content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
NEW YORK, MAREKANI GAZETI la New York Times la hapa limeripoti kuwa China, imewaua au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 na 20 wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita na kudhoofisha kabisa shughuli za kulichunguza taifa hilo kubwa la Asia. Gazeti hilo liliwakariri maofisa 10 wa zamani na sasa wa Marekani, ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa wakati wakilaani kitendo cha karibuni cha kuvujisha siri za kijasusi kwa Urusi kilichofanywa na Rais Donald Trump. Walisema kitendo hicho ni ukiukaji mbaya wa kiusalama zaidi kipindi cha miongo kadhaa. Walikumbushia vitendo kama hivyo vya uvujishaji siri vilivyoangamiza maisha ya majasusi na watoa habari wa Marekani nchini China, hali iliyopelekea kusambaratika kwa mtandao wake nchini humo. Baadhi ya maofisa hao wanasema wanadhani China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambao hutumiwa katika mazungumzo ya siri. Lakini wengine wanaoamini kulikuwa na mdukuzi ndani ya CIA aliyesambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani mwaka 2010. Ripoti ya gazeti hilo na Associated Press inasema idadi ya mali za CIA zilizopotea nchini China haitofautiani na zile zilizopotea wakati wa uliokuwa Umoja wa Kisovieti (USSR) na Urusi kutokana na usaliti uliofanywa na afisa wa CIA Aldrich Ames na kachero wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI), Robert Hanssen, ambao walikamatwa mwaka 1994 na 2001. Majasusi wa CIA nchini China walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine kuanzia mwanzoni mwa 2011 huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kupumzikia katika jengo la serikali mjini Beijing. Hata hivyo, CIA imekataa kuzungumzia suala hilo.
kimataifa
NA JESSCA NANGAWE MKURUGENZI wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, amesema moja ya vitu vinavyopoteza mwelekeo wa bendi hiyo kwenye muziki wa dansi ni pamoja na muda wa kufanya matamasha kuwa mdogo. Akizungumza na MTANZANIA jana, Asha alisema kitendo cha matamasha kufanyika mwisho saa 6 usiku, imekuwa moja ya changamoto kubwa inayowarudisha nyuma kwani wamekuwa wakikosa mashabiki, hivyo wanaiomba Serikali kuliangalia hilo. Alisema tayari wamekutana katika vikao mbalimbali na kuandika barua kwa waziri mwenye dhamana ya sanaa wakimwomba kusogezwa muda angalau wa saa mbili au tatu mbele, badala ya saa sita iwe saa nane au saa tisa. “Tulikutana na kuamua kuiomba Serikali iingilie kati suala hili kwa kuwa linatuumiza sisi kama wahusika, muda tulioomba umekwisha na tunachoangalia ni kuvuta subira na ikifika mwezi wa nne tutafanya jitihada za kumuona rais,” alisema kiongozi huyo. Alisema moja ya mambo waliyoomba wapewe kipaumbele ni pamoja na kupewa siku mbili kwa wiki kuweza kufanya matamasha yao, huku wakiamini hayataleta madhara kwao wala kuvunja sheria za nchi. Aliongeza pia wameandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuutangaza muziki huo ikiwemo kufanya ziara katika vyombo vya habari ambavyo ndivyo vyenye nafasi kubwa ya kurudisha heshima yao kama awali.
burudani
KULWA MZEE-DAR ES SALAAM WATUHUMIWA wanaosakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji  ‘Mo’ hawajapatikana na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Hayo yalibainishwa jana na Wakili wa Serikali, Daisy Makakala wakati kesi hiyo inatajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Makakala alidai upelelezi wa kesi hiyo unaendelea, hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa. Alidai wanaendelea kuwatafuta washtakiwa wengine ili waunganishwe katika kesi hiyo, ambapo imepangwa kutajwa  Oktoba 15. Mshtakiwa ambaye ameshafikishwa mahakamani hapo ni dereva wa teksi, mkazi wa Tegeta, Mousa Twaleb. Watuhumiwa wengine ambao upande wa mashtaka unawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wanaodaiwa kumteka mfanyabiashara huyo. Washtakiwa hao ni Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji. Katika kesi hiyo, inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, mwaka jana, katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Johannesburg nchini Afrika Kusini, kwa makusudi washtakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu. Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo Hoteli ya Colloseum wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara Mo kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari. Inadaiwa Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha Sh 8,000,000 wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga. Mo alitekwa nyara Oktoba 11, mwaka jana alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi, na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.
kitaifa
NAIROBI, KENYA GAVANA wa Kaunti ya Nyeri nchini Kenya, Wahome Gakuru, amefariki mapema jana baada ya kupata ajali barabarani katika eneo la Kabati, barabara kuu ya Thika-Sagana, Kaunti ya Murang’a. Alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura, lakini akaaga dunia. Kamishna wa Kaunti ya Murang’a, John Elungata, alithibitisha kifo hicho na kusema Kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila inaponyesha mvua. Maofisa wa polisi walisema kuwa gari la gavana huyo lilikuwa na abiria wanne wakati wa ajali hiyo ,akiwamo msaidizi wake binafsi, dereva na mlinzi wake. Mkono na mguu wa msaidizi wake binafsi ilivunjika, huku miguu ya mlinzi wake ikipata majeraha makubwa na dereva akielezwa yu katika hali nzuri. Mapema siku ya Jumatatu alipiga picha na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Alliance Boys wanaofanya mtihani wa kidato cha nne.                                                                                                                    Polisi walisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumu moja la gari hilo kupasuka wakati mvua kubwa ikinyesha. Mwili wa gavana huyo umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee jijini Nairobi. Inadaiwa kuwa gavana huyo alikuwa akielekea kuhudhuria kipindi kimoja cha redio na runinga wakati gari lake lilipokumbwa na ajali hiyo. Dk. Gakuru ni gavana wa pili wa Nyeri kufariki dunia akiwa madarakani baada ya Nderitu Gachagua kufariki Februari, mwaka huu.
kimataifa
SERIKALI imeanza kugawa ekari 972,500 za ardhi kwa wafugaji wanaotangatanga kutafuta malisho ya mifugo ili kumaliza kabisa migogoro baina yao na wakulima iliyodumu kwa miaka mingi na kusababisha uvunjifu wa amani.Pia wafugaji wengi walipata hasara kwa mifugo yao kutaifishwa, kutozwa faini na hata mingine mingi kufa kutokana na kukamatwa kisha kushikiliwa kwa muda mrefu bila huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu kwenye hifadhi mbalimbali za taifa nchini.Akizindua ugawaji wa ardhi hizo kwa wafugaji nchini katika Ranchi ya Kalambo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema uamuzi huo wa serikali umekuja kutokana na wafugaji wengi nchini kuhangaika kila mahali kutafuta malisho na kusababisha migogoro mingi baina yao na wakulima. Hivyo kwa upande wa Ranchi ya Kalambo, wafugaji wamegawiwa ekari 25,000 zenye uwezo wa kuhifadhi mifugo 6,000, na hadi sasa jumla ya ng’ombe 3,000 wameshaingia kwenye ranchi hiyo wakati serikali na wafugaji wenyewe wakiendelea kutafuta suluhisho la kudumu la kupata malisho.Waziri Mpina amewataka wafugaji wanaohangaika kutafuta malisho kutumia fursa hiyo ya serikali ya uwepo wa maeneo ya kulishia mifugo ili wawe karibu na huduma za tiba na chanjo pindi mifugo yao inapopata maradhi.Aidha, aliipongeza kamati maalumu aliyoiunda ya kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi kwa kufanikisha upimaji na ugawaji wa ardhi hiyo kwa wafugaji pamoja na kutatua migogoro yote iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.Pia alimwagiza Katibu Mkuu Mifugo kuhakikisha ukarabati wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya wanyama cha Kanda ya Kusini Magharibi kinakamilika ifikapo Februari mwakani ili mikoa ya Katavi na Rukwa kutokuwa na kituo hicho licha ya kuwepo mifugo mingi.Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Halfan Haule alisema kutokuwepo kwa maeneo ya malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo kumekuwepo na migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na kumshukuru waziri kwa uamuzi wa kugawa vitalu kwa wafugaji.Pia alisema Mkoa wa Rukwa umekuwa ukikabiliwa na magonjwa ya mifugo ikiwemo homa ya nguruwe (ASF), Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Homa ya mapafu ya mbuzi (CCPP), Ugonjwa wa miguu na midomo (FMD), Ugonjwa wa mapele ngozi (LSD), Ugonjwa wa kichaa cha mbwa na ugonjwa wa mdondo (ND).Katibu wa Umoja wa Wafugaji Ranchi ya Kalambo, Benuel Benzeth aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, kwa uamuzi wake wa kugawa maeneo hayo ya serikali kwa wafugaji katika kipindi ambacho wanaendelea kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto ya malisho.Benzeth alisema mifugo yao mingi imekufa na mingine kudhoofika kutokana na kukamatwa na kushikiliwa kwenye hifadhi bila matunzo na wakati wote serikali haijawahi kuchukua hatua za kuwasaidia wafugaji na kumshukuru waziri kwa uamuzi huo ambao umewezesha mifugo mingi kupona na kuendelea na uzalishaji.Awali akizungumza baada ya kutembelea Kiwanda cha Nyama cha SAAFI mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Waziri Mpina alisema serikali inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi haraka ili kusaidia upatikanaji wa mifugo takribani milioni sita iliyoko Rukwa, Katavi, Songwe na Mbeya.
kitaifa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa maombi ya Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera ya kutaka kwenda kushiriki Ibada ya kumuaga mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi aliyefariki dunia Desemba 31, 2019.Kabendera ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka ya utakatishaji fedha, alionekana kujifuta machozi huku ndugu zake ambao walifurika mahakamani,walionekana wenye majonzi kutokana na kifo cha mama huyo.Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi yoyote juu ya kesi hiyo ya uhujumu uchumi, isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).Hakimu Mtega pia alisema hakuna fursa ya waombaji kukata rufaa katika uamuzi huo. Hatua ya kukataliwa kwa maombi ya Kabendera, imekuja baada ya Wakili wake, Jebra Kambole kuiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki ibada ya kumuaga mama yake mzazi katika Kanisa Katoliki Chang’ombe, inayofanyika leo majira ya mchana kabla ya kusafirishwa kwa mwili huo kuelekea Bukoba mkoani Kagera kwa maziko.Kambole alidai kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya binadamu na ni suala la faragha. Alidai kushindwa kwake kuhudhuria maziko ya mama yake, watakuwa wamemuadhibu adhabu kubwa kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza, hivyo ni vizuri akatoa heshima ya mwisho. Pia alidai ni muhimu kwa Kabendera, kushiriki ibada hiyo kwa sababu mama mzazi ni mmoja na kwamba anapokufa anaagwa mara moja.“Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho,”alidai Kambole.Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alimpa pole Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi na kwamba mahakama isifungwe mikono, kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba huo.Simon alidai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake, yamewasilishwa wakati ambao si sahihi, kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia DPP hajaipa mahakama hiyo kibali cha kusikiliza kesi hiyo.“Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa, lakini mahakama isifungwe mikono,” alidai Simon.Awali, kabla ya maombi hayo, Wakili Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na shauri limefika hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na DPP. Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu, likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.Katika mashitaka ya kwanza, ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu, kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida. Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho bila ya sababu, alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
kitaifa
WABUNGE wamesisitiza haja ya serikali kuboresha huduma za matibabu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kulinda maisha ya Watanzania hususani wa vijijini na wasio na uwezo.Kwa nyakati tofauti, wakichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kujenga miundombinu ya sekta ya afya ameonesha kuwa mazo zaidi utolewe kwenye kuboresha matibabu katika sehemu za kutolea huduma za afya. Baadaye jana wabunge walipitisha bajeti hiyo ya Wizara ya Afya.Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) amesema katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa ipasavyo kwa wananchi ni vyema serikali kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.“Utaratibu kushirikisha serikali na watu binafsi utaratibu muhimu ambao unapaswa kuendelea kwa mapana yake. Pia tunapoboresha hospitali za serikali tusisahau umuhimu wa kuhakikisha kwamba zile ambazo tulikuwa nazo tunalinda uwezo wake kwa sababu tusije ikawa kama ule msemo wa ‘tusiwibie Paulo kumlipa Petro.’“Sina budi kusema kwamba hospitali siyo majengo ila ni huduma na katika hili, waziri pia aangalie hali halisi ya hospitali za Referal (rufaa), napongeza juhudi za serikali ya awamu ya nne iliyokamilisha Hospitali ya Mloganzila lakini hospitali hiyo ni hospitali majengo kwani hakuna hospital town pale kwa ajili ya madaktari kukaa karibu na hospitali,” aliongeza Profesa Tibaijuka.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) aliwapongeza wauguzi na madaktari kwa kazi nzuri wanazofanya nchi nzima na kuomba wizara kusaidiana na Tamisemi kuwezesha hospitali ya wilaya ili kupunguza mzigo wa wagonjwa.
kitaifa
Juhudi za kocha Ole Gunnar Solskjaer kuimarisha kikosi chake huenda zikagonga mwamba kwa sababu Manchester United ni klabu ambayo hutoa ofa ya chini kwa wachezaji wanaotaka kuwasajili. (Evening Standard) Solskjaer anataka kumuuza kiungo wa kati wa Man Utd Mfaransa Paul Pogba, 26, bada ya kufahamishwa kuwa ana pauni milioni 100 ya kuwasajili wachezaji wapya msimu huu. (Star) Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, hana mpango wa kuchezea tena Paris St-Germain. (Sport – in Spanish) Real Madrid wameweka dau la euro milioni 130 kumnunua Neymar, kutoka PSG, mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, au mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27. (Mundo Deportivo – in Spanish) Atletico Madrid wanakaribia kukamilisha sajili wa Joao Felix wa Benfica kwa kima cha euro milioni 120 sawa na (£106.7m) hii ina maanisha Manchester United watamkosa kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliye na umri wa miaka 19. (Evening Standard) Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Rodri, ameamua kujiunga na Man City badala ya Bayern Munich na kuhamia City kawa malipo ua £62m. (Kicker – in German) Manchester City wanapigiwa upatu kuipiku Man Utd katika usajili wa Harry Maguire, 26, kutoka Leicester kwa kima cha pauni milioni 65 baada ya kiungo huyo wa England kupita vipimo vya matibabu. (Star) Man City wanatafakari uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa bure Asier Riesgo wa ibar na kumfanya Mhispania huyo wa miaka 35 kuwa kipa wao wa tatu. (Manchester Evening News) Everton wameanza maungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa Kurt Zouma kwa mkataba wa kudumu baada ya mlinzi huyo wa Ufaransa, 24, kucheza Goodison Park msimu uliopita kwa mkopo katika. (Telegraph) Tottenham wamefanya mazungumzo na ajenti wa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, kuhusu uhamisho wake kutoka Sporting Lisbon. (Telegraph) Juventus wana matumaini ya kufukia mkataba wa kumsaini Adrien Rabiot kutoka Paris St-Germain, huku mkataba wa mchezaji huyo raia wa Ufaransa anaechezea safu ya kati ukitarajiwa kukamilika msimu huu wa joto. (Goal) Liverpool hawana mpango wa kumuuza Divock Origi msimu huu wa joto licha ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mweye umri wa miaka 24 kusalia na mkataba wa mwaka mmoja. (Liverpool Echo) Tetesi Bora Alhamisi Chelsea inapania kumuajiri kocha wa Derby Frank Lampard, kama maneja wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu kufikia mwisho wa wiki hii. (Standard) Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kusajili beki wa England anaechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail) Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror) Ajenti wa Gareth Bale amepuuziliambali madai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid wa miaka 29 huenda akahamia Bayern Munich kwa mkopo. (Mirror) Arsenal wanajianda kuweka dau la kumnunua winga wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai, 18. (Football Insider) Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley. Kipa huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 33 ataingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa katika uwanja waTurf Moor mwezi ujao. (Guardian  
michezo
Na AGATHA CHARLES – DAR ES SALAAM KAMPENI za uchaguzi mdogo wa udiwani zinazoendelea katika kata 43 nchini, zimegeuzwa kuwa majukwaa ya mikutano ya vyama vya siasa iliyokosekana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa baada ya kuzuiwa. Wanasiasa kutoka vyama vyote vyenye wagombea katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, wamekuwa wakitumia muda mrefu katika kampeni hizo ‘kutema nyongo’, wakizungumza hoja zinazohusu mwelekeo wa nchi, hali ya siasa ilivyo na kukosoa baadhi ya mambo, huku muda kidogo ukitumika kunadi wagombea. Vyama vyenye wagombea katika uchaguzi huo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo. Hali hiyo inatokea baada ya Juni, mwaka jana Rais Dk. John Magufuli kupiga marufuku vyama vya siasa kufanya ushindani wa kisiasa katika mikutano ya hadhara hadi mwaka 2020. Marufuku hiyo ya Rais Magufuli, ilikaziwa Novemba, mwaka jana na Jeshi la Polisi baada ya kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Kutokana na sababu hiyo, makada, wanachama na wafuasi wa vyama vyenye wagombea, wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo ya kampeni, kuwasikiliza viongozi wao baada ya kutowaona kwa muda katika majukwaa ya mikutano ya hadhara. Katika mikutano mbalimbali ambayo viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, wakiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, walienda kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wao wa nafasi za udiwani, pia walitumia majukwaa hayo kuzungumzia masuala mbalimbali ya nchi. EDWARD LOWASSA Akiwa Kata ya Moita jijini Arusha, Lowassa, alikumbusha mjadala wa Katiba mpya kwa kumwomba Magufuli kusikiliza maoni ya watu. Katika hoja hiyo, Lowassa alisema nchi itakwenda vyema iwapo itakuwa na Katiba bora kama ya Kenya inayoruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani. Pia Lowassa alisema hakuna chama kinachotawala peke yake duniani kwa sasa na nchi ina shida ya kitu alichokiita ‘coalition’, yaani muungano wa vyama. Akitoa mfano huku akirejea matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, Lowassa aliyepata kura milioni sita na kushika nafasi ya pili nyuma ya Magufuli, alisema kwa nchi nyingine, mwenye kura hizo anapata nafasi ya kuchangia wabunge, huku akitolea mfano Ufaransa kuwa ni nchi ya kibepari, lakini inaongozwa na ujamaa kutokana na aina ya wabunge iliyonao. Alisema ni bora Katiba ikafuatwa kwa sababu katika muungano, vyama vya siasa ni vingi na ukifika wakati wa uchaguzi, vinatumika vibaya. Pia alinukuliwa akisema kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Chadema lazima ichukue nchi. FREEMAN MBOWE Wakati Lowassa akizungumzia hayo, Mbowe, aliyeanzia Kimara Suka, Dar es Salaam katika Kata ya Saranga, aliomba wanaohamia Chadema kuacha kuambiwa kuwa ni mafisadi na badala yake kama ni kweli wahusika wawafikishe mahakamani kwa hatua zaidi. Pia Mbowe alizungumzia hatua ya kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa na kudai kuwa si sahihi na Chadema itaendelea kupigania haki hiyo na ikiwezekana kuna siku wataingia barabarani kuandamana. Katika hatua nyingine, akiwa Mtwara, Mbowe alizungumzia zaidi namna aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, walivyojiengua katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi. Pia hakuacha kugusia mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya kuwa uko pale pale, huku akirejea maneno aliyosema kuwa yalipatwa kuzungumzwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuwa kwa Katiba iliyopo mtawala akiamua kuwa dikteta anaweza kutokana na madaraka makubwa ya rais. MWIGULU NCHEMBA Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Mwigulu Nchemba, akiwa katika Kata ya Saranga, Dar es Salaam, aliwashangaa wanaodai kuna utawala wa kidikteta nchini na alisema watu hao wameshindwa kutofautisha dhana hiyo na utawala wa sheria. Katika hoja hiyo, Mwigulu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema Magufuli anajali zaidi utawala wa sheria na ndiyo sababu aliamua kuwa na mahakama ya mafisadi, huku akisimama kuwatetea wanyonge. Pia alitaka maneno ya wanasiasa wa upinzani kupuuzwa, huku akidai kuwa Magufuli analazimika kuwa mkali kutokana na uonevu dhidi ya wanyonge. TUME YA UCHAGUZI Kutokana na mwenendo na hoja za wanasiasa hao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilivionya vyama vya siasa kutogeuza kampeni za uchaguzi huo kuwa mikutano ya vyama vya siasa. Onyo hilo lilitolewa mwanzoni mwa wiki hii na na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage. Jaji Kaijage, alisema vyama vya siasa vinatakiwa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili na taratibu zilizoainishwa katika uchaguzi kupitia kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura ya 292. Pia alisema NEC ina mamlaka ya kuruhusu kampeni za uchaguzi kwa nia ya kushawishi watu na si mikutano ya vyama vya siasa.
kitaifa
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku makongamano ya wafugaji ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi aliochukua wa kuwasaidia, badala yake ametaka wafugaji watumie kipindi hicho kifupi kuainisha maeneo yaliyopoteza sifa za uhifadhi ili yachukuliwe kwa ajili ya malisho ya mifugo.Hivyo aliagiza wafugaji kote nchini kujipanga na kupendekeza maeneo yaliyopoteza sifa za uhifadhi, mashamba yasiyoendelezwa ili wafugaji wapatiwe kwa ajili ya malisho ya mifugo yao kama sehemu ya kuunga mkono uamuzi uliotolewa wa kusaidia sekta hiyo.Akizungumza katika mkutano wa kuwasikiliza wananchi waishio kando ya Hifadhi ya Pori la Akiba la Maswa wilayani Meatu mkoani Simiyu kwenye ziara ya Kamati ya mawaziri nane uliofanyika Mjini Mwandoya wilayani Meatu, alisema tangu mwaka 2000 tume zaidi ya 27 ziliundwa na Bunge na serikali kushughulikia migogoro zaidi ya 1,095.Hata hivyo, alieleza kuwa asilimia 99 ya mapendekezo ya tume hizo hayajatekelezwa hadi leo. Alisema tume nyingi zilizoundwa miaka ya nyuma kushughulikia migogoro hiyo zilichakachuliwa hata kabla ya kukabidhi matokeo ya mambo waliyobaini kwa kuwa kwenye migogoro hiyo wako baadhi ya viongozi wa serikali. Alisema baadhi ya watendaji wa serikali walilazimika hata kutoa rushwa ili kubadilisha maamuzi ya tume zilizokuwa zinaundwa kushughulikia migogoro hiyo kwa sababu wananufaika na migogoro hiyo.“Dk Magufuli akasema hapana nitaunda tume ambayo haitapokea rushwa timu ya Lukuvi mnaiona ina sura ya kupokea rushwa? Vichwa vya kina Mpina unaweza ukawapa nini wakakubali, akasema wananchi wangu watahangaika mpaka lini, watauana mpaka lini mifugo mingi imedhulumiwa kwa kivuli cha uhifadhi, na tume yenyewe ndio hii sasa ya mawaziri nane,” alisema Mpina.Mpina aliwahakikishia wananchi kuwa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi yatafika kwa Rais tofauti na tume zingine zilizotangulia zilikuwa hazina uwazi wa namna ya kuchukua maoni na namna ya kufikisha mapendekezo serikalini. Kutokana na hali hiyo aliagiza wafugaji wote nchini kutopoteza muda kwa kufanya makongamano na maandamano ya kumpongeza Rais kwa sasa kwani amewapa kazi wakulima, wafugaji, wavuvi kuangalia maeneo ambayo yamepoteza sifa yaweze kupendekezwa ili wafugaji wayapate.“Najua furaha yenu kwa uamuzi huu lakini kwa sasa sisi kama wafugaji tusipoteze muda wa makongamano na kumshangilia Rais wakati ametupa kazi kubwa ya kupendekeza maeneo hayo ili mwisho tuyapate, yafutwe tuweze kufanya shughuli kilimo, ufugaji,”alisema. Hivyo Waziri Mpina amekataa kuhudhuria makongamano ya vyama vya wafugaji ambao wamemualika kuhudhuria sherehe hizo na kuwataka kujipanga vizuri kupendekeza ili kuitumia vizuri nafasi ya pekee waliyopewa na Rais Magufuli.“Hakuna kiongozi mwingine yeyote katika historia ya Tanzania ambaye amekuwa na mtizamo wa kutatua kero za wananchi wake kama Rais, huyu historia itaandika ya Tanzania na hata ya dunia kwa mtazamo wake ambapo wananchi wengi wakitaka kupaza sauti zao wanazuiwa na watu wachache ambao walikuwa na masilahi katika mambo hayo sasa hayo yote yamefika mwisho,” alisisitiza Waziri Mpina. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Maalumu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliwahakikishia wananchi walioondolewa kupisha mita 500 warudi waendelee na shughuli zao kwani Rais Magufuli alishasitisha kuwaondoa wananchi hao.
kitaifa
Na KENNETH NGELESI-MBEYA SIKUKUU ya Mwaka Mpya imeanza kwa taharuki kwa wakazi wa Mtaa wa Soweto jijini Mbeya baada ya kuamka asubuhi na kukuta jeneza tupu likiwa limetelekezwa juu ya meza nje ya duka mtaani hapo. Hatua hiyo iliwafanya wananchi wa eneo hilo kuanza kuitana huku wengine wakipigana vikumbo kwenda kushuhudia tukio hilo la kufungua mwaka mpya, ambalo linanasibishwa na imani za kishirikina. Akizungumza na MTANZANIA jana jijini hapa, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Oscar Kilasi ambaye pia ni mfanyabiashara sokoni hapo, alisema kuwa alifika katika eneo hilo kufungua biashara mapema, lakini alipofika alijikuta akipigwa na butwaa baada ya kukuta jeneza lililotumika katika eneo hilo. Alisema jeneza hilo lilikuwa limetelekezwa mbele ya duka lake, jambo ambalo lilimfanya ashangae na akalazimika kuwaita walinzi wa soko na kuanza kuwauliza kuhusu masahibu hayo. “Nilipoliona jeneza likiwa juu ya meza nilimwita mlinzi ambaye nilimwona akiondoka kuingia ndani ya soko, nikamweleza na ndipo umati wa watu nao ukaanza kusogea kushuhudia tukio hili,” alisema Kilasi. Naye mkazi wa Ilemi jijini hapa, Kefas Nkonde, alisema kuwa tukio hilo linatisha kwa vile si kitu cha kawaida jeneza kuonekana sokoni, na aliiomba Serikali ifanye uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. “Jeneza sio mzinga wa nyuki kwamba tutapenda kuungalia, bali ni kitu kinachoogopesha jamii, hivyo linapoonekana katika maeneo ambayo haikutarajiwa kuwepo ni vizuri Serikali ikafanya uchunguzi wa kina kujua kiini cha uwepo wake mahali hapa,” alisema Nkonde. Mwenyekiti wa Mtaa wa Soweto, Ramadhan Tavee, alisema kuwa tukio hilo limewashtua wananchi wa eneo hilo kwa kuwa si jambo la kawaida. Alisema kuwa baada ya kuona tukio hilo, aliamua kuwasiliana na viongozi wake wa juu katika ngazi ya kata kabla hajapiga simu polisi kuomba msaada wa ulinzi. “Nilipopata taarifa hii kama kiongozi nilifika mahali hapa mara moja kujiridhisha na niliona jeneza hili, niliwasiliana na viongozi wangu wa kata kisha nikapiga simu polisi na ninashukuru maana askari wamefika kwa wakati na kuhakikisha mtaa wangu unaendelea kuwa na amani na utulivu,” alisema Tavee. Mwenyekiti wa Soko la Soweto, Fred Mwaiyongano alisema kuwa baada ya kuliona jeneza hilo, aliamua kufuatilia kwa kina ili kujua limefikaje sokoni hapo kwa sababu sio tukio la kawaida. Alisema aliwasiliana na vijana wanaoshusha mizigo sokoni hapo ambao walimweleza kuwa jeneza hilo lilishushwa na gari aina ya Fuso lililokuwa limeleta nyanya likitokea Makambako mkoani Njombe. “Pia tulipowasiliana na wapakiaji wa mizigo huko Njombe walisema jeneza hilo lilisafirisha mwili wa marehemu kutoka Mbeya kwenda Makambako na lilitakiwa kurudishwa Mbeya na ndipo wakalipakia kwenye Fuso hilo ili walipeleke kwenye msikiti mmojawapo uliopo Soko Matola Mbeya, lakini dereva akaliacha sokoni badala ya kulifikisha alikoelekezwa,” alisema Mwaiyonga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu za jeneza hilo kutelekezwa sokoni hapo. Kamanda Matei alisema kuwa mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.
kitaifa
Alisema chini ya uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, hilo litawezekana na hasa kutokana na kuwapo kwa mizengwe katika zao la pamba nchini.Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Michezo wa Mwamapalala wilayani Itilima katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu juzi.Majaliwa alikiri kuwa bei ya pamba inabadilika kutokana na bei katika soko la dunia, ambako kuna wazalishaji mbalimbali, lakini kitakachookoa hali hiyo ni kuwapo kwa viwanda vya kusokota nyuzi nchini ambavyo vitasaidia kuongeza thamani ya zao hilo.“Bei ya pamba huwa inabadilika katika soko la dunia, hivyo kusababisha bei hiyo kuporomoka hadi hapa nchini. Huku kwenu kuna michezo michezo katika bei ya zao hilo,”alisema Waziri Mkuu na kuongeza. “Nitarudi kutoa mwongozo kuhusu suala hili, nimeagiza kuwapo kwa kikao cha watu wa Bodi ya Pamba. Kuna mizengwe mizengwe sana katika suala hili. Mazao ya pamba, korosho na kahawa yamekuwa hayaendeshwi vizuri. Tatizo ni mfumo. Ushirika unatuumiza zaidi,” alisema kwa msingi huo, njia pekee ya kupandisha bei ya pamba ni kwa kujenga viwanda vya kusokota nyuzi ambavyo vitafanya uzalishaji wa nguo ufanyike nchini hivyo kuuzabidhaa nje.Aliwaahidi wananchi wa Itilima, Simiyu na Tanzania kwa ujumla kuwa serikali italifanyia kazi suala hilo la bei ya pamba na kuja na ufumbuzi wa kudumu.Waziri Mkuu alilazimika kulitolea ufafanuzi suala hilo baada ya wabunge wawili wa Viti Maalumu, Esther Midimu (CCM) na Gimbi Masaba (Chadema), kueleza masikitiko yao kuhusu kuporomoka kwa bei ya pamba katika soko la ndani.Wakati akijinadi kuomba ridhaa ya Watanzania kumchagua kuwa Rais, Dk John Magufuli aliahidi kuwa Tanzania itakuwa nchi ya viwanda chini ya utawala wake, na hivyo kuipeleka katika nchi zenye uchumi wa kati.Aidha, Waziri Mkuu aliwaambia wananchi hao wa Itilima kuwa ahadi ya Rais Magufuli ya kujenga barabara ya lami kutoka Busega – Bariadi – Itilima – Meatu na kuunganishwa na wilaya ya Mkalama mkoani Singida iko na pale pale naitatekekezwa.
uchumi
RENATHA KIPAKA-BIHARAMULO NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka watumishi kufuata sheria taratibu za kazi ya umma kwa kutekeleza miongozo inayotolewa na Serikali. Alisema hayo jana wilayani Biharamulo mkoani Kagera, baada ya kupokea taarifa ya utumishi na utawala iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya, Saada Malunde. Dk. Mwanjelwa alisema katika utumishi, suala la sababu binafsi lenye kufanya kupeana madaraka ya kukaimu nafasi ambayo haina mhusika, ni kuvunja mioyo ya kazi kwa watumishi wengine. Alisema Serikali ilitoa waraka mwaka 2018 ambao unatamka juu ya nafasi ambazo hazina wakuu wa idara zinapaswa kukaimiwa ndani ya miezi sita, endapo kuna sababu ya kuendelea itolewe  taarifa. “Waraka ulitolewa tayari wenye kurasa nyingi, nafasi zote zisiwe zaidi ya miezi sita, endapo mnaona kuna sababu toeni taarifa, acheni kupendekezana, fanyeni uwajibikaji,” alisema Dk. Mwanjelwa. Alisema taarifa ya wilaya imeonyesha kuna watumishi wamekaimu nafasi zaidi ya mwaka mmoja kwenye idara ya ardhi, fedha, maendeleo ya jamii na afya bila kufanya uamuzi wowote. Dk. Mwanjelwa alisema kukaimu muda mrefu kunafanya mhusika wa nafasi ile kushindwa kuona ufanisi wa kazi yake juu ya ukaimishwaji nafasi ambayo amepangiwa na mwajiri wake. Alisema kufanya hivyo kunatokana na mazoea kazini, bila kutambua uwajibikaji. “Jamani awamu hii siyo ya mazoea, fanyeni uwajibikaji, tambueni haki kila mmoja wetu, acheni upendeleo, ndani ya kazi hatuhitaji hayo, tuangalie nidhamu, weledi na ubunifu,” alisema Dk. Mwanjelwa.   Alisema upandishwaji wa madaraja umeshatolewa nchi nzima, tayari nafasi 193,000 zimetangazwa na watumishi wenye sifa na viwango vya elimu ya juu watapandishwa.
kitaifa
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), leo kitaweka wazi matokeo ya utafiti wake wa tiba ya ugonjwa wa selimundu nchini.Akizungumza na gazeti hili jana Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Hemotolojia na Uwekaji wa damu, Profesa Julie Makani, alisema Wizara ya Afya imekuwa ikiwahimiza kuanza harakati za kutibu ugonjwa huo.Alisema tafiti zilizowasilishwa mwaka 2018, zilionesha Tanzania ni ya nchi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye selimundu na inakadiriwa kila mwaka wanazaliwa watoto 11,000 wakati kidunia kila mwaka wanazaliwa 300,000. Hata hivyo, Profesa Makani alisema kwa sasa huduma hiyo ya upandikizaji wa uboho ‘bone marrow’ inafanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Muhas, Neema Edwin alisema tayari wataalamu mbalimbali wameenda nje ya nchi, kujifunza namna ya upandikizaji wa selimundu kwenye mifupa kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.“Wataalamu wetu wapo nchi mbali mbali kwa ajili ya kujifunza namna ya upandikizaji wa uboho, kuna waliopo China, India na nchi nyingine, mafanikio hayo yametokana na tafiti zilizofanywa za kutibu ugonjwa huo, ikiwamo ya kupandikiza uboho na vinasaba,” alisema. Tafiti mbalimbali zitakazowasilishwa leo ni kuhusu ugonjwa huo, ikiwemo kuangalia kwa nini mgonjwa anapata homa kali mara kwa mara, anapungukiwa damu na kupata kiharusi.Pia matokeo ya utafiti huo utaweka bayana kwa nini mgonjwa mmoja, anaumwa matatizo hayo yote na mwingine haumwi au anaumwa moja kati ya hayo. Profesa Makani alisema Hospitali ya Muhimbili ilifanikiwa kutengeneza dawa pekee, ambayo imeruhusiwa kutibu wagonjwa wa selimundu ndani na nje ya nchi ya hydroxycerea. Hata hivyo, watafiti hao leo wataweka wazi muendelezo wa tafiti zao kuhusiana na ugonjwa huo.
kitaifa
MKUU wa Wilaya ya Chunya Maryprisca Mahundi amesema vyombo vya dola vimeanza kufanya uchunguzi wa malalamiko dhidi ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa wilayani humo Joseph Challe, anayedaiwa kuwatoza fedha nyingi wachimbaji wadogo wa madini kwa ajili ya huduma ya zimamoto kinyume cha sheria na taratibu.Aliyasema hayo baada ya kukamilika kwa kikao baina yake na wadau wa sekta ya madini wilayani humo, ambapo malalamiko dhidi ya gharama zinazotozwa na askari huyo anayeliwakilisha jeshi wilayani humo lilichukua nafasi kubwa. Mahundi alisema msingi wa kufuatiliwa kwa askari huyo kunatokana na agizo alilotoa Rais John Magufuli alipozungumza na wadau wa sekta ya madini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo alitaka wachimbaji wadogo wanaozingatia sheria kutonyanyaswa.Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu huyo wa wilaya alisema kwa siku kadhaa sasa ofisi yake imekuwa inapokea malalamiko mengi kuhusu vitendo vya askari huyo na ndio maana iliamua kuitisha kikao hicho, ili kulitafutia ufumbuzi suala hilo na kuwawezesha wachimbaji wadogo kuendelea kufanya shughuli zao bila bughudha. “Nimekuwa napokea malalamiko mengi kuhusiana na ghamara hizi za huduma za zimamoto.Wachimbaji wengine wanasema wanashinikizwa kutoa shilingi milioni 12 kwa mwaka, wengine shilingi milioni sita kwa mwaka na wengine shilingi milioni tatu… jambo la kusikitisha ni kwamba askari huyu anawatoza wachimbaji wadogo fedha ambazo hata hivyo hazitumiki kwa maslahi ya serikali bali kwa maslahi yake binafsi, suala hili hatuwezi kukubali kuona likiendelea kutokea,”alisema.Alisema kutokana na kukithiri kwa malalamiko dhidi ya askari huyo, alimuita Challe ofisini kwake na kuzungumza naye ili kufahamu ukweli, lakini alikanusha kuhusika na tuhuma hizo, hatua iliyomfanya kuwasiliana na wakubwa zake na vyombo vingine vya dola ili viweze kufanya uchunguzi zaidi na kuwezesha hatua kuchukuliwa. “Nimewaambia wachukue hatua ikiwezekana wamuondoe katika wilaya hii ya Chunya ili kuleta amani na wachimbaji waendelee kufanya kazi zao kwa ufanisi. Imefikia hatua sasa wanashindwa hata kuchangia katika shughuli muhimu za maendeleo kutokana na vitendo kama hivi vya kuwatoza fedha zisizotambuliwa kisheria,”alisema.
kitaifa
SERIKALI imetangaza nafasi za ajira kwa watumishi 513 wa kada za afya kwa lengo la kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya waliotangazwa kuajiriwa awali kushindwa kuripoti vituo vya ajira.Aidha, imetangaza ajira mpya 171 za kada za sekta ya afya ambazo awali zilikosa waombaji wenye sifa. Hayo yamebainishwa jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.Amesema Mei 10 hadi 25 mwaka huu, Serikali ilitangaza nafasi za ajira kwa watumishi wa kada za afya ambapo waombaji 6,180 walipangiwa vituo vya kazi.“Awamu ya kwanza tulitoa ajira kwa watumishi wa kada mbalimbali za afya 6,180 na ambao wameweza kuripoti katika vituo vya afya ni watumishi 5,667 huku waombaji 513 wakishindwa kuripoti, "amesema.Waziri Jafo aliongeza kusema kuwa ili kuziba nafasi ambazo zimeachwa wazi na waajiriwa walioshindwa kuripoti katika vituo vya ajira walivyopangiwa ambavyo ni zahanati na vituo vya afya vilivyo chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Serikali imewaajiri watumishi wapya 513 wa kada hizo.Alisema watumishi hao 513 wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba Mosi, mwaka huu na watakaoshindwa kuripoti ndani ya huo muda nafasi zao zitajazwa tena na wengine.“Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo kwa namna yoyote ile, watakaoshindwa kuripoti katika vituo walivyopangwa, nafasi zao zitajazwa na wengine wa kada husika haraka iwezekanavyo," amesema.Jafo aliongeza ili kuepuka usumbufu, waombaji wote waliopangiwa vituo wanatakiwa kuzingatia vyeo walivyopangiwa kwenye orodha wawe na vielelezo vyote kabla ya kwenda kuripoti katika kituo husika.“Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa,"amesema.Aidha, Jafo alisema serikali imetangaza upya nafasi za ajira kwa watumishi wa kada ya afya wapatao 171 baada ya walioomba awali kutokuwa na sifa zinazotakiwa.Alizitaja kada ambazo hazijapata watu wenye sifa kuwa ni ile ya Ofisa Muuguzi Msaidizi daraja la pili, Ofisa Muuguzi Daraja la pili, Daktari daraja la pili, Tabibu daraja la pili na Tabibu Msaidizi.Alizitaja kada nyingine kuwa ni nafasi ya Mteknolojia Mionzi, Mfamasia daraja la pili na mtoa tiba kwa vitendo.“Mwisho wa kupokea barua za maombi kwenye mfumo wa kielektroniki ni Oktoba 12 mwaka huu saa 9:30 alasiri na kuwa maombi yatakayotumwa nje ya mfumo huo hayatashughulikiwa,” amesema Jafo.Aidha, Jafo amesema waombaji wa kada mbalimbali 342 wamekidhi vigezo vya kuajiriwa na vituo vya afya na zahanati zilizopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.Barua iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa wizara hiyo, Mathew Kwembe inabainisha sifa za waombaji kuwa awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiriwa wa Serikali au wa hospitali za mashirika ya dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali.Alisema pia asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini na kupata namba ya malipo ya mshahara na endapo itabainika alishaajiriwa, atatakiwa kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama inavyoelekezwa na Waraka wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2012.“Mambo ambayo waombaji wanatakiwa kuzingatia wawe tayari kufanya kazi halmashauri yoyote watakayopangiwa, kufanya kazi na mashirika au taasisi zilizoingia ubia na Serikali… pia waombaji waliosoma nje ya nchi wanatakiwa waambatanishe cheti cha uwiano kutoka NECTA/NACTE/TCU,” amesema Waziri Jafo.
kitaifa
New York, marekani RAIS Donald Trump amewashambulia wabunge wa Chama cha Democratic, akiwatuhumu kuchochea uchunguzi dhidi yake baada ya kutoa hati ya kumtaka wakili wake binafsi kutoa nyaraka za mawasiliano na Ukraine. Wakati Trump akimshambulia vikali Mbunge wa Chama cha Democratic, Adam Schiff na kusema anatakiwa kukamatwa kwa uhaini, Australlia imethibitisha kwamba rais huyo hivi karibuni alimwomba Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Scott Marrison na viongozi wa mataifa mengine, kumsaidia Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr kupata taarifa zitakazomsaidia kuufanya uchunguzi wa mshauri maalumu, Robert Muller kutiliwa shaka. Muller aliongoza uchunguzi wa uingiliaji wa Urusi katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwaka 2016. Trump pia hakuacha kuwashambulia watoboa siri ambao madai yao yalihusu mawasiliano yake ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymir Zelensky mwezi Julai, ambayo sasa yamesababisha kuanzishwa kwa uchunguzi wa Bunge linalodhibitiwa na Democratic wa kumshtaki. Mwanasheria wake binafsi, Rudy Giuliani, anatajwa kuwa sehemu muhimu ya juhudi za kuiomba Ukraine kufanya uchunguzi dhidi ya familia ya mpinzani mkuu wa Trump uchaguzi ujao, Joe Biden, ambayo haijatuhumiwa kwa kufanya kosa lolote lile. Juzi alipofanyiwa mahojiano na kituo cha utangazaji cha Fox, kuhusu hati hiyo ya Bunge, Giuliani alisema anatafakari hatua atakazozichukua. “Ninapima njia mbadala. Nitakusanya ushahidi wangu wote pamoja na mawasiliano ya ujumbe. Sijui, ikiwa wataniruhusu nitumie kanda za video na mawasiliano niliyorekodi. “Nilikusanya ushahidi huu wote kabla ya uchunguzi wa Muller kumalizika, kwa hivyo ilikuwa wazi kuwa jukumu langu kama wakili wa Rais, mkutano wa mwisho ambao Waukraine waliuitisha, nililifanya wakati uchunguzi ulipomalizika,” alisema. Schiff ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kijasusi, na wenyeviti wa kamati nyingine mbili zinazoongozwa na Democratic, wametoa hati hiyo kwa Giuliani na kumpa hadi Oktoba 15 kuwa amewasilisha nyaraka hizo. Huko Australia, Msemaji wa Serikali amethibitisha alipozungumza na kituo cha utangazaji cha ABC kwamba Trump aliwasiliana na Waziri Mkuu, Marrison, kuomba kumsaidia Mwanasheria Mkuu, Barr kupata taarifa zinazohusiana na uchunguzi wa Muller. Kulingana na Gazeti la New York Times, lililowanukuu maofisa wawili wa Marekani ambao hawakutambulishwa, nakala ya maandishi ya mawasiliano hayo ilitolewa tu kwa kundi dogo la wasaidizi wa Trump ambao wanataka udhibiti mkali wa mawasiliano hayo. Australia imesema iko tayari wakati wote kusaidia juhudi za kufungua njia kwenye uchunguzi wa masuala kadhaa na waziri mkuu huyo pia alikubali kufanya hivyo. Uchunguzi mpya wa maoni uliochapishwa jana umeonyesha Wamarekani wamegawika juu ya ama kuunga mkono mashtaka dhidi ya Trump au kujiweka pembeni.
kimataifa
Dar es salaam Ubalozi wa China nchini leo, umeungana na wenzao kwenye taifa la kwanza kukumbwa na virusi vya corona, kuomboleza waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo wa homa kali ya mapafu. Maombolezo hayo yameongozwa na Balozi wa China nchini, Wang Ke, yaliyofanyika kwa kupandisha bendera nusu mlingoti. Katika maombolezo hayo, Balozi Ke, Katibu Mkuu wa Jumuhiya ya Kuendeleza Urafiki kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wawakilishi wengine kutoka Ubalozi wa China na makampuni nchini Tanzania, wametoa heshima kwenye makaburi ya wataalamu ya kichina nje ya Dar ya Salaam, waliofariki dunia wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).Tanzania. Mapema leo China imefanya maombolezo ya nchi nzima kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona.  Bendera za taifa hilo zimepepea nusu mlingoti nchi nzima pamoja na kusitisha shughuli zote za burudani.  Siku hiyo ya maombolezo imeambatana na kuanza kwa sherehe za kila mwaka za kuwakumbuka mababu wa zamani nchini China.  Sherehe hizo zimeanza kwa nchi kukaa kimya kwa muda wa dakika tatu, ili kuomboleza waliofariki, wakiwemo wafanyakazi wa afya waliokuwa mstari wa mbele na madaktari.  Magari, treni na meli zilipiga honi na sauti za ving’ora zilisikika hewani.  Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wametoa heshima zao za kimya mbele ya bendera ya taifa mjini Beijing.  Zaidi ya watu 3,000 China bara walifariki dunia kutokana na COVID-19.
kimataifa
Na EVANS MAGEGE MAASKOFU wawili wa Kanisa Katoliki waliopatiwa mgawo wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow wameamua kuzirudisha serikalini ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za uhujumu uchumi unaomkabili muumini aliyewagawia, ambaye ni James Rugemalira. Maaskofu hao ni Method Kilaini na Eusebius Nzigirwa, ambao Februari, 2014 walipatiwa mgawo wa fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira. Katika mgawo huo, Askofu Kilaini alipokea Sh milioni 80.5 na Askofu Nzigirwa alipokea Sh milioni 40.4. Kwa mujibu wa tangazo la pamoja la maaskofu hao lililosambazwa juzi katika mitandao ya kijamii siku hiyo hiyo, kabla ya kuthibitishwa na Askofu Kilaini jana kwa njia ya ujumbe mfupi, limesema maaskofu hao wamechukua uamuzi wa kuzikabidhi serikalini fedha hizo hadi uchunguzi wa kesi hiyo utakapokamilika na uamuzi kutolewa. Tangazo hilo lilisomeka: “Mnamo mwezi Februari, 2014, sisi Maaskofu Method Kilaini na Eusebius Nzigirwa, tulipokea fedha zilizotumwa na James Rugemalira (kupitia kampuni yake ya VIP Engineering) kwenye akaunti zetu zilizopo Benki ya Mkombozi, Dar es Salaam. “Tulipokea matoleo hayo kutoka kwa muumini wetu kwa moyo wa shukrani na roho safi. Lakini mnamo Juni, mwaka huu Rugemalira alikamatwa na vyombo vya dola na kutuhumiwa na makosa ya kuhujumu uchumi, ambapo fedha alizozituma kwa watu mbalimbali zikihusishwa. “Kutokana na kuwepo kwa kesi kuhusu fedha hizo (bila kutoa hukumu) tumeona ni vema tuzikabidhi kwa Serikali hadi uchunguzi kuhusu kesi hiyo utakapokamilika na uamuzi kutolewa, ili yule mwenye haki ya kuwa na fedha hizo aweze kupewa kama ilivyostahili.” Januari 23, mwaka juzi, wakati sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Escrow likiwa bado limepamba moto, gazeti hili lilimuuliza Askofu Kilaini  kama ameshahojiwa na Serikali kuhusu mgawo wa fedha hizo na alijibu kuwa hajahojiwa na taasisi yoyote, ikiwamo Kanisa Katoliki au Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Katika maelezo yake, alisema wazi kuwa, yupo tayari kuhojiwa na Takukuru kama taasisi hiyo itamhitaji afanye hivyo, kwa sababu hana cha kuficha juu ya fedha alizogawiwa na Rugemalira. “Sijahojiwa na taasisi yoyote, liwe Kanisa au Takukuru. Hata wakinihitaji nipo tayari kwa kuhojiwa kwa sababu sina cha kuficha na hili jambo la kupokea fedha kwa wafadhili kwa ajili ya kusaidia jamii ni sehemu ya maisha yangu kwa kipindi cha miaka 40 sasa,” alisema Kilaini. Katika ufafanuzi wake, alisema kama fedha za Escrow zitathibitishwa kuwa ni chafu, atazirudisha kwa aliyemgawia. “Hizi fedha hazijathibitishwa kama ni chafu na kama ikitokea hivyo nitamrudishia Rugemalira,” alisema. Alipoulizwa kama fedha hizo zipo au katumia na kama amezitumia atazirudisha kwa utaratibu upi, alijibu kuwa fedha hizo ametumia kiasi, hivyo ikitokea zikathibitishwa kuwa ni chafu itambidi  azitafute. “Fedha zimetumika kiasi ambazo itabidi nizitafute kukamilisha kiasi nilichopewa, hii ni changamoto, lakini sitaacha au kukata tamaa katika azma ya kuendeleza kanisa na jamii nikitumia misaada mbalimbali, yalipoanza maneno nilisitisha matumizi ya fedha hizo hadi mambo yawe wazi,” alisema Kilaini. Alipoulizwa kiasi kilichotumika hadi anasitisha matumizi ya fedha hizo, alijibu kwa ufupi kwamba mahali alipo hakuwa na hesabu kamili, hivyo alihofia kusema uongo. Hata hivyo, alisema matumizi ya fedha hizo yalikusudia kuanzisha vituo vya wagonjwa wa saratani pamoja na kusaidia jamii yenye uhitaji. Alifafanua kwamba, wakati anachukua uamuzi wa kusitisha matumizi ya fedha hiyo alikuwa katika hatua ya upembuzi yakinifu wa kuanzisha vituo vya wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Kagondo, Lubya na Mgana, zote za Mkoa wa Kagera. “Tayari kulikuwa na wataalamu kutoka India niliwaleta kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa hospitali nilizozitaja, pia nilikusudia kuanzisha kituo cha wagonjwa wa saratani huko Biharamulo na Morogoro,” alisema Kilaini. Mbali na vituo vya wagonjwa wa saratani, pia alisema fedha hizo alizitumia kusaidia vikoba vinne vya akina mama wa Jimbo la Bukoba na wanafunzi 14 aliokuwa anawasomesha. “Kuna mambo mengi katika jamii ambayo yanahitaji misaada, kuna vikoba kwa ajili ya kuwakwamua akina mama kiuchumi, kuna wazee wasiojiweza, pia kuna vijana 10 wa shule za sekondari na wanne wa vyuo vikuu wote ninawasomesha, hivyo sehemu ya fedha ilitumika katika mahitaji yao,” alisema. Pia alifafanua uhusiano wake na Rugemalira kwamba ulianza tangu mwaka 1975, wakati huo akiwa Padri wa Parokia ya Bukoba na alimsifu kuwa ni mkarimu siku zote katika kanisa na jamii.
kitaifa
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapatia dhamana viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bila washtakiwa hao kuwapo mahakamani huku wakitakiwa kuripoti kila Alhamisi. Awali, viongozi hao akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, walidhaniwa kuletwa mahakamani hapo na mahakama ikaamua kuketi na mawakili wa pande zote mbili kujadili kama washtakiwa hao wataletwa au la ili itoe uamuzi wake. Baada ya makubalianao hayo, Inspekta Shabani wa Magereza ameieleza mahakama kuwa washtakiwa hao wameshindwa kuletwa mahakamani hapo kwa sababu gari la kuwaleta ni bovu. Akitoa uamuzi wake, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa hao kuwa wadhamini wawili kila mmoja na kusaini kwa maandishi ya Sh milioni 20. “Kila mshtakiwa atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20, wadhamini pia watasaini kiwango hicho, washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wanatakiwa kuripoti polisi mara moja kwa wiki, ambayo ni kila siku ya Alhamisi,” amesema. Pamoja na Mbowe, viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.  
kitaifa
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM TIMU ya soka ya Azam FC imeanza kupiga hesabu za mbali ikiwaza timu moja kati ya nane zitakazotolewa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ambayo itakutana nayo baada ya kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kimataifa. Azam imepata matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kutokana na matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 iliyopata dhidi ya timu ngumu ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa awali wa hatua ya 16 bora. Wawakilishi hao wa Tanzania waliofanikiwa kuitupa nje ya michuano hiyo timu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 7-3 ikiwa ni ushindi wa 3-0 ugenini na 4-3 nyumbani, wanakabiliwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance utakaochezwa Aprili 19, mwaka huu nchini Tunisia. Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Dennis Kitambi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wana matumaini ya kufanya vyema Jumanne ijayo hivyo wameanza kuumiza vichwa kuwaza timu watakayokutana nayo katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), iwapo Azam itasonga mbele itakutana na moja ya timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Alisema matarajio ya benchi la ufundi ni kuiondosha Esperance katika michuano hiyo jambo ambalo wanaamini linawezekana kutokana na maboresho yaliyofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Mwingereza, Stewart Hall. “Ni jambo zuri kuanza kuwafikiria wapinzani tutakaowakabili mbeleni ili kupanga mbinu na mikakati mapema, kama inavyofahamika kwamba klabu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni nzuri,” alisema Kitambi. Wachezaji wa Azam wanatarajiwa kuingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance utakaochezwa mjini Rades, Tunisia. Yanga ni moja ya timu zinazoshiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo Aprili 20, mwaka huu watacheza ugenini dhidi ya miamba ya soka barani Afrika Al Ahly ya Misri, ambao waliibana na kutoka sare katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.      
michezo
* Kuivaa Azam kwa kujiamini Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM BAADA ya kuona kikosi chake kimepoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, kocha mkuu wa timu ya Simba, Joseph Omog, juzi alifanyia kazi mapungufu hayo katika mazoezi ya jioni yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran, Dar es Salaam, tayari kwa kuivaa Azam. Omog ambaye anahitaji ushindi katika kila mechi, amekua pia akikataa ushindi mwembamba unaoweza kuwagharimu mbeleni na timu yake. Akizungumza juzi baada ya mazoezi, Omog alisema alikua anafanyia kazi jinsi ya kutumia vema nafasi za mwisho zinazotengenezwa na viungo ambazo washambuliaji wake wanashindwa kuzimalizia. “Kikosi kilikuwa na matatizo ya umaliziaji na ndio maana nimeona ni vema kuyafanyia kazi mapema kabla ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, ambapo pia yatanisaidia kutafuta kikosi cha kwanza kitakachoanza. “Katika mchezo wetu na Mtibwa licha ya kupambana na kushinda bao 2-0, wachezaji walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini walifeli kwenye umaliziaji. “Tumerekebisha vya kutosha na tupo tayari kuivaa Azam huku tukiwa tunajiamini,” alisema. Simba itacheza na Azam Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hizo.
michezo
HAKUNA aliyefahamu kwa nini vijana wengi waliokuwa wakisota na maisha magumu, jijini Dar es Salaam na kisha kupata zali la kazi ya ubaharia na kwenda kuishi nje ya nchi walirejea kwa wingi nchini ili kusherehekea Sikukuu ya Krismas na mwaka mpya wa 1985. Ilikuwa kama ni ndoto vile, kwani vijana wa maeneo ya Keko, Magomeni, Mwananyamala, Msasani, Ilala na sehemu nyingine walirejea wakiwa katika hali bora ya kimaisha. Wengi wao walitokea nchini Italia walikobahatika kupata kazi ya ubaharia, wachache walitokea katika nchi ya Ugiriki na baadhi katika nchi za Bara Hindi. Dar es Salaam ilionekana kuingiliwa na vijana hao ambao haikuwa kazi sana kuwafahamu kutokana na mavazi yao ya kisasa, utumiaji wa fedha lakini pia magari yao ya fahari ambayo mengi yalikuwa aina ya 504 enzi hizo yakiitwa Guruwe. Ukipishana na kijana wa aina hiyo hupati tabu kumjua hata kwa kusikia harufu ya manukato yake, wengi walipendeza na kuonekana kunawiri tofauti na wenzao waliokuwa wakiendelea kusota. Wapambe nao hawakuwa nyuma, maana waliwajua kabisa wageni hao ambao mara nyingi walionekana wakati wa kuingia tu lakini kutoka ilikuwa siri ya kila mmoja wao, wenyewe waliamini ukiaga unaweza kukutana na mikosi ikakufanya uendelee kusota Bongo. Kwa bahati mabaharia wengi waliondoka nchini wakiwa mashabiki wa bendi mbalimbali za muziki wa dansi, lakini waliporejea wakaachana kabisa na muziki huo badala yake wakajitosa katika ushabiki wa muziki wa disko. Kwa maana hiyo maeneo waliyokwenda kucheza muziki ilikuwa ni katika hoteli zilizokuwa zikipiga muziki wa aina hiyo kama vile YMCA pale Posta Mpya, Mbowe Hotel pale ilipokuwa Bilcanas na kando yake kidogo paliitwa Ushirika Club au 900 Vision. Vilevile kandokando ya bahati kulikuwa na kumbi kama Rungwe Oceanic, Kunduchi Beach Hotel na Mwananyamala kulikuwa na ukumbi maarufu wa Villa. Lakini baada ya kujirusha sana katika siku hizo za mwisho wa mwaka na kisha kuikaribisha Januari ya mwaka 1985, mabaharia hao waliamua kutafuta siku moja kwenda kuagana katika ukumbi utakaokuwa Uswahilini. Siku hiyo watacheza muziki wa dansi wa bendi yoyote, ilimradi iwe inapiga katika ukumbi waliokubaliana kukutana. Bahati ikaangukia Ukumbi wa Omax Bar uliokuwepo Keko sehemu ambayo kwa sasa ni maarufu kwa utengenezaji wa fenicha. Magari ya kifahari yalitapakaa nje ya ukumbi huo, na mabahari na wapambe wao walioneka kuingia kila baada ya dakika na haikuchukua muda mrefu ukumbi ule ukatapika. Kwa bahati nzuri siku hiyo ilikuwa Jumamosi, Januari 12, 1985 Bendi ya Orchestra King Kikii Double O ndiyo iliyokuwa ikifanya onyesho katika ukumbi huo. Kwa bahati nzuri tena bendi hiyo ilikuwa na wanamuziki waliokomaa kwa kupiga muziki wa aina mbalimbali, akiwemo Tabia Mwanjelwa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Ujerumani, Rizy, na King Kikii sambamba na kina Kapelembe Kokoo na wengine. Walipogundua kwamba siku hiyo ugeni waliokuwa nao haukuwa wa kawaida, basi wanamuziki wa bendi hiyo walianza kutumbuiza kwa nyimbo mbalimbali na mapigo ya aina Afrika Magharibi na vilevile magoma ya Ulaya, hali iliyowafanya mabaharia wachanganyikiwe na kuanza kucheza na pia kuhoji kama wanamuziki hao walikuwa wapo miaka yote. Wapo walioondoka wakimuacha King Kikii akiwa na OSS lakini ufanisi ule jukwaani uliwachengua kiasi cha jioni ilipohamishwa onyesho na kwenda Bahari Beach Hotel walisomba na mabaharia wote wakaenda kumalizia furaha yao katika ukumbi huo.
burudani
WAKATI michuano ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, (Kombe la Kagame) ikianza leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka ukanda huo, Cecafa, Nicholaus Musonye amesema viongozi wa vyama wanachama wanahujumu.Akizungumza na waandishi wa habari jana Musonye alisema wamejiandaa vizuri kufanikisha michuano hiyo inayoanza leo na kumalizika Julai 13 lakini hakusita kuweka wazi dukuduku lake kuwa viongozi wa vyama wanachama ndio wanaohujumu mashindano hayo kwa kuweka nguvu kwenye mashindano yenye fedha nyingi na kuacha kusapoti kazi ya kukuza michezo katika ukanda wao hali inayofanya kudorora.“Kuna mashindano yanayoendeshwa kwenye nchi zetu na viongozi wa vyama wanayakumbatia kwa sababu yana pesa nyingi na kusahau jukumu letu kama Cecafa la kuandaa mashindano ambayo ndiyo chimbuko la kuendeleza soka kwenye ukanda wetu, mimi nilikuwa Nairobi lakini sikwenda kuangalia,” alisema Musonye na kukataa kutaja amelenga mashindano gani.Pia Musonye alisema yeye amehudumu kwa muda mrefu kwenye Cecafa kama Katibu Mkuu lakini akitakiwa kuondoka ili waweke mtu mwingine yeye yupo tayari.“Kesho (leo) tutafungua mashindano rasmi na naamini tutafanya michuano bora na yenye wachezaji bora wanaoweza kupambana kwani kila timu hasa zile zinazoshiriki mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika zimeleta timu nzima,” alisema Musonye.Aidha Musonye aliziombea timu zilizojitoa kwenye mashindano hayo kwa madai ya kujiandaa na michezo ya kombe la Shirikisho Afrika kufika mbali na hata kutwaa ubingwa kwani hakupenda kuzitamkia maneno mabaya kwa wakati huu.Yanga na St George ya Ethiopia ndizo zilizojitoa kwenye michuano hiyo zikidai kutaka muda wa kujiandaa zaidi na michuano ya Afrika.Kaimu Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani alisema wamejiandaa ipasavyo kukamilisha michuano hiyo ya Kombe la Kagame.Michuano hiyo inazinduliwa leo ambapo mechi ya ufunguzi itakuwa saa nane mchana kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Vipers ya Uganda kabla Azam FC haijacheza na Kator ya Sudan Kusini na saa kumi jioni na saa moja usiku utachezwa mchezo wa Kundi C kati ya Singida United na APR ya Rwanda. Mechi zote zitachezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi.
michezo
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM WAKATI mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu zimeshika kasi, hakuna dalili yoyote inayoonyesha kama mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam utatoa bingwa wa ligi hiyo. Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 46 sawa na Azam, ambayo inashikilia nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Simba ikiwa nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi 45 katika mechi 20 ilizocheza. Yanga imefunga mabao 44 na kufungwa 9, huku Azam ikiwa imeziona nyavu za wapinzani wake mara 34 na kufungwa 11 kutokana na mechi 19 walizocheza ikiwa ni pointi moja nyuma ya Simba, ambayo imefunga mabao 35 na kufungwa 13. Pambano la Yanga dhidi ya Azam litachezwa huku timu zikiwa zimebakiwa na michezo 10 kila moja, wakati Simba imebakiwa na 9 ili kupatikana bingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Michezo hiyo itakuwa na jumla ya pointi 30 ili timu iweze kuwa kwenye nafasi nzuri ya kujihakikishia ubingwa inatakiwa kunyakua zaidi ya pointi 15 hadi 18. Pointi hizo zinatokana na kuwapo kwa michezo 10, ambapo mitano kati ya hiyo inawezekana kutoa taswira halisi ya bingwa msimu huu. Yanga itacheza mechi 6 ugenini, huku 4 ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani, Azam itacheza michezo mitano ikiwa kwenye dimba lake la Azam Complex na mingine mitano ikiwa ugenini, wakati Simba itacheza mechi 3 ugenini na mingine 6 ikiwa uwanja wake wa nyumbani. Moja ya mechi zinazoonekana kuwa ngumu kwa timu zilizopo kwenye nafasi tatu za juu ni ule utakaochezwa Aprili 2 kati ya Yanga na Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa, siku chache baadaye Azam itakutana na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Presha itapanda zaidi Aprili 16 wakati Simba ikiikaribisha Azam kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam, ambapo siku moja baadaye Yanga nao wataikaribisha Mgambo Shooting kwenye uwanja huo. Aidha, mchezo wa Machi 13 wa Simba dhidi ya Prisons utakuwa miongoni mwa michezo migumu ya mwishoni mwa msimu, ambayo inaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa. Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu anaweza kufikisha pointi 64 ambazo ni nyingi, ukilinganishwa na msimu uliopita wakati bingwa alikuwa na jumla ya pointi 55. Kutokana na hesabu hiyo, huenda bingwa wa msimu huu akapatikana baada ya michezo itakayochezwa kuanzia Aprili, ambapo timu nyingi zitakuwa zimefikia michezo kuanzia 25 na kubakiza mitano. Hatua hiyo inafanya nafasi ya ubingwa kuwa wazi kwa timu zote tatu zilizopo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. Kwa kuwa michezo iliyochezwa na timu za Ligi Kuu hadi sasa ni 20 kati ya 30, Yanga na Azam zitakuwa zikikamilisha hesabu hiyo huku zikiwa na viporo vya mchezo mmoja mkononi.
michezo
KAMATI ya Baraza la Wawakilishi ya Fedha, Biashara na Kilimo imefurahishwa na kuwepo kwa kitengo ambacho kitarahisisha na kuondoa urasimu kwa wawekezaji katika kuwekeza miradi ya maendeleo.Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akisoma maoni ya kamati kuhusu muswada wa kuimarisha vitega uchumi nchini uliowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed.Alisema kwa muda mrefu yapo malalamiko kutoka kwa wawekezaji kusumbuliwa wakati wanapotaka kuwekeza katika miradi, ikiwemo nenda rudi katika taasisi mbalimbali za serikali. ''Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi imefurahishwa kwa kuletwa kwa muswada huu ambao lengo lake kubwa kuondoa vikwazo na usumbufu kwa wawekezaji na kuwepo kitengo kimoja kitakachoshughulikia miradi ya wawekezaji moja kwa moja,'' alisema.Wakichangia muswada huo, Mwakilishi wa jimbo la Tunguu, Simai Mohamed Said alisema matarajio makubwa na kupungua kwa malalamiko ya wawekezaji ya kuchelewa kupata vibali kwa miradi ya uwekezaji wanayotaka kuwekeza.Aidha Mwakilishi wa Konde, Omar Seif Abeid alisema Zanzibar ipo katika mikakati ya uwekezaji ambapo vitendo vya urasimu vinatakiwa kuondoshwa mara moja ili kujenga matumaini mazuri.Alisema wapo wawekezaji waliokata tamaa na kufuta miradi yao kwa sababu ya kuwepo kwa matukio ya urasimu ya uwekezaji ikiwemo miradi ya utalii.''Muswada wa sheria hii kwa kiasi kikubwa utasaidia na kuondoa urasimu wa matukio ya uwekezaji yaliyokuwepo awali ambapo baadhi yake yaliwavunja moyo wawekezaji na kuondoa miradi yao,'' amesema.Akiwasilisha muswada huo mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed amesema Zanzibar imejipanga kujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji mbalimbali na kukifanya kuwa kituo bora cha uwekezaji katika Afrika ya Mashariki
uchumi
Na JOHANES RESPICHIUS   WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, ameitaka Bodi ya Chuo cha Maji kufanya kazi ya kukiboresha chuo hicho kwa kasi na kama haitaweza kufanya kulingana na matarajio yake, anaweza kuivunja muda wowote. Waziri Lwenge aliyasema hayo jana, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya chuo hicho. Alisema kwa kuwa wajumbe wa bodi walikubali uteuzi wake, wanatakiwa kuendana na kasi ambayo inahitajika ya kuhakikisha wanaboresha chuo hicho kulingana na wakati uliopo. “Kwa kawaida huwa tunateua bodi kwa miaka mitatu, lakini kwa utaratibu wangu nataka ‘performance’ zaidi kuliko kuweka muda, kwahiyo kama bodi hamtaweza kwenda na matarajio ninayoyataka naweza kuivunja wakati wowote. “Kwasababu mmekubali kwenda na kasi ambayo naitaka ya kuhakikisha mnaboresha chuo hiki kwa kutoa wanafunzi walioiva, mmeona Serikali inavyoendelea kuwawekea miundombinu mizuri, kuna mitambo hapa ukienda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakuna, hivyo ninafuatilia na nitaendelea kufuatilia utendaji wa bodi hii kwa ukaribu  sana,” alisema Waziri Lwenge. Kutokana na azma ya Serikali kutaka kuhamia Dodoma, Mhandisi Lwenge alisema jengo linalojengwa Ubungo, Dar es Salaam la Maji House italitoa kwa chuo hicho kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa. “Suala la majengo tutaliboresha, tunajenga jengo la Maji House tutawakabidhi, sisi tunahamia Dodoma, kwahiyo tumeshawekeza kwa ajili yenu ili kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi. “Kwenye awamu ya kwanza ya programu ya sekta ya maji, hadi kufikia Juni mwaka huu miradi ya maji 1,210 vijijini ilitekelezwa. Kukamilika kwa miradi hii kumetuwezesha kufikia asilimia 72 ya watu kupata maji safi na salama. “Katika mwaka 2016/2017 jumla ya miradi 386 iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Lengo letu ni kufikia asilimia 80 ya watu waishio vijijini ifikapo mwaka 2020,” alisema Mhandisi Lwenge. Awali akitaja changamoto zinazokikabili Chuo hicho, Mwenyekiti Mteule wa bodi hiyo, Profesa Felix Mtalo, alisema kuna upungufu wa madarasa na mabweni. “Mwaka 2008 wakati huo kinabadilishwa kuwa Wakala wa Serikali, kikiwa na wanafunzi wasiozidi 200, mwaka huu kina jumla ya wanafunzi 1,922, ambapo mabweni yaliyopo yana uwezo wa kupokea wanafunzi 700 tu, hivyo zaidi ya wanafunzi 1,000 inabidi waishi nje ya Chuo,” alisema Profesa Mtalo. Alisema changamoto nyingine ni pamoja na ukosefu wa maabara za kutosha, mfano maabara ya ‘Hydrogeology and Water Well Drilling’, kwa ajili ya kozi za uchimbaji visima pamoja na ‘Soil Plant’ (uhandisi wa umwagiliaji). Kwa mujibu wa Profesa Mtalo, kutokana na changamoto hiyo, chuo kimekuwa kikilazimika kuwapeleka wanafunzi kwa ajili ya uzoefu kwa vitendo kwa Wakala wa Uchimbaji Visima (DDCA) na Taasisi ya Utafiti ya Mlingano, iliyoko Tanga.
kitaifa
Asha Bani Kundi la matapeli linadaiwa kutumia jina la Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) Dk. Athumani Kihamia kwa lengo la kutapeli watu ili kujipatia fedha. Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu leo Jumamosi Juni 15, Dk. Kihamia amesema kuna watu wamefungua akaunti feki ya mtandao wa kujamii wa facebook na  kuwatapeli watu kwa kuwatumia ujumbe wa maneno (Messenger), ambapo ametoa tahadhari kwa wananchi kua makini na utapeli huo unaoendelea. “Kuna baadhi ya watu wamefungua akaunti kwa jina langu na kulitumia kwa kujipatia fedha kwa njia hiyo ya utapeli huku wakijua ni kosa kisheria, baadhi ya jumbe wanazotuma ni pamoja na kwamba Dk. Kihamia anauwezo wa kuwatafutia kazi katika mbuga ya Hifadhi ya Serengeti,” “Yaani tayari kuna watu wameliwa fedha na hao matapeli hao kupitia sehemu ya ujumbe unaosema sema hivi “angalia kama kuna mtu amemaliza chuo na hajapata kazi uniambie maana kuna kazi shirika la Marekani la Thomson Zoology  kule Serengeti national park na wanahitajika watu wawili wenye diploma au degree kwa ajili ya kazi ya reservations na mshahara milioni moja na laki nane kama kuna mtu aniambie mapema nimpe namba ya huyo mzungu ahsante,” amesema. Dk. Kihamia amesema aliishawahi kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii lakini anaona hali inazidi kuwa mbaya hivyo amewataka wananchi kupuuza ujumbe huo.
kitaifa
NA OSCAR ASSENGA- TANGA JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limesema litawakamata watuhumiwa wote watakaobainika kujihusisha kusafirisha dawa za kulevya kwa njia mbalimbali ikiwamo angani, majini na bandari bubu. Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa bandari bubu 45 katika mkoa huo ambazo zinadaiwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nchi za jirani. Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Mwandamizi Benedict Wakulyamba, alisema bandari bubu zilizopo wilaya za Mkinga, Pangani, Muheza na Tanga mjini zimekuwa zikitumika kufanya shughuli mbalimbali za kibiashara kwa njia haramu sambamba na kutumia vyombo ambavyo ni hatari kwa usafiri wa majini. Kamanda Wakulyamba alisema kuwa vita ya dawa za kulevya inahitaji ushirikiano wa vyombo vya ulinzi, usalama na wananchi ili kutokomeza mtandao ambao unajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya mkoani Tanga. “Niseme tu ndugu zangu wanahabari nyie pia mna nafasi ya kuhakikisha suala hilo linamalizika kwa kuwafichua watumiaji na wasafirishaji, lakini pia jamii husika. Hivyo tushirikiane kuimaliza vita hii kubwa. “Lakini sisi kama Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, tutapambana vikali na dawa za kulevya kwa kuhakikisha tunadhibiti watu wote wanaoingiza kwa njia ya angani, majini, barabarani na njia zote ambazo zinaweza kutumika ili kutokomeza suala hili,” alisema. Wakati huo huo, Jeshi la Polisi kupitia operesheni zake zinazoendelea mkoani hapa, limemkamata askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Koplo Rashid Mohamed mwenye namba MT 82494 akiwa na bunda 23 za mirungi. Kamanda Wakulyamba alisema tukio hilo lilitokea Februari 9 mwaka huu na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na pikipiki.
kitaifa
ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM BAADA ya kuambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa, amesema kiu yake ni kuhakikisha anawafunga Watani zao hao, na hilo atahakikisha linatimia endapo atakutana nao katika michuano ya Mapinduzi. Yanga iliilazimisha Simba sare ya mabao 2-2, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza na MTANZANIA, baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa alisema walikuwa na kila sababu ya kupata ushindi dhidi ya Simba juzi kwani wapinzani wao hao walipoteana hasa kipindi cha pili. “Simba waliidharau sana Yanga, kwa kuona wana kikosi kizuri huku wakiwa wamesahau mchezo ni mbinu unayoingia nayo, mwisho tumerudisha mabao wakiwa wameshatangulia na kupata sare. “Matokeo haya hayajamaliza kiu niliyokuwa nayo kwa Simba, lakini sina shaka tunakwenda katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, tutapambana tufikie hatua ya kukutana na Simba ili tuweze kuwafunga na kumaliza kelele zao,”alisema Mkwasa. Michuano ya Mapinduzi ambayo ni maalum kwa ajili ya Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar itaanza kutumua vumbi leo, ambapo safari hii inaendeshwa kwa mtindo wa mtoano . Yanga imepangwa kundi A, ikiwa pamoja na Azam, Mlandege na Jamhuri,  Simba ipo Kundi B sambamba na Mtibwa Sugar, Chipukizi na Mapinduzi.
michezo
Na Mohamed Saif – Busega NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa maji katika mji mdogo wa Lamadi  wilayani Busega mkoani Simiyu ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 93. Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa ziara ya mradi na washirika wa maendeleo wanaowezesha utekelezaji wa miradi ya maji kupitia programu ya uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira ijulikanayo kama LV Watsan ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD). Kalobelo alisema amefarijika kushuhudia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi na aliongeza kuwa hadi kufikia Agosti, mwaka huu utakuwa umekamilika. Alisema Lamadi ni mji ambao kwa muda mrefu ulikuwa na ukame na kwamba mradi huo ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo na unadhihirisha matumizi sahihi ya Ziwa Victoria. Aliwataka wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria kuhakikisha wanatunza mazingira, hasa ikizingatiwa manufaa wanayoyapata ni makubwa kwao na kwa vizazi vijavyo. Kwa upande wake, Mratibu nradi kutoka EIB, Raoul Pedrazzani alisema miradi inayotekelezwa chini ya LV Watsan, imeonesha mafanikio makubwa na aliipongeza Mamlaka ya Maji Mwanza (Mwauwasa) ambayo inajukumu la kusimamia miradi hiyo kwa niaba ya Wizara ya Maji kwa usimamizi mahiri wa utekelezaji wake. Naye Ofisa Miradi kutoka AFD, Clement Kivegalo alisema wameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi na kwamba AFD itaongeza udhamini kadiri itakavyohitajika kufanya hivyo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera ambaye alikuwa mwenyeji wa ugeni huo wilayani hapo, alisema mradi unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye wilaya na hususan katika mji wa Lamadi. Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Anthony Sanga alisema mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka EIB na AFD kwa gharama ya Sh bilioni 12.83.
kitaifa
Uchaguzi Mkuu wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa mujibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, mjumbe wa bodi hiyo Francis Kifukwe alisema uchaguzi huo utafanyika kwa mujibu wa katiba ya Yanga kama itakavyopangwa na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo kwa kushirikiana na bodi ya wadhamini.Awali, uchaguzi wa Yanga ulikuwa ufanyike mwaka jana lakini uliahirishwa kwa kushauriwa na serikali kwa sababu za uchaguzi mkuu. Hata hivyo uongozi huo chini ya Mwenyekiti wake Yusuf Manji umemaliza muda wake mwaka wa tatu sasa.“Kama bodi tunaunga mkono uchaguzi ufanyike, lakini hatuwezi kufanya uchaguzi huo huku mechi zinaendelea, kwa sasa tunahitaji kuelekeza nguvu zetu kwenye mashindano yanayoendelea,” alisema.Kifukwe hakuweka wazi ni katiba ipi itakayotumika zaidi ya kusema katiba ya Yanga.Licha ya kushindwa kuweka wazi, tayari BMT na TFF zilitangaza uchaguzi huo utafanyika kwa kutumia katiba ya Yanga ya mwaka 2010, na Baraza hilo likisema kuwa uchaguzi utasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF kwa kuwa Yanga kwa sasa haina uongozi kwani muda wao umekwisha.Kifukwe ambaye aliongozana na viongozi wengine wa bodi hiyo akiwemo Mama Shadya Karume na Mohamed Katundu alizungumzia pia maendeleo ya ujenzi wa uwanja mpya wa Yanga kuwa wamewasilisha na kukumbushia ombi la kuongezewa eneo Jangwani.Alisema wamekumbushia mchango wao wa kukamilisha ‘master plan’ ya bonde la Jangwani kwa kushirikiana na Baraza la Mazingira (NEMC), Jiji na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.“Bodi yetu inatoa shukrani kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki na meya mstaafu wa Ilala Jerry Silaa kwa juhudi na ushirikiano wao, tungependa kukumbushia na kuwasilisha ombi letu kwa Serikali ya Rais John Magufuli ambayo tunaiamini kwa sera yake ya hapa kazi tu,” alisema.Katika hatua nyingine, Kifukwe aliomba wanachama wa Yanga kuendelea na utulivu na mshikamano na wakati huo huo akiupongeza uongozi wa klabu hiyo, wachezaji na benchi la ufundi kwa kuonesha kiwango kizuri katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.
michezo
Wuhan, China IDADI ya watu walioathirika na virusi vipya nchini imeongezeka mata tatu zaidi, huku ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo  ukielezwa kuenea katika majiji mengine makubwa. Jiji la Wuhan ulikoanzia ugonjwa huo limeripotiwa kuwa na kesi mpya 136 za  ugonjwa huo ambao husababisha mgonjwa kushindwa kupumua vizuri. Tayari Jiji la Beijing zimekwisharipotiwa kesi mbili, wakati Shenzhen ikithibitisha moja. Idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo inaelezwa kuzidi 200, na watatu tayari wamekwishafariki dunia. Taarifa hizi za kushtua zimekuja wakati mamilioni ya Wachina wakijiandaa kusafiri kwa ajili ya mapumziko wa mwaka mpya wa China ‘The Lunar New Year’. Kutokana na hilo mamalaka  za nchini humo zimesema zitachunguza kila mtu anayesafiri. Tayari maofisa wa afya wameubaini ugonjwa huo ambao ulianzia Wuhan mwezi Desemba mwaka 2019 kuwa ni aina ya virusi vya ‘corona’ lakini mengi kuhusu ugonjwa huo bado hayajajulikana. ‘Corona virus’  ni ugonjwa ambao huathiri  mfumo mzima wa pua, macho, koo na karibu na paji la uso na hivyo kumfanya mgonjwa apate homa kali na zaidi kushindwa kupumua. Pamoja na kwamba ugonjwa huo unasadikika kuanzia katika soko la vyakula vya baharini, Serikali na wataalamu wa afya bado hawajabaini ni kwa namna gani ulisambaa. Taarifa hizi mpya zimekuja ikiwa ni mwishoni mwa wiki iliyopita wanasayansi wa Uingereza walilidokeza Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kwamba ugonjwa huo mpya ulioibuka nchini China umeathiri mamia tofauti na idadi inayotolewa na maofisa wa serikali nchini humo. Wataalamu hao wa Uingereza wanasema wanakadiria kuwa idadi ya walioathirika inaweza kukaribia 1,700. Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko, Profesa Neil Ferguson, amesema ana wasiwasi idadi ikawa ni kubwa zaidi. Singapore na Hong Kong  wamekuwa wakiwachunguza abiria wanaotoka Wuhan na Marekani pia imetangaza kuchukua hatua kama hizo katika viwanja vya San Francisco, Los Angeles na New York. Taarifa zinaeleza kuwa wakati mlipuko wa ugonjwa huo ukitajwa kuanzia Wuhan, kesi mbili zinazohusu ugonjwa huo zimeripotiwa katika nchi za Thailand  na moja nchini Japan “Hii inasababisha wasiwasi,” alisema Prof. Ferguson. Aliongeza kuwa: “Wuhan kupeleka kesi tatu katika nchi nyingine inamaanisha kwamba huenda kuna kesi zaidi ambazo hazijaripotiwa.” Alisema japo inaweza kuwa ni vigumu kupata idadi kamili lakini kutokana na ugonjwa huo kuenea kwa virusi na mazingira ya nchi yenyewe yenye idadi kubwa ya wananchi na idadi ya wasafiri wa ndege hilo linaweza kutoa taswira nini kinaendelea. Pamoja na hayo Prof. Ferguson alisema ni mapema mno kutangaza hali ya hatari. Mamlaka za nchini China zimesema hakuna kesi yeyote ya virusi hivyo kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Badala yake wamesema kuwa virusi hivyo vimetoka kwa wanyama walioathirika kutoka katika soko la vyakula vya baharini na wanyama la Wuhan. Taarifa hizi mpya zimekuja ikiwa ni takribani wiki mbili zimepita tangu mamlaka ya China ianzishe utafiti kuchunguza virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa ajabu ambao umewaambukiza watu kadhaa katika mji wa Wuhan. Ugonjwa huo ulizua hofu mtandaoni na kuhusisha virusi hivyo kuwa unaweza kusababisha kuwa na mtindio wa ubongo na madhara mengine yanayoweza sababisha vifo. Awali ilidaiwa kuwa kuna uwezekano wa ugonjwa huo kufanana na ugonjwa wa ‘sars’ ambao uliua watu zaidi ya 700 ulimwenguni kote mwaka 2002-03, baada ya kutokea nchini China. Shirika la Afya duniani la WHO lilisema linaangalia kwa karibu mlipuko huo na itaweza kutoa taarifa zaidi watakapozipata.
afya
NORA DAMIAN, DAR Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA RAIS Dk. John Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (Standard gauge), kutoka Dodoma hadi Morogoro, huku akisema anataka Tanzania iwe kama Ulaya, kwamba mtu anaweza kufanya kazi Dodoma na kuishi Dar es Salaam. Akizindua reli hiyo, alisema miundombinu imara ya usafiri ni kichocheo muhimu cha ukuaji uchumi katika nchi na kwamba bila miundombinu hiyo ni ndoto kupata maendeleo. “Kukosekana kwa miundombinu imara na ya uhakika, imesababisha gharama za usafiri kuwa juu kulinganisha na maeneo mengine duniani,” alisema Rais Magufuli. Alisema wastani wa bei ya kusafirisha kontena moja la futi 20 kwenye nchi za Afrika Mashariki umbali usiozidi kilomita 1,500 ni Dola za Marekani 5,000 na kwamba bei hiyo ni sawa na gharama ya kusafirisha kontena lenye ukubwa kama huo kutoka China hadi Tanzania umbali wa kilomita 9,000. “Tafiti zinaonyesha pia kukosekana kwa miundombinu imara ya usafiri kunashusha pato la nchi za Afrika kwa asilimia kati ya moja na mbili na kuongeza gharama za usafirishaji kwa asilimia 40. “Hali hii inasababisha nchi zetu zishindwe kushindana na nchi zingine katika masuala ya biashara, uwekezaji na maendeleo ya viwanda,” alisema. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) ya 2015 kuhusu usafiri wa reli, inaonyesha usafiri wa reli ni muhimu kwani ni mhimili mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na usipoboreshwa, Afrika haitaweza kutumia rasilimali na utajiri ilionao. Alisema utendaji kazi wa reli zilizopo sasa si wa kuridhisha kutokana na uwekezaji mdogo na ubovu wa miundombinu na matatizo ya uongozi yaliyokuwapo. “Siku za nyuma reli hii ilibinafsishwa kwa kampuni moja na ilikaa kwa miaka zaidi ya mitano, lakini hakuna ilichofanya,” alisema.   FAIDA RELI YA KISASA Magufuli alisema nchi yoyote ili iweze kujitegemea, ina wajibu wa kumiliki vitu muhimu kama reli, bandari, nishati, barabara, mawasiliano na vingine. Alisema ujenzi wa reli ya kisasa utaongeza tija na ufanisi katika usafiri wa reli nchini kwani utarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria. “Mtu atasafiri kwa kutumia saa tisa hadi Mwanza kutoka saa 36 kwa kutumia usafiri wa reli uliopo sasa, itaongeza biashara hapa nchini na nchi jirani,” alisema. Alisema kati ya nchi nane ambazo Tanzania inapakana nazo, sita hazina bahari na zinategemea kusafirisha mizigo kupitia hapa nchini. “Itaimarisha biashara kati ya nchi yetu na nchi za Burundi, DRC, Rwanda na Uganda. Itasaidia kutunza barabara na kupunguza gharama za kuzikarabati mara kwa mara. “Itakuza sekta zingine za kiuchumi kwani nyingi zinategemea miundombinu ya usafiri wa uhakika. “Nchi nyingi zimeshindwa duniani, zinakopa halafu zinapewa masharti makubwa, wapo wengine wamejaribu lakini wamejenga ya ovyo tu,” alisema. Alitoa wito kwa Wizara ya Ujenzi, mshauri msimamizi na mkandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.   VYUMA KUKAZA Alisema ujenzi wa kilomita 726 za reli ya kisasa utatoa ajira 30,000 za moja kwa moja na 600,000 zisizo za moja kwa moja zitatolewa, hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini. “Suala la ajira tumelijibu kwa vitendo kwa kuwa na miradi mikubwa kama hii, hivyo nawaomba Watanzania msichague kazi. “Serikali inahamia Dodoma na mimi mwaka huu nahamia, fursa nyingi zimekuja hasa za ujenzi. “Mkandarasi akishaanza hapa, nitashangaa sana kama wananchi wa Ihumwa watakuwa hawaji kufanya kazi, vya bure hakuna na asiyefanya kazi asile na asipokula afe, hii ndiyo lugha ya ukweli na siku zote tutawaambia ukweli. “Kama kuna miradi yote hii halafu awepo mtu analalamika njaa, vyuma vimebana, amejibanisha yeye mwenyewe vyuma, avifungue kwa kufanya kazi,” alisema. Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.  
kitaifa
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana ilisema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake iwapo atarudia kufanya tukio la aina hiyo.Mapunda alifanya hivyo katika mechi hiyo ambayo timu yake ilishinda kwa bao 1-0 ambapo aliingia uwanjani na taulo hilo akilazimisha kulining’iniza golini, lakini mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro alimtaka aliondoe na ndipo alipokwenda kulitundika kwenye moja ya mabango yaliyokuwa na matangazo ya wadhamini wa ligi hiyo kabla ya kutakiwa tena kulitoa ambapo aliamua kulitandika pembeni ya goli.Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari jana, maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kilichoketi Machi 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kupitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu.Mbali na Mapunda, wachezaji Haruna Niyonzima na Dan Mrwanda wa Yanga, mchezaji wa Azam FC Salum Abubakar na mchezaji wa JKT Ruvu Richard Maranya wamepigwa faini ya Sh 500,000 kila mmoja kwa makosa tofauti waliyofanya katika michezo yao mbalimbali ya Ligi Kuu bara.Aidha, tuhuma inayomhusu mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe kwa kitendo cha kumshika korodani beki wa Simba, Juuko Murshid zimepelekwa kwenye Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Niyonzima alipigwa faini hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 37(f) kwa kupiga teke meza ya mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Machi 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Aidha, Mrwanda alipigwa faini hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 14(12) kwa kutopeana mikono na wachezaji wa timu ya Simba, huku Abubakar wa Azam na Maranya wa JKT Ruvu wakipigwa faini hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) kwa kupigana uwanjani kwenye mechi namba 123 ambapo walitolewa nje kwa kadi nyekundu.
michezo
PARIS, UFARANSA UONGOZI wa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa, PSG, unaripotiwa kuwa kwenye mipango ya kutaka kumpiga faini mshambuliaji wao Neymar de Santos kitita cha pauni 340,000, ambazo ni zaidi ya milioni 972 za Kitanzania kutokana na kuchelewa kuripoti kambini. Wachezaji wa timu hiyo walitakiwa kuripoti mapema wiki hii na tayari wengi wao wamewasili jijini Paris kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, lakini Neymar raia wa nchini Brazil hadi sasa hajawasili na hakuna taarifa yoyote alioitoa juu ya kuchelewa kwake. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la nchini Hispania, mchezaji huyo atakatwa bonasi yake ya pauni 340,000 ambayo alitakiwa kuchukua Julai kwa sababu hadi sasa hajajiunga na mabingwa hao. Fedha hizo ambazo atakatwa Neymar, moja kwa moja zitaingia kwenye mfuko wa timu hiyo wa kusaidia mambo mbalimbali ya maendeleo ya soka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akionekana nyumbani kwao nchini Brazil hasa katika michuano ya Copa America ambayo imemalizika wiki iliopita kwa Brazil kushinda mabao 3-1 dhidi ya Peru, lakini Neymar hakucheza hata mchezo mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeruhi wakati wa maandalizi ya michauno hiyo. Neymar alijiunga na PSG mwaka 2017 akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania, Barcelona kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 198 na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha katika historia ya soka. Hata hivyo, kwa sasa mchezaji huyo anaonekana kuwa na uhusiano mbaya na uongozi wa timu yake ya PSG na kufikia hatua ya kutangaza kuwa anataka kuondoka wakati huu wa uhamisho wa wachezaji. Mchezaji huyo anahusishwa kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona, lakini awali kulikuwa na taarifa kwamba anaweza kwenda kujiunga na kikosi cha kocha Zinedine Zidane, Real Madrid.
michezo
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM WEKUNDU wa Msimbazi Simba kama wataamua kuleta mzaha katika usajili wa dirisha dogo, basi isahau suala la kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba ambayo inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo, bado haijawa kwenye fomu yake kama ilivyokua misimu mitatu iliyopita, licha ya kujitutumua kutaka kurudi kwenye nafasi mbili za juu ambazo ilikua ikipishana na mahasimu wao Yanga. Timu hiyo ina nafasi mbili pekee za kuweza kuongeza wachezaji kwenye usajili huu wa dirisha dogo, hivyo wanahitaji kuwa makini katika kupata wachezaji hao. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya klabu hiyo, Said Tully, alisema hawataki kufanya usajili ambao utawagharimu na kuweza kukwamisha harakati zao za kumaliza katika nafasi nzuri kwenye ligi kuu msimu huu. “Tumekuwa kimya tukitafakari wachezaji tutakaowaongeza katika nafasi hizo, tunataka kujiridhisha hasa na aina ya wachezaji tutakaowasajili kabla ya kuwapa mikataba. “Tutafanya usajili wetu kwa kushirikiana na kocha ili kuongeza wachezaji ambao ataridhika na kiwango chao, hatutasajili bila yeye kuridhika kwani tunaweza kusajili mshambuliaji kumbe yeye hitaji lake ni kwa beki hivyo tutakuwa hatumsaidii,” alisema. Simba kabla ya ligi kuanza ilikua na hitaji la mshambuliaji, matokeo yake wakaleta washambuliaji ambao hawakidhi haja ya timu. Awali walimleta Msenegal, Papa Niang, ambaye hakufanya vizuri akatupiwa virago vyake na kuondoka, ndipo akasajiliwa Msenegal, Pape N’daw ambaye hadi sasa ameonekana garasa na anatajwa kutemwa katika usajili wa dirisha dogo na Mganda Simon Sserunkuma. Wakati uongozi unajipanga hayo tayari mchezaji Paul Kiongera amepewa asilimia kubwa za kutua kwenye kikosi hicho ikiwa ni kuziba nafasi ya Simon Sserunkuma ambaye tayari ameshatemwa rasmi kuchezea kikosi hicho huku Pape N’daw naye akiwa njiani kutemwa.
michezo
JESHI la Polisi mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Muungano wa Jamii Tanzania (Mujata), wameandaa ziara ya pamoja katika wilaya zote mkoani hapa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kupinga vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji na ukatili wa kijinsia.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei, msukumo wa ziara hiyo unatokana na vitendo mbali mbali vya uhalifu vilivyotawala ndani na nje ya mkoa huo ikiwemo mauaji ya watoto yaliyotokea kwa mfululizo hivi karibuni katika mkoa jirani wa Njombe. Kamanda Matei alisema ziara hiyo itajumuisha wajumbe kutoka Mujata na maofisa wa jeshi hilo wakiwemo wakuu wa polisi wa wilaya na italenga zaidi kutoa elimu kwa jamii.“Baada ya yale matukio ya Njombe, tumeona tushirikiane na Mujata kupita katika kila wilaya ili kutoa elimu. Si mauaji ya Njombe tu hata hapa kwetu tuna tatizo la lambalamba…tumewakamata wengi, lakini kukamata pekee haitoshi tunapaswa kutoa elimu.“Tumekuwa tukiwafikisha mahakamani, lakini haisaidii sana, ni muhimu jamii ikatambua athari zitokanazo na vitendo hivi, yapo pia mauaji ya watu kujichukulia sheria mikononi. Haya yote jamii inapaswa ielimishwe ili itoe ushirikiano,” alisema Kamanda Matei. Kamanda Matei alisema kwa kuwa Mkoa wa Njombe ni jirani na Mbeya, ameona kuna kila sababu ya kukaa na jamii na kuzungumza nayo sambamba na matukio ya waganga wa jadi wapiga ramli maarufu kwa jina la lambalamba ambayo yamekithiri mkoani hapa.Kamanda Matei alisema ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na Mujata haukuanza leo wala jana, bali pande zote zimekuwa zikishirikiana kwa pamoja katika kukemea uharifu na zitaendelea kufanya hivyo. Ili kufikia malengo ya ziara hiyo, kamanda huyo aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi pale watakapofikia na wajumbe kutoka Polisi na Mujata ili wapate elimu na hatimaye kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale watakapoona kuna dalili za uvunjifu wa amani na utulivu.
kitaifa
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
uchumi
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua kongamano la Wiki ya Uwekezaji Kagera leo pamoja na kitabu za mwongozo wa uwekezaji mkoani humo, ambapo jumla ya wadau wa biashara na uwekezaji 300 watashiriki.Kati ya washiriki hao magavana wa majimbo ya nchi zilizo mpakani mwaka mkoa wa Kagera kutoka Burundi, Rwanda na Uganda pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.Pamoja na hayo, Mkoa wa Kagera umepanga kuanzia mwezi Novemba kuanza kufanya ziara katika nchi za jirani zinazopakana na mkoa huo, Burundi, Uganda, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), kwa ajili ya kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji katika nchi hizo.Hayo yalielezwa mjini Bukoba jana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akizungumzia kuanza kwa maonesho hayo juzi na maandalizi ya uzinduzi wa wiki hiyo unaofanyika leo mjini hapa.“Maonesho yanaendelea na yameanza jana (juzi), leo (jana) tunatarajia kupokea wageni kutoka nchi zinazotuzunguka kutoka DRC, magavana kutoka Burundi, Rwanda na Uganda na wafanyabiashara kutoka Rwanda na DRC,” alisisitiza.Mkuu huyo wa mkoa alisema jambo kubwa ni kwamba leo kutakuwa na ugeni maalumu wa Waziri Mkuu Majaliwa ambaye pamoja na kuzindua rasmi wiki hiyo ya uwekezaji Kagera pia atazindua kitabu maalumu cha mwongozo wa uwekezaji Kagera.“Kitabu hiki kimeanisha fursa zote za uwekezaji na biashara zinazopatikana mkoani hapa. Kinatoa mwongozo wa namna ya kuwekeza na kuanzisha biashara,” alieleza Gaguti.Akielezea mkutano wa juzi uliowakutanisha mabalozi watano wa Tanzania katika nchi za EAC, Burundi, DRC, Uganda, Kenya na Rwanda, alibainisha kuwa mkutano huo umezaa matunda mazuri kwani umehuisha maeneo yenye fursa zinazopatikana katika nchi hizo.Alisema ndio maana kupitia mkutano huo wamekuja na maazimio ya ofisi ya mkoa kuungana na jamii ya wafanyabiashara wa Kagera kufanya ziara maalumu katika nchi hizo za EAC kujionea fursa hizo na namna ya kuzitumia. Alisema tayari wameshapanga tarehe ya kufanya ziara hiyo ambayo ni wiki ya tatu ya mwezi Novemba mwaka huu.“Dhamira kubwa ni kwamba hatuna muda wa kupoteza, wakati ni sasa ni lazima tujikite katika kutumia masoko haya katika nchi zinazotuzunguka zenye watu takribani milioni 190,” alisisitiza.Aidha, alieleza kuwa pia mkoa huo umejipanga kuhakikisha unakuwa kitovu cha biashara kanda ya ziwa kwa kuanzisha masoko ya mipakani ambayo bidhaa zote za Tanzania ikiwemo Kagera zitapatikana.“Tunataka kufanya Kagera kuwa hub ya biashara katika kanda ya ziwa. Na ili tuwe hub ni lazima tuwe na masoko ya mipakani. Sisi tuna mipaka ya ardhini mitatu Burundi, Rwanda na Uganda, ukiacha huo wa majini kwenda Kenya, pia tunaweza kufikia nchi za Sudan Kusini na DRC,” alisema.
kitaifa
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM MTANZANIA Mbwana Samatta, anayekipiga katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amebakisha mabao mawili tu kuweza kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu. Mpaka sasa timu yake ikiwa imeingia fainali ya michuano hiyo, Samatta anashika nafasi ya pili kwenye chati ya ufungaji bora akiwa na mabao sita, sawa na Mouhcine Iajour wa timu ya Moghreb Tetouan ya Morocco iliyotolewa, anazidiwa bao moja tu na kinara Bakri Al-Madina anayekipiga El Merreikh ya Sudan aliyetupia saba. TP Mazembe inatarajia kucheza na USM Alger ya Algeria katika fainali ya michuano hiyo, mchezo wa kwanza utafanyika kati ya Oktoba 30 na Novemba mosi, mwaka huu huku wa marudiano ukifanyika kati ya Novemba 6 na 8 mwaka huu. Mshambuliaji huyo, 23, ana nafasi ya kumzidi Al Madina kama atafanikiwa kufunga mabao mawili katika mechi mbili zijazo za fainali watakazocheza dhidi ya USM Algier. Wachezaji wanaoweza kuyafikia mabao ya Samatta ni mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe, Roger Assale, aliyefunga matano, Youcef Belaili (USM Algier) aliyetupia manne sambamba na Kaddour Beldjilali na Mohamed Meftah (USM Alger) waliotupia matatu kila mmoja. Mwaka jana mshambuliaji mwingine wa Tanzania, Mrisho Ngassa, aliyekuwa akikipiga Yanga alikuwa ni miongoni mwa wafungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake sita, akilingana na wenzake watatu, El Hedi Belameiri (ES Setif, Algeria), Haythem Jouini (Esperance, Tunisia) na Ndombe Mubele (AS Vita, Kongo). Samatta anayecheza TP Mazembe sambamba na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu, wana nafasi ya kuandika rekodi ya kuwa Watanzania wa kwanza kutwaa ubingwa huo mkubwa wa Afrika kwa ngazi ya klabu kama wataifunga USM Algier.
michezo
WAZEE wa jamii ya Kalenjin wamewataka viongozi wakuu wa jamii hiyo katika mbio za urais wa mwaka 2022, Naibu Rais, William Ruto na Seneta wa Baringo, Gideon Moi kuzika tofauti mbio za kuwania urais uchaguzi ujao.Wazee wa kabila la Kalenjin wameanza kupata hofu kuwa tofauti za viongozi hao huenda zikaleta madhara katika uchaguzi ujao kwa upande wa mgombea kutoka kabila hilo. “Tofauti zao zinatuweka katika hatari ya kukosa urais mwaka 2022, hivyo tumeamua kuwaweka chini na kuwasihi wamalize tofauti zao na kuwa kitu kimoja, wote watoto wetu,” alisema Meja mstaafu John Seii, kiongozi wa wazee hao. Seii aliwalalamikia Ruto na Gideon ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Kenya, Mzee Daniel arap Moi kwa kuwa wabishi na kutotaka kusikiliza wazee wa jamii yao wanapowashauri.“Hawa wote ni watoto wetu lakini wameamua kutokutusikiliza tunachowaambia. Tumejaribu kuwasiliana na makatibu wao tuweze kukutana ana kwa ana na wakati mwingine tumejaribu kukutana katika mikutano ya hadhara, lakini juhudi hizo zimekwenda mrama,” alisema Seii. Sababu ya kushindwa kukutana na viongozi hao inatajwa na wazee hao kuwa ni kutokana na watu wanaoandamana nao wanaozidisha ugomvi wa maneno. “Kama wangekuwa peke yao ungekuta tumeshakutana nao,” alisema Seii.
kitaifa
Na David Andy Kuna msemo usemao “dhahabu safi ni lazima ipite motoni,” msemo huu unatukumbusha katika maisha kuwa hakuna aliyefanikiwa bila kupitia changamoto. Safari ya Taifa Stars imefika ukingoni lakini siyo mwisho wa mapigano. Kuna kitu kikubwa kama Taifa tumejifunza kutoka katika michuano ya AFCON nchini Misri: hakuna njia fupi katika mafanikio. Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa katika morali ya hari ya juu sana, ijapo matokeo hayakuwa ya kuridhisha. Kauli aliyoisema naodha wa Stars, Mbwana Samatta, baada ya mechi ilikuwa ni ya kiungwana sana alisema, “Moja ya jambo kubwa lililotufanya kukosa ushindi siku ya leo, ni kukosa umakini na kushindwa kulinda ushindi” Binafsi, napenda sana kuwapongeza vijana wa timu ya taifa. Uwepo wao nchini Misri tutaukumbuka ijapo si kwa muda mrefu. Hakuna aliyependezwa na matokeo waliyopata Taifa Stars katika michuano ya AFCON nchini Misri, lakini hatuna budi kushukuru ata kwa uwepo wetu katika michuano hii mikubwa. Nini kifanyike baada ya Mmichuano ya AFCON Kama taifa, ni vizuri sana vijana hawa wakirudi nchini wafanyiwe sherehe na wapongezwe kwa jitihada walizozionyesha wakiwa katika mashindano haya, pia wasisahau kuwapa motisha mbalimbali vijana ili wasikate tamaa. Jambo la pili ambalo ndio haswa limepelekea niandike makala haya, ni kuomba wadau wa mpira wa miguu kufanya tathmini ya baada ya michuano (Post tournament evaluation). Ni muda wadau mbalimbali wa michezo kuanzia Wizara, TFF, serikali, pamoja na washabiki wa soka nchini kufanya tathmini nini kifanyike. Michuano ya AFCON isiishe nchini Misri, tunatakiwa kuanza pale tulipoishia. Mara nyingi kinachotufelisha kama nchi katika sekta zote ni kuanza upya. Badala ya kuanzia pale waliotutangulia walipoishia, kila anayepokea anataka kuanza upya. Kitaalamu (Benchmarking) ni mbinu ambayo hutumiwa na watalaam, kuokoa fedha, rasilimali pamoja na muda (kuanza pale ulipoishia). Tunachotakiwa hivi sasa ni kutengeneza sera safi ya michezo; sera hii itakuwa na mikakati ya muda mrefu na muda mfupi. Mikakati ya muda mfupi iwepo kuhakikisha tunakuwa hatupwayi sana tunapotekeleza mikakati ya muda mrefu. Kamati za hamasa, michango pamoja na ushindi, ziundwe kutoka chini zisijitokeze tu pale timu fulani au mwanachezo fulani wanapofanya vizuri. Tunaitaji kuwa na wanamichezo ambao washindani (competitive) tuhakikishe tunawapata kwa kuwa na shule safi kuanzia kwenye ngazi ya klabu, uwekezaji pamoja na serikali. Pia timu inapokuwa katika mashindano, sisi kama taifa tunatakiwa kuwa wamoja. Yaliyoliyojitokeza baada ya wabunge kwenda nchini Misri na baadae kurudi nchini hayakuwa yanafurahisha. Wote tunajua kuwa lengo kuu lilikuwa ni kuwapa vijana motisha lakini mgawanyiko uliojitokeza baina ya viongozi wa serikali pia ulikuwa na athari kwa timu ya taifa; tujitahidi sana haya yasijitokeza tena. Mwalimu Amunike, amesisitiza taifa linaitaji kuwa na wachezaji wengi ambao wanashiriki katika ligi zenye ushindani ndani ya Afrika na nje ya mipaka ya Afrika tusipuuze maoni yake mfano mzuri ni siku ya jana. Sote tuliona jinsi gani kikosi cha Algeria kilivyopendeza kutokana na idadi ya wachezaji wengi ambao tunawaona katika timu kubwa balani Ulaya. Yote haya yanawezekana kama tukiweka mikakati ambayo haibadiliki kila wakati. Maandiko yanatuasa kushukuru kwa kila jambo basi nasi hatuna budi kushukuru kwa hili kubwa ambalo Taifa Stars wamejaribu kulifanya tunawatakia mema tukutane tena AFCON ijapo hatujui ni lini. David Andy ni mzalisha maudhui kupitia mitandao na blogu anapatikana kupitia email: [email protected], Instagram : @davidandy2001
michezo
“Mechi ilikuwa ngumu sana,Toto African walianza vizuri kipindi cha kwanza, tulitengeneza nafasi nne au tano hivi lakini tulishindwa kutumia, tumepigana kwa nguvu sana kusawazisha goli lakini yote sawa wachezaji wangu wamecheza vizuri na tumeweza kushinda,” alisema.Pluijm alimpongeza kiungo wake Haruna Niyonzima kwa kiwango kizuri alichoonesha katika mechi hiyo.Pluijm alisema walijitahidi kupigana ili kusawazisha goli katika dakika za mapema kutokana naToto kuonesha kila dalili ya kutaka kushinda toka mapema.Pluijm aliwapongeza Toto kwa mchezo mzuri waliocheza na kusema walicheza kwa kiwango kikubwa kulinganisha na ile mechi ya kwanza ambayo Yanga ilishinda mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Pluijm alisema goli walilofungwa Yanga na Toto ni jepesi na ameshangaa kwa nini kipa wake Deogratias Munishi ameruhusu goli la vile.Akielezea maandalizi dhidi ya mechi na Stand United, Pluijm alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu lakini anachoshukuru ni kuwa hakuna majeruhi.Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Toto, Dominik Glawogger alisema mechi dhidi ya Yanga ilikuwa ngumu kwa kuwa Yanga ina wachezaji wazuri wengi na wenye uwezo mkubwa.“Tulicheza vizuri sana haswa kipindi cha kwanza na tukaweza kupata nafasi ya kufunga na kuitumia vyema, kipindi cha pili tulijitahidi kutengeneza nafasi lakini hatukutumia nafasi zetu,” alisema. Glawogger amewaomba wachezaji wa Toto kusahau matokeo ya Yanga na kujiandaa na mchezo dhidi ya Prisons.
michezo
Pinda alisema hayo juzi wakati akitembelea banda la asali katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kuwataka Watanzania kutumia bidhaa hizo za asali alizosema ni zaidi ya sukari kwa kuwa ni chakula na tiba.Pinda alisema jamii lazima ijenge mazoea ya kutumia asali kwa kuwa ni tiba ya magonjwa mengi hatarishi.Aliwataka wafugaji wa nyuki kupata elimu ya kutosha jinsi ya kufuga nyuki na kurina asali ili kupata mazao mengi stahili. Pinda alisema amepata faraja baada ya kutembelea banda hilo na kukuta wafugaji hao wamebadilika hasa katika vifungashio kwa kuachana na ufungaji wa kienyeji.“Nashukuru nimeona mabadiliko makubwa hasa kwa wafugaji wa nyuki tofauti na mwaka jana na ningependa kwani wengi wamefikia viwango vya kimataifa kwa kuwa na nembo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),” alisema Pinda.Alisema asilimia 90 ya mazao yanayolimwa nchini yakiwemo mahindi, ukuaji wake unasaidiwa na nyuki, hivyo kuongeza kilimo cha asali kutasaidia pia ukuaji wa mazao mengine kwani mazao yote yenye maua yanategemea nyuki hivyo watajitahidi kulinda misitu.Alisema katika nchi za Afrika nchi inayoongoza kwa kilimo cha asali ni Ethiopia na kwa duniani ni China na Marekani.
uchumi
THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM UONGOZI wa Yanga, umesema una uhakika wa kuwatandika watani wao wao wa jadi, Simba, lakini umewataka waamuzi kuhakikisha wanachezea  kwa haki bika upendeleo. Yanga na Simba zinatarajia kushuka dimbani kuumana , katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Marchi 8 mwaka huu, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kwanza matokeo baada ya  dakika tisini kukamilika yalikuwa sare ya mabao 2-2. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Alliance ambao Wanajagwani walishinda mabao 2-0 juzi Uwanja wa Taifa, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugas, alisema safari hii hawatafanya makosa ya mchezo wao kwanza zaidi ya kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao hao. “Tumejipanga vizuri , tuna uhakika tutapata ushindi mnono nachowaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi katika mchezo huu ukizingatia sisi ndio tutakuwa wenyeji. “Lakini pamoja na yote tunawaomba Waamuzi watakaopangwa wachezeshe kwa haki ili mshindi apatikane kwa haki,” alisema. Alisema dalili nzuri imeanza kuonekana katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance ambao walipata ushindi wa mabao 2-0, hivyo wanaamini burudani hiyo kuendelea kwa mara nyingine. Nugas aliwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia ufundi utakaonyeshwa na wachezaji wao wakiwemo Benard Morrison ambaye amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika mechi zao.
michezo
MASHABIKI wa Manchester United wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuachana na kiungo wao, Paul Pogba, mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, kutokana na mchezaji huyo kuonesha mapenzi na klabu ya Real Madrid. Mapema wiki hii, mchezaji huyo alishindwa kuzuia hisia zake na kuweka wazi kuwa, ndoto zake siku moja ni kuja kuwa mchezaji wa Real Madrid, huku akidai kila mchezaji ana ndoto za kuitumikia timu hiyo kutokana na ukubwa wake. Mashabiki hao wanaamini mchezaji huyo ana lengo la kutaka kuungana na kocha Zinedine Zidane, ambapo wote wanatoka nchi moja, Ufaransa. “Kama ninavyosemwa kila siku, Real Madrid ni sehemu ya ndoto kwa kila mchezaji. Ni moja kati ya klabu kubwa duniani, hasa kwa sasa Zidane ndiye kocha wao, hivyo kila mchezaji anatamani kuja kuitumikia timu hiyo kwa wale ambao wanapenda soka. “Lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa Manchester United, hatujui nini kinaweza kutokea hapo baadaye, nipo Manchester United na nina furaha kuwa hapa,” alisema Pogba. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa anahusishwa kuwindwa na klabu zote, Real Madrid na Barcelona. Hivyo kutokana na kauli hiyo, inaonekana kumuweka katika wakati mgumu hasa kwa mashabiki wa timu hiyo, ambao wanadai ni vizuri akaondoka kwa kuwa tayari ameonesha mapenzi ya wazi na Madrid. Pogba alianza kutangaza nia ya kutaka kuondoka Manchester United tangu alipopishana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho na kumfanya mchezaji huyo akose namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini baada ya kuondoka kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer, Pogba amekuwa akipata nafasi ya kudumu, lakini bado mashabiki wanautaka uongozi kuachana na mchezaji huyo.
michezo
    Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM MTOTO Shukuru Kisonga (16) ambaye ameishi muda mrefu kwa kula sukari robo tatu, mafuta ya kula lita moja na maziwa lita tatu, amesema ndoto yake ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu. Shukuru alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA kuhusu maendeleo ya afya yake na kuongeza kuwa ataongeza juhudi katika masomo yake afikie ndoto yake hiyo. "Niliteseka muda mrefu, namshukuru Mungu sasa sijambo naendelea na matibabu wodini, nikiruhusiwa kurejea nyumbani nitaongeza juhudi katika masomo yangu nitimize ndoto yangu ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu, " alisema. Shukuru alisema anataka kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu   awasaidie watu wengi hasa wanaoteseka na ugonjwa kama unaomsumbua yeye. " Namshukuru daktari wangu hapa Hospitali ya Taifa Muhimbili, amenisaidia mno ndiyo maana na mimi ninataka kuwa kama yeye   niweze kuwasaidia wengine wanaougua Mungu akinijalia, " alisema. Daktari Bingwa wa magonjwa ya damu, Stella Rwezaula, juzi alisema mtoto huyo anaugua selimundu, ugonjwa ambao amezaliwa nao baada ya kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi wake.  
afya
AVELINE KITOMARY NA ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM  ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 77341 Johanes Kubambi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa shtaka la kuomba rushwa ya Sh 700,000. Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Wakili wa Takukuru, Vera Ndeoya, alidai kuwa katika ofisi za jeshi la akiba, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa aliomba rushwa kwa Kelvin Fabian ili aweze kumpatia nafasi ya mafunzo ya jeshi. Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Ndeoya alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine. Hata hivyo, Hakimu Kiliwa alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao sio wanajeshi wala polisi na wawe na barua zinazotambulika kisheria, watakaotoa bondi ya Sh milioni 1 kila mmoja. Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Juni 28 kwa ajilii ya kutimiza masharti ya dhamana. Wakati huo huo, Takukuru imempandisha kizimbani mfanyabiashara wa Kariakoo, Husen Khimji (41) kwa shtaka la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Wakili wa Takukuru, Lupyana Mwakatobe, aliiambia mahakama kuwa Januari 22 maeneo ya Pub ya Junction, Khimji kwa udanganyifu alijipatia kiasi cha Sh 300,000 kutoka kwa Fatuma Mshumbuzi akimdanganya kumsaidia kumuwekea dhamana katika Mahakama ya Kisutu. Mshtakiwa alikana madai hayo na Wakili Mwakatobe alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena. Hakimu Joyce Mushi alisema dhamana kwa mshtakiwa iko wazi kwa kuwa na wadhamini wawili watakaokuwa na vitambulisho vya taifa watakaosaini bondi ya Sh 500,000. Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Julai 9.
kitaifa
['Timu ya kandanda ya taifa Stars kutoka tanzania imeiondoa timu ya harambee Stars kutoka kenya katika mashindano ya CHAN 2020', 'Timu ya Kenya Harambee Stars ilidondoka katika michuano ya kufuzu kombe la CHAN 2020 baada ya kupoteza kwa Tanzania taifa Stars 4-1 kupitia mikwaju ya penalti katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi baada ya kutoka sare 0-0 katika dakika 90 za mchezo. ', 'Mkufunzi wa Harambee Sebastien Migne alichagua washambulia waliokuwa na kasi akiwemo Samuel Onyango na Duke Abuya lakini hawakuweza kucheka na wavu, na ilipofikia majira ya penalti Taifa Stars ilithibitisha kwamba wao ndio magwiji watakaoelekea Camroon ambapo michuano hiyo itachezwa mwezi Januari.', 'Harambee Stars walikuwa wametoka sare ya 0-0 siku ya Jumapili iliopita mjini Dar es Salaam na kufuatia ushindi huo Taifa Stars sasa itakutana na Sudan katika raundi ya pili na ya mwisho ya kufuzu.', 'Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars. ', 'Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.', 'Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars. ', 'Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.', 'Iddi Alli alikosa bao la wazi kufuatia uvamizi wa Taifa Stars katika lango la Kenya baada ya Isuza kupokonywa mpira.', 'Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare tasa lakini Harambee Stars ilikaribia kufunga katika kipindi cha pili baada ya Miheso wa Kenya kuvamia lango la taifa Stars.', 'Tanzania ilikaribia kufunga kupitia mshambuliaji wake Mkudde lakini ulinzi mzuri wa Miheso ulimzuia mshambuliaji huyo matata.', 'Kunako dakika za mwisho Mkudde alivamia tena lango la Harambee Stars baada ya kumpokonya mpira Oyemba wa Kenya na kusalia na goli lakini mshambuliaji huyo mrefu wa Tanazania akapiga nje.']
michezo
Halmashauri ya Mji Kibaha imesema ina fursa ya kipekee kwa biashara ya uwekezaji kutokana na jiografia yake ukiwemo ukaribu wake na bandari ya jiji la Dar es Salaam na uwepo wa bandari kavu.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Jennifer Omollo amesema ofisini kwake mjini Kibaha kuwa, mji huo upo umbali wa takribani kilomita mbili kutoka jiji hilo kuu la kibiashara Tanzania.Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.Maonesho hayo yatafanyika kuanzia Oktoba Mosi hadi saba kwenye viwanja vyaa CCM Sabasaba Picha ya Ndege, na Kongamano litafanyika Oktoba tatu.“Lakini sisi tupo kwenye barabara kubwa ya Morogoro na sasa hivi ujue Mheshimiwa Rais anajenga barabara ile kwa line sita kwa hiyo usafiri ni rahisi hata kutoka bandarini”amesema Omollo.Amesema bandari kavu iliyopo takribani kilomita nne kutoka mjini Kibaha ni fursa muhimu kwa biashara.“Lakini pia tuna reli ya kisasa inayojengwa na Mheshimiwa Rais hiyo nayo ipo karibu sana na Kibaha” amesema na kuongeza kuwa Kibaha inafikika kwa urahisi kuliko maeneo mengine mkoani humo.Kwa mujibu wa Omollo ukiwa Kibaha ni rahisi zaidi kusafiri na kusafirisha bidhaa kuliko maeneo mengine ya Pwani, na pia huduma nyingine wezeshi kwa biashara zinapatikana na ni za uhakika ukiwemo umeme na maji.
uchumi
Katika mchezo huo uliochezwa usiku, JKT Ruvu ndio waliokuwa wa kwanza kufunga bao mapema lililowekwa nyavuni na Gaudence Mwaikimba ambaye alisajiliwa na timu ya JKT akitokea timu hiyo ya Azam.Aidha, Kipre Tchetche alisawazisha baadaye na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa na sare ya bao 1-1. Kipindi cha pili dakika zikiwa zinaelekea mwishoni mwa mchezo mchezaji wa JKT Ruvu Najim Magulu aliifungia JKT Ruvu bao la pili baada ya beki wa Azam Bryson Raphael kuanguka wakati akijaribu kuokoa na kipa Aishi Manula kupotea na kumpa nafasi mchezaji huyo kufunga kiulaini.Ushindi huo umevunja rekodi ya Azam ambao walionekana kuwa moto kwa kutopoteza mchezo wowote kuanzia michuano ya Kombe la Kagame hadi michezo yao ya kirafiki waliyocheza sehemu tofauti.Kocha Mkuu Hall alikuwa akijaribu kuwapa nafasi vijana ambao wamepandishwa na kupima uwezo wao kutokana na wachezaji wengi tegemeo kuwepo katika kambi ya timu ya taifa.Msemaji wa Azam Jaffar Idd alisema licha ya kupoteza mchezo huo, tayari Kocha ameona mapungufu kwa baadhi ya wachezaji wake hivyo atayafanyia kazi. “Mchezo ulikuwa ni mzuri kila timu ilionyesha kujiandaa vyema, Kocha ameshaona mapungufu tunaamini atayafanyia kazi katika mchezo mwingine wa kirafiki utakaochezwa Ijumaa,” alisema.Azam FC wanatarajiwa kucheza na Ruvu Shooting kesho kwenye uwanja wa Mabatini, timu zote zikijiimarisha kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza wiki ijayo.
michezo
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Rais ameridhia hifadhi tatu mpya kuingizwa katika orodha ya Hifadhi za Taifa.Alibainisha hayo jana wakati akihitimisha na kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika hotuba yake ya makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.“Hapa nina hati kutoka kwa Rais, ameridhia hifadhi mpya tatu kuingia katika orodha ya hifadhi za taifa,” alisema na kuzitaja hifadhi hizo mpya kuwa ni Hifadhi ya Burigi Chato, Hifadhi ya Rumanyika Karagwe na Ibanda Kyerwa. Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla amesema biashara ya kuuza wanyama hai nje imefungwa na haitafanyika tena hata awe mnyama mdogo wa aina gani.“Biashara hii ya kuuza wanyamapori hai nje ya nchini haitafanyika tena, imefungwa, kama bado mimi ni waziri katika wizara hii nimeifunga na sitaifungua na haitafanyika kamwe, hata awe chawa…haijalishi mnyama ana ukubwa gani,” alisema. Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Muheza Adadi Rajabu.Akichangia mada Msigwa aliomba biashara ya kuuza wanyamapori hai irejeshwe kwa kile alichodai waliokuwa wakifanyabiashara hiyo wameingia katika umasikini na wengine kupoteza maisha kutokana na kukosa biashara wakati Adadi akichangia hoja alitaka biashara ya kuuza vipepeo nje ya nchi iruhusiwe.“Hakuna mnyama hai akayetoka na kuuzwa nje ya nchi iwe kwa njia halali au la…naona Msigwa ananiangalia uniangalie tu vizuri, biashara hii imefungwa, hata Adadi pia alichangia lakini uamuzi ndio huo hakuna kipepeo au mnayama hai atatoka nje… kuna vipepeo wanapatikana msitu wa Amani, ni wa kipekee hakuna sehemu wengine tunaendelea kuboresha ili watalii wazaidi wafike kuangalia lakini pia kwenye maporomoko yaliyopo karibu na pale,” alisema.Waziri Kigwangalla alisema kama kuna mtu anafuga wanyamapori wake basi afungue ‘Zoo’ watu waende wakaangalie kwenye hifadhi hizo binafsi, lakini hakuna biashara ya kununua wanyama hapa nchini na kuuzwa nje ya chini hata awe mdogo kiasi gani. Awali wakichangia hoja ya wizara hiyo wabunge walisema utalii ni biashara kubwa, hivyo serikali inatakiwa kutafuta namna ya kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo badala ya kupoteza muda katika kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu.Pia wameitaka serikali kujipanga na kuangalia namna ya kupunguza tozo nyingi ambazo walieleza zimekuwa kikwazo katika sekta hiyo muhimu nchini ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha mapato ya kigeni kwa asilimia 25.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ni nyeti na inahitaji uwekezaji mkubwa, lakini imekuwa ikicheleweshwa na migogoro ya muda mrefu kati ya mamlaka ya hifadhi na wananchi. “Tumekuwa badala ya kufanya biashara ya utalii ni kutatua migogoro tu, tuseme sasa inatosha tufanye biashara kwa kupata suluhisho la kudumu... tuichukulie biashara ya utalii kwa upeo wa kibiashara zaidi kama wenzetu katika nchi nyingine wanavyofanya na tutajiingizia mapato zaidi ya tunayopata sasa,” alisema Msigwa na kuongeza kuwa serikali iangalie haraka mipaka na kumaliza kabisa suala la migogoro ya ardhi.Msigwa pia alizungumzia kukinzana kwa sheria mbali mbali na kusababisha utekelezaji wake kuwa mgumu na kukwamisha mazingira ya kuvutia biashara ya utalii. “Wizara hii inategemewa kuleata mapato, acheni urithi, tunaona kuna sehemu ya kazi inafanyika na mawaziri waliopo sasa... mkiendelea kazi hii nzuri, tutaondokana na hali ya kufukuzana fukuzana katika wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo.Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), alisema sekta ya utalii imekuwa ikichangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa, lakini imekuwa haichukuliwi kwa umakini na kutaka serikali kujipanga kwa kutegemea fedha zake za ndani badala ya wadau wa nje ili kuiingua sekta hiyo.Owenya pia alizungumzia kodi ambazo alizielezea kuwa ni nyingi na kutoa mfano kwenye hoteli wamekuwa wakitozwa kodi na Osha Sh milioni 1.5, Cosota kodi sh milioni 1.5, Nemc Sh milioni 1.5 na taasisi zingine na kuhoji tozo hizo zote fedha zake zinapelekwa wapi na zinafanyia kazi gani ya kumfaidisha mfanyabiashara wa hoteli. Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema anaona kodi ya wizara hiyo ni ndogo na kupendekeza serikali iache maduhuli ya wizara hiyo angalau kwa miaka mitano ili watumie kuendelea kuboreshea wizara ili iweze kufikia mafanikio makubwa zaidi na kuliingizia taifa kipato. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), alichangia alisema tozo zimekuwa nyingi kwa wadau wa utalii na kuwa sekta hiyo haiwezi kuendelea kwa kujaza matozo kwenye biashara ndio maana hazikui. Aliitaka wizara hiyo kuwa na mbinu za kuutangaza utalii wa Tanzania na kutoa mfano wa Malaysia imekuwa ikipata watalii milioni 25 kwa mwaka na kuwa wamekuwa wakitumia vitu vya kawaida tu kutangaza utalii wao. Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba iidhinishiwe na Bunge Sh 120, 202,638, 734 kwa matumizi ya wizara, na kati ya fedha hizo, Sh 71,312, 649,000 ni matumizi ya kawaida na Sh 48,889,988, 734 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
kitaifa
BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na wawakilishi wa kimataifa Simba leo wana kazi nzito ya kusaka ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ya Congo.Kitendo cha kutinga hatua hiyo ni historia nyingine mpya baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2003. Kipindi hicho kutinga hatua ya makundi ilikuwa ndio robo fainali tofauti na sasa mambo mengi yamebadilika kwenye michuano hiyo. Sasa wawakilishi hao wanatamani mafanikio zaidi na nia yao ni kucheza fainali za michuano hiyo. Wekundu hao wa Msimbazi waliwahi kufika hatua hiyo miaka 26 iliyopita mwaka 1993 na tangu hapo uwakilishi wao kwenye michuano ya kimataifa haukuwa wa kuridhisha.Bila shaka kutokana na ubora walionao sasa chini ya mwekezaji wao Mohamed Dewji anayependa mafanikio, kila kitu kinawezekana lakini mtihani walionao ni kuwatoa TP Mazembe. Simba ilibezwa kufika mbali ikadhihirisha mbele ya mashabiki wake na watanzania kwa ujumla kuwa inaweza. Ikahakikisha maadui zake wote hawatambi nyumbani kwake. Ili kuwadhibiti kwa kutumia uwanja wa nyumbani Al Ahly ya Misri anayeogopwa Afrika kwa ubora lakini kwenye uwanja wa Taifa alifungwa bao 1-0, ikampiga AS Vita ya Congo aliyefanya vizuri Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kwa kufika fainali, mabao 2-1, JS Saoura ya Algeria.Hiyo ilikuwa ni harakati za makundi lakini leo wapo katika hatua ya robo fainali hatua ngumu kwa vile ni mtoano. Simba inatakiwa kuendeleza ule moyo wa kushinda nyumbani ila ni muhimu kwao kubadilika kwa kushinda mabao mengi zaidi na kutowapa nafasi wapinzani wao kupata bao la ugenini. Kuna makosa yalifanyika kwa wekundu hao katika mechi tofauti kuanzia hatua ya awali walizocheza nyumbani kwa kuruhusu wapinzani kupata mabao ya ugenini. Dhidi ya Mbabane walishinda 4-1, dhidi ya Nkana 3-1 na dhidi ya Vita 2-1 jambo ambalo ni hatari kwao hasa katika hatua hii waliyofikia sasa ambapo umakini unahitajika.Kingine wamekuwa wakiwadharau Mazembe na kusema msimu huu eti sio bora kama miaka mingine. Kama wangekuwa sio bora wasingefika hatua hii muhimu hivyo, wakiwadharau wanaweza kuwaadhibu kwasababu ni timu yenye uzoefu mkubwa na ina wachezaji wengi wazuri. Mazembe sio mara ya kwanza kuja kucheza katika ardhi ya Tanzania, wanaujua vizuri uwanja wa taifa, Dar es Salaam. Waliwahi kucheza nao mwaka 2011 katika mchezo wa pili hatua ya makundi kwenye uwanja huo Mazembe ikashinda 3-2 na ule wa kwanza uliochezwa kwao ikashinda 3-1.Kwa maana nyingine, mechi hii ni wakati sahihi kwa Simba kulipa kisasi kwa Mazembe. Timu hiyo ya Lubumbashi, Congo tayari itakuwa imeshawasoma wapinzani wake kwa kujua kuwa kumbe inakuwa wakali hasa kwenye uwanja wa nyumbani, wanaweza kuja na mbinu zao nyingine kuwadhibiti wekundu hao. Udhaifu uliopo kwa Simba ni kushindwa kumudu michezo ya ugenini.Takwimu za hatua ya makundi katika michezo iliyopita inaonyesha hawakupata bao hata moja katika michezo mitatu tena wakiruhusu kufungwa mabao mengi. Ukitizama kule Misri ilifungwa 5-0 dhidi ya Al Ahly, kule Congo ikafungwa 5-0 dhidi ya Vita na kule Algeria ilifungwa 3-0 dhidi ya JS Saoura. Kutokana na udhaifu huo, hawana budi kubadilika kama wanataka kusonga mbele kwa sababu huenda Mazembe wakaja kutafuta sare kisha wakaona wanaweza kumaliza mchezo wakiwa kwao. Ni ukweli usiopingika kuwa Simba kwa upande wa Tanzania ndio timu tishio kwa sasa kwa sababu kati ya timu 20, ndio pekee imepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 22, ikishinda 18 na kupata sare tatu, ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 57.Wanapewa uwezekano wa kuwaengua vinara Azam inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 62 katika michezo 29 na Yanga inayoongoza katika michezo 29. Sababu wekundu hao wako nyuma michezo saba, ikiwa watashinda watachukua uongozi huo kiulaini. Ukiachana na ubora wao katika ligi, wana kikosi kizuri chenye washambuliaji hatari na tegemeo kama Mnyarwanda Meddie Kagere, Mganda Emmanuel Okwi na Mtanzania John Bocco. Kagere ameifungia timu yake mabao 15 kwenye ligi na michuano hiyo ya kimataifa mabao sita hivyo sio wa kubezwa.Bocco ana mabao 11 na Okwi ana saba kwenye ligi. Simba ikiwa nyumbani bado inajivunia safu bora ya ulinzi baada ya kuruhusu nyavu zake kuguswa mara saba pekee ikiwa ndio timu iliyofungwa mabao machache ingawa kimataifa bado hawako vizuri. Kwa upande wa TP Mazembe sio timu ya kudharauliwa kwani katika ligi ya kwao bado wapo kwenye ubora, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 58 nyuma ya AS Vita inayoongoza kwa pointi 65. Timu hiyo ina wachezaji wengi hatari na wenye uzoefu mkubwa kama Tresor Mputu, Kelvin Zatu, Meshaki Elia na Jackson Muleka.Katika michezo yao iliyopita ya hatua ya makundi timu hiyo inaonekana kutokuwa na rekodi nzuri ugenini. Michezo mitatu waliocheza, miwili walipata suluhu dhidi ya Africain, sare ya bao 1-1 dhidi ya Ismaily na kufungwa 3-0 dhidi ya Constatine. Kwa kutizama na takwimu hizo inaonesha kuwa wanaweza kuja na lengo la kutafuta sare wakiamini nyumbani kwao ndio sehemu wanakoweza kupindua matokeo.Mechi zao za marudiano dhidi ya timu hizo walizocheza kwao zinaonesha namna gani matokeo ya nyumbani yaliwabeba. Ilishinda mabao 8-0 dhidi ya Africain, 2-0 dhidi ya Constatine na 2-0 dhidi ya Ismaily. Mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa kila mmoja, hasa wekundu hao wanahitaji matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani kisha kujipanga na mechi ya marudiano ya ugenini itakayochezwa April 13, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems anasema anawaheshimu Mazembe hivyi ataingia kwa tahadhari. “Mazembe nimeifuatilia, ni timu bora na inafanya vizuri kwenye mechi zake, nimewaandaa wachezaji wangu, tutaingia kwa tahadhari kubwa,” anasema.
michezo
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema kuanzia sasa, vikao vya kiserikali na mikutano yote ya viongozi wa ngazi za juu serikalini itafanyika rasmi katika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.Akizungumza Ikulu Chamwino na Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Balozi Kijazi alisema baada ya kuandaa jengo hilo kubwa na la kisasa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiofisi za serikali, sasa limekamilika na mikutano na vikao mbalimbali vya viongozi vitafanyika hapo.Balozi Kijazi alisema baada ya jengo hilo kukamilika, viongozi wa kitaifa ikiwa ni pamoja na Rais, Makamu wake, Katibu Mkuu Kiongozi na viongozi wengine, watafanyia mikutano yao katika jengo hilo.Balozi Kijazi alisema baada ya kukamilika kwa jengo hilo kubwa na la kisasa, hakutakuwa tena na suala la viongozi kuhamahama au kufanyia mikutano na vikao katika jengo la Tamisemi bali Ikulu Chamwino.Alisema tangu Rais Magufuli ahamie jijini Dodoma Oktoba 12, mwaka huu, uhamaji wao umekuwa ukiendelea ikiwemo kukamilisha jengo hilo, hivyo sasa mikutano mbalimbali itafanyika Ikulu Chamwino. Alisema yeye, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wameandika historia kwa kufanyia mkutano wa kwanza katika jengo hilo.Alisema kuhama si kazi ndogo, kunahitaji rasilimali nyingi za watu, fedha, nguvu na shughuli nyingine hivyo wanajivunia kukamilisha uhamaji huo kwani katika miezi miwili haikutarajiwa uhamaji kukamilika. Balozi Kijazi alisema serikali tayari imeshahamia Dodoma rasmi na hivyo shughuli zake mbalimbali za huduma kwa wananchi na kufanya mikutano nazo zimehamia Dodoma, hakuna tena kurudi Dar es Salaam.Alisema baada ya serikali kuhamia Dodoma, kila ofisi ya serikali sasa imejaa ambapo mikutano ya viongozi wa juu serikali itafanyikia hapo na hakuna tena kwenda jengo la Tamisemi au kuhamahama. Balozi Kijazi alisema tangu Rais John Magufuli aende wiki iliyopita, viongozi wamekuwa wakijipanga, lakini kuanzia sasa ni rasmi kutumia jengo hilo kwa ajili ya mikutano ya viongozi wa juu wa serikali.
kitaifa
Mwandishi Wetu -Tokyo WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Toshiba nchini Japan. Katika mazungumzo hayo, amewashawishi kuja na wafungue ofisi kubwa ili waanzishe viwanda vya bidhaa za elektroniki watakavyoona vinafaa hapa nchini.  Waziri Mkuu ameyasema hayo jana, baada ya kutembelea makumbusho ya sayansi ya Toshiba na kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni hiyo.  Aliwashawishi waje nchini na wafungue viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali za elektroniki kama vile redio, televisheni, pasi na viwanda vingine watakavyoona wao vinafaa kujengwa nchini.  Aliwahakikisha hawatojuta kuwekeza Tanzania kutokana na sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji.  “Wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza Tanzania, wakiwemo wa kutoka Japan na Kampuni ya Toshiba, watambue Serikali imeboresha mazingira ya uwekezaji na kuyafanya yawe rafiki, nina uhakika wawekezaji watakaoamua kuwekeza Tanzania hawatajutia uamuzi wao huo”. Alisema ujio wa kampuni kubwa utawapa Watanzania fursa ya kujifunza teknolojia mpya na namna bora ya uendeshaji wa biashara unaozingatia viwango vya  kimataifa.  Mkurugenzi wa Makumbusho ya Sayansi ya Toshiba, Takano Lwakiri, alimwambia Majaliwa kampuni yake iko tayari kupanua ofisi yake ya Tanzania na kufungua biashara, na ameomba yafanyike mazungumzo yatakayotoa dira sahihi ya kufanikisha jambo hilo. Kuhusu mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TICAD 7), utakaoanza leo jijini Yokohama, alisema anaamini utakuwa na mafanikio makubwa kutokana na ajenda zilizoandaliwa. Lwakiri alisema miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni namna ya kuunganisha kibiashara shughuli za Serikali na sekta binafsi.  Alisema kwa kutumia mkutano huo, wafanyabiashara wa Tanzania wanayo fursa ya kunufaika kwa kuunganisha nguvu zao na kampuni kubwa za nchini Japan.
kitaifa
Na Mwandishi Wetu MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, amezungumzia matukio ya uhalifu wa kupiga watu na risasi yanayoendelea nchini, akisema vyombo vya ulinzi vipo kazini na hivi karibuni hali itakuwa shwari. Matukio makubwa ya watu kupigwa risasi yaliyotokea nchini hivi karibuni, ni pamoja na lile la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyepigwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na watu wasiojulikana. Jingine ni lile la Jenerali mstaafu, Vincent Mritaba, aliyepigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam akitoka benki siku tatu zilizopita. Lissu kwa sasa yupo Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu, huku hali yake ikielezwa kubadilika badilika wakati Jenerali Mritaba, anatibiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam na afya yake inaelezwa kuimarika.   HALI ITAKUWA SHWARI Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jenerali Mabeyo alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinashughulika na matukio kadiri yanavyojitokeza na anaamini hali itakuwa shwari. “Matukio yanayoendelea tunakabiliana nayo, vyombo vya ulinzi na usalama wakati wote vinakabiliana na matukio kadiri yanavyojitokeza, Ninaamini hali itakuwa shwari na sasa vinashughulika. “Hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka wapi, hawa watu ni wa aina gani. Sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake, msitoe majibu haraka, tukio linapotokea lazima uangalie limetokeaje, chanzo ni nini, na ‘motive’ (sababu) ni nini,” alisema Jenerali Mabeyo.   ASHANGAA MATUKIO YA SASA KUSHTUA WATU Katika hatua nyingine, alionyesha kushangazwa na matukio ya sasa kuonyesha kushtua watu wengi, tofauti ya yaliyotokea Kibiti mkoani Pwani, yaliyoua zaidi ya watu 35. “Kwa nini matukio yaliyotokea Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa wakati watu walioathirika Kibiti ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa, mimi sitaki kuingia huko,” alisema.   WANAOTEKELEZA MATUKIO YA KUPIGA WATU RISASI Alisema kwa matukio ya sasa ya kupiga watu kwa risasi, uzoefu unaonyesha wanaoyatekeleza ni watu ambao hawajapita kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). “Vijana wanaohusika katika uhalifu hawajapitia Jeshi la Kujenga Taifa, kwa hiyo tuna imani kabisa vijana wetu wanaopitia Jeshi la Kujenga Taifa wanakuwa na maadili, wanakuwa na nidhamu, nitaomba ninyi mtusaidie katika wale watakaokuwa wamekamatwa katika kuwahoji, tuone kama watakuwa wamepitia Jeshi la Kujenga Taifa,” alisema Jenerali Mabeyo.   SIRRO ATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO Mbali na Jenerali Mabeyo, Mkuu wa Polisi, IGP Simon Sirro, alizungumzia suala la Lissu kupigwa risasi akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahalifu waliohusika. “Naomba wananchi wasidanganywe kwenye suala zima la siasa na vitu vingine, huwa nasema siku zote, kama hakuna amani na usalama siasa haiwezi kupata nafasi, tukio hili limetokea, tunapeleleza na tupo makini na hili tukio. “Kwa sasa tumeongeza vikosi vya upelelezi Dodoma, wale waliofanya lile tukio ni lazima tutawakamata, ila upelelezi huu unaweza kuzaa matunda mazuri zaidi endapo wananchi watatupa ushirikiano wa kutosha,” alisema IGP Sirro.
kitaifa
Mwanambilimbi alifikishwa mahakamani hapo jana pamoja na wanamuziki watatu wa bendi hiyo, Alain Mulumba (39), Michael Mwenabuntu (33) na Basizi Fayed (27), wanaodaiwa kuishi nchini na kufanya kazi bila kibali.Akisoma mashitaka, Wakili kutoka Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma alidai, Februari 10, mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach, Mulumba, Mwenabuntu na Fayed wakiwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikutwa wakiishi nchini bila kibali.Aliendelea kudai kuwa, siku hiyo hiyo katika hoteli hiyo, Mulumba, Mwenabuntu na Fayed walikutwa wakijishughulisha na muziki katika bendi ya Kalunde bila kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.Katika mashitaka manne yanayomkabili, Mwanambilimbi, Wakili Kagoma alidai huku akijua wanamuziki hao hawana kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini, aliwaajiri katika bendi ya Kalunde na kuwahifadhi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya Uhamiaji.Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na kuomba kesi ipangiwe tarehe nyingine kwaajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya awali.Mwanambilimbi aliachiwa kwa dhamana baada ya kupata mdhamini mmoja kutoka taasisi ya serikali, aliyesaini hati ya Sh milioni 1, pia aliwasilisha hati yake yakusafiria mahakamani. Washitakiwa wengine walirudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini.
michezo
WATU zaidi ya milioni tatu katika nchi za Tanzania na Kenya, watanufaika na Euro milioni 345 kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kusaidia ujenzi wa barabara.Barabara zitakazohusika ni za Mombasa-Lunga Lunga/Horohoro na Tanga-Pangani-Bagamoyo katika awamu ya kwanza, ikiwa ni asilimia 78.5 ya gharama zote ya ujenzi za Euro milioni 399.7. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na benki hiyo juzi, ilieleza kuwa Umoja wa Ulaya umechangia Euro milioni 30 ikiwa ni asilimia 7.7 ya gharama za mradi kwa serikali ya Kenya.Barabara ni muhimu kwa mtandao wa usafiri Afrika Mashariki, inayounganisha Kenya na Tanzania ili kuwezesha wazalishaji, wenye viwanda na wafanyabiashara kusafirisha bidhaa kwa haraka na gharama nafuu. Pia wakulima na wavuvi, watanufaika na ujenzi wa barabara hizo kwa kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.“Mradi huu utanufaisha pia nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini zinazotegemea Bandari ya Mombasa kulifikia soko la dunia,” alisema Meneja wa Miundombinu, Sekta Binafsi na Viwanda katika benki hiyo, Hussein Iman.Barabara hizo zitapunguza muda wa kusafirisha bidhaa, kuhamasisha biashara na muingiliano wa watu mipakani , kuvutia watalii, huku zikiunganisha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa na kukuza uchumi wa Pwani.Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa barabara kilometa 175 ikiwamo kilometa 121 za barabara ya Mkanga-Pangani nchini Tanzania na Kilometa 54 za barabara ya Mombasa-Kilifi nchini Kenya.Wiki hii, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ilitiana saini makubaliano ya Dola za Marekani milioni 440 na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano Japan (JICA) na serikali ya Kenya kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa daraja, linalounganisha kisiwa cha Mombasa na Likoni.Bandari ya Mombasa ni ndefu Afrika katika Bahari ya Hindi. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara za Mombasa – Lunga Lunga/Horohoro na Tanga - Pangani – Bagamoyo kwa ujumla wa fedha zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 1.2 .“Tuna imani kuwa tutafanya kazi pamoja kukamilisha suala hili muhimu na miradi mingine ijayo,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo.
kitaifa
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Mbao FC ya mkoani Mwanza, Amri Saidi amesema anaihofi a Yanga kutokana na soka safi inayocheza. Akizungumza na gazeti hili jana, Said aliyewahi kuichezea Simba alisema timu yake bado inaendelea kujiandaa ili kuwakabili Yanga na kupata ushindi. “Tunacheza na timu kubwa sana nchini na barani Afrika. Tutaingia na tahadhari ya kucheza mchezo wa kuzuia tuweze kupata sare dhidi ya Yanga.Yanga ni timu kubwa hata hivi karibuni imetoka sare na timu ya Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi,’’ Amri alisema. Hata hivyo, kikosi cha Said kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba nyumbani kwao CCM Kirumba Mwanza. Aliwaomba wadau na wapenzi wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa keshokutwa kuwapa sapoti ya kuondoka na pointi.Aliahidi kuwasistiza vijana wake kuwa wapambane kwa hali na mali ili wahakikishe wanapata sare na Yanga. Timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Gf trucks & Equipment ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi13. Mbao FC imepoteza michezo miwili mpaka sasa dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Tanzania.
michezo
KIWANGO cha ufaulu kwa wahitimu wa darasa la saba mkoani Morogoro kimeongezeka mwaka huu, ambapo wahitimu 37,111 wamefaulu sawa na asilimia 77.38. Mwaka jana asilimia 70.78 ya wahitimu, ndio waliofaulu, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la ufaulu la asilimia 6.6.Hayo yalisemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi upande wa Uchumi, Ernest Mkongo kwenye kikao cha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza Januari mwakani, kilichofanyika mjini hapa. Mkongo alisema kuwa hali ya ufaulu kwa kipindi cha mwaka 2018 imepanda, ukilinganisha na mwaka jana, ambapo ilikuwa ni asilimia 70.78 pekee.Alisema kuwa wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la saba Mkoa wa Morogoro ni 47,961, ambapo waliofanulu ni 37,111, ambao ni sawa na asilimia 77 ambapo lengo la mkoa ni kufikia asilimia 82. ‘’Kwa kuwa hatujafikia lengo la asilimia 82 tulilojiwekea upo umuhimu wa kuweka nguvu kazi ya pamoja na mikakati ili kuweza kufikia malengo hayo,’’ alisema Mkongo.Alisema kuwa kati ya watahiniwa 48,301 waliosajiliwa kufanya mitihani, watahiniwa 340 sawa na asilimia 0.7 hawakufanya mitihani huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.Aliziagiza halmashauri zote tisa mkoani Morogoro, kutathimini matokeo hayo na kisha kuibua changamoto na kuzitafutia mikakati ya ufumbuzi na shule ambazo hazikufaulisha hata mwanafunzi mmoja na zenye watahiniwa wachache, zifanyiwe ukaguzi ili kubaini sababu za msingi zilizosababisha hali hiyo.Alipongeza Halmashauri ya Ulanga, Manispaa ya Morogoro na Malinyi kwa kufanya vizuri na kuzitaka Halmashauri za Wilaya ya Kilosa, Gairo na Morogoro kuongeza juhudi.Alitoa agizo kwa shule ambazo hazikufaulisha mwanafunzi hata mmoja, kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 shule hizo zinafaulisha walau wanafunzi asilimia 50 ya watahiniwa wake. Katibu tawala huyo alimpongeza mwanafunzi, Innocent Seleli wa Shule ya Msingi Carmel iliyopo Manispaa ya Morogoro, kwa kuwa mwanafunzi bora wa mkoa na pia kuwa mwanafunzi kumi bora kitaifa.Ofisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Joyce Baravuga alisema anapongeza shule na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao na hivyo kupelekea mkoa kuwa miongoni wa waliochangia ufaulu wa kitaifa kupanda.Alisema kuwa mbali na ufaulu kupanda kwa mwaka huu, alizihimiza halmashauri zote kufanya tathimini ya mitihani kila mwaka na kubuni mbinu sahihi zinazolenga kuboresha taaluma kulingana na mazingira yao, hasa kurekebisha utendaji wa kazi, unaolenga kuinua taalumu kuanzia ngazi ya wilaya hadi shule.
kitaifa
Na JOHANES RESPICHIUS STAA wa muziki wa Bongo Fleva aliyeibuliwa na kibao ‘Na Yule’, Hellen George ‘Ruby’ ameibuka na kueleza mengi kuhusiana na muziki wake baada ya kimya cha muda mrefu. Msanii huyo ambaye amepitia katika Jumba la Vipaji Tanzania (Tanzania House of Talent) ‘THT’, amekuwa gumzo baada ya kuachana na uongozi uliokuwa ukimsimamia na kugeukia kufanya kazi zake kama msanii binafsi. Mbali hilo, hivi sasa amekuwa katika majibizano kwenye mitandao ya kijamii na mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho cha Radio Clouds FM cha jijini Dar es Salaam, Loveness Malinzi ‘Diva’ na hivyo kuzidi kuwaacha mashabiki katika hali ya sintofahamu. Ruby ambaye vibao vyake Sijutii, Forever na Suu alioshirikishwa na Yamoto Band vinamng’arisha, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu alipoachana na uongozi wake na kudai kuwa anaamini atafanya vizuri zaidi akijisimamia mwenyewe. Hapa chini Paparazi wa Swaggaz anakuletea sehemu ya mahojiano hayo, ambapo Ruby anaeleza yanayoendelea katika staili yake mpya ya maisha ya kimuziki. Swaggaz: Kwanini tangu uachane na uongozi wako wa awali kumekuwa na malumbano katika mitandao ya kijamii  kati yako na Diva? Ruby: Kwanza kwa jambo linalohusu uliokuwa uongozi wangu siwezi kulizungumzia kabisa kwa sasa. Lakini kwa faida ya mashabiki wangu, ni kwamba wategemee mazuri zaidi. Najisikia huru na naamini nitafanya vizuri zaidi nikijisimamia. Kuhusu Diva, bora tu niachane naye maana sioni vitu vya kumuongelea kama anavyofanya yeye. Zaidi namuonea huruma tu, namsikitikia na ninamwombea kwa  Mungu amrudishie akili zake. Nahisi ana ugonjwa wa kusahau, jambo ambalo ni baya sana kulingana na umri wake. Swaggaz: Umesikika kwenye wimbo wa Suu wa Yamoto Band, lakini kwenye video yake hujaonekana kushirikiana nao, badala yake sehemu yako amecheza msichana mwingine. Nini kilitokea? Ruby: Ukweli ni kwamba sikukataa kufanya video hiyo… tatizo ni mapatano hayakuwa mazuri, walishindwa kutimiza kile nilichokuwa nakihitaji. Swaggaz: Kuna tetesi kwamba kilichosababisha uachane na uongozi wako ni kutaka kuwa chini ya mwanamuziki Jide, ikoje hiyo? Ruby: Siyo kweli na sijawahi kuongea jambo hilo sehemu yoyote wala kumtafuta Jide kuhusiana na suala hilo. Swaggaz: Kwahiyo hutegemei kufanya naye kazi? Ruby: Nategemea lakini kwa sasa bado, kulingana na mambo yanayoendelea miongoni mwa watu lakini kuhusu mimi kukutana na  Jide  ni ndoto yangu ya muda mrefu kwakweli. Swaggaz: Changamoto gani kubwa ambazo umepitia katika safari yako ya sanaa? Ruby: Jambo kubwa ambalo lilikuwa likinipa huzuni ni watu kunikashfu, kunichukulia poa na kutengenezewa chuki bila sababu. Watu hatufanani. Siyo kila nilichonacho mimi mwenzangu anacho, vipo vitu vingi sana ninavyo lakini Beyonce hana. Hivyo hivyo anavyo vingine ambavyo sina,   kibongobongo ni vigumu kuelewa ndiyo maana wasanii tunawekeana chuki. Swaggaz: Jambo gani la huzuni na la furaha yaliyowahi kukutokea maishani mwako kiasi huwezi kusahau? Ruby: Nilihuzunika sana niliposikia watu wakisema mimi nakataa kufanya video na wasanii wenzangu, kitu ambacho siyo cha kweli. Ukweli ni kwamba wengi wanaotaka hivyo wanashindwa kufikia makubaliano. Jambo la furaha ambalo siwezi kulisahau ni pale nilipokubaliwa na mama yangu kuanza kufanya muziki wa Bongo Fleva na kuachana na nyimbo za Injili. Ilikuwa siku nzuri sana kwangu. Swaggaz: Kwa ufupi nini kilisababisha ukaamua kuachana na nyimbo za Injili na  kuingia kwenye Bongo Fleva? Ruby: Muziki wa Bongo Fleva na Injili ni vitu viwili tofauti kabisa kwani kwa upande wa Injili ni kama kuhubiri lakini Bongo Fleva uko kibiashara zaidi, hivyo niliingia huku kwa sababu ya biashara.
burudani
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amekunwa na miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali, ikiwamo uboreshaji usafi ri wa anga, huku akishangazwa na watu waliobeza uamuzi wa Rais John Magufuli kununua ndege.Pinda ambaye amesema binadamu anapotenda mambo mema asitegemee watu wote kumpongeza, alisema zilipotolewa kauli za kuponda, alijisemea moyoni kwamba, wanaobeza watapata majibu polepole na sasa wameshayapata. Alisema hayo mjini hapa wakati akifunga Maonesho ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani katika hotuba ambayo pia alitoa rai kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuangalia uwezekano wa kutoa elimu inayoendana na mahitaji ya soko la ajira na kuishauri serikali kuhusu viwanda vinavyojengwa na kufa akitaka ivifuatilie.Akizungumzia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano, alisema ina uhusiano mkubwa na uboreshaji wa maisha ya wananchi.“Jambo jingine ambalo serikali ya awamu ya tano imefanya ni kuboresha Shirika la Ndege la ATCL, mambo haya na mengine ndiyo maana tunakubali. Mtu unapotenda mambo mema mazuri usitegemee tu kwamba watu watakunyamazai tu, hongera, asante sana.”“Maana nakumbuka bwana mkubwa (Rais) alipofanya uamuzi huu, ulileta mjadala mkali sana. Nakumbuka siku za mwanzo watu walisema ndege yenyewe haina hata watu. Yanaruka tu matupu tu. Nikajua tu watakuja kupata majibu polepole.”“Ilikuwa inakwenda mara moja sehemu nyingine, sasa tunakwenda mara mbili na bado tutalazimika hata kwenda mara tatu, usafiri nao una mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi,” alisema.Pinda alisema kwa kutumia ndege hizo, sasa mfanyabiashara anaweza kutoka Dodoma kwa dakika 50 mpaka Dar es Salaam na kisha akageuza kurudi jambo ambalo lilitakiwa kuwapo tangu awali.“Hivyo lazima tukubali kuwa hii ni miradi ya kimkakati kikwelikweli wala siyo lele mama hata kidogo,” alisema.Akieleza mchango wa usafiri katika uchumi, alitoa mfano wa Wachina akisema wanapenda kuja nchini kutalii lakini wamekuwa wakihoji kuhusu uwapo wa ndege ya moja kwa moja kutoka nchini kwao.“Sasa nashukuru madege yameingia makubwa na mpango utakapokamilika yataruka kwenda Guangzhou (China) pale utaona sasa Wachina watakavyokuwa wakija kwa wingi kutalii,” alisema.Pinda pia alitaja Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Nyerere katika Mto Rufiji na kusema ulikuwa na hadithi ndefu na kila aliyejaribu kuutekeleza alirudi nyuma hadi Rais Magufuli alipoingia madarakani.Alisema miongoni mwa sababu zilizotolewa kuhusu kutotekelezwa mradi huo ni gharama na uharibifu wa mazingira. Akimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliofanya, kwani mradi huo ukikamilika viwanda vitakuwa na uhakika wa umeme. Akizungumzia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), alisema mradi huo ukikamilika utatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa viwanda, kwani utatoa fursa ya kusafirisha malighafi na bidhaa zinazozalishwa.
kitaifa
SERIKALI iko katika hatua ya mwisho ya makubaliano na Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Milki za Ardhi ikiwa ni katika kuhakikisha ardhi inatumika kwa tija. Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwenye wizara yake kwa mwaka 2019/20. Wizara imeomba kupitishiwa bajeti ya Sh bilioni 62.69 kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 ambapo zaidi ya Sh bilioni 27.3 zikitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku ikiweka lengo la kukusanya Sh bilioni 180. Katika hotuba yake alisema ifikapo Agosti mwaka huu, Mkoa wa Dar es Salaam utaanza kutoa hati za kielektroniki hii ni baada ya kukamilisha ufungaji wa mfumo kwenye halmashauri zote za manispaa ya mkoa huo. Alisema programu hiyo ambayo awali ilikuwa itekelezwe kwa mwaka wa fedha 2018/2019 itakuwa ni nyenzo muhimu katika kuleta mageuzi sekta ya ardhi ikiwamo kuondoa na kudhibiti migogoro ya matumizi ya ardhi miongoni mwa watumiaji, kupanua wigo wa mapato ya serikali na kuhakikisha ardhi inatumika kwa tija. Alisema pia kwa mwaka mpya wa fedha NHC, inaendelea na mikakati endelevu ya kuuza nyumba za makazi na linatarajia kujenga nyumba 1,000 katika jiji la Dodoma. Aidha, Lukuvi alisema imeandaa mfumo maalumu wa kieletroniki utakaowezesha kutoa leseni za makazi zinazotambulika kisheria kwa kutumia simu janja ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na matapeli wa ardhi. “ Mfumo huo utawezesha urahisi kwenye utambuzi wa vipande vya ardhi mijini pamoja na taarifa za wamiliki na umeanza kutekelezwa katika jiji la Dar es Salaam na utaendelea kutumika nchi nzima. Hadi kufikia Mei 15 mwaka huu, vipande vya ardhi vya matumizi mbalimbali 150,000 vimesajiliwa.” Lukuvi alisema mfumo huo utawapa wananchi uhakika wa miliki zao na kuwezesha ardhi zao kutumika kama mtaji wa kiuchumi na kwa mwaka wa fedha 2019/20 wizara yake inakusudia kusajili hatimiliki na nyaraka za kisheria 152,000. Aidha, Lukuvi alisema Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) linakuja na mfumo wa ‘Mpangaji Mnunuzi’ ili kuwezesha wananchi wa kada mbalimbali kumiliki nyumba za makazi. Lukuvi alisema katika kipindi cha utekelezaji wa bajeti hiyo, wizara itatekeleza kazi mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya TEHAMA ya utunzaji kumbukumbu na kuboresha taarifa za ardhi.Alisema kazi nyingine ni kurahisisha ukadiriaji kodi ya pango la ardhi na tozo zitokanazo na sekta ya ardhi kwa kutumia vifaa vya kieletroniki vinavyohamishika. Lukuvi alitaja majukumu mengine ambayo wizara imepanga kuyatekeleza ni kuhakikisha watu wote wa mjini wenye nyumba na ardhi isiyopimwa wanarasimishwa na kupewa hati na leseni za makazi.Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mjumbe wa Kamati hiyo, Shaban Shekilindi kamati iliipongeza serikali kwa kubuni mradi wa kujenga nyumba 1,000 kupitia Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) kwa ajili ya makazi jijini Dodoma ambalo ni makao makuu ya nchi.Kwa upande wa maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, msemaji wa kambi hiyo kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wlifred Lwakatare, upinzani unaamini katika mfumo wa umiliki ardhi ambao kila mwananchi atamiliki ardhi na rasilimali zake juu na chini ya ardhi hiyo.
kitaifa
KIFO cha Winnie Madikizela-Mandela, mke wa zamani wa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye pia alipigana vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kimezua mjadala nchini mwake namna ambavyo mwanaharakati huyo anastahili kukumbukwa. Upande wa viongozi wa jadi pamoja na wafuasi wake, wanataka Winnie akumbukwe kama mwanamke asiyekuwa na hatia nchini humo. Huku wengine hasa wale ambao bado wapo katika mapambano ya awali wakiwa chini ya mwavuli wa watu weupe wanataka Winnie Mandela kukumbukwa kama mtu mbaya sana na aliyetenda uasi. Lakini kwa mtu yeyote ambaye anataka kumwelewa vizuri Winnie Mandela, anapaswa kurejea historia na kuona namna ambavyo alinyanyaswa, kuaibishwa na kuteseka wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi. Makala haya yanaelezea mambo muhimu yanayoendelea kwa sasa nchini Afrika Kusini ambayo ni kiashiria cha wazi cha kupata majibu kwamba iwapo Winnie Mandela alikuwa shujaa na muasi. Kupigania uhuru Winnie alikuwa mpigania uhuru, aliyeleta mapinduzi kwa kuwa mpambanaji wa ubaguzi wa rangi, hakuwa mwanaharakati wa kushika silaha na kutegemea mashabiki wa mitandaoni. Mume wake wa zamani, Nelson Mandela, alimwachia watoto wadogo wawili wa kike kuwalea wakati alipofungwa gerezani mwaka 1962. Winnie kuitwa mwanaharakati ni haki yake, kwa kuwa ni mwanamke aliyewahi kukakamatwa na kuwekwa gerezani akiwa na nguo zake za kulalia tu, huku polisi wakiwazuia ndugu zake kwenda kumwona na kuzuiwa kuwaona watoto wake. Siku 491 ndani ya chumba cha mateso Mwaka 1969, Winnie alifungwa gerezani kwa muda wa siku 491 na hakupata msaada hata wa pedi wakati alipokuwa katika siku zake kama ilivyo kawaida ya wanawake. Gereza lake halikuwa la kawaida, ila maalumu kwa ajili ya kumtesa. Mateso aliyoyapata gerezani yaliandikwa katika kitabu kiitwacho “491 Days”, kinachoelezea kelele ya mwanamke aliyekuwa anapigwa na kuteswa gerezani kila kukicha. Lakini Winnie hakukosa kupaza sauti ya kuwatetea watu weusi waliokuwa wakipambana dhidi ya ubaguzi wa rangi ulioendeshwa na wazungu wachache nchini humo. Baadaye wakati ambapo viongozi wengi walipokuwa wanafungwa jela, Winnie alikuwa mstari wa mbele katika kuongoza harakati hizo akiwa pamoja na hayati Nelson Mandela. Kiufupi ni kwamba, Winnie aliamua kuongoza mapigano ya kutetea watu weusi bila kuchoka wala kujali matatizo aliyokuwa akikabiliana nayo katika juhudi hizo. Alipobainika kuwa ana ushawishi mkubwa, Winnie alihamishwa katika makazi yake yaliyokuwa katika mji wa biashara wa Johannesburg, kwenda kukaa katika mji mdogo wa Brandfort ambayo ilikuwa ngome imara ya watu weupe. Mji wa Brandford upo Jimbo la Orange Free ambapo katika miaka ya 1970 baada ya operesheni mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama “The Soweto Uprising”. Lengo lao kubwa lilikuwa kumdhibiti pamoja na kupunguza nguvu zake kwenye harakati za kutetea watu weusi. Hakuruhusiwa kupokea wageni ingawa alikuwa anaweza kusafiri kila siku kwenda posta kupiga simu, ili kuuambia ulimwengu juu ya mfumo wa ubaguzi wa rangi. Tangu kifo chake kitokee Aprili 2, mwaka huu, kile kilichoandikwa na watu wengi katika mitandao ya kijamii, kinaonesha wazi kuwa kuna baadhi ya watu hawafahamu historia ya Winnie Mandela. Kuna wengine wamezungumzia juu ya urembo wake na wengine jitihada zake katika kutetea nchi yake. Tukubaliane kuwa Winnie pia hakuwa mkamilifu, alikuwa na makosa yake pia. Aliwahi kuhukumiwa kwa kosa la udanganyifu na alikamatwa kwa kosa la utekaji nyara. Licha ya misukosuko hiyo, Winnie, alibaki kuwa mtu muhimu sana katika siasa za Afrika Kusini na kuwa mwakilishi muhimu wa wanawake waliopambana kufa kupona dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendelezwa na wazungu walio wachache nchini humo. Katika siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa miongoni mwa wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, katika kushutumu na kulaani vikali vitendo vya kuwashambulia wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika Kusini, ambayo yalibadikwa jina ‘Xenophobic’. Pia amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema, kilichojiengua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali rais aliyeng’atuka Jacob Zuma. Historia ya Winnie hadi kifo chake inabaki akikumbukwa zaidi kama mama wa Taifa la Afrika Kusini aliyesimama kidete dhidi ya ubaguzi wa rangi katika umri wake wote. Licha ya kuibuka kundi la watu ambalo linadai kuwa Winnie hakupaswa kupewa heshima yoyote bado ukweli umedhihirika wenyewe kuwa mwanamama huyo anazidi kung’ara kama alivyokuwa enzi zake ingawaje amefariki dunia. Kuzungushwa nchi nzima Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa na kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC), pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Ramaphosa, amekaribisha ushujaa wa Winnie Madikizela-Mandela katika harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Rais Ramaphosa alisema, Afrika Kusini inaomboleza kifo chake na Serikali itashirikiana na familia wakati wa mazishi yake rasmi Aprili 14 mwaka huu. “Kutakuwa na shughuli kubwa ya kuzunguka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kumuaga Winnie, itakuwa kila jimbo. Tunapenda kutoa heshima na shukrani zetu kutoka kila kona ya nchi hii na duniani kwa ujumla,” alisema Ramaphosa. Ramaphosa alikutana mara ya mwisho na Winnie mnamo Machi 10, wakati wa kuandikisha wapigakura. “Mimi kama rais wa ANC, nimehuzunishwa kwa sababu nilikwenda kuhakikisha taarifa kwenye daftari la wapigakura nikiwa naye. Nilikula naye chakula. Wafuasi wa Winnie mjini Soweto walikusanyika, wakiimba nyimbo za vita walizokuwa wakiimba wakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Mazishi ya Kijeshi Pamoja na mjadala huo kukolea kwamba Winnie ni shujaa au la, Serikali ya Afrika Kusini imetangaza jambo jingine ambalo linazima kabisa majigambo ya wakosoaji wa Winnie. Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri, Dk. Nkosazana Dlamini-Zuma, akiwa na Waziri wa Habari, Nomvula Mokonyane, juzi aliviambia vyombo vya habari akiwa ndani ya Uwanja wa Orlando, shughuli za mazishi ya Winnie Madikizela-Mandela zitafanyika katika uwanja huo uliopo mjini Soweto na kushuhudiwa na mamia ya wabunge na wananchi wa nchi hiyo. “Serikali yetu inathibitisha kuwa taratibu zote za kijeshi zitafanyika ili kutoa heshima ya mwisho kuaga mwili wa Winnie Mandela. Licha ya huzuni tuliyonayo, tunalazimika kukubali kuwa hayupo nasi tena duniani,” alisema Dlamini-Zuma.  
kitaifa
Masanii Gigy Money amesema ana wivu sana kwa mpenzi wake wa sasa na akishika tu simu inakodolea macho kama fundi saa. Katika ukurasa wa Instagram Gigy ameposti picha akiwa pamoja na mpenzi wake huyo wa sasa huku akiwa anachungulia simu yake. Binadamu tumeumbwa na wivu lakini wangu umezidi kila akishika simu mimi mijicho yangu inatoka kama nimepoteza nati ya saa.. achana na swala lakuchungulia cm ata Beyoncé anafanyaga ivi 🤣 yani mapenzi ayana mazoea nikulinda mzigo wako tu ❤️ wivu kidonda 🤦🏻‍♀️ @hunchyhuncho najua ujaelewa ila jua Nakupenda sana ❤️❤️❤️🥰 A post shared by 𝐊𝐢𝐤𝐢 𝐍𝐢 𝐆𝐢𝐠𝐲 🇹🇿 (@gigy_money_og) on Jan 20, 2020 at 10:32pm PST Amesema binadamu wote wana wivu ila wa kwake umezidi na mapenzi hayana mazoea kikubwa kulinda mzigo wako, “Wivu ni kidonda”. Gigy sasa ni mtu wa kula bata nchi za nje na huyo mpenzi wake ambaye ameamua amkabe mpaka penati. Ana Tamani niwe wake ….. akiniona niko Nawe akithubutu anifate ukimuona rusha mawe Zaddy 💕💓 my life is nothing without you ❤️ A post shared by 𝐊𝐢𝐤𝐢 𝐍𝐢 𝐆𝐢𝐠𝐲 🇹🇿 (@gigy_money_og) on Jan 18, 2020 at 5:44am PST
burudani
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo amesema hajawahi kufi kiria tuzo ya ufungaji bora msimu huu, zaidi anawaza kuisadia timu yake kutwaa ubingwa.Makambo alisema kila anachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yake na atajituma ili kuisaidia kutwaa ubingwa msimu huu, kwani hajawahi kuwaza mafanikio binafsi kama kuwa mfungaji bora. Nawaza ubingwa zaidi, sifikirii tuzo yoyote binafsi, kila ninapofunga bao nafanya hivyo ili timu ipate pointi tatu iweze kutwaa ubingwa sifanyi ili niwe mfungaji bora,” alisema Makambo.Makambo ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa sasa amefunga mabao 11 katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwa sasa mshambuliaji huyo amekuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa timu za Ligi Kuu kutokana namna ya anavyowazidi ujanja na kufunga mabao. Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 18 na kushinda michezo 16 na sare michezo miwili ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 40 na Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 33.
michezo
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM IKIWA imepita mwezi mmoja tangu majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuacha kazi kwa wakati mmoja  na kuibua mjadala, jaji mwingine amejiuzulu wadhifa huo. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi na Mawasiliano ya Rais Ikulu jana ilieleza kuwa Rais Dk. John Magufuli ameridhia ombi la Jaji wa Mahakama Kuu, Mwendwa Judith Malecela kujiuzulu wadhifa wake. Majaji wengine waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,  Jaji Aloysius Mujulizi na mwenzake Upendo Msuya ambao ombi la kujiuzulu kwao liliridhiwa na Rais Magufuli Mei 16, mwaka huu. Jaji Mujilizi alikubwa na tuhuma za kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow kwa kupewa fedha, huku Jaji Upendo ikielezwa kuwa ni mgonjwa. “Rais Magufuli ameridhia kujiuzulu kwa Mheshimiwa  Mwendwa Judith Malecela kuanzia leo (Juni 20, 2017),” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu. Chanzo kingine cha habari kililieleza MTANZANIA kuwa tangu alipoteuliwa mwaka 2010 na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, jaji huyo hajawahi kusikika wala katika shughuli zake za ujaji. Taarifa hizo zilielezwa kuwa jaji huyo wakati wote alikuwa akisumbuliwa na maradhi hali iliyomfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa utaratibu. “Tangu alipoteuliwa Jaji Mwendwa, amekuwa akisumbuliwa na maradhi hali iiliyokuwa ikimfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake. Nafikiri kwa hali hiyo ndiyo huenda ni sababu ya yeye kuamua kuomba kujiuzulu wadhifa wake,” alisema mtoa taarifa huyo. Mbali na majaji hao Mei 16, mwaka huu pia Rais Magufuli aliridhia kuacha kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, huku kilichowafanya kuacha kazi kikiwa hakijaelezwa. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa walihusisha kuomba kuacha kazi kwa Jaji Mujulizi, kuwa kunatokana na kashfa ya Escrow, wakisema amesoma alama za nyakati. Jaji Mujulizi alikuwa ni mmoja wa vigogo waliotajwa kupokea mgawo wa Sh milioni 40.4 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, uliotokana na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Jumla ya Sh bilioni 321 ziliwekwa katika akaunti hiyo na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kusubiri suluhu ya kesi yake na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Siku chache baada ya kuibuliwa kwa kashfa hiyo, Rugemalira aliyekuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL, alisema kati ya fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo, alilipwa Dola za Marekani milioni 75 sawa na Sh bilioni 120  ambazo aliziita ‘vijipesa vya ugoro’.
kitaifa
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imeeleza mafanikio yake katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2099, ikiwemo kuunganisha nchi wanachama kwa mtandao wa barabara za lami, usalama, kuimarisha biashara na utengamano wa wananchi kuelekea kuundwa kwa shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki.Katika kipindi hicho cha miaka 20, jumuiya hiyo pia imefanikiwa kuunda soko la pamoja, kuongeza idadi ya nchi wanachama, ushuru wa forodha na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kijamii kama elimu, afya, taaluma, na mafunzo kwa majeshi ya nchi wanachama.Mafanikio hayo yamekuwa kielelezo kizuri kwa mataifa na ukanda mwingine na yamevutia nchi nyingine ikiwamo Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo (DRC) kutaka kujiunga.Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Steven Mlote, wakati alipokutana na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo, Liberat Mfumukeko.Alisema jumuiya hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nyanja mbalimbali katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.Mfumukeko amesema kuna mafanikio mengi yamepatikana katika kipindi cha miaka 20 iliyopita ikiwamo kuongezeka kwa nchi wanachama kutoka tatu za Tanzania, Kenya na Uganda, mpaka sita zikiongezeka Rwanda na Burundi na baadaye Sudan Kusini.Alisema hali hiyo imetokana na nchi kuona mafanikio na kutamani kujiunga kwani hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imevutiwa na mafanikio hayo na kutaka kujiunga ili iweze kujitanua kibiashara, uwekezaji na kuimarisha amani na utilivu.Soko la pamoja Mfumukeko alisema soko la pamoja na ushuru wa pamoja kwa nchi wanachama umewezesha watu wa nchi hizo kufanya biashara bila vikwazo, pamoja na kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara za lami ili kuimarisha mahusiano hayo.“Mfano mzuri kwa Tanzania ni mkoa wa Arusha ambao ni makao makuu ya EAC, ambapo mbali na barabara ya lami ya Arusha-Namanga-Taveta- Voi ambayo imekamilika kwa kiasi kikubwa, kuna barabara maarufu ya njia mbili zimejengwa na EAC, pia barabara ya ‘Arusha by Pass’ au maarufu Jumuiya ya Afrika Mashariki imejengwa mkoani humo,” alisema.Katibu Mkuu huyo wa EAC alisema pia kuna barabara ya lami inajengwa kutoka Nyakanazi-Kibondo- Kasulu mpaka Manyovu na Bunjumbura nchini Burundi, ambapo wakandarasi wanaendelea na ujenzi ili kuwezesha mfanyabiashara kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka Bujumbura.Alisema kuelekea nchini Rwanda kuna barabara ya Lusaunga-Lusumo-mpaka Kayonza na Kigali ambayo inatafutwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Lusaunga-Lusumo na Kayonza mpaka Uganda na tayari usanifu kwa ajili ya ujenzi.Akizungumzia barabara ya Uganda, alisema wanaendelea kufanya muundo wa barabara hiyo kutoka Masaka kwenda Mutukula mpaka Kyaka na Bugenda, Karagwe mpaka Kasulo mpakani mwa Rwanda na kuungana na barabara ya Lusonga.Alisema nchi zote za EAC zinaunganishwa na mtandao wa barabara za lami ili watu waeze kufanya biashara bila vikwazo.Ushuru wa forodha Mlote alisema katika ushuru wa forodha sheria nyingi zimefanyiwa marekebisho hivyo kulipiwa katika kituo kimoja cha nchi wanachama, huku wataalamu kama wahandisi au wasanifu majengo wameungana kwa makubaliano kuwa aliyehitimu nchi yoyote anakuwa na sifa sawa hivyo kufanya kazi popote katika nchi za EAC.Sarafu moja na takwimuNaibu Katibu Mkuu huyo wa EAC alisema sheria za takwimu na sheria ya pamoja ya taasisi za fedha zimepitishwa na jumuiya hiyo katika kuelekea kuwa na matumizi ya sarafu moja.Umoja wa kisiasa Mlote alisema wiki iliyopita, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alizindua mchakato wa Katiba ya pamoja ya umoja wa kisiasa na kwamba kwa sasa unaendelea vizuri.Rais Museveni alisema umuhimu wa nchi za EAC kuwa na umoja wa kisiasa ni kuimarisha utengamano na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi zote ambayo yamepatikana kupitia biashara na ukuaji wa uchumi
kitaifa
Kosa la Yondani ni kitendo cha kumtemea mate mchezaji wa Simba, Asante Kwasi katika mchezo uliopita dhidi ya watani zao wa jadi, Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam na Yanga kufungwa bao 1-0.Akizungumzia adhabu hizo Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema, “waamuzi hawakuona lile tukio ndio maana suala lake limepelekwa kwenye Kamati ya Maadili, na adhabu ya kusimamishwa imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu usimamizi wa ligi”.Kuhusu Malima alisema pia, suala lake limepelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu. Kosa la mchezaji huyo alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini akatoka kwenye chumba cha kuvalia nguo kwenda kushangilia bao la kusawazisha la timu yake.Kwa upande wa Obrey Chirwa wa Yanga alionywa kwa kadi ya njano kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Mbeya City ingawa kwenye picha za televisheni inaonekana kama alipiga kiwiko hivyo, kamati hiyo haikutoa adhabu nyingine kwa vile tayari ameadhibiwa.“Klabu ya Yanga imeandikiwa barua kuhusu kumuonya mchezaji huyo kwa vile kumbukumbu zinaonesha ameshafanya matukio ya utovu wa nidhamu mara kadhaa akiwa uwanjani,” alisema.Pamoja na hilo, pia Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.Wambura alisema kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
michezo
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya taasisi sita, baada ya kufanya vibaya katika manunuzi.Pia Mpango amewataka wahusika katika taasisi hizo, kukaa kando kupisha uchunguzi huo. Dk Mpango alitoa maagizo hayo jjini Dar es Salaam jana, wakati akipokea ripoti ya tathmini ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kutoka Mamlaka ya Ununuzi kwa Umma(PPRA), iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Dk Matern Lumbanga.Taasisi zilizotajwa kufanya vibaya katika manunuzi kupitia ripoti hiyo ni Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Wakala wa Mbegu za Kilimo, Taasisi ya Utafiti wa Dawa (NIMR), Kituo cha Diplomasia na Halmashauri za Wilaya za Kaliua mkoa wa Tabora na Nsimbo mkoa Katavi.Aidha, ripoti hiyo pia ilibainisha uwepo wa viashiria vya rushwa katika taasisi na miradi ikionesha kuwa miradi 12 yenye thamani ya Sh bilioni 25.8, ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa kwenye baadhi ya miradi Miradi hiyo inazihusisha taasisi tisa ambazo ni Wizara ya Maji, Shirika la Reli Tanzania(TRC), Mamlaka ya Bandari(TPA), Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Singida, Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Wang’ing’ombe, Halmashauri za Manispaa za Kigamboni na Ubungo jijini Dar es Salaam na Halmashauri ya Mji wa Kahama.Aidha, Waziri Mpango alisema hajaridhishwa na utekelezaji wa mfumo wa manunuzi ya umma kwa njia ya mtandao (TANePS). Aliagiza ripoti ya utekelezaji iwasilishwe kwake ifikapo Oktoba 15 mwaka huu, hasa kuhusu taasisi ambazo tayari zilipewa mafunzo ya kuutumia mfumo huo na kushindwa kutoa matokeo mazuri.Pia alizitaka taasisi zote za umma, kuhakikisha zinazjiunga na mfumo huo kabla ya Desemba 31 mwaka huu na kusisitiza kuwa endapo wahusika wa taasisi hizo, watashindwa kutekeleza agizo hilo hati za uteuzi wao zitatenguliwa kisheria.Awali, akizungumza wakati wa kuiwasilisha ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Lumbanga, alisema mbali na kufanya ukaguzi wa kawaida, PPRA pia ilifanya uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi katika taasisi tano kuhusu mikataba na zabuni 13 ya manunuzi inayokadiriwa kuwa na tha mani ya Sh bilioni 375.05.Alitaja taasisi hizo kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Benki Kuu ya Tanzania(BoT), Mamlaka ya Viwanja vya ndege(TAA), Wakala wa Umeme Vijijini(REA) na TBS, hatua iliyotokana na maagizo kutoka mamlaka za juu au maombi kutoka taasisi zenyewe, ambapo kupitia chunguzi hizo Serikali iliweza kuokoa Sh bilioni 3.39.Aidha kupitia uchunguzi huo uliofanywa katika taasisi hizo, ilibaini kuwa serikali ilipata hasara ya takribani Sh bilioni 4.36 kwa kukosa ada ambazo zingelipwa na wazabuni na taasisi nunuzi kufanya mabadiliko katika usanifu wa miradi ambayo yalisababisha kutelekezwa kwa baadhi ya kazi na bidhaa ambazo zilikuwa zimeshafanyika na kugharamiwa, hatua iliyomfanya Waziri Mpango kuagizwa kuchukuliwa hatua kwa maofisa ugavi wa taasisi hizo.“Naziagiza taasisi zote zilizohusika katika upotevu wa fedha hizo kuzirudisha fedha hizo lakini mamlaka za nidhamu ziwachukulie hatua maofisa ugavi wa taasisi zote zilizohusika ikibidi wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo, lakini wakuu wa taasisi husika nao wajipime kutokana na hayo hatuwezi kusababisha hasara katika fedha ambazo zingeweza kusaidia masuala mbalimbali ya kimaendeleo.“Wahusika wangekuwa hapa ningewaagiza Takukuru muondoke nao, lakini nawaomba mawaziri wenzangu katika wizara zilizotajwa mnisaidie katika suala hili, haiwezekani Rais John Magufuli akwamishwe katika mipango yake ya maendeleo ya taifa hili, ni vizuri washughulikiwe ili waonje joto la jiwe,”alisema Dk Mpango.Aidha Waziri Mpango alitaka PPRA kufuatilia kwa karibu manunuzi ya taasisi kubwa, ambazo manunuzi yake yanazidi Sh Bilioni 20 huku akisisitiza kuwa Wizara yake ipo tayari taifa.Awali, Dk Lumbanga alisema RRPA ilifanya ukaguzi wa upatikanaji wa thamani ya fedha katika miradi mbalimbali ili kupima thamani halisi ya fedha katika miradi 290 ya manunuzi yenye thamani ya Sh trilioni 8,478.33, ikijumuisha miradi ya ujenzi ya miundombinu ya majengo, barabara, madaraja, reli, umeme, maji na umwagiliaji pamoja na miradi ya bidhaa na huduma za ushauri wa kitaalamu.Alisema katika ukaguzi huo, wastani wa jumla katika ukaguzi wa upimaji wa upatikanaji wa thamani halisi ya fedha kwa taasisi zilizokaguliwa ilikuwa asilimia 84.4 ambao ni wastani mzuri.
kitaifa
NA CHRISTOPHER MSEKENA UKITAJA orodha wasanii wa Bongo wenye hadhi ya kuwa wanamuziki basi jina la Dotto Bwakeya ‘Lameck Ditto’ ni lazima liwemo. Mwimbaji huyu  wa Moyo Sukuma Damu amekamilika kila idara yaani mbali na kuimba ni mtunzi na mpigaji wa ala za muziki. Ni wasanii wachache sana Tanzania wenye uwezo wa kutumbuiza mubashara (live) kwenye jukwaa. Ditto anaweza kufanya hivyo, mashabiki wanaopenda muziki mzuri bila shaka watakuwa wamenielewa. Juma3tata leo, tumepata nafasi ya kupiga stori mbili tatu na Lameck Ditto, alipotembelea ofisi za gazeti hili mwishoni mwa wiki ambapo amefunguka mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yake na tasnia nzima ya muziki hapa nchini. Karibu.. FAMILIA Mashabiki wa muziki wamekuwa wakimfahamu, Lameck Ditto kupitia muziki, si rahisi sana kukuta akizungumzia mambo yanayohusu mapenzi yake binafsi kama wanavyofanya mastaa wengin, sababu gani inafanya awe hivyo? “Familia yangu ipo vizuri kabisa ndiyo maana mimi nipo hapa, naishi na mzazi mwenzangu tuna mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka minne,” anasema Ditto. NAFASI YAKE THT Ditto ni zao la nyumba ya vipaji, Tanzania House Of Talent (THT) na hapa anazungumza nafasi yake kwenye jumba hilo lililo nyuma ya mafanikio ya mastaa wengi wa Bongo Fleva. “Mimi pale THT n mwanafamilia, ni kama nyumbani, muda wangu mwingi nautumia pale. Toka nilivyoingia miaka 7 iliyopita asilimia 75 ya siku yangu huwa naitumia pale, labla niwe na shoo au niwe kwenye mahojiano kama hivi leo nipo hapa kwenye gazeti la MTANZANIA,” anasema. AMETUNGA NYIMBO ZIPI? Kama nilivyosema hapo awali, Ditto amejaliwa kuwa ni vipaji vingi ikiwa ni pamoja na kutunga mashahiri ya muziki, Juma3tata lilitaka kujua mpaka sasa ametunga nyimbo zipi zilizobamba, mwenyewe anafunguka.. “Sina idadi kamili ya nyimbo ambazo nimetunga, kwa sababu kuna nyimbo nimetunga wameimba wasanii wengi, nimetunga nyimbo kama Miaka 50 ya Uhuru, Tuulinde Muungano Wetu na Ishi na Mimi ule ambao wasanii waliimba wakati Rais anazindua ujenzi wa bomba la mafuta kule Tanga, kwa upande wa wasanii nimeandika nyimbo kadhaa za Linah (Malkia wa Nguvu) na wengine,” anasema. HALI YA CHID BENZ Ikumbukwe kuwa Chid Benz ndiye aliyemuonyesha, Ditto, Jiji la Dar es salaam baada ya kumpokea na kukuza kipaji chake kwenye kundi la La Familia akiwa ametokea watu Pori chini ya Afande Sele kama hajajiunga na THT. Lakini hivi karibuni rapa huyo anayefanya vyema na wimbo wake, Muda amekuwa akipita kwenye changamoto ambayo kila mmoja wetu anaifahamu ikiwa ni pamoja na kutangaza kufanya kolabo na JAY-Z, Je Lameck Ditto anaizungumzia vipi hali ya mlezi wake huyo? “Mimi binafsi nimekutana na Chid Benz na kuongea naye, nikagundua ni mtu ambaye anatamani kutoka kwenye ile hali, kwa hiyo namna nzuri ya kumsaidia ni kumpa msaada kimya kimya, haina haja ya kumtangaza mabaya yake au kumwongelea vibaya, hiyo itamsaidia zaidi,” anasema. SIRI YA KAZI YAKE MPYA Baada ya kufanya vizuri na Moyo Sukuma Damu na Atabadilika hivi sasa anatamba na audio ya wimbo wake unaoitwa, Nabembea. Ipi ni mipango kazi yake kwa sasa baada ya kuachia ngoma hiyo? “Huu ni wimbo wa kwanza kuandikiwa, nimekuwa nikiwaandikia sana nyimbo wasanii wenzangu, lakini huu ameniandikia dogo mmoja anaitwa Mario, aliuleta kwangu ukiwa umekamilika na ni mzuri, mimi nikauboresha ukawa hivyo ulivyo, video inatoka baada ya wiki moja kutoka sasa kwa hiyo mashabiki waendelee kuisapoti Nabembea,’ anasema Ditto.
burudani
WAFANYAKAZI 32 wa iliyokuwa Hoteli ya Kitalii ya 77 ya jijini Arusha walioachishwa kazi Agosti 3, 2000, wamefariki dunia bila kulipwa mafao yao; na baadhi ya wafanyakazi walio hai sasa wanamwomba Rais John Magufuli awasaidie kupata stahiki yao.Wakizungumza katika ofisi za gazeti hili jijini Arusha, Mwenyekiti wa wafanyakazi hao 220 walioachishwa kazi mwaka huo, Ramadhani Issa alisema mbali ya kufariki kwa wenzao, hali za wafanyakazi wengine walio hai ni mbaya sana kimaisha.Alisema wanamuomba Rais Magufuli awasaidie kupata haki zao kwani wamehangaika katika kila ofisi ya serikali wilayani Arusha na mkoani Dodoma bila mafanikio.Issa alidai kwa mujibu wa ripoti ya Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali aliyetambuliwa kwa jina la J.M. Kachenje, ya Februari 28, 2003, ilionesha kuwa wafanyakazi 220 walipaswa kulipwa Sh milioni 217.3 kipindi hicho.Mwandishi wa gazeti hili aliiona ripoti ya Kachenje na kueleza kuwa wafanyakazi hao, walipunjwa mafao yao na kuambulia kulipwa Sh milioni 188.9, hivyo ni tofauti ya Sh milioni 29 ambazo hazijulikani zilipo hadi sasa.Mwenyekiti huyo alisema viongozi wote wa serikali Arusha ngazi ya wilaya, mkoa na Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma, wanajua kilio chao, lakini hawana majibu ya msingi, badala yake hukiri kuwa fedha zilizolipwa zilikuwa pungufu kinyume cha fedha zilizoidhinishwa na Ofisi ya Hazina.“Mheshimiwa Rais tunakuomba sana utusaidie kupata stahiki yetu kwani wenzetu 32 wameshafariki dunia na familia zao ziko taabani bila kupata haki yao, sisi tuliobaki na familia zetu tunahangaika bila mafanikio na hakuna ofisi yako isiyojua hili jambo, lakini hawana majibu mbali ya kukiri kuwa pesa yetu tumepunjwa,” alisema Issa.Katibu wa Wafanyakazi hao, Imelda Singano alisema Serikali ya Rais Magufuli ni serikali sikivu yenye kujali wanyonge na kwa hili ni vema Rais akatoa nafasi kwa baadhi ya viongozi wa Hoteli 77, kumwona na kusikia kilio chao ili aone ni jinsi gani watendaji wake wanavyomwangusha katika utendaji wake wa kila siku.Singano alidai pamoja na jitihada za Rais kuwafagia wala rushwa na wajanja serikalini, bado kuna baadhi ya watendaji wanajiona miungu watu na wanashindwa kusikiliza kero za wananchi, kitu ambacho sio kizuri katika utendaji.“Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa Hoteli 77 kwa sasa tunaishi kama wakimbizi, hatuna pa kulala, kula ya shida, tunakuomba utusaidie kupata stahiki zetu maana naona kila mtendaji wa serikali anaogopa kutoa maamuzi,” alisema Singano.Kwa mujibu wa nyaraka za wafanyakazi hao kutoka Hazina, wafanyakazi hao walipaswa kulipwa kiasi hicho cha fedha, lakini hawakulipwa, mbali ya Hazina kutuma hundi ya kiasi hicho kwa meneja wa wakati huo.
kitaifa
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
uchumi
SERIKALI imepongeza mradi wa XPRIZE kwa kuonesha njia nyingine ya kuwapatia elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu watoto wengi walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo wakati alipotembelea Wilaya ya Mkinga, ikiwa ni mojawapo ya wilaya sita za Mkoa wa Tanga, zinazonufaika na mradi huo.Akizungumza katika mahojiano, Katibu Mkuu huyo alisema kwamba kinachowaondoa watoto wengi katika masomo si lazima iwe mimba kwani wapo watoto wengi hasa wakiume ambao wanakimbia majumbani na kukosa haki yao ya msingi ya elimu.“Huu mradi umetuonesha njia nyingine kabisa ya kukabiliana na tatizo hili,” alisema Dk Akwilapo na kuongeza kuwa ni sera ya serikali ya kuhakikisha kwamba watoto wote hata wale ambao hawakuingia katika mfumo rasmi wanaingizwa katika mfumo wa elimu kwa kupitia taratibu mbalimbali. Miongoni mwa taratibu hizo ni utaratibu wa MEMKWA kwa elimu ya msingi na MESPA kwa sekondari.Alisema mradi huo umeonesha matokeo mazuri kwa sasa kwani tayari watoto 800 wamefikishwa katika shule wakafanyiwa mitihani na kuingizwa kuendelea na madarasa ya pili. Mradi wa XPRIZE ambao utamalizika mwaka kesho ukitumia vishkwambi katika mafunzo kwa watoto waliokosa elimu ya msingi kufikia miaka 9, ni mradi wa dunia ambapo teknolojia inajaribiwa kusaidia wale waliokosa nafasi ya kuingia shule.Akizungumzia hatima ya mradi huo, Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert alisema kwamba mafanikio yake yatawezeshwa kutengenezwa kwa moduli za kufundishia watoto walio nje ya mfumo rasmi wanaotumia lugha ya Kiswahili.Alisema mradi huo wa kutumia vishkwambi kufundisha watoto kwa kutumia programu za kujifunza unahusisha nchi kadhaa na baada ya kukamilika mwakani matokeo yake yatawekwa wazi na hivyo teknolojia kujulikana inavyoweza kutumika kupeleka mafunzo kwa waliokosa elimu rasmi. Imeelezwa kuwa mradi utakapokamilika mwakani utakuwa umewatoa kimasomaso wanafunzi 2,697 katika vitongoji 170 vinavyofanyiwa mradi huu wa majaribio.Vishkwambi hivyo vinachajiwa kwa kutumia nishati jadidifu ya jua katika maeneo maalumu yaliyotengenezwa kwa ajili ya kuzichaji. Mradi huo wa XPRIZE unaotumia ubunifu wa teknolojia unafanyika chini ya uangalizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Kamati ya kitaifa inayohusisha pia Wizara ya Elimu na TAMISEMI. Lengo kuu baada ya mradi huo kukamilika ni kuwapata watoto ambao wataweza kuingizwa darasa la pili na kuendelea na pia kuongeza uwezo wa kumudu masomo kwa watoto wa darasa la pili.
kitaifa
CAIRO, MISRI OFISA wa Polisi wa Misri na washukiwa saba wa genge la kigaidi wameuawa katika makabiliano ya risasi baina ya pande mbili hizo jijini Cairo. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ilisema jana kuwa makabiliano hayo yalitokea juzi Jumanne katika Wilaya ya al-Amiyira, viungani mwa mji mkuu, Cairo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa, askari polisi wengine watatu walijeruhiwa katika mapambano hayo ya risasi, lakini maofisa usalama walifanikiwa kuwaangamiza magaidi saba, mbali na kutwaa silaha zilizokuwa zinatumiwa nao. Wiki iliyopita pia, jeshi la Misri lilizishambulia ngome za magaidi katika eneo la Sinai Kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mashambulizi ya magaidi.  Operesheni hiyo ya maofisa usalama ilijiri siku chache baada ya magaidi kufanya mashambulizi pambizoni mwa eneo la Rafah na kumuua mwanajeshi mmoja wa Misri na kuwajeruhi wawili.  Makundi ya kigaidi huko Misri yameelekeza hujuma na mashambulizi yake katika Mkoa wa Sinai ya Kaskazini na wakati huo huo pia yanafanya hujuma katika maeneo ya katikati na Kusini mwa Sinai na vile vile katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Kundi liitwalo Ansarul Baitul Maqdis ambalo limebadili jina lake na kuwa kundi la Mamlaka ya Sinai baada ya kuungana na kundi la kigaidi la Daesh, ndilo linalotekeleza mashambulizi mengi dhidi ya askari wa Misri.
kimataifa
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
uchumi
KIPANDE cha barabara za magari ya kawaida kutoka eneo la Ubungo hadi Shekilango jijini Dar es Sal aam, kitafungwa kwa takriban miezi miwili kuanzia sasa ili kupisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaofanywa Ubungo katika makutano ya barabara za Mandela na Morogoro.Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kampuni ya Ujenzi ya CCE CC inayojenga barabara hizo, barabara hiyo itafungwa kuanzia O ktoba 6, mwaka huu hadi Novemba mwishoni ili kupisha ujenzi eneo hilo. Ilisema wakati utekelezaji utakapoanza, barabara mbadala itakayotumika ni ile ya Mabasi  Yaendayo Haraka (DART), ambazo mbili zitatumiwa na magari ya kawaida kuanzia kituo cha mabasi hayo cha Ubungo hadi eneo la Benki ya NB C eneo la Ubungo Stendi ya Mabasi ya mikoani.Aidha, barabara hizo mbili zitatumika pia kipindi cha msongamano mkubwa nyakati za asubuhi na jioni na mabasi ya DART yatatumia barabara yake moja kwa eneo hilo. H ata hivyo, katika kutekeleza matumizi ya barabara hizo, ipo michoro inayoongoza magari yenye rangi kijani, nyekundu na nyeupe huku madereva wakitakiwa kuwa waangalifu wakati wa kutumia barabara hizo. Ujenzi wa barabara hizo za juu ulizinduliwa Machi 20 mwaka jana na Rais John Magufuli na mradi huo utagharimu Sh bilioni 247 na utajengwa kwa muda wa miaka mitatu.Wakati ujenzi huo ukisubiriwa kukamilika kwa hamu na kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo na barabara nyingine zinazoingiliana nayo, Septemba 27 mwaka huu, Rais Magufuli alizindua Daraja la Juu la Mfugale eneo la Taraza lililojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 106.9. Daraja hilo lilijengwa na mkandarasi Kampuni ya Japan ya Sumitomi Mitsui kwa muda wa miezi 29, hivyo kukamilika kabla ya muda uliopangwa ambapo lilikuwa likamilike O ktoba 31, mwaka huu.
kitaifa
Zainab Iddy – Dar es salaam KOCHA Msaidizi wa timu ya Yanga, Charles Mkwasa, amesema kuwa katika mazoezi ya siku tano ambayo wachezaji wamefanya mazoezi amebaini uwepo wa nyota walioongezeka uzito jambo lililosababisha awape programu tofauti na wengine. Mkwasa alisema hayo jana wakati akizungumza na vyombo vya habari kabla ya kuanza kwa mazoezi katika  Chuo cha Sheria, Dar es Salaam kwaajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Halmashauri ya Kinondoni (KMC). Mkwassa alisema sababu kubwa ya wachezaji hao watano kuiongezeka uzito ni kushindwa kujipangilia aina ya vyakula walivyokuwa wakitumia pamoja na mazoezi kipindi  cha mapumziko ya janga la Corona. “Kuna wachezaji wameongezeka uzito na kushindwa kuendana na aina ya mazoezi ninayoyatoa sasa hii, imetokana na kushindwa kwao kuchagua aina ya vyakula na  kutofanya mazoezi kipindi cha mapumziko ya corona. “Kutokana na hilo nimelazimika kuwapa programu maalumu ambayo itawapunguza uzito na kuendana na wenzao,bila shaka hadi wiki ijayo watakuwa sawa,”alisema Mkwasa. Wakati huo huo Mkwassa alisema kesho watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya KMC ambayo kwa upande wao wanatarajia itakuwa ngumu kutokana wapinzani wao kuanza mazoezi mapema. “Hii itakuwa mechi ngumu kwetu kwa sababu kwanza tuna tatizo la uzito kwa wachezaji lakini pia wenzetu wameanza mazoezi siku nyingi tofauti na sisi, hata hivyo kitakuwa kipimo kizuri kwetu,”alisema. Katika hatua nyingine kikosi cha Yanga kinatarajia kuingia kambini mara baada ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya KMC. “Kambi itakuwepo mara baada ya mchezo na KMC, tayari viongozi wameshafanya mipango ya jambo hilo hili, yote ni kutaka wachezaji wawe katika ‘levo’ moja,”alisema Mkwasa. Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Juni 13 mwaka huu, ikiwa ni baada ya Serikali kuruhusu shughuli za  michezo kuendelea. Awali Serikali ilipiga marufuku shughuli zinazosababisha mikusanyiko ikiwemo michezo, katazo lililoanza Machi 17 mwaka huu, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona. Ugonjwa wa corona ambao mwa mara ya kwanza ulibainika nchini China, umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani. Athari za ugonjwa huo zilisababisha ligi za michezo mbalimbali, matamasha ya burudani na shughuli nyingine za michezo kusitishwa na mataifa mbalimbali.
kitaifa
Na BADI MCHOMOLO MWAKA 2016 unamalizika leo hii, kuna watu ambao wanafurahia leo hii kumaliza mwaka salama huku wakiwa wametimiza malengo yao, lakini wapo ambao wanamaliza mwaka huu huku wakiwa katika wakati mgumu. Rapa Clifford Harris maarufu kwa jina la T.I ni miongoni mwa wasanii ambao wanamaliza mwaka huku wakiwa katika wakati mgumu, hii inatokana na mke wake Tameka Cottle, kuweka wazi kuwa anataka talaka kutoka kwa baba wa watoto wake watatu. T.I alifunga ndoa na mrembo huyo ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Marekani tangu mwaka 2010, lakini walikuwa katika uhusiano kuanzia mwaka 2001 na kufanikiwa kupata watoto watatu – wawili wa kiume na mmoja wa kike. Chanzo cha mgogoro wa wawili hao kinadaiwa kuwa ni bilionea Floyd Mayweather, bingwa wa mchezo wa ngumi, ambaye hana maelewano mazuri na rapa huyo kwa kipindi kirefu sasa. Mwezi Novemba, mwaka huu mke wa T.I alikuwa jijini Las Vegas ambapo alipata mwaliko kwenye ‘Bush’ ya nyota wa muziki nchini Marekani Mariah Carey. Katika sherehe hiyo ya Mariah, ilionekana kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo nyota wa ngumi duniani Mayweather. Katika kupiga picha za Selfie, mke wa T.I alionekana akipiga picha na bondia huyo ambapo picha hiyo ilisambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Kitendo hicho kilimfanya rapa T.I ajisikie vibaya na kukosa kabisa amani kwa kuwa nyota huyo wa muziki wa Hip Hop ana bifu kubwa na bondia hiyo, ambapo T.I aliwahi kuweka wazi kuwa yupo tayari kupigana na bondia huyo popote watakapokutana. Hilo ni bifu ambalo limedumu kwa muda mrefu, hivyo kitendo cha mke wa T.I kupiga picha na Mayweather kimeleta msuguano kila siku ndani ya nyumba ya wasanii hao, hivyo inadaiwa kwamba Tameka amechoshwa na maneno ya kila siku kutoka kwa rapa huyo hivyo ameona bora adai talaka. Kutokana na hali hiyo ni wazi kwamba T.I ataendelea kujenga uhusiano mbaya na bingwa huyo wa ngumi duniani, kikubwa ni kwamba kwenye mitandao ya kijamii inamwangalia msanii huyo analichukuliaje suala hilo? Kwa upande wa Mayweather, amekuwa bondia ambaye anapenda sana wanawake warembo, amekuwa akihusishwa kutoka na warembo mbalimbali hasa kutokana na matumizi mabaya ya fedha. Inadiwa kwamba endapo anampenda mrembo yeyote yupo tayari atumie kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kutoka naye hata kama yupo mbali na nchini Marekani ambapo Mayweather anaishi, yupo tayari kutuma ndege maalumu kwa ajili ya kumfuata mrembo ambaye anataka kutokana naye na baadaye anapiga picha ambazo zinaonesha wazi kuwa alitoka naye. Mayweather baada ya kutangaza kustaafu ngumi, aliweka wazi kwamba kilichobaki kwake ni kufanya starehe, hivyo aina yenyewe ya starehe ni pamoja na kutoka na warembo mbalimbali. Kutokana na kauli hiyo, leo hii ukiona bondia huyo amepiga picha na mpenzi wako ni kitu cha kujiuliza mara mbilimbili japokuwa inawezekana ikawa ni picha ya kawaida tu isiyo na madhara yoyote. Hadi sasa T.I hajataka kuweka wazi juu ya kuenea kwa taarifa hizo, lakini kwa upande wa watu wa karibu na familia hiyo, wamedai kuwa mke wa T.I yupo tayari kuondoka na anataka talaka, yote hayo ni kutokana na Mayweather.
burudani
NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimetakiwa kupaza sauti ya pamoja kutaka jumuiya ya kimataifa kuiondolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi.Rais John Magufuli ametoa mwito huo kupitia hotuba yake baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa SADC katika mkutano wa 39 wa jumuiya hiyo unaohitimishwa leo jijini Dar es Salaam ambapo siku kama ya jana, ndipo jumuiya hiyo ilipoanzishwa ikiwa na nchi 11 tu.“Kama tunavyojua, hawa ndugu zetu wamekuwa kwenye vikwazo kwa muda mrefu...nchi za SADC zizungumze kwa sauti moja, vikwazo viondolewe Zimbabwe,” amesema Rais Magufuli anayeongoza jumuiya kwa mwaka mmoja kuanzia sasa hadi Agosti mwakani.Alisema licha ya vikwazo kuathiri serikali na wananchi wa Zimbabwe, pia vina athari kwa ukanda wa kusini mwa Afrika.Akifananisha na mwili ambao sehemu moja ikiumia, unaumia wote, alisema athari za vikwazo kwa nchi hiyo zina athari kwa wana- SADC wote.Alisema vikwazo vilivyowekwa havina nafasi tena ikizingatiwa kwamba nchi hiyo imeshaandika ukurasa mpya kwa kufanya uchaguzi na kumpata Rais ambaye ni Emmerson Mnangagwa.Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC, alisema Tanzania katika uenyekiti wake, itahakikisha nchi wanachama zinakuwa na amani na utulivu wa kujiletea maendeleo.Profesa Kabudi ambaye baraza analoongoza lina jukumu la kushauri na kuwasilisha masuala mbali mbali kwa wakuu wa nchi kwa ajili ya uamuzi, alisema Zimbabwe ilishafanya uchaguzi na chini ya Rais Mnangagwa inaendelea vizuri hivyo hakuna sababu za kuendelea kuwekewa vikwazo.Mei mwaka huu, Rais Magufuli akiwa katika ziara ya kikazi nchini Zimbabwe, alimpongeza Rais Mnangagwa kwa hatua madhubuti za mageuzi ya kiuchumi katika nchi hiyo na alitoa mwito jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa.Takribani miaka 17 imefika tangu Zimbabwe ilipowekewa vikwazo na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutoridhishwa na uongozi wa Rais Robert Mugabe aliyeondoka madarakani mwaka juzi.
kitaifa
Na BADI MCHOMOLO TUPO mwishoni mwa mwaka, kama kawaida kwa wiki ya tatu sasa tunakuletea matukio muhimu yaliyopata kutingisha kwa mwaka huu. Leo tunakuletea listi ya mastaa wa mbele ambao walivalishana pete kwa lengo la kuoana, lakini ndoto zao hizo hazikukamilika hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Orodha hii ni hadi juzi Alhamisi wakati makala hii ikiandaliwa. Mariah Carey na James Packer Taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii duniani zilienea habari za nyota wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, bilionea James Packer raia wa nchini Australia. Uhusiano wa wawili hao ulianza tangu 2015 mara baada ya Mariah kuachana na baba watoto wake Nick Cannon, ambaye alifanikiwa kupata naye watoto wawili mapacha, hivyo kuachana kwao kulimpa nafasi mfanyabiashara huyo kutoka nchini Australia kuonesha jeuri ya fedha. Hawakuchelewa kuonesha uhusiano wao, hivyo James aliamua kununua pete ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya bilioni 21 za Kitanzania, hapo hapo kutangaza ndoa ambayo waliweka wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika watakuwa wamefunga. Wengi walikuwa wanaisubiri ndoa hiyo kwa hamu kutokana na fedha zilizotumika kwenye kununua pete, lakini mambo yalikuwa tofauti siku chache baadaye, ambapo ndoto za wawili hao za kufunga ndoa mwaka huu zikafikia mwisho mwezi Oktoba. Kwa sasa wamebaki kuwa na mgogoro wa kupotezana muda. Blac Chyna na Rob Kardashian Blac Chyna ni mwanamitindo maarufu nchini Marekani ambaye alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza akiwa na uhusiano na rapa Tyga, lakini Januari mwaka huu aliweka wazi kuwa anatoka na kaka wa Kim Kardashian, Rob Kardashian. Aprili mwaka huu, mrembo huyo alivishwa pete na mchumba huyo huku wakitangaza kutaka kufunga ndoa Desemba mwaka huu mara baada ya kufanikiwa kupata mtoto wao, kwanza walianza kwa kufanikiwa kupata mtoto mapema Novemba na ndipo watu wakawa wanasubiri ndoa ya wawili hao Desemba. Kwa sasa imebaki stori kwa kuwa wawili hao tayari wameachana mapema Desemba hii kwa madai kwamba familia ya Rob amekuwa na michepuko mingi, hataki ushauri kutoka kwa mrembo, pamoja na migogoro ambayo inaendelea ndani ya familia hiyo ya Kardashian, kwa sasa kila mmoja anaishi kivyake japokuwa wakiwa na mtoto wa mwezi mmoja. Nicki Minaj na Meek Mill Wawili hao wanafanya muziki wa Hip Hop nchini Marekani, walianza uhusiano wao tangu 2015, lakini mapema mwaka huu walitangaza kutaka kufunga ndoa mara baada ya Meek Mill kumvisha pete mchumba huyo. Mapema Novemba mwaka huu kulikuwa na taarifa kwamba wawili hao wameachana, lakini hakuna ukweli huo, bado wapo pamoja na wanaendelea na ratiba yao ya kutaka kufunga ndoa. Ukweli ni kwamba dalili za ndoa hiyo kufanyika mwaka huu hazipo japokuwa wapo kwenye uhusiano, hivyo kwa wiki hii moja iliyobaki kuingia 2017 ni asilimia chache wawili hao kufunga ndoa.  Judith Nyambura ‘Avirl’ na Leslie Mugadza Judith Nyambura ni maarufu kwa jina la Avirl, ni nyota wa muziki kutoka nchini Kenya, tangu mwaka 2015 aliweka wazi kuwa anataka kufunga ndoa na mpenzi wake Leslie Mugadza kutoka nchini Afrika Kusini mara baada ya kumvisha pete. Juni mwaka huu, wawili hao walipanga kulimaliza jambo hilo lakini baada ya muda mrembo huyo aliweka wazi kwa mashabiki wake kwamba hakuna tena ndoa baada ya familia za pande zote mbili kushindwana katika mila, ndoa ya wawili hao ikabaki stori. Miley Cyrus na Liam Hemsworth Wawili hao ni wapenzi wa muda mrefu tangu 2012, na wamekuwa wakiachana na kurudiana ambapo ni zaidi ya mara mbili sasa, lakini Januari mwaka huu waliweka wazi kuwa wanataka kufunga ndoa lakini cha kushangaza hadi sasa dalili za kufunga ndoa hazipo kabisa wamebaki kuvishana pete. Jason Statham na Rosie Whiteley Hao ni nyota wa filamu, wamekuwa kwenye uhusiano wa wazi tangu 2010, lakini mapema mwaka huu Statham alifanikiwa kumvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambapo hafla hiyo ilifanyika nchini Thailand, lakini hadi sasa kimya hakuna dalili zozote za ndoa yao.
burudani
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO   SERIKALI ya China imeisifu Tanzania kwa kuzingatia sera ya uwazi katika ushindanishaji wa zabuni za miradi ya ujenzi, ikilinganishwa na nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa  Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki. Hayo yamesemwa hivi karibuni mjini hapa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya nchini China, Hu Bo wakati  akizungumza na waandishi wa habari  wa Kituo cha Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo (CCTV) waliofika nchini kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali yao nchini Tanzania. Mwenyekiti huyo alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zinazoongoza kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za zabuni za ujenzi, ambapo Serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa kipaumbele kwa makampuni ya ukandarasi ya wazawa kwakukubali maombi yao ya zabuni za ujenzi. “CRJE inafanya shughuli zake katika mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, katika sehemu zote hizoTanzania imekuwa  nchi bora zaidi kwani pamoja na mazingira bora ya kazi zetu lakini pia wakandarasi wazawa wamekuwa wakipewa nafasi katika miradi ya ujenzi,” alisema Hu Bo. Kwa mujibu wa Hu Bo tangu mwaka 1977 kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini Tanzania, hatua inatokana na ushirikiano na uhusiano wa kirafiki uliopo baina ya Serikali ya China na Tanzania. Alitaja baadhi ya  miradi ya Serikali iliyokamilishwa  kampuni hiyo nchini ni pamoja na ujenzi wa ukumbi wa Bunge Dodoma, Jengo  la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Jengo la Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
kitaifa
NA WINFRIDA MTOI TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo itarusha karata yake ya mwisho, itakaposhuka dimbani kuumana na Algeria, katika mchezo wa hatua ya makundi wa fainali za Mataifa ya Afrika(AFCON) zinazoendelea nchini Misri. Stars itashuka dimbani  kucheza mchezo wa tatu huku ikiwa tupu, baada ya kupoteza michezo miwili, ikianza kudungwa mabao 2-0 na Senegal kabla ya kutandikwa mabao 3-2 na majirani zao Kenya ‘Harambee Stars’. Kwa upande wa Algeria,  itaingia uwanjani ikiwa na morali ya juu, baada ya kushinda mechi zake mbili, ikiifumua Kenya mabao 2-0, kisha  kuiliza Senegal bao 1-0. Mchezo huo utakuwa wa kukamilisha ratiba kwa Stars, kwakua matokeo ya aina yoyote hayataivusha hatua ya 16. Hiyo inatokana na kupoteza michezo miwili  iliyopita dhidi ya wapinzani wake katika kundi C, Senegal na Kenya huku Algeria  ikiwa tayari  imefuzu kabla ya mchezo wake wa leo. Kanuni za za mashindano hayo za Shirikisho la Soka Afrika(CAF)zinaeleza kuwa, kama timu  zitalingana pointi, kigezo cha kwanza  kitakachotumika ni kuangalia matokeo ya michezo ya husika zilipokutana. Ieleweke kwamba, tayari Kenya na Senegal kila moja ina pointi tatu, hivyo hata kama Stars  itaifikia moja wapo bado itakosa kigezo cha kusonga mbele kama timu mshindwa bora(best Looser), ambazo timu nne zinapewa nafasi. Hata hivyo, Watanzania wanasubiri kuona namna gani kikosi chao kitaondoka Misri, ikiwa ni kwa heshima kwa kupata ushindi dhidi ya Algeria au fedheha kwa kuangusha pointi. Mara ya mwisho Stars kukutana na Algeria ilikuwa Machi mwaka jana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika kwa Algeria kushinda mabao 4-1,Uwanja wa Mustapha Tchaker. Rekodi za jumla zinaonyesha timu hizo zimekutana mara10, Stars ikishinda mara moja, mabao 2-1 mwaka 1995, ukiwa mchezo wa kufuzu Afcon uliopigwa jijini Dar es Salaam. Matokeo yanaendelea kusalia vichwani mwa Watanzania wengi, ni kipigo cha mabao 7-0 ilichokipata Stars kutoka kwa Algeria ugenini mwaka 2015. Akizungumzia Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, aliielezea Algeria kama timu imara lakini kwa upande wao  wamejiandaa kupata ushindi. “Tumecheza na Algeria mara kadhaa, nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam  tulifungwa 2-0, baadaye tukatoka nao sare  ya mabao 2-2, pia nakumbuka walikuja kutufunga 7 -0, hiyo yote ni historia. “Kwa sasa tunaangalia  namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopita kwa kufanya uamuzi sahihi. “Jumatatu (leo) tunafungua ukurasa mwingine na ni safari nyingine kwa Tanzania na Algeria, huwezi kutabiri nani atakuwa mshindi, lakini tutaingia uwanjani kupambana na kusaka pointi tatu,” alisema Amunike. Algeria inaongoza kundi C, ikiwa na pointi sita, ikifuatiwa na Senegal yenye pointi tatu sawa na Kenya.
michezo
Katika uzinduzi huo, rais amesema kuna haja ya kutafuta majawabu kuhusu namna ya kuongeza maghala ya kuhifadhia mazao kwani kadiri kilimo kinavyoboreshwa mazao yanayozalishwa yanakosa pa kuhifadhiwa.Rais Kikwete aliyasema hayo- Dar es Salaam juzi wakati akizindua kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya Mamlaka ya Soko la Bidhaa Tanzania (CMSA). Alisema uzinduzi wa soko hilo ambalo litaanza kufanya kazi rasmi mwezi Mei, mwakani kwa kuanzia na mazao ya korosho, ufuta, alizeti na mpunga ni muendelezo wa jitihada za serikali katika kuleta mageuzi ya kilimo nchini.“Hii ni habari njema kwa wakulima wa Tanzania kwani katika jitihada zetu za kuleta mageuzi ya kilimo zisingefanikiwa kama Tanzania kusingekuwa na soko la uhakika. Mfumo uliopo sasa unawakandamiza wakulima na kuwanufaisha walanguzi,” alisema Rais Kikwete.Alisema pamoja na kuanzishwa kwa sera ya kilimo kwanza, stakabadhi ghalani, uanzishwaji wa benki ya wakulima na vyama vya ushirika kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo nchini, bado sekta hiyo ilikabiliwa na tatizo la ukosefu wa uhakika wa masoko.Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi wa TMX, Peter Noni alisema kampuni hiyo ilisajiliwa Agosti, mwaka jana kama kiungo muhimu katika mchakato wa kuanzisha soko la bidhaa nchini.Aliwataja wanahisa waanzilishi wa kampuni hiyo kuwa ni msajili wa hazina, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Benki ya Maendeleo (TIB) na Shirika la Vyama vya Ushirika.
uchumi
MAMBO yameanza kuiva kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na kuanzia leo wadau wataanza kutoa maoni yao kuhusu kanuni za uchaguzi huo. Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanaenda vizuri na kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa kanuni za uchaguzi huo.Vyama vya siasa vyenye usajili vinatarajia kutoa maoni yao kwenye kanuni zitakazoongoza uchaguzi huo kuanzia leo Aprili Mosi na kesho Aprili 2, mwaka huu jijini Dodoma.Jafo aliyasema hayo alipozungumza na gazeti hili jijini hapa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika baadaye mwaka huu. Alisema maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya uchaguzi huo yamefanywa na kuwa kwa sasa wanasubiri kukamilika kwa kanuni zitakazosimamia uchaguzi huo.Jafo alisema ofisi yake imepanga kukutana na vyama vya siasa vyenye usajili kwa ajili ya kupata maoni yao kwa ajili ya kanuni hizo kwa siku mbili za Aprili Mosi na 2, mwaka huu jijini Dodoma. Alisema Aprili 3, mwaka huu, utakuwa ni fursa kwa asasi za kiraia kutoa maoni kwenye kanuni hizo na baada ya hapo kurekebishwa tayari kwa kuanza kutumika.“Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yanakwenda vizuri, na kwa sasa tuko katika hatua za mwisho za kukusanya maoni ya wadau kuhusu kanuni za uchaguzi zilizoandaliwa,” alisema Jafo. Aliongeza, “baada ya kupokea maoni ya vyama vya siasa vyenye usajili na kutoka kwa asasi za kiraia, na baada ya kukamilika kwa kanuni tutatangaza tarehe ya uchaguzi. Kimsingi maandalizi yote ya awali yamekamilika.”Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotumika kuchagua viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14 na 21, mwaka 2014, ulishirikisha vyama 15.Katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya vizuri kwa kupata asilimia 84 za kura na kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) kikishika nafasi ya tatu.
kitaifa
NAIROBI –KENYA Mwanamke mmoja mwenye miaka 83 aliyekutwa na gramu 600 za bangi amekutwa na hatia nchini Kenya. Taarifa zilizoripotiwa na Kituo cha Redio cha Capital fm  cha nchini Kenya zinaeleza kuwa mwanamke huyo alitiwa hatiani jana mbele ya Hakimu Mkazi Nelly Kariuki. Akiwa mbele ya hakimu Kariuki jana, Lydia Mumbi Ndirangu alikiri kuwa alikutwa na bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 500 sawa na shilingi za Kitanzania 12,000  katika eneo la Muthinga, jimbo la Tetu. Mtuhumiwa ataendelea kushikiliwa na  atatakiwa kurudi tena mahakamani Julai 15 mwaka huu wakati atakaposomewa hukumu. Kesi inayomkabili bibi hiyo ni ya pili ikihusiana na bangi katika kipindi cha miezi miwili tu nchini Kenya. Mwezi Mei mwaka huu, Mahakama ya Nyeri ilimhukumu mwanamke mmoja wa makamo, kifungo cha miaka 30 bila faini kwa makosa ya kusafirisha bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 2,820  ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania 63,000. Gazeti la daily Nation la nchini Kenya limeandika kuwa inaaminika bibi huyo amekuwa akinunua bangi  mjini Nyeri na kuipeleka kwa mtoto wake wa kiume ambaye huwauzia wateja. Mei 2019 ilitoka ripoti inayoonyesha kuwa Tanzania na Kenya zinaongoza kwa uvutaji wa bangi Afrika mashariki. Kulingana na utafiti wa watumizi wa marijuana uliofanywa na shirika la New Frontier Data kutoka Uingereza, Tanzania ambayo iko katika nafasi ya tano kwa idadi ya watumiaji wa mmea huo barani Afrika, inaongoza eneo la Afrika mashariki ikiwa na watu milioni 3.6 wanaotumia bangi ikifuatiwa na Kenya ambayo iko nafasi ya sita na watu milioni 3.3 na Uganda katika nafasi ya nane ikiwa na watumiaji milioni 2.6. Ripoti hiyo iliyataja mataifa yanayoongoza kwa uvutaji wa bangi barani Afrika ni Nigeria iliyo na watumiaji milioni 20.8, ikifuatiwa na Ethiopia yenye watu milioni 7.1, Misri watu milioni 5.9 huku taifa la Kongo likiwa la 4 na watu milioni 5. Mataifa ya Burundi na Sudan Kusini hayakuorodheshwa. Lakini taifa la Sudan linashikilia nafasi ya 7, ilikiwa na watumizi milioni 2.7, likifuatiwa na Madagascar lenye watu milioni 2.1, Ghana milioni 2, Msumbiji watu milioni 1.9, na Angola watu milioni 1.8. Mataifa ya Afrika yalio na watumizi wa wachache wa bangi kulingana na ripoti hiyo ya 2019 ni pamoja na Zimbabwe iliyo na watu milioni 1.1, Malawi watu milioni 1.2, Niger watu milioni 1.2 na Zambia watu milioni 1.4
kimataifa
ZANZIBAR na Comoro zimeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria wenye lengo la kuzidisha ushirikiano kwenye sekta za maendeleo, kwa manufaa ya pande hizo mbili. Ahadi hiyo ilitolewa jana wakati wa mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, alipokutana na Rais wa Comoro, Azali Assoumani aliyepo mapumzikoni Zanzibar. Katika mazungumzo yao, kwa pamoja waliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria ambao hata hivyo wanakiri kuwa umeimarika kwa muda mrefu na kuleta manufaa kwa nchi na wananchi wake. Viongozi hao walieleza kuwa licha ya kuwa ni majirani, ni ndugu wa damu pia hivyo, kuna haja ya kuendeleza uhu- siano na ushirikiano uliopo. Akizungumza kwa upande wake, Rais Shein alimueleza Rais Azali Assoumani kuwa Zanzibar inathamini uhusiano huo na ushirikiano uliopo sambamba na kuendeleza mkataba. Rais Shein alisema katika mkataba huoo masuala mbalimbali yalitiliwa nguvu yakiwemo ushirikiano katika sekta ya afya, elimu, mila na utamaduni pamoja na masuala mengineyo ambayo tayari yameshaanza kufanyiwa kazi na kuleta tija.
kitaifa
Na Mwandishi Wetu STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na kundi lake zima la Wasafi Classic Baby (WCB), wanatarajia kuanza kupiga ‘live’ kwa kutumia vyombo nyimbo zao zote kuanzia Sikukuu ya Krismasi mwaka huu (Desemba 25) ndani ya Uwanja wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na gazeti hili, Diamond anayetamba kwa wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Utanipenda, alisema mwaka huu umekuwa na mabadiliko makubwa kwake kimuziki na hatua aliyofikia ni kuupeleka muziki huu kimataifa zaidi. “Natarajia kupiga ‘live’ kwa kutumia vyombo nyimbo zangu zote kuanzia Krismasi hii pale Dar Live. “Ujue muziki wetu unatakiwa uendelee kuwa katika ngazi za juu zaidi na ili liwezekane hili inatakiwa tufanye kile wenzetu wanachokifanya,” alisema Diamond. Diamond ambaye kila kukicha anajizolea tuzo za kimataifa, alisema miongoni mwa nyimbo atakazozipiga siku hiyo ni pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa, Utanipenda, Nasema Nawe, Nana, Mdogomdogo na nyingine nyingi. Mbali na Diamond kuburudisha siku hiyo ya Krismasi, Dar Live, bingwa wa muziki wa Singeli, Msagasumu naye atakuwepo jukwaani kuwapa burudani wapenzi wa muziki huo kwa kupiga nyimbo zake zote kali. Burudani itashereheshwa pia na mabingwa wa sarakasi na kucheza muziki wa kila aina, Wakali Dancers ambao watakuwepo kukamilisha hamu ya mashabiki wa burudani kwa kuonesha mbwembwe zote za mjini.  
burudani
MANCHESTER, ENGLAND  BEKI wa kati wa zamani wa timu ya Manchester United, Rio Ferdinand, amethibitisha taarifa zinazosambaa kuwa anaweza kuja kuwa Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa BBC RM Sport, beki huyo ambaye alicheza katika kikosi cha timu hiyo kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 12, tayari amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward kwa ajili ya kutaka kumpa nafasi hiyo. Wamiliki wa timu hiyo kutoka familia ya Glazer, wameonesha nia ya wazi kutaka kumrudisha Ferdinand kwenye bodi ya timu hiyo ambaye alistaafu soka miaka minne iliopita. Bila ya kujali kuwa kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa michezo kwenye kituo cha BT Sport, ameweka wazi kuwa, hatoweza kupata usingizi endapo atapata nafasi hiyo ndani ya Manchester United. “Mwisho wa siku mimi ni binadamu, ninaamini kila mmoja anajua uhusiano wangu na Manchester United, upendo uliopo pande zote mbili. “Endapo nitapewa nafasi hiyo ndani ya klabu kubwa kama ya Manchester United, bila shaka siwezi kukataa, lakini kwa sasa naomba niweke wazi kuwa, nina furaha na kazi yangu ya sasa, ninapenda kukaa kwenye kiti, napenda kuwa studio,” alisema Ferdinand. Aliongeza kwa kusema, endapo atapata nafasi hiyo anaamini atakosa kabisa usingizi kwa kuwa atakuwa kwenye majukumu mazito kwa ajili ya klabu. “Siku zote nimekuwa nikifanya mazungumzo na Ed Woodward tangu nilipoondoka United, hivyo ni wazi nipo kwenye uhusiano mkubwa na kiongozi huyo, sijakutana mara kwa mara lakini muda mwingi tunawasiliana kwa kutumia simu. “Kila kitu kinawezekana na kama nitapata nafasi hiyo basi ninaamini sitoweza kulala kwa kuwa nitakuwa na majukumu mazito kwa ajili ya kuipigania timu,” aliongeza mchezaji huyo wa zamani raia wa nchini England.
kimataifa
SERIKALI imekabidhi vipima ulevi kwa ajili ya wasimamizi na madereva wa treni za abiria na mizigo ambavyo vitasaidia kubaini kiwango cha ulevi.Vifaa hivyo vimetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema wametoa vifaa hivyo kuhakikisha usalama unakuwapo na matukio ya ajali yanapungua kutokana na ushughulikia ulevi unaoathiri miundombinu na maisha ya watu.Ngewe amesema vifaa vitano vimekabidhiwa kwa Tazara na 11 kwa TRC. Kaimu Mkurugenzi wa Reli katika Sumatra, Lameck Kamando alisema vifaa hivyo kila kimoja kina uwezo wa kuhifadhi matukio 65,000 na kina uwezo wa kutoa taarifa za mahali tukio liliporekodiwa (GPS).Vina uwezo wa kuhamisha taarifa kwenda kwenye kompyuta, na kuchaji kwenye gari, umeme wa nyumbani. Vina kifaa maalumu cha kuhifadhi chaji, uwezo wa kufanya kipimo kila baada ya sekunde 30 na inafanya kazi kwenye mazingira ya joto na baridi.Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema vitasaidia kubaini kiwango cha ulevi kwa wafanyakazi wa treni kabla ya kuanza safari, wawapo safarini na wanapomaliza safari ili kudhibiti ipasavyo matukio hatarishi na ajali zinazoweza kujitokeza.Kamwelwe alisema ajali zinazosababishwa na makosa ya kibinadamu ni nyingi.Alisema asilimia 65 ya ajali zinazotokea kwenye reli zinachangiwa na makosa ya kibinadamu ukiwamo ulevi. Pia kwa upande wa barabara asilimia 80 huchangiwa na makosa hayo.“Kwa kuwa serikali imewekeza na inaendelea kuwekeza katika usafiri wa reli, juhudi hizi haziwezi kuzaa matunda endapo waendeshaji na watoa huduma wa vyombo husika hawatakuwa makini kulinda usalama wa abiria, mizigo, vyombo na miundombinu hiyo,” alisema Kamwelwe.Alisema makabidhiano ya vifaa hivyo ni ishara ya namna serikali inavyozingatia kwa vitendo usalama katika reli.Alisema serikali inategemea baada ya kuanza kutumika vifaa hivyo, vihatarishi au matukio ya ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu zitapungua.“Iwapo vifaa hivi vitatumika ipasavyo tutajihakikishia usalama wa abiria, mizigo na wafanyakazi wenyewe na kuweza kufikia azma ya Tanzania ya viwanda kwa kupunguza ajali na kuongeza tija katika huduma za reli,” alisema.Waziri alitoa mfano wa ajali za hivi karibuni ni pamoja na tukio la Agosti 29 ambalo treni za mizigo kugongana uso kwa uso kati ya stesheni za Itulu na Tabora. Lingine ni la Agosti 13 mwaka huu la treni ya abiria kushindwa kusimama kwenye stesheni ya Malongwe na baadaye dereva kulazimika kurudi nyuma.“Ni dalili tosha za kukosekana kwa umakini na viashiria hatarishi katika uongozaji na uendeshaji wa treni,” alisema na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitafupisha uchunguzi wa ajali iwapo itatokea kwani suala la ulevi halitakuwa na nafasi.Aliagiza Tazara na TRC kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kufika kazini wakiwa wamelewa au kutumia kilevi wawapo kazini.“Tumezoea kusikia kuwa hatua hazichukuliwi kwa kusubiri uchunguzi, suala la kumbaini mfanyakazi aliyetumia kilevi halina uchunguzi zaidi ya matokeo mara baada ya kupima ulevi,” alisema.Alikitaka Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU) kuendelea kuelimisha wafanyakazi juu ya madhara ya ulevi na matumizi ya kilevi kazini.“Trawu iwe ya kwanza kuwakemea na ikiwezekana iwe ya kwanza kuripoti matukio ya aina hiyo kwenye vyombo husika. Mara nyingi mmekuwa mkionekana kuwatetea wafanyakazi wanapochukuliwa hatua na kudai kwamba wameonewa, lakini wanapofanya makosa hamuwaonyi, badilikeni,” alisema waziri.Meneja Mkuu wa Tazara Tanzania, Fuad Abdallah alisema maagizo yote wameyapokea na watayatekeleza.Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema watatekeleza na kutoa mrejesho lengo likiwa ni kuhakikisha usafiri wa reli unakuwa wa uhakika na salama wakati wote.
kitaifa
RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka ameahidi kutoa Sh 500,000/- kwa kila mwanariadha atakayefikia viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.Mtaka aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akiwaaga wanariadha wanane wa Tanzania watakaoshiriki mbio za kimataifa za Nagai Marathon zitakazofanyika Oktoba 21, ambazo zinatambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF).Amesema, yuko tayari kutoa kiasi cha Sh milioni 4 endapo wanariadha hao wote wanane watafuzu kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki 2020, ambapo viwango hivyo pia vitawawezesha kushiriki mashindano mbalimbali kuanzia mwakani.Amesema ni vizuri endapo wanariadha hao watafuzu mapema kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki kwani watakuwa na muda mwingi wa kufanya maandalizi ya kushiriki michezo hiyo.Pia alisema watakuwa pia wamefuzu kwa mashindano yote makubwa ya mwakani, hivyo aliwataka kwenda Nagai kupambana iwezekanavyo ili kufuzu kwa michezo hiyo mikubwa na kupata fedha hizi.Alisema moja ya jukumu la RT mwakani kuwa na idadi kubwa ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na imeahidi kuandaa wanariadha wazuri , walioandaliwa vizuri, ambao pia watafanya vizuri kwa ajili ya mashindano.Aliwaambia kuwa watumie vizuri mchezo huo kwani utawawezesha kupata fedha nyingi, ajira na hata vyeo kwa wale walioajiriwa tayari.Alisema kwa wale walio majeshini endapo watakuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali, watapanda vyeo haraka na kuwapita hata wale walioingia jeshini kwa ajili ya visomo vyao.Alisema matarajio ya RT ni kuona vijana hao nane wanaokwenda Nagai, wanafuzu kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpiki na kuahidi kuwaweka kambini mapema kwa ajili ya maandalizi ya mashindano mbalimbali.Balozi wa Hiyari wa Shirika la Misaada ya Kimaendeleo la Japan (Jica), Juma Ikangaa aliwataka wanariadha hao kutotoa visingizio endapo watafanya vibaya katika mbio hizo na zingine.Mkuu wa msafara wa timu hiyo iliyoondoka nchini jana kwenda Nagai, Mohamed Kiganja alisema kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika mbio hizo na kuwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi wowote.Wanariadha hao wakiwa Nagai, Japan watashiriki katika mbio za kilometa 21 na 42, yaani nusu marathon pamoja na zile za full marathon.Wanariadha waliomo katika timu hiyo ni pamoja na Sylivia Masatu, Amina Mohamed, Marco Joseph, Fabian Sulle, Angelina John, Rozalia Fabian, Nilbaldo Peter na Neema Gadiye.Mbali na Kiganja, viongozi wengine katika msafara huo ni pamoja na katibu msaidizi wa RT, Ombeni Zavalla, Lucy Henry wa Jica, Kassim Saleh, Benson Chacha wa BMT na Ikangaa.
michezo
Derick Milton, Simiyu Serikali imetaifisha pamba inayodaiwa kuwa ya magendo ikiwa ni siku mbili baada ya kukamatwa kwa gari aina ya scania yenye namba za usajili T917 BCN ikiwa na pamba tani zaidi ya 20. Pamba hiyo ilikamatwa katika kijiji cha Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 12, mwaka huu saa tano usiku, ikisafirishwa bila kibali maalumu huku ikiwa haijulikani wapi inapelekwa wapi imenunuliwa wapi. Akitoa uamuzi ya kuitafisha pamba hiyo leo Jumatano agosti 14, Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga amesema uchunguzi umeonyesha kuwa pamba hiyo ilinunuliwa kwa njia za machinga kwa Sh 700 hadi 900 kutoka kwa wakulima. “Wakati serikali ikipambana na watu wanaonunua pamba kwa njia za kimachinga, bado wako wafanyabishara wanaendelea kupiga vita juhudi hizo kwa kuendeleza biashara hiyo na kuwanyonya wakulima. “Baada ya wahusika kushindwa kujitokeza, sasa kama Mkuu wa Wilaya nachukua uamuzi wa kuitaifisha pamba hii na tunaenda kuiuza kwenye viwanda vya kuchambua pamba leo hii na fedha zote zitapelekwa kununua vifaa vya kukamilisha ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Simiyu,” amesema Kiswaga. Amesema Ofisi yake haitalala ili kuhakikisha inapambana na biashara hiyo ili wakulima wa pamba waweze kunufaika na zao hilo. Aidha, amesema pamba hiyo ina thamani ya zaidi ya Sh milioni 10, na mara baada ya kuuzwa uchunguzi utaendelea kujua nani mhusika mkuu na wakati huo huo gari litaendelea kushikiliwa.
kitaifa
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
uchumi
WASHINGTON, MAREKANI URUSI na Marekani zimerushiana maneno makali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa juzi, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwa kutishia kuanzisha mapambano mapya ya kutengeneza silaha. Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa mataifa hayo mawili kwa upande wake  China imesisitiza  kuwa haitojihusisha kwenye makubaliano yoyote mapya ya makombora. Mapema mwezi huu, Marekani na Urusi zilisitisha mkataba unaozuia kutengeneza makombora ya masafa mafupi – INF, uliofikiwa wakati wa enzi ya vita baridi, baada ya kila mmoja kumlaumu mwenzake kwa kukiuka makubaliano hayo. Urusi inasema Marekani inajiandaa kwa “mashindano ya kujirundukia silaha.” Marekani kwa upande wake inasema haitaki “kupakata mikono” wakati Moscow inaendelea kujiimarisha kijeshi. Urusi imependekeza kuitishwa kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya Marekani kufanya jaribio la nyuklia na kufyatua kombora la masafa ya wastani mapema wiki hii. Kombora hilo ni miongoni mwa yale ambayo yamepigwa marufuku kufanyiwa majaribio.
kimataifa
Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 ikizidiwa pointi moja na vinara Yanga wanaoongoza ligi hiyo kwa sasa wakiwa na pointi 46.Akizungumza na gazeti hili Hall, alikiri ugumu uliopo msimu huu lakini ameahidi kikosi chake kitaendelea kupambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha wanawavua Yanga taji hilo na kulivaa wao.“Najua siyo kazi nyepesi kwasababu ligi ni ngumu na ushindani kati ya timu na timu ni mkubwa lakini najivunia kuwa na kikosi bora ambacho naamini kinaweza kupambana na kupata matokeo mazuri katika mechi zilizopo mbele yetu,’ alisema Hall Kocha huyo kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa Coastal Union, kimevuruga mikakati yao ya kuhakikisha hawapotezi mchezo lakini bado wana nafasi ya kuhakikisha hawarudii makosa hayo ya kupoteza mchezo mwingine hadi mwisho wa ligi.Alisema hilo linawezekana kutokana na kuwa na imani kubwa aliyokuwa nayo kwenye kikosi chake ambacho siku zote kimekuwa kikicheza kwenye kiwango cha juu na kupata matokeo yanayowaweka kwenye nafasi hiyo waliyopo kwa sasa.Aidha kocha huyo alisema kikosi chake kwa sasa kipo kwenye mikakati kabambe kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa Jumatano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.“Itakuwa mechi ngumu, kwasababu tunacheza ugenini na wapinzani wetu wameimarika sana tofauti na ilivyokuwa mzunguko wa kwanza lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kama tulivyofanya kwa Mbeya City Jumamosi,” alisema Hall.Azam na Yanga ndiyo timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo kwa sasa baada ya Simba kupoteza mchezo wa Jumamosi dhidi ya watani wao wa jadi vijana wa Jangwani.
michezo
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limependekeza kuanzisha mfumo wa ulinzi wa waandishi wa habari nchini wakati wa kutekeleza kazi zao za kila siku ili wasidhuriwe na mtu yeyote.Mapendekezo hayo ni pamoja kuunda kikosi kazi ambacho kitajumuisha waandishi wa habari, vyombo vya ulinzi na usalama, mashirika ya kiraia na wadau wengine kuona jinsi mfumo huo utafanya kazi.Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema hayo wakati anafunga mkutano mkuu wa nne wa mwaka wa mashauriano kati ya baraza hilo na wahariri na wadau mbalimbali wa habari jijini Arusha.Amesema suala la kuunda mfumo wa kitaifa wa kusimamia mwandishi na mfanyakazi katika vyombo vya habari limekuwa likipigiwa kelele na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) na kwamba mpaka sasa baadhi ya nchi tayari zina mfumo huo, bado Tanzania.“Baada ya kumaliza mkutano huu wa siku mbili tulijigawa katika makundi na kujadili kuanzisha mfumo wa kitaifa wa kusimamia mwandishi na mfanyakazi katika vyombo vya habari,” amesema Mukajanga.Amesema mapendekezo hayo yamelenga kujua jinsi ya kumlinda mwandishi wa habari kimwili dhidi ya matukio ya kupigwa, kutekwa na kudhuriwa, kumlinda kidijiti, taarifa zake, takwimu za vyombo anavyotumia katika kazi, kompyuta, simu ili visiweze kuingiliwa na kuharibiwa taarifa alizochukua.Katibu huyo Mtendaji alibainisha kuwa baada ya mapendekezo hayo, kazi hiyo itaanza mara moja kwa kuratibu uundwaji wa kikosi kazi hicho ndani ya muda wa kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja.Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Neville Meena amesema ili kulinda usalama wa mwandishi wa habari, lazima taasisi za kihabari zifanye kazi kwa ushirikiano ili kuleta matokeo chanya kwao.Amewataka pia waandishi wa habari kujilinda wanavyoishi, ili ratiba zao za kila siku zisitabirike.“Ili kufanikiwa lazima taasisi za habari zifanye kazi kwa ushirikiano. MCT, TEF, MISA-TAN, UTPC zikifanya kazi pamoja zitaleta matokeo mazuri kumlinda mwandishi na mfanyakazi wa habari,” amesema.“Mwandishi wa habari unatakiwa ujilinde, ratiba zako zisitabirike... siyo unakuwa katika njia moja au eneo moja kila siku. Hii ni kazi ya hatari ingawaje ukitafutwa utapatikana lakini jilindeni na vile vile jiungeni kwenye vyama vya habari katika mikoa yenu ili mkipata matatizo mjue pa kuanzia,” amesema.
kitaifa
SHIRIKA la Posta (TPC) limetapanya zaidi ya sh. Milioni 10 na viwanja 198. Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dk. Harun Kondo katika kikao cha viongozi waandamizi wa shirika hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Dk. Kondo alisema utapanywaji wa mali na fedha za shirika hilo uligunduliwa na bodi ambayo baada ya kuteuliwa kazi yake ya kwanza ilikuwa kuhakiki mali za shirika na ukaguzi wa fedha. Alisema wakati wa ukaguzi huo, bodi ilibaini kuwepo kwa akaunti 120 za shirika katika benki mbalimbali ambazo iliamua kuzifunga wakati ikiendelea na ukaguzi. Dk. Kondo alisema ukaguzi ulibaini viwanja 198 vya shirika vilikuwa vimeporwa na kumilikishwa kwa watu na binafsi huku kukiwa hakuna maelezo yeyote kuhusu viwanja hivyo kuhamishwa umiliki wake. “Tulibaini matumizi ya fedha yalikuwa ya ovyo na shirika halikuwa na akiba hata shilingi moja huku likiwa linawadai wateja wake Sh. bilioni 16. Watendaji walikuwa hawazifuatilii. “Kuna methali inasema anayeficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Kwa kuwa shirika hili ni mali ya umma ni vema jamii ikatambua madudu tuliyoyabaini na sisi kama bodi tulisema liwalo na liwe madudu lazima yabainike na watendaji wabovu wawajibishwe,” alisema Dk.Kondo. Akizungumzia mwenendo wa ukaguzi wa mali za shirika mikoani, alisema bodi ilibaini baadhi ya viwanja vilivyoporwa vilishajengwa nyumba na watu binafsi. Alisema hivi sasa utaratibu wa kuvirudisha kwenye miliki ya shirika unafanyika. “Tulipokuwa tukikabidhiwa ripoti ya utendaji kazi na mali za shirika hakukuwa na orodha ya kiwanja hata kimoja kinachomilikiwa na shirika, tuliingiwa na wasiwasi tukaamua kufuatilia. “Wakati tunaanza kazi hii tulipigwa vita kweli lakini wengi waliotupiga vita ni wale waliokuwa wanafahamu madudu ndani ya shirika hivyo waliona tunaweza kuwaumbua na tunashukuru hadi sasa tumefanikiwa kuvirejesha viwanja 198,” alisema Dk. Kondo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, bodi pia ilibaini shirika lilikuwa halijawahi kufanya hesabu za mwaka ndani ya miaka tisa na deni lililokuwa nje lilikuwa kubwa. Kwamba iliamua kuwafuatilia wadaiwa sugu ambao walilipa Sh. bilioni 10. “Ajabu, baada ya kuzikusanya fedha hizo, baadhi ya watendaji walichukua Shilingi Bilioni Nane, wakazitumia bila kuishirikisha bodi. Tulipowabaini tulichukua hatua, baadhi yao tuliwafukuza kazi. “Wengine tliwashtaki mahakamani na wapo tuliowafikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU),” alisema Dk. Kondo. Alisema ili kukabiliana ubadhirifu wa mali za shirika bodi iliamua kununua mashine mpya ya kisasa ya ukaguzi. Aidha, mwenyekiti huyo alisema wakati wa ukaguzi wav yeti vyeki, wafanyakazi 65 waliondolewa kazini. Naye Mtendaji Mkuu wa TPC alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), wapo kwenye mchakato wa kuanzisha anuani za makazi.
kitaifa
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemwachia huru Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Theophillo Bwekea, baada ya Jamhuri kuonyesha haina nia ya kuendelea na kesi hiyo. Bwekea alikuwa akituhumiwa kupokea rushwa ya Sh milioni 161.7 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira. Wakili wa Serikali, Odossa Olombe, alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respiciou Mwijage kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Hivyo aliomba kuondoa kesi hiyo chini ya kifungu cha sheria namba 98(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) aya ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hakimu Mwijage aliyakubali maombi ya upande wa Jamhuri na kuamuru mshtakiwa kuachiwa huru chini ya kifungu cha sheria namba 98(a) cha CPA. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka Januari 20, 2015. Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai, awali akisoma mashtaka alidai kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 161,700,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow. Kabla ya kufanya kazi REA, Theophillo alikuwa Wizara ya Nishati na Madini, kitengo cha kusimamia umeme, ambako anadaiwa alishiriki kutunga sera ya kampuni binafsi kuuza umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na ilipoanza kutumika, Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ilikuwa ya kwanza kupata zabuni. Wakili Swai, alidai Februari 12, 2014 katika Benki ya Mkombozi, mshtakiwa akiwa Mhandisi Mkuu wa REA, kwa rushwa alijipatia Sh milioni 161.7 kupitia akaunti namba 00410102643901 fedha ambazo ni sehemu ya zilizokuwapo katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Alidai fedha hizo aliingiziwa katika akaunti yake na Rugemalira ambaye ni mshauri binafsi wa kimataifa, Mkurugenzi wa VIP Engineering na alikuwa Mkurugenzi wa IPTL. Fedha hizo zinadaiwa alipewa zawadi kwa kuwa alikuwa mmoja wa wajumbe walioandaa sera zilizoruhusu sekta binafsi kuuza umeme Tanesco. Mshtakiwa huyo alikuwa nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali ama kutoka taasisi inayotambulika waliotakiwa kuwa na barua za utambulisho na kila mmoja kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 25.
kitaifa
['Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski ametoa kauli ya kebehi kwa wapinzani wake wa zamani Tottenham kwa kusema kuwa Serge Gnabry inabidi awe mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal. Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii. ', 'Kocha wa zamani wa England Fabio Capello amefichua kuwa alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa mkopo kipindi akiinoa timu ya Juventus. (Sky Sports Italia via Mail)', 'Mchezaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33, na Callum Wilson, 27, wa Bournemouth wapo katika rada za usajili wa klabu ya Manchester United ambao wanatafuta kwa nguvu zote mshambuliaji wa kusajili katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Sky Sports)', 'Kiungo nyota wa Norway Martin Odegaard, 20, anapanga kurejea Real Madrid japo klabu za Manchester United na Liverpool. Kiungo huyo kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Real Sociedad. (Goal)', 'Kiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen bado anaamini mipango yake ya kuhamia Real Madrid inaweza kufanikiwa, na wakala wake mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kwenda Uhispania kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madrid. (Star)', 'Real Madrid walifikiria kumteaua Antonio Conte kuwa kocha wao mwaka jana, kabla ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea kurudi dimbani na klabu ya Inter Milan. (Fichajes.net, via Calciomercato)', 'Klabu ya soka ya LA Galaxy ya Marekani inaripotiwa kumnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Rangers ya Uskochi na raia wa Colombia Alfredo Morelos, 23. (Star)', 'Kocha wa Arsenal Unai Emery amegoma kukanusha uwezekano wa kiungo Mesut Ozil kuihama klabu hiyo mwezi Januari. (Sun) ', 'Kocha wa zamani wa Brighton Chris Hughton amekataa ofa ya kuinoa klabu inayosuasua ya daraja la kwanza, Stoke City. (Mirror)', 'Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anatumaini kuwa ataungana tenza na winga Willian katika klabu ya Juventus. Hata hivyo kocha wa Chelsea Frank Lampard amefichua kuwa mchezaji huyo raia wa Brazil yupo katika "mazungumzo" ya kuongeza mkataba. (Calciomercato, via Sun)', "Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri ana matumaini ya kuungana tena na kiungo mkabaji N'Golo Kante, 28. Sarri ambaye kwa sasa anainoa Juventus yupo tayari kumnunua kiungo huyo raia wa Ufaransa kwa kitita cha takribani pauni milioni 70. (Mail)", 'Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kama sehemu ya kufufua kikosi cha Manchester United. (Manchester Evening News)', 'Manchester United pia wanaendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 22, ambapo wanaweza kumsajili kwa pauni milioni 80. (Mail)', 'Mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 24, anaamini wakati wa klabu yake kushinda michuano ya Champions League umekaribia, japo amewaasa wachezaji wenzake kusalia na subira.(Mirror)', 'Wachezaji wa Tottenham wanahofu juu ya mustakabali wa wa kocha wao Mauricio Pochettino, na wanaamini raia huyo wa Argentina anatafuta njia ya kuondoka klabuni hapo. (Mail)', 'Mshambuliaji fundi wa zamani wa Spurs na Manchester United Dimitar Berbatov anaamini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy atafanya mazungumzo na Pochettino "wiki hii" ili "kupata majibu sahihi na njia muafaka ya kusonga mbele." (Star)']
michezo