content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Juzi Tiboroha alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo hali ambayo imezua mtafaruku mkubwa kwa wanachama wa klabu hiyo, ambao baadhi yao hawataki ajiuzulu. Manji jana alizungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi suala hilo la kuondoka kwa Tiboroha.Alisema kuwa hali ya kutokuelewana na katibu huyo ilitokana na sakata la mchezaji Niyonzima, ambapo alisema kuwa katibu huyo alikuwa na chuki binafsi na mchezaji huyo akitaka afukuzwe kuichezea Yanga.Alisema kuwa Tiboroha alificha taarifa muhimu za mchezaji huyo kutoka Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) zilizotumwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuhusiana na kuchelewa kwa mchezaji huyo kuichezea.Alisema kuwa badala yake aliendesha kampeni kuwa mchezaji huyo amechelewa bila ya taarifa hali iliyosababisha kuonekana kuwa hana nidhamu.Alisema kuwa sio kawaida kwa mchezaji mwenzake Niyonzima anayechezea Azam FC ambaye barua yake ilipokelewa na klabu ya Azam, lakini ile ya Niyonzima kuja Yanga ilipokelewa na Tiboroha na hakuiwasilisha kunakohusika ili kumharibia mchezaji huyo.Alisema kuwa hali hiyo ilikuwa ni kutokana na chuki binafsi kutoka kwa katibu huyo hali ambayo ilizua hali ya chuki kwa mchezaji huyo dhidi ya mashabiki na wachezaji wenzake kwa ujumla.Manji alisema kuwa, hiyo ni moja kati ya mambo mengi ambayo katibu huyo amekuwa akiyafanya, ambapo amekuwa akificha uozo wake huo kwa kujidai kuwa yeye ni mtendaji mwema huku akitumia baadhi ya vyombo vya habari kumtetea na kumsafisha.Alisema kuwa ndani ya miezi 12 ya uongozi wake amechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kasi mapato ya klabu hiyo huku matumizi ya klabu yakizidi kupanda mara nne kutoka milioni 500 kwa mwaka hadi kufikia bilioni 2.“Kabla yake klabu ilikuwa imekaribia kujikomboa na kuanza kujitegemea, lakini alipofika aliamua kujishirikisha kwa ukaribu zaidi na TFF na kukubaliana nao karibia kwa kila kitu na kujikuta akishusha mapato ya klabu,” alisema Manji.Alisema kuwa katibu huyo alikuwa kwa maslahi yake binafsi huku akichukua kila fursa ambayo ilikuwa inaenda klabuni hapo kwa maslahi yake binafsi.Alisema kuwa Yanga ilialikwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA, kwenye semina ya mafunzo iliyofanyika nchini Ghana, lakini katibu huyo alijichagua mwenyewe bila ya kushirikisha Kamati ya Utendaji, alichukua cheti cha ugonjwa na kisha akajidai anaumwa, lakini akasafiri kwenda kwenye mafunzo hayo.Alisema kuwa katibu huyo alimwathiri mchezaji Ngoma wa klabu hiyo kwa kumwambia kuwa anatakiwa kwenda Uturuki kwa majaribio huku mchezaji huyo akitakiwa kuwa katika michuano ya Mapinduzi hali ambayo iliathiri uchezaji wa Ngoma kwenye michuano hiyo.Alisema kuwa amesababisha kupotea kwa kitita cha dola za Marekani 5,000 baada ya kuikopesha timu ya Botswana ya BDF, lakini fedha hizo hazijarejeshwa hadi leo. Alisema kuwa alimtaka katibu huyo aandike barua ya kijiuzulu ili kulinda heshima yake baada ya kurejesha fedha hizo na katibu huyo alifanya hivyo Ijumaa iliyopita.Alisema kuwa kwa sasa nafasi yake inashikiliwa kwa muda na Mhazini wa Yanga, Baraka Deudeit huku Omar Kaya akisimamia wanachama wa klabu pamoja na kusaidia maandalizi ya uchaguzi.Alisema kuwa Jerry Muro anaendelea kuwa ni msemaji wa klabu huku Mkuu wa Kitengo cha Fedha Faidhal Mike atashirikiana na Justina atakayekuwa Mhazini msaidizi wa klabu hiyo.Alisema kuwa klabu ya Yanga itatumia kampuni binafsi kushugulikia masuala ya masoko pamoja na sheria. Alisema kuwa amemwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kuhakikisha kuwa anaandaa tarehe ya uchaguzi ikiwa pamoja na kupewa majina mapya ya kamati hiyo.Aliongeza kuwa hata kwa upande wake yeye kama Mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo pia atagombea nafasi hiyo. Pia Manji aligusia suala zima la kuuzwa kwa mchezaji wa klabu hiyo Kpah Sherman, kuwa ameuzwa kwa kitita cha Sh milioni 33 katika timu ya Black Aces ya Afrika Kusini.
michezo
HARARE, Zimbabwe MASWALI yameibuka iwapo kiongozi wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe au mkewe Grace wamepanga kutumia chama kipya kuwania urais katika uchaguzi ujao. Mjadala huo umezuka baada ya wanasiasa wakongwe ambao ni washirika wa karibu wa Grace, kuunda chama kipya cha New Patriotic Front (NPF). Hata hivyo, binamu yake Mugabe, Patrick Zhuwao amekanusha madai hayo huku akisema kuwa kiongozi huyo mkongwe aliyeng’atuliwa madarakani  Novemba, mwaka jana, hatawania urais tena. Wanasiasa wakongwe wanaodaiwa kuunda chama hicho, wameishutumu Jumuiya ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika (AU) kwa kushindwa kuyashutumu mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Serikali ya Mugabe, mwaka 2017. “Si kweli kwamba Mugabe analenga kurejea tena katika siasa. Hatuwezi kumtwika tena mzigo wa kuongoza nchi, mzee anapumzika,” alisema Zhuwao bila kugusia kuhusu Grace. Mugabe, 93, ambaye aliongoza nchi hiyo tangu 1980, aling’olewa mamlakani mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo katika kile kilichoonekana ni ‘kuzima’ ghafla ndoto ya mkewe Grace, kumrithi.
kimataifa
KOCHA Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja (pichani) amesema kazi iliyoko mbele yao ya kuwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sio ndogo hivyo, wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri.KMC itaanza kucheza mchezo wake wa kwanza ugenini Agosti 8, mwaka huu dhidi ya AS Kigali ya Rwanda na baadaye kurudiana Agosti 23, mwaka huu Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili Mayanja alisema “tunahitaji maandalizi mazuri, uzuri ni kwamba tulikuwepo katika michuano ya Kagame, baadhi ya wachezaji wasiokuwa na uzoefu wa kimataifa, tunajipanga ili kuwa vizuri zaidi”.Alisema baadhi ya wachezaji wana uzoefu wa kimataifa na wengine hawana na kwamba wametumia michuano ya Kagame kujijenga na kujiweka vizuri zaidi. KMC imesajili wachezaji wengi msimu huu wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuhakikisha inawakilisha kwa mara ya kwanza vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kuonesha ushindani mzuri katika msimu wake wa kwanza wa ligi iliyopita. Mmoja wa nyota wake, Jean Mugiraneza aliyewahi kuichezea Azam FC, alisema kwa kile alichokiona katika timu yake mpya ya KMC anaamini watafanya vizuri.“Tutatumia mbinu zaidi tutakapokwenda ugenini. AS Kigali ni timu nzuri imebadilika sana, imebadilika kwasababu imefukuza wachezaji 17 na kusajili wengine,”alisema.Kiungo mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba, Haruna Niyonzima kwa sasa anaitumikia timu hiyo ya Rwanda aliyojiunga nayo msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake kwa wekundu wa Msimbazi.
kitaifa
SIMBA itacheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa mashindano ya Mapinduzi yanayochezwa visiwani Zanzibar kesho kutwa.Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Unguja baada ya jana kuifunga Zimamoto kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Azam FC ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, anakutana na Simba ambayo katika fainali zilizopita waliifunga kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani Pemba, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Simba ambayo ipo Kundi B iliifunga Zimamoto jana kwa mabao 3-1 inakutana na Azam FC ambayo ipo Kundi A ambayo iliitoa Mlandege kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Amaan kwa bao la Obrey Chirwa dakika ya 57.Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya nne likifungwa na John Bocco na dakika tano baadaye iliongeza bao la pili lililofungwa Sharaf Shiboub katika dakika ya tisa akiunganisha kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu, lakini dakika ya 28 Zimamoto walipata bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ahmada na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa 2-1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na katika dakika ya 53 Ibrahim Ajib aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Zimamoto, bao lililodumu hadi dakika 90 kipyenga cha mwisho kilipopulizwa.Kwa mara ya kwanza Simba ilimchezesha Louis Mequissone raia wa Msumbiji iliyemsajili juzi katika dirisha dogo ambaye aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga.Baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, John Bocco, alisema wanakwenda kuangalia makosa yao na kuyafanyika kazi na mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa wa ushindani na wao watahitaji kushinda mchezo huo ili kuwapa raha mashabiki.“Azam FC ina wachezaji wazuri kama ilivyo Simba hivyo mchezo huo tumeuchukulia kwa uzito mkubwa na tunakwenda kujiandaa ili tuweze kushinda,” alisema Bocco.Mtibwa Sugar ambayo ipo Kundi B inatarajiwa kucheza nusu fainali kesho na mshindi wa mchezo wa Yanga dhidi ya Jamhuri ambao ulichezwa jana usiku. Mtibwa Sugar iliifunga Chipukizi kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba, ambapo kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ aliokoa penalti mbili.Chipukizi ilitangulia kufunga bao dakika ya tano lililofungwa na Suleiman Nassor na Haroun Chanongo kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 63. Shujaa wa Mtibwa alikuwa Nduda ambaye aliokoa penalti za Jumaa Kassim na Abdallah Mohamed, huku penalti za Mtibwa Sugar zikifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job na zile za Chipukizi zilifungwa na Salim Abui na Abdallah Khalisan.Mashindano hayo ya 13 yanashirikisha timu nne za Zanzibar na timu nne za Tanzania Bara na mecho zitachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka na Sh milioni 15 pamoja na kombe. Fainali za mashindano hayo zitafanyika Januari 13 katika Uwanja wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku.
michezo
Leo Julai 12, 2020 ni siku ya kukumbukwa kwenye macho ya wapenda soka nchini na nje ya nchi kutokana na mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la shirikisho la Azam, mchezo huu unakuwa wa aina yake kwakua unawakutanisha maasim wawili. Ni Simba Vs Yanga timu zilizokutana takribani mara 99 mpaka kufikia mwaka 2019 huku rekodi zikiibeba Yanga kutokana na kufanikiwa kushinda takribani michezo 36 huku Simba wakiwa wameshinda mara 28 na wakiwa wametoka sare mara 35. Uzuri wa mechi hii ni kutokana na uwezo wa wachezaji wake wanaocheza kwenye vikosi vyote viwilii ambao wamesaidia timu zao kuchukua makombe mbalimbali, Simba wamechukua jumla ya mataji 20 huku Yanga wakiwa wamechukua takriabani mataji 27. Simba na Yanga kukutana leo kwenye hatua ya nusu fainali ni hostori ya aina yake kwakua ni mara ya kwanza kukutana kwenye hatua hiyo tangu kuanzisha kwa kombe hilo la shirikisho ambalo Yanga ameshinda mara moja na Simba mara moja.    Nani anatoka Leo endelea kufuatilia OperaNews kwa Habari za Moja kwa moja kutoka uwanjani.
michezo
NILISHAPATA kusema huko nyuma, leo narudia tena; uongozi wa wasanii wetu nchini ni mzuri zaidi kwa sasa pengine kuliko kipindi kingine chochote cha uongozi kwa siku za hivi karibuni. Kuwapo kwa Waziri Nape Nnauye kwenye wizara inayoshughulikia sanaa (Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) ni sawa na kusema upele umepata mkunaji. Wasanii nchini mnahitaji nini tena? Tangu mapema Nape ameonyesha nia yake ya dhati ya kuwasaidia wasanii nchini. Tumemshuhudia mara kadhaa kupitia matamshi yake akisema kwamba wasanii wasiwe na wasiwasi kwa sababu yeye (waziri) ni msanii na anapenda kuona mafanikio ya wasanii nchini. Pengine tungeweza kusema labda waziri alikuwa akizungumza maneno ya kujifagilia tu, lakini sivyo. Anafanya kwa vitendo. Anaishi katika maneno yake. Kumbukumbu zinaonyesha ni kwa namna gani anapigania haki za wasanii wetu nchini. Hivi karibuni tumemshuhudia akiingia mwenyewe mitaani, maeneo ya Kariakoo na kukamata maharamia wanaodurufu kazi mbalimbali za wasanii wa filamu kinyume cha sheria. Huyu ndiyo waziri tuliyekuwa tunamtaka. Waziri ambaye anaingia mwenyewe mzigoni kuangalia kuna nini na anatakiwa kufanya nini. Sanaa iliyokuwa imesahauliwa nchini, sasa tunaona waziri mwenye dhamana akipambana kwa ajili ya haki ya wasanii wake. Wasanii ambao wamekuwa wakilia kila kukicha kuhusu kunyonywa na maharamia wasiojua uchungu wa jasho lao. Jumatatu ya wiki hii, Waziri Nape ameonekana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenye mapokezi ya mwigizaji Mike Ezuruonyes ambaye ametua nchini kwa ajili ya kurekodi filamu na wasanii wa Bongo Muvi. Ni ushirikiano mzuri. Anafanya kazi karibu kabisa na wasanii wenyewe. Mimi namshauri Nape akaze zaidi kwenye eneo la wasanii ambalo lilikuwa limesahaulika. Lakini hata hivyo asijikite kwenye muziki na filamu pekee. Wizara yake inahusisha utamaduni pia. Viko wapi vikundi vya ngoma? Vipi kuhusu haki na thamani ya waandishi wa miswada ya filamu, vitabu na majarida? Wale wasanii wa mazingaumbwe na kuruka sarakasi wamepotelea wapi? Nadhani kuna kitu kinatakiwa kufanywa ili kurudisha ari iliyokuwepo awali. Ni dhamana yako Nape, ambapo pia unapaswa kuwatazama kwa jicho la karibu. Wapo watunzi wa hadithi wazuri sana hapa nchini, lakini kazi zao zinaibwa ovyo na wahuni na kuzidurufu isiyo haki. Chondechonde mheshimiwa Nape, angaza jicho lako pande zote ili wasanii wote wapate haki zao kupitia wizara yako ambayo kwangu mimi nasema bila shaka kwamba inakutosha!
burudani
MSONGO wa mawazo umetajwa kuwa moja ya chanzo cha mifarakano na ugomvi katika familia na kuvunjika ndoa nyingi, pamoja na kuathiri ufanisi sehemu za kazi. Hayo yalisemwa na Mkurungenzi Mtendaji wa shirika la Endless Success Foundation (Esufo), Amina Feruzi, wakati wa warsha ya kukabiliana na msongo wa mawazo sehemu za kazi, kwenye ndoa na familia iliyohusisha wabunge, wanandoa na wafanyakazi wa ofisi mbalimbali, jijini Dodoma juzi. Alisema msongo wa mawazo umekuwa chanzo cha migogoro mingi na mafarakano katika familia pamoja na kuvunjika kwa ndoa nyingi. “Hii ni changamoto kubwa sana na ndio maana shirika letu tumeona tutoe mafunzo kwa watumishi wa umma na wanandoa ili kuwajengea uwezo wa kuyabaini haya,” alisema. Feruzi alisema msongo wa mawazo unaweza kuanzia ofisini au nyumbani na unasababisha mhusika kushindwa kufanyakazi au kutekeleza majukumu yake ipasavyo.“Unaweza kumkuta mtu nyumbani au ofisini anakuwa na hasira kila anayemgusa ni tatizo, kumbe ana msongo wa mawazo na asiposaidiwa anaweza kuharibu kazi au familia.”“Msongo wa mawazo umekuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi na kusababisha familia za wahusika hasa watoto kupoteza mwelekeo wa maisha,” alisema. Alisema warsha hiyo ina lengo la kuyajengea uwezo makundi hayo ili yaweze kukabiliana na msongo wa mawazo. Alisema shirika hilo linafanyakazi nchi nzima na linatoa ushauri wa kuondoa msongo wa mawazo kwa makundi mbalimbali na mtu mmoja moja
kitaifa
Pambano hilo linatarajiwa kupigwa kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni na kushirikisha mabondia wengine 10 wakisindikiza pambano hilo.Akizungumza na gazeti hili promota wa pambano hilo, Shomari Kimbau alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kwamba wanategemea ushiriki wa watu wengi.“Maandalizi yanakwenda vizuri tunategemea mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkali, kila bondia ana shauku ya kumtwanga mwenzake hivyo litakuwa ni pambano la aina yake,” alisema.Aliwataja mabondia watakaosindikiza mpambano huo kuwa ni Rahim Maokola dhidi ya George Demoso uzito wa kilo (60) light middle raundi nane na Shaban Kaoneka dhidi ya Sweet Kalulu uzito wa kilo 72 middle raundi nane.Wengine ni Chid Mbishi dhidi ya Mbwana Mdani kilo 52 flyweight raundi sita, Aman Mssy dhidi ya Pete Nunda kilo 86 heavy weight raundi nne na Hans Mawe dhidi ya Bakari Chuma kilo 86 heavyweight raundi nne.Kimbau alisema mshindi katika pambano hilo atacheza na Mkenya Daniel Wanyonyi katika pambano la Afrika Mashariki litakalofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
michezo
KIKOSI cha Yanga jana kilitarajiwa kutua mjini Musoma mkoani Mara kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho.Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe amesema, wachezaji wote wako vizuri na salama tayari kwa mchezo huo isipokuwa beki Gadiel Michael atakayekosekana katika mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.Alisema anatarajia mchezo huo kuwa mgumu kwa vile Biashara iko nyumbani mbele ya mashabiki wake, itapambana kutafuta matokeo mazuri.“Biashara sio timu ya kubeza wana kikosi kizuri na wako nyumbani kwao, kwa hiyo mchezo unaweza kuwa mgumu wakipambana kutaka kushinda na kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja,”alisema.Hivi karibuni Kocha wa kikosi hicho Mwinyi Zahera alisema licha ya kutokuwa na uhakika na ubingwa wa ligi, nia yao ni kupambana katika michezo yao iliyobaki na kushinda yote.“Hatuwezi kukata tamaa, tutapambana mpaka mwisho, kila mchezo ni muhimu kupata pointi tatu, tumejipanga vizuri naamini mambo yatakuwa mazuri,”alisema.Kwa upande wake, Kocha wa Biashara United Amri Said alisema wamekuwa wakifanya mazoezi ya kusuasua kutokana na wachezaji wengi kudai stahiki zao.Alisema tangu wamemaliza mechi dhidi ya Lipuli, wachezaji wao wengi kiakili hawajakaa sawa kwa sababu hawajapata kile wanachokidai.Said alisema pamoja na changamoto hizo bado wanaendelea kujiandaa na kujipanga dhidi ya mchezo huo kuhakikisha wanashinda.
michezo
MAWAZIRI Charles Mwijage wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Dk Charles Tizeba wa Kilimo, wametemwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri waliyofanywa na Rais John Magufuli leo  jioni.Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri kwa kuteua mawaziri wawili na Naibu Mawaziri wanne.  Taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Dk Tizeba.Aidha, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimbadili Mwijage. Taarifa hiyo ya Ikulu iliongeza kuwa Rais Magufuli amemteua Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Kanyasu ambaye ni Mbunge wa Geita Mjini mkoani Geita, anachukua nafasi ya Hasunga. Aidha, Rais Magufuli amemteua Dk Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo, Dk Mwanjelwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
kitaifa
JOSEPH HIZA NA MITANDAO WATU wenye kudhamiria kitu iwe chenye manufaa fulani kwa maisha yao, au ambacho kitaandika historia isiyofutikia huwa hawakati tamaa katika kufikia lengo walilojiwekea. Hawa ni watu, ambao hawawezi kuwa na amani bila kufanikiwa malengo na ndoto zao. Huwa hawajali ugumu au changamoto yoyote iliyopo mbeleni, wala kukata tamaa katika harakati za kufikia lengo lao. Huweza kurudia njia moja au mbalimbali ama kufanya majaribio ya kufanikisha dhamira hizo. Kwa sababu hiyo, huwa wana sababu nzito ya kutekeleza hiyo dhamira bila kujali iwapo kulifikia lengo hilo kunahitaji kuhatarisha kwanza maisha yao. Kwao ni bora kuhatarisha maisha kuliko kukaa bila kujaribu vinginevyo ili wasije ishi maisha ya kujutia kutotimia kwa hiyo dhamira. Watu hawa wanaweza kuwa na dhamira tofauti tofauti; wanaweza kuwa wenye malengo ya kibiashara, siasa, utajiri na hata kutaka tu kuweka rekodi au kumbukumbu ama tuseme historia na heshima. Kundi la watu 32 nchini Afrika Kusini lililojiteketeza kwa moto katikati ya mwaka jana, katika tukio ambalo ndilo kusudio ya makala haya, ni moja ya watu wenye dhamira hizi. Lililenga kuvunja na kuweka tu rekodi ya dunia, yaani kuingia katika vitabu vya kumbukumbu zitakazoishi kwa miaka mingi ijayo. Unaweza kusema ni watu wenye wazimu, watu hawa waliojaa ujasiri wa kujiteketeza kwa moto kwa malengo ya kuingia katika rekodi mpya ya dunia kwa kuungua mwili mzima. Bila kujali tukio hilo linaloweza kuonekana kutokuwa la maana au la kijinga, kuangalia watu wakiteketea vikali kwa moto na kisha mwishoni mwa tukio wakiruka ruka kushangilia ‘ushindi.’ Hakuna shaka ni sehemu ya utumbuizaji au kuburudisha watu. Wataalamu wa mazingaombwe 32 walikusanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini na taratibu kuanza kujiteketeza moto huku wakitembea kuufuata mstari wanaotakiwa kuishia. Ni kitu ambacho waliripotiwa kufanikiwa na kuvunja rekodi ya kundi kubwa zaidi la watu kujiteketeza pamoja moto mwili mzima. Dhamira yao ikatimia kwa kufanikiwa kuingia katika Kitabu cha rekodi za dunia yaani Guinness Book of World Records. Kanuni ya rekodi hii ya kutisha inasema kwamba wataalamu hao wa mazingaombwe wanapaswa kustahimili moto kwa sekunde 30. Waandaaji wa tukio hilo walilieleza kama la kuburudisha. Washiriki hao 32 walitembea pamoja kuelekea mstari wa mwisho na mara walipomaliza walianguka sakafuni ili kusaidiwa kuzimwa moto uliokuwa ukiwaka kwa hasira miilini mwao. Tukio hilo lililofanyika katika viwanja vya Grand Parade na kuandaliwa na Kevin Bitters, Grant Powell na Veron Willemse lilikuwa maalumu pia kwa kupromoti vipaji vya wasanii. Lengo lilikuwa ni kupata kundi la watu wenye ujasiri wa kidunia na ujuzi wa aina yake kwa ajili ya kitu cha kufurahisha na kuburudisha. Hata hivyo, licha ya hatari waandaaji waliratibu vyema tukio hilo kwa kuwa makini kuhakikisha usalama na afya ya washiriki hao wakati na baada ya tukio la kuteketea kwa moto. Awali kabla ya rekodi hiyo ya watu wengi zaidi kuteketea moto kuvunjwa nchini Afrika Kusini, rekodi kama hiyo ilikuwa ikishikiliwa na wakazi wa mjini Cleveland, Ohio nchini Marekani. Iliwekwa Oktoba 19, 2013 na watu 21, ambapo licha ya kufanikiwa kuingia katika kitabu cha Guinness Book of World Record, tukio hilo lilikuwa la kuchangisha fedha za taasisi moja ya hisani. Tukio hili la kuteketea kwa moto lilidumu kwa sekunde 32. Na kabla ya rekodi hiyo, katika mji huo pia mwaka 2009, rekodi ya watu 17 iliwekwa.
kimataifa
WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji imeunda Tume kuchunguza ajali ya meli ya mafuta ya Mt Ukombozi iliyotokea miezi miwili iliyopita katika Bandari ya Wesha Pemba na kuua wafanyakazi watatu.Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mohamed Ahmada ameyasema hayo leo wakati anajibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kufahamu tume iliyoundwa wajumbe wake na majukumu yake kwa ujumla.Ahmada amesema ni kweli SMZ imeunda tume ya kuchunguza kuungua kwa meli ya mafuta ya MT Ukombozi na kusababisha vifo vya mabaharia watatu.Ahmada amesema, uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kujitokeza kwa hitilafu za umeme na mlipuko wa gesi.“Huo ni uchunguzi wa awali katika tukio la mlipuko wa meli ya Mt Ukombozi.....sasa tumeunda tume rasmi kujua chanzo cha ajali hiyo,” amesema.Amewataja wajumbe wa tume hiyo ni Jaji Shaaban Ramadhan Abdalla, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyefahamika kwa jina moja la Fatuma, Kepteni Makame Hassan Ameir wa Shirika la Bandari la Zanzibar na Abdalla Kombo ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini.Katika timu ya uchunguzi wapo, wajumbe wataalamu kutoka Tanzania Bara kutoka taasisi za vyombo vya baharini na meli.Ahmada alisema tume hiyo inatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha taarifa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.“Kazi ya uchunguzi wa kitaalamu imeanza ikiwahusisha wajumbe kutoka Zanzibar pamoja na wenzetu kutoka Tanzania Bara...tunatarajia kuchukuwa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo na taarifa yake itatangazwa kwa wananchi,” amesema Ahmada.Meli ya Mt Ukombozi iliungua moto huko katika Bandari ya Wesha Pemba baada ya kujitokeza hitilafu za umeme huku wafanyakazi wa meli hiyo wakiwa katika harakati za usafi katika sehemu ya moja ya chumba cha injini.Ajali hiyo ilisababisha kujeruhiwa vibaya kwa mabaharia wake watatu kwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na baadaye kufariki.Waliofariki dunia ni Ali Juma (54), Hafidh Silima Kona (25) na Issa Daud Omar (30).
kitaifa
NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM   MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekubali kupokea ripoti za mkemia zinazothibitisha kwamba sampuli ya mkojo wa Mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu, imekutwa na chembechembe za bangi na majani yalibainika kuwa dawa za kulevya aina ya bangi.   Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, alikubali kupokea ripoti hizo mbili na kuzitambua kama kielelezo namba moja cha upande wa mashtaka, baada ya kutupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala.   Hakimu Simba alisema hakuna ulazima wa ripoti ya mkemia kuwasilishwa mahakamani ikiwa imeambatana na fomu ya maombi iliyotoka Polisi, ikielekeza mshtakiwa afanyiwe uchunguzi.   “Kazi ya mkemia ni kufuata maelekezo kwa kuchunguza, Jamhuri ndiyo yenye jukumu la kujua ni nani anayestahili kuitoa fomu hiyo mahakamani kama kielelezo, mahakama imepokea ripoti zote mbili kama kielelezo namba moja,” alisema Simba.   Agosti mosi mwaka huu, Mkemia Elias Mulima, akiwa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, alidai mahakamani kwamba alivyoufanyia uchunguzi mkojo alibaini mshtakiwa huyo anavuta bangi na akataka kutoa kielelezo ambacho kilipingwa na upande wa utetezi.   Wakili Peter Kibatala, anayemtetea Wema, alipinga ripoti hiyo isipokelewe kwa sababu haijakidhi kifungu cha 63 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.   Kibatala alidai kuwa, kifungu hicho kinaeleza utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kitabibu kwa mshtakiwa ambaye yupo chini ya ulinzi kuwa ni lazima Polisi awasilishe maombi mahakamani.   Kibatala aliomba ripoti hiyo ikataliwe kwa sababu hakukuwa na ombi wala amri kutoka mahakamani.   Pia alipinga ripoti hiyo kupokelewa kwa sababu haijaambatanishwa na fomu namba DCEA 001 iliyotoka Polisi kwenda kwa mkemia kuomba mteja wake afanyiwe uchunguzi.   Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, akijibu hoja hiyo, alidai fomu  yenye namba 001 inatumiwa na  Polisi wanapopeleka sampuli  na fomu namba 009 ni taarifa ya Mkemia na kwamba fomu moja haitegemei nyingine kwa kuwa zinaandaliwa na watu tofauti.   Kakula alidai kuwa, sheria haijasema muda wote ni lazima maombi yapelekwe mahakamani amri itoke ndiyo mshtakiwa afanyiwe mchunguzi wa kitabibu, ila pale ambapo mshtakiwa hataki Polisi wanaweza kufanya maombi mahakamani.   Katika ushahidi wake, Mulima alidai Februari 8, mwaka huu, alipokea sampuli ya mkojo wa Wema na Februari 6 alipokea majani ambayo aliyafanyia uchunguzi kujua kama yalikuwa dawa za kuleya ama la.   “Wema aliletwa ofisini kwa Mkemia na Inspekta Willy na WP Mary, alipofika nilimfanyia usajili na kumpa namba ya maabara 321/2017.   “Walimleta kwa sababu walitaka Wema apimwe mkojo na nilimpa kontena maalumu na kumpatia WP Mary ambaye aliongozana naye hadi kwenye vyoo akatoa sampuli ya mkojo.   “Baada ya kupatikana mkojo nilipokea sampuli hiyo na kuendelea na uchunguzi ambapo hatua ya kwanza ni kuangalia chembechembe za dawa za kulevya ndani ya mkojo wa Wema na baada ya uchunguzi nilibaini kuna dawa za kulevya aina ya bangi,” alidai.   Mulima aliendelea kudai kwamba, kitaalamu bangi inaweza kuonekana kwenye mkojo ndani ya siku 28.   Alidai baada ya kuthibitisha kwamba anatumia bangi aliandaa taarifa ya mchunguzi ambayo aliisaini yeye mwenyewe na ikathibitishwa na Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Februari 8, mwaka huu.   Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa, Februari 6 mwaka huu, akiwa ofisini kwake, alipokea kielelezo kutoka Jeshi la Polisi Tanzania kupitia kwa D/Koplo Robert, kikitakiwa kufanyiwa mchunguzi kuthibitisha ni dawa ya kulevya aina ya bangi ama la.   Alidai alikipokea kwa njia ya fomu DCEA 001, akakisajili na kukipa namba ya maabara 291/2017.   Anadai alifungua na kukuta msokoto mmoja na vipisi viwili, ndani yake kuna majani yadhaniwayo kuwa ni bangi.   “Niliyapima na kuyakuta yana uzito wa gramu 1.08, nilifanya uchunguzi kwa kutumia kemikali na kubaini ni bangi,” alidai.   Washtakiwa katika kesi hiyo ni Wema, Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas, ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.   Inadaiwa Februari 4, katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio,  washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Kwa upande wa Wema, yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka huu, katika  eneo lisilojulikana, jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.   Hata hivyo, kesi imeahirishwa hadi Agosti 15 na 16, mwaka huu, kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.
kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi (pichani) amesema kuwa kila mtumishi wa serikali mkoani mwake, kuanzia mwaka huu atatakiwa kuonesha mafanikio, yanayotokana na mshahara anaolipwa na serikali, kupitia kauli mbiu iliyoandaliwa na mkoa ya “Mshahara Wangu Upo Wapi” ifi kapo mwisho wa mwaka huu.Amewaonya watumishi kuachana na mambo ya siasa, badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dk John Magufuli.Amesisitiza kuwa watumishi wazembe, hawatavuka mwaka 2020 kwani wataondolewa mara moja, kupisha watumishi wanaoendana na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu’. Dk Nchimbi alisema hayo alipozungumza na watumishi wa umma wa mkoa wa Singida katika mkutano kwanza kwa mwaka huu 2020 mjini Singida jana.Alisema mkoa umeamua kuiishi kauli mbiu hiyo ya ‘Mshahara Wangu Upo Wapi’, baada ya kuona mafanikio ya kupigiwa mfano, yaliyopatikana kutoka kwa wanufaika wa mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).Mpango huo unalenga kunusuru kaya masikini, ambapo baada ya muda wa mradi, walenga husimama wenyewe. Mradi huo ulizinduliwa Septemba 2014 mkoani humo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa.Katika mpango huo, ruzuku ya Sh 20,000 hutolewa kwenye kila kaya yenye sifa katika Halmashauri 6 kati ya 7 za mkoa pamoja na fedha za masharti ya afya na elimu, ambayo kila kaya yenye mtoto anayesoma shule ya msingi na sekondari na wale chini ya miaka 5 hupewa kuanzia Sh 2000 hadi Sh 6000. Alisema ruzuku hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa kaya masikini, katika kuwanunulia sare, madaftari na kulipia matibabu hasa kujiunga Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii(NHIF).Aliongeza kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2020, jumla ya kaya 38,136 kutoka katika vijiji 278 zinanufaika na ruzuku hiyo na jumla ya takribani Sh bilioni 37.9 ziliwafikia walengwa.Aidha Dk. Nchimbi alisema pamoja na kuhakikisha kuwa mishashara ya watumishi, inaleta tija kwenye familia na kuboresha uchumi, tayari mkoa unatekeleza mikakati mahususi ya kilimo cha kisasa cha pamoja cha zao la korosho kwa wananchi wa Mkoa wa Singida. Alitoa rai kwa watumishi na wananchi, kujitokeza ili kupatiwa maeneo hayo ili kuyaendeleza kwa pamoja.“Hadi sasa Singida siyo masikini, kame wala yenye njaa, kama iliyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu hapo awali. Tayari hekta elfu kumi na mbili (12,000) za kilimo cha pamoja (block farming) zimepandwa mikorosho na zimeanza kuzaa korosho katika wilaya ya Manyoni. Natoa shukrani na pongezi zangu za dhati kwa Rais Dk John Magufuli kwa kutupatia pikipiki 10 ili ziweze kusaidia katika kazi hii” alisisitiza Dk.Nchimbi.Alisema tafiti zilizofanyika hivi karibuni, zimeonesha kuwa ardhi ya mkoa wa Singida, ina ubora mkubwa wa kusitawisha zao la korosho kwa muda mfupi, ukilinganisha na maeneo mengi hapa nchini. Hivyo, alisema hakuna sababu ya watumishi na wananchi kutochangamkia fursa hiyo adimu. Alionya kuwa wananchi ambao watabainika kuwa hawapo makini, wataondolewa katika programu hiyo.Pia alisema uzinduzi siku za hivi karibuni wa Kituo cha Hija na Maombezi cha Bikira Maria kilichopo katikati ya nchi ya Tanzania eneo la Sukamahela wilayani Manyoni mkoani Singida, ni fursa nzuri kwa wananchi wa mkoa huu, kufanya uwekezaji katika eneo hilo kwenye sekta za biashara ili kunufaika na wageni, wanaofika kujihi hapo kutoka sehemu mbalimbali duniani.“Uchumi wa Kituo cha Hija cha Bikira Maria, siyo tu kwamba kitabadilisha uchumi wa watu wetu, bali kitasaidia nchi yetu kukuza amani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla” aliongeza Dk. Nchimbi
kitaifa
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema ushindi waliopata juzi dhidi ya Cercle de Joachim ulikuwa ni moja ya lengo walilojiwekea kuhakikisha wanatinga raundi ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Yanga ambao waliwafunga Cercle de Joachim bao 1-0 ugenini wiki mbili zilizopita, juzi waliendeleza ubabe kwa wapinzani wao hao kwa kuwachapa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Mauritius wiki mbili zilizopita, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0, ambapo wamefanikiwa kusonga mbele wakiwa na jumla ya mabao 3-0. Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya mchezo huo, Pluijm alisema matokeo ya ushindi yamezidi kuwapa wachezaji morali ya kuendelea kufanya vizuri katika raundi ya kwanza ambayo watakutana na APR ya Rwanda. “Tumefurahi kuanza vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika, tumefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 na kufanikisha mipango tuliyojiwekea, sasa tunajiandaa kwa mchezo unaofuata dhidi ya APR,” alisema. Alisema pamoja na ushindi waliopata, wachezaji wake walishindwa kuzitumia vyema nafasi nyingi walizopata kufunga mabao mengi, huku akiahidi kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili yasijirudie katika michezo inayofuata. Kocha huyo raia wa Uholanzi, alisema wanaendelea kujinoa kujiandaa na michezo mingine ili kupata matokeo mazuri zaidi, huku wakielekeza nguvu zaidi katika pambano dhidi ya Azam FC. Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa wanaanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam uliopangwa kufanyika Machi 5, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga walitakiwa kucheza na Mtibwa Sugar kesho lakini wameomba mchezo huo usogezwe mbele hadi Machi 30, mwaka huu kupisha maandalizi ya kuwavaa wapinzani wao Azam na APR ya Rwanda katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Yanga wanaongoza katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 46 sawa na Azam waliopo nafasi ya pili kwa tofauti ya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
michezo
WABUNGE wa Bunge la Tanzania wadai kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mnigeria Emmanuel Amunike kukosa mbinu ndiko kumechangia timu hiyo kufanya vibaya katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, dhidi ya Senegal juzi.Taifa Stars juzi ilianza vibaya kampeni zake katika mashindano hayo Cairo, Misri baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa June 30.Wabunge hao, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba mkoani Dodoma na Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo waliyasema hayo jana kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakati wakirejea nchini pamoja na Spika Job Ndugai baada ya kushuhudia mechi ya ufunguzi Misri kati ya Taifa Stars na Senegal.Nkamia ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa wizara inayoshughulikia michezo wakati wa uongozi wa awamu ya nne, alisema Amunike kukosa mbinu ni sababu iliyosababisha kikosi hicho kufanya vibaya kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Senegal.Hoja hiyo iliungwa mkono na Bulembo, ambaye kwa miaka mingi huko nyuma aliwahi kuwa kiongozi wa soka ndani ya kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (Fat) kabla ya kuwa Shirikisho la Soka (TFF).Bulembo alisema mbali na kukosa mbinu pia kocha huyo hadi sasa hana kikosi chake cha kwanza, ambacho anaamini ni chanzo cha timu hiyo kukosa muunganiko kutoka sehemu ya ulinzi hadi ushambuliaji, hali iliyowafanya wapinzani wao kutumia makosa hayo na kuwazidi kila idara.Nkamia alisema Stars ni timu ya serikali, lakini muda wote walikuwa wanacheza kwenye eneo lao hali iliyowafanya kushambuliwa wakati wote na kufanya makosa ambayo yaliwagharimu na kupoteza mchezo huo.“Kama kocha Amunike angekuwa na mbinu, basi tulipaswa kupata ushindi, kukosa mipango ya kuwafanya wachezaji wa kikosi hicho kuwa wajanja kuwazidi wapinzani wetu tuliendelea kubaki kulinda lango, jambo ambalo ni hatari pale unapocheza na timu iliyotuzidi ubora kama Senegal,” alisema Nkamia.“Niwaombe Watanzania tusirudi nyuma tuendelee kuisapoti timu yetu, ingawa ili tuweze kufanya vizuri lazima kocha awe na kikosi cha kwanza, Samatta ni mchezaji mmoja, lakini hapati ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wengine,” alisema.Bulembo alisema wakati wanaachana na wachezaji hao Misri walikuwa wanaendelea vyema na wana morali kubwa ya kuendelea kupambana hadi mwisho.Naye Ndugai amesema ili kikosi hicho kiweze kuwa na nguvu na ari ya kushindana na timu zilizoendelea kama Senegal, kama nchi tunatakiwa kuwekeza kwenye miundombinu itakayozalisha wachezaji watakao kuwa na hazina kwa taifa.“Kama taifa tunatakiwa kuwekeza kwenye kujenga viwanja bora na vya kisasa, kuwa na vituo vya kuvumbua vipaji na kulea watoto wenye vipaji na kuwa na Ligi bora, na kupinga vitendo visivyokuwa vya kiungwana kwenye mchezo huo kama rushwa,” alisema Ndugai aliyekuwa kiongozi wa msafara huo wa wabunge.
michezo
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kupitia mradi wa pamoja wa mashirika 16 limezikabidhi kwa halmashauri nne za mkoa Kigoma shilingi milioni 430 kwa ajili ya kukopesha  kwa vikundi vya wanawake kusaidia mkakati wa serikali wa kupambana na umasikini na kusaidia makundi maalum. Mchambuzi wa mipango wa shirika hilo,Ann Moirana amekabidhi fedha hizo kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, Emanuel Maganga na sambamba na kukabidhi pikipiki 13 na kompyuta 10 ambazo zitatumika katika utekelezaji wa mpango huo. Akizungumza muda mfupi kabla kukabidhiwa kwa fedha na vifaa hivyo Mratibu wa mpango wa pamoja wa umoja wa mataifa, Evance Sangicha alisema kuwa uwezeshaji huo kwa vikundi vya wanawake ni kusaidia kuinua uchumi wa wanawake mkoani humo kutokana na historia na hiyo ni kusaidia ile asilimia 10 ambayo inatolewa na halmashauri. Sangicha alisema kuwa pamoja na uwezeshaji huo wa kifedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi vikundi hivyo vimepewa mafunzo ya uanzishaji na uendeshaji wa biashara wenye taja mambo ambayo yataenda sambamba na ujenzi wa masoko ya mpakani. Mkuu wa mkoa Kigoma, Emanuel Maganga alisema kuwa bado halmashauri hazijatekeleza majukumu yake kikamilifu katika kutumia asilimia 10 ya mapato yake kuwezesha utoaji mikopo kwa makundi maalum kuanzisha shughuli za ujasilimali na kuondokana na umasikini. 
kitaifa
TANZANIA inajivunia kufanya vizuri katika huduma na mafunzo yanayohusu afya kutokana na hospitali zake za umma kufanywa vituo vya mafunzo ya ubingwa wa hali ya juu wa tiba na afya katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.Miongoni mwa taasisi za afya zinazojipambanua kufanya vizuri katika eneo hilo ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI). Kwa Muhimbili, robo tatu ya wagonjwa wanaohudumiwa na hospitali hiyo kutoka nje ya nchi, wanatoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Umma cha MNH, Aminiel Aligaesha, aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa, ushirikiano wa nchi za SADC katika masuala ya afya, tiba na mafunzo ni makubwa kwa Muhimbili kutokana na hospitali hiyo kuwa na huduma za ubingwa wa hali ya juu.Kwa mujibu wa Aligaesha, MNH inapokea wastani wa wagonjwa 288 kwa mwaka kutoka nje ya nchi kupata matibabu yanayohitaji madaktari bingwa na robo tatu yao wanatoka nchi za SADC.“Licha ya kuwaona wagonjwa hawa, tunafikiri nchi za SADC zina vitu vingi zaidi zinaweza kushirikiana na Muhimbili. Kwa mfano, hospitali ya Muhimbili imeanzisha baadhi ya huduma za ubingwa…nchi zilizo ndani ya SADC wanaweza kuja hapa kujifunza kupata utaalamu na ujuzi,”“Naomba niseme Muhimbili tuna huduma za ubingwa wa hali ya juu, tuna vyumba wa uangalizi maalumu wa wagonjwa (ICU) kulingana na makundi na wataalamu wake. Miaka mitatu iliyopita tulikuwa na vitanda 25 pekee katika ICU lakini sasa vipo 78,” alifafanua Aligaesha.Aligaesha alitaja baadhi ya maeneo ya matibabu yenye huduma za ubingwa wa hali ya juu kwa sasa katika MNH kuwa ni pamoja na kupandikiza figo kulikoanza Novemba mwaka juzi (2017) na zaidi ya wagonjwa 40 wamefikiwa.“Kabla ya huduma hiyo kutolewa nchini kwa miaka zaidi ya 15 wagonjwa zaidi ya 200 walilazimika kwenda nje ya nchi kwa tiba lakini sasa chini ya miaka miwili, zaidi ya wagonjwa 40 wamepatiwa huduma… tiba kwa njia ya radioloji (CTScan, MRI) sasa tunaifanya hapa tangu mwanzoni mwa mwaka 2018, matibabu ya vivimbe vya kinywa asilimia 99 tunafanya hapa, hakuna rufaa ya nje tena,”alisema Aligaesha.Eneo jingine ni kupandikiza uroto kutakaoanza mwishoni mwa mwaka huu. Akifafanua namna ushirikiano wa nchi za SADC unavyoweza kumgusa mwananchi wa kawaida katika eneo la matibabu, Aligaesha alisema unaongeza ujuzi, kuboresha huduma na hivyo wananchi wananufaika na huduma bora za kisasa.Kwa upande wa MOI, Ofisa Habari wake, Patric Mvungi, alisema taasisi hiyo ni kituo kikubwa Afrika kinachoaminika kwa matibabu ya mifupa na mishipa na ilichaguliwa na chuo cha COSESCA (The College of Surgeons of East, Central and Southern Africa) kuwa kituo chake cha kufundisha madaktari bingwa.Akitolea mfano, alisema miaka miwili iliyopita, nchi ya Malawi iliyo miongoni mwa nchi 16 za SADC, ilituma ujumbe Muhimbili ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara yao ya Afya, kujifunza namna ya kuanzisha hospitali ya taifa nchini mwao. Kwa mujibu wa Mvungi, MOI kwa wastani inapokea wagonjwa 96 kwa mwaka sawa na wagonjwa wanane kwa mwezi kutoka nje ya nchi.Nchi zinazoongoza kwa raia wake kutibiwa MOI ni Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na Sudan Kusini (kwa upande wa Afrika Mashariki) na kwa nchi za SADC ni Comoro na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
kitaifa
HOSTELI bubu katika maeneo ya vijijini zimetajwa kuwa ni moja ya chanzo cha mimba za utotoni katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Sababu nyingine za mimba za utotoni ni wengi kutoka familia maskini hawana magodoro wanalalia mifuko ya salfeti au maboksi huku bajeti ya chakula ikiwa ndogo hali inayosababisha kuingia kwenye vishawishi.Wakizungumza wakati wa mafunzo ya vikundi vya malezi kwa wanaume wanaotoka katika kata za Berege na Kibakwe yanayotolewa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), walisema shule nyingi za sekondari ziko mbali na makazi hali inayosababisha wanafunzi kupanga mitaani.Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mohamed Kizungu, mkazi wa kata ya Kibakwe, alisema wazazi wengi wanawapangishia vyumba watoto mitaani bila kujali watoto hao wana ulinzi kiasi gani. “Utakuta wengi hawana magodoro, wametandika mifuko ya viroba, visalfeti au maboksi wanalala chini, bajeti ya chakula ndogo, akikutana na kijana akimsaidia kidogo hapo ndio mambo yanaanza kuharibika,”alisema.Alisema watoto wanaishi nyumba za kupanga maeneo ya vijijini huku wakiwa hawana ulinzi wowote na nyumba nyingi wanazopanga zimejengwa kwa udongo huku madirisha na milango yake ikiwa si imara.“Mtoto wa namna hiyo hana ulinzi wowote ataenda disko na kwenye kumbi za video, serikali za kata zimekuwa zikiongelea sana suala hilo lakini mwisho wa siku wanashindwa kuchukua hatua,”alisema. Alisema kunahitajika hosteli kwa ajili ya mabinti, kuna hosteli za misheni lakini wazazi wengi wanashindwa kutokana na uwezo wao kwa kifedha kuwa mdogo.Pia alisema ukosefu wa uzio katika shule ya sekondari ya kata hiyo umekuwa ukisababisha vijana kuwanyatia wanafunzi hasa nyakati za jioni, jambo ambalo husababisha tatizo la mimba. Kwa upande wake, Baini Mkwangule kutoka kata ya Berege alisema tatizo la mimba za utotoni lipo kwa kiasi kikubwa na sababu kubwa ikiwa ni umaskini na huduma za jamii ikiwemo shule kuwa mbali na makazi.
kitaifa
    Na MWANDISHI WETU, KUNA msemo usemao mama ndiyo kila kitu katika maisha. Mtoto anapokosa mama huwa mpweke hivyo kujikuta akiishi maisha asiyoyapenda. Upendo wa mama hauwezi kufananishwa na kitu chochote kile, ndiyo maana wazee wanakwambia radhi ya baba inapoteza mawazo wakati ya mama inaua. Ukimdharau mama maisha yako ni lazima yatakuwa ya kubabaisha hapa ulimwenguni. Schamica Stevenson maarufu kwa jina la Mimi (34) ni mwanamke aliyeungua moto mwili mzima lakini anadiriki kumnyonyesha mtoto wake wa pili licha ya uchungu anaoupitia. Mimi anasema anafanya hivyo ili kuwahamasisha wanawake wengine ambao hawaoni umuhimu wa kunyonyesha watoto wao. Mimi aliungua vibaya na moto akiwa na umri wa miaka miwili, nyumbani kwao katika Jimbo la Michigan, nchini Marekani. Alipopata mtoto wa kwanza hakumnyonyesha akihofia majeraha aliyokuwa nao, lakini baada ya kujifungua mtoto wake wa pili aliamua kumpa haki yake ya kunyonya ziwa la mama. ''Nafanya hivi ili wanawake wenzangu wasikate tama iwapo wana matatizo, kama nilivyofanya mimi nikiwa na miaka 20,'' anasema Schamica na kuongeza: ''Kama matiti yanafanya kazi, basi yanastahili kutumika kwa kuwanyonyesha watoto.'' Katika ajali hiyo ya moto uliosababishwa na sufuria ya maji yaliyokuwa yakichemshwa jikoni, Mimi alimpoteza kaka yake ambaye alikuwa na miaka minane. Mimi anasema kuwa mama yao alishindwa kuwaokoa kutokana na chuma zilizokuwa madirishani. Anasema amekuwa akifanyiwa upasuaji wa ngozi mara kwa mara katika maisha yake, hali iliyomfanya awe na wasiwasi wa  kubeba ujauzito, pindi alipofikisha umri wa miaka 20 kutokana na alama alizokuwa nazo tumboni. Mimi, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya ukaguzi msimamizi wa afya, anasema mara ya kwanza hakunyonyesha licha ya kwamba alitamani kufanya hivyo. “Nilikuwa mdogo na sikuwa na uvumilivu wa kustahimili maumivu kwa wakati huo. Ila huyu mtoto wangu wa pili niliamua kujaribu kumnyonyesha baada ya kumuona wifi na binamu yangu wakifanya hivyo kwa watoto wao,” anasema Mimi. Anasema alikuwa na maziwa kidogo hivyo ilimlazimu kutumia pampu na sirinji kabla ya kumpa mtoto titi. ''Muuguzi wa unyonyeshaji alinisaidia mno pindi nilipokuwa hospitalini,” anasema. “Nakumbuka muuguzi aliniambia hali hii itakuwa ngumu huku akijaribu kulitoa na kulifinya titi langu. “Nilikamua maziwa baada ya saa tatu na baada ya kula nikiwa bado hospitali, lakini sikuwa napata maziwa mengi,” anasema. Mimi anasema alikuwa akifanyiwa upasuaji wa ngozi kila mwaka huko Cincinnati hadi alipofikisha miaka 17. Licha ya kuwa na alama mwilini, Mimi anatumia picha zake anazonyonyesha kuhamasisha wanawake wengine kujivunia miili yao. “Inanivunja moyo nikisikia mtu anajitoa uhai kutokana na sura zao zilizoathirika na majanga mbalimbali,” anasema na kusisitiza kuwa yeye hajali lolote na kwamba anatembea kila mahali akijilinganisha na mwanamuziki Beyonce au Tamar Braxton. Anaongeza: “Sikupata ujasiri kwa siku moja, lakini najivunia kuwa mjasiri kwa sasa. Kuna wakati nilijihisi mnyonge kwa sababu mimi ni binadamu, lakini narudi na kumshukuru Mungu kwa maisha yangu na watoto wangu ambao niliweza kujifungua na kuwalea.” Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa BBC
afya
AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM Idadi ya Wagonjwa wanaougua homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona  (Covid-19) imeendelea kuongezeka kutoka 13 na kufikia 19. Taarifa iliyotolewa na waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu zimesema kuwa wagonjwa hao wamegundulika baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara ya Taifa. “Ninapenda kutoa taarifa kuwa leo Machi 30, tunathibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa Covid-19 baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara ya Taifa, Kati ya wagonjwa hawa watatu ni kutoka Dar es salaam na wawili kutoka Zanzibar. “Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa Covid -19 nchini ni 19 akiwemo mgonjwa mmoja ambaye aliyetolewa taarifa na waziri wa Afya wa Zanzibar Machi 28 mwaka huu. Katika taarifa hiyo waziri Ummy alianisha wagonjwa waliko Dar es salaam ambapo wanaume ni wawili na mwanamke mmoja. “Mwaume (49) Mtanzania alikutana  na raia kigeni kutoka miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi, mwingine ni mwanamke (21), Mtanzania ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa na mwaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia ni miongoni mwa watu wanaofatiliwa,”amesema. Hata hivyo waziri Ummy amesema kuwa kazi ya kuwafatilia watu wa karibu wote waliokutana na wagonjwa hao bado inaendelea na kuwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari ili kujikinga na virusi hivyo.
afya
Grace Shitundu – Simiyu NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amewataka wakulima nchini kutumia fursa ya kujiunga na bima ya afya inayotolewa na Shirika la Bima ya Afya la Taifa (NHIF) ili kupunguza gharama za matibabu katika kaya. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili baada ya kutembelea banda la NHIF katika maonyesho ya Nanenane Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, Bashe alisema bima hiyo itawapunguzia gharama ya matibabu. Alisema kwamba bima hiyo inayokatwa kwa Sh 70,000 inaweza kukatwa na mkulima yeyote. “Bima hii kila mwananchi atalipa Sh 70,000 ambayo itamsaidia yeye na familia yake watahudumiwa kwa pamoja. “Bima itampunguzia gharama za matibabu kwa sababu gharama za matibabu ni kubwa sana katika kaya, na kaya zetu za kiafrika nyingi unakuta pamoja na baba na mama huwa kunakuwa na wengi. Alisema kwa hiyo ni vizuri wakulima kutumia fursa hiyo kwenda ofisi za NHIF zilizopo kwenye mkoa, wilaya na kanda kupitia ushirika wao. “Vyama vya ushirika ndio vyenye dhamana ya kwenda kuwajazisha fomu wenzao, kwa hiyo niwaombe wote washirikiane kuiunga mkono NHIF, hii itatusaidia sana kupunguza sana gharama za matibabu katika ngazi ya familia,” alisema Bashe.   Aidha, Bashe amewapongeza NHIF kwa kuja na mfumo wa bima ya afya kwenye vikundi vya wakulima inayoitwa jina la Ushirika Afya. “Ningependa kutumia nafasi hii kuwaomba wakulima ambao wapo kwenye Amcos waweze kutumia nafasi hii na kuweza kuitumia,” alisema Bashe.
kitaifa
TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM  JUMUIYA ya watu wenye Ulemavu ndani ya  Chama Cha Mapinduzi(CCM), wameanza kuchangisha fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu ya kugombea urais, Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. John Magufuli. Akizungumza wakati wa mkutano wao  uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyetiki wa Jumuiya hiyo, Peter Sarungi alisema wamefurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli hasa kwa  kuwajali watu wenye ulemavu. Alisema ilani ya sasa imebadilisha maisha ya walemavu kwa kuwa imetekelezwa kwa asilimia 99. “Awamu hii imeweza kuwashirikisha vema walemavu kwa kuwateua viongozi wenye ulemavu  na kuunda wizara inayoshughulikia walemavu, haijawahi kutokea,” alisema Sarungi. Alisema sababu nyingine ya kumchukulia fomu, ni kuweka  mazingira rafiki na wezeshi kwa kuwapa mikopo kupitia halmashauri nchi nzima ambapo wengi wamenufaika.  “Kwa Manispaa ya Ilala pekee, zaidi ya bajaji 2,000 ndani ya mwaka 2018/19. “Pongezi kwa Mkurugenzi wa Ilala (Jumanne Shauri) kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 1.3. kukuza na kuwesha michezo ya walemavu katika ngazi za kimataifa ambapo timu ya Tembo Warriors kwenda Angola,” alisema Sarungi. Alishauri chama hicho kuendelea kuwawezesha walemavu kushiriki masuala ya kiuchumi kwa kuweka sera wezeshi zitakazowawezesha kushindana na wasio na ulemavu katika ilani. “Tunaomba Serikali kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kutoa ruzuku  kugharamia elimu kwa walemavu wanaochaguliwa vyuo badala ya mikopo ilivyo sasa,” alisema Sarungi. Alisema wanaomba kuanzishwa kwa  mipango maalumu wa bima za afya kwa walemavu kutoka kwa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma hizo kama ilivyokuwa kwa wazee na watoto. Baadhi ya watu wenye ulemavu wameziomba manispaa nyingine za jiji hilo kuiga mfano wa manispaa ya Ilala kwa kutoa asilimia mbili ya mapato yake kuwakopesha watu wenye ulemavu. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MTANZANIA, baada ya mkutano walisema halmashauri zingine zinachelewesha kutoa mikopo hiyo na kusababisha watu wenye ulemavu kukimbilia katika manispaa ya Ilala. Mmoja wao, Said Mwigombi alisema alipeleka maombi ya kupata mkopo Manispaa ya Temeke, lakini kutokana na kuchelewa alilazimika kujiunga na wenzke Ilala. Katibu wa Jumuiya hiyo, John Labu alisema wanatoa shukrani kwa serikali kutekeleza ilani ya CCM kwa kuwajali watu wenye ulemavu. Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel alisema haijawahi kutokea tangu uhuru mambo ya walemavu yakabebwa na kutekelezwa vema kama yanavyotekelezwa sasa.
kitaifa
Alisema kuwa michezo ni udugu, urafiki na mapenzi baina ya wanaocheza wenyewe kwa wenyewe na waalimu wao na mashabiki na wapenzi wao kwani huwezi kuwa mchezaji mzuri kama hujafundishwa.Alisema kuwa katika suala la michezo kunahitajika kuweka kando hasira zako ukaingia uwanjani ukafikiria utacheza hapo hutocheza na badala yake utafanya mambo ambayo hayamo kabisa katika malengo ya michezo, ambayo ni udugu, urafiki na mapenzi.“Ni lazima tukubaliane na malengo ya kuanzisha kwa michezo yetu, mwenye hasira hawezi kucheza, mwenye hasira anakwenda pahali pengine, kwenye kucheza wanakwenda watu wenye furaha, kwa hiyo michezo ni furaha si Zanzibar tu dunia nzima huwezi kuamka nyumbani kwako asubuhi umeudhiwa ukaenda kucheza itakuwa haichezeki tu, “ alisisitiza Rais Shein.Hivyo alisema kuwa michezo haitakiwi kuwa na bugdha inatakiwa kuwa na furaha. “Na mimi nasisitiza hilo hilo kwamba tucheze kwa furaha, kwani mambo ya michezo ni mila, desturi na tamaduni zetu ambayo zinakwenda pamoja hivyo inahitaji kulindwa,” alisema.Sambamba na hilo aliwataka viongozi wa michezo kuziendeleza timu ndogo za madaraja ya chini ili kuweza kuwa na timu bora na za kudumu za wachezaji wakubwa. Alisema kuwa kuviendeleza vipaji vya vijana kutoka madaraja ya chini kama Juvinile, Junior na Central ni jambo la faraja kwani kunatoa timu kubwa nzuri na zenye ushindani.“Nayasema haya kwa sababu hata hizo timu za Ulaya zikiwemo Liverpool, Manchester, Chelsea na Bacelona pamoja na timu nyingine zinatamba kutokana na kuwa na msingi mzuri wa timu za watoto wadogo, “alisema.Alifahamisha kwamba na hilo si kwa ajili ya mpira wa miguu pekee bali ni kwa michezo yote ambayo bila ya kuwa na timu za watoto haitawezekana kuwa na timu nzuri. “Lazima tuzitafute timu za watoto, tuziunde, tuzilee, baadae ziweze kuchezea michezo yao katika timu kubwa, zile timu tunazozipenda za Uingereza zote zina timu za watoto wachezaji wao wakiwa na miaka 15 wanawaweka katika timu nyingine, hawa kina Rooney, David Beckam wote wamelelewa vizuri, ”alisema.Hatahivyo, alisema kuwa kwa sasa Zanzibar haioni vuguvugu sana la timu ndogo kulelewa na timu kubwa zikakuzwa zikachezea timu kubwa, “Vugu vugu hilo silioni kwa michezo yote, pointi yangu hapa nasisitiza kuimarisha michezo na kuwaandaa vijana wetu”, alisema.Katika hafla hiyo rais Shein alitoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa vyama vya soka, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, netiboli, mpira wa meza, mikono, Olimpiki Maalum, Vinyoya, Viziwi, Kuogelea, Judo, Karate na Chama cha Kunyanyua Vitu Vizito.
michezo
MBUNGE wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara maarufu Bwege ameimwagia sifa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo jimboni mwake.Mbunge huyo machachari wa Chama Cha Wananchi (CUF), ametoa pongezi hizo bungeni wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mwongozo wa Bajeti ya Mwaka 2020/21.Huku Bunge ambalo lilikuwa limekaa kama Kamati ya Mipango likiwa kimya kumsikiliza, Bwege aliitaja miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya Rais John Magufuli na kuisifu kwa kutekeleza ahadi zake hizo.Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ya vituo vitatu vya afya, barabara, na mahakama ambayo alisema iko mingine inaendelea kukamilishwa katika jimbo lake hilo.“Mwenyekiti kwanza napenda kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa maendeleo iliyoleta jimboni kwangu,” amesema Bwege huku akipigiwa makofi na wabunge waliokuwa wakimsikiliza.Kuna miradi ya afya, nimejengewa vituo vitatu vya afya, kuna barabara ya Kwamkocho – Kivinje ambayo niliipigia kelele tangu Awamu ya Nne, sasa imeisha. Asante sana.“Kuna Chuo cha Maendeleo ya Wananchi wamejenga, kinaendelea vizuri sana, Alhamdullilah. Kuna Mahakama nzuri sana imeisha, Alhamdulillah. Kwa kweli nashukuru sana… mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Sisi wanasiasa kwenye mabaya tunakosoa, likiwa zuri sema, ndio siasa,” amesema Bwege na kushangiliwa na wabunge wenzake katika mchango wake huo.Aidha, alipongeza kwa kutengewa fedha kwa miradi ya maji jimboni mwake, ambayo imepatiwa fedha kutoka Serikali ya India, akisema, “In Shaa Allah, nimeona.”Bwege aliyekuwa amevalia suti ya rangi ya bluu bahari, wakati akichangia alikuwa amesimama jirani na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi).Katika mchango wake, mbunge huyo kutoka mkoani Lindi, pia alizungumzia Bandari ya Kilwa Masoko akisema ina kina kirefu cha asili na hajaona katika mpango wa maendeleo kama imewekewa utekelezaji.Mwishoni mwa mchango wake, alizungumzia utawala bora, akisema licha ya mambo mazuri ya maendeleo yanayofanywa na serikali, kuna tatizo la utawala bora.Alijikita kuzungumzia sintofahamu iliyojitokeza katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambao baadhi ya wagombea wameenguliwa kwa kukiuka Kanuni za Uchaguzi wa
kitaifa
UONGOZI wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetembelea kiwanda cha sukari cha Zanzibar kilichopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja, kinachomilikiwa na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Gabriel Silayo aliushukuru uongozi wa kiwanda cha sukari Zanzibar kwa kuwapatia fursa ya kujifunza stadi za kilimo cha miwa na uendeshaji wa kiwanda cha sukari.“Tunaushukuru uongozi wa kiwanda cha sukari Zanzibar kwa fursa hii ya kujifunza, NSSF tunatekeleza shughuli kama hii kule Mkulazi ambapo tayari tumeshalima shamba la miwa lenye ukubwa wa hekta 1,200 na tupo katika hatu za mwisho za kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha sukari,” alisema Silayo.Meneja Uhusiano wa Kiwanda cha Sukari Zanzibar, Frank Mtui alisema kiwanda hicho kiliazishwa mwaka 1974, lakini kilisimama kufanya kazi na mwekezaji mpya aliingia mwaka 2013 na kuanza shughuli za uwekezaji mwaka 2015.Alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 30,000 kwa mwaka, lakini kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo ufinyu wa ardhi kiwanda hicho kina zalisha tani 8,000 kwa mwaka. NSSF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, wameanzisha Kampuni ya Mkulazi Holding Company Limited inayoendesha mashamba ya Mbigiri mkoani Morogoro, ambako kunatarajiwa kujengwa kiwanda cha sukari.
kitaifa
ACCRA, GHANA MFANYAKAZI mmoja wa kiwanda cha samaki nchini Ghana, amewaambukiza kirusi cha corona kinashosababisha maradhi ya Covid-19 wafanyakazi wenzake 533 wa kiwanda hicho. Hayo yameelezwa na Rais Nana Akufo-Addo katika hotuba kwa taifa jana na kusisitiza kuwa, watu wote hao 533 waliambukizwa virusi vya corona na mtu mmoja.  Hata hivyo hakutoa ufafanuzi ni vipi  ugonjwa huo wa Covid-19 ulienea kiwandani humo na kama hatua za tahadhari za kiafya zimechukuliwa kufuatia maambukizi hayo. Kwa mujibu wa Rais Akufo-Addo, maambukizi hayo ya watu 533 waliothibitika kuwa na virusi vya corona, ikiwa ni takribani asilimia 11.3 ya maambukizo yote ya nchi nzima ni sehemu ya kesi mpya 921 za watu waliobainika kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 katika kipindi cha karibu wiki mbili zilizopita ambazo takwimu zake zimetolewa hivi karibuni. Katika hotuba yake hiyo ya jana, Rais wa Ghana alirefusha tena marufuku ya mikusanyiko ya umma hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Mei huku shule na vyuo vikuu nchini humo vikiendelea kufungwa. Mamlaka za Afya za Ghana ziliripoti siku ya Ijumaa kuhusu mripuko huo wa maambukizo ya corona katika kiwanda hicho cha samaki kilichoko kwenye mji wa kando ya bahari wa Tema lakini hazikutoa maelezo zaidi. Maambukizo mapya ya corona yaliyotangazwa jana yameifanya Ghana kuwa na jumla ya watu 4,700 wenye virusi vya corona tangu mripuko wa janga hilo lililoikumba dunia nzima ulipotangazwa nchini humo kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Machi. Takwimu za jana zimeifanya Ghana kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya corona katika eneo la Afrika Magharibi. Hadi sasa watu 22 wamefariki dunia kwa maradhi ya Covid-19 nchini humo na wengine 494 wamepata afueni.
kimataifa
FESTO POLEA, ZANZIBAR Kuimba kwa umahili mkubwa idadi kubwa ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na wasanii wa kundi la Yamoto, kundi la Muziki la Mkubwa na Wanawe limetoa ishara kuwa wanauwezo mkubwa wa k ukonga nyoyo za mashabiki wapenzi wa nyimbo hizo. Kundi hilo limeonyesha uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo hizo katika shoo yao waliyoifanya Februari 7 katika Tamasha la 16 la Kimataifa la Sauti za Busara linloendele viunga vya Ngome Kongwe, Unguja visiwani Zanzibar. Kundi hilo limeweza kuonesha umahri wao wa kuimba na kucheza jukwaani huku wakiendana sambamba na mapigo na ala za muziki wa bendi iliyopiga live. Vijana hao wa waliweza kuimba nyimbo zaidi ya tano (5) ikiwemo ya Stata ukiimbwa na mwanadada Catrima Wegesa huku nyimbo zingine zikiimbwa na Abdala Mustapha ‘Kisamaki’ huku kijana mdogo kabisa wa kundi hilo, Abdul Kadry ‘Dogo Kadry’ mwenye miaka 15 akiwa kidato cha kwanza alikuwa kivutio kila alipopanda jukwaani kuimba nyimbo tofauti hasa alipoimba wimbo wa Asu uliimbwa na mwanamuziki wa taarabu, Abdul Misambano. Kundi hilo lililo chini ya Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule wilayani Temek jijini Dar es Salaam hadi sasa lina vijana wanaofanya kazi za Sanaa za Muziki zaidi ya 100. Miongoni wa wasanii waliowahi kuwa kwenye kundi la Mkubwa na wanawe ni pamoja na Dogo Aslay, Mboso, Beka Fleva, Enock Bella, Getu, Madada Sita na wengine wengi.
burudani
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga Jerry Muro alisema kuwa ushindi huo wa juzi umetoa mwanga wa mwelekeo wa timu hiyo kushinda michezo ijayo. Alisema timu imeshakwenda Morogoro tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa keshokutwa.Alisema kuwa ana uhakika Mtibwa itafungwa mabao mengi zaidi ya yale ya Simba na kusisitiza kuwa wachezaji wake wamejiandaa kutimiza hilo. Mara kwa mara Yanga imekuwa ikipata tabu kuifunga Mtibwa kila inapokutana nayo.Alisema kuwa ana imani mchezo huo utakuwa rahisi kwao kwa kuwa ana imani na mafunzo ambayo wachezaji wake wamepewa na kuwa kila mmoja anajua nini cha kufanya. “Sisi tunaijua vyema Mtibwa na kwa sasa hatuna wasiwasi nao kabisa kwa kuwa tunajua mchezo wao na tunajua uwezo wao na Yanga kama treni lililokosa breki yani tumejipanga kuwamaliza kabisa yani tunawashukia kwelikweli,” alisema Muro.Aliongeza kuwa “ Yanga inajua kuwa Mtibwa ni timu nzuri na hata kocha amejipanga zaidi kuhakikisha kuwa inashinda mchezo kwa zaidi ya mabao mawili ili kuonesha uwezo wetu”.Pia Muro aliongeza kuwa ushindi wao dhidi ya Simba ni mkubwa na umeongeza hamasa zaidi kwa wachezaji wake na mashabiki kwa ujumla lakini aliipongeza Simba kwa uwezo wake iliouonesha wa uchezaji kuwa ilicheza vyema zaidi.
michezo
*Kutafutwa kumbi za starehe, nyumba za ibada *Wanaosoma nchini China kukosa mikopo   Na CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema kuanzia Januari mwakani itaanza kudai fedha za mikopo kwa kupita nyumba kwa nyumba, hasa muda wa usiku. Mbali na hilo, HESLB wamesema kuwa wapo kwenye mpango wa kuzungumza na washereheshaji wa sherehe (ma-MC), hasa harusi na viongozi wa nyumba za ibada ili waweze kutumia maeneo yao kuwakumbusha wadaiwa hao walipe madeni yao. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru, alisema kuwa sasa ni wakati mwafaka kuhakikisha madeni yote yanalipwa kwa kutumia kila aina ya njia. Aliwataka walionufaika na mikopo hiyo kuanza kujisalimisha wenyewe kulipa madeni yao kuepuka kusakwa majumbani na katika nyumba za ibada. “Tumefanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuwashirikisha washereheshaji katika shughuli mbalimbali pamoja na nyumba za ibada ili waweze kuwakumbusha wadaiwa wa bodi kurejesha mikopo na ifikapo Januari Mosi, mwakani majina na sura za wadaiwa sugu tutazichapisha gazetini. “Si hilo tu, pia tutapita nyumba kwa nyumba nchi nzima, hasa muda wa jua linapozama ili kuweza kuwafikia wadaiwa wote ambao walipata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo. Mkopo si zawadi ni lazima ulipwe. “Walipe ili na wengine waweze kunufaika na fursa ya mikopo. Na wale ambao watakaidi tutawafikisha mahakamani ambako watalipa gharama za uendeshaji wa kesi pamoja na deni wanalodaiwa,” alisema Badru. Mkurugenzi huyo alisema hivi sasa wameanza utekelezaji wa marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ambapo kwa sasa wanufaika wa mkopo watalazimika kukatwa asilimia 15 badala ya asilimia nane ya awali. Badru alisema sheria hiyo mpya imeipa meno bodi hiyo pia kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani waajiri endapo watashindwa kukata makato kwa waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo au kuchelewesha kuwasilisha fedha za makato hayo. “Kwa mabadiliko haya ya sheria, mwajiri sasa ana wajibu wa kuwasilisha majina, kukata na kuwasilisha makato stahiki kutoka katika mishahara ghafi ya waajiriwa wake walionufaika na mikopo ya elimu ya juu,” alisema Badru. Alisema kwa waajiri ambao hawatawajibika, watalipa faini isiyopungua makato hayo au kifungo cha miezi 36. Badru alisema pia wametoa siku 14 kuhakikisha kila mwajiri anapitia kumbukumbu zake na kuangalia kiasi walichokata na kuwasilisha katika bodi hiyo kabla timu iliyoundwa kufuatilia madeni hayo haijaanza kufanya kazi. Alitoa wito kwa waajiri na waajiriwa kuhakikisha wanakusanya kumbukumbu muhimu ili kuepusha usumbufu endapo wataajiri wadaiwa sugu wa bodi hiyo na wakakwepa kutoa taarifa zao mapema. Alisema kuhusu wanufaika ambao hawapo kwenye mfumo rasmi na mikopo yao imeiva, watalazimika kulipa Sh 100,000 au asilimia 10 ya kipato kinachotozwa kodi kwa mwezi. “Sheria hii imepita mikononi mwa wadau ambao wamejaribu kupunguza ukali wa maisha, ambapo kwa wanufaika ambao hawako kwenye mfumo rasmi watalazimika kulipa deni lao baada ya miaka miwili badala ya mmoja wa sasa na kwa wale ambao wana ajira wataanza kulipa mara baada ya kuajiriwa,” alisema Badru. Sambamba na hilo, bodi hiyo imesema hadi sasa  imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 140 kutoka kwa wanufaika wa mikopo iliyoiva. Awali deni lilikuwa ni Sh bilioni 300. Mkurugenzi huyo alisema kiwango cha makusanyo ya mikopo ambayo awali yalikuwa ni Sh bilioni 2 kwa mwezi, hadi kufikia Novemba, mwaka huu yameongezeka na kufikia Sh bilioni 8 kwa mwezi. Pia wadaiwa sugu waliojitokeza kulipa au kupunguza madeni yao wamefikia 42,700 kati ya 100,000 waliokuwa wanadaiwa awali. “Katika kuhakikisha waajiri wanakusanya makato yetu, tumekutana na waajiri zaidi ya 10 na kuzungumza nao, ambao wengi wao walikuwa hawafahamu wajibu wao,” alisema Badru. Kwa upande wa mwanasheria wa bodi hiyo, Luhano Lupogo, alisema mwajiri ana wajibu wa kupeleka makato ya mwajiriwa wake kwa bodi ndani ya siku 15, vinginevyo atalipa faini isiyopungua makato au kifungo cha miaka mitatu jela. Alisema sheria hiyo ya mwaka 2004, namba 21 (2) imeanza kutumika Novemba 18, mwaka huu ambapo pia mwajiri ana wajibu wa kuwasilisha katika bodi orodha ya waajiriwa wake ambao ni wahitimu wa Stashahada au Shahada.   WANAFUNZI CHINA KUKOSA MIKOPO Wakati huohuo, Mwandishi JOHANES RESPICHIUS anaripoti kuwa bodi hiyo imesema haitatoa mikopo kwa wanafunzi wote wa Tanzania waliofadhiliwa masomo katika nchi rafiki, ikiwamo China. Hiyo ni kwa mujibu wa barua ya Desemba 20, mwaka huu iliyokuwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa imesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, kwenda ubalozi wa Tanzania nchini China. Barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Kuchelewa kwa Fedha za Malipo kwa wanafunzi wanaosoma nchini China’, ilisema kuwa bodi hiyo haikupanga mikopo kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China kutokana na maelekezo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. “Kupitia barua ya wizara Kumbu. Na FB.54/283/01A/82 ya Septemba 14, mwaka huu, ilielekeza wanafunzi wote watakaopata ufadhili wa masomo (scholarship) kutoka katika nchi rafiki watakuwa wanajitegemea katika kununua tiketi za ndege kwenda masomoni. “Pia barua hiyo ilielekeza kwamba wanafunzi wanaosoma katika nchi hizo hawatanufaika na mikopo ya nyongeza ya ada (topping up loan) kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” ilieleza barua hiyo. Ilieleza kuwa kutokana na maelekezo hayo, bodi imeshindwa kupanga mikopo kwa wanafunzi hao waliopata ‘scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2016/17 na wale waliokuwa wakiendelea na masomo China hadi itakapopata maelekezo zaidi. MTANZANIA lilimtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa HSELB, Badru ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hilo. “Siwezi kusema ndiyo ni ya kwetu au hapana kwa sababu barua hiyo sijaiona, kwanza bodi haina utaratibu wa kuweka barua kwenye mitandao ya kijamii. “Kama ina taarifa yoyote inataka kuitoa huwa inatumia utaratibu wa kawaida wa utoaji taarifa na kama kuna umuhimu kuweka kwenye mitandao ya kijamii ndipo huweka,” alisema Badru.
kitaifa
Mwandishi Wetu – Dar es Salaam WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Zungu amezungumzia umuhimu  wa matumizi ya  nishati mbadala ya gesi ambayo ni rafiki kwa mazingira ukilinganisha na mkaa na kuwataka watanzania kugeukia matumizi ya gesi ili kulinda mazingira. Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Circle Gas, Volker Schultz,  alisema kuwa elimu na uhamasishaji zaidi unahitajika kuhusu matumizi mbadala ya nishati. “Tanzania kama nchi ina hamasisha matumizi ya nishati mbadala kama suluhisho pekee la kulinda misitu na mazingira kwa ujumla. Tumekua tukichukua hatua mbalimbali kushirikiana na wadau wa mazingira,” alisema. Alisema Schultz alimtembelea kumwelezea mpango wa kampuni yake kuhamasisha matumizi  ya gesi katika majiji ili kupunguza ukataji miti hovyo ambao umekuwa  ukiathiri mazingira. “Kwa sasa matumizi ya mkaa yamekuwa makubwa kutokana na ongezeko la watu, ukataji wa miti umeongezeka na mpaka sasa kwa tafiti zilizopo zaidi ya tani milioni mbili za mkaa zimekuwa zikitumika kwa mwaka kama nishati ya kupikia majumbani, hali hiyo imeleta athari kubwa za kimazingira,” alisema Zungu. Alisema mpango huo ambao utekelezaji wake bado  haujaanza, unalenga kuhudumia majiji makubwa na kwa Tanzania utaanza na  jijini la Dar es Salaam na kuenea katika majiji mengine kutokana na mafanikioyatakayopatikana. “Pindi mazungumzo yatakapokamilika, awamu ya kwanza ya mradi huo utaanzia Dar es Salaam ambapo wakazi zaidi ya elfu kumi wanategemea kunufaika. Ni furaha kwetu iwapo mpango huu utakamilika kwani zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wake wanatumia mkaa,” alisema
kitaifa
NA RAMADHAN LIBENANGA – KILOSA MIMBA za utotoni 4,186 sawa na asilimia 30 ya wajawazito waliohudhuria kliniki, zimeripotiwa wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa kipindi cha mwaka jana. Mbali ya hiyo, kesi za wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na ujazito zimeripotiwa kuwa 15. Akizungumza na MTANZA NIA ofisini kwake jana, Meneja Kanda wa Shirika la World Vision, Faraja Kulanga, alisema wameibaini tatizo hilo kutokana na kukusanya takwimu za maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Kulanga alisema kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, hasa mimba na ndoa za utotoni, itasaidia kuwafanya watoto wa kike kufikia malengo yao ya maisha. Alisema shirika hilo kwa kuona ukubwa wa tatizo, liliamua kupita na kuchunguza chanzo cha wingi wa watoto kupata mimba, jambo ambalo linapaswa kupata ufumbuzi wa haraka. Kulanga alisema kesi za mimba zilizoripotiwa kwa shule za sekondari ni nane, saba zikiripotiwa kwa shule za msingi. Naye Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kilosa, Tumaini Mohammed, alisema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Shirika la World Vision limekuja na mradi wa kupiga vita ukatili kwa watoto wadogo. Aliwaomba wananchi wilayani humo kushirikiana na Serikali kutoa taarifa kwa vyombo vya dola juu ya wazazi au mzazi anayeozesha mtoto aliye chini ya miaka 18. “Msikae kimya kuona mtoto wa jirani yako amepewa mimba, wakati unajua anasoma, lete taarifa tufanye kazi sheria ifuate mkondo wake,” alisena Tumaini. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi, alisema kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka, hivyo kuwataka viongozi wa ngazi ya vijiji, kata hadi wilaya kushirikiana na shirika hilo.
kitaifa
NAIROBI, KENYA RAIS Uhuru Kenyatta, Jumatatu alidai kuwa katu hawezi kushindwa na kiongozi wa NASA, Raila Odinga kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumanne ijayo. Akizungumza kwenye mikutano ya kisiasa katika kaunti za Kisii na Bomet, Rais Uhuru aliyeandamana na naibu wake William Ruto, alisema ni kichekesho kwa NASA kudai kuwa watamshinda. “Kama nilimshinda nilipokuwa nakabiliwa na kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2013, atanishinda vipi sasa hivi nikiwa ndani ya Serikali?” alihoji. Aliwataka wakazi wa Kisii wasipotoshwe na Raila, na wajitokeze kwa wingi Agosti 8 wampe nafasi nyingine ya kukamilisha maendeleo aliyoyaanzisha. Alikuwa akizungumza katika uwanja wa michezo wa Gusii ambako pia alisema kuwa eneo la Etago litakuwa kaunti ndogo. “Watu wa jamii ya Kisii nawaomba mnipigie kura na nitazidi kufanya kazi na nyinyi hadi nitakapomaliza muhula wangu,” alisema Rais Uhuru. Alijipiga kifua huku akisema kuwa tangu mwaka 2013 Jubilee imewafanyia kazi watu wa jamii ya Abagusii bila ya kujali kama walimuunga mkono katika uchaguzi mkuu uliopita. Pia alisema kuwa reli ya kiwango cha SGR ambayo imeunganisha Nairobi na Mombasa, itajengwa na kupitia Kaunti ya Kisii ikielekea Kisumu.
kimataifa
WATU 12 wakiwemo maaskari polisi nane wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi Na.1 ya mwaka 2019 wakishitakiwa kwa makosa 12 yakiwemo ya kushawishi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa.Waliofikishwa katika mahakama hiyo ya Kaimu Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza jana, Gwayi Sumayi ni mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, Sajid Abdallah Hassan, Kisabo Nkinda almaarufu kama Paulo Nkinda, Emmanuel Ntemi, Hassan Saddiq na SSP Moris Okinda.Wengine waliofikishwa mahakamani ni pamoja na mshitakiwa wa sita E.6949, Detective Koplo Kasala, F.1331 d/PL Matete , G 6885 Detective Alex, G 5080 Detective Maingu, G 7224 Detective Timothy , G1876 Detective Japhet na H.4060 Detective David Kadama.Awali ilidaiwa mahakamani hapo na waendesha mashtaka watatu wa serikali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Castuce Ndamugoba na Mawakili wa Serikali Robert Kidando na Jackline Nyantori kuwa katika shitaka la kwanza mshitakiwa wa kwanza Sajid Abdallah Hassan, Kisabo Nkinda ( Paulo Nkinda), Emmanuel Ntemi na Hassan Sadiq kati ya Desemba 15 mwaka jana na Januari 5 mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Jiji la Mwanza na Mikoa ya na Dar es Salaam na katika maeneo mbalimbali kati ya mikoa ya Geita na Kagera ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maeneo ya Jamhuri ya Rwanda walishirikiana kwa pamoja wakiwa sio watumishi wa umma lakini kwa kushirikiana na watumishi wa umma huku wakijua ni kosa walikula njama kwa kuwezesha biashara haramu ya fedha kwa lengo la kujipatia faida ambayo ni kosa la jinai.Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali akitaja baadhi ya makosa, aliieleza mahakama hiyo katika kosa la pili kuwa watuhumiwa SSP Moris Okinda, E. 6948 Detective Koplo Kasala, F.1331 Detective Pl Matete, G. 6885 Detective Alex, G.5080 Detective Maingu, G. 7224 Detective Timothy, G.1876 Detective Japhet na H.4060 Detectve David Kadama kuwa kati ya Januari 4 na 5 mwaka huu katika maeneo ya Kigongo Feri wilayani Misungwi na Kigongo cha Busisi wilayani Sengerema na maeneo tofauti ndani ya Jiji la Mwanza wakiwa ni watumishi wa umma wakiwa kazini kwa pamoja walitenda kosa la jinai kwa nia ya kuvuna faida.Aidha, katika kosa la tatu, ilidaiwa mahakamani kuwa Januari 5 mwaka huu akiwa katika eneo la Mission wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Sajid Abdallah Hassan, alikutwa akiwa anamiliki Kilo 319.59 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani 11, 747,377.46 ikiwa ni sawa na Sh 27,018,968,158 huku akiwa hana leseni ya madini, (Valid mineral rights), dealers licence au Brokers licence.Aidha katika kosa la nne, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Januari 4 na 5 mwaka huu, SSP Moris Okinda, E. 6948 Detective Koplo Kasala, F.1331 Detective Pl Matete, G. 6885 Detective Alex, G.5080 Detective Maingu, G. 7224 Detective Timothy, G.1876 Detective Japhet na H.4060 Detectve David Kadama katika eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi , Kigongo –Busisi na Kamanga Feri, wilayani Sengerema na maeneo ya jiji la Mwanza mkoani Mwanza, kwa pamoja walifanya ushawishi na kujipatia kiasi cha Sh 700,000,000 kutoka kwa Sajid Abdallah Hassan, Kisabo Nkinda, Emmmanuel Ntemi na Hassan Sadiq ili wasiweze kumkamata Sajid Abdallah Hassan ambaye alikuwa anamiliki kinyume cha Sheria kilo 319.59 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 11, 747,377.46 sawa na Sh bilioni 27.Katika kosa la tano ambalo ni la rushwa ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa Sajid Abdallah Hassan, Kisabo Nkinda, Emmanuel Ntemi na Hassan Sadiq kuwa kati ya Januari 4 na 5 mwaka huu katika maeneo ya Kigongo Feri wilayani Misungwi, Busisi- Kamanga Feri-Sengerema na maeneo ya jiji la Mwanza mkoani Mwanza kwa pamoja walitoa rushwa ya Sh 700,000,000 kwa SSP Moris Okinda, E. 6948 Detective Koplo Kasala, F.1331 Detective Pl Matete, G. 6885 Detective Alex, G.5080 Detective Maingu, G. 7224 Detective Timothy, G.1876 Detective Japhet na H.4060 Detectve David Kadama ili wasiweze kumkamata Sajid Abdallah Hassan ambaye alikutwa anamiliki kinyume cha sheria kilo 319.59 za dhahabu zenye thamani ya Dola za kimarekani 11, 747,377.46 sawa na Sh bilioni 27, 018,968,158.Wakati katika kosa la sita ambalo pia ni la rushwa, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Januari 4 na 5, mwaka huu watuhumiwa SSP Moris Okinda, E. 6948 Detective Koplo Kasala, F.1331 Detective Pl Matete, G. 6885 Detective Alex, G.5080 Detective Maingu, G. 7224 Detective Timothy, G.1876 Detective Japhet na H.4060 Detectve David Kadama wakiwa katika maeneo ya Kigongo Feri wilayani Sengerema na maeneo ya jiji la Mwanza kwa pamoja walishawishi kupata kiasi cha fedha Sh 305, 000,000 kutoka kwa Sajid Abdallah Hassan, Kisabo Nkinda, Emmanuel Ntemi na Hassan Sadiq waliokutwa wanamiliki kinyume cha sheria kilo 319.59 za dhahabu zenye thamani ya Dola za kimarekani 11, 747,377.46 sawa na Sh bilioni 27, 018,968,158. Kwa upande wake, Kaimu Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema washitakiwa wote hawatakiwi kusema chochote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kuendesha shauri hilo la uhujumu uchumi na walirudishwa mahabusu hadi Januari 28 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
kitaifa
Na Mwandishi Wetu-Dodoma KATIBU Mtendaji wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda, amewataka wanasiasa na viongozi wastaafu wa Serikali kuacha tabia ya  kujenga dhana inayokuza  mpasuko kwa jamii kwa kuwa makini na kauli zao. Hayo aliyasema   mjini hapa jana kutokana na kauli ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa   ya kuwatetea masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara (Umasho) kuwekwa mahabusu kwa miaka kadhaa bila kesi yake kuamuliwa kuwa uonevu. Shibuda alidai kauli ya Lowassa imekosa umakini na kutozifanya hoja zake zikose  uhalali . “Wanasiasa ni vema wajenge fikra na kauli zenye umakini, hekima na mafunzo ya utetezi wa haki kwa kufuata  usawa bila ya kuongeza chumvi  au shinikizo la  mgawanyiko katika jamii. “Masuala yanayobeba tuhuma za uhalifu au jinai ni vema vyombo husika vikapewa nafasi ili kujitosheleza na kujiridhisha katika taaluma,” alisema. Shibuda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,  alisema katika hoja iliyoibuliwa na Lowasa kuhusu waislamu,  mtu mwenye weledi na umakini itawia vigumu kubaini maono yake, shabaha na kusudio lenye msingi dhidi ya madai hayo kwa sababu  ni vigumu mtu mmoja kusafiria farasi wawili kwa wakati mmoja. “Dira ya siasa ilenge katika kuleta mapinduzi ya fikra na uchumi kwa kuzingatia matumizi  salama ya matamshi, mipaka ya utawala iwe na rutuba ya kuhami rasilimali  jamii inufaike.
kitaifa
Yanga itacheza na Al Ahly Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 9 mwaka huu, lakini Yanga ikitakiwa kucheza mechi tatu za viporo vya Ligi Kuu ndani ya siku 11, jambo ambalo Pluijm ameliita ni kuwachosha wachezaji wake.Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema ratiba hiyo mpya imevuruga mipango yake ya kuongeza umakini katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly.“Nilikuwa na programu za mazoezi ambazo nilikuwa nimeziandaa kwa ajili ya mchezo wetu na Al Ahly, lakini kwa ratiba hii ni kama imeharibika kwa sababu mechi za viporo tunazocheza ni ngumu ambazo tulazimika kucheza kwa nguvu ili kupata ushindi, lakini nyingine ni za mikoani hivyo inatubidi kusafiri,” alisema Pluijm.Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema kwa kiasi kikubwa ratiba hiyo haikuzingatia ushiriki wao kwenye michuano ya Afrika na imewapa wakati mgumu kujipanga.Alisema kutokana na ratiba hiyo wanalazimika kufanya mazoezi mara moja kwa siku ili kuwapa muda wa kutosha wachezaji wao waweze kupumzika, ili kupata nguvu za kupambana kikamilifu katika mechi zijazo.Katika marekebisho yaliyotangazwa juzi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara yanaonesha kuwa Yanga itaanza mechi zake za viporo Aprili 3 kwa kuikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na siku tatu baadaye itacheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo huo.
michezo
JUBA, SUDAN KUSINI MAKAMU wa Rais wa Sudan Kusini Dk. James Wani Iga amesema amebaini kuwa ana corona baada ya kufanyiwa vipimo. Akitangaza taarifa hiyo kupitia Shirika la Habari la Taifa la Sudan Kusini alisema: “Sampuli zangu zilichukuliwa siku chache zilizopatikana na leo nimepatikana na ccorona…kwa hiyo ninawaomba raia wote wa Sudan Kusini kwenda kupimwa, hii ni muhimu ili tupunguze kusambaa kwa virusi kwa watu wengi,” alisema . Taarifa ya kupatwa kwa maambukizi ya virusi vya corona kwa Dk. inakuja baada ya viongozi wengine wakuu wa nchi hiyo kutangaza kupatwa na Covid-19 akiwemo makamu rais wa nchi hiyo, Riek Machar na mkewe ambao pia waliambukizwa virusi vya corona mwezi huu. Miongoni mwao ni Dk. Machar aliyesema kwamba yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, walipata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo. Wakati huo Machar alisema kwamba hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa lakini atajiweka karantini kwa siku 14. Walitangaza kwamba virusi hivyo vimefikia kwenye kambi ya waliotoroka makazi yao ambao wamekuwa wakiitaka Umoja wa Mataifa iwalinde katika mji mkuu wa Juba tangu 2013. Nchi hiyo bado inakabiliana na baa la njaa hata baada ya Machar na Rais Salva Kiir,  waliokuwa mahasimu kuunda serikali ya Umoja wa Taifa Februari. Viongozi hao wawili bado hawajakubaliana masuala ya msingi kama udhibiti wa majimbo. Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi. Mawaziri 10 tayari wameambukizwa virusi vya corona nchini humo, kulingana na taarifa iliyotolewa mwezi huu na msemaji wa serikali katika mahojiano na BBC. Waziri wa Habari wa Sudani Kusini, Michael Makuei aliiambia BBC kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na corona nchini humo. Katika mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hakukutwa na maambukizi. Iliripotiwa kuwa mawaziri hao waliambukizwa Covid-19 baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona. Mawaziri wote 10 walijitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya. Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo pia walikutwa na virusi na na kuwekwa karantini. Mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kupata corona Sudani Kusini, huku watu wane wakipona na sita kufariki. Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya hatari ya kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya wa nchi hiyo ambao una uwezo mdogo kutokana na mgororo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambao umeathiri ustawi wa maendeleo. Kwa sasa Rais Kiir ameweka tofauti zao za kisiasa kando na kutengeneza serikali ya umoja wa kitaifa, japo hawajaweza kukubaliana katika baadhi ya mambo ya msingi kama udhibiti wa majimbo. Wakati corona ikiendelea kuleta wasiwasi, nchi hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa chakula kwa sasa. BBC
kimataifa
 NEW YORK, MAREKANI UMOJA wa Mataifa (UN) umetahadahrisha kuwa kuna uwezekano wa kujiri uhalifu wa kivita Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya watu kadhaa kuuawa na makundi ya watu wenye silaha. Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNJHRO) imechapisha ripoti inayosema mauaji, vitendo vya kikatili, ubakaji na vitendo vingine vinavyokiuka sheria za haki za binadamu vimekithiria na vinatekelezwa na wanamgambo wenye silaha Kaskazini Mashariki mwa DRC, hasa kabila la Walendu. Ripoti hiyo ilisema vitendo hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ripoti yake, Ofisi ya UNJHRO ilisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, watu wasiopungua 296 wameuawa, 151 kueruhiwa na wengine 38 kubakwa, wakiwamo wanawake na watoto. UNJHRO ilisema vitendo hivyo vya kikatili vilitekelezwa na waasi kutoka kabila la Walendu kati ya mwezi Novemba mwaka uliopita na mwezi Aprili mwaka huu. Baada ya miaka kadhaa ya utulivu, ghasia za kikabila zimeongezeka tangu mwezi Desemba 2017, hasa kutokana na mizozo ya ardhi.
kimataifa
NA TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Baga Investment imeshindwa kulipa kwa wakati posho za baadhi ya wafanyakazi wake kwa madai ya kuidai Mamlaka ya Bandari Tanzani(TPA) Sh bilioni mbili. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Jumbe Moshi, aliyasema hayo jana baada ya kuwapo kwa malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wanalipwa kwa siku kudai kutolipwa posho zao kwa siku 23. Alisema ni zaidi ya miezi mitatu sasa TPA imeshindwa kuwalipa fedha hizo hivyo kushindwa kulipa madeni yanayowakabili yakiwamo ya benki. “Kuchelewa kulipwa kwa wafanyakazi wetu kunatokana na TPA kushindwa kuilipa kampuni kwa miezi mitatu, jambo ambalo linarudisha nyuma utendaji wa kampuni. “Hali hii imetuweka katika wakati mgumu kutokana na kampuni kudaiwa na baadhi ya benki, hali inayofanya tushindwe kulipa na kujiendesha,” alisema Moshi. Awali baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Baga Investment, walidai kuwa hawajalipwa posho hizo kwa siku 23 sasa. Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema kila walipouliza walijibiwa kwamba chimbuko la kuchelewa huko kumesababishwa na TPA  ambayo haijailipa kampuni hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu. Akizungumzia malalamiko hayo, Msemaji wa Bandari, Janet Ruzangi, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu kampuni hiyo inalipwa kwa wiki. “Sijui mkataba wao na TPA unasemaje lakini mara nyingi malipo yao yanakuwa kwa wiki au mwezi kwa sababu Baga Investment mpaka wameingia mkataba na kuendesha shughuli hiyo ina maana walikuwa wanazo fedha za kutosha na si mpaka walipwe,” alisema Ruzangi.
kitaifa
MWENYEKITI wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ametoa onyo kwa wachimbaji na wanunuzi wa madini nchini, kuacha tabia ya kufanya biashara ya madini nje ya masoko rasmi na yanayoendelea kuanzishwa mikoa yote hapa nchini.Profesa Kikula amesema yeyote atakayekutwa anafanya biashara ya madini nje ya masoko rasmi atakumbana na mkono wa sheria, ikiwemo kutaifishwa madini na kila aina ya rasilimali iliyotumika kuwezesha ufanyikaji wa biashara hiyo.Profesa Kikula alisema hayo juzi muda mfupi mara baada ya kukagua soko la madini mkoani Iringa ambako hakuridhishwa na takwimu za uuzaji wa madini ya dhahabu katika soko hilo.Alitolea mfano wa takwimu zilizotolewa na Mkaguzi wa Madini kituo cha Iringa Severine Haule kuanzia Mei 30 hadi Juni 14, mwaka huu ni gramu 92 tu za dhahabu zimezalishwa na kupita sokoni hapo.Alisema kuwa ziko taarifa za ujanja ujanja kufanya biashara ya kuuziana madini usiku wilayani Tunduru, wengine kutorosha madini kuelekea Malawi kwa wilaya ya Songea na Mbinga, na Iringa wachimbaji wadogo, wanunuzi wa kati (Brokers) na wanunuzi wakubwa (Dealers) kuuziana madini kwa siri kutofikisha madini kwenye soko.Alieleza kuwa taarifa zote hizo serikali inazo hivyo aliwataka wadau wote wanaohusika na michezo hiyo waache mara moja na kama wataendelea wajue siku zao zinahesabika.Alisema serikali haina mzaha kuhusu suala hilo na alitoa wito kwa wadau wote kujiepusha na utoroshaji wa madini sambamba na kufanya biashara nje ya masoko.Alisisitiza kuwa jicho la serikali linaona mbali hivyo asijidanganye mtu. Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo aliendelea kuwasisitiza watumishi wa tume hiyo mikoa yote nchini kuzingatia uadilifu na kwamba kamwe wasikubali kushawishika kwa rushwa.Alisema laiti kama yeye angekuwa mwepesi wa kupokea rushwa pengine asingekuwa anaendelea kumsaidia Rais Magufuli kuwatumikia wananchi kwani yapo majaribu mengi na majaribio ya watu kumpelekea vifurushi na mabegi ya fedha, lakini hajawahi kuingia katika mitego hiyo katika miaka 46 ya maisha yake yote ya utumishi wa umma.
uchumi
ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM TIMU ya Chelsea ilianza msimu huu wa Ligi Kuu England kwa ushindi mfululizo na kufanya wasifungwe hadi ilipofika Novemba mwaka jana. Ushindi huo ulifanya kuwapo kwa majadiliano mengi kuhusu adithi nzuri inayimuhusu  Maurizio Sarri na  mtindo wake wa ufundishaji  uliompa mafanikio katika klabu yake ya awali ya Napoli. Katika wiki  za mwanzo Jorge Luiz Frello Filho ‘Jorginho’ alijiunga na  klabu hiyo na kuanza kibarua chake kama kiungo mchezesha wa timu hiyo akitokea chini wakati  N’Golo Kanté, akionekana kufurahia jukumu lake jipya akicheza kama winga baada ya kuondolewa kuwa kiungo mkabaji. Lakini  mabadiliko hayo yameanza kuwa na athari hasi kwa Sarri na inaonekana kama furaha ya mashabiki ya kumpokea mgeni huyo imemalizika pale Chelsea. Kwa sasa kiwango cha timu hiyo kimepungua na kitendo cha kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal wiki mbili  zilizopita  kilifanya kupoteza michezo minne kati ya 11  ya Ligi Kuu England. Mbali na  hayo yote kutokea lakini kitu cha kushangaza ni kitendo cha Sarri kuwavaa na kwashutumu wachezaji wake  kwa kushindwa kuelewa mfumo wake akitumia kauli mbalimbali pengine za kuudhi kwa wachezaji. Sarri anasema:“Nataka kuwa mkweli kwao nikiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo na wakati mwingine hata  hadharani.” Hii ni kauli ya Sarri baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu England ambao Chelsea ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya  Bournemouth wiki iliyopita, kichapo ambacho kilimfanya kocha huyo kujifungia katika vyumba vya kubadilishia nguo na wachezaji hao. Uamuzi wa Sarri kuamua kuishi katika njia hiyo  inaweza kuwa hatari anayoitengeneza hasa  kwa kuwa bado mgeni pale Chelsea. Kitecho chake cha kuwapinga wachezaji hadharani kinaweza kuwa na matokeo  mawili:Wachezaji wanaweza kutaka kumuonyesha  kwamba wanaweza kumudu vema mfumo wake wa ‘Sarri-ball’ tofauti anavyofikiria au kikosi hicho ndio kikapotea kabisa. Sarri anatakiwa kumalizana na vijana wake wakiwa faragha kwenye vyumba vya kubalishia nguo lakini si kuwasema ovyo hadharani. Kitendo anachofanya Sarri sasa kilionekana hivi karibuni katika klabu ya Manchester United wakati ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho, dhidi ya wachezaji kama Marcus Rashford, Luke Shaw na Paul Pogba. Kwa kawaida wachezaji huwa katika presha ya kutosha ya kufanya vema mbele ya mashabiki  na vyombo vya habari bila kocha kuweka matatizo ya wachezaji  wake hadharani. Wachezaji wakubwa katika timu hawataruhusu jambo hilo litokee na kuwaathiri kwa kuwa si matokeo ambayo wakati mwingine wanayataka. Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson, amekuwa mmojawapo wa makocha wakubwa wa wakati wote, alikuwa na utawala wa dhahabu usiopingana na wachezaji wake hadharani licha ya kuwa anajulikana sana kuwa mwenye hasira  wakati anapochukia jambo fulani akiwa ndani ya vyumba vya kubadili nguo. Ferguson alitumia njia hii kuwalinda wachezaji wake kwa  mashabiki na  ilimletea ufanisi usio wa kawaida na uaminifu kwa wachezaji wake. Lakini makocha wengi wa kisasa huwa hawapendi kuitumia njia hii.Bado sababu za kushindwa huko hazijawa wazi. Wote Mourinho na Conte waliondoka lakini walitwaa taji la Ligi Kuu kabla uhusiano wao na wachezaji kutofautiana. Katika kipindi hiki kigumu, Chelsea tayari imemsajili kwa mkopo mshambuliaji, Gonzalo Higuin, kutoka Juventus. Raia huyo wa Argentina amefunga mabao mengi wakati akiwa chini ya Sarri katika kikosi cha Napoli na inatarajiwa kufanya sawa kama alivyokuwa wakati huo. Ujio wake unafanya  Eden Hazard abadilishwe nafasi ambayo alikuwa akichweza kama namba tisa ya uongo. Mbelgiji  huyo alionekana kuifurahia nafasi yake  ambayo inamfanya mara nyiki awe na mpira  lakini kwa sasa atakuwa akitokea kushoto. Makocha wengi hupenda kusajili wachezaji ambao waliowahji kufanya nao kazi kwa mafanikio lakini hiyo haina maana kwamba wataendelea kufurahia mafanikio pamoja.
michezo
WAHADHIRI mbalimbali wa vyuo vya elimu ya juu wameunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kwamba baadhi ya shahada zinazotolewa na vyuo vikuu sasa hazina hadhi bali wanafunzi wanamaliza vyuo ili kupata vyeti.Aidha wameshauri kufanyika kwa maboresho ya elimu na kuwe na msukumo wa kuwajali walimu kimaslahi lakini pia kuwaendeleza kitaaluma. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema tatizo la shahada za ‘kudesa’ katika vyuo vikuu nchini ni kubwa na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha nchi inapata wasomi wazuri wanaomaliza vyuo na vyeti vinavyolingana na elimu waliyoipata.Juzi Rais Magufuli akizindua Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha shahada wanazotoa zina viwango vya juu na si shahada za ‘kudesa’ na kuwataka wahadhiri kuwa wakali.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Frank Tillya alisema walimu wanaowafundisha wanafunzi hao nao pia wanachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa elimu ya vyuo vikuu."Walimu nao wanachangia kwa kiasi kikubwa, wengi hawana maadili kwa sababu kama una maadili huwezi kukubali kuona mwanafunzi anatoka hajui kitu, wanafunzi wengi wanatoka hawana kabisa quality (kiwango) ya shahada kwa sababu hawakufundishwa kufikiri," alisema.Alisema wanafunzi wengi wanafanya tu mitihani ili kufaulu, lakini elimu yao haiakisi hadhi ya shahada hata wanapomaliza vyuo, jambo ambalo linaleta changamoto katika kupata kazi kwani wanakuwa hawana uwezo wa kushindana. "Hata ukiangalia 'interview' za kazi utabaini tatizo kubwa kwani vyeti wanavyokuja navyo vinakuwa na ufaulu mkubwa lakini wanapohojiwa unabaini kichwani hawana ujuzi unaofanana na ufaulu wao,” alisema.Dk Frank alisema ingawa Rais Magufuli hakueleza kwa kirefu ukubwa wa tatizo hilo, lakini ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu. Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema shahada ya sasa haimfanyi mhitimu kupata uwezo wa kuchanganua mambo wala kufikiri kwa mapana."Hili ni tatizo la kitaifa sijui tumejikita zaidi katika elimu nyingine, kijana amehitimu chuo lakini ukimwambia akuandikie barua au mpe habari ya kurasa tatu mwambie aifupishe hawezi," alisema Dk Bana. Hata hivyo, Dk Bana alisema moja ya sababu ya kushinda kuimarika kwa kiwango cha elimu ni mfumo wa elimu ya juu ambao alisema hauvidhibiti vyuo kuzalisha elimu bora kwa kiwango cha kutosha.
kitaifa
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao  Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40)  na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele  ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa  kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020  maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
uchumi
KAMATI ya maandalizi ya fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zilizomalizika hivi karibuni imeelezea kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa mlezi wa timu ya vijana, Serengeti Boys, Reginald Mengi aliyefi kwa na mauti usiku wa kuamkia jana, Dubai.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana katika kikao maalumu cha kushukuru waliofanikisha michuano hiyo, Mtendaji wa kamati hiyo Leslie Liunda alisema Mengi atakumbukwa kwa mchango wake kwenye jamii mbalimbali ikiwemo michezo. “Mengi alikuwa mlezi mzuri wa Serengeti na amefanya mambo mengi kwenye jamii, na yanayojulikana dunia nzima,” alisema.Mengi atakumbukwa namna alivyotoa motisha kwa timu hiyo ya vijana ambapo kabla ya kuanza kwa fainali za Afrika aliwaahidi wachezaji angewapa kila mmoja Sh milioni 20 kama wangefanya vizuri na kufuzu kombe la dunia.Aidha, kamati hiyo, imetoa shukrani kwa mdau Mtendaji wa Motisun Group, Subash Patel kutokana na mchango mkubwa aliotoa. Liunda, alisema Patel alitoa vyumba 66, kula na kulala bure katika hoteli ya Whitesands na Sea Clif kwa ajili ya viongozi mbalimbali wa Soka Afrika tangu kuanza kwa michuano hiyo Aprili 14 hadi mwishoni mwa mwezi uliopita Aidha, alitoa maji katoni 7,000 na 4,000 za juisi tangu kufika kwa wachezaji wote hadi kuondoka mwishoni mwa mwezi huu. Liunda aliwaambia waandishi wa habari jana, wameona wamshukuru mdau huyo kwa msaada huo, kwani ni miongoni mwa wadau waliofanikisha kumaliza mashindano hayo salama.
michezo
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana, ilieleza kuwa mradi huo uliozinduliwa mapema mwaka jana, unawakilisha uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 11 (sawa na takribani Sh bilioni 19) na utaongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kutoka mita za ujazo 141,000 hadi mita za ujazo 213,200 baada ya kukamilika.“Zaidi ya hayo, muundo mpya wa muunganiko wa bomba utaongeza ufanisi wa kupokea mafuta ya Automotive Gas Oil (AGO) kutoka kwenye Single Point Mooring (SPM) kutoka kwenye kiwango cha mtiririko cha mita za ujazo 1,500 kwa saa mpaka kufikia mita za ujazo 2,000 kwa saa, ambacho ni kiwango cha kasi zaidi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair.Ili kukidhi ukuaji wa mahitaji ya bidhaa ya mafuta, Belair alisema kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kutengeneza matangi mapya ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa mita za ujazo 100,000 zaidi ili kufikia mita za ujazo 313,200 katika siku zijazo.Kutokana na mradi huo, Belair alisema TIPER ina mpango wa kutandaza mabomba mapya ya kusafirisha mafuta kati ya Kigamboni na Kurasini.“Mradi huu utaongeza ufanisi wa kusukuma kwa kasi zaidi bidhaa kwa wateja wetu waliopo Kurasini,” alisema huku akiongeza kuwa uwekezaji huo utagharimu kati ya Dola za Marekani milioni 12 na 16.Wakati huo huo, kampuni itawekeza kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni 2 ili kubadilisha mfumo uliopo wa kupampu, kwa kuweka pampu zenye uwezo mkubwa zaidi na wenye kuaminika. Pia, mita za utiririkaji (flow meters) zitaongezwa.
uchumi
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemtangaza mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane (pichani) , kuwa ndiye mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal katika mchato wa kutangazwa aliwashinda mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah na winga wa Manchester City, Muargeria Riyad Mahrez, katika tuzo hiyo.Mane, 27, aliisaidia klabu yake hiyo ya London kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu wa mwaka 2018/19. Hadi sasa amefunga mabao 15 katika msimu wa mwaka 2019/20, huku Liverpool ikiwa na pointi 13 zaidi ya timu iliyopo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.“Kwa kweli nimefurahi sana na kujivunia hii kazi yangu ya kucheza soka, naipenda sana.”“Napenda kuishukuru familia yangu, timu yangu ya taifa, viongozi wangu na hata shirikisho la soka la nchi yangu na klabu yangu ya Liverpool, kwakweli hii ni siku kubwa sana kwang,” alisema Mane baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.Mane alipokea tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika mji wa Hurghada, Misri, lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo miaka miwili iliyopita au Mahrez aliyekuwepo ukumbini hapo.Mane alimaliza katika tatu bora katika tuzo za miaka mitatu iliyopita na kwa muda mrefu alikuwa akiisaka tuzo hiyo ili kufanikisha mafanikio yake ambayo aliyapata mchezaji wazamani wa Liverpool, El Hadji Diouf pia raia wa Senegal aliyeshinda mwaka 2002.LIGI KUU ENGLANDWachezaji wa Ligi Kuu ya England wamekuwa wakifanya vizuri katika tuzo za CAF, ambapo Mahrez alishinda tuzo moja ya bao la mwaka la Afrika baada ya mpira wake wa adhabu kutinga wavuni alipoifungia Algeria ilipocheza dhidi ya Nigeria katika nusu fainali ya Afcon.Salah, Mane na Mahrez wote wanaunda kikosi bora cha wachezaji 11 wa timu ya Afrika, huku beki wakati wa Liverpool Joel Matip, beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier na mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang nao wakiwamo.Wachezaji wanaounda kikosi bora cha wachezaji 11 wa Afrika: Andre Onana (Ajax/Cameroon), Achraf Hakimi (Borussia Dortmund/ Morocco), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal), Joel Matip (Liverpool/Cameroon) na Serge Aurier (Tottenham/ Ivory Coast).Wengine ni Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria), Idrissa Gana Gueye (Paris St-Germain/Senegal), Hakim Ziyech (Ajax/Morocco), Mohamed Salah (Liverpool/ Egypt), Sadio Mane (Liverpool/ Senegal), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/ Gabon) Beki wa kushoto wa Morocco Achraf Hakimi, 21, anayeichezea kwa mkopo Borussia Dortmund akitokea Real Madrid, ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka.Mshambuliaji wa Nigeria na Barcelona, Asisat Oshoala, alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa upande wa wanawake baada ya kuwashinda mshambuliaji wa Cameroon, Ajara Nchout na wa Beijing BG Phoenix na mshambuliaji wa Afrika Kusini, Thembi Kgatlana.Cameroon, ambayo ilifungwa 3-0 na England katika hatua ya 16 bora katika fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake mwaka 2019, imetwaa tuzo ya timu bora ya taifa ya Afrika ya mwaka, huku mabingwa wa Afrika Algeria wakutwaa tuzo hiyo kwa wanaume.Djamel Belmadi, aliyeiongoza Algeria kutwaa taji la Afcon, ametwaa tuzo ya kocha bora kwa upande wa timu za wamaume, huku Diseree Ellis, kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.
michezo
PEP Guardiola amesema ni wendawazimu na upuuzi kwa Manchester City kufi kiria kuhusu kutwaa taji licha ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burnley juzi usiku.City imejikongoja mpaka kufikia tofauti ya pointi nane dhidi ya vinara Liverpool, shukrani kwa Gabriel Jesus aliyefunga mabao mawili na mabao mengine kutoka kwa Rodri na Riyad Mahrez lakini Guardiola anaona bado hana nafasi ya kukipiku kikosi cha Jurgen Klopp.“Kwa umbali tuliona nao na Liverpool itakuwa wendawazimu kufikiria kuhusu kutwaa taji,” alisema Guardiola.“Kama kila mmoja anavyosema tupo nje ya mbio, hatuna nafasi.”“Tunajifikiria wenyewe na mechi ijayo, kufikiria njia za kushinda ili kuwakaribia ni upuuzi.”City ilijiandaa kwa mechi hiyo kwa kuimba wimbo wa Oasis, Wonderwall kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Na Guardiola alitania kwamba itakuwa hivyo kwenye Uwanja wa Etihad watakapokutana na Manchester United.Jesus ni kama alifanya mazoezi kwa ajili ya debi hiyo kwa kufunga bao lake la kwanza tangu Oktoba na Guardiola alikiri umuhimu wa Mbrazil huyo na namna anavyojiamini huku Sergio Aguero akiendelea kuwa nje kutokana na kusumbuliwa na nyama.“Tulimhitaji kufunga mabao haya,” alisema Guardiola.“Yatamsaidia yeye na timu, tumempoteza mshambuliaji hatari Sergio”.
michezo
NA MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu, yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini, Dar es Salaam. Kubainika kwa makontena hayo, yaliyokuwa yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binafsi ya TICTS, kumekuja siku tatu tu baada ya Rais Dk. John Magufuli kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa.      Rais Magufuli alifika bandarini siku hiyo kukagua utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kutoka migodini. Akizungumza baada ya kukamata makontena hayo, Mkurugenzi Mkuu wa  TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, alisema yalibainika jana  katika msako mkali unaoendeshwa na mamlaka hiyo. “Makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es Salaam,” alisema Mhandisi Kakoko. Alisema mbali na makontena hayo, TRA pia imegundua mengine sita yaliyokuwa yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa. Aliongeza kuwa orodha ya makontena hayo  inaonyesha yalifika bandarini hapo kwa nyakati tofauti kutoka mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama unaosimamiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia   na kontena nyingine zimetoka Pange Mines. Alitoa wito kwa kampuni za madini zenye shehena za mchanga zijitokeze na kuonyesha mizigo waliyonayo   kabla haijabainika katika msako unaoendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima. Wakati Mkurugenzi huyo wa TPA akisema hayo, Mhandisi Asa Mwaipopo ambaye ni Meneja Mkuu-Uhusiano na Serikali wa Kampuni ya Acacia, alisema makontena hayo ni halali kwani yamekaguliwa na kulipiwa kodi zote kupitia mamlaka za Serikali. “Tuna migodi miwili inayozalisha copper concentrate. Copper concentrate zinapakiwa kwenye makontena na kuyasafirisha nje, makontena hayo yanazalishwa kwa idadi kubwa, kwa siku  mgodi mmoja unazalisha kontena nne au tano. Kwa hiyo kwa siku ‘average’ ni kama kumi kwa migodi miwili. “Yanasafirishwa kwa idadi ya makontena 25 au 30, labda kwa wiki mara moja au mbili hivi, kwa hiyo ni ‘production chain’ ambayo ipo kwa miaka mingi na hata sasa inaendelea kwa sababu uzalishaji unaendelea,” alisema. Alisema lilipotokea katazo la Rais Magufuli Machi 2, mwaka huu la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa dhahabu, uzalishaji ulikuwa unaendelea kama kawaida. “Ni kama vile ukisimamisha kiwanda cha bia ku-produce (kuzalisha) bia, kuna bia zitakuwa kwenye bottling (chupa), kuna bia zitakazokuwa kwenye packaging, it’s a chain. Kwa hiyo kuna makontena ambayo yalikuwa kwenye yadi ya clearing and forwarding, ni wakala wetu, kuna makontena ambayo yalikuwa yamepelekwa bandarini kwa ajili ya kuwa loaded (kupakiwa), kuna makontena yalikuwa barabarani,” alisema na kuongeza: “Hayo makontena ndiyo idadi hiyo ambayo wamekwenda wameyakuta kwenye yadi ya mtu aliyekuwa anakaribia ku-export (kusafirisha nje), ni makontena halali yamepimwa, yamewekewa seal na TRA, yamewekewa seal na Tanzania Mineral Audit Agency, mamlaka za Serikali, yametolewa leseni ya export na Wizara ya Nishati na Madini, yana leseni yamelipiwa loyalty (mrabaha) asilimia nne na Serikali imechukua hizo hela,” alisema Mwaipopo. Machi 2 mwaka huu, Rais Magufuli alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini ya dhahabu nje ya nchi, akisema kuwa ni wizi kwa sababu mchanga ukifika huko unachambuliwa na kupatikana dhahabu.
kitaifa
NA FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM CHAMA cha wasambazaji filamu nchini kimesema kila msambazaji au msanii anapaswa kununua stempu za kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TCRA), kabla ya kuziiingiza sokoni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Moses Mwanyilu, alisema baada ya kupitia hatua mbalimbali kama vile BASATA kwa kazi za muziki, COSOTA na bodi ya filamu kwa ajili ya ukaguzi, zibandikwe stempu kabla ya kuingizwa sokoni. Alisema baadhi ya wafanyabiashara na wasambazaji wa muziki kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingiza na kuuza bidhaa hizo bila kufuata utaratibu, ikiwemo kutolipia kodi na kuuza kwa bei ya chini ukilinganisha na filamu za hapa nchini na kusababisha soko la filamu za ndani kushuka. “Filamu za nje zimekuwa hazina maadili ya Tanzania na filamu za ndani wanadurufu na kuziingiza sokoni bila wasanii kunufaika na kazi zao. “Tunapenda kutoa shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kufanya operesheni ya kukamata kazi ambazo zinauzwa kinyume cha sheria katika eneo la Kariakoo,” alisema. Hata hivyo, wameiomba Serikali operesheni hiyo iwe endelevu katika maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine.
burudani
Derick Milton -Simiyu IKIWA ni takribani mwezi mmoja tangu Januari 9, Baraza la Mitihani (NECTA), lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne na Yohana Lameck (19) kuibuka shujaa wa shule za kata kwa ufaulu wa A tisa licha mazira magum aliyokuwa nayo, baba yake aliyeikimbia familia kwa miaka saba, ameibukia kwenye hafla ya kumpongeza. Yohana aliyekuwa akisoma shule hiyo ya kata iliyopo wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, kwa miaka saba alikuwa akiishi na mama yake huku wakiwa na maisha magumu ambapo wakati mwingine, alilazimika kuacha shule na kufanya kazi za vibarua za kulima, kuchunga ngombe ama kusukuma mikokoteni ili aweze kupata chakula. Walimu wake wa shule ya msingi, ndio waliompeleka shule ya sekondari baada ya kumuona mtaani licha ya kwamba amefaulu na alipokuwa sekondari, kuna wakati aliacha shule kwa miezi mitatu baada ya kukosa mahitaji muhimu ikabidi walimu wake wamsake na kumrudisha shuleni na kumpa mahitaji kama sare na chakula. Katika shule aliyosoma Yohana wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa  88 ambapo yeye pekee ndiye aliyepata daraja la kwanza. Waliopata daraja la pili ni wanne, daraja la tatu 15, daraja la nne 54 na sifuri 13 huku shule yake ikishika nafasi ya 79 kati ya shule 100 kwenye mkoa na nafasi ya 1991 kati ya shule 3908 kitaifa. Kwa mujibu wa matokeo hayo masomo aliyofanya Yohana na ufaulu wake kwenye mabano ni Civics (A)  Historia (A), Jographia (A) Kiswahili (A) Kingereza (A) Phizikia (A) Kemia (A) Bayolojia (A) na Hisabati (A). Baba aibuka Juzi Mkoa wa Simiyu, ulifanya hafala ya kupongeza wanafunzi waliofaulu mtihani huo ambapo Lameck Lugedenga baba mzazi wa Yohana aliibuka na kufanya minong’ono kuibuka ukumbini. Aliwasili ukumbini hapo akiwa ameambatana na mke wake Mariamu Lulyalya pamoja na Yohana. Baada ya kutambulishwa kuwa ndiye baba mzazi wa Yohana, kulizuka gumzo na minong’ono ukumbini kwani taarifa za kutelekeza familia kwa miaka saba zilikuwa zinajulikana badaa ya kuandika na vyombo vya habari. Lugedenga  alimuacha Yohana akiwa darasa la nne Shule ya Msingi Igaganulwa, kutokana na umaskini na ilidaiwa alikimbilia mkoani Morogoro. Akiongea na Mtanzania mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo, Lugedenga alisema ni kweli alikiimbia familia yake, kutokana na kuchanganyikiwa mara baada ya kifo cha mtoto wake wa kike Magreth aliyefariki dunia mwaka 2011. Alisema Magreth alikuwa mmoja wa wanafunzi wenye uwezo mkubwa shuleni kumzidi Yohana, lakini baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hosptali ya Wilaya Bariadi (Somanda) alipoteza maisha. “Marehemu alikuwa na uwezo mkubwa darasani, lakini alipoteza maisha zikiwa zimebaki siku mbili afanye mtihani wake wa kuhitimu darasa la saba, baada ya hapo nilichanganyika nikaamua kuondoka maana nilikata tamaa,” alisema Lugedenga. Alisema mbali na hilo, ugumu wa maisha ulimfanya akate tamaa zaidi na kuamua kuondoka nyumbani kwake kwenda mkoani Morogoro kwa wazazi wake ambao walihamia huko muda mrefu. “Niliunganisha vitu vyote hivyo nikaona niondoke, maana sina msaada na sina uwezo wa kuisadia familia yangu ni bora kuondoka nikatufute maisha sehemu nyingine,” alisema Lugedenga Alisema mawasiliano na familia yake yalikuwepo ingawa kwa kiasi kidogo sana, kwani hata huko alipohamia hakuweza kufanikiwa kimaisha kutokana na kuendelea kupata matatizo ikiwemo kupoteza wazazi wake wote. Aisema hakuwa na uwezo tena wa kuisadia familia yake na taarifa za mtoto wake Yohana kutaka kuacha shule alizipata, lakini alimsihi asiache bali awe mvumilivu kwani na yeye hana huwezo wa kumsaidia. Aomba radhi Lugedenga aliwaomba radhi mke wake na mtoto wake, kwa alichowafanyia na kusema hawezi kurudia tena na imekuwa fundisho kwake. Alisema mtoto wake Yohana kufanya vizuri kwenye mtihani, kimefanya familia yake kuungana tena kwa mara nyingine na kamwe hawezi kurudia tena kuitelekeza. “Nimejifunza siyo vizuri kuitelekeza familia hata kama ni shida, lazima uvumilie upambane nazo ukiwa na familia yako, nakiri nilikosena na ninashukuru mke wangu amenipokea tuendelee na maisha,” alisema Lugedenga. Lugedenga alisema kwa kwa sasa hawezi tena kurudi Morogoro, bali ataanza maisha mapya na mke wake na mtoto wake licha ya kuwa hana uwezo atapamba kuhakikisha anahudumia familia yake. “Nimekuja moja kwa moja siwezi tena kurudi Morogoro, bado maisha yangu ni magumu lakini nitapambana hivyo hivyo na mke wangu tuweze kuishi kama zamani,” alisema Lugedenga Alisema kwa sasa anajisikia mwenye nguvu kutokana na alichokifanya mtoto wake, huku akiwashukuru walimu na wananchi ambao walimsaidia Yohana kupata mafanikio hayo. Lugedenga alisema licha ya kuishi Morogoro kwa muda mrefu hajawahi kuwa na familia nyingine, bali alikuwa akiishi na wazazi wake na kujishughuliza na kilimo hivyo hana mke wala mtoto mwingine. Mke anena Mariamu Lulyalya alisema amemsamehe mme wake, kwani anajisikia mwenye furaha kuweza kuungana tena naye  baada ya kuwakimbia kwa miaka saba. Lulyalya anasema licha ya kutendewa mambo yote na mme wake, na kuachiwa mzigo wa kulea watoto, hawezi kumkataa kwani ndiye mme wake halali na wamefanikiwa kupata watoto watano. “Leo najisikia mwenye nguvu sana, nashukuru mme wangu amerudi na tuko pamoja, alikuja nikampokea maana ni mme wangu na nimesamehe ili tuweze kuendeea na maisha,” alisema Lulyalya. Yohana. Yohana alisema kitendo cha baba yake kurudi nyumbani kumempa nguvu na anajisikia mwenye furaha kutokana na kukosa malezi yake kwa muda. “Ni kweli mimi ni shujaa, bila mimi nahisi Baba asingerudi nyumbani, lakini kutokana na hiki ambacho nilikifanya leo amerudi, najisiki mwenye furaha sana, kama mtoto nilikuwa najisikia vibaya kukosa malezi ya baba,” alisema Yohana. Mkuu wa Mkoa. Awali Mkuu wa Mkoa huo, Antony Mtaka, alimtaka mzazi wa Yohana kuwa karibu na familia yake na kuhakikisha anamsaidia Yohana afike mbele zaidi ili aje kuwa msaada kwake. Mtaka alimtaka Lugedenga kuhakikisha anashikamana na mtoto wake ikiwemo kuwasimamia wadogo zake kuhakikisha wanapata elimu, ili wawe msaada kwake na mke wake. Akizungumzia matokeo ya kidato cha nne, Mtaka alisema mkoa kushika nafasi ya tano ndiyo lilikuwa lengo. Aliwashukuru wadau wote wakiwemo wazazi, walimu na viongozi kwa kusaidia kufikia malengo hayo, huku akibainisha kuwa wataweka mikakati mipya kuhakikisha mkoa unashika nafasi tatu za juu.
kitaifa
UNAWEZA kusema kwamba, kwa sasa ni rahisi kununua umeme Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ).H ali hiyo inatokana na taarifa ya wachambuzi wa kimataifa wa bei za mafuta na umeme ambao katika ripoti yao mpya inayoelezea gharama za umeme inaeleza kuwa Tanzania, ndiyo nchi pekee ya jumuiya hiyo yenye umeme wa bei nafuu ikifuatiwa na Kenya.Taarifa iliyochambuliwa na kutolewa hivi karibuni kupitia tovuti ya globalenergyprices inaonesha kuwa, Mtanzania wa kawaida anaweza kununua umeme kilowati moja kwa Sh 228 tu na hivyo kuwaneemesha wale waliopo nchini kuliko wengine wa Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, taarifa iliyotoka O ktoba mosi mwaka huu ikichambua bei za umeme za tangu Juni mwaka huu ambapo zaidi ya nchi 80 duniani zilichambuliwa na bei ya wastani ya kilowati zilibainishwa, Tanzania ilionekana kuwa na bei nafuu zaidi ya umeme kwa matumizi ya nyumbani ukilinganisha na nchi zingine Afrika Mashariki.Mambo makuu waliyoyaangalia katika uchambuzi huo ilikuwa ni gharama za Kodi ya O ngezeko la Thamani (VAT), gharama za usambazaji na usafirishaji, mfumuko wa bei na thamani ya fedha ya Tanzania. Tanzania ilionekana kuwa na bei nafuu ikifuatiwa na Kenya ambapo bei ya kilowati moja ni Sh 338.9 huku Uganda ikitoza wananchi wake Sh 392 kwa kilowati moja.Nafuu zaidi yaja Kulingana na gharama hizo ambazo zina unafuu zaidi kwa wananchi wa Tanzania, ifikapo 2025 huenda wananchi wakapata unafuu mkubwa zaidi wa bei baada ya kukamilika kwa mradi wa Stiegler’s G orge unaotarajiwa kuzalisha megawati 2,100 zitakazoingia kwenye G ridi ya Taifa. Mradi huo wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji, ndani ya H ifadhi ya Selous utaongeza uzalishaji wa umeme nchini Tanzania maradufu na huenda bei ya umeme kwa kilowati ikapungua marudufu.Mradi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni mbili ambazo zitatolewa na Serikali ya Tanzania, utawanufaisha watanzania lakini pia kwa nchi wanachama wa EAC ambao watanunua umeme kutoka nchini. Kodi kwenye umeme Ikiwa moja ya viashiria kuwa umeme wa Tanzania una bei nafuu unatokana na uchambuzi wa kodi, usafirishaji na usambazaji, nchini Tanzania, Kodi ya O ngezeko la Thamani (VAT) inayotozwa kwa mteja wa umeme wa majumbani ni asilimia 18 wakati Kenya wanatoza asilimia 16 na Uganda wanatoza asilimia 15.Kwa takwimu hizo na mfumo wa uchambuzi iliotumika kwenye tovuti ya globalenergyprices ni wazi kuwa Tanzania imepunguza umeme kwa kutoza gharama ndogo kwenye huduma yaani usafirishaji na usambazaji pamoja na kupunguza matumizi ya mafuta. Pia huenda thamani ya sasa ya fedha pamoja na mfumuko wa bei nao ukachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa bei tofauti na V AT inavyotozwa.Kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya Mwaka 2008, Kifungu cha 23 (2) na 23 (3) marekebisho ya umeme hutokana na mabadiliko ya bei za mafuta, thamani ya fedha na mfumuko wa bei huhusika kwenye kushuka au kupanda kwa bei. Bei duniani kote Wakati bei ya umeme ikipunguzwa mara kwa mara nchini, tathmini iliyofanywa kwa mataifa zaidi ya 80 inaonesha kuwa bei ya umeme imeongezeka kwa wastani wa asilimia 1.65 tangu Machi mwaka huu. Kwa mujibu wa takwimu zilizochambuliwa, wastani wa bei ya umeme kilowati moja dunia kwa sasa inauzwa dola za kimarekani 0.150 (sawa na Sh 339).Nchi zenye bei kubwa zaidi ya umeme duniani ni Bermuda (kisiwa chini ya himaya ya Uingereza) wanaouza kilowati moja kwa Sh 876.9 wakati Denmark nao wakiuza kwa Sh 849.75 Ujerumani hao wakiuza umeme kwa Sh 793. Kwa upande wa umeme unaouzwa kwa bei ndogo zaidi; nchi ya Iraq inauza umeme kwa Sh 18.1 kwa kilowati moja, ikifuatiwa na Misri inayouza kwa Sh 40.7 wakati Q atar ikishika nafasi ya tatu ikiuza kwa Sh 58.9.Aidha kwa mujibu wa uchambuzi wao, wananchi wa mabara ya Ulaya, Amerika Kusini na Australia ndiyo wanaolipa gharama za juu kwa kilowati za umeme wakati umeme wa bei nafuu unapatikana kwenye bara la Asia, hasa kwenye nchi zinazoongoza kwenye uchimbaji wa mafuta. Asemavyo mtaalamu Mhadhiri katika Shule ya Uhandisi ya C huo Kikuu cha Makerere, Dk Mackay O kure anasema Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine za EAC inatumia nishati mbadala ili kupambana na changamoto ya kuwa na umeme wa uhakika, lakini umeme utakapozalishwa kwa uhakika na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, huenda bei za umeme zikashuka muda hadi muda.Anasema, “Kuna sera ambazo zipo kwenye nchi za EAC , isipokuwa Burundi na Sudan Kusini, lakini zote zinalenga umeme wa uhakika. Nchi zote zinataka wananchi wake wawe na uwezo wa kupika kutumia umeme, lakini pia sekta ya usafirishaji itumie umeme… “… yote hii ni kurahisishia maisha wananchi, lakini iwapo miradi iliyowekwa na nchi hizo kama Tanzania, Kenya na Uganda itakamilika, hakika tunaweza kushuhudia bei ya umeme ikishuka, kwani bei inapangwa kulingana na upatikanaji wa uhakika wa umeme,” anasema mhadhiri huyo raia wa Uganda.
kitaifa
Kuna msemo unasoma ukienda Rumi ishi kama Warumi! Hebu anza na kavideo haka katamu kutoka kwa Konde Boy cha yeye na mpenzi wake. FANYA KAMA UNADUNDA….!!!!! AAAH UNADUNDA….!!! 🕺💃 #NIKOMESHE @princedullysykes x #KONDEBOY OUT NOW A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on Jun 10, 2019 at 4:39am PDT Ebwana licha ya kuwepo uvumi ulionezwa kwa kasi na yule mwanadada wa anayekaa Marekani kuwa Harmonize ama Konde Boy juu ya kupata mtoto nje.Hali inavyoonekana bado penzi lake na mrembo kutoka Italia, Sarah na Msafi huyo bado liko imara. Harmonize ni lazima atakua kwenye penzi zito sana na muitaliano huyo kwakua anamshirikisha karibia shughuli zake zote azifanyazo. Ukiangalia hata baadhi ya perfomances na baadhi ya nyimbo amethubutu kumtaja mpenzi huyo. Haya twende kwenye mada husika kwanza siku ya juzi Harmonize alishare kwenye insta story yake akiwapa magari wazazi wake na alisikika kumuita baby wake Sarah aje awachagulie magari baba na mama yake. Cheki hapa picha Sarah alivyotoka ndani.. Hiki ndicho kilichowakasirisha wabongo bana mtandaoni wakidai kuwa sio utamaduni wetu na kwenda mbali zaidi na kudai huwezi kuwa mbele kwa wakwe zako na kuwavalia alichovaa Sarah. Cheki hapa baadhi ya koment za wananchi wa mtandaoni (Netzens) Baadhi ya mashabiki wao waliingilia kati suala hilo kwa kuanza kumpa somo bibiye kuwa huo sio utamaduni wa mtanzania. Hope hatorudia sio kwa komenti hizi.. Kweli jamani lakini mbele ya wakwe kuvaa vile mhh sijuw labda mm mshamba nibaki iviivi😢😢😢 Sarah mama ulishindwa vaa ata diraa… Sema fresh pesa kumaanina apo ata ungevaa bikini 👙 mbele ya mkwe fresh🤣💃💃💃 SITAKI huu Uzungu kwa wanangu😆….. Aaamin inshallah Ila ata kama n uzungu sio Vizuri mwanamke kuvaa mavazi kama ya Sara mbele ya wakwe zake 😆 Sasa uyo mzungu ndo kashindwa jistiri jaman mbele ya wazaz mhh Hicho kimini   Best Couple In My Life..!!! 🤴👸 A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on Jun 13, 2019 at 9:45am PDT Sema it seem Harmonize yuko sawa na mavazi ya baby wake huyo, kukukumbusha tu kuwa Harmonize ashawahi mtumie baby wake huyo kama video vixen kwenye wimbo wake wa Niteke uliokuwemo kwenye Ep ya AfroBongo. Enjoy hapa!      
burudani
Na LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema matukio ya uhalifu kati ya Januari na Novemba mwaka huu yamepungua ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Aliyasema hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alisema matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi vya kanda hiyo kwa mwaka huu ni 126,200 ikilinganishwa na matukio 129,602 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka uliopita. Alisema idadi hiyo ni sawa na upungufu wa matukio 3,405 ambayo ni sawa na asilimia 2.6 ya matukio yaliyotokea mwaka jana. “Katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2017, kulikua na jumla ya matukio makubwa ya jinai 9,736 ikilinganishwa na matukio 12,550 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho 2016 sawa na upungufu wa matukio 2,814 sawa na asilimia 22.4. “Hali ya uhalifu katika Kanda ya Dar es Salaam ilikuwa ya kuridhisha ingawa kulikuwa na matukio machache ya unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji, wizi wa magari na pikipiki,” alisema Mambosasa. Alisema jumla ya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha  yaliyotokea mwaka jana ni 127, huku mwaka huu yakiwa ni 59 tu, sawa na upungufu wa matukio 68, unyang’anyi wa kutumia nguvu yalikuwa 757 mwaka jana huku mwaka huu yakishuka na kufikia 328. “Polisi katika juhudi za kuimarisha usalama wa wananchi, iliimarisha doria na misako mbalimbali sehemu zote za jiji ambapo wahalifu wapatao 18,194  walikamatwa kwa tuhuma mbalimbali. “Majambazi sugu wapatao 36  walikamatwa kutokana na makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, nguvu, uvunjaji na wizi wa magari,” alisema Mambosasa. Alisema katika kipindi hicho jumla ya silaha 27 na risasi 1,147 zilikamatwa,  kati ya hizo SMG 2 na risasi zake 324, bastola 15 na risasi 127, Shortgun 6 na risasi 394 na riffle 4 na risasi 263 na watuhumiwa 25 walikamatwa. Alisema dawa za kulevya aina ya cocaine yenye uzito wa kilogramu moja na gramu 444, heroine kilogramu 2  na gramu 234, vilikamatwa huku jumla ya watuhumiwa 352 wakitiwa nguvuni. Pia Mambosasa alisema jumla ya noti bandia 102 zenye thamani ya Sh 53,794,000 zilikamatwa na watuhumiwa 1,124 walitiwa nguvuni. Wahamiaji haramu waliokamatwa ni 193 ambapo jumla ya kesi 109 zilifunguliwa kwa makosa ya kuingia nchini na kuishi bila kibali kwa raia hao wa nchi za  Kenya, Malawi, Uganda, India, Nigeria, Ethiopia na Somalia. Wakati huo huo, Mambosasa amepiga marufuku wakazi wa jiji hilo kusherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kuwasha matairi na fataki kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
kitaifa
WATU 12 wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Mbeya, Mwanza, Tabora, Arusha na Mara.Kati yao wamo watoto wawili waliokula ugali wa muhogo, wivu wa mapenzi, watatu wa ajali ya barabarani na dereva teksi aliyeuawa na kukutwa ndani ya gari lake akiwa amefungwa mikono yake kwa waya.Mkoani Mbeya, watu watatu wamefariki dunia Mbeya baada ya ajali ya barabarani, iliyosababishwa na kugongana kwa magari mawili jana asubuhi katika eneo la Kanyengele maarufu kwa jina la Airport Kijiji cha Ibula, Kata ya Kiwira wilayani Rungwe.Eneo hilo kwa miaka mingi, limekuwa na ajali kutokana na mteremko mkali wenye kona na chanzo cha kupewa jina la Airport.Gari nyingi zinazowashinda madereva barabarani, hupaa na kutumbukia katika korongo lililopo upande mmoja wa barabara, ambako gari ndogo ikitumbukia, mtu anayepita barabarani, si rahisi kujua kilichotokea.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilihusisha lori la mafuta lenye namba za usajili T257 CZA aina ya Howo, ikiwa na tela lenye namba ya usajili T.597 CRR mali ya Kampuni ya Camel Oil ya Dar es Salaam lililokuwa linatokea Mbeya kwenda Malawi, kupeleka mafuta ya dizeli, na gari namba T.840 CLY aina ya Canter mali ya Kampuni ya Rungwe Spring Water ya mkoani Mbeya.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni lori la mafuta, kufeli breki na kusababisha kwenda kuigonga Canter. Kwa kuwa lilikuwa katika mwendo mkali, lilisababisha vifo vya watu hao watatu, wakiwamo madereva wa magari yote mawili.Aliwataja waliokufa ni dereva wa tangi, Frank Sagumo maarufu kwa jina la Chota (48) mkazi wa Morogoro na utingo wake aliyetambulika kwa jina moja la Silasi pia mkazi wa Morogoro.Pia dereva wa gari ya Kampuni ya Maji Rungwe, Nelson Samson (35) mkazi wa Airport jijini Mbeya.Alisema magari yote mawili, yameharibika na kumwaga mafuta aina ya dizeli. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe ya Makandana.Katika tukio la Ukerewe mkoani Mwanza, Mkuu wa wilaya hiyo, Colonel Magembe alisema watu 25 wa familia nne, waliathirika baada ya kula ugali wa muhogo.Watoto wawili, Kumbuka Mtani (14) na Gidion Bihemo (3) walifariki dunia Novemba 18, mwaka huu, muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.Kutokana na tukio hilo, Magembe aliwaagiza wafanyabiasha wa mahindi na udaga wanaoingiza bidhaa hizo, kupata vibali vya uthibitisho wa ubora wa bidhaa zao kabla ya kuuza ili kuepusha madhara ya kiafya.Magembe alitoa ufafanuzi huo, akijibu hoja za madiwani wakati wa kujadili mipango ya Kamati ya Mipango, Ujenzi, Mazingira na Uchumi ya robo ya kwanza ya mwaka 2019/2020.Madiwani hao walitaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali, kushughulikia upungufu wa chakula, unaosababisha wananchi kutumia chakula kibovu.Ofisa Kilimo halmashauri ya wilaya hiyo, Issa Mugendi alisema kuna upungufu wa tani 43.5 za chakula sawa na asilimia 31.6 ya mahitaji.Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi alisema tayari tatizo hilo amelifikisha Wizara ya Kilimo. Mkoani Arusha, dereva teksi, Lembris Mollel (23) amekutwa ameuawa ndani ya gari lake akiwa amefungwa mikono kwa waya.Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Koka Moita, ilieleza dereva huyo ni mkazi wa Tengeru wilayani Arumeru.Alisema mwili huo ulikutwa ndani ya gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba T183 BAZ katika Mtaa wa Elikiroa, Kata ya Lemara jijini Arusha.Alisema ulikutwa nyuma ya viti vya gari hilo, ukiwa na majeraha kadhaa na mikono imefungwa kwa nyuma na waya na gari likiwa limetumbukia mtoni. Polisi wanaendelea na uchunguzi.Katika tukio jingine, mtoto Gift Michael(3) mkazi wa Kijiji cha Ilkuishini wilayani Arumeru, amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye shimo la kuhifadhia maji ya ujenzi, alipokuwa akicheza karibu na shimo hilo, lililokuwa limejaa maji ya mvua na kuzingirwa na majani.Mwili upo Hospitali ya Selian kwa uchunguzi zaidi.Katika Kata ya Ugala wilayani Urambo mkoani Tabora, Maduka Matulanya (59) amefariki dunia Desemba Mosi, mwaka huu baada ya kuteleza kutoka juu ya paa, alipopanda kurekebisha sola iliyokuwa inataka kuanguka, kutokana na upepo na mvua zinazoendelea kunyesha.Watoto wa marehemu, Gamba Maduka na Mbuke Maduka, kwa nyakati tofauti walisema baba yao alianguka kutoka juu ya bati na kupoteza maisha.Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Barnabas Mwakalukwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo. Alitaka wazee wenye umri mkubwa, kutumia vijana kufanya kazi kama aliyokuwa akitaka kuifanya marehemu.Wilayani Bunda mkoani Mara, watu wanne wamekufa akiwamo mwanamume ambaye ameua mkewe kwa kumkata mapanga na kisha kujinyonga. Mwanamume mwingine amefia gesti na mwendesha bodaboda ameuawa na kuporwa pikipiki.Katika tukio la kwanza, Novemba 30 usiku katika Kijiji cha Mhurura Kata ya Igundu wilayani Bunda, Mchaina Mkama (33) alimuua mkewe Jeska Adam (23) kwa kumkata na mapanga na kisha kujinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti wa mwembe, kisa kikiwa ni wivu wa mapenzi wa muda mrefu.Tukio hilo limetokea siku moja baada ya Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kufungua Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Bunda na kuwataka wanaume wasiwapige wake zao, kwa sababu huo pia ni ukatili wa kijinsia.Aidha, Chacha Werema (38) mkazi wa Bunda Mjini aliyekuwa mtunza stoo wa vifaa vya ujenzi vya nyumba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amekufa mwishoni mwa Novemba akiwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Serengeti eneo la Nyasura, alikokuwa amepanga. Anadaiwa alikuwa na shinikizo la damu.Naye mwendesha pikipiki, Tito Nyamatimo maarufu kwa jina la Bakonzie au Mlokole, ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutelekezwa eneo la Balili, hatua chache kutoka barabara kuu ya Mwanza-Musoma. Ilielezwa kuwa kijana huyo alikodishwa na watu na baada ya kufika katika eneo hilo, walimteka na kumuua na kisha wakachukua pikipiki, simu ya mkononi na fedha zote alizokuwa nazo.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Daniel Shilla, alithibitisha matukio haya.Imeandikwa na Joachim Nyambo (Mbeya), Jovither Kaijage (Ukerewe), John Mhala (Arusha), Lucas Raphael (Tabora) na Ahmed Makongo (Bunda).
kitaifa
NAIROBI, KENYA WATU 42 wamekufa baada ya magari 13 yakiwamo lori lililosheheni mafuta pamoja na gari lililokuwa na mitungi ya gesi kugongana katika barabara kuu inayounganisha Kenya na Uganda usiku wa kuamkia jana. Kwa mujibu wa Naibu Kamanda Mkuu wa Jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo ilitokea kaskazini mwa mji wa Naivasha katika eneo la Karai linalojulikana kwa shughuli nyingi. Afisa mmoja mjini Naivasha amesema watu 50 wameungua vibaya na wanatibiwa hospitali,wanane kati yao wako mahatuti. Akihutubia wanahabari jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph Nkaissery amesema miongoni mwa waliokufa ni polisi 11 wa kikosi cha Recce kinachomlinda rais na watu wengine mashuhuri. Nkaisssery alisema kuwa si gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya gesi inayoshika moto kwa haraka. Mitungi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda,. Mmoja wa mashuhuda alisema baada ya mgongano, magari kadhaa yalishika moto na kuanza kuteketea huku watu wengi waliofika eneo la ajali hiyo kushuhudia kilichotokea nao wakijikuta wakikumbwa na moto huo kutokana na mlipuko na kuanza kuteketea. Polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo. Kuna ripoti kuwa gari aina ya Canter iligonga tuta la barabarani na kisha kuyagonga magari yaliyokuwa yakitokea mbele kabla ya kulipuka. Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni basi moja la matatu lililokuwa na abiria 14, ambao wote wanahofiwa kufa. Ajali hiyo mbaya imetokea nchini Kenya, wakati ambao madaktari na wauguzi walikuwa wakiendelea na mgomo ambao umeripotiwa kumalizika jana.
kimataifa
WANAWAKE wanaongoza kwa kuwa na tatizo la unene unaozidi na kiribatumbo ukilinganisha na wanaume.Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya amesema,  wanawake wenye uzito uliozidi ni asilimia 37 na wanaume ni asilimia 15 na kiribatumbo wanawake ni asilimia 15 na wanaume ni asilimia 2.5.Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati anatoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya uzito unaozidi na kiribatumbo.Dk. Ulisubisya amesema, ukilinganisha tatizo kwa wanaume na wanawake, utafiti unaonesha kwamba wanawake wameathirika zaidi.Amesema takwimu za utafiti wa Step uliofanyika nchini mwaka 2012, unaonesha kuwa tatizo la uzito uliozidi kwa watu wazima ni asilimia 26 na kiribatumbo ni asilimia 8.7.Dk Ulisubisya amesema, kumekuwa na ongezeko la tatizo la unene uliozidi na kiribatumbo na ongezeko hilo limesababisha kasi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Inakadiriwa kuwa ukubwa wa tatizo hilo unaweza kupita ule wa magonjwa ya kuambukiza.Amesema magonjwa makuu yasiyo ya kuambukiza yanajumuisha kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na yale ya mfumo wa hewa. Nchi zenye kipato cha chini na kile cha kati, Tanzania ikiwemo, ndizo zinazoathirika zaidi."Na kwa bahati mbaya, bado tunakabiliwa na magonjwa ya kuambukiza kama vile kuhara, nimonia, malaria, kifua kikuu na Ukimwi,"amesema.Amesema kwa sasa, matatizo haya kwa kiasi kikubwa yapo maeneo ya mijini kwani inajionesha wazi kuwa watu wengi wanaohamia mijini hubadili mtindo wao wa ulaji ulio bora unaochangia kutunza afya zao.Amesema ulaji huo huwafanya watu wa mjini waachane na ulaji wa vyakula vya asili vilivyopikwa kwa njia za kiasili kwa mfano mihogo, viazi na magimbi ya kuchemsha, ulaji wa mboga za majani na matunda ya asili, kunywa vinywaji visivyo na sukari nyingi, matumizi madogo ya chumvi na mafuta, kufanya kazi za kutumia nguvu na kutembea kwa muda mrefu."Aidha, maeneo ya mijini watu hutumia usafiri zaidi kuliko kutembea, lifti kwenye maghorofa badala ya kupanda ngazi na hupendelea kukaa pasipo kufanya zoezi lolote la mwili," amesema.Amesema Tanzania huungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Uzito Uliozidi na Kiribatumbo Novemba 26, kila mwaka kama mkakati wa kuchochea na kusaidia ufumbuzi wa tatizo hilo kwa wananchi, ili kuwasaidia wawe na uzito unaokubalika kiafya.Dk Ulisubisya amesema wizara hiyo imeazimia kuadhimisha siku hiyo ili kuongeza ufahamu kwa jamii, jinsi ya kupambana na uzito uliozidi na kiribatumbo ambacho ni mojawapo ya kiashiria hatarishi kinavyochangia kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.Amesema uzito uliozidi na kiribatumbo unaweza kuepukika kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha unaojumuisha ulaji unaofaa, kuepuka matumizi ya vileo vya kupindukia, kujishughulisha na kazi za mikono na kufanya mazoezi ya kutosha angalau muda wa dakika 20 mpaka 30 kwa siku, mara tatu hadi tano kwa wiki.Alisema wizara pia ilianzisha kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan yenye kaulimbiu Afya Yako Mtaji Wako, kila mmoja katika eneo lake ashiriki katika kufanya mazoezi ili kukabiliana na tatizo la uzito uliozidi na kiribatumbo.
kitaifa
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameuomba Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kulipa kipaumbele Jukwaa la Wabunge wa SADC kuwa Bunge kamili.Ndugai amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na Serikali za SADC ikiwamo ya Tanzania, kutetea jukwaa hilo kuwa Bunge kamili na kuomba msukumo zaidi uwekwe katika mkutano huo rasmi, utakaofanyika Agosti 17 na 18 jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unawahusu wakuu wa nchi na serikali wa nchi 16 wanachama wa SADC. Unatanguliwa na Maonesho ya Wiki ya Viwanda, yaliofunguliwa juzi na Rais John Magufuli, yanayoendelea hadi Agosti 8 na kisha vikao vya wataalamu na mawaziri wa jumuiya hiyo.Akizungumza katika tafrija ya chakula cha jioni, iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kwa kushirikiana na kamati ya SADC na wadau wengine, Ndugai pamoja na mambo mengine, aliuomba mkutano huo wa wakuu wa nchi na serikali kuliangalia suala hilo ili kuongeza utekelezaji wa itifaki hasa katika eneo la sheria katika SADC.“Bunge la Tanzania limekuwa mstari wa mbele kuimarisha mtangamano wa jumuiya hii kupitia Jukwaa la Wabunge wa SADC. Masuala ya utekelezaji wa itifaki za biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), madini na kilimo ni maeneo muhimu yanayojadiliwa katika jukwaa hili,” alisema Ndugai.Alisema Bunge la Tanzania linatambua mchango mkubwa wa Tanzania kuwa mstari wa mbele kutetea uwepo wa jukwaa hilo ili siku moja liwe Bunge kamili.Aliomba nchi nyingine kutetea kuanzishwa kwa Bunge la SADC. Juni mwaka huu, Rais John Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa SADC, Veronica Dihova, Ikulu, jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Ndugai. Dihova ni Spika wa Bunge la Msumbiji.Wengine waliohudhuria ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la Wabunge wa SADC, Boemo Sekgoma.Katika mazungumzo hayo, Dihova alieleza kuwa jukwaa hilo litashiriki kikamilifu katika Mkutano huo wa Agosti 17 na 18. Jukwaa la Wabunge wa SADC linawahusu maspika wote wa nchi wanachama wa SADC.Aidha, Ndugai alimshukuru Rais Magufuli kufungua maonesho ya Wiki ya Viwanda, kwani yanaimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi na kuwataka Watanzania kutumia fursa ya soko la SADC lenye watu karibu milioni 350.“Bunge linatambua juhudi za serikali katika kuweka mazingira rafiki ya biashara, kuanzishwa kwa Blue Print kuondoa vikwazo na urasimu usio wa lazima na tozo zinazobugudhi wafanyabiashara. Tunajua Bunge lijalo serikali italeta maboresho makubwa kudhibiti mtawanyo wa biashara kuondoa muingiliano wa majukumu,” alisema.Akizungumza katika tafrija hiyo ya chakula, iliyoandaliwa kuwakaribisha wageni kutoka nje ya nchi na washiriki wa mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa aliwashukuru waandaaji na kuhimiza washiriki katika Wiki ya Viwanda kuitumia fursa hiyo kutengeneza mtandao wa mawasiliano na kujiongezea ujuzi.Bashungwa pia alitumia fursa hiyo, kuwakaribisha wageni wote kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kuwataka wajisikie nyumbani kwani Watanzania ni wakarimu kwa asili.Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia Mkurugenzi wa Masoko, Ernest Mwamwaja, ilionesha video fupi kwa waliohudhuria hafla hiyo, iliyohusu maeneo ya utalii yaliopo nchini na kuwaomba wageni kuhakikisha wanayatembelea, kwani hakuna kama hayo duniani ikiwemo Mlima Mrefu Afrika, Kilimanjaro.
kitaifa
ZAIDI ya ekari 200,000 za ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo zimetengwa kwa wafugaji mbalimbali kupitia mpango wa matumizi ya ardhi, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya taasisi za serikali na asasi za kijamii katika vijiji vya Alolle na Olengapa vilivyopo Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.Taasisi zinazotarajia kutekeleza mradi huo ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Mifugo, na asasi ya kijamii ya KINNAPA na kuvihusisha vijiji vya Amei, Loolera, Lembapuli na Lesoit ambavyo kwa pamoja vinaunda jina la Alolle ikiwa ni muunganiko wa vijiji hivyo.Mafanikio hayo yameanza kupatikana hivi karibuni kupitia mradi wa uendelezaji endelevu wa sera na sheria ya ardhi ya Tanzania uliovisaidia vijiji husika kutumia kwa pamoja rasilimali hiyo ya ardhi na zingine zilizopo kwenye mipaka ya vijiji hivyo.Awali mradi huo ulisaidia kutenga ekari 75,000 za ardhi ya malisho katika eneo linalojulikana kama Olengapa, linalotumiwa kwa pamoja na vijiji vinne vya Orkitikiti, Lerug, Ngapapa na Engang’uengare vilivyopo katika eneo hilo la malisho katika wilaya hiyo Kiteto.
kitaifa
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla, amesema ili kukuza utalii wameanza mazungumzo na klabu ya KRC Genk anayochezea Mbwana Samatta ili kutangaza utalii nchini Ubelgiji.Akizungumza jana Dk Kigwangalla alisema wapo kwenye kuandaa mkakati mahsusi, kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hiyo. “Tayari pia tumeanza mazungumzo na mchezaji wa soka la kulipwa, Mbwana Samatta, ili tutumie jina lake kufungua soko jipya la utalii nchini Ubeligiji,” alisema Dk Kigwangalla. Mbali na Samatta, Dk Kigwangalla amemuomba mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata kukubali uteuzi wake wa kuwa Balozi wa hiari wa utalii nchini.“Tunakushukuru na kukupongeza Flaviana Matata kwa uzalendo wako hivyo tunakuomba ukubali uteuzi wangu wa kuwa balozi wa hiari wa utalii. Tutakupa hati ya shukrani pia tunakupa safari ya siku tano ya kutembelea vivutio vyetu siku yoyote utakayokuwa tayari,’ alisema Dk Kigwangalla. Alisema tayari amekamilisha kazi ya kubuni kauli mbiu ya `Tanzania Unforgettable’ ambayo itaitambulisha nchi kwenye masoko ya utalii.
michezo
KATIKA kuhakikisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinafunguka zaidi kimiundombinu, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imeridhia kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara kuanzia mwaka kesho.Kwa uamuzi huo, barabara ya Rumonge- Gotaz nchini Burundi na ya Kabingo-Kasulu-Manyovu nchini Tanzania, zinatarajiwa kuunganishwa kwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, barabara ya kutoka Malindi-Mombasa-Lunga Lunga nchini Kenya hadi Horohoro-Tanga-Bagamoyo nchini Tanzania, maeneo yaliyopo Pwani ya Bahari ya Hindi, nazo zinatarajiwa kupata sura mpya.Hii ina maana kwamba fedha za AfDB zitagusa miradi mikubwa ya barabara katika nchi tatu kati ya sita za EAC, nyingine zikiwa Uganda, Rwanda na Sudan Kusini. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya EAC, Mkurugenzi Mkuu wa AfDB katika Ukanda wa Mashariki mwa Afrika, Gabriel Negatu alisema benki hiyo imeidhinisha Dola za Marekani milioni 322 kwa ajili ya barabara ya Rumonge-Gitaz na Kabingo- Kasulu-Manyovu.Fedha hizo zitahusisha pia ujenzi wa Kituo cha Huduma Kwa Pamoja Mpakani katika mpaka wa Manyovu- Mugina unaozihusisha Tanzania na Burundi. Vituo vya aina hiyo vimetengwa katika maeneo mbalimbali ya mipaka ya Tanzania na nchi jirani, cha mwisho kikizinduliwa mwishoni mwa wiki katika mpaka wa Namanga, unaozitenganisha Tanzania na Kenya.Vituo vingine vya aina hiyo ni Rusumo katika mpaka wa Tanzania na Rwanda, Mtukula mpaka wa Tanzania na Uganda, Tunduma katika mpaka wa Tanzania na Zambia na Holili mpaka wa Tanzania na Kenya upande wa mkoa wa Kilimanjaro.Alisema AfDB imelazimika kutoa fedha kutokana na kuridhishwa na faida za miradi ya barabara. Alitoa mfano wa Athi River (Kenya)-Namanga-Arusha iliyosaidia kupunguza urefu wa safari kutoka siku nzima hadi saa nne tu kati ya miji ya Nairobi na Arusha.Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Huduma Kwa Pamoja Mpakani Namanga, ulioshirikisha Rais John Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.“Njia hii ya kusuka miundombinu ina faida nyingi, moja ikiwa ni kurahisisha shughuli za kibiashara, hivyo kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla. Kwa kutambua hilo, ndiyo maana AfDB ikatoa Dola za Marekani milioni nane kwa ajili ya kituo cha huduma kwa pamoja upande wa Kenya,” alisema. Aliongeza kuwa upande wa Tanzania, kituo kimejengwa kwa fedha za watanzania na Shirika la Misaada la Maendeleo la Japan (JICA).Alisema kituo hicho ni sehemu ya barabara kuu ya Arusha-Namanga-Athi River iliyojengwa kwa Dola za Marekani milioni 147, kati ya hizo Dola milioni 79 zikitoka AfDB. Kiasi kingine kilitoka Serikali za Tanzania na Kenya na pia Benki ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JBIC).AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na kujikita katika miradi mingi, miongoni ukiwa wa maji mkoani, Arusha uliowekewa jiwe la msingi juzi na Rais Magufuli. Mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 520, unahusisha fedha za serikali ya Tanzania.
kitaifa
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani, Donald Trump ambaye anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu mkutano wake wa kilele na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mjini Helsinki wiki hii, amesema anakusudia kumwalika kiongozi huyo katika mkutano mwingine tena baadaye mwaka huu na tayari mazungumzo yanaendelea. Licha ya Rais Donald Trump kukumbwa na ukosoaji mkubwa baada ya mkutano wa kilele kati yake na Rais Vladimir Putin, wiki hii kuhusu kile kilichotazamwa kuwa kuukubali msimamo wa Putin kwamba Urusi haikuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016, msimamo ambao ni kinyume na msimamo wa mashirika ya ujasusi ya Marekani, msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Sanders, amesema kwenye ukurasa wa Twitter kuwa, mkutano kati ya Trump na Putin huenda ukafanyika baadaye mwaka huu mjini Washington. Sanders amesema Rais Trump amemwambia mshauri wake wa usalama wa taifa, John Bolton, kumwalika Rais Putin, mjini Washington na tayari mazungumzo kuhusu mwaliko huo yameshaanza. Mwaliko huo umemshangaza kwa mkurugenzi wa ujasusi wa Marekani, Dan Coats, wakati akihojiwa moja kwa moja katika kongamano la usalama la Aspen Jimbo la Colorado. Akizungumzia mkutano uliopita kati ya Trump na Putin, Coats alisema: “Sijui kilichojiri katika mkutano huo. Ninafikiri kadiri muda unavyosonga na tayari rais amedokeza baadhi ya yale yaliyojiri. Ninafikiri tutafahamu mengi. Lakini hilo ni jukumu la rais. Lau angaliniuliza namna lilivyopaswa au kulishughulikia, ningelipendekeza njia tofauti. Lakini hilo si jukumu langu, wala kazi yangu na ndivyo hali ilivyo.”
kimataifa
NA VERONICA ROMWALD – NAIROBI Waandishi wa habari wameshauriwa kutumia vema kalamu zao kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya uzazi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika nchi zao za kupambana na matatizo ya uzazi. Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Nairobi na Waziri wa Afya wa Uganda, Sarah Opendi alipozungumza katika hafla ya kuwatunuku tuzo ya uandishi wa habari za afya ya uzazi zilizotolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na masuala ya kijamii, kiuchumi na maendeleo, Merck More Than A Mother. Pamoja na hilo, Opendi alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani asilimia 25 ya wana ndoa duniani wanakabiliwa na matatizo ya uzazi yanayopelekea kukosa watoto maishani (utasa). “WHO linaeleza asilimia kubwa ya wanaokabiliwa na matatizo ya uzazi ni waishio katika nchi zinazoendelea, Uganda ikiwamo, ni changamoto kubwa lakini tunaendelea kufanya juhudi kukabiliana nayo,” alisema. Aliwataka pia kutumia vema mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe sahihi kuhusu masuala ya uzazi na kutoa taarifa zitakazowajenga na si kuwabomoa. Naye, Naibu Waziri wa Afya, Kenya, Dk. Rashid Aman alisisitiza kuwa kuwa ikiwa jamii itapewa elimu sahihi itasaidia kukabili changamoto hiyo kwani asilimia 80 ya matatizo yanaweza kuzuilika. “Ndoa nyingi zinavunjika kwa kukosa watoto, watu wanakumbana na unyanyasaji huko kwenye jamii, tunapaswa kupaza sauti kuzisaidia jamii zetu,” alisema. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dk. Rasha Kelej aliongeza kuwa matatizo hayo huwakumba watu wa jinsi zote hata hivyo katika jamii nyingi wanawake pekee ndiyo hunyooshewa kidole. “Kuna visababishi vingi vinavyoweza kuchangia hali hiyo kutokea, ikiwamo magonjwa ya ngono, utoaji mimba ovyo, sababu kama hizi zinaweza kuepukwa kwa kuelimisha jamii,” alisisitiza. Akizungumza na MTANZANIA, Mashaka Mgeta ambaye ni mwandishi pekee kutoka Tanzania (Gazeti la Jambo Leo) aliye miongoni mwa washindi katika tuzo hizo, alisema waandishi wa habari wanapaswa kuwekeza zaidi katika masuala yanayohusu afya ya uzazi. Alisema hatua hiyo itaiwezesha jamii kupata taarifa sahihi zitakazosaidia jamii kukabiliana na changamoto za afya ya uzazi na ambazo zimekuwa chanzo cha matatizo kadhaa ya kiafya na kijamii. “Ingawa vyombo vya habari vinashiriki katika kuandika na kutangaza masuala ya afya ya uzazi, lakini ipo haja ya kuongeza ubunifu na weledi vitakavyoyafanya masuala hayo kuwa moja ya ajenda za kuchochea mabadiliko katika sekta hizo nchini,” alisema Mgeta. Mgeta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Afya (THJ), alisema katika kuchangia ukuzaji uelewa, chama hicho kinaandaa mpango wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna bora zaidi ya kuandika na kutangaza habari za afya ya uzazi. Pamoja na Mashaka waandishi wengine waliotunukiwa tuzo hizo ni kutoka nchini Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Mozambique, Cameroon na Botswana Hafla hiyo ilihudhuriwa na waandishi wapatao 200 kutoka nchi 17 zilizopo barani Afrika na mwandishi wa Habari za Afya wa Gazeti la MTANZANIA, Veronica Romwald alitunukiwa cheti cha heshima kwa kuwasilisha kazi yake kushindanishwa katika shindano hilo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Merck, Dk. Kejel, mashindano hayo kwa mwaka 2018 yamezinduliwa na kwamba wakati wowote kuanzia sasa watatangaza ‘link’ ambayo waandishi wataitumia kuwasilisha kazi zao.
afya
RAIS John Magufuli amesema nchi za Afrika, zimetambua mustakabali wake uko mikononi mwao ; na uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana, kama zitaendelea kuwa tegemezi kiuchumi, kwa kuombaomba misaada nje.Ameonya kuwa ushirikiano wa namna hiyo, hauhitajiki tena katika mazingira ya sasa. Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Nordic (Norway, Sweden, Denmark, Iceland na Finland), unaowakutanisha mawaziri 34 na washiriki wengine 250.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wa dini, siasa na mabalozi.Rais Magufuli alisema Afrika haiwezi kuendelea na kuwa na uhuru wa kujiamualia mambo yake, iwapo mataifa yataendelea kuwa ombaomba, bali inapaswa kuamka na kutambua uchumi wake uko mikononi mwake.“ Kwa muda mrefu Afrika ilitafuta ukombozi wa kiuchumi kwa kujikita zaidi kupokea na kutoa misaada. Ushirikiano wa namna hii, sio endelevu na wala hauhitajiki katika mazingira ya sasa. Viongozi wengi wa Afrika tumetambua mustakabali wa bara letu uko mikononi mwetu na uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana sana, endapo mataifa yetu yataendelea kuwa tegemezi kiuchumi,”alisema Rais Magufuli.Alisema jukumu la viongozi wa sasa, kama walivyoachiwa na waasisi wa ukombozi ni kubadili mwelekeo na kuingia katika uhusiano wa kisasa, ambao mataifa yanajikita katika ushirikiano wa kiuchumi kupitia biashara, uwekezaji na diplomasia ya uchumi, ambayo ndio msingi wa uhusiano wa mataifa hayo kwa sasa.“Kwa bahati nzuri fursa, uwezo na mazingira ya kuingia kwenye ushirikiano huo wa diplomasia ya uchumi tunayo. Tutumie fursa hiyo kujenga nchi zetu na uchumi wa watu wetu,”alisema Rais Magufuli.Akitoa mfano, alisema nchi za Nordic ziko tano, lakini pamoja na kuwa na eneo dogo la ukubwa wa kilomita HABARI Kikwete ashauri SADC kupiga vita malaria Alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari, baada ya kuzungumza na mawaziri wa nchi za SADC wa sekta ya afya na Ukimwi katika mkutano wao, uliofanyika juzi Dar es Salaam.Kikwete ambaye ni mmoja wa wajumbe wa jopo la watu maarufu duniani la kupambana na malaria kupitia taasisi ya End Malaria Council, chini ya uenyekiti wa bilionea Bill Gates, alisema nchi za SADC zinapaswa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya malaria, kwa kuzingatia uongozi shupavu, fedha za mapambano na matumizi ya teknolojia sahihi.Alisema kuondoa malaria Afrika inawezekana, ikiwa nguvu ya pamoja itawekwa. Alitoa mfano mara ya mwisho mtu kuugua malaria Marekani ilikuwa mwaka 1956, hivyo malaria kuisha Afrika inawezekana. Alisema inasikitisha namna Afrika ilivyobeba mzigo mzito wa vifo, vinavyotokana na malaria, hivyo juhudi za kiuchumi zinazofanywa na nchi za SADC, hazitazaa matunda bila kuifuta malaria katika Afrika.“Nimetumwa na jopo letu la kupambana na malaria kwa mawaziri hawa wa SADC, kuzungumza nao kuhusu kuongeza kasi ya kuuondoa ugonjwa huu Afrika…tunafahamu jitihada kubwa imefanyika, mafanikio yameonekana, nguvu zaidi inahitajika...mwaka 2010 hadi 2015 kulikuwa na kasi kubwa sasa imepungua, ila tunasema tusiiache. Tuweke nguvu katika mambo matatu: dawa mseto; vyandarua vyenye dawa; na dawa ukoko,” alisema Rais Kikwete.Alisema katika maisha yake ni mtu wa matumaini, hivyo anaamini siku moja malaria Afrika itaisha. Alizitaka nchi za SADC kununua dawa za kuua viluilui vya mbu katika Kiwanda cha Viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Kibaha mkoani Pwani katika kufanikisha juhudi hizo.Mawaziri SADC wazuia matumizi ya maziwa ya kopo kwa ‘vichanga’ Mawaziri hao walipitisha kanuni za pamoja za katazo la kuhamasisha matumizi ya maziwa ya kopo kwa vichanga na kuondoa viribatumbo; na kuanzisha kikosi kazi cha uratibu wa pamoja maafa na kupambana na kushughulikia ebola.Ummy ambaye ni Mwenyekiti wa mawaziri wa sekta hiyo ya afya na Ukimwi wa nchi za SADC, alisema kwa kauli moja katika eneo la lishe ili kupunguza udumavu, wameweka kanuni za pamoja za katazo la uhamasishaji wa matumizi ya maziwa ya kopo na vyakula mbadala kwa vichanga, kumlinda mama anayenyonyesha.Akifafanua, Waziri Ummy alisema lishe bado ni tatizo kubwa kwa nchi za SADC na wamekubaliana pia matumizi ya kadi za alama za lishe kwa nchi hizo na kutumia mfumo wa kikanda kuboresha lishe kwa watoto na mkakati wa kikanda wa kudhibiti uzito uliozidi na kiribatumbo katika jamii.“Tumeazimia kuwe na uongezwaji wa virutubisho vya vitamini na madini wakati wa usindikaji kwenye unga wa mahindi, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kula na chumvi,” alisema.Aidha, Waziri Mwalimu alisema katika kukabiliana na changamoto ya lishe kwa nchi wanachama, wanatarajia kuweka kanuni za pamoja za katazo hilo la kuhamasisha maziwa ya kopo na vyakula mbadala kwa watoto wachanga na wadogo na kumlinda mama anayenyonyesha (likizo ya uzazi).“Tumeweka kanuni za pamoja za katazo la uhamasishaji wa matumizi ya maziwa ya kopo na vyakula mbadala kwa vichanga na watoto wadogo na kumlinda mama anayenyonyesha yaani likizo ya uzazi,” alisema.Aliongeza kuwa watoto wengi wanashindwa kunyonya kwa kipindi wanachohitaji, kiasi kwamba wanaanzishiwa maziwa mbadala mapema, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za afya.Ummy alisema wameazimia kutumia mfumo wa kikanda, kuboresha lishe kwa watoto na mkakati wa kikanda wa kudhibiti uzito uliozidi na kiribatumbo katika jamii. Alisema azimio hilo linataka uongwezwaji wa virutubishi vya vitamini na madini wakati wa usindikaji kwenye unga wa mahindi, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kula na chumvi. JPM: Afrika tujitegemee za mraba milioni 3.5 na idadi ya watu takribani milioni 27, bado zina uchumi mkubwa, ukilinganisha na nchi za bara lote la Afrika lenye watu zaidi ya bilioni moja.Rais Magufuli alisema pato la mwaka jana kwa nchi za Nordic, lilikuwa dola trilioni 1.7 huku pato la nchi zote za bara la Afrika kwa mwaka huo likiwa ni dola trilioni 2.334 wakati bara hilo lina ukubwa wa kilomita za mraba milioni 30.37.‘Kusema kweli Afrika tuna jambo la kujifunza kutoka Nordic, hatuwezi kuwa na uchumi mdogo wakati nchi tano tu, tena zenye eneo dogo, zikitupita kwa kiwango kikubwa kama hicho. Tutumie fursa ya rasilimali zetu kuweka mazingira ya uwekezaji ili wavutiwe kuja kuwekeza na tujenge viwanda vitakavyoleta mafanikio kwa pande zote,”alisema Rais Magufuli.Akitoa mfano Afrika ilivyobarikiwa rasilimali nyingi, Rais Magufuli alisema Afrika ina eneo kubwa la kilimo, ambapo asilimia 30 ya ardhi ya kilimo duniani iko Afrika. Lakini, alisema pia Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali za bahari ukanda wa Pwani, mifugo, madini, gesi na vitu vingine, hivyo lazima nchi hizo ziamke.Alisema nchi nyingi Afrika, sasa zimetambua maendeleo yao yataletwa na wenyewe, ndio maana mageuzi ya karibuni yamefanywa kwenye ulinzi na usalama, licha ya migogoro kwenye baadhi ya nchi kuendelea. Rais Magufuli alisema bara la Afrika, sasa limetambua nafasi yake katika kukuza uchumi wake, badala ya kuendelea kutegemea nchi wahisani.Alisema hivi sasa duniani, bara la Afrika linashika nafasi ya pili kwa kasi kubwa ya ukuaji uchumi, ambayo ni asilimia 4.1 kwa mwaka jana. Alisema kwamba katika takwimu za ukuaji wa uchumi, nchi 10 ambazo uchumi wake unakua kwa kasi duniani, hivi sasa tano ni nchi za Afrika. Rais Magufuli alisema Tanzania ina vivutio vingi na imeshika nafasi ya pili duniani kwa vivutio vya utalii, lakini bado kuna tatizo la ukosefu wa viwanda. Alisema nchi haiwezi kuendelea ikiwa muuzaji wa mazao ghafi.Alitoa mwito wa Afrika, kuwekeza na kujenga viwanda, kuzalisha bidhaa zilizoongezwa thamani. “Nordic wamepiga hatua kwenye viwanda, tushirikiane nao kwenye viwanda tupige hatua na tuzalishe bidhaa zilizoongezwa thamani. Washirika wetu hawa watuunge mkono ili tuinue uchumi wetu na kuwa na manufaa kwa pande zote, tuweke mazingira rafiki na kuondoa urasimu kuvutia uwekezaji,” alisema.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alizishukuru nchi za Nordic na Afrika, kukubali Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kusema utafanyika kwa amani na kuleta tija kwa pande zote. Alisema uhusiano wa mataifa ya Afrika na nchi za Nordic, una historia kubwa na baadhi ni misaada yao wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika, ambapo nchi hizo zilisaidia hata kujenga chuo cha wapigania uhuru wa nchi za Kusini Somafco mkoani Morogoro.“Nyakati hizo ikumbukwe ilikuwa sio rahisi nchi za Ulaya kuja kutuunga mkono, lakini Nordic walikuja na huo ndio upekee wao. Tunawashukuru sana na baadaye Nordic wameendelea kuwa washirika wetu wakubwa kwenye sekta mbalimbali kama afya, elimu na masuala ya amani. Tunaomba mfikishe salamu zetu kwa wakuu wa mataifa ya Nordic,”alisema Rais Magufuli katika hotuba yake hiyo kwa washiriki.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alisema mkutano huo, unatoa fursa ya wadau kutathmini wanavyoshirikiana na maeneo ya kuongeza ushirikiano. Alisema mawaziri hao walikutana juzi usiku katika kikao na walikubaliana kujadili ajenda mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi. Waliafikiana mabadiliko hayo na maendeleo endelevu ni kitu kimoja, hivyo nguvu ya pamoja inahitajika kuangalia changamoto na kuleta suluhu bila kuacha mojawapo.
kitaifa
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
uchumi
KINSHASA, DRC MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi ambaye pia ni baba wa Rais  Felix, ulitarajiwa kuwasili jana baada ya miaka miwili tangu afariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa ya familia, mwili huo utawasili kutoka   Ubelgiji kwa ajili  ya  mazishi. Kiongozi huyo alifariki dunia mjini Brussels Februari 2017,  akiwa na umri wa miaka 84,  lakini mwili wake ulibaki  katika mji huo mkuu wa Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa siasa kwa utawala wa Rais wa zamani wa taifa hili, Joseph Kabila. Kulingana na taarifa ya nduguye Askofu Gerard Mulumba, mazishi yake yatafanyika katika Viwanja vya Mashahidi. Askofu Mulumba alisema   baada ya kuukaribisha mwili katika uwanja wa ndege  utasafirishwa hadi katika uwanja huo kwa maombolezo. Alisema   tayari maandalizi katika uwanja huo ikiwemo ujenzi wa jukwaa umekamilika mbali na yale ya maofisa wa polisi ambao wataongoza gwaride   kumpatia heshima za mwisho baba huyo wa upinzani DRC. Alisema  takribani marais watano wa bara la Afrika wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake.  ”Ni zaidi ya miaka miwili tangu tulipoanza kutumia kila njia kuusafirisha mwili wake,”  alisema Askofu Mulumba. ”Na sasa kwa kuwa hali iko shwari tunashukuru,” aliongeza. Akiwa mwanasiasa wa muda mrefu, Tshisekedi alikuwa katika upinzani kwa miongo kadhaa lakini hakufanikiwa kuiongoza nchi hii. Akiwa mkosoaji mkubwa wa aliyekuwa dikteta Mobutu Sese Seko, alianzisha chama cha Union for Democracy and Special Progress (UDPS) mwaka 1982 baada ya kuachiliwa kutoka jela na mwaka 1997. Baada ya Mobutu kung’olewa madarakani na kundi lililoongozwa na Laurent Kabila, Tshisekedi alianza kuwa mpinzani wa utawala mpya , msimamo aliokuwa nao hata baada ya mauaji ya Kabila mwaka 2001 huku mwanawe, Joseph akipanda katika hatamu za uongozi. Baada ya kushindwa katika uchuguzi wa 2011 uliodaiwa kukumbwa na udanganyifu mkubwa , Tshisekedi alikataa kutambua utawala wa Kabila hadi kifo chake.
kimataifa
IKIWA ni siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kujitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Serikali imesisitiza kuwa uchaguzi huo uko palepale.Pia, imewaonya viongozi wa vyama vya siasa na wananchi, wanaohamasisha fujo au kususia shughuli za maendeleo kwa njia ya mitandao, kuwa watachukuliwa hatua kali. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitaanza wiki moja kabla ya kufanyika uchaguzi huo.Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara alitoa msimamo huo bungeni jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Kaskazini, Justine Monko (CCM). Katika swali lake, Monko alisema Chadema kutangaza kujitoa, kunawakosesha wananchi haki yao kimsingi, hivyo alitaka kujua kauli ya serikali kutokana na kadhia hiyo.Akijibu swali hilo, Waitara alisema taarifa ya Chadema kujiondoa kushiriki uchaguzi huo, wamezisikia kwenye mitandano na vyombo vya habari. Alisema hakuna tamko rasmi ambalo limefika ofisini kwake.“Ni kweli na sisi kama ofisi tumesikia Chadema kujitoa, tumeona kwenye mitandao, huenda wakatoa tamko rasmi, lakini kauli ya serikali ni kwamba uchaguzi unaendelea kama ilivyopangwa kwenye ratiba, uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 24 mwaka huu…wananchi ambao wamejiandikisha na vyama ambavyo vipo kwenye mchakato viendeleee na mchakato wao. Wametoa tamko jana (juzi) kwenye mitandao, lakini itakumbukwa kwamba kwenye taratibu zetu ni kwamba wale waliokuwa na malalamiko, wameandika mapingamizi yao na kesho (leo) ndio siku ya mwisho. Kama wamejiondoa hawana sababu yoyote ya kulalamika kwamba hawakutendewa haki,” alisema.Aliongeza kuwa, “watu wenye sifa ya kutoa mapingamizi ni wagombea, wenzetu walitaka watoe kauli bungeni, kwenye mitandao ya kijamii, serikali inafanya kazi kwa karatasi kwa mawasiliano, hatuna document mezani hatuwezi kujadili.”Aidha, Waitara alikemea maagizo yaliyotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na wananchi, ambao wanahamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo.“Mwenye mamlaka ya kutoa maelekezo nchi hii ni Rais, na siyo kiongozi wa chama cha siasa, kiongozi wa chama cha siasa anatoa maelekezo kwenye chama chake na wanachama wake tu” alisema.Waitara alitoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya, ambao ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama, kutafuta taarifa za watu wanaohamasisha fujo.“Naomba nitoe maelekezo kwa wakuu wa wilaya ambao ni wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama, tumepata taarifa kwenye mitandao wanahamasisha watu, wanaharibu mazao ya watu, wakuu wa wilaya popote mlipo kama kuna mtu anahisi hakutendewa haki kwenye uchaguzi huu na anafanya fujo mtaani, sheria stahiki zichukuliwe.“Hatujawahi kutunga sheria katika Bunge hili inayosema ukigombea ukanyimwa nafasi au ukahisi umenyimwa haki ufanye fujo, ila zipo taratibu za kisheria mzifuate, msipozifuata vyombo vya usalama vinashughulika na wewe, tusilaumiane mbele ya safari” alisema.Katika swali la msingi, Monko alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kuwepo uchaguzi mdogo, kama ilivyo kwa madiwani na wabunge. Akijibu swali hilo, Waitara alisema Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 (Kanuni ya 43 (1-4 na Kanuni ya 45), zinatoa fursa ya kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi iliyoachwa wazi, endapo Mwenyekiti wa Kitongoji / Kijiji/Mtaa atafariki au kupoteza sifa za kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kutokana na sababu zilizoainishwa kwenye Kanuni ya 44 (1 na 2). Alisema uchaguzi hautafanyika kama nafasi itakuwa imeachwa wazi, kabla ya miezi sita kabla ya uchaguzi.Miongozo Baada ya kipindi cha maswali na majibu, wabunge watatu walisimama kuomba mwongozo wa Spika kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa. Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) alitaka mwongozo wa kiti cha Spika, kuwa kanuni zinasemaje kwa chama kujitoa, hasa baada ya Chadema ambayo wabunge wake anawaamini na kuwaheshimu. Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) alitaka apewe ufafanuzi, endapo kama kuna chama kimejitoa, kanuni zinasemaje.“Wakati Waziri wa Tamisemi akijibu swali namba 40 kuhusu suala la uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikajitokeza kwamba kwa sababu serikali ilitoa siku tatu kwa ajili ya kukata rufaa, kwa bahati mbaya chama ambacho nakiamini na kukiheshimu pamoja na wabunge wake, kimeamua kujitoa katika uchaguzi huo navishukuru vyama vingine kwa kuamua kusubiri siku ya mwisho ya rufaa kesho (leo)…Nilikuwa naomba kwa mujibu wa Kanuni za Serikali za Mitaa endapo kuna chama kimejitoa hata kwa kutokushemimu kikaamua kujitoa Kanuni inasemaje?” alisema Ndassa.Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) alidai kwamba imekuwa kawaida kwa Chadema, kujitoa katika chaguzi mbalimbali, hivyo aliomba apatiwe ufafanuzi kuhusu chama hicho kujitoa.“Mwongozo wangu unaotokana na swali namba 40, jana (juzi) Mwenyekiti wa Chadema ambaye tunamheshimu sana alitangaza kujitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hoja sio hiyo, kitendo cha kujitoa kinaendana na vurugu ambazo zinaendelea, Mheshimiwa Mwakagenda (Sophia) amesema amemfukuza mpangaji kutokana na hilo hilo.“Jana (juzi) nimeona kwenye TV vijana wa Chadema Mbozi wameenda kufyeka shamba la msimamizi wa uchaguzi, vitendo hivyo vinaendelea nchi nzima. Mwenyekiti sisi wakongwe tuna historia ya chama hicho kugomea uchaguzi. Mwaka 2008 Chacha Wangwe alipotangaza kugombea uchaguzi Chadema nafasi ya mwenyejiti ilitokea tafrani.“Mwaka 2015 Zitto Kabwe alipotaka kugombea uenyekiti wa taifa Chadema ilitokea tafrani mpaka wakamfukuza kwenye chama. Mwaka 2018 walipotakiwa kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa taifa waligomea mpaka sasa hivi wana barua nne za Msajili vya vyama vya siasa kutaka kugomea uchaguzi, kwahiyo tuna historia ya chama hiki kugomea chaguzi, kwahiyo naomba mwongozo wako Mheshimiwa Mwenyekiti,”alisema Mlinga.Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonist (Chadema) alisema kwamba malalamiko yamezidi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku Serikali ikiwa imekaa kimya. Alitaka apewe majibu kuhusu sekeseke hilo. Kauli ya Lugola Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge alitoa nafasi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alitoe ufafanuzi wa suala hilo, ambaye alisema Jeshi la Polisi limejipanga wakati wote wa kampeni hadi uchaguzi na limeimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote nchini. Alisema polisi haitatoa mwanya kwa mtu yoyote, atakayejaribu kuvunja amani, ama kufanya vitendo vinavyoweza kuashiria kuvunjika kwa amani.“Jeshi la Polisi limejipanga wakati wote, kuanzia kampeni hadi siku ya uchaguzi, hakuna mtanzania yoyote atakayefanya fujo ya kuzuru watu. Natoa onyo kwamba hakutakuwa na nafasi kwa chama chochote kitakachopanga kuvuruga amani, serikali tumejipanga kupambana na hali hiyo,” alisema.Alisema atamuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro aanze kuchukua hatua kwa wahusika, waliofyeka shamba la msimamizi wa uchaguzi wilayani Mbozi, pamoja na mbunge aliyemtimua askari katika nyumba yake aliyopanga. Wakati wa kipindi cha maswali, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisimama na kusema: “Nimesimama kujibu swali la pili na nyongeza, nilikuwa na mpangaji ambaye ni askari nimemuondoa kwenye nyumba.”Kwa upande wa Waitara aliongeza: “Kuna vyama 22 vyenye usajili, kwa hiyo kujitoa hakuzii kitu na nawapongeza waliobaki, na viongozi watakaopatikana watapelekwa kwenye mafunzo Chuo cha Hombolo.”Mbunge wa Mtama, Nape Nnaye (CCM) alitaka kujua kama serikali haioni haja ya kuunganisha uchaguzi wa madiwani na vijiji, vitongoji na mitaa, ili uchaguzi wa wabunge na madiwani na rais uwe pamoja. Akijibu swali hilo, Waitara alisema jambo hilo ni la kisheria, hivyo wanapokea wazo hili ikiwezekana kufanya hivyo watafanya hivyo.Vyama 11 kushiriki uchaguzi mitaa Katika hatua nyingine, Umoja wa Vyama 11 vya siasa visivyo na wawakilishi Bungeni, vimetangaza kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa na kuvikebehi vyama vilivyotangaza kuususia. Uamuzi huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Umoja huo unaoundwa na vyama vya DP, NRA, AFP, UDP, ADC, Demokrasia Makini, Ada-Tadea, Sauti ya Umma (SAU), TLP, CCK na UMB. Vyama hivyo vimesema vitashiriki uchaguzi huo, kwa kuwa ni wajibu wao wa kidemokrasia kufanya hivyo.Vilisisitiza kuwa vyama vilivyosusia uchaguzi huo ‘vimeshiba’ “Vyama vilivyosusia vina mtaji wa wanachama, sisi katu hatuwezi kususia kwa sababu tunataka kutimiza matakwa ya demokrasia, waliosusia wana sababu zao za kufanya hivyo, kimsingi tunamuomba Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo aangalie mapungufu yaliyojitokeza kwa watendaji wake.“Tunamuomba Waziri Jafo awarudishe katika mchakato wagombea wote ambao hakutendewa haki katika uteuzi ili tukapambane katika kura, tunaamini kufanya hivyo kutazidi kuinua demokrasi yetu hapa nchini,” alisema Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdul Mluya.Katibu wa Umoja huo, Hassan Almasi ambaye ni Katibu Mkuu wa NRA, alisema kimsingi chaguzi huendeshwa kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu, hivyo vyama vimetoa mapangamizi yao kuhusu kuenguliwa kwa majina ya wagombea na vinasubiri majibu ya rufaa ya wagombea wao.“Vyama vimeundwa ili kushiriki uchaguzi, hatuwezi kususia kwa kuwa kushiriki chaguzi ndiyo hasa malengo ya kuanzishwa kwa vyama vya siasa, tunamuomba Waziri atoe maamuzi ya haraka ili tuweze kujua nini kifanyike,” alisema Almasi.ACT–Wazalendo nayo yajitoa Wakati huo huo, Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT-Wazalendo iliyoketi jana, imeelekeza wanachama wake wote waliobakizwa katika uchaguzi huo wajiondoe. Taarifa ya Kiongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo, Kabwe Zitto, ilieleza kuwa uenguaji wa wagombea kwa kutumia sababu zisizo na mantiki, umenyima wagombea haki yao kikatiba na pia umewanyima haki wananchi waliotimiza miaka 18 na zaidi.Alisema haki hiyo ipo katika Ibara ya 5 ya Katiba. “Kwa kuwa CCM imeondoa wagombea wetu asilimia 96 na sisi tumewasaidia kuondoa asilimia nne ya waliobakia,” ilidai sehemu ya taarifa hiyo ya Zitto. Alisema chama cha ACT Wazalendo, kikiwa chama cha siasa makini chenye usajili wa kudumu nchini, kiliitikia wito wa kushiriki katika uchaguzi huo wa Mitaa, utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu, kikiamini kuwa ni nafasi nyeti ya kuimarisha ushindani wa kisiasa nchini, lakini sasa kimeamua kujitoa.
kitaifa
Na Veronica Kazimoto-Simiyu WAFANYABISHARA nchini wameshauriwa kutunza kumbukumbu za biashara zao ili kulipa kodi stahiki na hatimaye kupunguza kero ya madai yao kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakadiria kodi kubwa isiyoendana na uhalisia wa biashara wanazofanya. Akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Diana Masalla, aLIsema kuwa, wafanyabiashara walio wengi hawana tabia ya kutunza kumbukumbu za biashara zao suala linalosababisha malalamiko mengi baada ya kukadiriwa kodi na TRA. “Ndugu zangu wafanyabiashara sote tunajua kwamba, mali bila daftari hupotea bila habari hivyo basi, niwaombe mjenge tabia ya kutunza kumbukumbu za biashara zenu siyo tu kwa ajili ya TRA lakini pia kwa ajili yenu wenyewe kwani mtaweza kujua kama biashara zenu zinakua au zinashuka lakini pia mtaweza kupanga bajeti za mauzo na manunuzi yenu vizuri na mwisho wake mtalipa kodi stahiki na kuchangia maendeleo ya nchi yetu,” alisema Masalla. Masalla alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya mfanyabiashara anayetunza kumbukumbu na yule asiyetunza kumbukumbu kwani asiyetunza kumbukumbu kwa mauzo ya shilingi milioni 14 atalipa kodi shilingi 450,000 kwa mwaka wakati anayetunza kumbukumbu kwa mauzo hayo atalipa Sh 320,000 kwa mwaka. “Tukichukulia mfano wa wafanyabiashara wawili wenye mauzo ya shilingi milioni 14, lakini mmoja anatunza kumbukumbu na mwingine hatunzi kumbukumbu tunaona kwamba, kuna tofauti ya shilingi 130,000 kwa kuwa asiyetunza atalipa shilingi 450,000 na anayetunza kumbukumbu atalipa shilingi 320,000. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu,”  alisema Masalla. Meneja huyo wa Elimu kwa Mlipakodi amewaambia wafanyabiashara hao kuwa, nyenzo muhimu inayosaidia utunzaji wa kumbukumbu ni pamoja na mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) na kama mfanyabiashara hajafikia mauzo ya kutumia mashine ya EFD ambayo ni chini ya shilingi milioni 14 anashauriwa kutumia kitabu cha risiti za kuandika kwa mkono ambapo mfanyabiashara atakwenda na kumbukumbu hizo TRA kwa ajili ya kukadiriwa kodi. Kwa upande wake mfanyabiashara wa mbao wilayani humo, Zakaria Manyilizu, alisema elimu aliyoipata ya utunzaji kumbukumbu za biashara ni nzuri hata hivyo ameiomba TRA kutoa elimu juu ya namna ya kutumia mashine za EFD kwani walio wengi hawana utalaamu wa kutumia mashine hizo.
kitaifa
Na JANETH MUSHI -ARUSHA RUBANI wa ndege ndogo, mkazi wa Dar es Salaam, David Mbale (25), amefariki dunia baada ya ndege aliyokuwa akiendesha kuanguka kwenye vilima vya Monduli mkoani Arusha. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Engalaoni kilichopo mpakani mwa wilaya za Monduli na Arumeru. Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, Mbale alikuwa akiendesha ndege ndogo yenye namba za usajili 5HSAL 206 inayomilikiwa na Kampuni ya Safari Air Link. “Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria watano, iliondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha, majira ya saa 1:30 asubuhi ya siku hiyo ya tukio ikielekea katika eneo la Kogatende, Serengeti kuwachukua watalii. “Kwenye ndege hiyo, alikuwamo rubani peke yake na alikuwa anasubiriwa na watalii huko Serengeti. “Taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo zilianza kuenea juzi saa nne asubuhi, zikisema kuna ndege imeanguka katika vilima vya Monduli ambavyo ni maarufu kama Monduli Hills. “Baada ya taarifa hizo kutolewa saa 6:30, tuliwajulisha kikosi cha zimamoto na wenzetu wa uwanja wa ndege wa Arusha na walipofika kwenye kilima hicho, walikuta rubani ameshafariki dunia na mwili wake ulichukuliwa kwa uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Mkumbo. Wakati huo huo, Kamanda Mkumbo alisema uchunguzi wa tukio hilo umeanza jana na kwamba watashirikisha wataalamu waliobobea katika masuala ya ndege.
kitaifa
BAADA ya mastaa wa filamu nchini, kuziweka kando tamthilia na kujikita kwenye uandaaji na uchezaji wa filamu kwa kigezo cha maslahi, hivi karibuni wasanii hao wameamka tena nakuanza kuzitolea macho tamthilia mara baada ya tamthilia ya Siri za Familia kufanya mapinduzi makubwa. Akibonga na Swaggaz, mwongozaji wa tamthilia (DoP) hiyo inayoruka kwenye runinga ya EATV, Edson Suche ‘Od Y’, alisema kuwa wasanii wengi wakubwa wamesahau kuwa tamthilia ndiyo chimbuko la vipaji vya kweli kwa hiyo wamejikuta wapo wenyewe tu na hakuna vipaji vingine vipya vyenye haiba kama yao. “Tamthilia ina mjenga msanii na ndiyo chimbuko la vipaji vya kweli. Sisi tunafurahi kuona baada ya Siri a familia kuanza kuruka wasanii wakubwa kama kina Jb, Irene Uwoya, Ray na Johari nao wameamua kurudi huku kwenye tamthilia,” alisema Od Y. Od Y, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, aliongeza kuwa sababu iliyofanya tamthilia hiyo iwashawishi mastaa wakubwa warejee kwenye tamthilia ni ubora na mpangilio mzuri wa hadithi uliofanywa na kampuni ya Jason’s Production waliyoiandaa.
burudani
BARCELONA, HISPANIA UONGOZI wa klabu ya Barcelona umefikia makubaliano na mshambuliaji wa timu hiyo, Neymar ya kumuongezea mkataba mpya ambao utamfanya akae Nou Camp hadi 2021. Julai mwaka huu klabu hiyo iliweka wazi kuwa ina mpango wa kutaka kumwongezea mkataba mchezaji huyo wa miaka mitano, lakini walishindwa kufanya hivyo kwa wakati huo kutokana na mchezaji huyo kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya Olimpiki. Kupitia mtandao wa klabu hiyo, umeweka wazi kuwa tayari uongozi na mchezaji huyo umefikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya Oktoka 21 mwaka huu ambapo itakuwa kesho kutwa Ijumaa. Mchezaji huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu ya Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Brazil, alikuwa anawindwa na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Ufaransa, PSG, ambao walikuwa tayari kuweka mezani kitita cha Euro milioni 193, huku wakidai kuwa walikuwa tayari kumpa mshahara wa Euro 650,000 kwa wiki. Baada ya usajili huo ambao utafanyika Ijumaa, mchezaji huyo atakuwa anachukua kitita cha Euro milioni 16 kwa mwaka, wakati usajili wake utakuwa wa Euro milioni 200 kwa mwaka wa kwanza, Euro milioni 222 kwa mwaka wa pili na Euro milioni 250 kwa miaka mitatu ya mwisho. Hata hivyo, klabu hiyo tayari imemalizana na nyota wake Javier Mascherano ambapo wamempa mkataba mpya utakaomfanya akae ndani ya klabu hiyo hadi 2019. Beki huyo wa timu ya taifa ya Argentina mwenye umri wa miaka 32, alikubali kusaini mkataba na klabu hiyo tangu Julai mwaka huu, lakini mpango huo umekamilika tangu Jumatatu baada ya kukutana na rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu. Mchezaji huyo alihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Juventus katika kipindi cha majira ya joto kuungana na Dany Alves ambaye amejiunga na timu hiyo. Mascherano hadi sasa ameitumikia klabu hiyo na kucheza michezo jumla 290 tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Liverpool miaka sita iliyopita na kufanikiwa kutwaa mataji 17 kwa kipindi chote hicho.
michezo
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
uchumi
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema timu ya taifa ya wanawake ya Bara, Kilimanjaro Queens imewapa heshima kubwa kwa kutwaa ubingwa wa Cecafa na anaamini siku moja soka ya wanawake italeta kombe la Afrika nchini.Kilimanjaro Queens mwishoni mwa wiki iliyopita ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Ethiopia mabao 4-1 mjini Kigali, Rwanda.Aidha, Karia alimshukuru Rais John Magufuli kwa pongezi zake akiahidi hawatomuangusha na ikimpendeza watafuata maelekezo yake kutoka kwa wasaidizi wake.Rais Magufuli juzi alipomaliza kutangaza mabadiliko kwenye nafasi mbalimbali za uongozi katika serikali yake, aliipongeza pia Kili Queens kwa kutwaa ubingwa wa Cecafa.Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ethiopia katika mechi ya mwisho ndio uliohalalisha ubingwa kwa Kili Queens, na hasa baada ya wenyeji Rwanda kufungwa mabao 2-0 na Kenya.Timu hiyo ilitwaa ubingwa huo kwa kuwa na uwiano mzuri wa mabao baada ya kulingana pointi na Uganda iliyoshika nafasi ya pili. Timu hizo zote zilimaliza zikiwa zimelingana pointi, saba.Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kabla ya kupata nao chakula cha mchana Dar es Salaam jana, Karia alisema Kili Queens imeipa heshima kupwa kwa kutetea ubingwa mara mbili mfululizo na amaamini itaendelea na moto huo.“Mwakani tutatwaa tena ubingwa huu ili kombe libaki moja kwa moja Tanzania Cecafa watafute kombe lingine,” alisema.“Timu hii imekaa kambini muda miezi 11 ikifanya maandalizi na sasa tunajipanga na mashindano ya Afrika,” alisema.“Haijifichi nyie ndio mmetufungulia kutuletea vikombe,” alisema Karia.Alisema wataangalia uwezekano wa kuitafutia timu ya taifa ya wanawake kambi ya nje ya nchi japo kwa mwezi mmoja ili wachezaji wake wapate uzoefu.
michezo
NA THERESIA GASPER BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House, iliyo chini ya Msanii Mkongwe wa reggae, Innocent Nganyagwa, limeandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini itakayofanyika leo katika makao makuu ya Basata Ilala jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo lina lengo la kurudisha muziki wa reggae jukwaani na kujadili mwelekeo wa muziki huo ili urudishe hadi yake. Ofisa Habari wa Basata, Alistidesi Kwizela, alisema muziki huo haupigi hatua kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hivyo wasanii wakongwe, Innocent Nganyagwa, Innocent Garinoma, Justine Kalikawe na wengineo wameamua kuja na sera za kurudisha hadhi ya muziki huu. “Nia ya Basata ni kuona wasanii na wadau wote wa muziki nchini wanahudhuria kongamano hilo kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja hatima ya muziki huo, historia yake na namna ya kuburudisha jukwaani na mengine mengi yanayouhusu,” alisema. Aliongeza kwamba kupitia kongamano hilo muziki huo utakuwa na mwanzo mpya mwema kurudi katika ubora wake.  
burudani
Na ELIYA MBONEA – ARUSHA WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, amesema Serikali inakusudia kusitisha utoaji wa leseni kwa Kampuni ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation (OBC). OBC iliyoanza uwindaji mwaka 1992 baada ya kupewa leseni na Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Abubakar Mgumia, imekuwa ikiendesha shughuli hizo kwenye pori tengefu la Loliondo lililopo katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Akizungumza wilayani hapa juzi, wakati wa majumuisho ya ziara yake, Kigwangala, alisema uamuzi huo unatokana na kampuni hiyo kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, kuwa na migogoro isiyoisha na wananchi, hususani jamii ya wafugaji wa Kimaasi. Waziri Kigwangala alisema OBC haitakuwa sehemu ya kampuni za uwindaji zitakazopewa upya leseni ya uwindaji hapo mwakani, hiyo ni kutokana na kuwapo kwa madai ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwamo kujihusisha katika migogoro eneo hilo kwa zaidi ya miaka 25. Alisema kampuni hiyo haitapatiwa tena leseni mpya mwakani, kutokana na kuwa na mkono katika migogoro inayoendelea kwenye eneo hilo la pori tengefu la Loliondo. “OBC ipo nyuma ya vurugu hizi, siku zao zinahesabika, hawatapewa leseni mpya ya uwindaji Januari mwakani,” alisema Waziri Kigwangala. Aidha akiwa Loliondo katika ziara yake, Kigwangala aliagiza mifugo yote iliyokuwa ikishilikiwa na bado wamiliki wake hawajafikishwa mahakamani, iachiwe mara moja wakati mazungumzo kwa pande zote yakiwa yanaendelea. Pia aliagiza wafugaji walioondolewa mifugo yao katika pori hilo, ikiwamo pia maeneo ya mipakani mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, waanze kunyweshea mifugo yao katika mito iliyomo ndani ya pori tengefu la Loliondo. Akiwa mkoani Dodoma hivi karibuni, Kigwangala alisitisha leseni zote za uwindaji katika vitalu na kutaka utaratibu mpya wa kununua vitalu hivyo ufanyike kwa mtindo wa mnada. Akizungumza na wadau wa utalii na uhifadhi, alisema kwamba hatua hiyo inalenga kulinufaisha zaidi taifa kutokana na rasilimali zilizopo. Katika mkutano huo, Kigwangala aliwaambia wadau hao kwamba ni Tanzania pekee katika nchi zilizopo Kusini mwa Sahara ambayo imekuwa haikodishi vitalu vyake vya uwindaji kwa kutumia mnada.
kitaifa
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli, amelitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa na wilaya na mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta majawabu ya kwanini ajali zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani. Kauli hiyo aliitoa jana katika salamu zake za pole kutokana na ajali ya basi la Kampuni ya City Boy iliyosababisha vifo vya watu 12 wilayani Igunga mkoani Tabora juzi usiku. “Viongozi wa idara hiyo wanapaswa kujitafakari kwanini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi, ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali,” alisema katika taarifa yake iliyotolewa na Ikulu. Basi hilo lililokuwa linatoka Karagwe mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam, liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Njombe kwenda Mwanza. “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 iliyotokea Wilaya ya Igunga. Nawapa pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa,” alisema Rais Magufuli. Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, na amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi wote 46 wapone haraka ili waungane na familia zao katika ujenzi wa taifa.   MWIGULU Akitoa taarifa jana bungeni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, ameagiza dereva yeyote atakayekamatwa akiwa kwenye mwendo kasi, pamoja na kutozwa faini, awekwe mahabusi na kisha mahakamani. Hayo aliyasema wakati akijibu mwongozo ulioombwa asubuhi na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlanga (CCM), akihoji kama dereva akikutwa kwenye mwendo kasi anatozwa faini, je ajali ikisababishwa na ubovu wa barabara kama Wakala wa Barabara (Tanroads), itozwe fani ama laa. Akijibu mwongozo huo, Mwigulu alisema: “Taarifa za awali tulizopewa, chanzo cha ajali hiyo siyo mashimo ya barabarani peke yake, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. “Dereva yule alikuwa anaenda mwendo kasi sana, alipokutana na shimo lile gari likakata kifaa kimoja cha kwenye matairi, gari ikapoteza mwelekeo ndipo likaenda kugonga lile basi la abiria. “Kwa maana hiyo, kama alikuwa anaenda kwa mwendo unaostahili, yale hayakuwa mashimo ya kusababisha ajali, kwa sababu magari yalipita siku nzima yeye akaja kupata ajali baadaye, kwahiyo tatizo lilikuwa lilelile, mwendo kasi. “Kwa kuwa watu wameshazoea mambo ya kutozwa faini na anaona sisi tunatafuta fedha, naelekeza Jeshi la Polisi popote pale watakapokamata dereva anaenda mwendo kasi pamoja na kutoza faini, wamuweke ndani mpaka watakapompeleka mahakamani ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa,” alisema Dk. Mwigulu.   POLISI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa, alisema ajali hiyo ilitokea Aprili 4, mwaka huu saa 2 usiku, chanzo kikiwa ni lori aina ya Mitsubishi lenye namba T 486 ARB kupasuka tairi ya kulia na kuathiri mfumo wa usukani na kupoteza mwelekeo, hivyo kugongana na basi hilo lenye namba za usajili T 983 DCE aina ya Scania lililokuwa likitokea Karagwe mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam. Alisema dereva wa basi hilo, Emmanuel Chitemo (39) mkazi wa Dar es Salaam, alifariki papo hapo na dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Njombe kwenda Mwanza likiwa limebeba shehena ya viazi nviringo, Salum Abdallah (25) mkazi wa Ruvuma ametoroka na polisi wanaendelea kumsaka.
kitaifa
Akizungumza kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) hivi karibuni, Nyambui alisema wanariadha wakongwe kama Filbert Bayi na baadhi ya wengine walikuwa wakihudumiwa kama wafalme na kufuatiliwa maendeleo yao.“Kwa mfano Bayi, alikuwa akifanya kazi Jeshini, walikuwa wakimjali kwani walimpa nyumba na alikuwa akipewa gari la kupelekwa mazoezini na kurudishwa, mimi mwenyewe mkuu wa mkoa kipindi hicho alikuwa akifuatilia mienendo yangu sasa na kuuliza naendeleaje, kwanini usifanye vizuri,” alisema.Alisema ukilinganisha na sasa ni tofauti kwani wanariadha wengi wanashindwa kufanya vizuri kutokana na wengi kutoka katika mazingira magumu tena yakiwa hayana msaada kwa viongozi wa eneo husika.Nyambui alitolea mfano kuwa kuna wengine huonekana kufanya vizuri katika mashindano ngazi ya mkoa lakini hawana vifaa vya michezo.“Nakumbuka kuna mwanariadha mmoja aliwahi kuja kwenye mashindano ya kitaifa alikuwa hana viatu, hivyo alikimbia akiwa hajavaa viatu na akafanya vizuri. Lakini alipokuja kupewa viatu alitoka malengelenge na kufanya vibaya, kwa sababu wanatoka kijijini hawakuandaliwa namna na kutumia viatu,” alisema.Alizungumzia pia, wanariadha hufanya vibaya kutokana na mazingira magumu anayoishi, kwani wanahitaji chakula kizuri na chenye nguvu, lakini wengi wana hali ngumu.
michezo
Msuva ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza pamoja na chipukizi wa Simba Ibrahim Ajib, wamekuwa na kiwango kizuri msimu huu, huku wachezaji wawili wa kulipwa, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakikosekana kutokana na kufuzu kwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Wachezaji walioitwa ni timu zao katika mabano ni Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ally, Shomari Kapombe (wote Azam FC), Kelvin Yondani, Nadir Haroub (wote Yanga), Abdi Banda (Simba), Oscar Joshua (Yanga), Aggrey Morris (Azam FC), Isihaka Hassan (Simba) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar).Wengine ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Salum Abubakar (wote Azam FC), Said Juma Makapu (Yanga), Frank Domayo (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haruna Chanongo (Simba), Mwinyi Kazimoto (Al-Makhiya, Qatar), Simon Msuva, Salum Telela (wote Yanga), Ajib, Mrisho Ngassa (Yanga), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mwinyi Haji (KMKM) na Kelvin Friday (Azam FC).Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Nooij alisema ni lazima wachezaji wote waliotajwa hata kama ni majeruhi, wafike kambini kwenye Hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.“Tunatawaka wachezaji wote wafike siku hiyo, watafanyiwa vipimowale watakaobainika ni majeruhi watabaki na kwa ajili ya matibabu kisha watasubiri mechi nyingine za Afrika,” alisema kocha huyo raia wa Uholanzi.Nooij alisema kati ya wachezaji hao 28, 20 tu ndio watachaguliwa kwenda Afrika Kusini na wanane watabaki Dar es Salaam, na kwamba ikitokea baadhi wakaumia, waliobaki ndio watasafirishwa kuziba pengo, lakini kama sivyo, basi watasubiri kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afrika na ile ya Wachezaji wa Ndani (CHAN).Alisema kwa vile ligi bado inaendelea iwapo ikimalizika kuna ambao wataongezwa baada ya kumalizika kwa msimu kwa ajili ya michuano hiyo mingine ya Afrika.Naye Mratibu wa Taifa Stars, Martin Chacha alisema katika michuano hiyo ya Cosafa itakayochezwa katika Jimbo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, Stars inatarajiwa kucheza Mei 18, dhidi ya Swaziland na siku inayofuata dhidi ya Madagascar na kisha Lesotho.Alisema wachezaji hao wataondoka Jumatano saa moja usiku kwa ndege ya Fastjet. Chacha alisema timu ikirudi kwenye mashindano hayo, itajiandaa tena kwa michuano ya Afrika dhidi ya Misri na CHAN ambapo inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda mwezi ujao.
michezo
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ ametengua kauli yake ya kujiuzulu nafasi hiyo baada ya jana kuandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa twitter uliosababisha sintofahamu kwa mashabiki, wanachama na wadau wa soka.Awali, baada ya Simba kufungwa mchezo wa Fainali wa Kombe la Mapinduzi kwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar, Dewji aliandika ujumbe wa kuachia ngazi na atabaki kama mwekezaji tu.“Ni huruma Simba kutoshinda, baada ya kulipa mishahara inayokaribia Sh Bilioni nne kwa mwaka, najiuzulu kama Mwenyekiti wa Bodi na kubakia mwekezaji, Simba Nguvu Moja, nitatia nguvu kwenye kuendeleza miundombinu na soka la vijana,” ujumbe wa MO.Baada ya kutoa ujumbe huo uliozua mijadala mbalimbali kwenye vyombo mbalimbali vya habari, mwekezaji huyo kwa mara nyingine jana aliandika ujumbe mwingine kwenye mtandao huo akionesha kujutia kitendo hicho.Ujumbe huo ulisomeka hivi: “Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana (juzi) kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu, tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa Sugar kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba,” Kabla ya kuandika ujumbe wa pili, baadhi ya wadau waliguswa na ujumbe huo na kutoamini kama kweli ni yeye mwenyewe aliyefanya hivyo, huku wakiwatia moyo mashabiki na wanachama kuwa watulivu.Mmoja wa wadau hao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyeandika ujumbe huu: “Matokea ya mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole kwa timu yangu ya Simba pamoja na mashabiki wote na wanaoitakia mema Simba. “Sina uhakika na kinachoendelea kwenye akaunti ya MO kama ni Mo Dewji mwenyewe. Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga amani na utulivu wa timu zetu. Simba nguvu moja.”Mdau mwingine wa soka, Ridhiwan Kikwete aliandika ujumbe huu baada ya MO kutangaza kujiuluzu: ”Naheshimu sana maamuzi ya mtu lakini kaka sina hakika kama kafanya busara katika hili. Hela hazinunui ushindi, ni haki yao kulipwa kwa kazi wanayoifanya. Tafadhali usifanye hasira. Huu ni mpira tu na matokeo yako matatu. Ninaamini utalifikiria tena uliloamua,” Kuhusu mchezo wa juzi, Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alisema licha ya kushinda mchezo huo, Simba walikuwa ni bora mwanzo mwisho isipokuwa walichofanya ni kuzima mbinu zao.“Simba walikuwa bora mwanzo mpaka mwisho, siwezi kusema walikuwa dhaifu. Mimi niliwabana kwa mbinu wala sisemi kama nilikuwa bora, nilikuwa nacheza na timu bora ndio maana nilikuwa makini kuangalia mbinu zao ambazo walikuwa wanajaribu lakini yote yote tukashinda,” Alisema ushindi huo kwao ni historia kwani mara ya mwisho kuchukua ni mwaka 2010. Nahodha wa Simba, John Bocco alisema:“Tunashukuru Mungu tumemaliza salama, tunawapongeza Mtibwa kwa kucheza vizuri. Tunajipanga na michezo ya ligi iliyoko mbele yetu,”alisema.
michezo
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuacha kuwabughudhi wawekezaji ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na tija.Aidha amesema iwapo wawekezaji watafanikiwa katika shughuli zao, majirani na wawekezaji na taifa kwa ujumla litanufaika kwa kodi na pia kuchangia huduma mbalimbali za kijamii.“Msiwafanyie fujo wawekezaji, wapendeni kwa kuwa kila mwaka wanatakiwa kulipa kiasi fulani cha fedha kwenye kijiji kilichopo jirani nao. Hivyo, mwekezaji akifanya vizuri kijiji husika pia kinanufaika kwa kuboreshewa huduma za kijamii,” amesema.Makamu wa Rais alisema hayo akitoa salamu zake kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa vijiji vya Ulyampiti, Mang’onyi na kwenye Mkutano wa hadhara Ihanja akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida.Katika salamu zake Mama Samia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na utulivu nchini.“Kunapokuwepo na amani, sisi kama serikali tunapata fursa ya kufanya na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo bila bughudha,” alieleza Makamu wa Rais.Wakati huo huo Makamu wa Rais amemtaka Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuhakikisha anawajengea kisima kimoja wananchi wa kijiji cha Mang’onyi katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ili kuondoa adha ya upatikanaji maji kwenye eneo hilo.Alitoa agizo hilo jana alipotembelea zahanati ya kijiji cha Mang’onyi iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa kutumia sehemu ya fedha za fidia Sh bilioni 2.5 zilizolipwa kwao kumpisha Mwekezaji, Shanta Mining Ltd, ili kufanya uchimbaji wa dhahabu kijijini hapo.Alisema kuwa kwa muda mrefu wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakikabiliwa na shida ya maji lakini kutokana na serikali kutenga fedha kwa ajili ya visima 20 wilayani humo mwaka huu wa fedha, sasa kuna umuhimu mkubwa wa kuwapatia wananchi wake maji safi na salama.
uchumi
BERLIN, UJERUMANI KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi kuongeza hatua za Serikali yake katika kusaidia sekta binafsi barani Afrika dhidi ya misukosuko ya kisiasa na utaratibu wa malipo usio wa kawaida. Alitoa ahadi hiyo alipokutana na wafanyabiashara na marais 12 wa Afrika katika mkutano wa kilele mjini hapa unaonuia kuongeza uwekezaji binafsi barani Afrika. Merkel alisema fedha za maendeleo zitakazotolewa zinapaswa kusaidia uwekezaji wa kampuni ndogo na kiwango cha kati ya barani Ulaya na Afrika kupitia hisa na mikopo. “Tunataka kutoa ishara bayana, tunapendelea ushirikiano mwema na wenye faida wa ujirani mwema kati ya Afrika na Ulaya. Sisi ni majirani, washirika, na sisi wa Ulaya tuna masilahi makubwa zaidi kuona Afrika yenye nguvu na matumaini mema ya kiuchumi. “Na hilo kulifikia panahitajika si tu vitega uchumi vya Serikali bali zaidi kuliko vyote vya binafsi,” alisema Merkel. Lengo hasa la mkutano huu wa kilele ni kutoa nafasi nzuri za ajira kwa Waafrika, kupunguza umasikini ambao pamoja na misukosuko ya kisiasa na vurugu ndiyo mambo yanayosababisha idadi kubwa ya Waafrika kukimbilia barani Ulaya.
kimataifa
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
uchumi
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma, mchakato wake umesitishwa jana, kwa kile kilichoelezwa kutokuwapo kwa maelewano kwa wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho hilo Tayari kamati ya uchaguzi ya Shirikisho hilo ilifikia kufanya usaili kwa watu waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, huku wakishindwa kuwasaili wengine ambao wanakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Watu wanaokabiliwa na kesi ni Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, aliyehitaji kutetea nafasi yake na Geofrey Nyange ‘Kaburu’, aliyeomba kuwania nafasi ya makamu wa rais. Kwa pamoja wawili hao walikuwa katika mikono ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), wakikabiliwa na tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka na baadaye kufikishwa katika mahakama hiyo. Kutokana na Malinzi na Kaburu kuwapo rumande ya mahakama ya kawaida ya sheria, tumeelezwa kwamba, kumekuwa na mabishano makubwa ndani ya kamati ya uchaguzi, huku wengine wakitaka nao wapitishwe kwenye kinyang’anyiro hicho. Sababu hiyo imeifanya kamati kugawanyika katika hilo na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF, Revocatus Kuuli, kufikia uamuzi wa kusitisha mchakato wa uchaguzi huo, ambapo sasa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo itakutana kesho kujadili suala hilo. Tumesikia kabla ya kusitisha mchakato wa uchaguzi huo kulikuwa na mabishano makali ya kimtazamo kiasi cha baadhi ya wajumbe kutishia kuachia nafasi zao Kuna baadhi ya wajumbe wa kamati aliona kwa sasa hakuna haja ya watu wanaokabiliwa na mashtaka kuendelea kuwapo katika uchaguzi huo, lakini wengine wakiona kwa kufanya hivyo watakuwa hawajawatendea haki kwa sababu hawajatiwa hatiani. MTANZANIA tunaona  kuwa Kamati ya Utendaji ya TFF inatakiwa kuja na jibu moja ambalo litawezesha mchakato ya uchaguzi kuendelea na kuachana na figisufigisu ambazo zinaweza kuathiri mchakato mzima wa kupata viongozi wa soka. Tunahitaji kuona busara zaidi zitawale katika kikao cha kamati ya utendaji kitakachofanyika kesho, kwani wao ni mhimili mkubwa wa kuongoza soka nchini, lakini ni chombo chenye mamlaka ya kutoa uamuzi. MTANZANIA tunasema kwamba mawazo ya  kila mwana kamati  yatasaidia kujenga uelewano ndani ya kamati ya uchaguzi na baadaye mchakato kuendelea kama kawaida. Matarajio ya Watanzania wengi ni kushuhudia uongozi mpya ndani ya Shirikisho hilo ukipatikana, bila kuhusisha upendeleo wa upande mmoja. Malengo ni kusongesha mbele gurudumu la michezo ili kuiwezesha Tanzania kupiga hatua na kuendelea kuwa miongoni mwa mataifa yanayoweza kunufaika kupitia michezo. Tunarudia kwa kusema, kamati ya utendaji inatakiwa kutenda haki na kutoa muafaka wa jambo hili, ambalo tayari lilianza kusonga mbele na kufikia katika hatua nzuri ya kupatikana kwa uongozi mpya ndani ya shirikisho hilo.  
burudani
Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM LICHA ya kikosi chake kukamata nafasi za chini  kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed, amesema atahakikisha analinda rekodi yake ya msimu uliopita ya kutopoteza pointi tatu dhidi ya  Yanga. Prisons itakuwa mgeni wa Yanga kesho katika pambano la Ligi Kuu litakalopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Prisons inakamata nafasi pili katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 10, sawa na Biashara United iliyoko mkiani kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Prisons inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, msimu uliopita ilivuna pointi nne katika michezo miwili iliyokutana na Yanga , ikianza kwa sare ya bao 1-1, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine, katika mchezo wa mzunguko wa pili. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mohamed alisema nafasi yao ya sasa katika Ligi Kuu haiwezi kuwa kigezo cha kupoteza mchezo wao wa kesho, kwani amekiandaa kikosi chake ili kushinda. “Ni kweli tupo katika nafasi mbaya, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga, tumejipanga ili kushinda na kulinda rekodi yetu ya kupata matokeo mazuri msimu uliopita. “Tumekuwa na muda kutosha wa kujiandaa, tunataka kutumia uwanja wetu kujiongezea pointi tatu na kujitoa katika nafasi za chini, tunajua wapinzani wetu wana mwendelezo wa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita, sisi tutawavurugia kwa mara ya kwanza,” alisema Mohamed, kocha huyo bora wa msimu uliopita.
michezo
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja ametangaza kurejesha shilingi milioni 40.4, fedha za mgawo wa Escrow alizopokea kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemalira. Mbunge Ngeleja ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo. Pamoja na mambo mengine, Ngeleja anasema sababu zakurudisha fedha hizo ni kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyempa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow, amepima na kutafakari, na hatimaye ameamua, kwa hiari yake mwenyewe, kurejesha serikalini (TRA) fedha zote alizopewa kama msaada (TZS milioni 40.4) bila kujali kwamba alishazilipia kodi ya mapato, na risiti ya  ushahidi wa kurejesha fedha hizi serikalini ipo. “Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo,” amesisitiza Ngeleja Kwa mujibu wa Ngeleja, tarehe 12/02/2014 alipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40.4 za kitanzania kutoka kwa Ndugu James Rugemalira, mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd. Fedha alizipokea kupitia akaunti yangu namba 00110102352601 ya Benki ya Mkombozi. “Fedha hizo nilizipokea, kwa nia njema, kama msaada/mchango kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu ya kibunge, hususan,kusaidiana na wananchi wa jimbo langu la Sengerema na Taifa kwa ujumla, kutekeleza shughuli za kijamii (mfano ujenzi wa makanisa, misikiti, kusaidia kulipia karo za wanafunzi wasiojiweza, n.k) na shughuli za miradi ya maendeleo ambayo haipo kwenye bajeti ya serikali,” alisema Ngeleja Aliongeza kuwa, “Nilipokea Fedha hizo kutoka kwa ndugu Rugemalira bila kujua kwamba fedha hizo zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya akaunti ya fedha za Escrow kama ilivyo sasa,”. Zaidi ya hilo, tarehe 15/01/2015 alilipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiasi cha Shilingi 13,138,125/= ikiwa ni sawa na asilimia 30 (30%) ya msaada huo aliopewa, kama ilivyoelekezwa na TRA. Aliongeza kuwa, “Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma, na pia niliwahi kuitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa takribani miaka mitano na nusu ( Naibu Waziri/Waziri), lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi. Kwa hiyo nimesononeka na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma,”. Mbunge Ngeleja amesisitiza kuwa amerudisha fedha hizo ili kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi yake, chama chake (CCM), Serikali yake, Jimbo lake la Sengerema, familia yake na heshima yake mwenyewe. Hata hivyo amesema kuwa kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuwa msaada unaopewa una harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao. “Ninampongeza, kwa dhati kabisa, Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa maslahi ya Taifa letu. Nami naungana na watanzania wenzangu wazalendo kumuombea kwa Mungu na namhakikishia nitaendelea kumuunga mkono kwa kupigania maendeleo ya nchi yetu,” alisema Ngeleja
kitaifa
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imesema bado inaendelea kulifanyia kazi sakata la mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi mdogo ujao. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athumani Kihamia, alilieleza Habari- Leo jana kuwa muda ukifika, watalitolea maelezo jambo hilo, lakini kwa sasa hawezi kusema lolote kwa vile linafanyiwa kazi.Sakata hilo la Mnzava kuwa mgombea pekee wa ubunge kwenye jimbo hilo, limekuja baada ya fomu ya mgombea huyo kuwa pekee iliyorudishwa kwa wakati katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo saa 10 jioni Agosti 20, mwaka huu. Wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walidaiwa kushindwa kurejesha fomu zao ndani ya muda huo.Wagombea walioshindwa kurejesha fomu zao kwa wakati na vyama vyao kwenye mabano ni Amina Saguti (Chadema), Abdulazizi Abdallah Mahamoud (AAFP), Josephine Mpalahingwe (DP), Shabani Karata (ACT), Nurdin Mshangama (CUF), Catherini Mpalahingwe (SAU) na Juma Gao (ADA-TADEA). Wakati Dk Kihamia akisema kuwa suala la Mnzava kupita bila kupingwa litatolewa maelezo baadaye, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Kwame Daftari, alinukuliwa na gazeti hili juzi akisema kuwa wagombea hao, wana nafasi ya kufuata ngazi za kisheria ili kuwasilisha malalamiko yao. Kwa mujibu wa Daftari, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, ilipofika saa 10 jioni ya Agosti 20, mgombea aliyekuwa amerejesha fomu alikuwa ni mmoja tu, ambaye ni Mnzava wa CCM.
kitaifa
Na Asha Bani, Dar es Salaam Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) kwa kushirikiana, Mtandao Wa Wanafunzi (TSNP) na Kituo cha Haki za Binamu wamepeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kuitaka itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumpeleka Abdul Nondo Mahakamani au kumpa dhamana wakati shauri la msingi likiwa linaendelea. Onesmo Olengurumwa Mratibu Wa mtandao wa THRDC, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kijana huyo anashikiliwa kwa siku nane bila hata ndugu, jamaa na wanafunzi wenzake kujua alipo. “Kimsingi ananyimwa haki ya kikatiba ya kuzungumza kile kilichomkuta, wakati Jeshi la Polisi tayari limeshatoa taarifa,” amesema. Naye Katibu wa TSNP, Joseph Malekela amesema ni jambo la kushangaza kuona mwenzao anashikiliwa hadi leo bila hatua zozote kuchukuliwa. “Tumezunguka vituo vyote bila mafanikio, hatujui yuko wapi, tunajibiwa na wakuu wa vituo hawajui, hawajui ni jambo la ajabu wakati mzazi wake akiwa mgonjwa mkoani Kigoma yanatukia haya,” amesema. Kwa mujibu wa wanafunzi hao baba wa Nondo amewaomba wamsaidie katika kutafuta haki ya mwanawe ikiwamo kujua alipo kwa sasa.
kitaifa
Mwandishi Wetu -Dodoma MRADI wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo. Akizungumza n kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Issa Dinya,  alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula. Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77 na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake. Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko. Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.  “Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi,” alisema Redman. Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini. “Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka,” alisema
uchumi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli amesema, Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora ni jambo kubwa na ameomba majukwaa ya fursa za biashara yanayoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) yawe ya kudumu.Kuuli amesema ofisini kwake mjini Igunga kuwa, anatarajia mambo makubwa baada ya jukwaa la Tabora kwa kuwa TSN imefanya kazi kubwa ya kuzitangaza fursa ambazo watu wengi walikuwa hawazifahamu.Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia kesho.“Kwanza mimi nishukuru sana, hili wazo sasa nadhani litaendelea kuwa la kudumu, litaendelea kuwa la kudumu. Hata nilikuwa nafikiria juzi juzi hapa nikasema hawa mbona wanafanya kitu kikubwa sana au kwa sababu wenyewe ni taasisi ya Serikali wanapata ruzuku na hawafanyi biashara...“Kwa hiyo hiki ni kitu ambacho kama ninyi wenyewe mlivyoona kinafaa na sisi wadau muhimu tukaunga mkono jitihada zenu kitu hiki kinatakiwa kiwe kitu cha kudumu, kiwe kitu cha kudumu”amesema.Kwa mujibu wa Kuuli, kuna fursa nyingi za biashara na uwekezaji Igunga, ingekuwa vigumu na ingegharimu fedha nyingi kuzitangaza lakini TSN imefanya kazi kubwa kuzitangaza.Amesema, hata yeye kabla ya kwenda wilayani humo hakuwahi kufikiria kwamba, unaweza kulima mpunga na ukavuna.“Kwa hiyo hii publicity mliyofanya ni kubwa na tunaomba na kushauri ikiwezekana suala hili liwe suala la kudumu katika taasisi yenu” amesema Kuuli wakati anazunguma na timu ya TSN ilikwenda Igunga kuzifahamu na kuzitangaza fursa za biashara na uwekezaji.Amesema, Igunga wanalima sana mpunga, na wanahitaji uwekezaji mkubwa katika kilimo cha umwagiliaji, maghala ya kuhifadhia zao hilo, na viwanda vya uchakataji ili kuziongezea thamani sokoni.Kuuli amesema, kwa sasa kuna miradi 11 ya kilimo cha mpunga kwa kumwagilia na wana uhakika wa kulima na kuvuna magunia 100 hadi 120 katika hekta moja.“Mpunga tunaozalisha hapa ni kiwango kikubwa cha kutosha, hauwezi kuwa tu kwa ajili ya chakula, kwa hiyo tunauza kwenda mikoa mingine, tunauza pia kupeleka nje ya nchi kwa kufuata taratibu. Tuna watu wana magodown (maghala) hapa wanafanya uhifadhi wa mazao na kuna wakulima wanahifahi mazao yao wanasubiri bei ipande na wanahifadhi tu kwa maana ya kuhifadhi akipata mteja atamuuzia yakiwa kule ghalani” amesema.Kuuli pia amesema, Igunga kuna mifugo mingi wakiwemo mbuzi, kondoo na ng’ombe takribani 600,000 Igunga hivyo kuna fursa kubwa ya kuwekeza katika machinjio ya kisasa, na viwanda vya nyama na bidhaa za ngozi.“Hapa pia kwa sababu ya mchanganyiko wa mazao na mifugo ipo fursa kubwa ambayo watu wengi hawajaiona, tunaweza kuwa na kiwanda kizuri hapa kikatengeneza chakula cha mifugo. Utapata hapa hapa mashudu ya pamba, mashudu ya alizeti…“Utapata hapa hapa mifupa, utapata hapa hapa mtama, mahindi, hautahitaji kufuata zao lolote lile linalotumika kutengeneza chakula cha mifugo kutoka sehemu nyingine lakini hatuna nafasi hiyo. Kwa hiyo wawekezaji wa ndani na wale wa nje wanaweza kufikiria kufanya shughuli ya namna hiyo” amesema.Amesema, kiwanda hicho kitaboresha ufugaji ukiwemo wa kuku hivyo kuongeza vipato vya wananchi. Kuuli amesema, Igunga pia wametenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji sekta ya madini na kwa sasa wachimbaji wengi ni wadogo wadogo hivyo kuna fursa za kutosha.“Na maeneo bado yapo, kwa hiyo ni fursa kwa wananchi ambao hawafamu kwamba Igunga unaweza kupata dhahabu, unaweza kupata silver, wanaweza kuja na bahati nzuri sasa ili komisheni ya madini imerahisisha upatikanaji wa haya maeneo, unakwenda unaomba, ukishapewa eneo na leseni yako unapewa palepale kwenye mkoa ambapo umepata eneo la kuchimba madini” amesema.
uchumi
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM LIGI Kuu Tanzania Bara inaelekea ukikongoni, huku kukiwa na matukio lukuki ambayo huenda yakawa ndio chanzo cha kuporomoka kwa ubora wa ligi hiyo. Matukio hayo ni pamoja na  dosari za waamuzi ndani ya uwanja, kashfa ya upangaji matokeo na kashifa za Kamati za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupendelea upande mmoja wanapotoa uamuzi wao. Kwa kipindi kirefu dosari hizo zinatajwa kuwa chanzo cha Ligi Kuu kuwa na timu mbili kati ya Simba na Yanga, huku nyingine zikilalamika kuonewa. Waamuzi wamekuwa wakilalamikiwa sana kuhusu uamuzi wao ndani ya uwanja, kutokana na kugubikwa na utata mwingi, hasa katika michezo mikubwa ya Simba na Yanga. Vitendo vinavyofanywa na waamuzi ni kama tunakwenda hatua mbili mbele lakini tano nyuma, kwa kushindwa kutoa haki ndani ya uwanja. Klabu hizo mbili zimekuwa zikitajwa mara kadhaa katika kudumaza soka nchini wakitumia ushawishi wao wa mtaji mkubwa wa mashabiki walionao. Pia kuwapo kwa viongozi wanaofanya uamuzi wao kwa mahaba ndani ya TFF kitendo hicho kimetajwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayoirudisha nyuma tasnia ya mchezo wa soka nchini. Viongozi hao kupitia kamati wanazoziongoza wamekuwa wakilalamikiwa kufanya vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiongezeka msimu hadi msimu. Kingine ni matumizi ya fedha na kuwahadaa wachezaji kufanya vitendo ambavyo si vya kimichezo ndani ya uwanja, pia kimechangia kuondoa ladha ya mchezo huo. Kwa ujumla njaa na tamaa za fedha vimekuwa chanzo cha matatizo na soka letu kuporomoka kwa kupanga matokeo ya mchezo hata kabla ya kuchezwa. Tumeshuhudia mara kadhaa wachezaji  kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na uongozi wa klabu zao kwa madai ya kupokea fedha kutoka kwa timu pinzani na kusababisha kupoteza mchezo wao. Aidha, janga la klabu kukosa wadhamini pia ni tatizo lingine linalotajwa kuondoa ushindani ndani ya Ligi Kuu, huku nyingine zikikiri kushindwa kujiendesha kutokana na ukata wa fedha. Kwa haraka haraka yapo mambo mengi ambayo yanatakiwa kushughulikiwa ili msimu ujao uoneshe mabadaliko kwa kurejesha imani kwa wapenzi wa soka nchini. Ukiachana na hilo, lilikuwapo suala la wapi panastahili kufanyika fainali za Kombe la FA, linaloandaliwa na TFF, kati ya Mbao FC dhidi ya Simba, kabla ya kuamuliwa fainali hiyo kuchezwa Mei 28 mwaka huu, Jamhuri, mjini Dodoma. Jibu la kwanza lilitolewa na Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, kuwa itachezeshwa droo kabla ya kufanya uamuzi. Hivi kwa wanaofuatilia masuala ya soka ulimwenguni, kuna ambaye hajui fainali za kombe la dunia zinafanyika wapi, fainali za Uefa zinafanyika wapi au lile kombe la FA pale England fainali zake zitafanyika wapi? iweje fainali za FA za Tanzania hazikujulikana mapema kabla  ya  kuchezwa mechi za nusu fainali. Kwa hali hii, TFF wanahitaji kubadilika  kifikra na maarifa namna ambavyo tutaendesha Ligi kwa haki bila ya dalili za ubabaishaji kama ambavyo inatokea sasa.  
kitaifa
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Taifa Stars Cuper alisema Samatta ni mchezaji anayecheza katika kiwango cha dunia, lakini siku hiyo hakucheza kama anavyojulikana kwa kuwa walimzuia.Alisema timu yake ilijipanga na kucheza mchezo mzuri kiasi kwamba mchezaji huyo hakuweza kuonesha uwezo wake. “Namjua Samatta ndiye mchezaji bora ambaye ananivutia, lakini leo (juzi) hakucheza kwa kiwango chake cha kawaida, pengine ni kwa vile tulimzuia na kushindwa kupenya,” alisema.Licha ya kuweka wazi kuvutiwa na Samatta, mchezaji huyo alikosa penalti iliyopatikana baada ya mmoja wa wachezaji wa Taifa Stars kuchezewa madhambi eneo la hatari na kupoteza matumaini yao ya kufanya vyema.Kocha huyo alijaribu kupunguza makali kwa kukisifia kikosi cha Stars kuwa kilicheza vizuri. Alikisifu pia kikosi chake kuonesha mchezo mzuri kama alivyowaelekeza, na kufanikiwa kuondoka na ushindi huo ambao umeipa nafasi ya kufuzu moja kwa moja fainali za Mataifa ya Afrika kwa kufikisha pointi 10, huku Tanzania ikiwa na pointi moja na Nigeria pointi moja.
michezo
LAGOS, NIGERIA KAMPENI za uchaguzi zimemalizika nchini Nigeria kwa rais anayemaliza muhula wake, Muhammadu Buhari, kusifu kipindi chake cha uongozi, huku mpinzani wake mkubwa, Atiku Abubakar, akiwatolea wito wafuasi wake wahakikishe wanamnyima kura na kung’oa kabisa utawala wa Buhari. Atiku Abubacar amewatolea wito mkali wafuasi wake waliokusanyika katika jimbo alikozaliwa la Adamawa wahakikishe enzi za Buhari zinamalizika. Hayo yamejiri siku moja baada ya wagombea kuahidi mbele ya wanadiplomasia, wasimamizi wa uchaguzi na wananchi, watahakikisha uchaguzi unafanyika salama. Wagombea wote wawili, Atiku aliyewahi kuwa makamu wa rais na Buhari mtawala wa zamani wa kijeshi anayesema amegeuka kuwa mwanademokrasia, wanatokea kaskazini mwa Nigeria. Wapiga kura milioni 84 watateremka vituoni kesho kumchagua mmoja kati ya viongozi hao wawili. Wakati huo huo,  wagombea wamesema wapo tayari kwa zoezi la uchaguzi mara baada ya kumalizika kampeni, ambapo wapiga kura milioni 84 wanatarajiwa kupiga kura. Katika kambi inayomuunga mkono kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Atiku Abubakar Mjini Lagos wafuasi wake wamejitokeza kumuunga mkono. Walifanya kampeni za mwisho wakiwa na imani kuwa, mgombea wao atashinda kama alivyoniambia mfuasi huyu: “Tunamhitaji Atiku aje atuongoze sasa hivi, tumechoka kuteseka, tunawaomba sana Wanigeria wampigie kura Atiku, uchumi wetu utaimarika na mambo yatakuwa mazuri,” alisema mmoja wa wafuasi wake. Kwa upande wa chama tawala cha APC, wao walitumia matarumbeta katika eneo la Ikoyi, katikati mwa mji huu, kumwombea Rais Buhari kura. Mfuasi huyu anaamini kuwa Rais Buhari anastahili kurejea tena madarakani. “Buhari anajenga msingi, msingi wa maendeleo, ukweli na kupinga ufisadi, sababu hizi ndizo zilizotufanya kuacha kazi zetu na kuja hapa kumuunga mkono ili Nigeria iendelee,” alisema Buhari. Kuelekea uchaguzi wa kesho, Rais Buhari ambaye anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wake, Atiku Abukakar, alikuwa na ujumbe huu kwa raia wa Nigeria. Atiku naye alituma ujumbe wake wa mwisho kabla ya siku ya upigaji kura. Wagombea 72 wanawania urais, lakini ushindani ni kati ya Rais Muhammadu Buhari na makamu wa rais wa zamani, Atiku Abubakar.
kimataifa
RIO DE JANEIRO, BRAZIL  SIKU chache baada ya kuvuliwa unahodha katika timu ya taifa ya Brazil, mshambuliaji wa timu hiyo, Neymar, ametia hofu baada ya kuumia goti wakati wa mazoezi ya timu hiyo kuelekea michuano ya Kombe la Copa America. Brazil ni wenyeji wa michuano hiyo msimu huu ambapo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14 hadi Julai 7, mwaka huu kwa timu 12 kutoka Amerika ya Kusini zikioneshana ubabe kwenye miji mitano. Neymar aliumia wakati wa mazoezi ya pamoja juzi Jumanne na alionekana akitoa machozi huku akiugulia maumivu ya goti la kushoto. Hata hivyo, hakuweza kuendelea tena na mazoezi na alitolewa moja kwa moja nje. Nyota huyo ambaye anakipiga katika klabu ya PSG, aliungana na daktari wa timu hiyo, Rodrigo Lasmar, kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu. Mchezaji huyo ameumia ikiwa ni siku moja baada ya kuvuliwa unahodha. Katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi, Neymar alitajwa kuwa nahodha wa kudumu katika kikosi hicho cha Brazil chini ya kocha wao Tite, lakini sasa nafasi hiyo inachukuliwa na nyota mwenzake wa PSG, Dani Alves kuelekea michuano hiyo. Inasemekana kuwa Neymar amevuliwa kitambaa hicho kutokana na utovu wa nidhamu ambao anahusishwa nao. Wiki kadhaa zilizopita mchezaji huyo baada ya kuonekana akimshambulia shabiki wa timu ya Rennes, hivyo chama cha soka nchini Ufaransa kilimpa adhabu ya kufungiwa michezo mitatu. Hata kabla ya adhabu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mchezaji huyo alifungiwa michezo mitatu na Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA) kutokana na kauli chafu kwa mwamuzi wa mchezo kati ya PSG dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora kwenye Uwanja wa Parc des Princes. Kutokana na baadhi ya sababu kama hizo, kocha huyo wa Brazil ameamua kumvua unahodha mchezaji huyo ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya Copa America. 
michezo
Uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa timu hiyo itacheza mechi ya kwanza ya kuukaribisha msimu mpya wa 2019/20 Julai 27 mwaka huu, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam dhidi ya wapinzani kutoka nje ya nchi. Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla amesema hayo katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam. “Tarehe 27/07 tutakuwa na matukio matatu, moja ni kutambulisha jezi, pili kutambulisha wachezaji wapya na tatu ni tutakuwa na mchezo kimataifa wa kirafiki,”amesema Dk. Msolla, kocha wa zamani wa Taifa Stars. Aidha, Dk. Msolla amesema kwamba usajili walioufanya ni mzuri kwa sababu umezingatia vigezo vya kitaalamu kimpira. “Tumesajili kulingana na matakwa ya mwalimu, hata huko alipo lazima atakuwa ana furaha, maana wachezaji wote wa nje na ndani aliokuwa akiwahitaji tumewapata, pia siku tatu zilizopita mwalimu alituma programu ya mazoezi, sisi kama menejimenti tumejipanga kuhakikisha yote yanaenda sawa,”amesema Dk. Msolla. Hadi sasa Yanga SC tayari imekwishasajili wachezaji wapya 10, ambao ni beki Ally Ally kutoka KMC ya Kinondoni, viungo wa ulinzi, Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar, Mapinduzi Balama kutoka Alliance FC ya Mwanza, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana, Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia. Kwa upande mwingine, Dk. Msolla amewapa siku nne wote wanaotumia nembo ya klabu kwa ajili ya utengenezaji wa jezi na vifaa mbalimbali kuacha mara moja. Dk. Msolla amesema kwamba baada ya Juni 30 mtu yeyote atakayejihusisha na uuzaji wa jezi feki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake. Mwenyekiti amesema kwamba lengo la kuwaita watu hao wanaojihusisha na uuzaji wa jezi ni kufanya nao mazungumzo ni kujua ni namna gani wanaweza kusaidiana kwenye suala hilo la mauzo ya jezi na vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu.
michezo
Na Ramadhan Hassan -Dodoma RATIBA ya vikao vya Bunge la 11 imebadilika kwa mara nyingine tena, na sasa Rais Dk. John Magufuli atavunja Bunge Juni 16 badala ya 19 kama ilivyokuwa imetangazwa awali. Awali ratiba ya mwisho kutolewa na Bunge kabla ya hii ya jana, ilionyesha Rais Dk. Magufuli angevunja Bunge Juni 19. Ratiba hiyo imebadilika mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona. Kwa mujibu wa ratiba ya sasa, vikao vitafanyika kuanzia saa tatu asubuhi badala ya saa nane jioni na vitafanyika pia siku ya Jumamosi. Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, ilionyesha pia hotuba ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2020-2021 inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango leo saa 10 jioni huku asubuhi ikiwasilishwa taarifa ya hali ya uchumi. Kesho na keshokutwa kutakuwa na mjadala kuhusu hali ya uchumi na bajeti kuu na Juni 15 Bunge litahitimisha mjadala huo ikiwa ni pamoja na kupiga kura. Ratiba ya awali ilionyesha Bajeti Kuu ya Serikali na hali ya uchumi ingewasilishwa leo na kujadiliwa na wabunge kwa siku tatu na kisha kuhitimishwa Juni 17. Pia Juni 15 utawasilishwa muswada wa Sheria ya Fedha  za Matumizi wa mwaka 2020 (The Appropriation Bill 2020 – hatua zote) na muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill 2020 – kusomwa mara ya pili, kamati ya Bunge zima na kusomwa mara ya tatu). Siku hiyo pia kutakuwa na Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni kuhusu marekebisho ya kanuni za Bunge na Waziri Mkuu anatarajia kuwasilisha hotuba yake. Taarifa hiyo ilionyesha Juni 16 Rais Dk. Magufuli anatarajiwa kulifunga Bunge.  MABADILIKO Hivi karibuni Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema bajeti kuu ya Serikali itasomwa leo badala ya Mei 20 kama ilivyokuwa inaonyesha awali. Ratiba nyingine ambayo ilitoka na kubadilishwa ilionyesha bajeti ingewasilishwa bungeni Mei 20, saa 10 jioni na Rais Magufuli alitarajiwa kufunga Bunge Mei 29.
kitaifa
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona. Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano, alisema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo. Lakini amesema ”hatua kali zilizo na umuhimu” hazitaihusisha Uingereza, ambayo ina visa 460 vya virusi vilivyothibitishwa. Kuna visa 1,135 vilivyothibitishwa nchini Marekani na watu 38 wameripotiwa kupoteza maisha. ”Kuzuia visa vipya kuingia Marekani, tutaahirisha safari zote kutoka Ulaya,” Trump alieleza. ”Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa siku ya Ijumaa”. Aliongeza. Trump amesema Umoja wa Ulaya umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo zilizoanzishwa na Marekani. Alizungumza saa kadhaa baada ya Italia nchi iliyoathirika zaidi baada ya China kutangaza kuchukua hatua kali. Hatua hizo ni pamoja na kufunga maduka yote isipokuwa yanayouza vyakula na dawa kama sehemu ya kujitenga. Trump amesema kuahirishwa kwa safari pia kutahusu biashara na usafirishaji wa mizigo kutoka Ulaya kuingia Marekani. Pia ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi. HALI ILIVYO MAREKANI Maofisa wamesema hatari ya maambukizi ilikuwa chini, lakini hali ilibadilika baada ya ongezeko la idadi ya visa vipya vya maambukizi vilivyothibitishwa mwanzoni mwa mwezi Machi. Jitihada za kudhibiti zimeanza. Vikosi vimepelekwa kwenye mji wa New Rochelle, ulio kaskazini mwa New York, ambapo mlipuko huo unaaminika kuanzia huko. Vikosi vya ulinzi vitatoa chakula kwa baadhi ya watu ambao wametakiwa kujiweka karantini. Gavana wa jimbo la Washington amepiga marufuku mikusanyiko katika kaunti kadhaa. Jimbo lililo Kaskazini Magharibi ni kiini cha maambukizi nchini Marekani, kukiwa na idadi ya vifo 24 kati ya 38 nchi nzima. Mkuu Shirika la Afya Duninai (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyes ametangaza mlipuko wa Corona kuwa janga la kimataifa Shirika la Afya duniani limeutangaza mlipuko wa virusi vya corona kuwa ni janga la kimataifa, huku mlipuko huo ukiendelea kusambaa katika mataifa mbalimbali duniani. Ghebreyesus amesema kuwa idadi ya visa nje ya China vimeongezeka mara 13 kwa kipindi cha majuma mawili yaliyopita. Amesema kuwa ana hofu kubwa kutokana na viwango vya maambukizi ya virusi. Janga ni ugonjwa ambao unasambaa katika nchi nyingi kote duniani kwa wakati mmoja. ITALIA Waziri Mkuu, Giuseppe Conte alitangaza ongezeko la masharti ya kujiweka karantini kuongezeka. Alisema maduka mengi, migahawa, saluni, vitafungwa hadi Machi 25. Italia ina watu 12,000 waliothibitika kuambukizwa na idadi ya waliopoteza maisha ni 827. Karibu watu 900 wenye maambukizi wako kwenye hali mbaya, WHO imesema. Wakati huo huo Saudi Arabia imesitisha kwa muda usafiri wa raia wake na wakaazi wengine na kuzuia safari za ndege kwenda katika mataifa kadhaa kutokana na hofu ya virusi vya Corona. Shirika la habari la nchi hiyo SPA lilisema jana na kutaja chanzo rasmi katika wizara ya mambo ya ndani. Uamuzi huo unajumuisha mataifa ya Umoja wa Ulaya, Uswisi, India, Pakistan, Sri Lanka, Ufilipino, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini Eritrea, Kenya, Djibouti na Somalia, chanzo hicho kimeongeza, kikisema Uingereza pia imesitisha kuingia nchini humo kwa wale watu wanakuja kutoka nchi hizo. Saudi Arabia pia imesitisha kwa muda usafiri wa abiria na pia kwa njia ya barabara na Jordan, wakati usafirishaji wa mizigo na biashara vinaruhusiwa bado, na usafirishaji wa abiria wenye uhitaji maalum wa kiutu.
kimataifa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewaagiza maofi sa elimu wa mikoa kuhakikisha wanazipitia shule zote za serikali ili kubaini walimu wakuu wa shule za sekondari ambao wamedumu kwenye nyadhifa hizo kwa zaidi ya miaka mitano hadi kumi na hazijafaulisha wanafunzi kwa kiwango cha juu.Baada ya kufanya uhakiki huo wanapaswa kuchukua hatua za kuwabadilisha madaraka yao na kuwapangia majukumu mengine kwenye shule zao na nafasi zao wapewe walimu wenye uwezo wa kuleta mapinduzi katika elimu kwenye shule hizo.Jafo ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa shule ya Sekondari ya Mji Mpya iliyopo Manispaa ya Morogoro, ambayo imejengwa upya mara baada ya majengo yake ya awali kubomolewa ili kupisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) huku ujenzi wake ukigharimu kiasi cha Sh bilioni 1.4.Alisema serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa elimu ikiwa na utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha nne na kukarabati upya shule kongwe zikiwemo na za mkoa wa Morogoro.Pia Serikali imekuwa ikijenga shule ikiwemo ya sekondari ya Mji Mpya ambayo majengo yake yana ubora unaostahili sambamba na kutoa posho ya Sh 200,000 kwa walimu wakuu ili kuwawezesha kusimamia vyema uendeshaji wa shule zao.Waziri Jafo alisema kutokana na uwezeshaji huo mkubwa haoni sababu ya shule ambazo pia zina walimu wa kutosha kushindwa kufaulisha wanafunzi wake kwa ngazi ya madaraja ya juu.“Mkuu wa shule ana miaka 10 hadi 15 lakini shule yake hakuna daraja la kwanza , la pili wala la tatu bali ni daraja la nne na ziro nyingi ...na wapo walimu wenye uwezo mzuri , maarifa ya kufanya mapinduzi makubwa katika shule zao hawa sasa wapewe nafasi,” amesema Jafo.Mbali na walimu , aliwataka wanafunzi nao kuzingatia masomo wakiwa shuleni kwani baadhi yao wanadiriki kushiriki katika vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kielimu na hivyo kusababisha washindwe kufanya vizuri kwenye masomo hayo.Kwa upande wa utunzaji wa miundombinu ya shule, Waziri Jafo aliwataka wanafunzi wanaosoma shule za serikali kutunza miundombinu ya shule kwani hakuna mwanafunzi atakayevumiliwa endapo ataharibu miundombinu ya shule kwa makusudi .Waziri Jafo pia aliwasihi wazazi na walezi kuwa ni vyema kuwakanya watoto wao kuwa wamechagulia shule kwa ajili ya kusoma na kutunza miundombinu hiyo ili hata wao wakiondoka wanaaokuja shuleni waweze kusoma .Mbali na hayo , Waziri Jafo aliahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na viongozi wa mkoa wa Morogoro hasa kwenye kata ya Lukobe eneo ambalo shule hiyo ipo , Mkundi na Kihonda zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya barabara, kukosekana kwa zahanati na huduma ya maji.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare akimkaribisha Waziri Jafo alisema ataendelea kusimamia kikamilifu shule zote za Mkoa huo ili kuinua kiwango cha ufaulu.Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini (CCM) , Abdulaziz Abood alisema ataendelea kuunga mkono jitihada za kuinua kiwango cha taaluma katika mkoa huo na kuahidi kutoa zawadi ya Sh milioni 10 kwa shule yoyote ya msingi au sekondari itakayoingia katika kumi bora katika matokeo ya mtihani wa kitaifa.Awali , akisoma risala kwa Waziri Jafo , Ofisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro Dk Janeth Balongo aliomba serikali kutatua changamoto zinazoikabili shule ya Sekondari Mji Mpya ikiwemo kukosekana kwa maji, jengo la chakula, jiko, upungufu wa vyumba vya madarasa, uzio wa kuzunguka shule hiyo na kuiomba shule hiyo iwe ya kidato cha tano na sita.
kitaifa
CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeshika nafasi ya 13 kati ya vyuo vikuu huria 102 kwa ubora duniani na kwa Afrika kimeshika nafasi ya pili. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo chuoni hapo juzi.Profesa Bisanda alisema Februari, mwaka huu ilitolewa taarifa ya ubora wa vyuo vikuu huria duniani ambapo vipo vyuo vikuu huria 102 kati ya hivyo, OUT imeshika nafasi hiyo ya 13 kwa ubora. Aliongeza kuwa katika Afrika vyuo vikuu huria vipo tisa, chuo hicho nchini kimeshika nafasi ya pili kwa ubora na Chuo Kikuu Huria Afrika Kusini ndicho kilichoshika nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa Profesa Bisanda, katika vyuo vyote 49 vilivyopo nchini, OUT ni namba sita kwa ubora.Kwa upande mwingine alielezea changamoto iliyopo katika chuo hicho kuwa ni Jumuiya ya Watanzania kutoelewa vizuri mfumo wa elimu masafa, wakifikiria kuwa ni elimu ya chini na hafifu. Alisema katika chuo hicho wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa kwa kuwa hawafundishwi darasani lakini wanapewa maeneo yote ya kusoma ili wayapitie waweze kufanya vizuri katika mitihani yao. “Mtihani unatungwa kulingana na mtaala. Na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapa hauwezi kulinganishwa na vyuo vingine kwa kuwa mwanafunzi anasoma katika wigo mpana,” alisema.Alisema hata wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Sita hawaelewi ubora wa elimu unaotolewa na chuo hicho, hivyo wamekuwa wakifanya kampeni shuleni kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi hao kujiunga na OUT. Mwaka jana chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 8,000 lakini sasa wamefikia wanafunzi 12,994 na kabla ya kuondolewa kozi ya foundation mara ya kwanza na hatimaye kurudishwa chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 16,000.
kitaifa
WAMILIKI wa Mabenki nchini (TBA) wametekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuwataka kutoa mikopo kwa wanunuzi wa pamba nchini.Majaliwa alitoa wito huo mwishoni mwa wiki mwishoni mwa wiki alipozungumza na wakuu wa mikoa inayolima pamba ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita, Tabora na Singida pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmaji Nsekela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabenki (TBA). Majaliwa alisema mikopo hiyo itawasaidia wanunuzi wa pamba katika kukamilisha taratibu za kununua zao hilo kutoka kwa wakulima. Akizungumza na gazeti hili jana, Nsekela alisema agizo hilo la Waziri Mkuu limeshaanza kutekelezwa katika mikoa yote inayolimwa pamba hapa nchini. Nsekala alisema japo mikopo hiyo ilikuwa ikitolewa tangu zamani, lakini kauli ya Waziri Mkuu imeongeza msisitizo kwa mabenki kuhakikisha yanatoa huduma hiyo kwa wanunuzi kwa haraka. Alisema mabenki ambayo yalikuwa hayafanyi hivyo au yaliyokuwa yanasuasua katika hilo, ndiyo hasa yaliyokuwa yanalengwa. Majaliwa aliagiza kuwa ununuzi wa pamba utakapoanza kipaumbele kiende kwa pamba iliyokusanywa tayari ili isombwe na kutoa nafasi kwa pamba mpya kuendelea kununuliwa na kupelekwa kwenye maghala.
kitaifa
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrka, Azam FC imesema itahakikisha inautumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kupata mabao mengi kadiri wawezavyo ili yawasaidie kuwavusha katika hatua inayofuata. Azam FC leo Jumapili itawaalika Triangle United FC kwenye dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni kucheza mechi ya kwanza ya hatua ya kwanza kusaka nafasi ya kutinga hatua ya mtoano. Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Mtendaji Mkuu wa Azam , Abdulkarim Nurdin ‘Popat’ alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakishindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kupata ushindi wa mabao machache na wakienda ugenini wanafungwa mabao mengi na kutolewa.Aliweka wazi kuwa msimu huu wanataka kukwepa mtego huo na wameona njia pekee ni kupata mabao mengi nyumbani ili mechi za ugenini zisiwe ngumu kwao. Aliongeza kuwa kikosi cha Azam kwasasa kimeongezeka makali baada ya wachezaji wao Mudathir Yahya pamoja na David Mwantika kuanza mazoezi baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua.“Tulishinda 2-0 hapa nyumbani dhidi ya Al Mareikh lakini tulipokwenda kwao tukafungwa 3-0 na kutolewa, pia Esparence walitutoa baada ya kuwafunga hapa nyumbani 2-1, kwao wakatufunga tatu, tumeona mabao machache hayatoshi hivyo angalau tupate matokeo ya kuanzia 3-0 na kuendelea,” alisema Popat.
michezo
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Charles Singili (pichani) ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Taasisi za Fedha za Maendeleo ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC -DFI) yenye jukumu la kuhamasisha na kuwezesha taasisi za fedha za ukanda huo kupata fedha na kuwekeza kwenye sekta zinazokuza uchumi.Akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam juzi, Singili alisema nafasi hiyo ni muhimu kwa nchi kwani imekuja wakati mzuri ambapo viongozi wa juu wa SADC kwa sasa wanatoka Tanzania akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Marais wa Jumuiya hiyo kwa sasa, ambaye ni Rais John Magufuli ambaye Agosti mwaka huu atakuwa mwenyekiti rasmi wa jumuiya hiyo. Singili alisema nafasi aliyoteuliwa ni ya kipindi cha miaka miwili na kwamba katika uteuzi huo, TIB itahamasisha ushiriki wa hali ya juu wa taasisi za fedha nchini katika ukanda wa SADC ili kupata fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta za kukuza uchumi.“Tunashukuru kwa kupata nafasi hii imekuwa wakati mzuri ambapo hata viongozi wa juu wa SADC kwa sasa Tanzania inaongoza, tunapokea majukumu haya na tunaahidi kufanya kazi ili iwe chachu ya maendeleo katika ukanda huu nan chi yetu ifaidike pia,” alisema Singili. Alisema moja ya majukumu ya SADC DFI ni kushiriki kwenye miradi na kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye ukanda huo kwa kusaidiana na taasisi wahachama ili kusiwezesha kutekeleza wajukumu yao. Alisema kwa uteuzi huo Tanzania ina nafasi ya kipekee katika ukanda wa Sadc kutukana na nafasi yake kijiografia na pia uwepo wa maliasili nyingi kama vile madini, maji mimea na wanyama pori.Aidha alisema benki hiyo itashirikiana na benki nyingine na serikali kwa kujenga mazingira wezeshi ili nchi iwe mwenyeji wa mfuko wa Sadc wa kuandaa miradi ambao utatoa kipaumbele kwa miraid ya Tanzania kupata fedha . Katika hatua nyingine, benki hiyo imeorodheshwa katika jedwali la heshima la Afrika miongoni mwa taasisi bora za fedha za maendeleo zinazofanya vizuri katika eneo la utawala bora na makundi ya uendeshaji. Akizungumzia hilo Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Singili alisema Katibu Mkuu wa Chama cha Taasisi za fedha na Maendeleo ya Afrika (AADFI) alitaja benki hiyo kuwa bora kwa kupata asilimia 80 katika tamko lililotangazwa hivi karibuni. Alisema vigezo mbalimbali vimetumika kupata taasisi bora ikiwemo kuchunguza jinsi wanavyozingatia kanuni za utawala bora.
kitaifa