumo wa kutafuta majibu wao wenyewe. Mradi wa NGL unatuthibitishia kuwa mwalimu akiwezeshwa anaweza kutafsiri mtalaa huu unaodaiwa kuwa haufai kuibua kiu ya kutafuta majibu. Kanuni ya tatu ni kumtarajia mwanafunzi kutumia maarifa yake kutengeneza ujuzi. Mwanafunzi wa NGL si tu anahitajika kujibu maswali ya kufikirisha, bali kuonesha ujuzi mahususi. Mathalani, baada ya mwanafunzi kujifunza namna mimea inavyotengeneza sukari kwa kutumia mwanga wa jua, lazima aoneshe anavyoweza kutumia maarifa hayo kutatua matatizo katika mazingira yake. Inaendelea Mwandishi ni Mhadhiri wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU).  Blogu: http://bwaya.blogspot.com, 0754870815
kitaifa
MFUMO wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya nauli kwenye mabasi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), unatarajiwa kukamilika Machi mwaka huu. Sambamba na hilo, serikali imeanza mchakato wa kumpata mtoa huduma kamili wa mabasi hayo ifikapo Julai mwaka huu.Akiwasilisha bungeni jana ripoti ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za Mitaa ya kuanzia Februari mwaka jana hadi Januari mwaka huu, Mwenyekiti wake, Jasson Rweikiza amesema kwa sasa wataalamu wa DART, Tamisemi na eGA(eGovernment) wanashirikiana kutengeneza mfumo huo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya nauli.“Tangu Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam ulipoanza kutoa huduma ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam Mei, mwaka 2016 umekuwa ukitumia mtoa huduma wa mpito na ameshindwa kutoa huduma kwa kiwango kinachotakiwa kutokana na uchache wa mabasi aliyonayo, pamoja na kukosa mfumo madhubuti wa ukusanyaji nauli.Aliingiza nchini mabasi 140 kati ya 305 yanayohitajika, na kukosa mfumo wa uhakika wa tiketi, hivyo serikali imechukua hatua kadhaa ili kukabili changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuanza mchakato wa kumpata mtoa huduma kamili ifikapo Julai mwaka huu,”amesema.Wakala huo ulianzishwa mwaka 2007 kwa Tangazo la Serikali Na. 120 ili kusimamia utekelezaji wa mfumo wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam kwa ufanisi na hivyo kupunguza msongamano, ambao ni kero kubwa. Mradi wa DART utatekelezwa kwa awamu sita na utahusisha barabara zenye urefu wa kilomita 146.Awamu ya kwanza ilikamilika na kuanza kutoa huduma Mei 2016. Kamati hiyo ilisema kuwa DART, haina sheria mahususi ya kusimamia utendaji na utekelezaji wa majukumu yake, hivyo kuathiri utendaji na utekelezaji wa majukumu ya wakala.Rweikiza alitaja athari hizo za utendaji kuwa ni pamoja na kukosa kanuni za kusimamia na kudhibiti matumizi mabaya ya miundombinu yake.“Kamati inalishauri Bunge kuitaka serikali kuiwezesha DART kupata sheria mahususi ambayo itasaidia kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumu ya wakala. Sheria hiyo itawezesha kutungwa kwa Kanuni za DART ili kusimamia na kudhibiti uvamizi na matumizi mabaya ya miundombinu ya wakala,”alisema.Akichangia Mbunge wa Viti Maalumu, Ruth Mollel (Chadema) alisema kila kunapotokea mafuriko jijini Dar es Salaam, ofisi za DART zilizopo Jangwani zinajaa maji. Alisisitiza “Ingekuwa kuna nyumba za watu pale zingebomolewa, nashauri bajeti ijayo hizo ofisi ziondolewe,” alisema.
kitaifa
Na Johns Njozi, Dar es Salaam Kampuni ya Maxcom Africa (Max Malipo), imekanusha taarifa kuwa mkataba wake na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) unamalizika hatua itakayosababisha kampuni hiyo kushindwa kutoa huduma ya kuuza umeme wa LUKU kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Deogratous Lazari taarifa hizo  zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza hayo, si za kweli. Amesema taarifa hizo zinasema baada ya Machi 31, mwaka huu Wananchi na wabia wa Maxcom wataendelea kujipatia huduma mbalimbali kupitia kwenye mfumo wa Maxmalipo ikiwamo huduma ya LUKU hazina ukweli wowote na hali halisi. “Kilichotokea ni kwamba, tumeunganishwa kwenye mfumo wa serikali wa malipo kielektroniki (GEPG), hivyo baada ya Machi 31, wananchi na wabia wetu wataendelea kujipatia huduma mbalimbali ikiwamo ya LUKU kupitia Maxmalipo. “Hivyo, tunapenda kuwahakikishia wananchi kwamba, malipo ya huduma ya LUKU na huduma nyingine zitaendelea kupatikana kupitia kwa mawakala na wabia wote wa Maxmalipo nchi nzima,” amesema Lazari katika taarifa yake hiyo. Aidha, kampuni hiyo imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wabia na wananchi wanaotumia huduma ya Maxmalipo.  
kitaifa
SPIKA mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, ametaja mambo mawili makubwa yaliyomuumiza kabla ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1999. Aidha, alisema yeye ni kiongozi wa mwisho nchini, aliyeongea na Mwalimu Nyerere kabla kiongozi huyo hajakata kauli. Alitaja mambo hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Dar es Salaam mintarafu Kumbikizi la Miaka 20 tangu kufariki kwa mwalimu Nyerere, Oktoba 14, 1999. Matukio hayo kwa mujibu wa Msekwa, ni lile la kumpelekea Nyerere zawadi aliyotumwa na Bunge, lakini akakuta Baba wa Taifa anaumwa akiwa nyumbani na anajiandaa kwa safari ya kwenda London Uingereza kwa matibabu. Lingine alisema ni lile la kumkuta ameruhusiwa kutoka hospitali mjini Londoni Uingereza na Nyerere kumwambia anajiandaa kurudi nyumbani, lakini siku hiyo hiyo, hali ya mwalimu hali ikawa mbaya, akarudishwa hospitali na kukata kauli. “Mwezi Oktoba 1999, tulikuwa na mkutano wa maspika wa bunge huko West Indies ambako kwenda na kurudi lazima upite London. Siku ya kurudi nikapita hapo kumjuliana hali baada ya balozi kunifanyia mpango nimuone. Nikamkutana mkewe Mama Maria Nyerere,” alisema Msekwa. Aliongeza kuwa, “ nikafurahi kumuona amepata nafuu na akaniambia, ‘Pio (Pius) ninajiandaa kurudi nyumbani wiki ijayo...” Alisema siku hiyo usiku, Msekwa aliondoka Uingereza kwa ndege kurudi Tanzania na alipofika, aliwajulisha viongozi wa juu akiwamo Waziri Mkuu, Frederck Sumaye (wakati huo) kuhusu maendeleo ya kiafya ya Mwalimu Nyerere na kwamba, anajiandaa kurejea Tanzania baada ya hali kuimarika...kesho yake, waziri mkuu akaniita na kuniuliza wewe si ulisema Mwalimu anaendelea vizuri na anarudi nyumbani wiki ijayo, mbona balozi anasema jana amerudishwa hospitali na amekata kauli,” alisema Msekwa. Spika mstaafu huyo alisema: “nikamwambia hayo ni mapenzi ya Mungu; ndivyo nilivyomkuta hata balozi aliniambia hivyo hivyo na hiyo ilikuwa Septemba 25, 1999... Kwa kweli, hiyo iliumiza na kunitia huzuni sana, lakini nafurahi aliyoniambia niyafikishe kwa watawala, niliyafikisha na ninaamini yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi vizuri.” Kuhusu kumpelekea Nyerere zawadi baada ya kuliaga Bunge kwamba anang’atuka, Msekwa alisema Bunge lake liliazimia kumpa zawadi ya vitabu aina ya Encyclopedia Britanica juzuu 32. “Ilinitia huzuni wakati alipoaga Bunge kuacha urais na Bunge likaazimia kumpa zawadi ya vitabu maalumyu visivyopatikana kwa urahisi madukani vinaitwa Encyclopedia Britanica Vulume 32. Tulijua hawezi kuvipata hapa nchini kutokana na bei yake kuwa kubwa hivyo, maduka ya huku hayaviagizi,” alisema. Aliongeza kuwa, “nikatumwa niviagize kutoka London. Walisema vimekwisha, lakini baada ya kujua kuwa ni kwa ajili ya Mwalimu Nyerere, wakasema watachapisha toleo maalumu.Ilipita kama miaka mitatu, nikatumwa kumpelekea hiyo zawadi Butiama. Sasa nimepeleka zawadi, nikakuta Mwalimu ninayempelekea zawadi anaumwa mkanda wa jeshi,” madonda yapo tumboni. Akanieleza namna anavyopata tabu.” Kwa mujibu wa Msekwa, Watanzania hawana budi kumshukuru Mungu kwa kuwapa Rais John Magufuli kuliongoza taifa kwa kuwa mambo mengi anatoyafanya sasa, anatimiza ndoto za Mwalimu likiwamo suala la serikali kuhamishia makao makuu jijini Dodoma.
kitaifa
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amenusurika kifo baada ya kupuliziwa kwa inayodaiwa kuwa gesi ya kuwasha katika Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), jijini Mwanza. Uchaguzi huo uliolazimika kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba baada ya mmoja wa vijana kudaiwa kupulizia gesi hiyo ya kuwasha iliyozua taharuki ndani ya ukumbi wa Rock City Mall jijini humo, hali iliyosababisha Naibu Waziri huyo kusaidiwa kutolewa nje haraka na alipatiwa huduma ya kwanza huku wajumbe wengine wa mkutano huo waliofanikiwa kutolewa ndani ya ukumbi huo wakiwa hoi ambapo walipatiwa maziwa na maji kwa ajili ya kuondoa gesi hiyo iliyokuwa ikiwasha. Tukio hilo limetokea leo Jumatano Novemba 29, baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM kuwasili na kuelekezwa kuingia ndani ya ukumbi tayari kwa kumpokea mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela. Wakiwa ndani ya ukumbi huo huku wakiimba nyimbo za chama, ghafla hali ya hewa ilibadilika baada ya watu kuanza kukohoa na kupiga chafya kutokana na hewa nzito na kusababisha wajumbe kukikimbilia nje kujiokoa. Hofu ya usalama ilitanda ndani ya ukumbi huo hivyo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alilazimika kukutana na Mkuu wa Mkoa John Mongela na kukubaliana mkutano huo kuhamishiwa uwanja wa CCM Kirumba na kuendelea na uchaguzi. Hata hivyo, tukio hilo liliwalazimu kuita polisi ambao baada ya kufika walianza kufanya upekuzi kwa baadhi ya wajumbe waliokuwa na mabegi na mikoba na kufanikiwa kumkamata mjumbe mmoja ambaye walimtilia shaka na kuondoka naye hali iliyozua vurugu zaidi kwa vijana kupinga kukamatwa kwake. Lakini inadaiwa kijana aliyekamatwa alikuwa na pafyumu ya kawaida wakati polisi wakiifananisha na gesi ya kuwasha ambapo walianzisha vurugu wakishinikiza aachiwe ndipo Mkuu wa Mkoa alipoingia kati kuwatuliza kwa kuamuru polisi kumwachia kijana huyo ambaye alirejea mkutanoni.
kitaifa
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesema limepokea kwa  mshtuko na majonzi taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media na mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana U17 (Serengeti Boys) Dk. Reginald Mengi. Dk. Mengi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 2, nchini Dubai alipokuwa akipatiwa matibabu. Katika taarifa ya Rais wa TFF, Wallace Karia, iliyotolewa leo na Afisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo leo imesema Dk. Mengi alikuwa na mchango mkubwa katika mpira wa miguu ambao bado ulikuwa unamuhitaji. “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za msiba wa mlezi wetu wa Serengeti Boys, sote ni mashahidi kwa namna alivyojitolea katika mpira wa miguu kuanzia ngazi ya klabu hadi timu za Taifa hakika mchango wake bado unahitajika kwa niaba ya TFF natoa pole kwa familia yake, makampuni  ya IPP, ndugu na wanafamilia ya mpira wa miguu nchini kote,” imeeleza taarifa hiyo. Aidha taarifa hiyo imeeleza kwamba Dk. Mengi alikuwa mlezi wa Serengeti boys ambapo mara ya mwisho alikuwa na timu hiyo iliposhiriki katika fainali za Afrika za Vijana U17 (AFCON) zilizofanyika nchini na kumalizika Aprili 28 mwaka huu, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
michezo
NAIROBI, KENYA KATIBU binafsi wa Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki amekanusha taarifa kwamba kiongozi huyo amelazwa katika Hospitali ya Nairobi. Katibu huyo, Ngari Gituku amesema kuwa Kibaki mwenye miaka 88 alifika katika hospitali ya Nairobi Jumatatu kwa ajili ya utaratibu wa kawaida wa  kuangalia afya yake.  “Ilikuwa ni safari ya kawaida na hakuna kitu kipya,” aliliambia gazeti la Daily Nation la nchini Kenya kwa njia ya simu. Wakati ikielezwa kuwa Kibaki anasumbuliwa na tatizo la goti baada ya kupata ajali ya barabarani huko Machakos  mwaka 2002,  Gituku kwa upande wake hakuthibitisha kama ni sababu ya sasa ya yeye kwenda hospitalini. “Kwa umri wake, wanaweza kumchunguza kitu chochote, kama macho, kibofu cha mkojo na vitu vingine,”  alisema. Chanzo kimoja cha habari ambacho kimekataa kutajwa jina kwa sababu yeye si msemaji wa familia kilisema kuwa rais huyo mstaafu hali yake inaendelea kuimarika na kwamba alikuwa katika hali ya tahadhari. Hatua ya Kibaki kufika katika hospitali ya Nairobi kulikuja katika siku ambayo Rais wa Mstaafu wa Kenya na ambaye ametawala nchi hiyo kwa muda mrefu, Daniel Arap Moi naye akirejea hospitalini hapo kutokana na kile ambacho msemaji wake Lee Njiru kusema kuwa ni “uangalizi wa kawaida”. Ingawa chanzo cha habari kutoka katika familia ya Moi kilisema kuwa kiongozi huyo ambaye ana miaka 95 alikimbizwa hospitalini hapo Oktoba 18 mwaka huu baada ya kupata tatizo la kupumua. Kwa upande wake Kibaki, ambaye ni kiongozi wa zamani wa chama cha Narc, anajiandaa kusheherekea miaka 89 ya kuzaliwa Novemba 15 mwaka huu. Mara ya kwanza alifikishwa hospitali ya Nairobi Januari 20, 2004. Timu ya wataalamu waliokuwa wakimtibu walisema kuwa walibaini kuganda kwa damu katika mguu wake wa kulia. Mwezi Agosti 2016,  kiongozi huyo wa zamani alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya  Netcare Sunninghill iliyoko nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuondoa kuganda huko kwa damu katika mshipa wa kwenye shingo yake.
kimataifa
THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM BAADA ya kupiga kambi ya muda Singida, kikosi cha Simba kimepanga kuondoka mkoani humo leo kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Stand United. Simba itakuwa mgeni wa Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho kutwa Uwanja wa Kambarage mkoani humo. Simba itakutana na Stand United ikitoka kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli FC, katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Samora, Iringa. Akizungumza na MTANZANIA jana, kocha wa viungo wa timu hiyo, Aden Zrane, alisema kwa ujumla hali za afya za wachezaji wao ziko timamu. “Tulifika juzi usiku Singida na leo (jana) jioni tutaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Stand United kisha kesho tutaondoka, tunafahamu bado tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema Zrane na kuongeza: “Wachezaji wetu wapo fiti kucheza mchezo huo isipokuwa Erasto Nyoni  ambaye ameshaanza mazoezi mepesi lakini hawezi kucheza kwa sasa,” alisema. Zrane alisema kusudio lao ni kuendeleza rekodi ya ushindi katika mechi zao zinazowakabili mbele, hivyo wamejiandaa kwa mapambano bila kujali wanacheza nyumbani au ugenini. “Wachezaji wote wana morali ya juu ukizingatia tumetoka kushinda michezo mfululizo, lazima tuongeze juhudi ili kupata pointi tatu nyingine ugenini,” alisema. Simba inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 48, baada ya kushuka dimbani mara 19, ikishinda 15, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja. Yanga ndiyo inakamata uongozi wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 61, baada ya kucheza michezo 25, ikishinda 19, sare nne na kupoteza michezo miwili, nafasi ya pili iko Azam FC yenye pointi 50, ikishinda 14, sare nane na kupoteza mara tatu.
michezo
UGANDA imeanza kutimiza ndoto ya kutengeneza magari yake yenyewe, badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi na sasa yapo katika majaribio.Hatua hiyo ya kupigiwa mfano, inadhihirisha nia ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kutaka kupunguza uagizaji wa magari kutoka nje. Uganda, kupitia kampuni yake umma ya Kiira Motors Corporation (KMC) ambayo kwa kiasi kikubwa inamilikiwa na serikali, imekamilisha kutengeneza moja ya magari yake, aina ya Kiira EVS na tayari limeanza kufanyiwa majaribio katika miji mbalimbali ya Uganda. Gari hilo dogo linalotumia mafuta, linatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa umbali wa kilometa 1,600.Mengine, aina ya Kiira EVE linalotumia umeme pekee, na jingine aina ya Kayoola ambalo ni basi linalotumia nishati ya umemejua, tayari yameshatengenezwa na kuingizwa katika hatua mbalimbali za majaribio. Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa KMC, Allan Muhumuza, amethibitisha kuanza kwa majaribio hayo katika Jiji la Kampala na baadaye Masaka, Mbarara, Kabale na Kisoro. Aidha, linatarajiwa kuendeshwa pia hadi Magharibi mwa nchi. “Tumeandika historia. Kote tulikopita, kuanzia Kampala, watu hawaamini kama ni gari lililotengenezwa katika ardhi ya Uganda.Tunatarajia kuendelea na majaribio kwa kilometa 1,600 zaidi,” alisema Muhumuza aliyeongeza kuwa, baada ya majaribio wanajipanga kutengeneza magari mengi zaidi kwa ajili ya soko la Afrika Mashariki na nchi nyingine kupitia kiwanda chao kinachojengwa katika eneo la kilometa 100 katika wa Jinja. Nchi nyingine za EAC kama Tanzania, zina magari yake.Mfano Tanzania ina kiwanda cha magari ya Nyumbu ambacho hutengeneza zaidi magari ya kijeshi. Kenya na Rwanda pia zimo katika ujenzi wa viwanda vya kisasa, vikiwemo vinavyotengeneza na kuuza nje ya nchi magari binafsi, ya kubeba ya watalii, malori ya takataka na pikipiki za aina mbalimbali. Kwa Uganda inayoagiza wastani wa magari 50,000 kwa mwaka, kuunda magari yake yenye alama ya ndege Korongo au Crane anayepatikana pia katika alama zote za taifa, ikiwa ni pamoja na bendera na fedha, ulikuwa mpango wa muda mrefu na sasa umeiva baada ya Rais Yoweri Museveni kuingilia kati na kuagiza kazi za ujenzi wa kiwanda ianze mara moja.Wazo la ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji wa magari, lilianza mwaka 2011 baada ya juhudi na maarifa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere kutengeneza gari linalotumia umeme la Kiira EV na basi linalotumia nishati ya jua la Kayoola EV mwaka 2016. Kutokana na mafanikio hayo ya wanafunzi wa chuo hicho kikubwa barani Afrika, mwaka 2014 serikali ilitenga kipande cha ardhi Mashariki mwa Jinja kwa ajili ya KMC.Mradi huo mkubwa katika historia ya Uganda, unatarajiwa kutengeneza nafasi za ajira za moja kwa moja zaidi ya 2,000 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 12,000. Kiwanda hicho kitakapokamilika na kuanza uzalishaji wa magari, Uganda itapata soko kubwa katika nchi za Afrika Mashariki kutokana na mahitaji makubwa ya magari. Afrika Mashariki huagiza magari 250,000 kwa mwaka na mahitaji yanatarajiwa kupanda hadi kufikia magari 500,000 kufikia mwaka 2030.Magari ya Tanzania Nchi hii kubwa kuliko zote Afrika Mashariki, ina kiwanda chake kinachotengeneza magari ya nyumbu ambacho ni mali ya Serikali. Aidha, kampuni binafsi, mathalani Hanspaul Automechs Limited (HAL) iliyopo eneo la viwanda Njiro jijini Arusha, inatengeneza magari makubwa ya kubeba watalii maarufu kwa jina la ‘War Bus’.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Satbir Hanspaul, yanauzwa Kenya, Afrika Kusini na nchi za Ulaya. Kampuni hiyo imebuni na kutengeneza pia magari maalumu ya kubeba taka, yanayofaa kwa mazingira ya Tanzania, ikiwemo hali ya hewa, aina ya barabara na mfumo wa maisha wa wananchi wake.“Lakini aina mpya ya malori ya kubeba takataka si kwa ajili ya kampuni yetu au kiwanda chetu tu, kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na TBS (Shirika la Viwango Tanzania), wazalishaji wengine wanaweza kuyatengeneza lakini kwa kutumia utambulisho wa ubunifu wa HAL kama kielelezo,” alisema Hanspaul. Alisema, magari ya kubeba takataka na yale ya watalii ni ubunifu wa Tanzania unaozivutia nchi nyingine zikiwemo za Ulaya na magari ya watalii yanakubalika kwenye soko la kimataifa. Kwa mwezi huweza kutengeneza zaidi ya magari 35.“Watu wengi hawataamini kwamba, nchi zenye viwanda vya kutengeneza magari kama Afrika Kusini na zile za Ulaya sasa zinanunua magari kutoka Tanzania, lakini wanafanya hivyo,” alisema. Magari hayo yenye nembo za Toyota, Nissan na Land Rover, yanatengenezwa kwa kutumia mashine za kisasa zikiwemo roboti kama ilivyo kwenye viwanda vya magari katika nchi zilizoendelea. HAL ilianzishwa mwaka 2007 na imelenga kuteka asilimia 25 ya soko la magari na spea zake katika nchi za EAC.Gari la kwanza RwandaGari la kwanza kutengenezwa katika ardhi ya Rwanda liliingia barabarani Juni, mwaka jana. Ni matunda ya kampuni ya Volkswagen (VW) ya Ujerumani ambayo imeamua kutengeneza aina tatu za magari madogo nchini humo, ya Volkswagen Passat, Volkswagen Polo na Volkswagen Teramont.Ofisa Mtendaji Mkuu wa VW Afrika Kusini, Thomas Schafer mwanzoni mwa mwaka huu alisema uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 20 ni matunda ya upembuzi yakinifu uliofanywa na kuonekana ni mradi `utakaolipa’ kwa nchi za EAC. Kufikia mwishoni mwa mwezi huu, itakuwa imekamilisha kutengeneza magari 90 na kwamba dhamira katika siku za baadaye ni kutengenea kati ya magari 1,000 na 5,000 kwa mwaka huku ajira zinazotarajiwa kuzalishwa ni kati ya 500 na 1,000.Volvo yaingia KenyaMoja ya kampuni kubwa katika utengenezaji wa magari ya aina mbalimbali, Volvo imeingia nchini Kenya na kuwekeza Sh bilioni 2.5 za nchi hiyo ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda kinachotarajiwa kuanza na uzalishaji wa magari 500 kwa mwaka na baadaye kufikia magari 2,000 kwa mwaka.Kiwanda hicho kilichoingia ubia na kampuni ya NECST Motors ya Kenya, kinatarajiwa kuzalisha ajira 300 za moja kwa moja kiwandani hapo, lengo likiwa kushika asilimia 20 ya soko la Afrika Mashariki. Ni kiwanda cha tatu barani Afrika, vingine vikiwa Morocco ambako imeshika asilimia 20 ya soko na Afrika Kusini inakoshika asilimia 18 ya soko la magari.Kwa Kenya, kitakuwa kiwanda cha nne cha magari. Volkswagen kimeanza tena kazi baada ya kusitisha uzalishaji miaka 40 iliyopita. Kampuni za Peugeot, Toyota, wameanza pia uzalishaji, huku Iveco, Ashok Leyland pia wakitangaza nia ya kuanza uzalishaji wake nchini Kenya.
kitaifa
KATIBU wa Itikati na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amewataka wanachama wa chama hicho kuacha kutafuta uongozi kwa kutumia makundi na ukabila. Kauli hiyo aliitoa jana jijini Mbeya, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa huo, ambapo alisema kuwa moja ya mambo ya ovyo yanayokitesa chama hicho ni baadhi ya watu kutafuta uongozi kwa makundi na ukabila jambo linalotoa fursa kwa wapinzani kushinda uchaguzi. Alisema suala la ukabila na makundi limesababisha vijana wa Mkoa wa Mbeya kukosa mwelekeo na kuyumba hivyo viongozi wa chama hicho wanapaswa kubadilika. “Kama kuna jambo la ovyo kabisa kwenye chama chetu ni hili la kuendelea kucheka na makundi pamoja na kuukumbatia ukabila, mambo haya yanaturudisha nyuma. “Makundi yanatugawa, yanadhoofisha umoja wetu, yanaleta chuki, yanapunguza upendo na kutuacha tukiwa dhaifu mbele ya adui,” alisema Polepole Alisema CCM inatafuta na kuweka kiongozi atakayehudumia wananchi kwa usawa na haki badala ya kuwagawa watu kwa makundi na ukabila. “Msitupe viongozi kazi ya kuja kuvunja makundi, hatuwezi kupoteza muda na kama mtafanya mchezo wengi wetu tumewaona vijana wanavyoumia kwa kuwanyima haki yao ya uongozi na kwamba kabila za Mbeya si za nchi nzima,” alisema Alisema makabila hayana faida yoyote zaidi ya kuwakumbusha watu walipotoka, hivyo viongozi wa CCM Mkoa wa Mbeya, wanapaswa kubadilika na kufanya kazi kwa bidii kama Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli alivyoelekeza. Alisema watu wa Mbeya wanamwamini Rais Dk. Magufuli kwa sababu ya kazi ya kuleta maendeleo kwa nchi na watu wake, inayofanya na Serikali anayoiogoza. Aidha, aliwataka viongozi na watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa bidii pamoja na kutekeleza ilani ya CCM huku akionya kuwa viongozi dhaifu watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa utaratibu na sheria za nchi zinavyoelekeza.
kitaifa
NA WAANDISHI WETU – DAR/MIKOANI MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amejikuta aking’ang’ania ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Dodoma akikwepa kukamatwa na polisi. Hatua hiyo iliwafanya askari waliokuwa wamepiga kambi nje ya mahakama hiyo, kujikuta wakikwama kumtia nguvuni mbunge huyo ambaye anadaiwa kutoa matamko yenye utata dhidi ya Serikali na Rais Dk. John Magufuli. Hata hivyo hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ilikuwa na ujumbe dhidi ya Serikali, huku ikiibuka hofu mhimili huo unaosimamia haki kuwekwa kwenye mtego kwa mwanasheria huyo kukamatwa bila agizo la mahakama. Alipoulizwa Lissu sababu za kung’ang’ania mahakamani, alisema kuwa hakuna maana yoyote kisheria, bali ameamua kufanya hivyo kwa sababu ndiyo sehemu salama kwa nchi zinazoheshimu utawala wa sheria duniani kokote. “Nimeamua kung’ang’ania mle ndani kwa kuwa ni salama zaidi… mbali na mahakama, kwingine ambako ningeweza kwenda ambapo ni salama ni msikitini au kanisani, kwenye nchi zinazoheshimu demokrasia na utawala bora hawawezi kukukamata,’’ alisema Lissu. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema dunia nzima kama utakuwa umekimbilia mahakamani ni sehemu salama, huwezi kukamatwa na askari. Alisema aliingia mahakamani hapo saa 2 asubuhi kuwatetea wateja wake ambao ni walimu walioamua kukishtaki Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Dodoma na kulazimika kukaa humo kwa saa saba. Alisema baada ya kumalizika kwa kesi hiyo saa 8:23 mchana, alilazimika kubaki ndani ya mahakama kutokana na taarifa aliyodai  kupewa ya kukamatwa na askari waliokuwa nje. Lissu alisema kuwa alilazimika muda wote kuwa na mazungumzo na viongozi wa Chadema waliofika mahakamani hapo baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwake. Hali hiyo ilizua taharuki na kumfanya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa kufika mahakamani hapo saa 10:04 jioni akiwa na mlinzi wake na kumtaka Lissu aondoke ndani ya mahakama hiyo kwani hakuna atakayemkamata. Mazungumzo kati ya Lissu na Kamanda Mambosasa yalikuwa kama ifuatavyo: Lissu: Kamanda nipo Dodoma hapa tangu juzi, nipo mahakamani naendesha kesi, naambiwa kuwa polisi wananisubiria nje wanikamate, nikasema kama ndiyo hivyo  siku ile nilikamatiwa getini bungeni na siku nyingine nilikamatiwa nyumbani, nikasema ‘this time’ nipo kazini. Kamanda: Niliwatuma mimi? Lissu: Uliwatuma wewe? Kamanda: Wale waliokukamata niliwatuma mimi? Mimi sina ‘issue’ na wewe wala Afande Inspekta Jenerali (IGP) hana ‘issue’ na wewe, likitokea jingine tutakwambia, leo hakuna. Lissu: Asante Kamanda: Sasa kwa nini unajiweka ndani? Lissu: Nimekwambia sababu zilizonifanya  niwe hapa. Kamanda: Nimekwambia wamekuchanganya na ngoja nikutoe wasiwasi, mimi kama ningekuwa nakutafuta, nakukamatia hapa hapa mahakamani, kwani hili ni jengo la mahakama. Lissu: Eeeh. Kamanda: Yaani hapa sio kwamba huwezi kukamatwa. Lissu: Nilisema hivi, mara hii nitakamatiwa mahakamani, ndivyo nilivyosema labda kwa vile umesema niko salama basi. Kamanda: Walionipigia ni kina nani? Kuna watu walinipia ni waandishi, nilichowaambia nipo mbali labda kama mmeenda kuwinda, hivyo kuna askari wa wanyama pori wanawatafuta. Lissu: Nimekusikia. Kamanda: Tafuteni mambo mengine, hili halipo, habari ndiyo hiyo. Lissu: ‘Ok I’m free’. Baada ya mazungumzo hayo kati yake na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lissu aliondoka katika eneo hilo la mahakama saa 10:12 jioni. Awali akizungumza na waandishi wa habari ndani ya mahakama hiyo, Lissu alisema amechoka kuona nchi namna inavyoendeshwa. Alisema jana asubuhi alipokea taarifa kutoka kwa mke wake kuwa polisi walifika nyumbani kwake Dar es Salaam, wakiwa wanamtafuta. “Wakaambiwa sipo nyumbani kwa sababu tangu juzi nipo Dodoma kwa sababu ya hii kesi iliyoanza kusikilizwa jana (juzi) walivyoambiwa sipo wakaondoka. Wakati kesi hii inaendelea, nikaletewa ujumbe unaosema kwamba askari waliovalia kiraia wa hapa Dodoma wametumwa kuja kunikamata baada ya kesi hii kumalizika,’’ alisema. Alisema pamoja na hali hiyo, yeye ni wakili ila kwa nchi inayoendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria, mawakili huwa hawakamatwi mahakamani wakati wakifanya kazi zao. Rais huyo wa TLS alisema haitakuwa mara yake ya kwanza kukamatwa na kwamba kwa mwaka huu itakuwa mara yake ya nne, huku akidai tangu Juni mwaka jana itakuwa mara yake ya saba au ya nane kutiwa mbaroni. Lissu alisema katika siku za nyuma viongozi wa ngazi za juu wa polisi walikuwa wakitumia njia za kiungwana za kumwambia anahitajika polisi, lakini kwa sasa imekuwa hali tofauti. “Mfano mwaka jana kabla sijafunguliwa kesi ya uchochezi, ile inayohusu gazeti la Mawio ambayo washtakiwa tupo wanne, washtakiwa wenzangu watatu, waandishi wa habari wale walisomewa mashtaka yao mwezi wa nne. “Na RCO wa Kanda Maalumu ya Dar es Saalam, Camilius Wambura, alinipigia simu na akaniuliza nipo wapi, nikamwambia nipo bungeni, akaniuliza ‘ratiba yako ikoje’ nikamwambia nikitoka bungeni nitaenda Masasi katika kesi ya uchaguzi ya mbunge wetu Cecil Mwambe kisha nitaenda Kilombero kwa Lijualikali. “Kamanda Wambura aliniambia kwamba watasubiri nikamilishe hayo majukumu na kweli nilipomaliza tarehe 26 Juni, Jumatatu iliyofuata ya tarehe 28, nilienda polisi na kesho yake nikapelekwa mahakamani kuungwaniswa na wale watuhumiwa watatu,’’ alisema. Mwanasheri huyo mkuu wa Chadema, alisema hawezi kukimbia Tanzania kwani ndipo watu walipomchagua kuwa mbunge. “Na Mkubwa Rais Magufuli aliishasema ukifukuzwa bungeni anatusubiria nje, kwa hiyo hayo ni maelekezo ya Serikali yake kuhakikisha wapinzani wanakamatwa, wanadhalilika na mikutano inazuiliwa,’’ alisema. Pamoja na hali hiyo, alisema kwa sasa ahofii jambo lolote kwani unapokuwa katika mapambano ya kidemokrasi, kunyanyaswa na kudhalilishwa na vyombo vya dola ni jambo la kawaida, hasa katika mazingira ya sasa ya nchi. “Kila Mtanzania mwenye nia njema na mwenye akili timamu apaze sauti kupinga huu ujinga unaofanywa,’’ alisema.  MAJALIWA ATOA ONYO Wakati hayo yakiendelea, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali itawashughulikia watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi bila ya kujali nyadhifa zao. Amesema ni vema watu wakawa makini na kujiepusha kutoa matamshi ambayo yataathiri mfumo wa maisha kwa wananchi wengine. Hayo aliyasema jana wakati wa ibada ya mazishi ya Linah Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, iliyofanyika Kyela mkoani Mbeya. “Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo,” alisema. Aliwaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa na viongozi wake na kwamba Serikali inawategemea na iko pamoja nao. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Askofu wa Kanisa la Evarinjerical Brother Hood, Rabison Mwakanani kuonya vitendo vya baadhi ya watu kumtukana Rais Dk. John Magufuli. Alisema ni vema watu hao wakajifunza namna ya kuwasilisha hoja zao bila ya kutumia lugha za matusi. “Rais Dk. Magufuli amefanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya maendeleo. Wanaofanya hivyo wasidhani kama wanamtukana Rais tu, bali wanawatukana Watanzania wote waliomchagua wakiwemo viongozi wa dini,” alisema Askofu Mwakanani. MASHINJI, WENZAKE WASOMEWA MASHTAKA MAWILI Wakati huo huo, viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Katibu Mkuu, Dk. Vicent Mashinji, jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka mawili yanayowakabili. Viongozi hao, wamesomewa mashtaka yanayowakabili na Wakili wa Serikali Mwandamizi Mkoa wa Ruvuma, Renatus Mkude ambaye alikuwa akisaidiwa na Shaban Mwigole, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Simon Kobelo. Wakili Mkude, aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Cecil Mwambe (Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini ambaye pia ni Mbunge wa Ndanda mkoani Mtwara), Philberth Ngatunga (Katibu wa Kanda ya Kusini), Irineus Ngwatura (Mwenyekiti Mkoa wa Ruvuma) na Delphin Gazia (Katibu Mkoa wa Ruvuma). Wengine ni Zubeda Sakuru (Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma), Sanguru Manawa, (Katibu wa Oganaizesheni na Mafunzo), Curthberth Ngwata (Mwenyekiti Wilaya ya Nyasa) na Charles Makunguru (Katibu Mwenezi Wilaya ya Nyasa). Mkude alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa mawili. Kosa la kwanza wote kwa pamoja, wakiwa wilayani Nyasa tarehe isiyofahamika walikula njama ya kutenda kosa ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Alisema kosa la pili, inadaiwa Julai 15, mwaka huu katika mji wa Mbambabay,  washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio halali, ambao ungesababisha uvunjifu wa amani kwa jamii. Aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa. Washtakiwa wamekana mashtaka yote. Kwa upande wake, Hakimu Kobelo alisema dhamana ya washtakiwa iko wazi hivyo kila mmoja anapaswa kuwa na wadhamini ambao ni wakazi wa Songea mjini wanaotakiwa wapeleke uthibitisho kutoka kwa maofisa watendaji wa mitaa wanayoishi. Pia washtakiwa hao, wametakiwa kudhaminiwa kwa Sh milioni 2. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu  itakapotajwa tena. Wakati taratibu za kukamilisha dhamana zao zikiendelea, washtakiwa walirudishwa mahabusu kwa taratibu za kiusalama kutokana na kile kilichodaiwa kuwapo mkusanyiko wa watu hadi taratibu zitakapokamilika ambazo zinafanyiwa kazi na mawakili wa upande wa washtakiwa, Edison Mbogoro, Dickison Ndunguru na Banabasi Pomboma. Hata hivyo, viongozi hao jana wamelala gerezani kutokana na kushindwa kukamilisha dhamana. Akizungumzia hali hiyo, Wakili Mbogoro alisema Mashinji na wenzake wamefunguliwa kesi ya Jinai namba 173 ya 2017 na upande wa Jamhuri haukuwa na pingamizi juu ya dhamana. “Ilikuwa ni barua ya wadhamini wawili wawili ambao walikamilisha nyaraka zao, lakini mahakama iliomba kuzipitia ili kupata uhakiki wa nyaraka hizo. “Hadi sasa tulikuwa tumekaa tunasubiri nyaraka za wadhamini ziweze kuthibitishwa, lakini hadi sasa saa tisa sidhani kama litatekelezwa kwa leo kwa kuwa muda umeenda ni hadi hapo kesho,’’ alieleza Mbogoro. Naye wakili Pomboma alisema wameshangazwa na kilichotokea. Walimtafuta wakili wa Serikali na hakimu wakawa wanaondoka kwa kupishana katika eneo la mahakama. Alisema mazingira hayo ya kutokuwapo kwa watendaji ambao wamepewa dhamana, bado hayajawa ‘comfortable’ kwao na hawajui ni mazingira gani yamewafanya wasiwepo kiasi cha kwamba wateja wao wameshindwa kupata haki yao. Habari hii imeandaliwa na RAMADHAN HASSAN (DODOMA), ASHA BANI (DAR ES SALAAM) na NA AMON MTEGA (SONGEA)
kitaifa
Mweyekiti wa Klabu ya AICC, Adolf Olomi alisema kuwa bonanza hilo linalenga kuimarisha wachezaji na kuhamasisha watu wengi waweze kujitokeza kuupenda mchezo huo kama ilivyo soka.“Tayari tumepata udhamini kupitia kampuni ya Mzalendo Industies Ltd na wachezaji 18 watachuana vikali kwa kuonesha juhudi zao ili kuwa na klabu ambayo ina wachezaji wenye uwezo mzuri kwa ajili ya kujiweka tayari kwa michuano ya ndani na nje, ”alisema Olomi.Alisema mchezo huo kuwa na wachezaji wengi ni ngumu kutokana na kuhitaji gharama kubwa kwa wachezaji kuliko michezo mingine, huku akisema ndio sababu mchezo huo vijana wachache ndio wanashiriki.“Mpira mmoja wa mchezo wa Skwashi Sh 15,000 huku mavazi yake humgharimu mchezaji hadi Sh 80,000 na kila mchezaji lazima awe na vifaa vyake vya michezo mwenyewe, ” aliongeza.AICC Klabu inategemea kuendesha mashindano ya kila mwezi mara moja kwa kushirikisha baadhi ya klabu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Arusha zikiwepo klabu kutoka mkoa wa Dodoma , Mwanza, Kilimanjaro na TGT klabu -Arusha, na Gymkhana Klabu kutoka Arusha.
michezo
MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM BAADA ya kuchapwa mabao 2-1 na Simba katika mchezo wa mwisho wa kundi D, Kocha Mkuu wa AS Vita, Frolent Ibenge, amekiri wazi kuwa wapinzani wao walikuwa bora katika mechi hiyo ambayo walicheza vizuri na walistahili kushinda. AS Vita ilijikuta ikikumbana na kichapo hicho kulichowafanya kushindwa kutinga robo fainali, baada ya kumaliza mkiani mwa msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi saba katika michezo yake sita waliyocheza kwenye michuano hiyo. Licha ya AS Vita kuichapa Simba mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza  uliochezwa Januari 19, mwaka huu jijini Kinsasha, lakini walishindwa kufurukuta katika mchezo huo wa marudiano. Akizungumza baada ya mchezo huo, Ibenge alisema wapinzani wao walikuwa bora sana hasa katika kipindi cha pili cha mchezo huo, hivyo kikosi chake kilishindwa kuhimili vishindo hivyo na kupoteza mchezo huo. “Simba ni timu nzuri, ilicheza vizuri sana hasa kipindi cha pili, walikuwa na kasi mno, tulijitahidi kupambana nao lakini ilishindikana, tumepoteza mchezo huo na tulistahili kufungwa, wachezaji wangu walionyesha kupoteza umakini na kushindwa kuendana na kasi ya wapinzani wetu. “Bado nasisitiza kuwa Simba ni timu nzuri na itafanya vizuri sana huko mbeleni, ina wachezaji wazuri na wanajituma zaidi, hivyo wana nafasi nzuri ya kwenda mbali, mimi nawatakia kila la heri kuelekea kwenye michezo hiyo,” alisema Ibenge ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
michezo
UONGOZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wilayani Kibiti mkoa wa Pwani umetakiwa kuhakikisha kaya 420 za wakazi wa kata ya Ruaruke wanaunganishiwa umeme ndani ya kipindi cha miezi miwili. Agizo hilo lilitolewa katika kijiji cha Ruaruke na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata hiyo na kuzindua uwashaji umeme kwenye kijiji hicho kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) unaosimamiwa na Tanesco.Alisema wananchi hao wamesubiri huduma hiyo kwa muda mrefu tangu mwaka 2013 lakini kutokana na sababu mbalimbali ikashindikana. “Meneja hakikisha ndani ya miezi miwili kaya hizi 420 za awali zinaunganishiwa umeme kwa gharama ya Sh 27,000 tu na uwake kwani wamesubiri muda mrefu na hii itasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi,” alisema.Mgalu alisema tayari transfoma sita zimeshawekwa tangu wakati huo kwa ajili ya vijiji saba kwa akili ya kusambaza umeme umbali wa kilometa 10 na gharama iliyotumika ni Sh bilioni tano na kuwataka wananchi na hofu kwani watapata huduma hiyo ndani ya muda aliotoa. Katika hatua nyingine, naibu waziri huyo ameitaka Rea na Tanesco kuwadhibiti watu wanaojifanya wafanyakazi wa vitengo vya taasisi hizo (vishoka) ili wasikwamishe mradi wa kupeleka umeme vijijini.Alisema kuna baadhi ya watu wanajifanya wanatoka kwenye taasisi hizo wakidai wana uwezo wa kuwaunganishia umeme wananchi jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.
kitaifa
UDITH NYANGE NA CLARA MATIMO -MWANZA KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema taifa linakabiliwa na viashiria vya mpasuko na mmomonyoko wa msingi wa amani uliojengwa na viongozi waliotangulia. Alifafanua hoja hiyo kwa kusema hali hiyo inachochewa na kauli au matamko ya vitisho dhidi ya watu wanaotumia uhuru wao wa kutoa mawazo mbadala. Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, alisema hayo jana wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama chake. Kiongozi huyo alisema ufinyu wa demokrasia ni moja ya changamoto inayolikabili taifa kwa sasa. Alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya viongozi kuamini kuwa maendeleo yanakuja kwa kuminya uhuru wa watu, hususani viongozi wa vyama vya upinzani. Katika hoja hiyo, Zitto aliwataka wananchi kupaza sauti zao kwa kukemea udikteta kwa lengo la kuilinda amani iliyopo nchini. “Kauli na matamko ya vitisho na vitendo vya bughudha vimeshamiri kwa wale wanaotofautiana mtazamo na watawala. “Hii inaashiria mpasuko na mmomonyoko wa msingi wa amani uliojengwa na viongozi waliotangulia na kusababisha athari za uchumi pamoja na kukosekana kwa sauti mbadala ya kuleta marekebisho ya kisera,” alisema Zitto.   MDORORO WA UCHUMI Katika hatua nyingine, Zitto alielezea mdororo wa uchumi kwa kusema tayari nchi imeanza kuona madhara hasi ya kuminywa kwa demokrasia. Alisema mtazamo huo unatokana na vitendo vya kamatakamata ya viongozi wa vyama vya upinzani, ambao ni wawakilishi wa wananchi. Zitto alisema vitendo hivyo vimechangia kuporomoka kwa mshikamano uliokuwa umeanza kujengeka ndani ya nchi bila kujali itikadi za vyama. Alisema kuporomoka kwa mshikamano kumejenga chuki na matokeo yake hali hiyo imesababisha mdororo wa kiuchumi. “Mwaka 2016 kilimo cha mazao kilikua kwa asilimia 1.4 tu kutoka asilimia 2.2 mwaka 2015 na asilimia 4 ya miaka iliyopita. “Ukichukua kasi ya ongezeko la idadi ya watu Tanzania ya asilimia 2.8 kwa mwaka, maana yake ni kwamba mwaka 2016 Watanzania tuliongezeka maradufu na  wengi walidumbukia kwenye umasikini kuliko 2015. “Wakati Serikali inaimba viwanda, mauzo ya bidhaa kwenda nje ya nchi yetu yameshuka sana, Mei 2016 Tanzania iliuza nje bidhaa za viwanda zenye thamani ya dola bilioni 1.5, mwaka ulioishia Mei 2017 Tanzania imeuza nje bidhaa zenye  thamani ya dola bilioni 0.8 tu, anguko la mauzo ni takribani dola milioni 700, sawa na thamani ya ndege 23 za Bombadier Q 400,” alisema. Pia alisema uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umeongezeka kwa asilimia 14 ndani ya mwaka mmoja wa Mei 2016 hadi Mei 2017, kwamba Tanzania imetumia dola milioni 480 kuagiza sukari, nafaka na mafuta ya mawese kutoka nje ya nchi. Zitto ambaye alisema mauzo ya nje ya zao la pamba yameshuka kutoka dola milioni 52 kwa mwaka 2016 hadi dola milioni 42 Mei, mwaka huu na uagizaji wa malighafi umeporomoka kwa asilimia 25 ndani ya mwaka mmoja kati ya Mei 2016 na Mei mwaka huu. Alisema takwimu hizi chache zinaonyesha  hali ya nchi si imara na kuna hatari  Watanzania wengi wakatumbukia kwenye umasikini zaidi, hivyo alishauri ni vyema viongozi wakaacha vitisho kwa wote wanaotumia uhuru wao wa kutoa mawazo mbadala nchini, kuimarisha uhuru wa kidemokrasia bila kujali tofauti za kisiasa, kiuchumi, kidini na kikabila ili kulinda demokrasia na kusukuma mbele maendeleo. “Wananchi wenzangu, ni muhimu  kuendelea kupaza sauti kupinga kubanwa kwa demokrasia, hatupaswi kabisa kukaa kimya, huu ni wajibu wetu wa kizalendo, tusiwaachie nchi wahisani, tusiache kupaza sauti juu ya udikteta ili kulinda amani yetu. “Vyama vya upinzani vinaongoza halmashauri zaidi ya 35 nchini, kuzuia mikutano ya hadhara ni uvunjifu wa katiba, lakini pia ni kuondoa uwajibishaji, tunaongoza halmashauri hizo kutoka kwa CCM ambao ni wapinzani wetu katika maeneo hayo,” alisema Kabwe.
kitaifa
Mwandishi Wetu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba ametembelea Kampuni ya kutengeneza viatu ya BORA ikiwa ni hatua za awali katika kuingia ushirikiano. Katika ziara hiyo, Profesa Ndimba ameambatana na Mkurugenzi wa Kampasi ya DIT Mwanza, Dk Albert Mmari, na Mkuu wa Idara ya Mafunzo Viwandani Dk John Msumba. Timu hiyo kutoka DIT imepata nafasi ya kutembelea kiwanda hicho cha BORA kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho ambapo DIT Kampasi ya Mwanza inatoa mafunzo ya uchakataji ngozi ikiwa ni pamoja na utengenezaji viatu, itanufaika kwa wakufunzi wake kuongeza ujuzi na utaalamu kiwandani hapo na pia wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo katika kiwanda hicho na kwa upande wa kiwanda watanufaika kwa kupata wataalamu kutoka DIT. Kwa mujibu wa Profesa Ndomba, DIT kupitia kampasi ya Mwanza inalenga kuwa kituo cha umahiri katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi na teknolojia zake ambapo Mkurugenzi Mkuu wa BORA, Rajesh Sajinan aliahidi kushirikiana na DIT ili kupata wataalamu.  Makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo yatatiwa saini hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu muhimu za kiutendaji.
kitaifa
SAO PAULO, BRAZIL NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid na AC Milan, Ricardo dos Santos ‘Kaka’, ametangaza rasmi kustaafu soka huku akiwa na umri wa miaka 35. Mchezaji huyo ambaye alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, amestaafu soka akiwa anaitumikia klabu ya Sao Paulo ya nchini Brazili, ambapo alikuwa anacheza kwa mkopo akitokea klabu ya Orland City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani. Nyota huyo wa Brazili mara ya mwisho kucheza soka katika klabu yake ilikuwa Oktoba mwaka huu, huku timu yao ikikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Colombus Crew, hivyo aliamua kuweka wazi kuwa muda wake umefika wa kustaafu soka. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Kaka aliamua kuwaaga mashabiki zake huku akisema ni maamuzi sahihi kwa upande wake. “Baba, ninaweza kusema maisha yangu sasa ni zaidi ya vile ambavyo nilikuwa nafikiria, naomba maisha yangu yawe chini ya Yesu. “Nakushukuru sana kwa kunifanya niwe hapa, safari yangu ilikuwa ndefu na sasa nipo tayari kwa safari nyingine ya maisha yangu. Kwa jina la Yesu. Amen,” aliandika Kaka. Mchezaji huyo alianza kuonesha ubora wake kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2002 ambapo walifanikiwa kulitwaa akiwa na kikosi chake cha Brazili, baada ya hapo klabu mbalimbali barani Ulaya zikawa zinagombania saini yake kuanzia mwaka 2003 AC Milan walifanikiwa kumsajili nyota huyo. Mbali na kutwaa Kombe la Dunia, lakini alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Italia msimu wa 2003/2004, Italian Super Cup 2004/05, Confederations Cup 2005 na 2009, Ligi ya Mabingwa 2006/07, UEFA Super Cup 2007/08, Spanish Cup 2010/11, Ligi Kuu Hispania, 2011/12. Amewahi kuchukua tuzo mbalimbali ikiwa pamoja na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2006/07, mchezaji bora wa mwaka nchini Italia, 2004 na 2007, mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya wa UEFA 2007 na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA Ballon d’Or 2007. Mchezaji huyo aliongeza kwa kusema lengo la kustaafu soka ni kuwapisha vijana wenye damu changa waweze kutumia nafasi hiyo na kuonesha vipaji vyao kwa ajili ya kupigania Taifa pamoja na klabu zao kwenye michuano mbalimbali duniani.
michezo
Na Erick Kamugisha-DAR ES SALAAM  UPANDE  wa Jamhuri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es salaam umesema jarada la kesi inayowakabili wanakwaya wa Kanisa la Sabato, Kinondoni (SDA) dhidi ya uongozi wa kanisa hilo, limepelekwa kwa hakimu mfawidhi kwa ajili ya  kupanga hakimu wa kutoa usuluhisho. Hakimu Esther Mwakalinga alitoa uamuzi wa kufunga jarada na kupelekwa kwa hakimu mfawidhi, wakati kesi hiyo itapokuja kwa kutajwa tena tarehe husika. “Jarada la kesi hili,litapelekwa kwa hakimu mfawidhi kwa ajili ya kuteua hakimu mwingine wa kuendesha kesi hii na kutoa suluhisho Desemba 27, mwaka huu”,alisema Hakimu Mwakalinga. Katika kesi ya msingi, wanakwaya wa Kanisa la Sabato, Barnas Katikiro na David Maiba wameishtaki bodi ya wadhamini na Mchungaji wa Kanisa hilo, Masunya Antory na Joseph Mgwabi. Wanakwaya hao, walilalamika kwa uongozi wa kanisa hilo wamewatumia waimbaji wengine kufanya mkanda wa video ,wakati watu hao hawakuingiza sauti katika mkanda huo. Pia wanalalamikia kuwapo mkanganyiko wa Katiba ya kwaya na kudai  mahakama ina mamlaka ya kudhibitisha kuwapo jambo hilo. Kutokana na malalamiko hayo, walifungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni dhidi ya viongozi wa kanisa hilo, hata hivyo viongozi hao waliweka pingamizi lenye hoja tatu zilizotaka kesi  itupuliwe mbali. Novemba 27, mwaka huu pingamizi hilo lilisikilizwa na mahakama na kulitupiliwa mbali na kupanga kesi hiyo kusikilizwa na  kutoa usuluhisho Desemba 27, mwaka huu.
kitaifa
TANZANIA jana ilifuzu hatua ya makundi ya mbio za kusaka nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia 2022 Qatar baada ya kuichapa Burundi kwa penalti 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam. Hatua hiyo ya kupigia mikwaju mitano kwa mi tano ya penalti ilikuja baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 za kawaida zikiwa sare ya 1-1 na baadae kuendelea na sare hiyo hata baada ya kuongezwa dakika 30 na hivyo kufanya mchezo huo kuchezwa kwa dakika 120. Mashujaa wa Taifa Stars walikuwa Juma Kaseja (Tanzania One) baada ya kuokoa penalti ya kwanza ya Burundi, Erasto Nyoni, Himid Mao na Gadiel Michael waliofunga penalti zao na kuiwezesha Taifa Stars kupiga hatua moja mbele kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.Burundi wenyewe walikosa penalti zao tatu, ambazo zilipigwa na Ngado Omary, Berahino Saido na Bigirmana Gael. Katika dakika 90 za kawaida, Taifa Stars ilipata bao la kuongoza kupitia kwa nahoha wake, Mbwana Samatta katika dakika ya 29 akiusukuma kwa tumbo mpira wa kona uliochongwa na Mohamed Hussein kutokea upande wa kulia.Kaseja akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo alisema kikubwa watanzania wanatakiwa kuwa na mshikamabo mkubwa ili kuendelea kufanya vizuri na kutokuwepo kwake katika timu ya taifa kwa mrefu sio kama alishuka viwango, ila ni mpango wa makocha waliokuwepo.Taifa Stars sasa inasubiri kupangwa katika makundi na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) ili kujua wataangukia katika kundi gani na wapinzani gani katika mbio hizo za kusaka tiketi ya kwenda Qatar 2022.Tanzania sasa itaungana na timu zingine 14 zilizofuzu baada ya kupata ushindi wa jumla kutoka katika mechi mbili walizocheza na kuungana na zingine 26 ambazo ziko katika nafasi ya juu na hazikucheza raundi hiyo ya awali ili kutimiza timu 40, zitakazopangwa katika makundi 10, katika hatua ya pili ya kufuzu. Dakika ya 40 Burundi walilisakama lango la Stars baada ya mshamnbuliaji wao kupokea pasi baada ya Kelvin Yondan kukosea kuokoa kutokana na walinzi wa Stars kujichanganya.Dakika 45, Burundi walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Abdul Fiston kwa mkwaju hafifu baada ya walinzi wa Taifa Stars kujichanganya baada ya kushindwa kuondosha hatari.Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika, timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1. Dakika ya 57 Samatta nusura afunge licha ya kuwa katika nafasi nzuri, alipiga shuti kubwa juu ya lango la Burundi.Dakika ya 75 Idd Seleman Nado nusura afunge baada ya Gadiel Michael kufanya kazi kubwa ya kuwatoka wachezaji kadhaa wa Burundi na kutoa pasi kwa Nado, aliyepiga mpira nje.Kikosi cha Taifa Stars: Juma Kaseja, Hamis Ramadhani, Mohamed HusseinGadiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Gerald Mkude, Idd Seleman, Aboubakar Salum/ Shaban Idd, Mbwana Samatta/Himid Mao na Hassan Dilunga/Farida Mussa.
michezo
Editha Karlo, Kigoma Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepiga marufuku Vituo vya Afya, zahanati na Hospitali za Serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo leo mjini Kigoma wakati alipotembelea Zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma kuangalia hali ya matibabu dhidi ya malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya malaria duniani. “Nawaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuweka matangazo yanayoonyesha kipimo cha haraka cha malaria, dawa mseto za kutibu malaria kali ni bure kwenye kila vituo vya kutolea huduma za afya za Serikali. “Endapo mtoa huduma yeyote atamtoza mwananchi malipo  ya matibabu na vipimo vya malaria hatua stahiki itachukuliwa bila kumuonea huruma,” amesema. Pamoja na mambo mengine, Waziri Ummy amewataka waganga wakuu wa vituo kwa ngazi ya zahanati na waganga wakuu wa wilaya kuweka namba zao za simu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia wananchi kutoa malalamiko yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo hazikidhi viwango ili kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.
afya
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imejipanga kuendeleza bandari kiushoroba kuongeza ufanisi wa huduma na kuzisogeza karibu zaidi na wateja.Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema, ili kuweza kupata manufaa hayo, bandari hizo hazina budi kwenda sambamba na maendeleo ya ushoroba ndani ya nchi na kieneo.Amesema kwa upande wa ushoroba wa Kati Kaskazini (Mwanza), imelenga uboreshaji wa bandari ya ziwa Victoria na ujenzi wa bandari kavu ya Fela- Mwanza na utasogeza huduma za bandari kwa wateja wa Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Uganda na Sudan Kusini.Aidha alisema kwa upande wa Kati- Kaskazini-Magharibi inayohusisha Isaka- Kibanga/Rusumo, wataboresha bandari kavu ya Isaka kwa kushirikiana na TRC ambapo kwa pamoja kutarahisisha usafirishaji wa shehena ya bandari kwenda na kutoka nchi za Rwanda na Burundi.“Sambamba na juhudi hizi ni mpango wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali…Pia uboreshaji na ujenzi wa bandari za Ziwa Tanganyika na Bandari Kavu ya Katosho-Kigoma utasogeza huduma za bandari kwa wateja wa magharibi mwa Tanzania na nchi jirani za Burundi na DRC,” alisema.Amesema TPA inashirikiana na TAZARA ili kuhakikisha huduma za reli ya TAZARA zinarejea angalau kwa kiwango cha kuridhisha ili kuhudumia wateja wa Kusini Magharibi mwa Tanzania, sambamba na mpango wa kujenga bandari Kavu ya Inyala-Mbeya ili kuhudumia shehena inayokwenda nchi jirani za DRC, Malawi na Zambia.“Kwa upande wa ushoroba wa bandari ya Tanga, tunaendelea na uboreshaji ikiwa ni pamoja na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa namna bora ya kuongeza kina cha bandari ya Tanga,” amesema.Amesema ili kusogeza karibu huduma za shehena kwa wateja wa ushoroba wa Tanga, TPA imebainisha eneo karibu na Arusha ili kwa na bandari kavu itakayotoa huduma za bandari ikiwa ni pamoja na kuhimili ushindani kutoka bandari ya nchi jirani.“Ushoroba wa Tanga utaimarika zaidi kama reli ya Tanga-Arusha-Musoma itajengwa ili kuhudumia wateja wan chi jirani za Uganda na Sudan Kusini,” amesema.Aidha amesema hivi sasa wanaendelea na maboresho ya bandari ya Mtwara ili pamoja na juhudi za wadau wengine, ushoroba huo uwe na uwezo wa kuhudumia wateja wa kusini mwa Tanzania na kuhimili ushindani kutoka bandari za nchi jirani za Afrika Kusini, Msumbiji na Namibia.
uchumi
Okwi amefikia hatua ya kusema hivyo baada ya kutapakaa habari kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juzi kwamba amerudi Yanga. Mchezaji huyo kwa sasa yupo kwao Uganda kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na kuisaidia Simba kumaliza nafasi ya tatu.Hata hivyo tetesi hizo zilikanushwa na viongozi wa Simba na wa Yanga pia wakisema hawana mpango wa kumsajili mchezaji huyo. “Hizo taarifa za Yanga kumsajili Okwi hazina ukweli wowote,” alisema ofisa habari wa Yanga Jerry Muro.“Hayo mambo ya porojo bwana, Okwi ni mchezaji wetu halali hawezi kwenda Yanga, yupo Uganda kwenye mapumziko,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zakaria Hanspope.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana Okwi alisema: “Mimi nina akili zangu timamu, siwezi kurudi Yanga kule nilishamalizana nao na sasa mimi ni mchezaji halali wa Simba, nina mkataba nao na ninauheshimu,” alisema. Aidha mchezaji huyo alisema hafikirii kuondoka Simba kwani amejiona ni mwenye bahati na klabu hiyo.Akizungumzia mwenendo wa Simba msimu uliopita Okwi alisema kilichotokea kwa timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu ni suala la soka na ana imani itafanya vizuri msimu ujao.“Nafasi ya tatu sio mbaya, lakini hiyo ndio soka, kutokuchukua ubingwa ni mambo ya soka, timu yangu inafanya usajili kwa sasa naamini ni usajili mzuri utakaotufanya tufanye vizuri msimu ujao,” alisema Okwi. Okwi alisajiliwa tena na Simba Agosti mwaka jana akitokea Yanga aliyojiunga nayo akitokea SC Villa ya Uganda.Villa ilimtumia Okwi na Fifa baada ya mchezaji huyo kuingia kwenye na Etoile du Sahel ya Tunisia aliyojiunga nayo badaa ya kuuzwa na Simba, alijiunga na Etoile kwa dola za Marekani 300,000 mwanzoni mwa mwaka 2014 kabla ya kurudi Uganda baada ya kukorofishana na klabu hiyo ya Tunisia na ndipo alipojiunga Villa kwa mkopo kabla ya kusajiliwa na Yanga na baadaye kurudi Simba.
michezo
    Na FREDY AZZAH-DODOMA WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, leo anatarajiwa kuwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Serikali ya takribani Sh trilioni 31.6, ambayo itatoa dira ya mpango wa Serikali kwa mwaka ujao wa fedha – 2017/18. Wakati hilo likisubiriwa kwenye bajeti hiyo inayotegemea takribani asilimia 60 ya mapato ya ndani na 40 ya nje, baadhi ya wabunge wameeleza matarajio yao ni kuona Serikali inaweka vipaumbele kwenye miundombinu, afya, maji na elimu. Baada ya kusomwa kwa bajeti hiyo, baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuliwa wakati wa mjadala, ni pamoja na deni la taifa ambalo limeongezeka kwa kasi siku za usoni, misamaha ya kodi hasa kwenye sekta ya madini, upanuzi wa vyanzo vya kodi na hazina kutotoa fedha zinazotengwa kwa wizara mbalimbali. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2015/16 hadi Juni 2016, deni la taifa lilifikia Sh trilioni 41 ikilinganishwa na Sh trilioni 33 za deni hilo Juni 2015. Ripoti hiyo inasema kiasi cha deni hilo la Juni 2016, hakijajumuisha Sh trilioni nane ambalo ni deni katika hifadhi za jamii. “Deni la taifa linakua kwa kasi, zaidi ya 20% ikimaanisha baada ya miaka mitano litakuwa mara mbili. Si vizuri deni kukua kwa namna hii,” inasema ripoti hiyo ya CAG. Kwa mwaka ujao wa fedha, Serikali inatarajia kutumia Sh trilioni tisa kulipa deni la taifa lililoiva. Kwa upande wa misamaha ya kodi ambayo pia inatarajiwa kutawala mjadala huo, ripoti ya CAG inaonyesha hadi Mei 2016 ilibaini kuwapo kwa matumizi mabaya ya msamaha wa kodi wa Sh bilioni 3.46 ambao ulitolewa kwa walengwa wawili walioagiza magari 238.
kitaifa
MRADI wa Kukarabati na Kuimarisha Mifumo ya Umeme (REDAP) umewezesha Tanzania kuachana na umeme kutoka Kenya kwa matumizi Wilaya ya Longido mkoani Arusha. TEDAP ni mradi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na umetekelezwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam.Kwa Arusha na Kilimanjaro, mradi umejenga na kukarabati vituo vinane vya umeme kwa gharama ya Dola za Marekani 13,083,948.07. Akizungumza na wahariri waliotembelea vituo hivyo vya umeme jana jijini Arusha, Meneja Mwandamizi wa Miradi wa Tanesco, Emmanuel Manirabona alisema TEDAP umesaidia kuwapo umeme wa uhakika na wa kutosha mikoa hiyo.Alivitaja vituo vya Arusha vilivyojengwa na kukarabatiwa kuwa ni Njiro B, Kiltex, Sakina, Themi, Unga Limited, na Mount Meru. Alisema ujenzi wa kituo kipya cha Sakina umewezesha Wilaya ya Longido kupata umeme wa uhakika Gridi ya Taifa na kuachana na umeme wa Kenya uliokuwa ghali, usioaminika. “Kwa sasa watu wa Longido wanapata umeme kutoka katika kituo hiki cha Sakina. Hii ni faida ya mradi wa TEDAP,” alisema Manirabona. Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Herini Mhina alisema Longido imeanza kupata umeme huo tangu kukamilika kituo cha Sakina mwaka juzi. Mhina alisema mahitaji ya umeme Longido ni megawati moja na kuna wateja 2,893 waliounganishwa na huduma ya umeme.Mhandisi Mkuu Usambazaji Umeme Tanesco Arusha, Donasiano Shamba alisema vituo hivyo sita vimesaidia mkoa kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika, huku kukiongezeka laini nyingi zaidi za kupeleka umeme kwa wateja. Alitoa mfano wa faida za ujenzi huo kuwa ni viwanda kupata umeme kikiwamo Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) ambacho kina laini yake pekee ya megawati 2.5 kutoka kituo cha Kiltex.Shamba alisema vituo vingi ya hivyo vina umeme wa ziada na ndio maana mkoa huo unawaalika wawekezaji katika sekta ya viwanda kwani wana umeme wa ziada na wa kuaminika. Kwa Kilimanjaro, vituo vya mradi wa TEDAP ni viwili wakati Dar es Salaam kumejengwa vituo vipya na kukarabtiwa Kurasini, Gongolamboto na Mbagala kilichowezesha mikoa ya Kusini kupata umeme Gridi ya Taifa. Mbali ya hivyo, vituo vingine ni City Centre, Mburahati, Mikocheni, Oysterbay, Ubungo, Chang’ombe na Kariakoo, vyote vya mkoa huo vikigharimu Dola za Marekani milioni 20.83.
kitaifa
WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji imeunda Tume kuchunguza ajali ya meli ya mafuta ya Mt Ukombozi iliyotokea miezi miwili iliyopita katika Bandari ya Wesha Pemba na kuua wafanyakazi wake watatu.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohamed Ahmada wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kufahamu tume iliyoundwa wajumbe wake na majukumu yake kwa ujumla.Ahmada alisema ni kweli serikali imeunda tume ya kuchunguza kuungua kwa meli ya mafuta ya MT Ukombozi ambayo ilisababisha vifo vya mabaharia watatu. Alisema uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kujitokeza kwa hitilafu za umeme na mlipuko wa gesi.“Huo ni uchunguzi wa awali katika tukio la mripuko wa meli ya Mt Ukombozi.....sasa tumeunda tume rasmi kujuwa chanzo cha ajali hiyo,” alisema Naibu Waziri.Aliwataja wajumbe wa tume hiyo ni Jaji Shaaban Ramadhan Abdalla, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyefahamika kwa jina moja la Fatuma, Kepteni Makame Hassan Ameir wa Shirika la Bandari la Zanzibar na Abdalla Kombo ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini.Katika timu ya uchunguzi wapo, wajumbe wataalamu kutoka Tanzania Bara kutoka taasisi za vyombo vya baharini na meli. Ahmada alisema tume hiyo inatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha taarifa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.“Kazi ya uchunguzi wa kitaalamu imeanza ikiwahusisha wajumbe kutoka Zanzibar pamoja na wenzetu kutoka Tanzania Bara.....tunatarajia kuchukuwa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo na taarifa yake itatangazwa kwa wananchi,” alisema Ahmada.Meli ya Mt Ukombozi iliungua moto huko katika Bandari ya Wesha Pemba baada ya kujitokeza hitilafu za umeme huku wafanyakazi wa meli hiyo wakiwa katika harakati za usafi katika sehemu ya moja ya chumba cha injini.Ajali hiyo ilisababisha kujeruhiwa vibaya kwa mabaharia wake watatu kwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na baadaye kufariki. Waliokufa ni Ali Juma (54), Hafidh Silima Kona (25) na Issa Daud Omar (30).
kitaifa
    CHRISTINA GAULUHANGA NA SAID ABDALLAH (OUT) BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Ilala limesema licha ya kupokwa vyanzo vya mapato, limefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo ya mapato walilojiwekea katika mwaka 2016/17. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam, katika kikao cha Baraza la Madiwani wa manispaa hiyo na Naibu Meya, Omary Kumbilamoto (CUF). Alisema walipanga kukusanya Sh bilioni 13.5 kwa mwaka ambako hadi sasa katika robo nne ya mwaka wamekusanya tayari Sh bilioni zaidi ya 13.5. “Mbali ya kupitia changamoto za watumishi hewa, vyeti feki, kupokonywa ukusanyaji kodi za majengo, tumeathirika katika utendaji na uchumi kuyumba, lakini hata hivyo tumejitahidi kuvuka lengo,” alisema Kumbilamoto. Alisema hali ngumu ya uchumi imepunguza kasi ya ongezeko la biashara mpya na kusababisha biashara nyingi kufungwa na kuhama. Kumbilamoto alisema ucheleweshaji wa ruzuku kutoka serikalini nayo ni sababu kubwa ya manispaa kushindwa kutekeleza baadhi ya miradi kwa wakati. Alisema hata hivyo, halmashauri na madiwani wanatakiwa kuibua vyanzo vipya vya mapato kuifanya manispaa hiyo kuwa endelevu. Meya wa Manispaa ya Ilala (Chadema), Charles Kuyeko, alisema bado kuna upungufu wa madawati katika shule za msingi za manispaa hiyo, kwa sababu ya ongezeko la wanafunzi wanaohamia. “Ongezeko la ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa linasababisha pia uhaba wa madawati,” alisema Kuyeko.
kitaifa
kutangazwa kuwa mshindi, Arusha jana. ABRAHAMU GWANDU NA ELIYA MBONEA-ARUSHA WAKILI machachari, Tundu Lissu, amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliofanyika mkoani hapa jana. Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), sasa ataiongoza TLS kwa muda wa mwaka mmoja. Ushindi wa Lissu unatajwa kuchagizwa na mambo mengi, huku makubwa kati ya hayo yakitajwa kuwa ni kauli ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa Februari 2, mwaka huu akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, pale aliposema TLS imeshakuwa kama chama cha siasa baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa mgombea wa nafasi ya urais ambaye ni mwanasiasa na kutokana na hilo hawezi kuwateua majaji kutoka ndani ya chama hicho. Kutokana na kauli hiyo, Lissu aliibuka na kusema hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya msingi iliyomsukuma kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo. Jambo jingine linalotajwa, ni kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyoitoa Februari 15, mwaka huu mjini Dodoma, pale aliposema kwamba Serikali haiwezi kuona TLS inajiingiza katika siasa na kama watataka hivyo, hatosita kuifuta Sheria ya TLS sura ya 307 iliyosababisha kuanzishwa kwa chama hicho. Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo mjini Dodoma alipozungumza na wanachama wa TLS wakiongozwa na aliyekuwa Rais wao, John Seka, walipomtembelea ofisini kwake. Alisema kitendo cha kuwaingiza wanachama wanasiasa au viongozi wa vyama vya siasa ni kuruhusu mgongano wa masilahi. Jambo jingine linalotajwa ni kitendo cha Lissu kukamatwa Februari 6, mwaka huu mjini Dodoma akiwa anahudhuria vikao vya Bunge kwa maagizo ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na ilidaiwa alikamatwa ili achelewe kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo. Kitendo cha mawakili Godfrey Wasonga na Onesmo Mpinzile ambao ni wanachama wa TLS, kufungua kesi Dar es Salaam na Dodoma wakipinga uchaguzi huo, ambazo hata hivyo zilitupwa ni sababu nyingine inayotajwa kuchangia ushindi wa Lissu. Si hilo tu, pia jambo jingine linalotajwa kusababisha ushindi wake ni kitendo cha Lissu kukamatwa Machi 16, mwaka huu nyumbani kwake mjini Dodoma akiwa anajiandaa kwenda Arusha na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kosa la kutotii sheria na juzi kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alikosomewa mashitaka matano ikiwamo kutoa maneno ya uchochezi yenye hisia za kidini. Lissu alifikishwa mahakamani hapo, ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi huo kufanyika jana na kulikuwa na taarifa kwamba pengine asingeweza kushiriki, lakini baadaye taarifa zilisema taratibu na kanuni za TLS zinaruhusu mgombea kuchaguliwa hata kama hatokuwapo katika ukumbi wa kupigia kura.       Baada ya kuachiwa kwa dhamana Lissu alisafiri kwa ndege ya kukodi na kuwasili Arusha jioni na kwenda moja kwa moja Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) ambako alisababisha wajumbe wa mkutano huo kulipuka kwa shangwe wakimshangilia huku wakimwita ‘jembe’, hali iliyomlazimu Seka kuwatuliza kwa kuwaambia kitendo hicho kitawakatisha tamaa wagombea wengine.   MATOKEO YA UCHAGUZI Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika Ukumbi wa Simba uliopo AICC, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Dk. Kibuta Omung’wana, alisema idadi ya wajumbe waliojisajili walikuwa 3,556 na kati yao waliohudhuria ni 2,560 huku waliopiga kura ni 1,682 – zaidi ya nusu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo. Kwa mujibu wa Dk. Omung’wana, nafasi ya urais iligombewa na wajumbe watano ambao ni Victoria Mandari, Godwin Mwaipongo, Fransis Stolla, Lawrence Masha na Lissu. Licha jina la Masha kujitokeza katika karatasi ya wagombea. lakini wajumbe hawakumpigia kura baada ya kujitoa wakati akiomba kura. “Naomba nianze kutangaza matokeo nafasi ya rais, Mwapongo amepata kura 23, Mandari amepata kura 176, Stola amepata kura 64 na Lissu amepata kura 1,411. “Hivyo namtangaza Lissu kuwa ndiye mshindi katika nafasi ya Rais wa TLS,” alisema Dk. Omung’wana. Pia alisema mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais ni Godwin Ngwilimi aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanesco kabla kufukuzwa baada ya yeye mwenyewe kudai kupinga sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow. Alipata kura 1,269 na Wakili Mary Mwasongwe kura 414. Wajumbe waliochaguliwa ni Lambaji Madai, Jeremia Mtobesi, Aisha Sinda, Steven Aweso, Husein Mtobwa, Goodluck Walter na Madeline Kimei. MWELEKEO MPYA TLS Akizungumza baada ya kuapishwa, Lissu alisema chini ya uongozi wake itakuwa ni mwisho kwa chombo au mtu yeyote kukitishia chama hicho. “Ni sisi wenyewe tulioruhusu Serikali ituingilie, iwe ni mwisho. hivyo tuanze mwanzo mpya na turuhusu siku mpya ije.  “Iwe mwisho sasa kwa chama hiki kutishwa na mtu au chombo chochote, iwe mwisho kwa mawakili kutishwa na kukamatwa ovyo, iwe mwisho kwa mahakimu na majaji kupokea maelekezo. “Mimi ni mwanachama wa Chadema ni kiongozi, ni mbunge, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzai Bungeni, nawahakikishia sitaileta Chadema ndani ya TLS na sitaipeleka TLS ndani ya Chadema. “Sijagombea kama mwanachama wa Chadema bali nimegombea kama mwanachama wa TLS aliye ndani ya Chadema,” alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki. Akizungumzia uchaguzi huo, Wakili James Marenga, alisema umefanyika kwa uhuru, haki, uwazi na kwa kutumia kanuni zote za uchaguzi wa TLS za mwaka 2016. Marenga alisema uchaguzi huo umeonyesha ni jinsi gani mawakili wanataka kuona mabadiliko ndani ya TLS itakayokuwa na uwezo wa kutoa maoni juu ya utawala wa sheria na masuala ya haki za binadamu. LOWASSA  Naye Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amempongeza Lissu kwa ushindi mkubwa alioupata. Lowassa alisema ushindi wa Lissu ni joto la moto mkubwa wa mabadiliko uliotuama ndani ya mioyo ya Watanzania.  “Uchaguzi ule naweza kusema ulikuwa kama kura ya maoni kwa wanasheria dhidi ya Serikali jinsi inavyoheshimu demokrasia ya umma na utawala wa sheria,’’ alisema Lowassa. PROFESA MKUMBO Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo, akizungumza na MTANZANIA Jumapili kwa simu jana, alimpongeza Lissu kwa kushinda nafasi hiyo na alisisitiza kuwa ushindi wake umechangiwa na Serikali iliyokuwa ikimfanyia kampeni.  “Ushindi wake ulitarajiwa, ulifanyiwa kampeni na Serikali, tunampongeza na tunawapongeza wanasheria kwa weledi katika kusimamia taaluma na kuonyesha wanaweza kufanya uamuzi wao binafsi bila kujali mashinikizo ya viongozi,” alisema Profesa Mkumbo. Pia alisema wanasheria wameonyesha utashi wa kitaaluma jambo ambalo ni la kishujaa na endapo  matokeo yangempa ushindi mtu tofauti na Lissu yangeleta  picha mbaya katika jamii. RIPOTI YA FEDHA Pia mkutano huo umetishia kuuburuza mahakamani uongozi unaomaliza muda wake kutokana na kunusa harufu ya ufisadi wa Sh milioni 78 za ada na Sh milioni 34 zilizokosa viambatanisho katika taarifa ya fedha ya mwaka 2015/2016. Kutokana na kuibuka kwa mjadala mzito juu ya fedha hizo kwa zaidi ya saa tatu bila kufikia makubaliano, ndipo waliamua kuunda kamati ya watu watano itakayoshirikiana na uongozi mpya kuchunguza tuhuma za ufisadi huo. Katika mkutano huo uliokuwa ukiongozwa na Seka, uliwasukuma wajumbe kutoa hoja mbalimbali zilizolenga kujua juu ya fedha zao wanazochanga kupitia ada za uanachama, baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa mbele yao huku ikiwa imeonyesha makosa ya kiuhasibu. Wajumbe watano wa kamati itakayoshughulikia kuchunguza tuhuma hizo ikishirikiana na uongozi mpya inaudwa na Rweikiza Rweikama, Lawrance Masha, Nicholaus Duhia, Magdalena Sylvester na Ana Julia.
kitaifa
NA SHOMARI BINDA-RORYA WAZEE wa Wilaya ya Rorya mkoani Tarime, wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na vijana kwa kuchukua hatua ya kuwachapa viboko kwa kile kinachodaiwa kuendeleza mila potofu ambazo pia zimekuwa zikiwadhalilisha na kuendeleza ukatili. Wakizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na shirika la Masister wa Moyo Safi wa Maria Afrika na kuwashirikisha wazee wa mila wa wilaya hiyo katika kampeni ya kupambana na ukatili wa kijinsia, walisema maadili kwenye jamii yamepungua na ndiyo kunapelekea kuendelea kwa vitendo vya ukatili. Walisema si wanawake pekee wanaofanyiwa ukatili bali hata wazee pia wamekuwa wakifanyiwa hivyo kwa kuendeleza mila za kuwachapa viboko pale wanapodaiwa kutenda kosa jambo ambalo wamedai linawadhalilisha na ni moja ya ukatili wanaofanyiwa. Mmoja wa wazee hao aliyejitamulisha kwa jina la Andrecus Nyazam wa Kijiji cha Kwibuse, alisema zipo taratibu za kufuata pale mtu anapokuwa amekosa kwenye jamii lakini si vijana kuchukua hatua ya kuwachapa wazee viboko. Alisema mila hiyo ni ya ukatili sawa na ule ambao wamekuwa wakifanyiwa wanawake kwenye jamii na kudai elimu bado inapaswa kuendelea kutolewa zaidi ili kuachana na mila ambazo zimekuwa kikwazo. “Tunashukuru kwa semina hii ambayo tumeshirikishwa ili kwa pamoja tuweze kuimarisha haki za wanawake walioathiriwa na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yetu lakini na sisi wazee tumekuwa na kilio chetu cha kudhalilishwa na kufanyiwa ukatili na vijana kwa kuchapwa viboko. “Tunakwenda kutoa elimu kwa jamii juu ya kuachana na vitendo vya ukatili kwenye jamii zetu tunaomba pia sauti zisikike za kukemea mila zisizofaa ambazo kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha ukatili unaokuwa unatendeka,”alisema. Mratibu wa mradi wa kuimarisha haki za wanawake walioathiriwa na ukatili wa kijinsia unaotekelezwa kwenye Kata 13 za Wilaya ya Rorya, Nollasko Mgimba, alisema jamii inapaswa kuweka mpango wa kutokomeza mila ambazo hazifai kwenye jamii. “Pamoja na ukweli kwamba mila zina umuhimu wake mkubwa katika jamii, lakini tunapaswa kubadilika na kuachana na mila zisizofaa kulingana na maendeleo ya kijamii hasa katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” alisema. Mwisho
kitaifa
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatarajia kuhudumia tani 14,374,400 yakiwemo makontena (TEUs) 208,000 katika vitengo vinavyoendeshwa na mamlaka hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.Kitengo cha Kontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) pia kinatarajia kuhudumia makontena (TEUs) 489,300 katika mwaka huo wa fedha.Mkurugenzi Mkuu wa (TPA), Deusdedit Kakoko amesema hayo Dar es Salaam wakati akielezea mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ya mamlaka hiyo."Tunatarajia kukusanya mapato ya jumla ya Sh bilioni 1,012.586, matumizi ni Sh bilioni 778.297 na kupata ziada ya Sh bilioni 234.289," amesema.Pia alisema wanatarajia kuhudumia meli 2,736 zenye ukubwa wa (GRT) milioni 35.880 na kati ya hizo meli 1,307 ni za Kimataifa (Deep Sea), meli 786 ni za mwambao na meli 670 zitahudumiwa katika bandari za Maziwa.Kakoko alisema, wataimarisha mfumo na kuongeza matumizi ya Tehama kwa malipo kwa kutumia mtandao (e-payment) na kukamilisha mradi na kutumia mfumo mpya wa 'Enterprise Resource Planning'(ERP) katika kutoa huduma na ukusanyaji wa mapato.Aidha amesema watakusanya mapato kwa wakati na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na kukusanya kwa kupitia benki sambamba na kuzingatia matumizi ya 'flow meters' na skana katika kuhakikisha shehena ya mafuta na shehena kwenye kontena."Tumejiwekea mikakati ya kuvutia shehena kwa kuboresha huduma za mamlaka kwa kutekeleza miradi mbalimbali kwa wakati uliopangwa sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama katika bandari za Mamlaka," amesema.
uchumi
BRISBANE, AUSTRALIA BINGWA wa ngumi uzito wa juu duniani, Manny Pacquiao, raia wa Ufilipino, amekubali kichapo kutoka kwa mpinzani wake, Jeff Horn wa nchini Australia, kwenye ukumbi wa Suncorp Stadium, mjini Brisbane jana. Katika pambano hilo, Pacquiao alikuwa anatetea ubingwa wa WBO, likiwa la raundi 12, lakini bingwa huyo alishindwa kuonesha uwezo wake na kuwapa mashabiki wasiwasi kwa kipindi kijacho. Mashabiki wengi kutoka nchini Ufilipino walijitokeza kwa wingi, huku wakiamini bingwa wao anaweza kufanya maajabu mbele ya watazamaji 50,000 ambao walijitokeza kushuhudia pambano hilo. Ushindani ulikuwa wa hali ya juu, ambapo kila mmoja alikuwa anafanya shambulizi la kushtukiza kwa mpinzani wake na hatimaye Pacquiao akikubali kupoteza mchezo huo kwa pointi 117-111, 115-113, 115-113. Katika pambano hilo, kila mmoja aliweza kumtoa damu mwenzake, kutokana na kushambuliana. Jeff Horn, mwenye umri wa miaka 29, aliweza kuonesha kuwa na damu changa dhidi ya Pacquiao, mwenye umri wa miaka 38. “Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama nitakuja kupigana na bingwa kama Pacquiao na nikaweza kushinda, lakini tayari nimeweka historia mpya na kutwaa ubingwa wa WBO mbele ya bingwa huyo. “Ninayo furaha kubwa kuwa bingwa, ninaamini historia hii inaweza kunisaidia kwenye mapambano yangu yajayo,” alisema Horn. Kipigo hicho cha Pacquiao kinaweza kumfanya bingwa huyo kuwa ni mwisho wake wa ngumi, kwa kuwa uwezo wake unazidi kupungua siku hadi siku, kwa mujibu wa mwalimu wake, Freddie Roach. “Pambano lilikuwa gumu sana, wala sikutegemea kama ningeweza kukutana na ushindani wa aina hiyo, lakini natakiwa kukubaliana na matokeo, kwa kuwa ni sehemu ya pambano na hayo yalikuwa matokeo kutoka kwa majaji, natakiwa kuheshimu na kukubaliana nao. “Nampongeza mpinzani wangu kwa kuibuka na ushindi, nadhani alikuwa na maandalizi mazuri na ndiyo maana amefanikiwa kushinda,” alisema Pacquiao. Uwezo wa Pacquiao ulionekana kushuka tangu alipochezea kichapo dhidi ya bingwa Floyd Mayweather, Mei mwaka 2015, hata hivyo, mabondia hao walitangaza kustaafu mchezo huo, huku Paquiao akidai kuwa, anataka kutumikia jamii katika mambo ya kisiasa, wakati huo Mayweather akidai muda wake umefika. Hata hivyo, Mayweather alirudi tena ulingoni na Agosti 26 mwaka huu anatarajia kurudi tena uwanjani dhidi ya mpinzani wake, Conor McGregor, pambano ambalo linadaiwa kuwa la kihistoria.
kimataifa
BERLIN, UJERUMANI SERIKALI  ya China imeishutumu Marekani kwa kueneza hofu dhidi ya virusi vya corona badala ya kutoa msaada. Kauli  hiyo  ya China inatokana na uamuzi wa Marekani kutangaza hali ya dharura na kupiga marufuku raia yeyote wa kigeni ambaye alitembelea nchini China kuanzia Desemba kutoingia nchini humo. Si tu Marekani Hong Kong imefunga mpaka wake na China huku nchi kadhaa nyingine duniani nazo zikitangaza uamuzi kama huo. Hadi sasa kesi za virusi hivyo  zilizothibitishwa ni zaidi ya 17,000 huku watu karibu 361 wakiwa wamekufa nchini China pekee. Nje ya China kuna wagonjwa zaidi ya 150 waliothibitishwa kukumbwa na virusi hivyo na kifo kimoja kimetokea nchini Ufilipino. Virusi hivyo vinasababisha mtu kushindwa kupumua sawasawa na kufanya maambukizi katika mfumo wa upumuaji na dalili zake huanza kwa homa kali  kikufuatia kifua kikavu. HATUA ZA MAREKANI Januari 23, Marekani iliamuru maofisa wake pamoja na familia zao kuondoka kwa dharura katika jiji la Wuhan  lililoko jimbo la Hubei ambako virusi hivyo vilianzia. Siku chache kabla ya wiki, iliruhusu kuondoka kwa kujitolea kwa maofisa wake na waajiri wake wote walioko China. Januari 30, Shirika la Afya duniani lilitangaza hali ya dharura kuhusiana na virusi hivyo. Kutokana na hilo, Marekani iliamuru kuondoka kwa maofisa wake wote pamoja na familia zao wakiwamo wale wenye umri wa chini ya miaka 21. Raia yeyote wa Marekani ambaye alikuwa Hubei akiingia nchini humo anawekwa karantini kwa siku 14. UJERUMANI WAGONJWA WAFIKA 10 Wakati huo huo watu kumi wamethibitika kuugua ugonjwa wa virusi vya corona nchini Ujerumani. Hatua hiyo imekuja baada ya watu wawili kati 124 waliosafirishwa kwa ndege ya Ujerumani kutoka mji wa China wa Wuhan ambao ni kitovu cha homa itokanayo na virusi vya Corona, kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo.  Shirika la Msalaba Mwekundu lililotoa taarifa hiyo, limesema watu hao hivi sasa wamewekwa chini ya karantini katika hospitali ya mjini Frankfurt.  Watu hao walithibitishwa kuwa na maambukizi wakati vipimo vilipochukuliwa katika kambi ya jeshi ya Germasheim, ambako watu waliotoka Wuhan wamepewa hifadhi.  Waziri wa afya wa Ujerumani, Jens Spahn amesema amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani, na wamekubaliana juu ya haja ya mawaziri wa jumuiya ya nchi saba zilizoendelea kiviwanda, G7 kukutana kupanga mkakati wa pamoja dhidi ya homa hiyo hatari.
kimataifa
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka dimbani kuivaa Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kushinda ili kuendelea kujihakikishia nafasi yao ya kuwa karibu na kutetea taji la ligi hiyo. Unaweza kuwa ni mchezo wa presha kwa Wekundu hao kwasababu wametoka kupoteza mchezo mmoja na kupata sare moja, tofauti na matarajio yao ya awali hivyo, kwa vyovyote vile hawatakubali kupoteza tena au kupata sare. Mpaka sasa Simba ina nafasi ya kutetea taji kama tu itashinda michezo minne kati ya mitano iliyobakiza. Inashika nafasi ya pili kwa pointi 82 katika michezo 33 nyuma ya Yanga inayoongoza kwa pointi 83 katika michezo 36m ikiwa imebakiza michezo miwili.Timu hizo zimekuwa zikipishana katika uongozi wa ligi kwa maana Simba ikishinda leo au kupata sare itarudi katika uongozi kutokana na kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Yanga inaweza kuwa na nafasi ya ubingwa kwa kuwaombea mabaya watani zao wapoteze michezo mitatu na wao washinde waliyobakiza. Simba inakutana na Mtibwa Sugar leo, ambapo mara ya mwisho kukutana Wekundu hao walishinda bao 1-0, Aprili mwaka jana.Mtibwa Sugar haina cha kupoteza kwani inashika nafasi ya tano kwa pointi 49 katika michezo 35 labda kugombea nne bora. Iwapo watashinda huenda wakapanda hadi nafasi ya nne na kumshusha KMC, lakini wakipoteza wanaweza kubakia nafasi hiyo. Lakini hawapo katika mbio za ubingwa, wanaweza kupambana kupata matokeo kwa ajili ya kuweka heshima. Mtibwa itakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia washambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi ambao muda wote wamekuwa wakipambana bila kukata tamaa ili kufunga.Safu ya ulinzi ya Simba iko vizuri kwani mpaka sasa imepoteza michezo mitatu tu.
michezo
RAIS John Magufuli amemuomba Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini, Shehe Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi, kuwaleta wawekezaji wengi wa nchi hiyo kuja kuwekeza nchini kutokana na kuwapo mazingira mazuri ya uwekezaji.Amemweleza Balozi huyo kuwa, pamoja na misaada inayoendelea kutolewa na UAE kwa Tanzania, kuna maeneo mazuri na mengi ya uwekezaji ikiwamo katika sekta za uvuvi, mifugo, kilimo na viwanda.Rais Magufuli aliyasema hayo juzi katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Chato na visima vinane vilivyojengwa na Islamic Foundation kwa ufadhili wa UAE, wilayani Chato.“Balozi ukienda nyumbani (EAU) ujue maeneo haya tunahitaji uwekezaji si misaada tu. Huku Chato kuna Hifadhi ya Rubondo, kisiwa kilichopo kwenye ziwa lakini pia kuna tembo, mamba, sokwe mtu, nyoka na wanyama wengine. Ndio eneo kubwa linalotumika kwa uvuvi wa maji baridi, ndege kutoka Ulaya wa aina mbalimbali wanakuja kutaga pale.”“Burigi ni hifadhi inayounganisha wilaya tano za Ngara, Muleba, Karagwe, Biharamulo na Chato. Hakuna tatizo la vyakula, samaki ni wengi mnaweza kusafirisha kwenda nchi za Kiarabu. Ng’ombe, mbuzi wapo, Tanzania ni ya pili kwa wanyama wengi, wapo milioni 32.5. Mje muwekeze popote, si lazima hapa, tembea nchini kote,” alimweleza Balozi Al-Marzooqi.Rais Magufuli alimueleza Balozi huyo kuwa Watanzania ni wakarimu na wapenda amani na wapo tayari kufanya biashara na nchi yake. Alisema amethamini mradi huo wa maji uliogharimu Sh milioni 340 na ndiyo maana ameamua kwenda mwenyewe kwenye hafla hiyo badala ya kuwakilishwa.
kitaifa
Na MWANDISHI WETU, BIHARAMULO RAIS Dk. John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini wawe wameanza kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti. Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wananchi wa Biharamulo mkoani Kagera muda mfupi kabla ya kufungua barabara ya lami ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga. Kauli hiyo ya Dk. Magufuli imekuja siku chache baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuvifungia kuuza mafuta vituo vyote ambavyo havitumii mashine za kielekroniki za kutolea risiti (EFDs) na kusababisha uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo katika mikoa mbalimbali nchini. Katika agizo lake, Dk. Magufuli amewataka Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini vinatumia mashine hizo na kusisitiza kuwa wamiliki watakaokiuka agizo hilo, vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni. Taarifa ya Ikulu iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilisema: “Na kwa hili natoa siku 14, wale wenye vituo vya mafuta wote,  uwe upo  Chato, uwe Biharamulo, uwe Kagera, uwe Dar es Salaam, hakikisha una hiyo mashine, ndani ya siku 14.” Aidha Dk. Magufuli amewataka wafugaji waliovamia Hifadhi ya Taifa ya Burigi mkoani Kagera kuondoa mifugo yao mara moja na amemwagiza Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kuendelea na operesheni ya kuondoa mifugo yote iliyovamia hifadhi hiyo na maeneo mengine yasiyoruhusiwa kulishia mifugo. Katika hatua hiyo, Dk. Magufuli aliwataka wafugaji kote nchini kuchunga mifugo yao katika maeneo waliyotengewa, huku akionya kuwa vitendo vya wafugaji kuingiza mifugo yao katika hifadhi na mashamba ya wakulima havikubaliki. “Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya simamieni hilo, ninajua bado kuna ng’ombe mle hifadhini, simamieni kwa kuzingatia sheria za hifadhi. “Kwa hiyo wafugaji wajifunze namna ya kufuga, kama unaona una ng’ombe wengi na huwezi kuwatunza uza, hata mimi nimeuza ng’ombe wangu, niliona wamekuwa wengi siwezi kuwatunza, viwanda vipo,” alisisitiza. Kuhusu kero ya uhaba wa maji inayowakabili wananchi wa Biharamulo, Dk. Magufuli alielezea kusikitishwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka maji katika mji huo na alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Bukoba (BUWASA), Alen Mwita kuhakikisha mashine zilizonunuliwa zinafungwa na kuanza kutoa maji ifikapo Julai 30. Baada ya kuzungumza na wananchi wa Biharamulo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi, Dk. Magufuli alifungua barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga ambayo inaunganisha barabara ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Kigoma, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Rwanda na Uganda. Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 154 na imejengwa kwa gharama ya Sh bilioni 190.4 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania. Mapema jana asubuhi, Dk. Magufuli alitembelea Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga Katoke, alikosoma elimu ya sekondari, ambako aliendesha harambee iliyofanikisha kupatikana mifuko 1,000 ya saruji na mabati 150 kuchangia ujenzi wa Seminari hiyo. Aidha Dk. Magufuli pia alitoa Sh milioni 1 za kutengeneza dirisha la bweni alilolivunja wakati akiwa kidato cha pili na madirisha mengine yanayohitaji matengenezo. Akiwa njiani kuelekea Ngara, Dk. Magufuli alisimamishwa na wananchi wa Nyakahura ambao aliwahakikishia kuwa Serikali itaifanyia matengenezo barabara ya Nyakahura – Rusumo – Ngara akiahidi kumtuma Waziri wa Maji na Umwagiliaji kwenda kuangalia namna ya kutatua tatizo la maji na pia amechangia Sh milioni 10 katika ujenzi wa majengo ya shule. Dk. Magufuli kesho ataendelea na ziara yake mkoani Kagera ambako atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Ngara.
kitaifa
N’daw ni mmoja wa wachezaji wawili wa kimataifa wanaotarajiwa kutemwa kwenye dirisha dogo la usajili baada ya kushindwa kuisaidia timu hiyo huku akionekana kama hasara kutokana na kupokea kiasi kikubwa cha mshahara huku siku zote akisota benchi.Akizungumza na gazeti hili Kerr, alisema hawezi kupinga maamuzi ya viongozi wake kwa sababu ndiyo wanaotoa pesa, lakini akawatahadharisha kuhakikisha nafasi yake wanamleta mchezaji mwenye kiwango cha juu kuzidi waliopo kwenye nafasi hiyo.“Viongozi wangu wamekosa uvumilivu na inaonekana wanataka mabadiliko kwa muda mfupi kitu ambacho siyo rahisi kwa mchezaji kama N’daw, ni msaada mkubwa kwa Simba pindi atakapochanganya ndiyo sababu nimekuwa nikimpa dakika 15 za mwisho ili kuzoea mazingira ya soka ya Tanzania, anachohitaji ni muda tu,”alisema Kerr.Kocha huyo raia wa Uingereza alisema kama kocha kuna vitu ambavyo ameviona kwa mshambuliaji huyo na ndiyo sababu akapendekezwa kusajiliwa na kwa kuwa alikuwa nje kwa muda mrefu, hivyo kusisitiza apewe muda wa kuonesha makali yake halisi.Alisema kitendo cha uongozi kutaka kumtema mshambuliaji huyo ni sawa na hasara kwa Simba kutokana na gharama kubwa iliyoingia klabu hiyo katika kumsajili, achilia mbali gharama itakazoingia kuvunja mkataba wake.N’daw amesajiliwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Niary Tally ya Senegal na wakati anatua, alitarajiwa kuwa mtambo wa mabao kutokana na rekodi yake nzuri ya ufungaji aliyokuwa nayo wakati akiichezea Dynamo Bucuresti ya Romania kitu ambacho kilimvutia kocha Kerr, lakini mambo yanaonekana kwenda kinyume.
michezo
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), aliyetaka kujua kwanini Serikali isiwaongezee muda waendesha bodaboda hao wa kusajili na kusogeza huduma hiyo, maeneo ya wilayani.“Kesho (leo) ndio mwisho wa kusajili pikipiki hizi kwa namba mpya, kwanini Serikali isiwaongezee muda hawa waendesha bodaboda wa kusajili na kusogeza huduma hiyo wilayani ili iwe rahisi kwao,” alihoji.Akijibu swali hilo, Nchemba, alisema tayari Serikali imewasiliana na Mampaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wamekubaliana kuongeza muda huo wa usajili wa namba mpya hadi Desemba mwaka huu.Alisema wameongeza muda huo ili kutoa muda zaidi kwa wamiliki wa pikipiki hizo kujisajili kwa wakati, huku akionesha kuwa ifikapo Desemba, kila mmiliki atatakiwa chombo chake kiwe na namba mpya ya usajili.Katika swali la msingi la mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukumazina (CCM), aliitaka Serikali ibainishe lini itakuwa makini katika kukusanya na kutumia mapato yake na endapo ina mikakati ya kupunguza safari za viongozi za ndani na nje ya nchi.Akijibu maswali hayo, Nchemba, alisema ili kuwa na nidhamu na umakini katika matumizi ya Serikali, imekuwa ikifanya matumizi yake kulingana na mapato na kwa kuzingatia vipaumbele kama vinavyoainishwa katika bajeti inayoidhinishwa na Bunge.“Si kweli kuwa misafara ya viongozi haina tija, viongozi wa Serikali hufanya ziara ndani na nje ya nchi, kukagua, kuhimiza na hata kushiriki na kuhamasisha harambee za kuchangia shughuli za maendeleo kama zahanati, barabara na hata Vicoba na Saccos,” alisisitiza.
uchumi
Ramadhan Hassan – Dodoma WAFANYAKAZI sita wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  waliokuwa kwenye kamati ya utekelezaji wa makubaliano  na Kampuni ya Rom Solutions Co. Ltd ya nchini Romania, jana walihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa. Wajumbe hao wanahojiwa kutokana na kashfa ya watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya zabuni ya kununua vifaa vya zimamoto vyenye thamani ya Euro milioni 408 (Sh trilioni moja). Inadaiwa walipoenda kwenye mazungumzo, walipewa  kompyuta mpakato (Laptop) na walilipwa Dola za Marekani 800 kwa kila kikao walichohudhuria na Kampuni ya Rom Solution. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Takukuru waliohojiwa jana ni Kamishna wa Zimamoto, Mbaraka Semwanza, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Fikiri Salala, Naibu Kamishna wa Zamamoto, Lusekela Chaula, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Ully Mburuko, Ofisa Ugavi Mkuu wa Zimamoto, Boniface Kipomela na Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Felis Mshana. Wakiwa na nyuso za huzuni, wafanyakazi hao walifika majira ya saa nne asubuhi kwa pamoja katika Ofisi za Makao Makuu ya Takukuru jirani na Uwanja wa Jamhuri jijini hapa. Waliingia kila mmoja akiwa na Laptop ambazo walipewa na kampuni hiyo ya Rom Solution ambapo walianza kuingia mmoja mmoja kwenda mapokezi na kisha baadae kuingia ndani kuhojiwa. Wiki iliyopita Takukuru waliwahoji watendaji wa juu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwamo Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni. Wengine waliohojiwa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. Baada ya kuhoji watendaji hao, Takukuru inakuwa imekamilisha kazi ya kuwahoji watendaji 11 wa wizara hiyo kufuatia agizo la Rais Dk. John Magufuli kuhusiana na mkataba ulioingiwa na wizara hiyo wa Sh trilioni 1 kununua vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Kampuni ya Rom Solutions Co. Ltd. “Watu wamekosa uadilifu, hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unaotengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni 1. Mradi huo umesainiwa na Kamishna Jenerali wa Zimamoto,” alinukuliwa Rais Magufuli katika sehemu ya hotuba yake.
kitaifa
JUMUIYA ya Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Dar es Salaam umewahamasisha wanawake katika mkoa huo kujitokeza na kujiandisha ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Mwenyekiti wa UWT, Gaudentia Kabaka alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wanawake wa umoja huo walipokutana kwa ajili ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.Kuhusu uchaguzi alisema wanawake wengi wamekuwa wakibaki nyuma kw akutokujua maana ya kujiandikisha bila kujua kuwa ni sehemu mojawapo ya kupata viongozi waona ambao ndio wenye kuwatambulisha kwa ngazi za juu.“UWT iwe bega kwa bega na wanawake wote wa mkoa huu kuhakikisha wanajitokeza na kujiandikisha ili waweze kupiga kura kuchagua viongozi wao wa mitaa,” alisema Kabaka na kuwataka pia kuwapa motisha wanawake watakaogombea nafasi mbalimbali.Aliwaambia wanawake hao kutambua kuwa muda wa siku tano uliopangwa wa kujiandikisha ni mdogo sana hivyo ni muhimu kuutumia kikamilifu.Hata hivyo alikemea upotoshaji unaotolewa na watu katika baadhi ya maeneo nchini kuhusu azma ya kujiandikisha katika uchaguzi huo, kwamba wenye vitambulisho vya kupigia kura hawatakiwi.“Nimepata ujumbe mfupi kutoka mkoani Tarime kuwa wapo watu wanapita katika nyumba za watu hususani wanachama wa CCm wakiwaambia kuwa wale wenye vitambulisho wasiende kujiandikisha,” alisema.Kuhusu kumuenzi Nyerere UWT mkoa huo walitoa misaada mbalimbali ya vyakula pamoja na vifaa kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wazee cha Mama Teresa kilichopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT Queen Mlozi aliwataka wanawake wa UWT mkoa huo kutambua kuwa iwapo hawatojiandikisha jitihada za kufikia ushindi zitakuwa ni bure.Aliwataka wanawake haok uhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba, shuka kwa shuka ili elimu ya kujiandikisha iweze kuwafikia wote.
kitaifa
Na BENJAMIN MASESE – MWANZA SERIKALI imepiga marufuku taasisi za umma kutuma mizigo au vifurushi kwa kutumia kampuni binafsi za usafirishaji, badala yake zitumie Shirika la Posta Tanzania (TPC), ikidai ni kuziba mianya ya upotevu wa fedha. Agizo hilo lilitolewa   hivi karibuni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati akizungumza na watumishi walio chini ya wizara hiyo katika kikao maalumu kilichofanyika jijini Mwanza. Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa  ipasavyo pamoja na mambo mengine ya maadili ya kiutumishi, Profesa Mbarawa aliamua kutoa namba zake za simu za mkononi; 0622000001 na 0686955116 ili kuwasiliana naye pale itakapobainika mtumishi anafanya vitendo kinyume na taratibu za kazi. “Shirika letu lazima lifufuliwe ili lipate mafanikio, hili tutalisimamia kweli kweli na naomba watu tuzingatie maagizo, kama Serikali  tunaendelea kufanya maboresho kuanzia kwa watumishi wa kawaida hadi kwa postamkuu,  kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria,” alisema. Profesa Mbarawa pia aligusia juu ya mali za TTCL na kuahidi kuanza kuzifuatilia kwani alidai wapo baadhi ya waliopanga kwenye majengo la shirika hilo lakini nao wanapangisha wengine. Alisema  hadi sasa majengo  ya TTCL hayana tija kwa shirika kutokana na udalali unaofanyika na kuwataka viongozi kuanza kupitia mikataba upya kabla ya wizara kuanza  uchunguzi.
kitaifa
TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia mkazi wa Chalinze, Halima Juma (23) kwa tuhuma za wizi wa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema Novemba 11 mwaka huu walimkamata Halima akiwa katika ATM za Benki ya CRDB tawi la Mbagala akijifanya kuwasaidia wazee. “Halima alijifanya kuwasaidia wazee hasa wastaafu, wasiojua kutumia mashine hizo kwa lengo la kuchukua namba za siri na kuwabadilishia kadi na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao,” alisema Mambosasa. Alisema alikuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwabadilishia kadi zao halisi za benki na kuwapa nyingine na baadaye kuiba fedha zilizopo kwenye akaunti zao. Alisema askari walimtilia shaka na kumkamata na baada ya kukaguliwa ambapo alikutwa na kadi 23 za benki kutoka kwa watu tofauti alizokuwa amezificha kwenye pochi aliyokuwa ameificha sehemu za siri. “Tumemkuta na kadi za benki ya CRDB saba, NMB sita, NBC mbili, Amana mbili, Benki ya Posta mbili,  ACB mbili, Stanbic moja, DCB moja na Equity kadi moja,” alisema Mambosasa. Alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na jeshi hilo na atafikishwa mahakamani ushahidi utakapokamilika. Kulinda uchaguzi kwa helkopta, mbwa Katika hatua nyingine, alisema jeshi hilo litafanya doria za miguu, pikipiki, mbwa farasi na helkopta kuimarisha ulinzi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemvba 24. Aidha alisema jeshi hilo litaimarisha ulinzi katika vituo vya kupigia kura, ofisi zote za kata, na vyama vya siasa katika kipindi cha uchaguzi huo.  “Tutashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama chini ya Mwenyekiti wetu Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kuhakikisha jiji lipo salama,” alisema Mambosasa. Mvua zaua wawili Mambosasa pia alisema mvua zinazoendelea kunyesha zimeua watu wawili na kujeruhi mmoja . “Mtu mmoja alisombwa na maji akivuka mto na mwingine alipigwa na radi na kufa palepale huku mmoja akijeruhiwa na radi hiyo,” alisema Mambosasa. Aliwataka wazazi kuchukua tahadhari kwa kuwazuia watoto kucheza katika madimbwi na kuchukua tahadhari wakati wa kuvuka mito. “Wazazi wawazuie watoto wao kuvuka makolongo wanapokwenda shuleni kwani maji hayapimwi,” alisema Mambosasa.
kitaifa
Uchaguzi huo umemalizika huku kukiwa na kujirudia kwa viongozi waliopita kutetea nafasi zao kutokana na kuwa wagombea wengine hawakuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwa wajumbe wa chama hicho. Katika uchaguzi huo, nafasi ya Katibu imenyakuliwa na Hamiss Issa wakati Mweka Hazina ni Joseph Laizer.Nafasi ya Mjumbe Mwakilishi wa mkoa imekwenda kwa Mohammed Jumbe na nafasi ya Mjumbe Mwakilishi wa Klabu imekwenda kwa Geoffrey Mika.Nafasi nyingine ambayo imepata kiongozi kwa mara ya kwanza ni mwakilishi wa kwa upande wa soka ya wanawake, Hellen Moses.Wengine ni Wajumbe wa kamati ya Utendaji ambao ni Hamisi Mponda na Hamisi Komba.Akizungumza baada ya kuchaguliwa tena kukiongoza chama hicho, Katibu wa ADFA Issa alieleza kuwa uongozi uliopatikana umeandaa mikakati mipya zaidi katika kuhakikisha unabadilisha mwenendo mzima wa soka wilayani humo.“Pamoja na uchaguzi kufanyika bado kuna nafasi mbili hazikupata uongozi ikiwemo mwenyekiti msaidizi na katibu msaidizi ambapo tunatarajia kuitisha uchaguzi mdogo baada ya kupatikana kwa wagombea,”aliongeza Issa.
michezo
NA ASMA BASHIR, DAR ES SALAAM (DSJ) TIMU 17 zimethibitisha kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli yaliyopangwa kufanyika Julai 12 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA), Anna Kibira, alisema timu hizo zimethibitisha kushiriki mashindano hayo huku timu tatu za Filbert Bayi ambao ndio mabingwa watetezi, Teachers ya Kinondoni na Polisi ya Mbeya wakijiondoa. Alizitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni Jeshi Stars, JKT Mbweni, Polisi, Uhamiaji, CMTU zote kutoka Dar es Salaam. Nyingine ni JKT Ruvu, TTPL ya Morogoro, Polisi Dodoma, Magereza Morogoro, Polisi Shinyanga, Polisi Mwanza, Polisi Kigoma, Mbeya City Queens, CIDT Arusha, Polisi Arusha, Nyanyembe ya Tabora na Polisi Morogoro. Timu zitakazoshika nafasi ya kwanza hadi ya nne zitashiriki Ligi ya Muungano itakayoanza Agosti mwaka huu. “Tutatumia mashindano hayo kuteua wachezaji wenye nidhamu na uzalendo watakaoungana na wenzao wa Zanzibar kuunda timu yetu ya Taifa,” alisema.
michezo
WANANCHI wa Mwanza wameguswa kwa aina yake na uamuzi wa serikali kuamua sherehe za Uhuru kufanyika mkoani humo wakidai haijawahi kutokea katika historia ya maisha yao kwani wamezoea kuona sherehe hizo zikifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kila mwaka.Katika hali ya kuwa na hamasa na sherehe hizo, wananchi hao walisema watajitokeza kwa wingi leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kushuhudia moja kwa moja maadhimisho hayo ambayo yanaweka historia muhimu katika maisha yao.Ikumbukwe kwamba leo Tanzania inaadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo ilipata uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza Desemba 9, 1961.Miongoni mwa wananchi waliozungumza na gazeti hili jana ni mkazi wa Kilimahewa jijini Mwanza, Muzamiru Shabani (50) ambaye ni fundi magari. Shabani alisema Uhuru umewasogelea karibu tofauti na zamani walikuwa wakishuhudia sherehe hizo kwa njia ya televisheni zikifanyika jijini Dar es Salaam.“Sherehe za Uhuru kutekeleza EPA zilikuwa zinaishia Dar es Salaam tu, lakini mwaka huu Rais John Magufuli amebadilisha utaratibu na kuamua kutuletea Mwanza, sijawahi kuona jambo hili tangu kuzaliwa kwangu, napenda sherehe za uhuru zibebe mantiki ya maendeleo kwa kutuletea mambo mapya,” alisema Muzamiru.Naye mkazi wa Kishiri, Joseline Paul (32) anayefanya biashara ya matunda katika Soko la Kirumba, alisema amefurahishwa na uamuzi wa serikali kuukumbuka Mkoa wa Mwanza kwa kuufanya kuwa mwenyeji wa sherehe za Uhuru.Alisema kupitia sherehe hizo, wangefurahi kama soko lao la Kirumba nalo lingejengwa upya kwani hali ilivyo sasa halitamaniki kwa matope kutokana na mvua zinazoendelea.Kwa upande wake, mkazi wa Nyasaka, Ephraim Gerald (37) ambaye ni fundi cherehani alisema Mkoa wa Mwanza umeandika historia ya aina yake kwa sherehe hizo kufanyika mkoani humo. Gerald alisema sherehe hizo kufanyika Mwanza zimekuwa fursa muhimu kwake kwa kuwa amepata wateja wengi waliofika kushona sare za Uhuru.Alisema amepata kazi nyingi za kushona sare hizo, lakini pia akatoa wito sherehe za uhuru ziwe chachu ya kuongeza uwajibikaji katika sekta zote na kupiga vita ukandamizaji wa aina yoyote.“Ni fursa muhimu kwa Mwanza kupata heshima ya kuwa mwenyeji wa sherehe za Miaka 58 ya uhuru. Sherehe hizi ziwe chachu ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwani wengi wanaomaliza masomo yao hawana kazi,” alieleza mkazi wa Nyamanoro, Shabani Minangi (44).Katika kunogesha sherehe hizo leo, Wasukuma 1,500 kupitia utamaduni na mila yao inayoitwa ‘Masalama’ ikimaanisha ulinzi watatumbuiza uwanjani hapo.Mmoja wa viongozi wa mila hiyo, Selemani Marko alisema mila hiyo inabeba ujumbe kuwa ulinzi wa taifa ni jambo muhimu. Gazeti hili jana lilishuhudia Jiji la Mwanza likipambwa kwa Bendera ya Taifa katika maeneo mengi, upambaji wa Uwanja wa CCM Kirumba, wanafunzi wakiendelea na mazoezi ya halaiki, lakini pia ulinzi ukiwa umeimarishwa.
kitaifa
Na SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM MCHEZAJI wa gofu kutoka Arusha, Nuru Molel, juzi ameibuka bingwa katika mashindano ya gofu ya Kombe la Waitara, kipengele cha wachezaji wa kulipwa (Professionals) ambayo yalifanyika viwanja vya Lugalo, jijini Dar es Salaam. Molel aliwashinda jumla ya wachezaji wa kimataifa 21 walioshiriki michuano hiyo, kwa gloss 71, huku nafasi ya pili ikimwendea John Loence pia wa Arusha, aliyeshinda kwa gloss 72. Hassan Kabio wa Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam alimaliza nafasi ya tatu baada ya kushinda kwa gloss 72, ambapo washindi walitarajiwa kukabidhiwa zawadi zao jana jioni. Waitara Trophy iliendelea jana kwa kushirikisha vipengele vyingine, isipokuwa watoto wenye umri chini ya miaka 18. “Hakutakuwepo na ushiriki wa watoto wenye umri chini ya miaka 18 kutokana na mashindano haya kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti,” alinukuliwa nahodha wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Japhet Masai. Waitara Trophy hufanyika kila mwaka, lengo ni kukumbuka mchango wa mwanzilishi wa Uwanja wa Gofu Lugalo, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jenerali Mstaafu George Waitara.
michezo
KUANZIA Novemba 5 hadi 10, mwaka huu, Maonesho ya 2 ya Kimataifa ya China, maonesho ya kwanza ya dunia yenye mada ya kuwezesha uingizaji wa bidhaa, yatafanyika Shanghai. Jumla ya nchi 64 pamoja na Tanzania na mashirika matatu ya kimataifa, yatashiriki kwenye maonesho ya nchi.Zaidi ya watazamaji 3,000 na wanunuzi 400,000 wamejiandikisha katika maonesho hayo. Zaidi ya shughuli 200 za kusaidia na kuwezesha zitafanyika. Wiki ijayo, China itakaribisha wageni kutoka duniani kote na dunia itakuwa makini tena kufuatilia Shanghai na China. Maonesho ya kimataifa ya China yafungua zaidi soko la China duniani Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa Uchina. Kwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, kiwango cha biashara ya nje ya China kimeongezeka kutoka dola bilioni 1.1 za Marekani hadi dola trilioni 4.6.Uuzaji wa rejareja wa bidhaa za walaji, umeongezeka kutoka chini ya bilioni 30 RMB hadi takribani trilioni 40 RMB (sawa na dola za Marekani trilioni 5.4). China imekuwa nchi kubwa zaidi ya biashara ulimwenguni na soko la pili kubwa la watumiaji. Maendeleo adhimu ya China katika miaka 70 iliyopita, pia ni mchakato ambao China ilijijumuisha katika uchumi wa dunia, iliendeleza mageuzi kwa dhati na ikafunguka zaidi duniani.Kama Rais Xi Jinping alivyosisitiza, ukuaji wa uchumi wa China hapo awali umepatikana kwa kujitolea kufungua, vivyo hivyo maendeleo ya hali ya juu ya uchumi wa China katika siku zijazo, yanaweza tu kuwa na dhamana kwa uwazi mkubwa. Kuwa wenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya China ni uamuzi muhimu kwa China kusukuma mbele duru mpya ya ufunguzi wa kiwango cha juu, na hatua muhimu ya kufungua soko la China duniani. Maonesho ya 2 ya kimataifa ya, China yatakuwa ni ushuhuda kwamba China inafungua milango zaidi na zaidi.Maonesho ya kimataifa ya China yanaingiza msukumo mpya katika uchumi wa dunia Mpango wa China wa kufanya Maonesho ya Kimataifa ya China na kupanua uagizaji, sio chaguo la kuongeza faida. Ni hatua iliyoelekezwa baadaye kukumbatia dunia na kukuza maendeleo ya kawaida. China imekuwa injini yenye nguvu zaidi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia kwa miaka 13 mfululizo tangu 2006. Katika miaka 15 ijayo, uagizaji wa bidhaa na huduma nchini China inatarajiwa kuzidi dola za Marekani trilioni 30 na dola za Marekani trilioni 10 kwa mtiririko huo.China ina uwezo mkubwa wa soko, na iko tayari kushiriki faida za ukuaji wake wa haraka na nchi zote duniani. China ingependa kufanya kazi pamoja na jamii ya kimataifa, kukuza Maonesho ya Kimataifa ya China kuwa jukwaa la wazi na la kushirikiana kwa nchi zote duniani ili kuimarisha ushirikiano na kubadilishana na kufanya biashara ya kimataifa, na kutoa michango mikubwa kwa maendeleo bora ya biashara ya kimataifa na uchumi wa dunia. Maonesho ya Kimataifa ya China hutoa nguvu mpya ya kuendesha kwa utandawazi wa uchumi Ua moja halitengenezi chemchemi.Kushikilia Maonesho ya Kimataifa ya China si onesho la pekee la China, bali linalojumuisha nchi kutoka duniani kote. Haioneshi tu bidhaa za kwanza, teknolojia na huduma kutoka kwa nchi zilizoendelea, lakini pia inaweka jukwaa la nchi zingine zinazoendelea, haswa nchi ndogo zilizoendelea, kuanzisha bidhaa zao za hali ya juu na tofauti kwa China na kuingia kiubora zaidi kwenye soko la kimataifa. Kati ya washiriki wa maonesho ya nchi 64, wengi wao ni nchi zinazoendelea barani Asia, Afrika na Amerika ya Kusini.Kujibu ongezeko la umoja na ulinzi, China inachukua hatua kadhaa za ufunguzi, ikiwa ni pamoja na Maonesho ya Kimataifa ya China, kukuza zaidi uwazi duniani na kutoa kasi mpya ya utandawazi wa uchumi. China itafanya kazi kwa pamoja na nchi zote, zinazoshiriki na mashirika ya kimataifa, kudumisha biashara ya bure na mifumo ya biashara ya kimataifa na kukuza uchumi wazi duniani. Maonesho ya Kimataifa ya China, fursa mpya kwa China na Tanzania kuimarisha ushirikiano kwa vitendo Uwazi umeibadilisha China sana.Wakati huo huo, uwazi wa China umefanya mabadiliko makubwa kwa ulimwengu na kutoa fursa zaidi kwa ulimwengu na kwa ushirikiano wa nchi mbili China na Tanzania. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Innocent Bashungwa, ataongoza ujumbe wa Tanzania kuhudhuria Mkutano wa 2 wa Maonyesho ya Kimataifa ya China katika siku zijazo. Wakati Tanzania ilishiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya China ya kwanza Novemba 2018, Tanzanite, ya kipekee duniani, ilipendwa na watumiaji wa China. Mada ya Maonesho ya nchi ya Tanzania katika Maonesho ya 2 ya Kimataifa ya China ni “Tanzania isiyoweza kusahaulika”.Tanzania itaonesha bidhaa zake za hali ya juu na tofauti, ikiwemo korosho, kahawa, katani, chai, ufuta na kazi ya mbao, kuonesha mazingira yake ya biashara na rasilimali zake za utalii zenye utajiri na wa kipekee.Kwa kweli itaimarisha “hisia za watanzania” za watumiaji wa China, kusaidia makampuni ya Tanzania kupanua soko lake la China na kuongeza “Chembe za Kitanzania” kwenye Soko la China.China na Tanzania wanafurahia urafiki wa muda mrefu. Ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya China na Tanzania umekua haraka. China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara kwa Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo na ndio nchi kubwa ya uwekezaji nchini Tanzania. Tunashukuru Tanzania inashiriki kikamilifu katika Ukanda Mmoja, Njia Moja, Maonesho ya Kimataifa ya China, Maonesho ya Kwanza ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika, Maonesho ya Kimataifa ya Mimea 2019, Beijing, China.China iko tayari kuwezesha bidhaa kutoka Tanzania zinazostahili kuingia China na kwenye soko la kimataifa kupitia Maonesho ya Kimataifa ya China na majukwaa mengine ya biashara, kukuza zaidi kiwango cha uagizaji kutoka Tanzania, kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili katika biashara, uwekezaji na utalii, na kuunga mkono Tanzania kufikia lengo ya viwanda na nchi yenye kipato cha kati.Natumai na ninaamini kuwa Maonesho ya Nchi ya Tanzania kwenye Maonesho ya Pili ya Kimaitaifa ya China yatafanikiwa sana. Mwandishi wa makala haya ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini.
kitaifa
Ahmed Makongo -Musoma ZAIDI ya wanafunzi 270 wa Shule ya Msingi Wanyere B, Kata ya Suguti, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wanasoma wakiwa chini ya mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa. MTANZANIA ilizungumza na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Peter James ambaye alisema kuwa wanafunzi hao wanasoma wakiwa katika hali hiyo kutokana na upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa. James alisema kuwa kutokana na hali hiyo walimu wamekuwa wakipata changamoto ya ufundishaji na kwamba pia uelewa kwa wanafunzi hao unakuwa ni mgumu. “Ni kweli wanafunzi wa madarasa matatu yenye jumla ya watoto 274 katika shule yetu wanasomea nje kwenye mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa,” alisema James. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Wanyere, Thomas Musiba, alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walihamasishwa na kuanza kuchangia fedha ili kuiondoa changamoto hiyo. Musiba alisema kuwa hata hivyo fedha walizochanga wananchi kwa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, zimechakachuliwa na viongozi waliokuwa madarakani na kusababisha ujenzi huo kutokufanyika. Alisema kuwa wananchi hao walichanga fedha hizo kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 kutokana na agizo la Mkuu wa Wilaya, Dk. Vicent Naano, ili kuwanusuru wanafunzi hao waweze kupata mahali pa kusomea. “Wananchi walianza kuchanga fedha hizo tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2019 na kwa kila kaya kuchangia kiasi cha Sh 15,000, ikiwa ni pamoja na waliochelewa kuchanga mchango huo walipigwa faini ya Sh 10,000 kwa kila kaya,” alisema.
kitaifa
KAMPUNI uchimbaji madini ya Acacia inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imesema inathamini ushirikiano wa muda mrefu baina yake na Tanzania kwenye sekta ya madini.Pamoja na hayo, kampuni hiyo imebainisha kwamba itaisaidia Kampuni yake tanzu ya Barrick kwenye majadiliano na serikali ya Tanzania ya jinsi ya kulipa fedha zinazodaiwa na wanaamini watafikia muafaka wenye manufaa kwa pande zote.Aidha, Acacia wamesema kwa kutambua ushirikiano wao na Tanzania wataendelea kuwekeza kwenye sekta ya madini huku wakiweka wazi kuwa kwa mwaka 2019, wanatarajia kuzalisha kiasi cha wakia za dhahabu 500,000 hadi 550,000. Kauli ya Acacia imetolewa siku chache baada ya Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kudai kuwa Barrick hawajakubali kulipa fedha yoyote kwa Tanzania kuhusu sakata la mchanga wa dhahabu.Alisema hayo wakati akihojiwa na mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Steve Sucker kwenye kipindi cha Hard Talk. Kwa taarifa ya Acacia, maelezo ya Lissu katika kipindi hicho yanapingana na ukweli ulioelezwa na Acacia kuhusu mwenendo wake kibiashara nchini na juhudi zake za uzalishaji huku wakisimamia makubaliano yanayohusu kampuni zake tanzu.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa kazi zake za uchimbaji dhahabu kwa mwaka jana katika migodi tajwa nchini, Acacia ilisema imefanikiwa kuzalisha wakia za dhahabu 521,980. Akizungumzia taarifa hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu Mpya wa Acacia, Peter Geleta alisema wanathamini ushirikiano wao na Tanzania wa muda mrefu kwenye sekta ya madini ambapo kwa mwaka 2018 wamelipa kodi na mrabaha zaidi ya dola za Marekani milioni 127.Aidha, alisema mwaka 2018 walifanikiwa kuwalipa wasambazaji wa ndani zaidi ya dola milioni 273 huku pia wakitoa ajira kwa wazawa kwa asilimia 97 sambamba na kuwekeza kwenye miradi ya kijamii yenye thamani ya dola za Marekani milioni 8.8. “Hayo yote tumefanya kwa kuwa tunathamini ushirikiano wetu na Tanzania wa muda mrefu na pia tunatambua nafasi yetu ya kuboresha maisha ya jamii inayozunguka migodi yetu kwa kuhakikisha tunaboresha maisha yao kwa kuanzisha miradi yenye tija kwao itakayobadilisha maisha,” alisema Geleta.Aliongeza kwa kutambua ushirikiano wao wa Tanzania wa muda mrefu, wataisaidia Barrick kwenye mazungumzo kuhusu ulipaji wa fidia ya biashara ya madini ili kuhakikisha suluhu inapatikana kwa manufaa ya pande zote. Akizungumzia ripoti ya uzalishaji dhahabu kwa mwaka 2018, Geleta alisema uzalishaji kwenye migodi yote mitatu nchini ulikuwa nzuri na walifanikiwa kuzalisha wakia wa dhahabu 521,980 ambapo awali walitarajia kuzalisha wakia kati ya 435,000 hadi 475,000. Akifafanua kwa mgodi mmoja mmoja, Geleta alisema mgodi wa North Mara umeendelea kufanya vizuri na mwaka 2018 walifanikiwa kuzalisha wakia za dhahabu 336,055 ikiwa ni ongezeko la asilimia nne ya mwaka 2017.Mgodi wa Buzwagi nao walizalisha wakia za dhahabu 145,440 mwaka 2018 ikiwa ni pungufu kwa asilimia 46 ya mwaka 2017 na kwamba mgodi wa Bulyanhulu wenyewe uliendelea kupunguza uzalishaji lakini walifanikiwa kuzalisha kiasi cha wakia za dhahabu 40,485 . Mapema mwaka 2017, Rais John Magufuli alizuia usafirishaji nje wa mchanga wa madini na kuunda Kamati Maalumu ya kuchunguza mchanga huo maarufu (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.Matokeo ya uchunguzi huo yalibaini jumla ya makontena 277 ya mchanga huo katika bandari kavu jijini Dar es Salaam yakitaka kusafirishwa kwenda nje kuchenjuliwa na Kampuni ya Barrick. Hata hivyo, makontena hayo yalizuiwa kusafirishwa na kufanyiwa tathmini kubaini kiasi cha madini kilichopo na thamani yake ambapo ilibainika kuwa makontena 277 yalikuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya kati ya shilingi bilioni 676 na bilioni 1,147.Baadaye kampuni hiyo ilitakiwa kulipa fidia ya hasara ya kusafirisha madini hayo kwa muda wa mrefu kuanzia miaka ya 1970 ambapo baadaye Mwenyekiti Mtendaji wa Barrick, Profesa John Thornton aliwasili nchini na kukutana na Rais na timu ya kamati ya mazungumzo kuhusu kulipa deni hilo.Katika mazungumzo hayo, Kampuni ya Barrick ilikubali kulipa Dola za Marekani milioni 300 sawa na Shilingi bilioni 700 kama malipo ya kuonesha nia njema na kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara madini na kampuni hiyo. Mazungumzo hayo yako chini ya Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Barrick.
kitaifa
BENJAMIN MASESE-MWANZA SERIKALI imeombwa kupiga marufuku vitendo vya baadhi ya wazazi kuwapeleka  mabinti wao wenye umri kati ya miaka  10 hadi 15  kuogeshwa dawa la kuvutia wanaume maarufu ‘samba’ kwa kuwa  vinachochea maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mimba za utotoni. Ombi hilo, limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kivulini linalojihusisha  kupinga ukatili kwa watoto na wanawake, Yassin Ally. Alisema  vitendo hivyo vinakwenda kinyume na mikakati ya Serikali ya kutokomeza Ukimwi na mimba za utotoni. Alisema  vitendo hivyo, vinafanyika kwa wingi Mkoa wa Shinyanga  na kufafanua hivi karibuni alikwenda kutoa semina kwa baadhi ya shule ndani na kuelezwa wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo kutokana na kwenda kuogeshwa. “Wikiiliyopita nilikwenda Mkoa wa Shinyanga, nilifika baadhi ya shule na kukuta wasichana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15  ni watoro, nilipodadisi sababu ya kushindwa kufika niliambiwa wanakwenda kuogeshwa dawa za mvuto maarufu Samba. “Cha ajabu walimu wanajua kabisa, watendaji wa vijiji, vitongoji na hata waratibu elimu wanafahamu lakini wanashindwa kuchukua hatua ili kukomesha  mila na desturi za ajabu ambazo zinasababisha watoto kuingia kwenye  maradhi na  mimba za utotoni. “Wito wnagu Serikali kupitia kwa wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wapige marufuku vitendo hivyo na wafuatilie kwa ukaribu na kuwachukulia hatua wazazi ambao watabainika kujihusisha na imani potofu, haiwezekani ukamvutia mwanaume kwa dawa ili apende binti, acheni  binti akifikisha umri atachagua mwanaume  anayempenda,”alisema. Alisema vitendo hivyo, vinaibuka mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na kushamiri kwa waganga wa jadi ambao wamejiegesha  katika taaluma hiyo, lengo kubwa ni kutafuta kipato. Alisema vitendo hivyo kama vitaendelea kuachwa bila kuwekewa adhabu kali,  itakuwa kazi ngumu kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambao mwishowe huishia kwenye maradhi yakiwamo Ukimwi, mimba za utotoni na utelekezaji familia. Hivi karibuni Shirika  la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Masuala ya Wanawake (UN  Women),  liliwakutanisha wazee 225 maarufu wa mila kutoka mikoa  tisa ikiwa ni sehemu ya kuisaidia Serikali ya Tanzania  kutimiza malengo ya mikataba ya kimataifa na kikanda  ya kukomesha vitendo ukatili wa jinsia na kuleta usawa ndani ya jamii. Akizungumza katika ufunguzi wa semina kwa wazee hao waliokutanishwa jijini Mwanza, Ofisa Elimu na Uhamasishaji kutoka UN Women, Lucy Tesha alisema  wadau wakubwa wa mashirika ya kimataifa ni Serikali kwa pamoja hushirikiana masuala ambayo yamewekwa katika mikakati ya kimaendeleo kwa  kuwafikia walengwa ambao ni  wananchi.
afya
Mchezo huo ulioanza kwa kasi na kwa kushambuliana kwa zamu iliwachukua dakika 28 timu ya Bom Bom kupata goli la kuongoza baada ya Manzir Mwinyi kupiga faulo iliyoingia moja kwa moja wavuni.Goli hilo lilibadilisha kabisa sura ya mchezo huo ambapo timu zote zilizidi kushambuliana bila timu yoyote kuona lango la mpinzani wake na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Bom Bom walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Idios kutaka kusawazisha huku Bom Bom wakitaka kuongeza goli lingine.Iliwachukua dakika nne Idios kusawazisha kupitia kwa Lucas Richard baada ya piga nikupige katika lango la Bom Bom.Akizungumzia mechi hiyo kocha Bom Bom, Ahmed Mohamed alisema ilikuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao walijiandaa vizuri na kuwataka wachezaji wake kuongeza juhudi kwenye mchezo ujao.Katibu wa chama cha soka mkoa Ilala, Kanuti Daudi alitoa mwito kwa wachezaji wanaoshiriki Airtel Rising Stars kutumia fursa hii vizuri ili vipaji vyao vionekane ili waweze kusaidia familia zao kwa maana soka limekuwa ajira kwa vijana.Mashindano hayo yalitarajiwa kuendelea jana jioni katika dimba la Tandika kwa mechi kati ya Wakati Ujao na Dubu, hiyo ikiwa ni kwa upande wavulana, wakati kwa upande wa wasichana Evergreen Queens ilitarajiwa kucheza na Temeke Queens.Michuano hii ya vijana ambayo kwa jiji la Dar es Salaam imeshaanza kwa takriban katika mikoa yake yote ya kimichezo, inafuatiliwa kwa karibu na jopo la makocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) bila kusahau timu mbalimbali ambazo zinawanyatia kwa karibu vijana wenye vipaji kutoka michuano hiyo kwa ajili ya kuwasajili.Mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi ameungana na wadau mbalimbali wa michezo katika kuhakikisha wanalipeleka mbele soka la vijana huku akiitaja Airtel Rising Stars kama mfano bora.
michezo
HOMA ya pambano la Ngao ya Jamii kati ya Simba na Azam FC litakalofanyika kesho imezidi kupanda huku kila timu ikitamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Simba, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Azam FC mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) wanakutana katika mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 1:00 usiku.Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa pamoja na Azam kuwa na timu nzuri lakini wekundu wa Msimbazi ndio watakaoibuka na ushindi.Manara alisema huu ni mwaka wa Simba wa mataji na kwa kuanzia wanaanza na Ngao ya Jamii na wataendeleza makali hayo hata katika Ligi Kuu na kuhakikisha wanatwaa mataji ya Ligi Kuu mara 10 mfululizo.Aliwataka mashabiki wa Simba kuujaza Uwanja wa Taifa kama ilivyo ada kwa timu yao ili kudhihirisha kuwa wao ndio mabingwa wa soka nchini na timu bora zaidi kuliko yoyote.Akiizungumzia Azam katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Manara alisema timu hiyo ina kocha mzuri kwa sasa, Etienne Ndayiragije, ambaye ndiye anayeifanya kuwa bora.Alisema, anamheshimu kocha huyo kwa kuwa ana uwezo mkubwa tangu alipokuwa Mbao FC ya Mwanza na KMC ya Kinondoni Dar es Salaam, hivyo hawezi kuidharau Azam FC kwani sasa inafanya vizuri. Viingilio vya mchezo huo ni Sh 5,000 huku VIP ni Sh 10,000, ambapo wapenzi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo.Naye msemaji wa Azam FC, Jaffar Maganga alisema timu yao imejiandaa vizuri kwa pambano hilo na wataibuka na ushindi katika mchezo huo, ambao Simba wanataka kuitwaa ngao hiyo kwa mara ya tano wakati Azam ni mara ya pili.Wakati huo huo, Manara aliwatahadharisha wanaouza jezi feki za Simba kuwa watakumbana na nguvu ya dola uwanjani hapo, kwani watakamatwa na kuchukuliwa hatua mara moja. Alisema watu hao sio tu wanaikosesha Simba mapato, bali wanainyima mapato hata serikali kwa kutolipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
michezo
 Na RAMADHAN HASSAN–DODOMA  ZAIDI ya abiria 150 wamenusurika kifo huku 32 wakijeruhiwa baada ya gari aina ya Isuzu kuigonga treni iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jijini Dar es salaam katika eneo la Hazina jijini hapa.  Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema treni hiyo  ilikuwa na mabehewa 14 ambapo mawili yalianguka na kusababisha ajali hiyo. Alisema ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T 860 APW aina ya Isuzu huku akitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari alipokuwa akivuka makutano ya reli. Alisema mara baada ya gari hilo kuzima, dereva wake Hamisi Salum (49), Mkazi wa Nkuhungu jijini Dodoma, aliruka na kukimbilia na baadaye kujisalimisha polisi. Alisema treni hiyo ilikuwa ikitokea Kigoma  kupitia Mwanza na Mpanda kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa tisa za daraja la  tatu, mbili daraja la kwanza, mgahawa mmoja, behewa la vifurushi na behewa la breki.  “Majeruhi 10  wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wodi namba 1,16 na 17, wengine tumewaruhusu waendelee na safari,”alisema  Kamanda Muroto Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Abul Pumzi, alisema majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo.
kitaifa
THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amefurahi na kusema wachezaji wake walicheza kama watoto, licha ya ushindi wa mabao 3-1 ilioupata timu yake dhidi ya JKT Tanzania juzi Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam. Simba ilipata ushindi huo katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Aussems alisema anaamini kikosi chake kilistahili kushinda idadi kubwa zaidi ya mabao katika mchezo huo, lakini kutokana na umakini mdogo wa wachezaji wake wakapata matokeo waliyopata. “Tumepata ushindi wa mabao 3-1, matokeo ambayo sijaridhishwa nayo kutokana na aina ya wachezaji nilioa nao kikosini, tulitakiwa kufunga mabao manne hadi sita lakini makosa ya kitoto waliyofanya yamesababisha tupate tulichopata,” alisema. Alipoulizwa sababu ya kuwatumia wachezaji ambao baadhi wamekuwa wakianzia benchi alijibu kuwa alifanya hivyo kutokana na wengine kusumbuliwa na majeraha. Aussems alisema wanaanza upya na kuachana na matokeo ya nyuma baada ya timu yake kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya awali na  timu ya UD Songo ya Msumbiji. Wekundu hao walifungashiwa virago, baada ya kulazimisha suluhu ugenini jijini Beira, kisha kutoka sare ya bao 1-1 , Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yaliifanya UD Songo isonge mbele kwa faida ya bao la ugenini. Aussems alisema amewatengeneza wachezaji wake kisaikolojia ili wasahau yaliyopita na kuwekeza akili zao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri Ligi Kuu na kutetea ubingwa wao. “Tulihuzunika kwani haikuwa rahisi kupokea matokeo yale, lakini kwenye mpira lolote linaweza kutokea, hata hivyo tumesahau yaliyopita na sasa macho na nguvu zetu zote tumehamishia Ligi Kuu,” alisema. Simba inashika nafasi ya pili wa Ligi Kuu, ikiwa na  pointi tatu, sawa na Lipuli, Azam, Kagera Sugar, Namungo, Mwadui, Polisi Tanzania na Ruvu Shooting, zikitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
michezo
WASHINGTON, MAREKANI WASIWASI umeibuka barani Asia na kwingineko kutokana na uamuzi wa Serikali ya Marekani kutuma majeshi na mtambo wa kujilinda dhidi ya makombora na meli ya kivita katika eneo la Mashariki, huku uhusiano wake na taifa la Iran, ukiwa kwenye msuguano mkali. Kwa mujibu wa maofisa wa jeshi la nchi hiyo na kukaririwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC wanasema meli hiyo ya kivita iitwayo USS Arlington, inayosafirisha magari na ndege, inatarajiwa kujiunga na kundi la kijeshi la USS Abraham Lincoln katika ghuba. Aidha, wamesema makombora ya US B-52 Bombers pia yamewasili katika kambi moja nchini Qatar, huku Serikali ya Iran ikisisitiza kuwa hatua hiyo ni kitisho kufuatia operesheni za vikosi vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo. Marekani imetoa habari chache kuhusu uwezo wa tishio hilo, ambao utawala wa Iran umepinga na kuita ni kama ujinga, ikitaja hatua hiyo ya Marekani kama vita ya kiakili yenye lengo la kuitishia nchi hiyo. Wakati huo chombo cha habari cha Isna News Agency, kilimnukuu kiongozi mmoja mkuu wa dini, Yousef Tabatabai-Nejad, akisema kuwa ”msafara huo wa Marekani unaweza kuharibiwa na kombora moja pekee.” Idara ya Pentagon ya Marekani juzi ilisema kuwa haitaki vita na Iran lakini wapo tayari kulinda vikosi vya Marekani na mali yake katika eneo hilo. “Idara ya ulinzi inaendelea kufuatilia kwa karibu vitendo vya utawala wa Iran,” ilisema katika taarifa. Iliongezea kuwa mfumo huo wa makombora ambao unaweza kutungua makombora ya masafa marefu na yale ya chini na ndege za kijeshi pia utapelekwa katika eneo hilo iwapo kuna uwezekano wa shambulio lolote. Maofisa wameambia vyombo vya habari vya nchini Marekani kwamba meli hiyo ya USS Arlington ilitarajiwa kuwasili katika eneo hilo lakini imepelekwa katika eneo hilo mapema ili kutoa uwezo wa amri zitakazotolewa na udhibiti. Mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani, John Bolton, alisema kupelekwa kwa vifaa hivyo vya kijeshi kutatoa ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran kwamba shambulio lolote dhidi ya mali ya Marekani katika eneo hilo litajibiwa na uwezo mkubwa wa kijeshi. Idara ya Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa meli hiyo ya USS Abraham Lincoln, ilipita kupitia rasi ya Suez siku ya katikati ya wiki hii. Mwandishi wa BBC anayeshughulikia masuala ya ulinzi na diplomasia, Jonathan Marcus, anasema hilo si jambo la kawaida kwa meli ya kubeba ndege kutumwa katika Ghuba, hatua hiyo itasababisha hofu ya uwezekano wa vita kuepuka kwa ajali ama mipango. Mwaka jana Rais wa Marekani, Donald Trump, alijiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran ambao Marekani na mataifa mengine yalikuwa yameingia makubaliano na Iran 2015. Katika makubaliano hayo, Iran ilikuwa imekubali kupunguza vitendo vyake vya utumizi wa nyuklia na badala yake kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini humo kukagua ili waondolewe vikwazo. Ikulu ya Whitehouse mwezi uliopita ilisema kuwa ingeyaondolea msamaha mataifa matano ikiwemo China, India, Japan, Korea Kusini na Uturuki ambayo yalikuwa yakiendelea kununua mafuta ya Iran. Wakati huo huo Marekani pia imeliorodhesha jeshi la Iran kuwa kundi la kigaidi. Utawala wa Rais Trump unatumia kuishinikiza Iran kuanzisha mazungumzo ya makubaliano mapya ambayo yatasimamia si tu vitendo vyao vya kinyuklia bali pia mipango yake ya uundaji wa makombora ya masafa marefu mbali na kile maofisa wanasema ni tabia yake ya ukandamizaji katika eneo lote la Mashariki ya Kati. Vikwazo hivyo vimesababisha kushuka kwa uchumi wa Iran, vikisukuma thamani ya sarafu yake chini mbali na kuwafukuza wawekezaji wa kigeni na kusababisha maandamano. Iran imetishia kulipiza kisasi kwa kufunga mlango wa Hormuz ambapo mafuta mengi yanayotumika duniani hupitia. Awali Iran wiki hii ilitangaza kwamba imesitisha utekelezwaji wa sheria 2 za makubaliano ya 2015 kutokana na vikwazo ambavyo vimewekwa na Marekani. Pia ilitishia kuanzisha upya mpango wa kutengeneza madini ya Uranium iwapo vikwazo hivyo vitaendelea katika siku 60 zijazo. Mataifa yenye uwezo mkubwa barani Ulaya yamesema kuwa yataendelea kuheshimu makubaliano hayo ya Iran lakini yatakataa masharti yoyote ya utawala huo wa Tehran ili kuyalinda.
kimataifa
NA MWANDISHI WETU, GEORGE Lwandamina amevutiwa kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga, baada ya kuahidiwa mshahara wa dola za Marekani 18,000 (shilingi 38,448,500) ikiwemo marupurupu endapo atashinda ligi na kufanya vyema kwenye michuano ya kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Zambia, Lwandamina ambaye anatajwa kuchukua mikoba ya Hans van der Pluijm aliyejiuzulu mapema wiki hii, aliamua kuitema Zesco United baada ya klabu hiyo kushindwa kumpa mkataba mpya au kuboresha ule uliopo. Taarifa hizo zinaendelea kusema Lwandamina aliyeiongoza Zesco United kufika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu, alikua anapokea mshahara wa dola za Marekani 3,500 (shilingi 7,476,110). “Lwandamina ataondoka baada ya msimu huu wa Ligi Kuu Zambia kumalizika baada ya kufikia makubaliano na Yanga, ukizingatia Zesco wameshindwa kumpa mkataba mpya au kuboresha wa awali,” ilisema taarifa hiyo. Kuondoka kwa Lwandamina anayetajwa miongoni mwa makocha bora Zambia kwa sasa, kumefungua milango kwa wachezaji nyota wa Zesco United kuihama timu hiyo. Wachezaji wanaotajwa kuondoka Zesco United na huenda wakamfuata Lwandamina ni mshambuliaji Mkenya, Jesse Were, beki raia wa Kenya, David Odhiambo ‘Calabar’ na kiungo mchezeshaji, Cletus Chama. Were amekua akihusishwa na Bidvest Wits ya Afrika Kusini, lakini ni moja wa washambuliaji wanaotajwa kuwa kipenzi cha Lwandamina kama ilivyo kiungo Chama.
michezo
Waamuzi hao watakaochezesha mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Azam Tv kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) ni Brian Nsubuga atakayepuliza kipenga na wasaidizi wake ni Bugembe Hussein na Katenya Ronald.Kamishna wa mchezo atakuwa Amir Hassan kutoka Somalia. Kocha Mkuu Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa atawakosa washambuliaji wake watatu katika kikosi ambacho kitaivaa Harambee Stars.Washambuliaji hao ni Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na John Bocco ambaye ni majeruhi wa mguu aliumia wakati wa fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Azam Jumatano wiki hii, Dar es Salaam.“Madaktari wamempa Bocco saa 72 za mapumziko. Bila shaka kabla ya kucheza na Misri atakuwa amepona,” alisema Mkwasa jana asubuhi na kuongeza kuwa Samatta ametuma taarifa kukosa mchezo dhidi ya Kenya kwa kuwa ana ratiba ya kucheza mchezo muhimu Mei 30, mwaka huu, lakini atajiunga na wenzake Jumatano kwa ajili ya mchezo na Misri Jumamosi.Kwa upande wa Ulimwengu, uongozi wa TP Mazembe nao waliomba kumtumia katika mchezo wa ushindani na mpinzani wake AS Vita. Pia kocha huyo anaangalia namna ya kuipanga vyema safu yake ya ulinzi baada ya kumkosa Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano.Mabeki anaotarajia leo ni wale wa pembeni Juma Abdul na Mohammed Hussein, wakati katikati atawategemea Erasto Nyoni, Aggrey Morris na David Mwantika. Viungo waliopo na timu ni Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Farid Mussa na Shiza Kichuya.Washambuliaji ni Elias Maguli na Ibrahim Ajib, ambapo makipa ni Deogratius Munishi au Aishi Manula. “Nimeiandaa timu kucheza mifumo miwili ambayo ni 4-3-3 ambao ni mfumo wa ushambuliaji na pale tutakapokuwa tunazuia basi mfumo utakuwa ni 4-5-1,” alisema Mkwasa.Katika mchezo wa leo Mkwasa anayesaidiana na Hemed Morocco na Manyika Peter anayewanoa makipa atapata nafasi ya kubadili wachezaji hadi sita ambao ni utaratibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mechi za kirafiki za kimataifa, pia makubaliano katika mkutano wa kabla ya mchezo.Stars iliwasili Nairobi, Kenya juzi asubuhi na kupokewa na wenyeji Shirikisho la Soka Kenya, ambako mchana kabla ya kwenda mazoezi ilitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk John Haule. “Msaada wowote mnaotaka na chochote mnachohitaji tunaomba mtutaarifu tujue namna ya kuwasaidia. Msiwe na wasiwasi kabisa,” alisema Dk Haule.
michezo
MBUNGE wa Geita Mjini (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu amewataka wakulima wa zao la pamba kuwa wavumilivu badala ya kuuza pamba yao kwa walanguzi kwa bei ya chini huku serikali ikiendelea kuwatafutia soko zuri.Amesema serikali imeahidi kuwa kama pamba hiyo haitanunuliwa kwa bei elekezi ya kilo moja kwa Sh 800 hadi Agosti, mwaka huu itainunua ili kuwasaidia. Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya wafanyabiashara wengi kushindwa kununua kwa bei hiyo kutokana bei ya soko la pamba duniani kuporoka. Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita juzi, Kanyasu alisema wafanyabiashara wameshindwa kukopa fedha benki kwa ajili ya kununua pamba hiyo kutokana na kukosekana kwa soko la kuiuza.Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya wakulima wamekuwa wakiuza pamba hiyo kwa Sh 500 kwa kilo moja kwa walanguzi hali inayowadidimiza kiuchumi. Kanyasu alitaja hatua ambazo serikali inachukuwa kuwatafutia soko wakulima hao kuwa ni kuzungumza na serikali ya Vietnam ambayo imeonesha kuwa tayari kununua pamba hiyo kwa wakulima.Aidha, aliwaeleza wakulima hao kuwa waziri wa kilimo anapanga kutembelea mkoa huo kwa ajili ya kuzungumza nao. Naye Juma Kaludushi ambaye ni mkulima wa zao la pamba alisema wakulima wengi akiwamo na yeye wamekuwa wakiuza pamba yao kwa walanguzi kwa bei ya chini kwa hofu kuwa itaharibikia mikononi mwao. “Pamba ipo majumbani mwetu muda unakwenda bora tuuze tu kwa walanguzi ili isiharibike kuliko kupata hasara kabisa,” alisema.Mkulima mwingine, Ester Nalamo, alisema amelazimika kuuza pamba kwa bei ya chini ili aweze kuwalipia ada watoto wake kwa kuwa hana chanzo kingine cha mapato zaidi ya zao hilo.
kitaifa
Na MALIMA LUBASHA -SERENGETI FAMILIA ya watu watatu wa Mtaa wa Chamoto, Kata ya Stendi Kuu, Tarafa ya Rogoro wilayani Serengeti mkoani Mara, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watoto wawili wa kike kwa njia ya ukeketaji. Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Pascal Nkenyenge, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Amaria Mushi, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Ikwabe Charali (32), Robi Petro (31) wakazi wa Chamoto na Nyangi Charali (35) mkazi wa Kijiji cha Matare wilayani hapa. Alisema washtakiwa hao ambao ni baba, dada na mke wa mshtakiwa wa kwanza Ikwabe, wanatuhumiwa kuwafanyia ukatili watoto wa kike kwa kuwakeketa Desemba 19, mwaka huu ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi. Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka mawili  yanayowakabili  katika kesi hiyo, walikana kuhusika na tukio hilo kwani walitenda kosa hilo. Hakimu Mushi, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 2, mwakani itakapotajwa tena hivyo kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu. Wakati huo huo, Mkazi  wa Kijiji cha Bonchugu, Kata ya Manchira wilayani Serengeti mkoani Mara, Chacha Matiko (53), amehukumiwa na mahakama hiyo kifungo cha miaka  mitatu  jela na kulipa faini ya  Sh 800,000 baada ya kupatikana  na makosa  ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kuchunga ng’ombe bila kibali. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile. Alisema mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
kitaifa
Na WAANDISHI WETU -MBEYA/IRINGA MAWAZIRI wawili wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, jana walifanya uamuzi mgumu wa kufukuza na kuwasimamisha baadhi ya watendaji ndani ya wizara zao. Wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akivunja Bodi ya Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori Idodi na Pawaga (MBOMIPA), Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Idara ya Forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia, mjini Tunduma. Mbali na kuvunja Bodi ya MBOMIPA kwa tuhuma za ufisadi, Prof, Maghembe pia amevunja mikataba yote ambayo bodi hiyo ilikuwa imekwisha ingia na wawekezaji mbalimbali. Prof. Maghembe pia ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kuanza uchunguzi wake na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuhusika na ufisadi katika jumuiya hiyo. Alichukua uamuzi huo wakati wa ziara yake katika jumuiya ya MBOMIPA na kufanya mkutano na wajumbe wa bodi kabla ya kuivunja. Alisema kuwa anashangazwa kuona MBOMIPA inajiendesha kwa hasara na kuomba kwa wahisani fedha za kujiendesha wakati kimsingi asasi hiyo ilipaswa kuwa msaada mkubwa kwa wanachama wao ambao ni vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo. “Hii ni aibu kubwa kwa chombo hiki ambacho kinapaswa kuwa msaada kwa jamii, chenyewe kimegeuka kuwa ombaomba. Hivi inawezekana vipi MBOMIPA kuomba hadi msaada wa sare na matairi mawili kwa wahisani? Hili ni jambo la aibu, kifupi halikubaliki… hakuna cha mwekezaji hapa wala cha bodi, tunaanza upya, vitu vyote tunaanza sifuri,” alisema Prof. Maghembe. Katika hatua nyingine, waziri huyo ameagiza askari wa vijiji wa wanyamapori (VGS) ambao wanajihusisha na ujangili kukamatwa mara moja. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alimweleza waziri huyo kuwa MBOMIPA ni moja kati ya asasi ambazo zimekuwa zikimsumbua na ndiyo maana siku zote alikuwa hachoki kumtafuta na kumwomba kuingilia kati kutafuta ufumbuzi wake. “Kazi hii nitaisimamia  mwenyewe na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, kama itatushinda basi tutakuwa tumeshindwa kumsaidia Rais Dk. John Magufuli na sitakubali kushindwa na naagiza wote wanaotakiwa kuondoka waondoke wenyewe,” alisema. Mjumbe wa Kamati ya MBOMIPA, Vicent Kibiki, alimpongeza Waziri Maghembe kwa hatua alizochukua na kudai kuwa shida kubwa ni wanasiasa – madiwani na wenyeviti wa vijiji kuvuruga jumuiya hiyo. Diwani wa Kata ya Idodi, Onesmo Mtatifikolo, alikanusha tuhuma dhidi yao akisema hazina ukweli kwani wao huingia katika mkutano mkuu mmoja ambao wanapokea taarifa za jumuiya hiyo na kupitia wao wameweza kuvunja mkataba mmoja baada ya kushinda kesi mahakamani, hivyo alidai wao kazi yao ni kuinusuru jumuiya hiyo. Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Dk. Christopher Timbuka, alisema kuyumba kwa taasisi hiyo ni pigo kwa hifadhi hiyo, hivyo lazima chombo hicho kuwa imara zaidi na uamuzi wa waziri utasaidia uhifadhi na kukomesha ujangili.   Dk. Mpango Kwa upande wake, Waziri Dk. Mpango aliwasimamisha kazi watumishi wanne wa Idara ya Forodha, katika mpaka wa Tunduma kupisha uchunguzi wa madai ya rushwa dhidi yao na kuhusishwa na upotevu wa lakiri 10 zinazotumika kufunga kwenye shehena ya mizigo inayopita mpakani hapo kutoka nje ya nchi. Dk. Mpango aliwataja watumishi hao kuwa ni Harrison Mwampashi, John Makorere, Stephene Josia na Frank Kessy na kuviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama mpakani hapo vinawahoji kuhusu tuhuma hizo. Watumishi hao wanadaiwa kuiba lakiri hizo kutoka ofisi za TRA – Tunduma wanakofanyia kazi, na kwamba nne kati ya hizo zilikutwa zimefungwa kwenye mizigo ya malori yanayoshikiliwa katika mpaka huo baada ya uchunguzi kufanyika, huku malori mengine matano yakizuiwa baada ya kuonekana yana lakiri zilizochezewa. Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya uchunguzi, mawakala ama wamiliki wa malori hayo wamedai kwamba walipewa lakiri hizo na watuhumiwa na kwamba uchunguzi zaidi umebaini kuwa kiwango cha mizigo kilichomo katika makontena yaliyobeba mizigo ya magogo na kufungwa lakiri hizo za wizi, hakilingani na idadi ya mizigo iliyoko katika nyaraka. Kwamba jambo hilo linaashiria kuwa wanazitumia lakiri hizo kudanganya idadi na uzito wa mizigo yao ili kukwepa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali. “Hakuna kitu muhimu kama uadilifu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato na hatutasita wala hatutamwonea aibu mtu yeyote, tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda fedha za umma,” alisema Dk. Mpango. Alisema kuwa Serikali imebaini baadhi ya watumishi wa TRA na idara za forodha mipakani wanashirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuingilia mifumo ya kukusanyia mapato, kitendo ambacho kinaweza kurudisha nyuma juhudi za Serikali kuwahudumia wananchi. Aliwataka wafanyakazi wote wa forodha na Mamlaka ya Mapato, kuwa wazalendo na waaminifu katika kukusanya mapato ya Serikali na kuacha kujihusisha na vitendo vinavyokwaza ufanisi wa mamlaka hayo. Wakati huo huo, Dk. Mpango, ametoa muda wa siku 30 kwa wanaobadilisha fedha za kigeni kiholela mipakani, waache mara moja, badala yake waheshimu sheria za nchi na kuunda vikundi vinavyoweza kuanzisha maduka ya kubadilisha fedha hizo. Pia ametoa muda wa siku ishirini kwa wamiliki wote wa vituo vya mafuta ambao wameomba kupatiwa mashine za kielektroniki kuunganishwa na mfumo wa kodi na utoaji wa risiti wawe wamepata mashine hizo vinginevyo watafungiwa vituo vyao.
kitaifa
Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), imekamata boti moja iliyokuwa inatumika kubeba mafuta wizi kutoka kwenye bomba la mafuta katika Bahari ya Hindi. Boti hiyo imetelekezwa na watu wasiojulikana baada kukurupushwa na walinzi wa doria bandarini hapo  na kufanikiwa kukimbia kwa kupiga mbizi baharini huku boti hiyo ikikutwa na mabomu na milipuko kadhaa. Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, ameiomba serikali kuipatia mamlaka hiyo vitendea kazi muhimu ili kukabiliana na vitendo vya uharamia wa bomba la mafuta katika bahari ya hindi. “Tunaomba tupatiwe vitendea kazi kwa ajili ya kikosi chetu kinachofanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu wa aina mbalimbali bandarini hasa magari ili kukiwezesha kikosi hicho kufanya kazi yake kwa ufanisi,” alisema Kakoko. Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ameahidi kuipatia Bandari hiyo vitendea kazi ambavyo viko ndani ya uwezo wake kama Waziri ili kuongeza udhibiti wa eneo la maji ya bahari lenye bomba la mafuta. “Vitendo vinavyofanywa na wahalifu hao vinakwamisha juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu yake na kusabisha hasara kwa wenye mafuta na kuikosesha Serikali mapato kutokana na vitendo hivyo vya kutoboa bomba na kuiba mafuta,” amsema Dk. Mpango.  
kitaifa
Na CHRISTIAN BWAYA MAJUZI nilizungumza na rafiki yangu mmoja aliyestaafu utumishi wa umma miaka kadhaa iliyopita. Mzee huyu ana vijana wawili ambao kwa sasa ni watu wazima. Wote wawili ni wasomi wenye elimu ya kiwango cha chuo kikuu na wana umri wa zaidi ya miaka 30. Katika mazungumzo yetu, mzee hakufurahia maisha waliyokuwa wanaishi vijana wake hao. “Wote wawili naishi nao hapa nyumbani. Hawataki kuajiriwa na hakuna mwenye dalili ya kuwa na familia inayoeleweka,” anasema kwa masikitiko na kuendelea:  “Huyu wa kwanza mwenye miaka 39 sasa amezaa na mwanamke mmoja hata sijui alimtoa wapi. Walijaribu kuishi hapo Survey kwa miezi sita maisha yakawashinda. Imebidi waje kuishi hapa nyumbani,” “Huwa nikifikiria nasikitika. Hawa vijana wakiwa wadogo niliwapa kila walichokihitaji. Unajua nilipitia maisha magumu enzi za ujana wangu. Tulitoka kwenye familia duni. Sikupenda na wanangu nao wapate shida. Nilijitahidi kuhakikisha hawapitii shida nilizopitia mimi,” anakumbuka kwa masikitiko. Nilimtazama rafiki yangu vile anavyojisikia fedheha kuelezea mambo ya namna hii. Najua katika umri wake angependa kuwa na simulizi la mafanikio ajisikie kama mtu mwenye mafanikio.  Huku akinitazama kama mtu anayejisikia hatia, alijisemea: “Sijui nilikosea wapi. Huwa najiuliza hili swali mara kwa mara. Vijana wakubwa namna hii hakuna kitu wanafanya. Uwezo wa kufikiri maisha ni kama hawana pamoja na kuwa na hizo ‘degree’ walizonazo. “Wakati mwingine najuta. Naona nimechelewa. You get my point? (Sijui unanielewa?) Mtu huwezi kuwa na amani kuwa na mijitu mikubwa hivi haijui kazi. Miaka mitatu imepita nilimkabidhi [mmoja wao] biashara aiendeshe. He was so rough (hakuwa anafanya mambo yake kwa utaratibu) ilibaki kidogo biashara ifilisike. To cut the story short (kufisha habari) ilibidi nimwondoe,” anatikisa kichwa kwa uchungu. Kwa ujumla vijana wa mzazi huyu hawakuwa wanafahamu maisha. Walitegemea kupata mahitaji yao mengi kwa baba yao ambaye kimsingi tungesema ilikuwa zamu yake sasa kutunzwa na watoto wake. Je, nini kimefanya watoto wawe na uzembe wa kiwango hiki? Kuna ukweli kwamba watoto wanaokulia kwenye mazingira yenye kila kitu wanakuwa kwenye hatari ya kunyimwa changamoto. Wanakulia kwenye mazingira ambayo karibu kila wanachokipata kinapatikana. Mtoto akiomba fedha za matumizi hakosi. Mzazi anaamini kwa kumpa kila anachokihitaji basi mtoto atakuwa na utulivu wa kujifunza maisha. Hata hivyo, watoto hawa mara nyingi wanakuwa tofauti na wenzao wanaokulia kwenye maisha ya uhitaji. Shida ya kukosa mahitaji ya kila siku, shida zinazomfanya ajione mtu duni akilinganisha na wenzake wenye nafuu zinaweza kuwa motisha kubwa ya kumsukuma kijana kupanua ufahamu wake. Shida zinakuwa mwalimu wa maisha ya mtoto.  Tunawafahamu watu wengi waliokulia kwenye familia duni lakini waliweza kufika mbali. Watu hawa walikosa ada ya shule, walibangaiza fedha za matumizi lakini kupitia changamoto hizi wakajifunza namna ya kupangilia matumizi, namna ya kuishi na watu ili kupata msaada na hata kujifunza uvumilivu mambo yanapokuwa magumu. Ipo sababu ya mzazi mwenye mafanikio kumsaidia mtoto kutafuta maisha yake. Badala ya kumpa kila senti anayohitaji, mathalani, ni vizuri kumtengenezea mtoto upungufu kidogo utakaomsaidia kujenga nidhamu ya kile alichonacho. Kwa kufanya hivi, mtoto atajifunza namna ya kukabiliana na upungufu hali itakayomfunza upande wa pili wa maisha.
afya
TEL AVIV- ISRAEL MWANAUME wa kwanza  kutangaza wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja, Amir Ohana ameteuliwa kuwa waziri wa sheria na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Waziri huyo Ohana, kutoka chama cha Netanyahu cha Likud, ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa sheria baada ya waziri aliyekuwepo kufukuzwa kazi. Ohana, mwenye umri wa miaka 43, ni mfuasi sugu wa Netanyahu, na aliunga mkono hatua za kumlinda dhidi ya kushtakiwa. Uteuzi wake unakuja siku kadhaa baada ya bunge kuvunjwa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mpya. Inaelezwa kuwa Ohana ametumia juhudi zake zote kuunga mkono muswada tata uliomuwezesha Netanyahu kuwa na kinga ya kutoshtakiwa. Netanyahu alimfuta kazi waziri wa sheria aliyekuwepo madarakani, Ayelet Shaked, miezi mitatu iliyopita. Chama cha Shake, ambacho kilikuwa sehemu ya serikali ya muungano wa Netanyahu, hakikupata viti vya kutosha kukiwezesha kurejea bungeni katika uchaguzi wa mwezi Mei. Waisrael watafanya tena uchaguzi mwezi Septemba baada ya Netanyahu kushindwa kupata uungaji mkono wa kutosha kutoka kwa vyama kumuwezesha kuunda serikali ya mpito. Ikitangaza uteuzi wake, ofisi ya waziri mkuu ilisema Ohana ambaye ana taaluma ya sheria ni mwenye uelewa mkubwa sana mfumo wa sheria. Ohana ni mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja , ambaye anatetea ndoa za jinsia moja, jambo ambalo halitambuliki nchini Israeli isipokuwa kwa wale watakaoamua kufunga ndoa yao nje ya nchi .  Mwaka jana alipinga muswada wa sheria uliopiga marufuku ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja kwa kuzingatia utambulisho. Ingawa haki za wapenzi wa jinsia moja zinapingwa na jamii ya Wayahudi nchini Israeli, kwa ujumla taifa hilo limekuwa na mafanikio katika sheria inayowalinda wapenzi wa jinsia moja . Ohana ni mmoja wa wabunge kadhaa waliotangaza wazi kuwa wanashiriki mapenzi ya jinsia moja na mwaka jana mji wa Israel uliopo karibu na Tel Aviv ulikuwa wa kwanza kuwa na Meya mpenzi wa jinsia moja anayetangaza wazi kuwa anashiriki mapenzi hayo.
kimataifa
RAIS John Magufuli amesisitiza kuwa hakuna mwananchi yeyote atakayelipwa fi dia kutokana na upanuzi wa barabara ya Morogoro katika njia nane kutoka Kimara jijini Dar es Salaam hadi Kibaha, Pwani yenye urefu wa kilomita 19.2.Alisema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi eneo la Kimara Stop Over, Dar es Salaam kwa ajili ya upanuzi wa barabara hiyo. Barabara hiyo ambayo itakuwa ikijulikana kama Tanzania One, upanuzi wake unafanywa na Kampuni ya Mzawa inayojulikana kwa jina la Estim Construction Company Ltd kwa gharama ya Sh bilioni 141.5, ambazo zote zimetolewa na serikali.Wananchi waliokuwa wakiishi kando kando ya barabara hiyo, walivunjiwa nyumba zao miaka ya hivi karibuni kutokana na kujenga kwenye hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi huo. Kabla ya kuvunjiwa nyumba zao, wananchi hao waliitaka serikali iwalipe fidia ya nyumba na viwanja vyao, kwa madai kuwa barabara ndiyo iliwafuata wao; na siyo wao kuifuata barabara.Madai hayo yalipingwa na serikali na kazi ya kubomoa nyumba hizo ikaendelea. Kutokana na wananchi kuendelea kusisitiza kutaka kulipwa fidia, Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kuwadanganya wananchi kuwa wanatakiwa kulipwa fidia, kitu ambacho hakipo. Rais Magufuli alisema serikali ilipotaka kuipanua barabara hiyo ya Morogoro mwaka 1997, waliibuka watu walioongozwa na Profesa Mgongo Fimbo aliyekuwa akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuishitaki serikali Mahakama Kuu kwa kesi Namba 39 ya mwaka 1997.“Mshitakiwa wa kesi hii ilikuwa Wizara ya Ujenzi kwa maana ya Serikali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika kesi ile, Serikali ilishinda na aliyekuwa akiitetea Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, alikuwa Jaji Frederick Werema,” alieleza Rais Magufuli. Alisema baada ya serikali kushinda kesi hiyo na wakati huo yeye (Rais) akiwa Naibu Waziri, walianza kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara na watu waliokuwepo wakati huo wanafahamu.Katika kuhakikisha sheria inafuatwa, bila kumpendelea mtu yeyote, Rais Magufuli alisema miongoni mwa watu waliokumbwa na bomoabomoa hiyo ni pamoja na ndugu yake aliyemtaja kwa jina la Msabila, ambaye sasa ni marehemu. Msabila alibomolewa nyumba tatu, kupisha upanuzi huo. Sheria ya barabara Awali, Rais Magufuli alitumia muda wa kutosha, kuuelimisha umma wa Watanzania kuhusu Sheria ya Barabara iliyokuwepo tangu miaka ya 1930.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko mwaka 1967 na kutamka kuwa upana wa barabara ya kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam eneo la Mnara wa Askari uliopo Posta hadi Ubungo ni mita 22.5 kila upande. Sheria hiyo pia iliendelea kutambua upana wa barabara kutoka Ubungo hadi Kimara Stop Over kuwa ni mita 90 kila upande; kutoka Stop Over hadi TAMCO Kibaha upana wa barabara ni mita121 kila upande; kutoka TAMCO hadi Mlandizi upana mita 22.5 kila upande; kutoka Mlandizi hadi Ruvu upana mita 90 kila upande na kutoka Ruvu kwenda mbele upana mita 22.5 kila upande.“Sheria hii ilifanyiwa tena marekebisho mwaka 2007 na kuongeza upana wa barabara kutoka mita 22.5 hadi mita 30 kila upande nchi nzima na eneo la barabara kutoka Ubungo hadi TAMCO Kibaha, upana uliendelea kuwa mita 90, mita 120 na kwenye Daraja la Ruvu zikiendelea kuwa mita 90,” alieleza Rais Magufuli. Ili kudhibiti uvamizi wa hifadhi ya barabara, Rais Magufuli alisema Serikali iliamua kuweka alama nchi nzima. Aliwataka wananchi kuheshimu alama hizo na wakitaka kuwa maskini waendelee kujenga kwenye hifadhi ya barabara.Alisema kuwa mwelekeo wa nchi ni kujitegemea katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo, kama mpango huo ulivyoasisiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa badala ya kutegemea ufadhili kila wakati, hivyo wananchi hawanabudi kuheshimu sheria kwa kuwa bado miradi mingi itatekelezwa. Demokrasia Licha ya kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya, wabunge wa Chadema, John Mnyika wa Kibamba na Saed Kubenea wa Ubungo, walimwomba Rais Magufuli pia kudumisha demokrasia.Kutokana na hoja hiyo, Rais Magufuli alisema kuwa demokrasia, siyo maandamano na vurugu, bali ni pamoja na vyama vyote kukaa kwa pamoja kama wabunge hao walivyojitokeza, kushiriki sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi. “Hapa leo tumekaa wote na tumewaita viongozi wa vyama vyote na wamezungumza yote waliyotaka, hii ndiyo demokrasia, hata ukifunikwa mdomo usiongee, nayo ni demokrasia, demokrasia siyo fujo, haiwezekani watu wanaandamana kila siku, wanapora maduka wengine wanashindwa kufanya biashara, demokrasia nzuri inahamia bungeni,” alieleza Rais Magufuli.Kauli ya Makonda Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alimshukuru Rais Magufuli kwa kuondoa kero ya maji jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya asilimia 60. Alisema kwa sasa wananchi wa Ubungo hadi Kiluvya wameanza kuunganishiwa maji. Alisema jumla ya Sh bilioni 516 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji kwenye mkoa wake pamoja na ujenzi wa visima 20, vitakavyozalisha lita 200 za maji.
kitaifa
Twalad Salum – Mwanza MKAZI wa Kijiji cha Usagara, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Dementilia Saidia (22), amehukumiwa kifungo cha nje miezi mitatu kwa kujaribu kujiua kwa kujinyonga kwa kitenge. Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Eric Marley, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Ramsoney Salehe alidai kuwa mtuhumiwa huyo alijaribu kujiua kwa kutumia kipande cha kitenge. Alisema katika Kijiji cha Usagara saa 7 mchana Januari 28, mwaka huu, mshtakiwa Dementilia Saidia, akiwa ni mtumishi wa ndani kwa Melesiana Marco (35) alijaribu kujinyonga na kujifunga kitenge shingoni na kujining’iniza jikoni kwenye kenchi na kuokolewa, kinyume cha sheria kifungu cha 217 kujaribu kujiua sura ya 16. Baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka, Hakimu Marley alimuuliza kama ni kweli tuhuma hiyo, na alikiri kutenda kosa hilo baada ya mwajiri wake kumfukuza alipobainika kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu na aliyempachika aliikataa. “Nilichangayikiwa nikaona nijinyonge kwani mwajiri ananifukuza nyumbani na aliyenipa mimba ananikataa,” alisema Dementilia. Mahakama baada ya kumsikiliza mtuhumiwa kwa kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu na ukubwa wa tatizo ilimfunga kifungo cha nje miezi mitatu na kipindi chote atakuwa chini ya maofisa Ustawi wa Jmaii kwa uangalizi wa karibu.
kitaifa
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amemuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kufanya utaratibu wa kuwarudishia silaha aina ya Magobole zilizochukuliwa na serikali wakati wa oparesheni tokomeza ujangili. Mbunge huyo ametoa ombi hilo kutokana na wananchi kulalamika, kuchukuliwa silaha zao na serikali na mpaka sasa hazijarudishwa. Muheshimiwa waziri kwa wazee wa Kiziguwa, Gobole ni heshima kule kwetu hivyo naomba kwa wale ambao hawajabainika kujihusisha na matumizi mabaya ya silaha hizo warudishiwe”, alisema Ridhiwani. Ameendelea kubainisha kwamba wapo wananchi wema na wengine sio wema hivyo serikali itazame namna bora ya kuzirudisha silaha hizo maana malalamiko kutoka kwa wananchi ni mengi kuhusiana na serikali kuwanyang’anya magobole hayo. Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangwalla amesema serikali inatambua kwamba wapo wananchi ambao wanazitumia silaha hizo vibaya kwa kufanya ujangili hivyo watalishughulikia kwa mujibu wa utaratibu.
kitaifa
MWAKA jana Serikali ilitangaza kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Ikaiagiza Hazina kutoa Sh bilioni 18.77 kila mwezi kwa ajili ya kugharimia mpango huo. Rais John Magufuli amekuwa akiutangaza mpango huo kila mara anapopata nafasi ya kuzungumza na wananchi akiwa ziarani mikoani au Ikulu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Suleiman Jafo, amekuwa akisema mara kadhaa kwamba, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya mitihani ya taifa, chakula cha wanafunzi, ada ya wanafunzi kwa wanafunzi wa bweni na kutwa pamoja na fedha za uendeshaji wa shule. Katika miezi sita ya kwanza ya utekelezaji wake, Serikali ilikuwa imetenga Sh bilioni 131.4 kwa ajili hiyo. Sisi pamoja na umma kwa ujumla tulitarajia mpango wa elimu bure uongeze ufanisi na kupandisha ubora wa elimu nchini, hususan katika shule za umma. Hata hivyo, matokeo ya darasa la saba mwaka huu hayaakisi mwenendo mzuri wa ubora wa elimu kwa shule za umma. Matokeo ya darasa la saba mwaka huu yanaonesha kupanda kwa ufaulu kwa asilimia mbili, huku shule nyingi za binafsi zikiongoza katika matokeo ya jumla.         Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), watahiniwa 10 (aliyeshika namba moja hadi 10) bora kitaifa  wanatoka shule zinazomilikiwa na watu au mashirika binafsi. Shule zilizoongoza ni za binafsi pia. Baadhi yake ni St. Peter (Kagera) iliyokuwa na watahiniwa 46 na imeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili imeshikwa na St. Severine (Kagera) iliyokuwa na wahitimu 66, Alliance (Mwanza) iliyokuwa na wahitimu 42 imeshika nafasi ya tatu, wakati nafasi ya nne ikichukuliwa na Sir John (Tanga) iliyokuwa na wahitimu 41. Shule 10 zilizoshika nafasi za mwisho ni Nyahaa (Singida), ya pili ni Bosha (Tanga), ya tatu ni Ntalasha (Tabora), ya nne ni Kishangazi (Tanga), ya tano ni Mntamba (Singida), ya sita ni Ikolo (Singida), ya saba ni Kamwala (Songwe), nane ni Kibutuka (Lindi), ya tisa ni Mkulumuzi (Tanga), huku shule ya mwisho kabisa ikiwa Kitwai ‘A’ (Manyara). MTANZANIA Jumapili tunasema lazima Serikali ijipange kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka katika shule za umma. Fedha inayotolewa na Serikali kugharimia mpango wa elimu bure lazima ionekane kutoa matunda. Na hakuna matunda bora kama kuona idadi ya watoto wanaofaulu kwenda sekondari ikiongezeka. Tunasema kutenga fedha kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa watoto wetu ni mpango mzuri, lakini lazima uendane na mambo mengine, kama kuboreshwa kwa maslahi ya walimu, vifaa, mazingira ya kufundishia pamoja na kudhibiti nidhamu ya walimu. Moja ya sababu ambazo tunadhani shule binafsi zimefanya vizuri ni pamoja na ukweli kwamba walimu wake wanalipwa vizuri zaidi kuliko wale wa shule nyingi za umma. Serikali ilichukulie hili kama changamoto. Ni kweli mpango wa elimu bure umeongeza idadi ya watoto wanaokwenda shule. Awamu zinazofuata za mpango wa elimu bure zijikite zaidi katika kuangalia ubora wa wanafunzi hao.
kitaifa
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC, leo watakuwa katika Uwanja wa Uhuru kumenyana na Ndanda FC, mchezo ambao kama watashinda watazidi kujitengenezea nafasi nzuri ya kuutetea ubingwa wao kwani watabakiza pointi moja kuutwaa.Ili Simba ijihakikishie ubingwa inatakiwa kufikisha pointi 89 ambazo hata ikifungwa mechi zilizosalia bado itakuwa bingwa kutokana na hazina kubwa ya mabao iliyojiwekeza.Yanga inao uwezo wa kufikisha idadi hiyo ya pointi ikishinda mechi zake zote lakini lazima iwe na idadi kubwa ya mabao kuizidi Simba, jambo ambalo ni gumu.Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 85 ilizozikusanya katika michezo yake 34 ilizocheza ikifuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi zake 83 ikiwazidi Simba michezo miwili.Ligi Kuu Tanzania inayoshirikisha timu 20 inaitaka kila timu kucheza mechi 38 ili kukamilisha msimu hivyo kama Simba watapata pointi nne katika mechi ya leo na inayofuata itakuwa mabingwa hata kabla haijamaliza mechi zake.Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu.Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema anajua mashabiki wa timu hiyo wanachokihitaji ambacho si kingine bali ni ushindi, atahakikisha wanafanya hivyo licha ya ratiba kuwabana kwa kuwalazimu kucheza mechi nyingi ndani ya kipindi kifupi.“Tunajua tuna muda mfupi ambao unatubana hata kufanya maandalizi ya nguvu, lakini kwa kuwa tunajua umuhimu wa mechi zetu zilizopo mbele yetu inatulazimu kupambana kivyovyote na kupata ushindi,” alisema Aussems.
michezo
TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa gari maalumu lenye uwezo kupima sampuli 100 za udongo kwa siku imezinduliwa kupima udongo kumhakikishia mkulima uzalishaji mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.Uzinduzi wa teknolojia hiyo kutoka Uholanzi ulifanywa Arusha na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na Naibu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.Akizungumza baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kutoa teknolojia yake nchini kwani italeta mapinduzi katika uzalishaji mazao.“Kupima afya ya udongo kunatoa majibu juu ya ubora wa ardhi, mazao yanayofaa kulimwa eneo hilo, kiwango cha mbolea kinachotakiwa na pia makadirio ya mavuno,” amesema Waziri Ulega.Amesema gharama ya kupima shamba ni Sh 25,000 hadi Sh 30,000 ambazo wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapime mashamba yao kabla ya kilimo kuanza ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake na nini kifanyike ili tija ya uzalishaji iongezeke zaidi.“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tuna kila sababu ya kuhamasisha wakulima kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao linalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema.Naibu Waziri Ulega alisema mageuzi katika sekta ya kilimo yatapatikana kupitia teknolojia ya kupima afya ya udongo na kusababisha kuongezeka uzalishaji wa mazao ya kilimo hali itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao.“Ushirikiano wa serikali na sekta binafsi unachochea kasi ya maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi kuiletea nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) kwa kuwekeza kwenye teknolojia hii,” amesema Naibu Waziri Ulega.Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dk Edmond Matafu amesema magari manne yapo tayari na mashine 100 za mkono za kupimia ambazo zitatumiwa na maofisa ugani kuchukua sampuli za udongo katika maeneo ya vijiji kote nchini.Amesema juhudi za serikali za kujenga uchumi wa kati na viwanda zitatekelezeka nchini kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali ili kuhakikisha vitu vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa maendeleo yaweze kufikiwa.“Upimaji afya ya udongo utafanyika kote nchini kwani tumejipanga vizuri kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo ushirikiano ndio kitu muhimu kufanikisha suala hili ambalo litaenda kuinua uzalishaji wa zao nchini,” ame  sema Dk Matafu.Uzinduzi wa maabara hiyo ulishuhudiwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka nchini Uholanzi, Marjolijn Sonnema na pia Balozi wa Uholanzi nchini, Joroen Verheul.Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Methew Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini, Geoffrey Kirenga.
kitaifa
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo ameipongeza kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kupewa kazi ya kuandaa Maonesho ya Pili ya Viwanda Mkoa wa Pwani na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji.Maonesho ya viwanda yanatarajiwa kufanyika kwa wiki moja kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu kwenye viwanja vya CCM Sabasaba Picha ya Ndege Kibaha.Kongamano linatarajiwa kufanyika Oktoba tatu kwenye eneo hilo. Jokate ameieleza timu ya TSN ofisini kwake kuwa anatarajia maonesho ya mwaka huu yatakuwa na tija kwa Kisarawe na mkoa wa Pwani kwa ujumla.“Mwaka huu mmekuja na timu nzito hivi na mmetembea katika wilaya zote hizi ni matumaini yangu kwamba kutakuwa kuna hamasa kubwa zaidi na hivyo basi tija itapatikana kubwa zaidi”amesema.Timu ya TSN ipo Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maonesho hayo na kongamano.Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo, viwanda visivyopungua 400 vitaonesha bidhaa kwenye maonesho hayo yanayotarajiwa kutembelewa na wananchi wasiopungua 100,000.
uchumi
Na ABRAHAM GWANDU-Arusha WASOMI, wadau wa elimu na wananchi wa kawaida wamekosoa tamko la Waziri  wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wakisema kwamba halijafanyiwa utafiti na halitekelezeki kisheria. Mwishoni mwa wiki, akiwa kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Ndalichako alisema kuanzia mwakani mwanafunzi yeyote hatajiunga na masomo ya Shahada bila kupitia kidato cha sita. Alisema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma. Wakizungumzia tamko hilo kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya wasomi  walisema kabla ya waziri kuanza kutoa amri na matamko, alitakiwa kufanya utafiti kujiridhisha juu ya agizo lake hilo. “Profesa Ndalichako hajasema ametoa wapi ujasiri wa tamko lake, ni kwa utafiti upi aliofanya yeye au hata kukasimu taasisi kwa niaba yake ili ifanye utafiti na kuja na majibu kuwa kidato cha sita ndicho kiwango bora cha kumpitisha mtu kusoma shahada ya kwanza? “Binafsi naona haya ni matamko ya kisiasa yasiyoweza kutekelezwa kisheria, arekebishe sheria kwanza ndio aje kutoa tamko la kurekebisha mfumo wa elimu, vinginevyo anaweza kuharibu kuliko waliomtangulia,” alisema mkuu wa chuo kikuu maarufu mkoani Arusha ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini. Naye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Tawi la Makumira, Mchungaji Profesa Josef Parsalao, alisema pamoja na lengo zuri la kurekebisha mfumo wa elimu, badala ya kuanza na amri na matamko, Serikali ilitakiwa kurekebisha kasoro zilizopo hatua kwa hatua. “Sijui yeye Ndalichako alipitia hatua zipi za elimu, lakini upo ushahidi wa kuwapo kwa wasomi wengi wakiwamo wale wanaofundisha vyuo mbalimbali nchini, kupitia ngazi ya chini kabisa ya cheti na sasa ni maprofesa na walifundisha hawa wanaobeza ngazi hizo. “Wapo majaji ambao walianza kazi ya ukarani mahakamani, wakajiendeleza kwa kusoma Chuo cha Mahakama Lushoto ngazi ya cheti, sasa ni madaktari na maprofesa wa sheria tunawategemea,” alisema Profesa Parsalao. BANA Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, yeye alisema haamini kama alichosema Waziri Ndalichako ni tamko na uamuzi wa Serikali, kwani suala hilo haliko kwenye sera ya elimu na kuonya kuwa alifute haraka kwani hiyo si njia sahihi ya kuboresha elimu nchini. Dk. Bana alikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa jinsi yeye alivyosoma kupitia mfumo huo unaopingwa na Ndalichako hadi hapo alipofikia. “Kama kachukua uamuzi huo, nafikiri amekurupuka, kama anafikiria kidato cha sita ndiyo njia pekee, ameshauriwa vibaya na huo uamuzi aufute haraka sana na ni kinyume na utaratibu wa elimu kote duniani… utakuwa ni uamuzi wa dhambi ya asili na dhambi ya ubaguzi. Kama anataka njia ya kuboresha elimu aje tumfundishe. “Mimi binafsi sikupitia kidato cha sita na kuna maprofesa zaidi ya 20 au 40 ninaowafahamu, yupo Profesa Baregu (Mwesiga Baregu) hakusoma kidato cha sita, kuna Profesa Mathew Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa miaka 14, yupo pia Profesa Cuthbert Kimambo ambaye alikuwa Mkuu wa Taaluma UDSM na wengine wengi, ni watu wanaoheshimika kote duniani,” alisema. PROFESA BAREGU Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu, hakutofautiana na Dk. Bana. Yeye alisema mfumo uliopo unakubalika duniani kote na ndio ulioleta msemo wa ‘elimu haina mwisho’. “Kauli ya waziri imeonyesha umuhimu wa kuwa na tume ya kitaifa ya kushughulikia suala la elimu, kwa sababu kweli kuna tatizo la ubora wa elimu yetu na halipaswi kunyamaziwa, lakini hii si njia sahihi ya kulitatua. “Sijamwelewa waziri kwanini ameona diploma kwenda chuo kikuu ndiyo tatizo na kusema kuwa watu wote wana haki ya kujengewa mazingira ya kujiendeleza kielimu,” alisema Profesa Baregu. PROFESA MPANGALA Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala, alisema anapinga uamuzi huo wa Profesa Ndachako kwani utawanyima watu uhuru wa kujiendeleza. Profesa Mpangala naye aliwataja baadhi ya maprofesa anaowafahamu ambao hawakupitia kidato cha sita na akasema wamekuwa msaada mkubwa kwa taifa. “Profesa Kimambo alikuwa mwalimu wangu wa Kiswahili, yeye alikuwa na elimu ya ualimu ‘Grade’ C wa shule ya msingi lakini amejiendeleza hadi amekuwa Profesa yupo pia Profesa Ndunguru na wengine wengi na waliopitia mfumo wa Cheti-Stashahada wanakuwa na uzoefu mkubwa kuliko wa kidato cha sita na wanafanya vizuri wakifika chuo kikuu,” alisema Profesa Mpangala. TAMONGSCO Akizungumzia kauli hiyo ya Profesa Ndalichako, Katibu Mkuu wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania, Benjamini Nkonya, alisema hawaelewi waziri huyo kutoa tangazo kama hilo ni kwa sababu watu wengi wamekuwa watumishi bora sana na wengi hawajasoma kidato cha sita au vinginevyo. “Wito wetu kwa Serikali ikamilishe mchakato kwa kupeleka rasimu ya sheria mpya ya elimu bungeni, ili pawepo na Baraza la Taifa la Elimu ambalo litakuwa na wawakilishi kutoka sekta ya umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na sekta binafsi kama TAMONGSCO, ambayo itaandaa nyaraka (regulations) zote kabla hazijawekewa sahihi na kamishna wa elimu,” alisema Nkonya. PROFESA MLAMA Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama, yeye alikubaliana na mawazo ya Waziri Ndalichako, akisema mfumo huo ni wa zamani na uliruhusiwa ili kutoa fursa kwa watu kusoma kwa kuwa nchi ilikuwa na wasomi wachache. “Sasa hivi kuna wanafunzi wengi wa kidato cha sita na fursa nyingi za kusoma kidato cha tano na sita zipo, tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma, hakuna ulazima sana wa watu kutegemea njia yingine wakati wanaweza kusoma kidato cha sita na kuwa sawa na wengine darasani,” alisema. LALTAIKA Kaimu Mkuu wa Idara ya Ubunifu, Usimamizi wa Teknolojia na Ujasiriamali katika Taasisi ya Sayansi ya Nelson Mandela, Dk. Amani Laltaika, alipongeza hatua ya Profesa Ndalichako, huku akisema amegundua tatizo katika elimu na amethubutu kuchukua hatua ya kurekebisha kuliko waliomtangulia ambao hawakuchukua hatua yoyote. “Sifa ya kwanza ya kiongozi ni ubunifu na kutatua matatizo yaliyopo, nampongeza waziri kwa kugundua upungufu katika elimu yetu, kwa sababu walikuwapo mawaziri wengi katika nafasi aliyopo sasa, lakini hawakugundua,” alisema Dk. Laltaika. SIFA ZA TCU KUJIUNGA NA VYUO Mwezi Juni mwaka huu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), ilitangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016 na 2017 wanaochukua shahada. Utaratibu huo mpya ulikuja baada ya miezi miwili tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Pamoja na sifa hizo ambazo ziliwahusu waliomaliza kidato cha sita, pia sifa hizo zilieleza kuwa wale watakaodahiliwa kujiunga na vyuo ni pamoja na watakaokuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39 na F=0-38. Sifa nyingine zinazotajwa ni wenye vyeti vya NVA daraja la tatu, wenye ufaulu si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza ka Taifa la Mitihani (NECTA) na Elimu ya Mafunzo ya Ufundi (VETA). Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo. Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni pamoja na kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye Stashahada zisizokuwa za NTA. Imeandaliwa na Abraham Gwandu (Arusha), Jonas Mushi na Mauli Muyenjwa (Dar)
kitaifa
Na Mwandishi Wetu, MAWAZIRI wa zamani, Nape Nnauye na Charles Kitwanga, wamegeuka kuwa mwiba kwa kutoa hoja za kukosoa utendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli. Mwenendo wa makada hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuikosoa Serikali, umeanza kuibuka siku za hivi karibuni baada ya wote kwa nyakati tofauti kuenguliwa katika nafasi zao za uwaziri. Kwa hatua yao ya sasa, wanasiasa hao wanadhihirisha ukweli kwamba wabunge wengi hushindwa kueleza matatizo ya majimbo yao pindi wanapopewa nyadhifa serikalini na wanapotenguliwa wanadai wanapata nafasi zaidi za kuwatumikia wapigakura wao. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai kuwa makada hao walikosa ujasiri wa kuikosoa Serikali walipokuwa wanashikilia nyadhifa zao kutokana na kubanwa na hoja ya uwajibikaji wa pamoja. NAPE Nape ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla uteuzi wake kutenguliwa Machi, mwaka huu baada ya kupokea ripoti ya tukio la kuvamiwa kwa Kituo cha Televisheni cha Clouds, amesikika mara kadhaa nje na ndani ya Bunge akiikosoa Serikali. Akiwa jimboni kwake Mtama alikoenda kuzungumza na wapigakura wake baada ya kutenguliwa, alisema kama matukio ya kuteka watu yataachwa yaendelee, basi CCM itakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Nape alitoa kauli hiyo wakati huo kukiwa na tukio la kutekwa kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki. Wakati akichangia hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wiki iliyopita, Nape alisema kuwa kama CCM isipotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kutowapatia maji wananchi, inaweza kuondoka madarakani. Kauli nyingine ya Nape aliitoa wiki hii alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, aliposema kuwa wananchi wa mikoa ya Kusini hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na kile alichodai vita iliyopo kati ya mataifa makubwa. Aliitaka Serikali isikubali kuona vita hiyo inaendelea kuwaumiza wananchi hao na kuongeza kuwa kama itashindwa kusimamia, wao hawatakubali. Pia kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii wa twitter, Nape, amekuwa akiandika baadhi ya kauli zenye mwelekeo wa kuikosoa Serikali KITWANGA Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alianza kuikosoa Serikali baada ya kutenguliwa mwaka jana, kutokana na ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya Bombardier kutoka Canada ili kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Alisema ndege hizo, si tu hazina mwendo, lakini pia ilikuwa ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia. Kitwanga aliibuka tena wiki iliyopita wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, akisema atawahamasisha wapigakura wake wakazime mtambo ulioko katika chanzo cha maji cha Iherere. Alisema jimboni kwake hakuna maji ya uhakika na tangu mwaka 2008 wananchi wamekuwa wakiyasubiri bila mafanikio. “Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii, sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose.  “Mshukuru nilipokuwa waziri nilikuwa siwezi kusema kitu, sasa nimetoka, tutapambana kwa sababu lazima tuwe na mipango mizuri ya kuwapelekea wananchi wetu maji kama inavyofanyika katika umeme kupitia REA (Wakala wa Umeme Vijijini),” alisema. Kauli hiyo iliibua hasira za Waziri Lwenge wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, ambaye aliita kuwa ni sawa na uasi. Kutokana na kauli hiyo, alimtaka ahame chama kama haoni jitihada za kupeleka maji jimboni kwake zinazofanywa na Serikali. “Kitwanga anaposema atakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Iherere maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake? “Kama ni hivyo, sasa ajitoe kwenye chama kwa sababu Serikali imepeleka fedha na kwa maendeleo yaliyofanyika, ni lazima tuwahamasishe wananchi kutunza miundombinu iliyopo badala ya kwenda kuibomoa.’ alisema. KAGASHEKI Mbali na kina Kitwanga, baadhi ya waliokuwa mawaziri katika Serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete nao pia wamegeuka kuwa wakosoaji wa Serikali. Mmojawapo ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, anayeikosoa Serikali kupitia akaunti yake ya twitter. Kagasheki aliyeangushwa katika ubunge wa Bukoba Mjini na mpinzani wake wa siku nyingi, Wilfred Lwakatare (Chadema), aliwahi kusema kuwa kama nguvu ya Ukawa ingemchagua mgombea makini, basi CCM ingekuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi. Kada huyo wa CCM aliyejiuzulu nafasi yake kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza, aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa twitter: “Kuikosoa Serikali yoyote ile ni jambo la kawaida. Ni vema kuchagua maneno na kulenga hoja bila matusi.” MULUGO Naye Philip Mulugo aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wa utawala wa Kikwete, pia amekuwa akiikosoa Serikali ya Magufuli. Mulugo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Songwe, amesikika bungeni wiki iliyopita akiikosoa Serikali alipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Akichangia bajeti hiyo, Mulugo aliishangaa Serikali kuruhusu vitabu vyenye makosa vitumike shuleni wakati kuna uwezekano wa kuviondoa. Katika maelezo yake, Mulugo alivitaja vitabu vya jiografia vya kidato cha tatu na kiingereza kidato cha nne, kuwa vina makosa yanayoweza kuharibu misingi ya wanafunzi. “Haiwezekani mbili mara mbili mtu aseme ni sita wakati sisi tunajua ni nne. Kwa hiyo, hili suala la vitabu mliangalie vizuri kwa sababu haliko vizuri,” alisema Mulugo. Pamoja na hayo, Mulugo alizungumzia michango inayotozwa na Serikali katika shule binafsi na kusema ni mingi na kwamba inatakiwa kupunguzwa kwa kuwa inawakatisha tamaa wamiliki wa shule hizo. WAPINGWA Kutokana na mwenenedo wa mawaziri hao wa zamani, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) alionyesha kushangazwa na kuamua kuwalipua bungeni. Wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji, Msukuma alisema: “Nilisikitika sana na nataka niwaulize kwamba, nyinyi mawaziri wa Magufuli hivi vile viapo mnavyokula mnajua maana yake? “Kama hamjui maana ya hivi viapo, basi sina hakika kama mko sawasawa na kama hamko sawasawa, Ndalichako (Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi), hebu pitisha operesheni ya vyeti feki huenda hapa penyewe kuna feki za kutosha. “Hivi inawezekana vipi mtu uliyekuwa waziri unasimama hapa na kusema ulipokuwa waziri ulikuwa umebanwa kuzungumza na baada ya kufukuzwa sasa uko huru kuzungumza?” Naye, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wakati wa utawala wa Kikwete, Dk. Cyril Chami, amewafananisha wabunge wa CCM ambao ni vinara wa kuikosoa Serikali kuwa ni kama mke anayetoa siri za ndani ya nyumba yake na mumewe. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili hivi karibuni, Dk. Chami aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema mbunge anapokuwa waziri anakuwa na nafasi nzuri ya kupata fursa na nyenzo za kuwatumikia wapigakura wake.  “Ukiwa waziri una nafasi ya kuwasiliana na waziri mwenzako anayeshughulikia kwa mfano maji. Inakuwa rahisi zaidi kuliko kupiga kelele bungeni. Unajua kupiga kelele sio lazima kwamba mbunge huyo anafanya kazi na hasa ukiwa mbunge wa chama kinachounda Serikali hutarajiwi kuongea kila kitu hadharani.  “Sisi tunafuata mtindo wa Westminster (Uingereza). Waziri hatarajiwi kuikosoa Serikali ambayo yeye ni sehemu yake. “Kama waziri husika ana dukuduku lake kuhusu wapigakura wake jimboni, basi anayo nafasi ya kulisema kwenye Baraza la Mawaziri, kumuona Waziri Mkuu au hata rais mwenyewe. “Hata ukiwa mbunge una jambo kubwa, basi unayo nafasi ya kulizungumza kwenye mkutano wa wabunge wa CCM,” alisema. Kwa mujibu wa Dk. Chami ambaye alipoteza kiti chake cha ubunge katika uchaguzi wa mwaka juzi, alisema mbunge anaweza kuikosoa Serikali ya chama chake, lakini ajue akivuka mipaka anajipotezea sifa za kuwa mbunge wa CCM. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo, alisikika hivi karibuni akisema kuwa chama hakina muda na wabunge wanaoikosoa Serikali. Mpogolo alisema wabunge hao watambue kuwa CCM ni kubwa kuliko wao.
kitaifa
  DODOMA SERIKALI imekana kuitambua Taasisi ya Mfuko wa Elimu ya Juu (TSSF), inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo, wakati akitoa ufafanuzi baada ya Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) kuomba mwongozo kuhusu uhalali wa taasisi hiyo inayojinasibu kutoa mikopo kwa wanafunzi. Amesema si wizara yake wala serikali inayoitambua taasisi hiyo ambayo imekuwa ikitoa matangazo kuwa inatoa mikopo. “Nieleze kwa masikitiko kwamba nimepewa gazeti sasa hivi ambalo linaonyesha tangazo kwamba hii taasisi inawatangazia wanafunzi na inawatoza Sh 30,000 na wanasema watakuwa na mkutano ambao mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako. “Siitambui taasisi hiyo, sitakuwa mgeni rasmi na wala hawajanikaribisha tarehe ya huo mkutano… kwa hiyo nitumie fursa hii kutoa tahadhari kwa Watanzania kwamba wawe makini kwa sababu unapoona mtu anatumia jina lako namna hii ni hatari. “Kama serikali niseme tumelipokea na tutalifanyia kazi ili kujua uhalali wake, lakini kwa kipindi hiki nitoe tahadhari kwa watakaoamua kutoa hizo Sh 30,000 wafanye lakini wajue kwamba serikali hailitambui jambo hili,” amesema Profesa Ndalichako.  
kitaifa
Na ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17 unatia nanga Jumamosi ijayo kwa mechi mbalimbali kuchezwa kwenye viwanja nane tofauti hapa nchini. Msimu huu jumla ya timu 16 zilipata nafasi ya kushiriki ligi hiyo, huku kila mmoja ikionekana kutoa changamoto kwa nyingine. Ushindani ulioonyeshwa msimu huu kwenye ligi umetokana na maandalizi yaliofanywa na kila timu, kulingana na nafasi na fedha walizonazo. Vigumu kutabiri bingwa ninani kutokana na timu zinazowania taji hilo kupishana kwa pointi ndogo, lakini kwa upande wa zile zinazoshuka daraja tayari JKT Ruvu imejiondoa, baada ya pointi walizonazo pamoja na michezo waliyobakisha kushindwa kuwabakiza. SPOTIKIKI wiki hii inakuletea walichopanda na kuvuna timu zote 16 zilizoshiriki ligi msimu huu, ikiwa ni kabla ya mechi za mwisho wa wiki iliyopita. Simba SC Huu ni msimu wenye mafanikio kwa Simba  kutokana na ubora wa kikosi chao, benchi la ufundi pamoja na umoja uliooneshwa na wanachama kwa ujumla wao. Msimu huu Simba ilionekana kufanya usajili makini kwa kuwapa nafasi wanandinga wenye damu changa, jambo lililosababisha kuwa na kikosi imara kila idara na hivyo kutoa upinzani mkubwa kwa Yanga, wanaoonekana ndio wapinzani wao katika mbio  za ubingwa msimu huu. Mbali na taji la ligi msimu huu,  Simba ilionekana kuchanga karata zake vizuri pia kwenye kombe la FA, baada ya kupigana na kufanikiwa kuingia hatua ya fainali  ya kuwania taji hilo litakalowapa nafasi ya kushiriki mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika mwakani iwapo kama watakosa lile la Ligi Kuu. Mbeya City Wagonga nyundo hao wa mkoa wa Mbeya msimu huu si wale walioonekana kwenye  misimu miwili iliyopita, kwani licha ya kuwa na  wachezaji mahiri kama Kenny Ally na wakongwe wa ligi,  Zahoro Pazi pamoja na Mrisho Ngassa,  bado wameshindwa kupata matokeo ya kuridhisha kwa asilimia 100. Mbeya City chini ya kocha wake Kinnah Phiri,imeonyesha ushujaa kwa Yanga tu wakiwa nyumbani, baada ya kuwafunga mabao 2-1 lakini kwenye mechi nyingine wamekuwa si jambo la ajabu kuona wakinyukwa mabao zaidi ya matatu na kuendelea, jambo lililohatarisha mipango yao ya kuwa ndani ya tano bora kwenye msimamo wa ligi, pia kuhatarisha pia kibarua cha kocha Phiri. Kagera Sugar Moja ya timu ambazo hazikuwa na mwanzo mzuri kwenye ligi na hii ni baada  ya kubadilishwa kwa benchi lake la ufundi na kukabidhiwa Mecky Mexime, ambaye alipigana hadi sasa kikosi hicho kuwa miongoni mwa vikosi vinavyowania nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi. Jambo kubwa lililoleta uzima ndani ya Kagera ni mabadiliko ya dirisha dogo la usajili, baada ya kusajiliwa kipa Juma Kasejana  mshambuliaji Ame Ally.  huku Mbaraka Yusuph akionekana kuimarika zaidi katika suala la kucheka na nyavu, hivyo kuipa matokeo mazuri timu yao ambayo kabla ya mechi za mwisho wa wiki ilikuwa ikishika nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 nyuma ya Azam wenye alama 49. Mwadui FC Haina mabadiliko makubwa katika misimu yake miwili ya ligi tangu ilipopanda daraja chini ya kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio', kwani matokeo ya kufungwa na kushinda ni jambo la kawaida kwao. Mwanzoni mwa msimu huu, mambo yameonekana kuwa tofauti baada ya Julio kuamua kuachia ngazi na sababu kubwa akilalamikia timu yake kunyongwa na waamuzi, huku wahusika Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) wakiwa kimya, jambo ambalo kiuhalisia ni kawaida lakini pia kikosi chake hakikuwa cha ushindani. Kuondoka kwa Julio kulitoa nafasi kwa kocha msaidizi Khalid Adam kuvaa viatu, vyake kabla ya kuja kukabidhiwa mikoba Ally Bushir, lakini hakuna mabadiliko yalioonekana kwani hadi michezo 28 imekujana pointi 35, ikiwa nafasi ya sita. Tanzania Prisons Kikosi hiki cha maafande wa Magereza msimu huu wa ligi umeonekana kutokuwa rafiki kwao, baada kutoonyesha cheche walizokuwa nazo msimu uliopita wakinolewa na Salum Mayanga aliyetimkia Mtibwa Sugar, kabla ya kupata dili la kufundisha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Katika msimu huu wakiwa na kocha Abdallah Mohammed ‘Bares’, Prisons wamejikuta wakipoteza michezo 11, sare 10 huku wakishinda mechi saba pekee, hadi sasa wakiwa na pointi 31 wakishika nafasi ya 11, kitu ambacho hakikuonekana kwenye ligi iliyopita na hiyo imetokana na kushindwa kujipanga kuanzia katika hatua ya usajili. Yanga SC Kosa kubwa wanaloweza kujilaumu Yanga msimu huu ni kufanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi kwa kumtoa Mholanzi Hans Van der Pluijm na kumpa majukumu mengine kama Mkurugezi wa ufundi kabla ya kuvunja mkataba wake na nafasi yake ya ukocha kuchukuliwa na Mzambia George Lwandamina, aliyeanza kazi katika duru la pili. Mabadiliko hayo yakichangiwa na migomo ya mara kwa mara kwa wachezaji kutokana na kudai fedha zao za mishahara, kumewafanya wachezaji kutocheza kwa hali na kujikuta wakipoteza mechi hata kwa timu ambazo hazikutegemewa. Licha ya kuwa na nafasi kubwa ya kutetea taji lao la ligi kimahesabu, lakini wanaweza kujikuta wakilipoteza iwapo kama wataruhusu kufungwa kwenye mechi zao zilizobaki kwani hadi sasa wanapointi 62 wakiwa wamecheza michezo 27 na kubaki mitatu mkononi mbele ya Simba, wenye alama sawa lakini wakiwazidi kwa idadi ya mabao ya kufunga kabla ya mechi za mwisho wa juma lililopita. Majimaji FC Imekuwa ni kawaida kwa Wanalizombe kuponea tundu la sindano kushuka daraja, kwani kwa mwaka wa pili sasa wanahaha kujinusuru kushuka daraja. Majimaji  ilianza kuonyesha dalili za kutouweza ushindani wa ligi, baada ya kufanya usajili usiokidhi viwango, kukosa fedha za kuwalipa mishahara wachezaji lakini hata baada ya kumrejesha kocha wao Kali Ongola aliyeinusuru msimu uliopita, bado hali tete inaonekana kuwaandama kwani kwenye msimamo wa ligi kabla ya michezo ya mwisho wa juma ilikuwa nafasi ya 15 ikiwa imecheza mechi 28 na kuwa na pointi 29 mbele ya JKT Ruvu iliyokwisha kuyaaga mashindano hayo. Azam FC Yaliowakuta msimu huu, hakuna aliyetarajia na hiyo inatokana na upinzani waliokuwa wakiuonyesha kwa miaka ya hivi karibuni, kwani wamezoeleka kuonekana kwenye mbio za kuwania taji la ligi na lile la FA, lakini mwaka huu wameshindwa licha ya kufanya usajili wa gharama kuanzia katika benchi la ufundi na hata wanandinga wa kigeni. Msimu huu Azam walianza ligi, wakiwa na benchi jipya la ufundi lililoongozwa na Wahispani  lakini matokeo ya kusuasua katika mzunguko wa kwanza wa yalisababisha Wanalambalamba hao kuvunja mkataba nao na mikoba ikikabidhiwa kwa Aristica Ciaoba, anayeinoa timu tangu kuanza kwa mechi za mzunguko wa pili, akisadiana na mzawa Idd  Nassoro 'Cheche.' Licha ya kubadili benchi la ufundi, Azam imeshindwa kuyafikia mafanikio ya kuliwania taji la ligi pamoja na lile la FA, hivyo kujikuta mwakani wakikosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa yale ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Stand United Ni timu iliyoanza vizuri msimu huu, kiasi cha kuwaaminisha wadau wa soka  kuwa uenda ikawa ndani ya timu mbili bora kwenye msimamo, lakini mgogoro wa viongozi umeweza kuchangia kuivuruga Stand iliyokuwa na kocha Patrick Liewig, kabla ya kukabidhiwa kwa Athumani Bilali ‘Bilo’ na kisha Hemed Morocco. Liewig aliamua kuvunja ndoa na Stand kwa kile alichokidai kuwa ni vuta nikuvute ya malipo ya mshahara wake, baada ya wadhamini wao wakuu kampuni ya madini ya Acacia kujiondoa, sababu kubwa ikiwa ni kuzuka kwa makundi mawili yanayokidhana ya Stand United na Stand Kampuni. Tangu kuondoka kwa Liewig aliyefanya usajili wa timu hiyo msimu huu, wachezaji walianza kupoteza  morari ya kucheza ikichagizwa na makundi yaliojitokeza na hivyo Stand kujikuta ikishuka kutoka nafasi ya pili iliyoshika hadi kuja kuwania nafasi ya tano, hivi sasa ikiwa na pointi 37 michezo 28 nyuma ya Mtibwa Sugar. Toto Africans Msimu uliopita Toto ilionekana kuwa tishio, lakini mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe ndani ya timu umeonekana kuwamaliza. Toto ilianza ligi msimu huu ikiwa na Rogatian Kaijage kabla ya kujiuzulu kwa kile alichodai uongozi kushindwa kutimiza mahitaji ya timu, huku kijiti chake  kikichukuliwa na Halfan Ngasa kisha majukumu kubaki kwa Flugence Novatus, lakini bado matokeo mabovu yaliochangiwa na ukata, migogoro ya mara kwa mara kwa wachezaji imewafanya kuwa katika hati hati ya kushuka baada ya kukusanya pointi 29 katika michezo 27 iliyocheza. Ndanda FC Imekuwa na bahati ya kufundishwa na wazee wawili Hamimu Mawazo na Meja Mstaafu Abdull Mingange, wanaobadilishana vijiti, lakini msimu huu timu hii imeonekana kuwa kwenye hali mbaya kiuchumi iliyoleta pia matokeo yasiyoridhisha uwanjani. Msimu huu wameonekana wakifanya usajili wa funika bovu kiasi cha kujikuta miongoni mwa timu zinazoweza kushuka daraja, kwani kwenye mechi 28 walizocheza wamepata pointi 30 ambazo kama wanaowafuata wataweza kushinda mechi zao zilizosalia nao kupoteza msimu ujao hawatokuwepo katika ligi. JKT Ruvu Licha ya msimu huu kufundishwa na makocha watatu katika vipindi tofauti, lakini imekuwa ya kwanza kuaga Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo msimu ujao wataonekana Ligi Daraja la Kwanza. JKT Ruvu ambayo imefia mikononi mwa kocha, Abdallah Kibaden, kabla ya hapo ilishafundishwa na Bakari Shime aliyepokea mikoba ya Felix Minziro, lakini  msimu huu walianza kuonyesha hali ya kutokuwa vizuri mwanzoni mwa ligi, baada ya kukubali vipigo vinne mfululizo kiasi cha kocha wake Minziro kuamua kujiudhuri. Kabla ya mechi za mwisho wa wiki iliyopita, JKT Ruvu walikuwa wakishika nafasi ya mwisho wakiwa na pointi 23, huku wakibakiwa na michezo miwili ambayo hata kama watashinda watafikisha alama 29 ambazo haziwatoshi kubaki kwenye ligi hiyo. Mtibwa Sugar Ni timu iliyoweza kutoa changamoto kubwa msimu huu, baada ya ujio wa kocha Salum Mayanga, lakini tangu kuondoka kwake imejikuta ikipokea vipigo vya aibu ikiwemo kile cha 5-0 walichokipata kwa Mbao FC, mzunguko wa pili lakini jambo baya kwao wameshindwa kulinda heshima yao ya kutofungwa na Yanga, wakiwa uwanja wao wa nyumbani. Ruvu Shooting Ilibahatika kurejea tena kwenye ligi msimu huu, baada ya kushuka na kujikuta wakishiriki Ligi Daraja la Kwanza  msimu uliopita. Baada ya kupanda  kikosi hicho kilichonolewa na makocha wawili hadi sasa, kimeweza kuonyesha wazi kuwa kushuka kwao daraja haikuwa na maana hawana uwezo,  baada ya kutoa changamoto kubwa kwa baadhi ya timu za Ligi Kuu ingawa wameshindwa kuvua uteja wao mbele ya Yanga. Hadi sasa Ruvu Shooting inasiliami 100 ya kusalia kwenye ligi msimu ujao, baada ya kucheza mechi 28 na kukusanya pointi 33 ambazo zinawabakisha na hii inatokana na kuanza vizuri kwenye mechi zake msimu huu. African Lyon Imepata nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikiwa ni baada ya kuikosa kwa misimu miwili iliyopita, lakini ujio wao haukuweza kuleta changamoto iliyotarajiwa na wengi kutokana na historia waliyowai kujiwekea katika ligi. Walianza ligi na Mreno Bernado Taveres, kabla ya ujio wa Mkenya Charles Otieno, lakini wameonekana kushindwa kutoa changamoto kiasi cha kujikuta mguu ndani, mguu nje kushuka daraja  na hadi sasa wapo nafasi ya 10 wakiwa na alama 31 ambazo wanapishana kwa alama  moja na timu zinazomfuata nyuma, ukiitoa JKT Ruvu iliyokwisha kushuka daraja. Mbao FC Wakati ikiteuliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kucheza Ligi Kuu, mashabiki wengi wa soka walitegemea kuwa  ingekuwa si tu ‘jamvi la wageni’, lakini pia ingekuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu  na hiyo ni kutokana na kuonekana iliteuliwa ghafla, baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembo zilizokubwa na mkasa wa upangaji matokeo katika mechi za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza, hivyo Mbao  kupandishwa kutokana na kuongoza kwenye kundi C. Kupata nafasi ya kushiriki ligi msimu huu, Mbao imeonyesha wazi kuwa haijaja kibahati kama inavyodhaniwa, baada ya kuonyesha usumbufu mkubwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo ikiwemo Yanga na Azam kiasi cha kuitishia pia Simba. Ikiwa na kocha wake Mrundi, Etienne Ndairagije, Mbao imeweza kuzifunga Azam na Yanga katika mechi za Ligi lakini pia kuwatoa Wanajangwani kwenye kutetea taji lao la FA, hivyo kutinga fainali watakayokipiga na Simba Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
michezo
Beatrice Kaiza Waumini wa dini zote watakiwa kuliombea Taifa la Tanzania ili kuepuka majanga. Wito huo umetolewa na mtumishi wa Mungu, Nabii Joshua ambapo amesema wakati mwengine taifa linapofikwa na majanga yanayohatarisha maisha ni muhimu waumini wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuliombea taifa kuepuka majanga na maafa. “Tumeungana kwa pamoja kuwaombea watu wa Moshi kwa kupoteza ndungu zao huu ni msiba wa taifa lakini kwa uwezo wa Mungu ametupa wasaa wa kumshukuru  kwa kila jambo na kumuomba amani,” amesema Nabii Joshua. Amesema Watanzania wanatakiwa kuitumia amani kama tunu ili kujipatia maendeleo. “Amani haiwezi kudumu pasipo kumuomba Mungu aendelee kutujaalia amani hiyo, waumini wote tuungane tuombe Mungu ili pasitokee mtu, kikundi kitakachoweza kuvuruga amani hii tuliyoachiwa na mababu zetu,” amesema Nabii Joshua. Hata hivyo amempongeza Rais John Magufuli kwa kuendelea kutetea wanyonge na kuimarisha uchapakazi hasa kwa vijana. “Rais Magufuli ni Kiongozi wa kipekee anaependa usawa kwa watu wote ndio maana anaitwa rais wa wanyonge hivyo tumuunge mkono na tumuombee pia kwa maana kazi anayofanya sio ndogo hasa linapokuja suala la kuliongoza Taifa,” amesema Nabii Joshua.
kitaifa
HAKUNA msanii ambaye hapendi kupanda juu kisanii. Kila msanii anapenda kufanikiwa. Muhimu kwao ni kuwa na mafanikio. Kinachoendelea ni kutafuta njia za kupanda zaidi na zaidi kisanii. Hapo sasa wengine hujikuta wakiingia kwenye njia zisizofaa. Wapo wale wanaoamini mambo ya kishirikina. Hao huenda kwa sangoma kwenda kuangalia namna ya kupandishwa nyota zao ili wapate mashabiki wengi. Wengine ni wale wanaoamini katika kiki. Hawa ni sampuli za akina Pen Pol, Diamond, Harmonize, Harmorapa na wengine wa namna hiyo. Hao wanaamini bila kiki hawataweza kuwa juu kisanii. Lakini kuna wale wenye mitazamo mizuri zaidi; hawa huamini katika kazi. Naweza kuwataja wasanii wachache ambao kazi zao zinaongea badala ya kiki. Msanii wa kike asiyechuja kwenye Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jaydee’ ni mfano wa wasanii wanaoamini katika kazi bora. Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni aina ya wasanii ambao wanaamini kwenye ubora wa kazi. Mfano ukimwangalia Profesa Jay, hata kabla hajawa Mbunge wa Mikumi, mavazi yake yalikuwa ya heshima. Ni wapi umemuona Profesa Jay akivaa mavazi ya hovyo? Hakuna. Wakati mwingine alipanda jukwaani na suti. yote hiyo ni kulinda heshima yake. Aliamini kwenye mashairi yake na si mavazi. Bongo Muvi yupo Jacob Stephen ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, Ahmed Salim ‘Gabo’ na wengine ambao kazi zao ndizo zinazowaweka juu badala ya kujiingiza kwenye kiki. Ni suala la staili tu, huku lengo likiwa ni lilelile – kutusua kisanii. Tatizo ni pale ambapo tayari msanii ameshapata mafanikio na anapotakiwa kutunza asitetereke. Wasanii wetu wengi wanashindwa kujua kuwa ustaa unatakiwa kutunzwa. Unaweza kuwa juu leo, lakini miaka mitatu baadaye ukashuka na kusahaulika kabisa. Ili jambo hilo lifanikiwe, lazima wasanii waache ubinafsi, washirikiane na wenzao na wasifanye starehe kupita kiasi. Ustaa unalindwa. Ni rahisi kupaa kisanii lakini ni ngumu sana kutunza ustaa wako. Lazima ubunifu uchukue nafasi, uwekezaji wa rasilimali sanaa na hata mali nyingine za kawaida. Mfano wewe ni msanii, lakini ni vyema kuwekeza kwenye biashara mbalimbali. Tumia jina lako kutengeneza fedha. Kipaji chako kiwe na maana kwako. Ukishtuka, badilika.
burudani
Aveline Kitomary -Dar es salaam TAASISI ya Tiba ya Mifupa (MOI) imeingiza nchini mitambo ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) itakayokuwa msaada mkubwa katika tiba hapa nchini. Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi, mitambo hiyo imewasili bandari ya Dar es salaam na inatarajiwa kusimikwa siku chache katika taasisi hiyo. Ujio wa mitambo hiyo mipya na ya kisasa inayotoka Nchini Ujerumani, ni juhudi za Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya hapa nchini. ” Mitambo, Vifaa vingine pamoja na ukarabati wa Chumba vimegharamiwa na Serikali  kwa gharama ya Sh bilioni 7.9.” Alieleza Patrick Mvungi. Awali Mkuu wa Kitengo cha Radiolojia,  Dk. Mechric Mango alisema huduma hiyo itaweza kupunguza rufaa za nje ya nchi. “Maabara hiyo itakuwa na faida ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi, hapo awali wagonjwa walikuwa wanahitaji upimaji wa mishipa ya damu ya kichwani hawa wote walikuwa wanapelekwa nje ya nchi kwahiyo mashine itakapofungwa hawataenda nje na itaokoa fedha nyingi,” alisema. Dk. Mango alisema uhitaji wa mashine hizo ni mkubwa kutokana na kutoa vipimo na matibabu kwa wakati mmoja. “Uhitaji wa huduma hiyo  ni mkubwa sana hapa tuna ‘deal’ na kichwa, uti wa Mgongo na mifupa  sasa wale ambao wana matatizo kwenye ubongo moja wapo ya vipimo vinavyohitajika vikubwa ni hivi. “Wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kufanya au mishipa ya damu ambayo sio ya kawaida  hao wanahitaji hiki kipimo pia mashine hii inatumika kutoa matibabu kuna wale wenye uvimbe kwenye ubongo pia tutatumia hii mashine kwa wale wenye mishipa ya damu kwenye uvimbe ili kuzuia damu nyingi isimwagike,”alieleza Dk. Mango.
afya
KAMPUNI za simu Tanzania zimesema zinaunga mkono agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuhakikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zinakuwa na kasi kubwa ya intaneti ili kuchochea maendeleo.Aidha kampuni hizo zimezishauri nchi wanachama wa SADC zisizo na mfuko maalum wa mawasiliano kama wa Tanzania; kuutumia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wa Tanzania au kuanzisha wa kwao ili kusukuma mbele utekelezaji wa malengo ya jumuiya hiyo ya kuwa na intaneti yenye kasi ifikapo 2025.Alhamisi iliyopita akifungua mkutano wa mawaziri wa sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa, Majaliwa aliziagiza nchi za SADC kuhakikisha mpango huo wa intaneti ya kasi wa mwaka 2018-2025 unatekelezwa kwa kuweka mifumo itakayochochea maendeleo.Kampuni ya Tigo Tanzania imesema inaendelea kupanua wigo wa huduma zake katika maeneo yote ya nchi hasa vijijini ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Mkurugenzi wa Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari, akiwasilisha mada katika mkutano huo wa mawaziri wa SADC mwishoni mwa wiki, alisema Tigo imefikia asilimia 90 ya Watanzania kwa kutoa huduma za mawasiliano, fedha na intaneti. “Nimewaeleza mawaziri wa SADC kuwa tumefanikiwa kufikia asilimia kubwa ya Watanzania wenye mawasiliano kwani zaidi ya asilimia 90 Tigo imewafikia wananchi ikiwa ni kampuni ya pili hapa nchini,” alisema. Alisema mikakati yao ni kuhakikisha nafasi ya pili ambayo wanashika kwa kutoa huduma za simu nchini, inabakia na baadae kuja kuwa viongozi kwa utoaji wa huduma hizo. Karikari alisema mikakati yao itafanikiwa kwa haraka, kutokana na mchango mkubwa wanaoupata kutoka kwa UCSAF na alishauri nchi nyingine za SADC kufanyia kazi agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania, kwa kuanzisha mfuko kama huo au kuutumia huo wa UCSAF. Alisema mfuko huo unatoa ruzuku kwa kampuni za simu ili kusambaza minara ya mawasiliano ili kuhakikisha wananchi wa kila eneo wanafikiwa na huduma za simu.Mkurugenzi huyo alisema iwapo mfumo wa UCSAF utapata nafasi katika nchi nyingine, ni dhahiri mitandao ya simu katika nchi hizo itasambaa kama Tigo ilivyo sambaa Tanzania. Mtaalam wa Uhusiano wa Huduma za Wateja, Tigo Business, Joachim Chuwa alisema kampuni hiyo inaendelea kubuni teknolojia mbalimbali, kuboresha huduma za mawasiliano kwa Tanzania na nchi zote za SADC.Kwa upande wake, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya simu ya TTCL, Laibu Leonard, alisema kampuni hiyo inaunga mkono agizo la Waziri Mkuu, Majaliwa na wana mkakati wa kupanua huduma zao vijijini. Leonard alisema TTCL ina dhamira ya dhati kuwafikia wananchi kote nchini ili kufikia lengo la kuwa na intaneti ya kasi kwa nchi za SADC kabla ya mwaka 2025. “Hivi sasa tupo sehemu nyingi mjini na tumeanza kuenea vijijini kwa kasi. Ukiangalia shughuli nyingi za kilimo zinafanyika vijijini, lengo ni kuwafikia wananchi wengi wa huko na kuwaunganisha katika mawasiliano ili kuchochea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
kitaifa
MADRID, HISPANIA STRAIKA wa Real Madrid, Karim Benzema, amedai kuwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane, ni kama kaka kwake. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi 11 tu za La Liga msimu huu, ambapo tatu aliingia kutokea benchi. Benzema alikabiliwa na lawama katika kampeni, lakini amefanya kazi njema katika mechi ya Real Madrid ya Kombe la Dunia la klabu ambapo walishinda dhidi ya Club America na kutinga fainali. Mshindi wa Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo, aliisaidia timu yake kushinda kwa kufunga goli lake la 500 kwa miamba hao wa Hispania. Baada ya mechi, Benzema aliueleza mtandao wa Teledeporte: “Zidane ni kama kaka kwangu, ni mfano kwangu na ninafurahi kufanya naye kazi. “Haukuwa mwaka mgumu kwangu, nimecheza vizuri katika mechi mbili au tatu. Umekuwa mwaka mzuri sana, ambao nimetwaa mataji na Real Madrid na kufunga mabao mengi.” Benzema amefunga mabao manne ya ligi msimu huu na amefunga idadi hiyo hiyo pia kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wakati klabu hiyo ikitinga fainali kucheza dhidi ya Kashima Antlers, CR7 binafsi amesherehekea goli lake la 500 tangu alipotua Real Madrid. Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, tayari alikuwa ameshafikisha mabao 500 kwa klabu na nchi yake katika goli alilofunga Ureno dhidi ya Malmo hapo awali Septemba 2015 na alitimiza idadi hiyo akiwa amecheza mechi 753 tu. Lakini sasa akiwa amecheza mechi 689 Real Madrid tayari ametimiza mabao 500. Pamoja na mabao 118 ya Manchester United katika mechi 292, mabao matano katika mechi 31 akiwa Sporting Lisbon, rekodi yake Real Madrid inasimamia mabao 377 katika mechi 367. Takwimu hizo zinamfanya kuendelea kuwa mchezaji wa pili kufunga mabao mengi La Liga akiwa amefunga mabao 270 katika mechi 247, akiwa wa pili kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi mwenye mabao 321 katika mechi 359.
michezo
NA FESTO POLEA SOKO la filamu za Tanzania limezidi kujitangaza nje ya nchi baada ya Filamu ya ‘Daddy’s Wedding’ iliyoongozwa na Mtanzania, Honeymoon Aljabri, kushinda tuzo ya filamu bora ya kigeni katika tamasha la filamu za kimataifa lililofanyika juzi katika Hoteli ya Double Tree mjini Houston Marekani. Honeymoon ambaye pia ndiye prodyuza wa filamu hiyo, alisema furaha yake kubwa ilikuwa ni kuitangaza vema tasnia ya filamu nje ya nchi jambo ambalo anaona amefanikiwa katika tuzo hiyo muhimu itakayosaidia kukuza tasnia ya filamu kwa kuongeza chachu kwa waongozaji na maprodyuza wengine kufanyakazi bora na kuzishindanisha katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi. Katika tamasha hilo filamu zaidi ya 5,000 zilishirikishwa lakini filamu 74 tu ndizo zilizofanikiwa kuonyeshwa kwenye tamasha hilo lililokamilika Jumapili. Tamasha hilo lilianzishwa miaka 49 iliyopita katika umri huo mkubwa kuliko matamasha yote ya Marekani, baadhi ya waongozaji wenye majina makubwa wa filamu duniani waliowahi kushinda tuzo katika tamasha hilo ni George Lukas, Steven Spielberg, Ang Lee na Jonathan Damme. Filamu hiyo iliyochezwa katika mbuga ya wanyama ya Saadani na kuandaliwa na kampuni ya True vision & motion art production ya Texas, Marekani, washiriki wake ni pamoja na mwandishi mkongwe na mchambuzi wa masuala ya siasa, Jenerali Ulimwengu, mwanamuziki Banana Zorro, mchora katuni, Nathan Mpangala, mkurugenzi wa kampuni ya PR Tabasam Lucy Ngongoseke, waigizaji, Mama Abdul, Natasha na binti yake, Monalisa pamoja na waigizaji wengine wasio na majina makubwa. Tasnia hiyo pia imejitangaza vema nje ya nchi kupitia kwa filamu mbalimbali zilizoshirikishwa katika baadhi ya matamasha hayo na kushinda ambapo mwigizaji, prodyuza na mwongozaji wa filamu nchini, Omary Clayton, aliibuka kidedea katika kipengele cha msanii bora wa kiume kwenye tuzo za California Online Viewers Choice Awards (COVCA) zilizotolewa nchini Marekani. Pia waigizaji, Elizabeth Michael (Lulu) alishinda tuzo kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi ya Mungu’ kipengele cha Filamu bora Afrika Mashariki ‘Best Movie- Eastern Africa’ na Single Mtambalike ‘Richie’ kushinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili, ‘Best Indigenous Language Movie/Tv Series-Swahili’ kupitia filamu yake ya ‘Kitendawili’.  
burudani
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 imeanza vibaya michuano ya kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Burundi jana.Bao la kuongoza la Burundi lilifungwa dakika ya 62 kwa mkwaju wa penalti na Shaban Mabano, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Prince Louis Rwagasore mjini Bujumbura. Baada ya kuongoza, Burundi iliongeza kasi ya mashambulizi langoni kwa Tanzania na kufunga la pili dakika ya 79 likiwekwa kimiani na Cedric Mavugo.Hadi mchezo unamalizika, Burundi ilitoka kidedea kwa ushindi huo unaowaweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele, iwapo watapata matokeo mazuri pia katika mchezo wa marudiano.Ni wazi sasa kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Bakari Shime kitarudi nyumbani kujipanga upya kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar es Salaam ambapo kikosi chake kitahitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 kusonga mbele.Awali, timu hizo kila mmoja alikuwa akicheza kwa tahadhari ambapo kipindi cha kwanza zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana, hali iliyoibua matumaini kwa upande wa Tanzania kwamba wangepata matokeo mazuri. Lakini hali haikuwa hivyo, kwani kipindi cha pili wenyeji walibadilika na kutumia vema makosa ya Tanzania.
michezo
Tofauti na matarajio ya wengi walioipa Mtibwa nafasi kubwa ya kushinda lakini hali ilikuwa tofauti kwani timu zote zilicheza soka safi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mchezo.Aliyewakosesha Mtibwa ubingwa jana alikuwa Vincent Barnabas aliyekosa penalti ya mwisho iliyopanguliwa na kipa wa Simba Ivo Mapunda.Barnabas hajawahi kukosa penalti katika michuano hiyo, ambayo Mtibwa Sugar ilifuzu hatua ya fainali kwa mikwaju ya penalti 7-6 dhidi ya JKU.Waliopata penalti kwa upande wa Simba ni Awadh Juma, Ramadhan Kessy Isihaka Hassan na Danny Sserunkuma huku Shaaban Kisiga penalti yake ikipanguliwa na kipa wa Mtibwa Saidi Mohamed.Simba ilicheza kwa presha dakika mbili za mwanzo na kuwachanganya Mtibwa huku Haruna Singano akikosa bao katika dakika ya pili. Wachezaji wa Mtibwa waliopata penalti ni Ali Lundenga, Shaaban Nditi, na Ramadhani Kichunga, huku Ibrahim Jeba penalti yake ikigonga mwamba na Barnabas ikipanguliwa na kipa Mapunda.Baada ya dakika chache Mtibwa walitulia na kuanza kushambulia lango la Simba na dakika ya 9 mchezaji wa zamani wa Simba Mussa Hassan Mgosi alikosa bao akiwa na kipa Manyika Peter lakini akapiga nje. Dakika ya 44, Mgosi aliikosesha Mtibwa bao baada ya kupaisha mpira akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.Sekunde chache baadaye, Said Ndemla aliikosesha Simba bao baada ya kupiga mpira nje akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga. Timu hizo ziliendelea kucheza hivyo mpaka dakika tisini ambapo zilitoka sare ya bila kufungana na ndipo ilipoamuliwa zipigiane penalti.
michezo
MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga leo wana kazi ya kuhakikisha wanasaka ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Huo utakuwa mchezo wa tatu wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu wa mwaka 2019/20 Yanga ikicheza kwenye uwanja huo ambapo katika miwili iliyopita imepoteza mmoja na kupata sare moja. Lakini kwa Coastal utakuwa ni mchezo wa nne baada ya kucheza michezo mitatu na kati ya hiyo, ikishinda mmoja, sare moja na kupoteza mmoja. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana msimu uliopita Februari 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Yanga ilishinda bao 1-0.Mchezo wa leo huenda ukawa mgumu na wenye presha hasa kwa wenyeji Yanga wanaohitaji ushindi angalau kuwatuliza mashabiki wao baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania katikati ya wiki hii. Sare hiyo haikuwafurahisha mashabiki wao hasa ikizingatiwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting hivyo, iwapo watashindwa kupata matokeo mazuri tena leo hali itakuwa ngumu kwa Kocha Mkuu Mwinyi Zahera. Timu zote mbili zina washambuliaji wazuri wenye madhara langoni, ukimtazama David Molinga aliyefunga mabao mawili katika mchezo uliopita anataka kuendelea kufunga ili kuendelea kudhihirisha ubora wake na kwa upande wa Coastal hatari zaidi ni Ayoub Lyanga.Safu ya ulinzi ya Yanga bado haijakaa vizuri sana kwa sababu katika mechi mbili wamefungwa mabao manne na kushinda matatu huku Coastal ikionekana kuwa vizuri baada ya kucheza michezo mitatu kufungwa mawili na kufunga mabao matatu.
michezo
Manchester, England KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ameweka wazi kuwa, anahofia kufukuzwa kasi baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kutimiza matakwa yake wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari. Solskjaer amedai kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, aliutaka uongozi huo kuweka mezani kitita cha fedha ambacho kitaweza kusajili wachezaji wanne ambao wangeweza kuboresha kikosi. Manchester United ikatenga kitita cha kusajili wachezaji wawili ambao ni kiungo kutoka Sporting, Bruno Fernandes, aliyejiunga kwa kitita cha pauni milioni 48, pamoja na kumsajili mshambuliaji Odion Ighalo kwa mkopo wa miezi sita. Kocha huyo raia wa Norwey, amedai alikaa chini na makamu mwenyeki Ed Woodward na kumtajia wachezaji ambao anawataka, lakini ameshangaa kuona anawapata wawili jambo ambalo anaamini badi ni mtihani kwake kuweza kufanya vizuri msimu huu. “Kumekuwa na uwekezaji mdogo wa kusajili wachezaji kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, zaidi ya pauni milioni 200 zimetumika kusajili wachezaji tangu nimekuja hapa, lengo la klabu ni kuwa na wachezaji wenye ubora mkubwa ili kuweza kuleta mataji kwenye kikosi. “Lakini kwa uwekezaji huo bado tutakuwa na wakati mgumu, wakati wa uhamisho wa Januari nilitaka wachezaji wanne, lakini wamepatikana wawili, hii inaweza kuwa ngumu kutimiza malengo, hivyo timu ikishindwa kufanya vizuri anayeangaliwa ni kocha, hivyo chochote kinaweza kutokea,” alisema kocha huyo. Leo Manchester United itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kupambana na wapinzani wao Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Manchester United wao wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza michezo 25, wakati huo Chelsea ikiwa nafasi ya nne kwa pointi 41.
michezo
WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji imesema meli ya mv Maendeleo haitauzwa, kwa sababu huduma zake zinahitajika za kusafi risha abiria na mizigo katika ukanda wa Unguja na Pemba.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohamed Ah- mada (pichani), wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Kiwani Pemba, Mussa Ali Mussa aliyetaka kujua lini meli hiyo itafanyiwa matengenezo baada ya kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu sasa. Ahmada alisema jumla ya dola za Marekani milioni 1.3 zinahitajika kwa ajili ya kuifanyia matengenezo meli hiyo ikiwemo kuisafirisha na kuipeleka Chelezoni Mombasa.Alisema hadi sasa jumla ya Dola za Marekani 500,000 tu zimepatikana kwa ajili ya kuifanyia matengenezo meli hiyo. Alisema meli hiyo haiwezi kufanyiwa matengenezo nchini, kwa hivyo lazima ipelekwe Mombasa. “Meli ya mv Maendeleo inahitaji Dola za Marekani milioni 1.3 kwa ajili ya matengenezo makubwa na kuiepeleka chelezoni ili iweze kufanya kazi zake za kutoa huduma za usafirishaji abiria na mizigo katika ukanda wa Unguja na Pemba,’’ alisema.Mapema, Ahmada alisema serikali haina nia ya kuiuza meli hiyo ambapo utafiti umebaini kwamba bado ina tija kubwa kwa serikali. Kwa mfano alisema wapo wafanyabiashara tayari wameonesha nia ya kuikodi meli hiyo kwa ajili ya shughuli zao za kibiashara.‘’Mwenyekiti napenda kuwajulisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba seri- kali haipo tayari kuiuza meli hiyo kwa sababu bado ina tija na faida kubwa za huduma za usafiri kwa wananchi wetu wa Unguja na Pemba,”alisema. Shirika la Meli za Zanzibar linamiliki meli tatu ikiwemo ya mv Mapinduzi 11 pamoja na Maendeleo na meli nyengine ni ya mv Ukombozi inayotoa huduma za mafuta.
kitaifa
FEDHA kutoka Benki ya Dunia zitakapopatikana, zitasaidia kuweka mazingira mazuri na salama shuleni, hasa kwa watoto wa kike.Pia, zitawasaidia wanafunzi wanaoacha masomo kwa kuwapa fursa ya kupata elimu kwa njia mbadala.Fedha hizo zitasaidia kuongeza idadi ya shule kwa ajili ya watoto wa kike, kwa kujenga shule za bweni 26 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 39,000 na shule za kutwa 1,000.Pia, zitatumika kwa ajili ya upanuzi wa shule kongwe 50 ili kuongeza nafasi za wanafunzi 100 wa kike kwa kila shule na kukamilisha maabara.Akizungumza jijini Dodoma wakati wa ziara katika Shule Sekondari ya Wasichana ya Msalato, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema ana matumaini kuwa Bodi ya Benki ya Dunia, itaidhinisha mkopo kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.Profesa Ndalichako aliwashauri Watanzania kuzingatia uzalendo na kuweka maslahi ya taifa mbele katika utekelezaji wa mradi huo, unaofahamika kama Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP).Amesema, mradi huo utawanufaisha wanafunzi milioni 6 katika kipindi cha miaka 5 ijayo.“Mradi huu utawanufaisha wavulana na wasichana, ambao kwa umuhimu mkubwa umelenga kusaidia kupanua upatikanaji wa elimu hususani kwa watoto walio mazingira hatarishi, kwa sababu kila siku inayopita watoto kutoka maeneo hayo wamekuwa wakikosa fursa ya kuendelea na masomo.Alisema inasikitisha kuona baadhi ya watu, wanasali kutaka Benki ya Dunia ikatae kutoa mkopo kwa Tanzania, wakati utawanufaisha ndugu na watoto wa ndugu zao. Hivyo, aliwataka watanzania kuwa wazalendo.“Ni matumaini yangu kuwa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) utapitishwa na Benki ya Dunia, kwa kuwa unakwenda kunufaisha wanafunzi zaidi ya milioni 6 nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kujiunga na elimu ya sekondari” amesema.Profesa Ndalichako amesema serikali imedhamiria kuboresha elimu ya sekondari katika mambo ambayo hayajadiliwa.Alisema pia serikali imeongeza bajeti ya elimu ya sekondari kwa asilimia saba.Akibainisha umuhimu wa mradi huo, Profesa Ndalichako amesema mradi huo utasaidia kukidhi mahitaji ya watoto na kutimiza ahadi za serikali chini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.Alisema mradi huo unatoa fursa ya kuzingatia ubora. Alisema serikali ilifanya utafiti na kuja na vipaumbele, kwa kushirikisha asasi za kiraia na wadau wengine ili kukidhi uboreshaji wa sekta ya elimu na kuwa na tija.“Mradi huo unatekelezwa ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi, mradi huu unaenda kuongeza idadi ya shule kwaajili ya watoto wa kike kwa kujenga shule za bweni 26 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 39,000 na shule za kutwa 1,000, upanuzi wa shule kongwe 50 ili kuongeza nafasi za wanafunzi 100 wa kike kwa kila shule na kukamilisha maabara” amesema.Profesa Ndalichako alisema mradi huo, utashughulikia changamoto katika sekta ya elimu, kwa kuhakikisha wanafunzi wanakuwa shuleni, kwa kuweka mazingira na program salama shuleni.Alisema mradi pia utasaidia wanafunzi wanaoacha masomo, kwa kuwapa fursa ya kupata elimu kwa njia mbadala, kwa kuongeza idadi ya shule za sekondari karibu na jamii na kuhakikisha vifaa, miundombinu, walimu, vitabu na vifaa vya kujifunzia vinapatikana.“Pia mradi huo utasaidia juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa tunatoa fursa ya elimu kwa watoto wa Tanzania, utaimarisha mfumo wa utoaji elimu kwa njia mbadala (AEP) utakaohakikisha wanafunzi wote wanapata fursa ya elimu kupitia njia mbadala yaani elimu nje ya mfumo rasmi” alisema.Mradi huo pia utachagiza ubunifu na tekinolojia ili kuondoa tatizo la kusoma masomo ya msingi, kuandaa wanafunzi kwa masomo na kukuza stadi. Profesa Ndalichako alisema mradi huo pia utapunguza tatizo la wanafunzi kuacha masomo.Alisema kuwa asilimia 5.7 ya wanafunzi, wanaacha shule kwa matatizo mbalimbal ikiwemo ujauzito.Pia alisema kuwa kuna asilimia kubwa ya wavulana wanaacha shule kwa ajili ya shughuli za kiuchumi. Profesa Ndalichako aliwataka wanafunzi wa shule hiyo ya Msalato, kusoma kwa bidhii na kuwa wazalendo kwa nchi na serikali, ambayo imewekeza katika sekta ya elimu kwa manufaa ya kizazi kijacho.Wiki hii Benki ya Dunia iliahirisha kupiga kura ya kuikopesha Tanzania Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya sekta ya elimu nchini.Inadaiwa Benki hiyo, imechukua hatua hiyo, baada ya baadhi ya wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani wa Tanzania, kuiandikia barua benki hiyo na kuiomba kuahirisha kuipatia Tanzania dola hizo milioni 500 za mkopo, kwa madai kuipa mkopo huo Tanzania ni kuwanyima haki wanafunzi wa kike, ambao wamezuiliwa kusoma huku wakiwa na ujauzito kwenye shule za Tanzania.Katika barua hiyo, wanaharakati na wanasiasa hao, walidai kuwa serikali imewanyima haki wanafunzi wajawazito kusoma na badala yake inawahamasisha wanawake kuzaa kwa kadri ya uwezo wao ili kuongeza idadi ya watu wa Tanzania.
kitaifa
 LONDON, UINGEREZA WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ameweka wazi kwamba mipango ya dharura ilikuwa imefanywa wakati alipokuwa mgonjwa sana hospitali akiugua ugonjwa wa virusi vya corona. Katika mahojiano na gazeti la the Sun jana Jumapili, Johnson alisema aliwekewa lita nyingi za oksijeni ili kumwezesha kuwa hai. Alisema uwepo wake katika hospitali ya St Thomas huko London ulimwacha akiwa na hamu ya kutaka wengine wasitaabike kama ilivyotokea kwake na kuhakikisha Uingereza inarejea katika hali yake ya kawaida. Awali, mchumba wake, Carrie Symonds, alisema mtoto wao wa kiume amepewa jina la Wilfred Lawrie Nicholas Johnson. Majina hayo yakiwa yametokana na babu yao na madaktari wawili waliomtibu waziri mkuu Johnson alipokuwa hospitali kwasababu ya virusi vya corona, Symonds aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram. Kijana wao alizaliwa Jumatano, wiki kadhaa baada ya Johnson kutoka hospitali alipokuwa anatibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Katika mahojiano yake kwenye gazeti hilo, Johnson alielezea alivyounganishwa kwenye nyaya kadhaa kufuatilia hali yake na kubainika kwamba “viashiria vilkuwa vinaenda katika upande usio sahihi”. “Ulikuwa wakati mgumu sana, hilo siwezi kupinga,” alinukuliwa akisema, akiongeza kwamba kila wakati alikuwa anajiuliza: “Nitawezaje kuepuka hili?”  Johnson alibainika kuwa na virusi vya corona Machi 26 na kulazwa hospitali siku 10 baadae. Siku iliyofuata, alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. “Ilikuwa vigumu kuamini kwamba ndani ya siku chache tu, hali ya afya ilikuwa imezorota kiasi kile. Madaktari walikuwa wamefanya maandalizi yote kuhusu kile kitakachofanyika iwapo hali itaendelea kuwa mbaya,” Johnson aliliambia gazeti la the Sun Jumapili. Kupona kwake, anasema kulitookana na huduma bora aliopata. Johnson alisema alijihisi mwenye bahati hasa ikizingatiwa kwamba wengi bado wanataabika, na kuongeza: “na iwapo utaniuliza mimi, ‘Je nimepata msukumo wa kuhakikisha wengine hawapitii tabu hii? ‘ Ndio, bila shaka uo ndio ikweli. “Lakini pia nimepata msukumo wa kutaka kuhakikisha nchi yetu inarejea katika hali yake ya kawaida, kuwa imara tena na nina uhakika tutafika tu,” alisema. Idadi kamili ya waliokufa kwa magonjwa yenye kuhusishwa na virusi vya corona nchini Uingereza hadi kufikia sasa ni 28,131, ikiwa ni ongezeko la watu 621 kutokea Ijumaa. Hata hivyo, Naibu Ofisa wa Matibabu Uingereza Dk. Jenny Harries alisema idadi ya wagonjwa wanaotibiwa hospitali kwasababu ya virusi hivyo imepungua kwa asilimia 13 katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
kimataifa
Mwandishi Wetu -Dodoma MRADI wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo. Akizungumza n kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Issa Dinya,  alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula. Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77 na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake. Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko. Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.  “Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi,” alisema Redman. Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini. “Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka,” alisema
uchumi
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Makazi imesema ujenzi katika eneo la Mji Mkongwe umedhibitiwa kulinda masharti ya mji huo ambao upo katika urithi wa kimataifa. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Juma Makungu wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya kuwapo ujenzi holela hususani wa hoteli katika Mji Mkongwe wa Zanzibar .Makungu alisema wizara inafuatilia kwa karibu harakati za ujenzi katika eneo la Mji Mkongwe kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya mji Mkongwe wa Zanzibar. Aliitaja mikakati inayochukuliwa na wizara ni pamoja na kudhibiti ujenzi wa hoteli za kitalii ziliopo katika eneo hilo. ‘’Mheshimiwa Spika nataka kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe imed hibiti kwa kiasi kikubwa ujenzi holela katika eneo hilo ikiwamo hoteli,’’ alisema.Alisema kwa sasa wizara kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya Mji Mkongwe imesitisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa hoteli za kitalii. ‘’Mheshimiwa Spika vibali vya ujenzi wa hoteli za kitalii katika eneo la Mji Mkongwe kwa sasa tumesitisha... tunataka kwenda kwa kufuata masharti ya miji iliopo katika urithi wa kimataifa’’alisema. Mji Mkongwe wa Zanzibar upo katika miji ya urithi wa kimataifa tangu mwaka 2000,ambapo usanifu wa majengo yake na ujenzi unatakiwa kufuata masharti ya kimataifa.
kitaifa
Pazia la Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2019 linafunguliwa leo nchini Misri ambapo Misri ‘Mafarao’  ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo watawaalika Zimbabwe ‘The Warriors’ kunako Uwanja wa Kimataifa wa Cairo (Cairo International Stadium). Misri ndiyo wameandaa michuano hii na wamefanikiwa kuchukua ubingwa wa fainali hizi mara sara watatumia viwanja sita vya kimataifa. Uwanja mkubwa kabisa wa Misri, ambao umewahi kutumika katika fainali za miaka ya 1957, 1974, 1986 na 2006, Uwanja wa Kimataifa wa Cairo (Cairo International Stadium) unaobeba mashabiki 74,100 utatumika pia katika michezo ya Kundi A linalojumuisha timu za Misri, Uganda, DR Congo na Zimbabwe. Mechi za Kundi B, ambalo linajumuisha timu za Burundi, Guinea, Madagascar na Nigeria zitafanyika katika ‘Uwanja wa Alexandria’ wenye uwezo wa kubeba mashabiki 20,000. Mechi zote za Kundi C linalojumuisha timu za Senegal, Tanzania, Kenya na Algeria zitafanyika katika Uwanja wa 30 June uliopo Cairo wenye uwezo wa kubeba watazamaji 30,000 kwa wakati mmoja. Uwanjani wa Al Salaam jijini Cairo unaobeba mashabiki 30,000, utatumiwa kwa mechi za Kundi Kundi D (Ivory Coast, Morocco, Afrika Kusini na Namibia) pamoja na mechi itakayozikutanisha Tanzania na Algeria. Uwanja wa Suez ‘Suez Stadium’ ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 27,000 utatumika kwa mechi za Kundi E linaloleta pamoja Tunisia, Mali, Mauritania na Angola pamoja na ile ya Kundi F kati ya Guinea-Bissau na Ghana. Uwanja wa mwisho utakaochezewa mechi za AFCON mwaka huu ni Ismailia. Unabeba mashabiki 18,525. Mechi zote za makundi za Cameroon zitachezwa humu pamoja na ile ya Kundi E inayokutanisha Angola na Mali. Cameroon iko katika Kundi F pamoja na Ghana, Benin na Guinea-Bissau. Viwanja hivi sita vitaandaa mechi mbalimbali za raundi ya 16-bora kati ya Julai 5 na Julai 7, huku viwanja vya 30 June, Al Salam, Suez na Cairo International vikitumiwa kwa mechi za robo-fainali mnamo Julai 10 na Julai 11. Uwanja wa 30 June utaandaa nusu-fainali moja nao Cairo International nusu-fainali nyingine. Nusu-fainali ni Julai 14. Fainali itakuwa Cairo International hapo Julai 19. Kabla ya fainali, mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itachezewa katika Uwanja wa Al Salaam mnamo Julai 17. Ni mara ya pili Tanzania inashiriki michuano hii ya AFCON. Ilishiriki mara ya kwanza mwaka 1979 nchini Nigeria.
michezo
Mapenzi ni sawa na gurudumu, ni lazima kutiwa nishati ili kubingiria Mapenzi ni gari, huelekea anakotaka dereva, mapenzi mto hufuata mkondo Katika kila uhusiano, upo wakati ule wa kwanza mpokutana na kuamua kuwa meli hii tunakubali kuipeleka ndumakuwili, basi yapo baadhi ya mambo ambayo kila anayetosa katika bahari la penzi hupaswa kujihadhari nayo. Haya ni baadhi ya makosoa ambayo hupaswi kufanya unapokutana na demu kwa mara yakwanza: 1. Kuchelewa. Unapokutana na mume au mke kwa mara ya kwanza usidhubutu kuchelewa. Ikiwa kuna jambo la dharura ambalo lazima linakuchelewesha basi jambo la heri ni kutuma arafa na kujieleza kwa mepema. 2.Kuuliza maswali. Unapomuuliza mtu maswali, anakuwa na Imani nawe. Katika kuuliza maswali, unapaswa kuwa makini ili kutouliza ama kuyajibu maswali ambayo hayafai maana maswali mengine huweza kuwa mtego. 3.Kuzungumza kuhusu mpenzi wa zamani. Usingumze lolote kumhusu mpenzi wa zamani ila unapoulizwa. Unapoongea kumhusi, inaonyesha wazi kuwa ungali na hisia zake na kuwa hupo tayari kusonga mbele. 4.Kuangalia simu. Unapoangalia simu yako kila wakati, unaweza kutatizwa ama kujihusisha kwa mambo mengine yasiyohusu mkutano wenu na hata kugeuza nia zima. 5.Kuzungumza kupita kiasi. Hakikisha kuwa mazungumzo yako yanatiririka na wala huibua masuala yasiyohusu mkutano wenu. Iwapo mlo naye hazungumzi, jaribu kumuuliza maswali mengine ya balagha. 6.Kujishaua kuhusu mapato yako, kazi na kisomo. Kwa jumla si vizuri kujishaua unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza, ijapokuwa una kisomo ama utajiri mkubwa, inakuwa vyema hayo yanapotambulika baada ya muda. Kunao wale ambao wataanza kukuambia eti wajua nimetoka ng’ambo jana na mambo kama hayo, hayafa kamwe.
burudani
Yanga yawatoa hofu mashabiki Na Grace Mkojera YANGA imewatoa hofu mashabiki wake kuhusu ubora wa timu yao na kuwaambia mambo mazuri yanakuja.Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara, wameahidi kufanya vizuri katika michuano ijayo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.Timu hiyo kwa sasa inaendelea na kambi ya mazoezi Morogoro kujiandaa na msimu mpya sambamba na michuano ya kimataifa.Akizungumza na gazeti hili jana Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe alisema kikosi kimeanza kurudi katika morali hivyo muunganiko ukikubali watakuwa na timu yenye ushindani mkali.“Muunganiko ukikubali tu wamekwisha, wachezaji wameanza kuonesha uhai wa timu, wana morali, wanaonyesha juhudi kwenye mazoezi na tunategemea wataendelea hivyo,” amesema.Salehe alisema kikosi hicho kinajipanga kwa mechi ya majaribio dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza Mawenzi itakayochezwa keshokutwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani humo.Alisema tayari wamecheza mechi moja ya kimazoezi na wachezaji wameonesha uwezo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo maalumu wa kumuaga nahodha wao, Nadir Haroub ‘Canavaro’.Kiongozi huyo aliwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwa vile kuna mambo mazuri yanakuja.Katika mchezo wa mazoezi waliocheza dhidi ya timu ya kituo cha michezo Tanzanite Morogoro walishinda mabao 5-1 huku mshambuliaji mpya Haritier Makambo akiwasha moto kwa bao moja, mengine yakifungwa na Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Emmanuel Martin na Pius Buswita.
michezo
Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi tisa, moja nyuma ya vinara wa kundi hilo, Gor Mahia ya Kenya ambayo jana iliishinda Telecom ya Djibouti kwa mabao 3-1 na kufikisha pointi 10.Kwa upande wao, Al Khartoum imefikisha pointi saba na kushika nafasi ya tatu na hivyo kuungana na timu za Gor Mahia na Yanga katika robo fainali kwa kutoa timu tatu katika kundi lililokuwa na timu tano ikiwamo KMKM.Azam FC imeongoza katika Kundi C ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu wakati KCCA ya Uganda imekuwa ya pili kwa kufikisha pointi sita, na katika Kundi B zilizosonga mbele ni APR ya Rwanda yenye pointi tisa na Al Shandy ya Jamhuri ya Sudan yenye pointi nne.Aidha, Malakia ya Somalia yenye pointi tatu imepata nafasi ya timu bora yenye matokeo mazuri na kuitupa nje KMKM katika timu nane zilizoingia robo fainali.Kwa mujibu wa ratiba ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Gor Mahia sasa itaikabili Malakia katika mechi itakayochezwa kesho saa 10 jioni ikitanguliwa na mechi ya saa nane kati ya miamba ya Rwanda, APR na Al Khartoum inayofundishwa na kocha wa zamani wa Ghana, Kwesi Appiah.Kabla ya mechi ya Yanga dhidi ya Azam FC saa 10 kamili jioni keshokutwa, Al Shandy itaanza kwa kuikabili KCCA kusaka tiketi katika nusu fainali zitakazochezwa Ijumaa wiki hii na mshindi wa tatu na fainali ni Jumapili.Yanga imewahi kukutana mara moja na Azam FC katika michuano hii ya Kagame ambayo ilikuwa katika fainali ya mwaka 2012 kwenye Uwanja wa Taifa, ambayo Yanga ilishinda mabao 2-0, ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi.Katika mechi ya jana, Tambwe alifunga bao pekee katika dakika ya 30 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona wa nahodha wa muda mrefu jana, Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye aling’ara katika mchezo huo.Kwa ujumla, katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza vizuri na kushambuliana kwa zamu, lakini Yanga ndio waliopoteza nafasi nyingi za mabao walizopata.Kipindi cha pili, Yanga ndio walioshambulia zaidi wapinzani wao na dakika ya 59, Tambwe alikosa bao baada ya kutengenezewa pasi nzuri na Msuva. Mshambuliaji huyo wa Burundi pia alipoteza nafasi nyingine nzuri tatu.Msuva pia alikosa nafasi nzuri baada ya kutengenezewa na Tambwe kama ilivyokuwa kwa Andrey Coutinho aliyepiga mpira juu ya lango la Al Khartoum baada ya shuti la Niyonzima kugonga mwamba na kurudi uwanjani.Yanga iliwatumia wachezaji wawili ambao hawajacheza katika michuano tangu ianze Julai 18 ambao ni Oscar Joshua, Pato Ngonyani, lakini Joshua alitolewa kabla ya kuanza kipindi cha pili na kuingia Haji Mwinyi Ngwali.Aidha, nyota wake kadhaa kama Donald Ngoma, Deus Kaseke na nahodha Nadir Haroub walikaa benchi, lakini Nadir aliingia dakika za lala salama kuchukua nafasi ya mkongwe mwenzake, Kelvin Yondani. Kipa Ally Mustapha alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.Yanga: Mustapha, Joseph Zuttah, Oscar/Mwinyi, Yondani/ Nadir, Ngonyani, Mbuyu Twite, Coutinho/Geoffrey Mwashiuya, Niyonzima, Tambwe, Malimi Busungu na Msuva.
michezo
NA BADI MCHOMOLO, KILA kukicha Watanzania wanapenda kusikia habari za mchezaji wao wa kimataifa, Mbwana Samatta, ambaye anakipiga katika klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji. Huyu ni mchezaji pekee ambaye anaipeperusha vema bendera ya Taifa kutokana na jitihada zake za kutaka kucheza soka barani Ulaya. Kujiamini kwake kumemfanya atimize ndoto zake, inawezekana kuwa bado hazijatimia lakini Watanzania wengi wanaamini ndoto zake zimetimia. Kwa maelezo ya Samatta ni kwamba, ndoto zake aje kucheza soka la kimataifa hasa katika Ligi Kuu nchini England. Dalili za kutimia kwa ndoto zake zinaanza kuonekana kwa kuwa mchezaji huyo hadi sasa anaonesha uwezo wa hali ya juu katika msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji, huku klabu yake ikishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo minne. Katika michezo hiyo ambayo amecheza, nyota huyo anaongoza kwa ufungaji huku akiwa na mabao 3 katika michezo hiyo aliyocheza, wakati huo anapambana na wapinzani wake watatu ambao wote wana mabao matatu kila mmoja, nyota wa Mouscron ambaye anajulikana kwa jina la Filip Markovic, Jeremy Perbe wa Gent na David Pollet wa klabu ya Charleroi. Samatta alivyoanza kuitumikia klabu ya Simba SC ya nchini Tanzania wala hakuwa na haraka kwa kuwa alikuwa anajua nini anakifanya akiwa uwanjani. Katika michezo yake ambayo alicheza tangu asajiliwe na klabu hiyo alionesha uwezo wake mkubwa na kuwashawishi klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo kuweza kufanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumsajili. Hata baada ya Mazembe kumsajili mchezaji huyo pia alionesha uwezo wake wa hali ya juu huku akiwa na lengo la kutaka kusonga mbele katika ligi kubwa hasa barani Ulaya. Hata hivyo, amefanikiwa kufanya hivyo japokuwa bado kuonekana katika ligi ya nchini England, lakini kuna uwezekano mkubwa wa msimu ujao kupata timu nchini humo kama ataendelea na kazi yake ya kujituma na kupachika mabao. Lakini kwa wachezaji wengine wa hapa nchini akili zao ni kuja kucheza soka katika klabu ya Simba, Yanga na Azam FC, lakini si wengi ambao wanafikiria kuja kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kama ilivyo kwa Samatta. Ninaamini kama wapo wachezaji wengi ambao wana mawazo kama Samatta, basi soka letu lingebadilika na lingekuwa na ushindani wa hali ya juu kwa kuwa wangeonesha uwezo mkubwa hasa pale wanapokutaka na timu nyingine za mataifa mbalimbali. Ninatamani kuona siku moja kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ akiita kikosi chake huku wachezaji mbalimbali wakiwa wanatoka katika klabu kubwa barani Ulaya na sehemu nyingine na kuungana pamoja kwa ajili ya kuja kulisaidia taifa lao. Lakini wachezaji hawa ambao wanacheza Ligi Kuu nchini Tanzania wakiendelea kufikiria kucheza soka katika klabu ya Simba, Yanga na Azam, basi tutashindwa kufanya vizuri kimataifa kama watashindwa kujituma na kupata nafasi ya kucheza soka nje na kupata changamoto mpya. Ni vizuri wachezaji wetu wakawa na wivu kwa mafanikio ya Samatta na wawe na lengo la kwenda kucheza soka nje, inawezekana kama watakuwa tayari na kujitoa.
michezo
KAMPUNI tatu kati ya tisa zilizoomba kununua ufuta katika wilaya tatu za mkoa wa Lindi kwa njia ya mnada zitanunua kilo milioni 1.8 kwa bei ya Sh 2,860 na Sh 2,852.Hiyo ilibainika katika mnada wa mwanzo kata ya Mbondo wilayani Nachingwea mkoani Lindi, kwenye eneo linalosimamiwa na chama kikuu cha ushirika cha Runali mkoani Lindi. Kwa mujibu wa taarifa, ufuta huo ni wa wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale na ulikuwa mnada wa kwanza kwa chama hicho cha Runali msimu huu.Katika mnada huo wa kwanza kwa msimu huu kwa wakulima wa wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale na kuendeshwa na chama kikuu cha Runali na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya Nachingwea, Rukia Muwango wito ulitolewa kwa wakulima kulipwa kulingana na mwongozo wa mkoa. Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango alisema pamoja na kuridhishwa na mnada ulivyoendeshwa na wakulima kuridhia kuuza alisisitiza malipo ya mkulima yamfikie ndani ya siku tatu za kazi baada ya kuuzwa mnadani.Naye, Kaimu Mrajis wa Ushirika Mkoa wa Lindi Robert Nsunza aliwataka viongozi wa vyama vya msingi kuandaa taarifa ya malipo kadri ya walivyopokea ghalani na kuiwasilisha benki haraka iwezekanavyo ili malipo kwa mkulima kupitia akaunti yake yaweze kulipwa kama ilivyofanyika kwa chama cha Lindi Mwambao katika minada ya wilaya za kilwa na Lindi.Akifunga mnada huo, Mwenyekiti wa chama kikuu cha Runali, Hassan Mpako alisisitiza wakulima kuzingatia ubora wa ufuta wanaopeleka ghalani ili kuvutia wanunuzi na kuimarisha bei. Hata hivyo, wako baadhi ya wakulima walieleza kuridhishwa na bei huku wakionesha wasiwasi wa kutolipwa kwa wakati.Wakizungumza kwa wakati tofauti wakulima Shaban Makeru, mkazi wa Mirui Liwale na Lucas Mchaya mkazi wa Mbondo Nachingwea walisema kwamba kila mtu anaelewa kinachoendelea katika korosho na kutaka hilo lisijitokeze katika ufuta. Msimu uliopita wa mwaka jana ufuta uliuzwa hadi Sh 3,800 kwa kilo na kuamsha ari ya wakulima kulima kwa wingi zao hilo kwa kutumia mbegu bora zinazozalishwa na kutafitiwa na taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Naliendele.
kitaifa
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MWANAHABARI mkongwe na mkuu wa wilaya mstaafu, Muhingo Rweyemamu ambaye alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Aga Khan   Dar es Salaam, atazikwa katika makaburi ya Kinondoni kesho. Muhingo alikutwa na mauti wakati akitibiwa katika hospitali hiyo, akisumbuliwa na ugonjwa wa Myelofibrosis ambao hudhoofisha uwezo wa kinga za mwili kutengeneza damu. Akizungumza na MTANZANIA, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda ambaye pia alikuwa rafiki wa marehemu, alisema baada ya kikao cha mashauriano, imekubaliwa kwamba  Muhingoi atazikwa kesho. “Shughuli za mazishi zitatanguliwa na ibada ya kumuaga ambayo itafanyika katika Kanisa la KKKT Mbezi (Kibanda cha Mkaa). “Mwili wa marehemu Muhingo unatarajiwa kufikishwa nyumbani kwake Mbezi Luis Jumatatu ambako utalala hadi  Jumanne. “Ratiba ya shughuli nzima na taratibu kamili za mazishi zinatarajiwa kutolewa kesho (leo) Jumatatu,”alisema Kibanda. Akizungumza juzi na gazeti hili, Msemaji wa familia ambaye pia ni kaka wa marehemu, Elisa Muhingo, alisema kwa   takribani miaka 11, Muhingo alikuwa anaumwa na kuwekewa damu mara kwa mara na kwamba mwaka jana alizidiwa. Enzi za uhai wake, Muhingo alitambulika vema kama mwalimu mbobezi na kiongozi mahiri katika masuala ya habari kwa waandishi wengi ambao wanaendelea kuitumikia tasnia hiyo. Pia ni mmoja wa waanzilishi wa gazeti la Mwananchi. Umahiri wake ndani ya tasnia ya habari ulijitanua na kufahamika vema kuanzia mwaka 1993 alipoanza kuripoti kwenye magazeti ya Mwananchi na The Express. Mazingira ya kubobea zaidi katika uandishi yalimpandisha hadhi mwaka 1995 na kuwa mwandishi mwandamizi, Mhariri wa Makala, Mhariri na Mkuu wa Kitengo cha Picha katika Gazeti la Mtanzania. Ndani ya utumishi wake katika ngazi ya uhariri, Muhingo, alitumikia magazeti mbalimbali   nchini na baadaye kuwa  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd. Mbali na ubobezi wake katika tasnia hiyo, pia Muhingo amepata kutumikia nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Makete na Morogoro Mjini.   WASIFU Mwaka 2004 Muhingo alihitimu masomo ya Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari (BAJ) katika Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa. Mwaka 1993 alihitimu Stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha TSJ. Mwaka 1989 alihitimu Stashahada ya Elimu katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dar es Salaam. Mwaka 1983 alihitimu Astashahada ya Elimu katika Chuo cha Ualimu cha Tukuyu na mwaka 1977 alihitimu Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Nyakato. UZOEFU KAZINI Mwaka 1984-1985 alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Igwata, Geita. Mwaka 1985-1987 alikuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Makongo, Dar es Salaam. Mwaka 1989 alikuwa Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Mwaka 1989-1992 alikuwa Katibu Uenezi Taifa wa Chama cha Wanataaluma ya Uenezi. Mwaka 1993-1995 alikuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi na The Express. Mwaka 1995-1998 alikuwa Mwandishi Mwandamizi , Mhariri wa Makala, Mhariri na Mkuu wa Kitengo cha Picha katika Gazeti la Mtanzania. Mwaka 1999 alikuwa Mhariri Mkuu wa Jarida la Wiki Hii. Mwaka 1999-2001, alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi. Mwaka 2003, alikuwa Mwakilishi wa Jarida la habari za mazingira la ENS la Marekani. Mwaka 2004-2005, alikuwa Mhariri Mshiriki akihusika na mambo ya siasa katika Gazeti la Citizen. Mwaka 2006-2008 alikuwa Mhariri wa Gazeti la Rai. Mwaka 2008-2010, alikuwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.
kitaifa
Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM SIKU moja baada ya vyombo vya habari vya kimataifa kuripoti tetesi kwamba Rais Mteule Burundi, Evariste Ndayishimiye mgonjwa, Rais Dk. John Magufuli amezungumza naye kwa njia ya simu. Zaidi Rais Magufuli amempongeza kwa uamuzi wa Mahakama ya Katiba nchini Burundi iliyoagiza Rais huyo mteule aapishwe haraka. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson  Msigwa, katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemtakia heri Ndayishimiye kuelekea kuapishwa kwake  hivi karibuni kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Rais Magufuli amemhakikishia Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa karibu na Burundi kwa kuwa nchi hizo ni majirani, marafiki na ndugu wa kihistoria. Rais Magufuli amerudia kumpa pole kwa msiba wa kuondokewa na Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia Juni 09, 2020. Amemueleza kuwa yeye na Watanzania wote wanaungana na Warundi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Amemuomba kufikisha salamu zake za rambirambi kwa Warundi wote na kuwasihi waendelee kuwa watulivu na wastahimilivu. Kabla ya uamuzi huo wa Mahakama ya Burundi kuagiza Rais huyo mteule aapishwe haraka juzi  Baraza la Mawaziri nchini humo lilisema litaongoza nchi hiyo hadi rais mpya atakapoapishwa. Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia mkutano uliyofanywa siku ya Alhamisi chini ya uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza Gaston Sindimwo. Wakati Baraza hilo la Mawaziri likifikia uamuzi huo kabla ya ule wa mahakama, Katiba ya nchini Burundi inaonyesha wazi kuwa Spika wa Bunge la kitaifa, Pascal Nyabenda alitakiwa kuapishwa kushikilia wadhifa wa Rais kwa kipindi cha mpito hadi Rais Mteule atakapoapishwa rasmi kuchukua hatamu ya uongozi. Awali kabla ya kifo cha Rais Nkurunziza, rais huyo mteule ilikuwa aapishwe mwezi Agosti baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwezi Mei. Juzi pia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC liliripoti taarifa ambazo ilisema hazijathitibitishwa zilizoeleza kuwa Rais huyo Mteule, Jenerali Évariste Ndayishimiye, pia ni mgonjwa. Taarifa hizo zilieleza kuwa mke tu ndiye aliyeonekana na  alipigwa picha akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Ndayishimiye lakini rais huyo mteule hajaonekana hadharani
kitaifa