content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Anna Potinus Rais Dk. John Magufuli ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbabwe ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo vimelemaza uchumi wa taifa hilo. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 17, alipokuwa akihutubia wakuu wa nchi Wanachama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo na Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob ambapo ataingoza kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe vinaathiri ushirikiano wake katika Jumuiya ya jumuiya hii ya SADC hivyo ninomba nchi hiyo ipewe nafasi ya pili kwa sababu ina utawala mpya,” amesema. Zimbabwe iliwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kutokana na hatua ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, kuchukua kwa lazima ardhi ya wahamiaji wenye asili ya kizungu. Aidha Rais Magufuli ameapa kuhakikisha amani inadumishwa ili kukwamua uchumi wa mataifa wanachama wa SADC. “Tunaahidi kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC kuhakikisha kupitia mkutano huu ndoto na mawazo ya Baba yetu wa Taifa pamoja na viongozi wengine waanzilishi wa Jumuiya hii yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo,” amesema.
kimataifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ukosefu wa uadilifu ni eneo ambalo lilitia doa utendaji wa sekta binafsi hususani pale ambapo ilishirikiana na Serikali.Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 18 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa niaba ya Rais John Magufuli.Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema, uadilifu ni changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali na TPSF.Waziri Mkuu ameitaka TPSF ijifunze kwa wenzao walioendelea kwa kutokuwa na vitendo vya rushwa, kwa kutoa adhabu kwa wanaoenda kinyume na misingi ya uadilifu walijiwekea.Amesema kufanya hivyo watakuwa wamejiongezea nguvu yao kama taasisi lakini pia kupeleka ujumbe kwa wanachama wao kuwa wanathamini haki na kuchukia rushwa. Aliongeza kuwa shughuli za sekta binafsi zimeendelea kuongoza katika kuchangia pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.Amesema, kwa mujibu wa takwimu sekta ya utalii inachangia asilimia tisa, huduma asilimia 35, kilimo asilimia 26.6, madini asilimia 3.3 na sekta ya viwanda inachangia takribani asilimia 10.Waziri Mkuu alisema serikali kwa upande wake, itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kuboresha miundombinu, kutoa vivutio kwenye kodi, kanuni na sheria ili kukuza sekta binafsi.Hivyo, Waziri Mkuu alisema sekta binafsi nchini nayo haina budi kutumia vema fursa hiyo ya uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa kuwekeza kwenye uchumi wa nchi.Mwenyekiti wa TPSF aliyemaliza muda wake, Reginald Mengi aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa hatua mbalimbali inayozichukua ikiwemo ya kupambana na rushwa na kuboresha mazingira mazuri ya kufanya biashara.Mengi amesema, takwimu za serikali na Benki ya Dunia zinaonesha uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2018 unatarajiwa kukua kwa kwa asilimia 6.9 na pato la mtu mmoja mmoja kuwa dola za kimarekani 1,000 kwa mwaka.Mbali ya kuishukuru serikali aliipongeza pia kwa maamuzi iliyochukua ya kutoa msamaha wa riba na adhabu za malimbikizo ya kodi kwa asilimia 100, alisema na kuongeza kuwa hiyo itahamasisha ulipaji kodi na pia kuondoa mizigo ya kodi na tozo kwa wafanyabiashara.Mwakalishi wa Wadau wa Maendeleo ambaye pia ni Mkurugenzi wa USAID hapa Tanzania, Andrew Karas alipongeza kuwepo kwa chombo kinachosimamia sekta binafsi kwani kinawawakilisha watu moja kwa moja.
kitaifa
WAKATI baadhi ya watu wakiwachukulia waendesha pikipiki za kubeba abiria (bodaboda), kuwa watu wasio na mwelekeo, katika nchi za Tanzania na Kenya, wameamua kuchukua mwelekeo mpya na kufanya mapinduzi makubwa, kwa kuanzisha mashirikisho na kuanzisha benki zao.Nchini Tanzania, waendesha bodaboda wameanzisha shirikisho lao, litakalozinduliwa mwezi huu.Pamoja na mambo mengine, shirikisho hilo litaweka mikakati ya kuwapatia wanachama wake bima za afya, kujenga benki na kuweka mfumo maalum wa kukabiliana na uhalifu.Katika hatua za awali, shirikisho hilo litatoa mikopo kwa waendesha pikipiki 1,000, huku likiendelea na mikakati ya kujenga benki yao na kujiwekea akiba, itakayowasaidia kukuza uchumi wao.Mbali na kutoa fursa za kimaendeleo na mikopo kwa wanachama wake, shirikisho hilo pia litaweka utaratibu wa madereva wa bodaboda kuvaa sare maalum, zitakazowatambulisha kila mahali walipo.Pia, pikipiki zao zitafungwa vifaa maalum, vitakavyowezesha kubaini watakaojihusisha na uharifu na kuvunja sheria za barabara. Pia, kutakuwa na kanzidata maalum.Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Pikipiki Dar es Salaam linalojumuisha vyama vyote vya waendesha pikipiki, Edward Mwenisongole, akizungumza na HabariLeo Afrika Mashariki alisema baada ya kuwa na changamoto katika kuungana pamoja, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwaita na kuwasaidia kuunda shirikisho hilo.Alisema katika uzinduzi wa shirikisho hilo, wataalika viongozi wa vyama vya waendesha pikipiki mikoani ili kuweka mikakati ya kuunda shirikisho la kitaifa, litakalowezesha kusajili wanachama na kuanza mikakati ya kujenga benki.Alisema siku hiyo ya uzinduzi, wanachama 1,000 watapatiwa mikopo ya pikikipi. Alisema wana mikakati ya kuwapatia bima ya afya, wanachama wote na kugawa gawio.Wakati Tanzania wakiweka mikakati hiyo, Chama cha Kuweka na Kukopa cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda Operators’ Saccos) kilichoundwa miaka minne iliyopita katika Kaunti ya Murang’a nchini Kenya, kimebadilisha maisha ya wanachama wake kiuchumi.Chama hicho maarufu kama Kabati Flyover Operators Saccos, kina wanachama 87 na kilipata faida ya Sh milioni 1.1 za Kenya mwaka jana.Alisema chama hicho, kinatoa mikopo nafuu kwa wanachama wake, inayowawezesha kusomesha watoto wao na kusaidia familia, hivyo kupata faida kutokana na riba wanazotozwa wanachama. Mwaka jana walitoa mikopo ya Sh milioni 5.6 za Kenya.Makamu Mwenyekiti wa Saccos hiyo, George Njoroge, alisema pia wamenunua ardhi ya ekari mbili yenye thamani ya Sh milioni 1.2 za nchi hiyo na kuanzisha programu ya kusaidia wanachama wanaoumwa au kufariki.
kitaifa
Hivi karibuni ilifanyika michezo kadhaa, ambapo moja kati ya malengo yake ilikuwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.Mchezo wa mwisho ulikuwa ni kati ya timu ya Yanga dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda uliofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita na pia uliwahi kufanyika mchezo kati ya timu ya wachezaji wa zamani wa Barcelona dhidi ya Taifa Stars.Akizungumza na gazeti hili jana Mwenyekiti wa TAS, Ernest Kimaya alisema kuwa chama hicho katika mchezo wa mwisho kati ya Villa dhidi ya Yanga hakikushirikishwa hata mara moja katika mazungumzo ya kuchangishiwa fedha.Alisema kuwa alikuwa akisikia tu katika vyombo vya habari kuwa kuna michango ambayo itapelekwa kwenye chama cha albino kutokana na mapato ya kiingilio lakini hata baada ya mchezo hakujawa na msaada wowote.Alisema kwa kawaida kabla ya kutumia kigezo cha kuwasaidia albino kunakuwa na mazungumzo kati ya TAS na wale wanaochangisha fedha lakini katika hilo hakuna kilichofanyika.Alisema kuwa alichukua uamuzi wa kuonana na maofisa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mwandaaji wa mchezo huo lakini hakukua na majibu ya kuridhisha.“Yule mwandaaji nilimpigia simu lakini alisema kuwa lengo ni kusaidia watu wenye shida na lakini hata hivyo nilipomuuliza mbona anatumia jina la albino kwenye kampeni zake na kutaka kujua ni kwa kiasi gani albino wananufaika alishindwa kutoa majibu,” alisema mwenyekiti huyo.Gazeti hili liliwasiliana na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto aliyesema kuwa kazi ya shirikisho hilo ilikuwa ni kuangalia kuhusu namna ya uendeshwaji wa mechi hiyo na sio vinginevyo.Alisema kwa upande wa TFF hawawezi kujua ni shilingi ngapi albino wamepewa, lakini anaweza kujua hilo ni muandaaji wa mchezo huo.“Sisi tulisimamia yale ambayo yalikuwa yanahusu upande wetu na kisha hayo mengine ni makubaliano na wale wahusika kwa maana ya Chama cha Albino na muandaaji na sisi tunakuwa hatupo,” alisema msemaji huyo.Gazeti hili lilifanya jitiada za kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza, Mossi Magere aliyesema kuwa fedha walizozipata zinalenga kuanzisha kituo cha kusaidia watoto wenye mazingira magumu.“Wiki ijayo tutaonesha waandishi wa habari mahala ambapo kituo kitakuja kujengwa na hiyo sio siri kabisa kwa kuwa ni fedha kwa ajili ya kusaidia jamii na sio kwamba ni wenye ulemavu wa ngozi peke yake ila watoto wote wenye kuishi mazingira hatarishi,”alisema Mossi.
michezo
Na Muhammed Khamis (UoI) Iringa, UCHAKAVU wa mabomba ya kusambazia maji safi na salama yaliyowekwa miaka ya 1960 katika Tarafa ya Isimani, Wilaya ya Iringa Vijijini, wana changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa miaka 20 sasa.  Uwepo wa changamoto hiyo unawalazimu wananchi wa eneo hilo kutumia maji yenye chumvi kwa mahitaji yao ya kila siku na hivyo kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza. Mkazi wa tarafa hiyo, Letisia Kalinga, alisema changamoto ya maji katika eneo lao ni ya muda mrefu, huku mabomba ya maji yakibaki kama maonyesho. Alisema hali hiyo inawaletea usumbufu mkubwa wananchi, hususani kina mama kwani hulazimika kufuata maji maeneo ya mbali zaidi, huku yakiwa si mazuri kwa kutumia. “Iwapo unataka maji mazuri, ni lazima ununue kwa gharama ya Sh 500 kwa dumu moja jambo ambalo ni changamoto kubwa kwa maisha ya kijijini kuweza kumudu,” alisema. Kwa upande wake, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Isimani, Gogfrey Kinyoya, alisema ukosefu wa maji katika eneo hilo ni changamoto pia kwa wanafunzi wa bweni shuleni kwao. Alisema imefika wakati sasa Serikali kuingilia kati jambo hilo kutokana na umuhimu wa huduma hiyo kwa wananchi, ukizingatia tarafa ya Isimani imezungukwa na vianzio vingi vya maji akitolea mfano Mto Ruaha. Mkazi mwingine wa eneo hilo, Maimuna Lumato, alisema kuwa wanawake ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa kadhia hiyo ya ukosefu wa maji safi na salama kwa miaka mingi sasa, huku akiwatupia lawama viongozi wao kwa kushindwa kuwaondolea kero hiyo. Alisema tangu wamchague Wiliam Lukuvi  ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa mbunge wao, hajawahi kufika kutaka kujua changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo. “Viongozi wetu wamekuwa na ahadi nyingi wakati wa mchakato wa kuomba kura, lakini mara baada ya kuchaguliwa wanasahau wajibu wao kwa wananchi waliowachagua. “Hebu angalia eneo letu hili la Isimani limezungukwa na vyanzo vikubwa vya maji, kwa mfano Mto Ruaha ambao upo karibu na hapa, lakini tumekosa kufaidika na rasilimali hiyo,” alisema Maimuna. Mwenyekiti wa kijiji katika Tarafa ya Isimani, Daudi Kombora, alikiri kwamba kero ya maji katika eneo hilo ni ya miaka mingi na hadi sasa bado hakuna ufumbuzi wowote.
kitaifa
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamepongeza ziara ya Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein katika nchi za Falme za Kiarabu(UAE) nakusema kuwa imeleta neema kubwa kwa vijana na sekta ya afya.Mwakilishi wa jimbo la Chakechake, Suleiman Sarhani alisema ziara ya Dk.Shein imeleta neema kubwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba kupata matumaini ya kujengwa kwa hospitali ya kisasa jimboni Wete.Alisema tatizo la ukosefu wa hospitali ya rufaa ya kisasa kwa wananchi wa jimbo la Wete limepata ufumbuzi wa kudumu kufuatia makubaliano ya kuanza kwa ujenzi huo.‘’Tumefarajika. Ziara ya Rais wa Zanzibar katika nchi za kiarabu imezaa makubaliano ya ujenzi wa hospitali ya kisasa jimboni Wete Pemba, itakayokuwa na hadhi ya rufaa,’’alisema.Mwakilishi wa jimbo la Wete, Harusi Suleiman Said, alisema ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Wete pamoja na upanuzi wake utasaidia kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa jimbo hilo. Alisema kwa muda mrefu wananchi wa Wete wanapata matatizo ya kusafiri masafa marefu kwenda mkoani kwa ajili ya kupata huduma za afya katika hospitali ya Abdalla Mzee.Mwakilishi wa jimbo la Ole, Mussa Ali Mussa, alisema ni faraja kwa wananchi wa Wete na maeneo mengine ya jirani kuwa na uhakika wa kuwa na hospitali ya rufaa. Waziri asiye na Wizara maalumu, Juma Ali Khatib alimpongeza Rais Ali Mohamed Shein na kusema ziara zake za nje zimekuwa zikilenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake.‘’Tumefarajika na ziara ya Rais Shein katika nchi za Falme za Kiarabu ambapo tumepata fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujiajiri katika ujasiriamali pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wete Pemba,’’alisema.Katika ziara ya wiki moja ya Rais Shein katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UEA) kupitia mfuko wa Khalifa zimetolewa Sh bilioni 23 kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana kujiajiri.
kitaifa
Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM VYUO vingi vinavyotoa mafunzo kwa walimu wa shule za awali nchini havitoi mafunzo ya namna ya kufundisha masomo kwa watoto wadogo na kusababisha walimu hao kufundisha kwa kutumia uzoefu. Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za awali iliyofanyika Dar es Salaam juzi, Mratibu wa semina hiyo, Kelvin Shola, alisema vyuo vingi nchini vinafundisha namna ya kuwalea watoto kuliko wanavyopaswa kufundisha masomo. Alisema  hali hiyo imechangia kuwapo na tatizo la walimu wengi kushindwa kutumia mtaala wa elimu ya awali na kushindwa kufahamu nini anachopaswa kufundishwa motto, jambo linalosababishwa watoto kufundishwa mambo makubwa yasiyoendana na umri wao.  “Moja ya matatizo tuliyonayo ni kutokuwa na walimu wanaomudu masomo husika kama hesabu, badala yake walimu wanatumia uzoefu wao kufundisha,” alisema Shola. Mmoja wa walimu waliohudhuria semina hiyo, Agness Mringo, alisema imemsaidia kufahamu eneo lipi anapaswa kuongeza bidii, hivyo anaamini atabadili mfumo wake wa ufundishaji aliokuwa akitumia awali.
kitaifa
MBUNGE wa Nanyamba, Abdalah Chikota (CCM), ameiomba serikali iipe kipaumbele sekta ya kilimo na kuzitengea fedha halmashauri, ili zijenge maghala na kuepusha uhifadhi wa mazao kwenye maghala ya watu binafsi ambayo ni gharama. Alisema kufanya hivyo kutaokoa zaidi ya Sh bilioni moja kwa mwaka zinazotumika kulipia uhifadhi mazao kwenye maghala hayo binafsi.Alitoa ombi hilo wakati akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa Serikali 2020/2021 bungeni na kusema kwa sasa kilo moja ya mazao inahifadhiwa kwa Sh 38 na kwamba tani 30,000 zinagharimu Sh bilioni moja kila mwaka. Chikota alisema ili kuokoa fedha hizo ni lazima serikali itenge bajeti itakayowezesha kujengwa maghala hususan kwa ajili ya kuhifadhi pamba na korosho.“Tutenge fedha na kuzipa mamlaka za Serikali za Mitaa ili zijenge maghala. Hii itasaidia kuachana na gharama tunayoitumia kuhifadhi mazao katika maghala ya watu binafsi, badala yake tutaongeza mapato ya Serikali,” alisema Chikota.Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM), aliishauri serikali ipanue bandari ya Mtwara sambamba na ujenzi wa reli na ili kufungua uchumi wa Kusini. Pia, aliishauri serikali kuwekeza kwenye lishe na kutilia mkazo siku 1000 za lishe kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora, hivyo kuweza kushiriki kuchangia maendeleo ya nchi.Mbunge wa Igalula, Mussa Ntimizi (CCM) aliitaka serikali kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ili kuweza kuzalisha chakula cha kutosha, jambo litakalochangia usalama wa chakula na kupunguza umasikini.Mbunge wa Manonga, Hashimu Gulamali (CCM) aliishauri serikali kuongeza fedha kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kwa kutenga asilimia 60 badala ya asilimia 30 ya sasa ili kukidhi mahitaji ya barabara za vijijini. Kwa sasa Tarura inapewa asilimia 30 na Tanroads asilimia 70, hivyo kuwafanya wabunge hao kusema kiasi hicho cha fedha ni kidogo ikilinganishwa na majukumu ya iliyonayo Tarura.Alisema katika baadhi ya maeneo Tarura hafungui barabara, kujenga madaraja kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha. “Hali hii imewafanya wakulima kupata wakati mgumu kusafirisha mazao yao wakati wa kuuza, lakini pia inalikosesha taifa mapato.”
kitaifa
Na Renatha Kipaka  ZAIDI ya lita milioni 97.8 za maziwa zilikusanywa  kwa matumizi mbalimbali kutoka kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa   kwenye wilaya nane za Mkoa wa Kagera  kwa kipindi cha mwaka 2016/017 ikilinganisha na  lita milioni 46.6   mwaka 2015/016  Makusanyo hayo yanatokana na taratibu zilizopo katika mkoa huo   kujua zao hilo linanufaishaje jamii. Ofisa Mifugo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Colman John   alisema lengo ni kila kaya kutumia  maziwa   na wafugaji kujipatia kipato.  Alikuwa akizungumza na wandishi wa habari   ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya maziwa kuanzia Juni  mosi mwaka huu.  John alisema  tofauti hiyo ya ukusanyaj inatokana na   mabadiliko ya tabianchi   ambako ukame ulitawala na kusababisha kutokuwapo   maji na nyasi za kutosha.  “Mabadiliko yanayotokea na kuonekana hapa   ni ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu  na kusababisha ng’ombe kukosa lishe na maji,”alisema.   Alisema  mkoa huo una  ng’ombe wa maziwa wapatao 21,438 na ng’ombe wa asili 52,8632.  ”Niseme tu kwamba taarifa hizo tunazipata kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya maana wao ndiyo wanaojua ni nani anafuga na nani anayekamua maziwa kiasi gani,” alisema.  Meneja wa Kiwanda cha Maziwa Kagera katika o Manispaa ya Bukoba,  Samwel John alisema kwa sasa upatikakanaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho ni wa kiwango cha chini ikizingatiwa hukusanya lita 200-300 za maziwa kwa siku   ndani ya manispaa hiyo.  Alisema awali kiwanda hicho kilikuwa kinapata maziwa kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya lakini kwa sasa hayapatikani kwa wingi.  “Kama sisi hapa tunazalisha maziwa aina tatu, maziwa fresh, yogati na mtindi kwa uwiano wa lita 150 ni fresh, lita 100 ni yogati na lita 50 matumizi ya watu majumbani,” alisema John. Naye Methodi Karikira, mtumiaji wa maziwa klra siku na mkazi wa Manispaa ya Bukoba, alisema   ulipotokea ukame maziwa yalikuwa ya shida kupatikana hata katika familia. Alisema   sababu nyingine ya upungufu wa maziwa ni ardhi kutokuwa na madini ya chumvi na kufanya wafugaji kuwapa ng’ombe wao chumvi ya kawaida kwa wingi.
kitaifa
WATAALAMU wa lugha ya Kiswahili zaidi ya 950, wamenolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita), tayari kwenda kufundisha lugha hiyo nje ya nchi, hususan nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Hivi karibuni katika kikao cha SADC, kilichofanyika nchini na kushirikisha wakuu wa nchi 16, huku Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti wake, kwa pamoja wakuu hao wa nchi waliridhia Kiswahili kuwa lugha ya nne ya kuendeshea mkutano huo kikiungana na lugha nyingine za Kiingereza, Kifaransa na Kireno.Lakini, kabla hata ya kukubaliwa huko katika ziara yake nchini Namibia na Afrika Kusini mwaka huu, Rais Magufuli alifanikiwa kuzishawishi nchi hizo kufundisha Kiswahili kwenye nchi hizo, huku Afrika Kusini ikiwa tayari imeshaonesha nia ya dhati ya kuanza kufundisha lugha hiyo shuleni.Akizungumza na gazeti jana, Mchunguzi wa Lugha Mwandamizi Idara ya Istilahi na Kamusi wa Bakita, Wema Msigwa alibainisha kuwa baraza hilo linaendelea na jitihada za kuwaandaa wataalamu wa lugha, huku akibainisha kuwa linachukua wahitimu wa Shahada ya Kiswahili na masomo yanaoendana na lugha hiyo.
kitaifa
Na ELIYA MBONEA-ARUSHA JOPO la majaji watano wa Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki (EACJ), limekubaliana na hoja za Serikali katika rufaa ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu. Kupitia kwa Wakili Mwandamizi Mark Mulwambo na Pauline Mdendemi, Serikali ilikata rufaa ikidai mahakama iliyompa ushindi Komu haikuwa na uwezo wa kisheria wa kutoa uamuzi kuhusu Bunge la Tanzania ambalo ni mwanachama wa EAC. Katika kesi hiyo namba 7 ya mwaka 2012 iliyosikilizwa na kutolewa uamuzi na majaji watatu wa Mahakama ya EACJ, Komu aliiomba mahakama hiyo itoe tafsiri ya kisheria juu ya Bunge kukiuka Ibara ya 50 ya mkataba wa EAC katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Aprili 17, mwaka 2012. Rufaa hiyo ilisikilizwa na kutolea hukumu juzi na jopo la majaji watano wakiongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Dk. Emmanuel Ugirashebuja, Makamu wake Libore Nkurunzinza, Edward Rutakangwa, Aaron Ringera na Geoffrey Kyiryabwirwe. Akisoma hukumu hiyo mjini hapa jana, pamoja na mambo mengine, Jaji Dk. Ugirashebuja alikubaliana na hoja za Serikali kuwa mjibu rufaa hakuwa na sifa za kuwasilisha maombi ya kuomba tafsiri katika mahakama ya chini. Alisema badala yake maombi hayo yalipaswa kuwasilishwa na taasisi ya Serikali kama Bunge au Mahakama Kuu kama ambavyo marekebisho yalivyofanywa baada ya kesi ya Professa Anyang’ Nyong’ wa nchini Kenya. “Haikuwa sahihi kwa mahakama ya chini kupokea na kusikiliza shauri hili. Hivyo tunakubaliana na hoja za Serikali kwa kutengua uamuzi uliotolewa awali. “Kwa vile shauri hili ni muhimu si kwa Tanzania tu bali kwa nchi zote wanachama, mahakama hii inaziagiza pande zote mbili kubeba gharama zake za kesi,” alisema Jaji Dk. Ugirashebuja. Akizungumza mara baada ya kusomwa kwa rufaa hiyo, Komu aliyekuwa mahakamani hapo, alisema kutokana na matokeo hayo amejipanga kumwandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai ili aweze kuanza mchakato wa kubadili baadhi ya kanuni. “Mimi ni mbunge, sina haja ya kufanya ligi dhidi ya Serikali au Bunge. Lakini ukiangalia mchakato wa hoja ambazo majaji wameziwasilisha, utaona faida kubwa ya shauri hili kusikilizwa hadi lilipofikia hapa. Alisema kutokana na uamuzi huo, Serikali haipaswi kuendelea kusubiria hadi ikamatwe, badala yake inapaswa kufanya marekebisho ya kanuni ili haki iwe inatendeka. Kwa upande wake, Wakili Edson Mbogoro aliyemwakilisha Komu, alisema hukumu ya rufaa hiyo haikuelekea kwenye stahiki za rufaa, badala yake ilishughulikia suala la kama mahakama ya chini ilikuwa sahihi kupokea na kushughulikia malalamiko ya mteja wake. Alisema kutokana na kupitia hoja hizo, mahakama hiyo ilifikia hitimisho la kumuona Komu kama mtu binafsi ambaye anaelekezwa na Ibara ya 30 na 33 na 51 kuwa alipaswa kuendelea na kesi aliyoifungua Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma. “Isipokuwa kama huko Mahakama Kuu wangefikia hatua ya kuomba tafsiri ya mkataba wa EAC, basi Mahakama Kuu ndiyo ingefanya marejeo kwenye Mahakama ya EACJ. Na suala hilo bado lingeamuliwa na Mahakama Kuu,” alisema Wakili Mbogoro.
kitaifa
Christina Gauluhanga na Sabina Wandiba – Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameiomba serikali kuhakikisha inafunga mipaka haraka kuzuia wageni wanaoingia nchini ambao nchi zao zimekumbwa na maambukizi ya virusi vya corona. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 19, Profesa Lipumba amesema kuendelea kuacha mipaka hiyo bila udhibiti wa wageni hao ni kuendelea kuhatarisha usalama wa afya za wananchi. Amesema ni vema kukaongezwa uwezo wa vipimo na wataalamu wa kutosha ili kuwabaini wasafiri wanaoingia nchini wanaotoka sehemu mbalimbali za nchi. “Wakati sasa umefika wa serikali kuamua kufanya uamuzi wa kufunga mipaka yetu, kuweka wataalam na vifaa vya kutosha kwani ugonjwa huu ni hatari na ukiendelea kuingia hapa nchini hali itakuwa mbaya zaidi kwakuwa hata mataifa tajiri wanahangaika nao,”amesema Profesa Lipumba. Profesa Lipumba ameongeza kuwa wataalamu wasiishie kupima tu kiasi cha joto bali ni vizuri wakajiridhisha zaidi kwa kuchunguza ffya ya wasafiri hao.
afya
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud awachukulie hatua watumishi wote watakaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za mapato ya serikali.Alitaka pia watumishi wa umma katika ngazi mbalimbali wajiimarishe katika ukusanyaji wa mapato na wahakikishe fedha zote zinazopatikana zinaingizwa kwenye mfuko wa serikali. Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na watumishi, viongozi wa mkoa wa Kusini Unguja katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, eneo la Tunguu.Waziri Mkuu ambaye yuko Unguja kwa ziara ya kikazi, alisema ni muhimu watumishi kushirikiana kukusanya mapato ili serikali iweze kupata fedha za kugharamia miradi ya maendeleo.“Mkuu wa Mkoa usiogope, chukua hatua kwa mtumishi yeyote atakayebainika kula fedha za mapato ambazo zinatolewa na wananchi kwa njia ya kodi. Mtumishi wa aina hiyo hafai kuwa mtumishi wa umma,” alisema.Waziri Mkuu alitaka kila mtumishi wa umma awajibike kwa kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhirifu na wavivu .Wakati huo huo, Waziri Mkuu aliwaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe wanasimamia vizuri uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao.Alisema huduma za jamii kama za afya, maji lazima ziimarishwe nchini na viongozi wa halmashauri wahakikishe zinapatikana ipasavyo. “Huduma zikiwa zinatolewa vizuri wananchi hawatolalamika.”Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub alisema halmashauri za wilaya zimeendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kutoa huduma kwa jamii kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Kusini ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Sh milioni 241 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Sh milioni 524.51 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 118.Alisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Sh milioni 304.27 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi kufikia Sh milioni 632.89 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 108 ya ukusanyaji wa mapato.
kitaifa
HATIMA ya kuendelea kusota rumande ama kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko itajulikana leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.Mpaka sasa Mbowe na Matiko wamesota rumande kwa takribani miezi minne tangu walipofutiwa dhamana yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, mwaka jana.Hivyo, mahakama hiyo kama itatupilia mbali rufaa hiyo, Mbowe na Matiko wataendelea kusota rumande hadi kesi ya msingi ya uchochezi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.Lakini endapo mahakama hiyo itakubali hoja za rufaa hiyo, washitakiwa hao wataachiwa huku wakiendelea kufuata masharti ya dhamana. Jana, Jaji Sam Rumanyika alisikiliza hoja za pande zote, ambapo wakata rufaa (Mbowe na Matiko) waliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya. Upande wa Jamhuri uliongozwa na jopo la mawakili watano wa Serikali, Faraja Nchimbi, Paul Kadushi ambao ni Mawakili wa Serikali Wakuu, Salum Msemo, Wankyo Simon (Mawakili wa Serikali) na Wakili Serikali Mwandamizi, Jakline Nyantori.Jaji Rumanyika alisema amesikiliza hoja zao na atatoa uamuzi huo leo saa saba mchana. Akiwasilisha hoja za rufaa, Kibatala alidai kuwa walikuwa na sababu nne za kukata rufaa, lakini baada ya mahakama hiyo kuziondoa mbili zimebaki mbili, kwa hiyo watajikita katika hoja hizo. Kibatala alidai kuwa Mahakama ya Kisutu ilifanya makosa kuwafutia dhamana Mbowe na Matiko wakati siku hiyo ambayo ilikuwa ni Novemba 23, 2018 washtakiwa wote walikuwepo mahakamani.Alidai washtakiwa hao walifika mahakamani hapo bila hata ya wao kukamatwa, licha ya kwamba kulikuwa na hati ya kukamatwa, waliingia mahakamani na kujieleza kuwa siku ambazo hawakuwepo walikuwa nje ya nchi.Wakili huyo alidai kama wateja wake hawafiki mahakamani, basi siku hiyo wadhamini wao wanafika mahakamani hapo na kutoa sababu cha kushangaza licha ya wadhamini hao kufika na kujieleza bado dhamana ilifuatwa. “Mahakama ilikosea kuwafutia dhamana washtakiwa hakukuwa na mantiki yoyote ya kufanya hivyo.Tunaomba Mahakama iridhie ione hoja zao zina mashiko kisheria,” alidai Kibatala. Pia, Kibatala aliendelea kueleza kuwa wakati hakimu anatoa uamuzi huo wa kuwafutia dhamana hakukuwa na ‘material’ yoyote, ambayo yaliiegemiza Mahakama kutoa uamuzi huo.Katika suala la kiapo kilichowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango katika Mahakama ya Kisutu, Kibatala anaeleza kuwa haikuwa sahihi kwa wakili huyo kuapa kiapo hicho kwa niaba ya Jamhuri, wakati na yeye ni mmoja wanaoendesha kesi hiyo, ambapo sheria hairuhusu kufanya hivyo.Mtobesya alidai ni maoni yao kwa Mahakama Kuu, ikatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ili wateja wao warudi kufurahia haki yao ya msingi ya kuwa nje kwa dhamana, kwa sababu uamuzi wa kuwafutia dhamana haukuwa sahihi. Wakijibu hoja hizo, Wakili Nyantori alidai kuwa hakuna hoja za msingi katika misingi ya kisheria, ambazo zimewasilishwa na wakata rufaa (Mbowe na Matiko), zitasababisha rufaa yao kukubaliwa.
kitaifa
Grace Shitundu, Dar es salaam MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Chadema ( Bavicha) Patrick ole Sosopi amekana kuwafahamu vijana waliodai kumchukuliwa fomu Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ya kugombea kwa mara nyingine nafasi  hiyo. Pia amedai kwamba ingawa vijana hao wanahaki ya kufanya hivyo, huo sio msimamo wa baraza kwani linaheshimu taratibu. Kauli hiyo ya Sosopi imekuja siku moja baada ya gazeti moja la kila siku (sio Mtanzania) kuripoti kuwa vijana wa Chadema wamejitolea kumchukulia fomu Mbowe ambaye hata yeye hajatangaza rasmi kama atagombea tena nafasi hiyo. Kwa mujibu wa Mratibu wa mchakato huo, Daniel Naftali aliliambia gazeti hilo kuwa wao kama vijana wamezunguka nchi nzima kuchangishana fedha kwa ajili ya kumchukulia Mbowe fomu na kumshawishi kugombea nafasi ya uwenyekiti wa chama na tayari vijana 10,000 wameshatia saini kuunga mkono zoezi hilo. Vijana hao wanatarajiwa kumchukulia Mbowe fomu na kumpelekea nyumbani kwake Novemba 24 mwaka huu. Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi Sosopi alisema mchakato huo unaofanywa na vijana hao sio msimamo wa Bavicha. “Si msimamo wa Baraza la Vijana, na hata hao vijana wenyewe siwafahamu, lakini kama ni wanachama wanahaki ya kufanya hivyo, hakuna sheria inayowakataza pale wanapoona mtu fulani anafaa lakini kama baraza hatuwezi kufanya hivyo”alisema Sosopi. Alisema Bavicha wanaheshimu taratibu zilizowekwa katika uchaguzi wa viongozi wa chama na mtu yoyote anaruhusiwa kugombea ili mradi atimize vigezo vinavyohitajika. Alisema kwa upande wa Baraza la vijana na lile la Wazee watakaowania pamoja na kuwa na kigezo cha kuwa mwanachama ni lazima umri uzingatiwe na kwa upande wa Baraza la Wanawake ni lazima uwe mwanamke. “Lakini katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu mwenyetiki Bara na Visiwani mwanachama yoyote anahaki ya kugombea nafasi hizo aingalii umri au jinsia mradi uwe na umri wa kupiga kura,” alisema Sosopi. Mbowe aliwahi kuweka wazi msimamo wake kuwa hana tatizo na mwanchama yoyote atakayeitaka nafasi hiyo ili mradi afuate utaratibu wa chama na kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hiyo. Tayari Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe alionesha nia ya kuwania nafashi hiyo. Katibu Mkuu wa chadema Dk. Vicent Mashinji alitangaza ratiba ya kuchukua fomu kuwa ni kuanzia Novemba 18 hadi 30 huku Mkutano Mkuu ukitarajiwa kufanyika Desemba 18 mwaka huu.
kitaifa
NA OSCAR ASSENGA- LUSHOTO WATU wawili wa familia moja, mke na mume wakazi wa Kijiji cha Baga. Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, wamefariki dunia baada ya kunywa chai ya rangi inayodhaniwa kuwa na sumu. Mbali ya hilo, mpwa wao amenusurika katika tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alithibitisha kutokea tukio hilo. Alisema lilitokea Juni 19, mwaka huu saa saba mchana wakati familia hiyo ilipoandaa kinywaji hicho. Aliwataja waliofariki wakati wakipatiwa matibabu katika Zahanati ya Baga kuwa ni Rajabu Ally (73) na Amina Rajabu (62). Kamanda Wakulyamba alisema katika tukio hilo, mpwa wao Adam Saidi (12), mwanafunzi wa darasa la tatu  Shule ya Msingi Mashine, alinusurika kifo. Alisema miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa awali na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi, huku Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi wa tukio hilo. “Katika tukio hilo ambalo limepoteza watu wa familia moja, mpwa wao alinusurika baada ya kunywa chai idhaniwayo kuwa ni yenye sumu, tunaendelea na upelelezi wa tukio hili,” alisema Kamanda Wakulyamba.
kitaifa
BAADA ya juzi jioni Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, gumzo mtaani limehamia kwenye leseni za udereva huku wengi wakipongeza serikali kwa hatua hiyo kwa kile walichodai kuwa kitapunguza usumbufu na rushwa kwa wanaohitaji.Baadhi ya wananchi, polisi kutoka maeneo mbalimbali nchini walisema kuwa uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano umelenga kupunguza gharama zisizokuwa na msingi lakini pia inasaidia kupunguza rushwa pamoja na kupunguza usumbufu utakao okoa muda wa ujenzi wa taifa.Katika uwasilishaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango katika mapendekezo ya Serikali alisema kuwa itaongeza muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi mitano huku tozo zake zikipanda kutoka Sh 40,000 ya sasa hadi Sh70,000.Mapendekezo hayo yamepokelewa kama ifuatavyo; Adam Lutta ambaye ni Balozi wa Usalama Barabani nchi alisema kuwa hatua ya kuongeza muda wa leseni ni jambo jema kwani litapunguza mchakato na usumbufu uliokuwa unatokea kwenye upatikanaji wa leseni.“Wakati mwingine watu walikesha na kupoteza muda mwingi wakishinda kwenye ofisi za leseni ili maombi yao ya leseni yashughulikiwe, lakini hata kama ilikuwa ni kwa mara moja kwa miaka mitatu, kusogezwa mpaka miaka mitano kutasaidia madereva kwa kuwapunguzia usumbufu,” alisema Lutta Kwa upande wake, ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi upande wa Usalama Barabarani alisema utoaji wa leseni mpya utapunguza usumbufu kwa madereva, lakini itatoa muda wa kutosha kwa madereva kufuatilia leseni pale ambapo unakuta leseni zao zimeisha muda.“Mara nyingi, unapomkamata dereva ambaye leseni yake imeisha muda wa kutumika huwa analalamika muda (miaka mitatu) kuwa mdogo wa matumizi ya leseni hiyo, lakini sasa miaka mitano sidhani kama watakuwa na visingizio,” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo itapunguzia adha kwa wananchi ambao wamekuwa wakidanganywa na vishoka kuwa watawasaidia kupata leseni. Ndeanka Alex, ambaye ni mkazi wa Mwanza alisema kuwa kwa muda kumekuwa na vishoka karibu na sehemu za kutolea leseni wakitafuta fedha zisizo halali na matokeo yake kusababisha madereva wasiokuwa na sifa wapate leseni.“Naamini miaka mitano ya leseni moja itawakatisha tama vishoka ambao wanategemea kuitapeli serikali kwa kunyonya wananchi wanaotaka leseni. Mfano gharama halali ya kubadili leseni iliyoisha muda ni shilingi 40000 lakini utakapokutana na vishoka huwa wanakuambia kama unataka haraka utoe Sh 60000,” alisema Alex.Mkazi wa mkoani Kilimanjaro, Andrew Mneney alisema kuwa Serikali imewabeba wananchi kwenye suala la leseni na kwamba vishoka watapungua sambamba na usumbufu wa kusimamishwa mara kwa mara na polisi kwa ajili ya ukaguzi. Dereva wa basi la abiria ‘daladala’ linalofanya safari zake kutoka Ubungo kwenda Temeke, Hassan Abdallah alisema kuwa tofauti ya bei ni ndogo isipokuwa upatikanaji wa leseni utakuwa ni rahisi. “Zile habari za kusubiri leseni muda mrefu zitaisha… mara unaambia vile vikadi havipo.Sasa naamini serikali haitatumia fedha nyingi hivyo upatikanaji wa leseni kwa wanaobadili utakuwa rahisi,” alisema dereva huyo. Kwa upande wake dereva wa pikipiki ‘ bodaboda’ aliyejulikana kwa jina moja la Side alisema kuwa serikali inaweka mikakati mizuri hivyo kilichofanywa kwa leseni ni kupunguza usumbufu na ile hali ya kwenda kumshawishi mtu ili akupe leseni. “Miaka mitano mingi, hapo unaaweza kufuatilia leseni vizuri. Hakuna presha ya kuipata hivyo siwezi kulazimika kumpa mtu fedha,” alisema.
kitaifa
NAIROBI, KENYA Jeshi la Polisi nchini Kenya limetangaza kutoa dola za kimarekani milioni 10 ambazo ni sawa na milioni 23  na nusu fedha za kitanzania kama zawadi kwa atakayefanikisha kupatikana kwa Silvia Romano ambaye ni mfanyakazi wa kujitolea wa kutoa misaada mwenye asilia ya Italia. Silvia (23) alitekwa na watu wenye silaha akiwa katika moja ya hoteli katika kata ya Kilifi kusini-mashariki mwa nchi hiyo, huku watu watano wakiwamo watoto watatu, walijeruhiwa katika shambulio hilo la kumteka na kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Jeshi la Polisi limesema kuwa linafanya kila linalowezekana kuhakikisha Silvia anapatikana na watekaji wake wanatiwa nguvuni. Bado haijafahamika wazi sababu za kutekwa kwa mfanyakazi huyo wa kujitolea, aliyetekwa na wahuni wa mtaani, lakini pia inasemekana kuwa watekaji wanaweza kuwa na uhusiano na wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabab. Hata hivyo, kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Joseph Boinett, mpaka sasa watu ishirini wamekwisha kamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo. Silvia ni mfanyakazi wa kujitolea katika shirika la Kiitalino la Africa Milele Onlus, ambaye ni mfanya kazi wa kwanza kutoka katika shirika la kigeni kutekwa nchini Kenya tangu nchi hiyo kukumbwa na kipindi cha mpito cha matukio ya utekaji nyara yaliyokuwa yamekithiri na kutishia sekta ya utalii kuporomoka mnamo mwaka 2011.
kimataifa
‘TUNZA misitu ikutunze’ ndiyo sentensi sahihi ya kuelezea faida za misitu katika maisha na umuhimu wa kuwapo hifadhi za mazingira ya asili zinazosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).Hifadhi za mazingira ya asili yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini, ni miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyotegemewa katika kuingiza mapato ya serikali. Ndiyo maana serikali imekuwa ikihimiza kutunza misitu kwa kupanda miti na kutoikata hovyo kwa kuomba wadau mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo. Nelly Kazikazi ni balozi wa TFS katika suala zima la utunzaji wa mazingira na ni miongoni mwa wadau wanaoitikia hamasa ya serikali ya kutunza misitu.Nelly ambaye ni mrembo wa Tanzania katika nafasi ya pili, anahimiza vijana wenzake kushiriki utunzaji wa misitu akisisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu wa kila mmoja kupanda misitu. Anasema vijana wanapaswa kutambua thamani ya misitu nchini na hivyo kushiriki kuilinda na wasijaribu kudharau kwani thamani yake kwa taifa ni kubwa. “Tuwe na uaminifu kwa kupanda miti kadri tunavyoweza…Nafahamu wapo wanaokata miti kwa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu lakini ni vyema kwa umoja wetu wote tukashiriki kupanda miti,” anasema. Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) katika tathmini yake ya misitu duniani ya mwaka 2015, linasema mwaka 1990 dunia ilikuwa na hekta milioni 4,128 za misitu lakini ilipofikia mwaka 2015 ilipungua mpaka hekta milioni 3,999.Tathimini hiyo inasema zipo sababu nyingi zinazohusishwa na suala hilo ikiwamo ongezeko la watu, upanuzi wa ardhi kwa ajili ya kilimo, matumizi ya kuni kama chanzo cha nishati pamoja na matumizi mengine ya ardhi yasiyozingatia faida endelevu. Hapa nchini, ripoti ya Taifa ya Ufuatiliaji na Tathimini ya Rasilimali za Misitu ya mwaka 2015 ilikadiria kwamba kiwango cha ukataji misitu kwa mwaka kilikuwa hekta 372,816. Mwaka 2018 makadirio na Kituo cha Kufuatilia Taarifa za Hewa Ukaa yalionesha kuwa kiwango cha ukataji miti kimeongezeka kufikia hekta 469,420 eneo ambalo inaelezwa kwamba takribani ni mara tatu ya ukubwa wa jiji la Dar es Salaam.Kutokana na tathmini hizo, wadau mbalimbali wanashauri elimu kuhusu utunzaji wa misitu na mazingira kwa ujumla itolewe kuanzia kwa watoto hadi watu wazima.“Elimu ya misitu inaweza kuhamasisha watoto wadogo kujifunza kuhusu umuhimu wa misitu na hata kuja kusomea masuala ya misitu,” anasema mdau wa mazingira, Fred Kafeero.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu anahimiza watendaji wa TFS kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi na jamii katika kusimamia misitu. Akifungua kikao maalumu cha utendaji kilichokutanisha viongozi wa TFS kuanzia makao makuu hadi ngazi ya wilaya kilichofanyika mkoani Dodoma Oktoba mwaka huu, Kanyasu ushirikiano ni tija katika ulinzi wa misitu. Kanyasu anasema ni vizuri jitihada za uhifadhi zikatangulia na kuungwa mkono na wananchi wote ili viwanda vipate kushamiri.“Na hii inamaanisha lazima kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake. Hapa kwenye misitu wote wenye dhamana wasimamie rasilimali misitu kwa weledi na umahiri wa hali ya juu,” anasema.Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo inaunga mkono dhana ya ushirikiano na kuhimiza kila mtu kushiriki utunzaji wa misitu na wakati huo huo kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi ya misitu wabaini faida zake. Profesa Silayo anasema kila mtu ana wajibu wa kutunza misitu kwa kupanda miti na kutoikata hovyo.Serikali inavyolinda misitu Silayo anasema serikali nayo inafanya mengi katika kulinda misitu miongoni mwake ikiwa ni kubadilisha hadhi maeneo ya hifadhi kuimarisha uhifadhi, ulinzi sanjari na kuendeleza utalii.Katika kutekeleza azma hiyo, TFS imepandisha hadhi misitu ya hifadhi ya Mwambesi (Tunduru); Pindiro (Kilwa), Itulu Hills (Sikonge), Magombera (Kilombero) na Kalambo Falls (Kalambo) kuwa misitu ya hifadhi ya mazingira asilia. Uamuzi huo unakwenda sanjari na uboreshaji wa miundombinu ya utalii ikolojia hususani kwa kujenga ofisi na vituo vya ulinzi katika hifadhi za mazingira asilia za Chome, Magamba, Mlima Rungwe, Mkingu, Minziro, na Uzungwa Scarp.Zimejengwa pia barabara zenye urefu wa kilometa 89.6 na njia za kutembea watalii zenye urefu wa kilometa 102.6 hadi kwenye misitu hiyo. Imejengwa ngazi yenye meta 183 kuelekea kwenye maporomoko ya Kalambo.Pia kambi 11 za kupumzikia wageni zimesafishwa katika misitu saba ya hifadhi za asilia za Mlima Hanang, Mlima Rungwe, Udzungwa, Uluguru, Kimboza, Rondo na Kilombero. Mashamba ya miti Anabainisha kuwa jumla ya hekta 9,292 zimepandwa miti katika mashamba mapya ya miti ya Wino (Songea), Iyondo Msimwa (Ileje), Biharamulo (Chato), Mpepo (Mbinga), Buhigwe (Kigoma) na Mtibwa/Pagale (Mvomero).Shamba jipya kwa ajili ya uzalishaji wa gundi inayotokana na miti ya migunga lenye ukubwa wa hekta 50,000 limeanzishwa katika Wilaya ya Iramba (Singida).“Ili kukuza viwanda vya ndani na kuhakikisha upatikanaji wa ajira, serikali imezuia usafirishaji nje ya nchi wa nguzo za miti ya aina yoyote ile isipokuwa zile zitokanazo na miti ya mkaratusi na miwato na ziwe zimeongezwa ubora,” anasema.Profesa Silayo anasema sambamba na nguzo, serikali pia imezuia usafirishaji wa magogo ya aina yoyote nje ya nchi. Utaratibu huu unakwenda sambamba na azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda.“Magogo yote lazima yapasuliwe kwenye viwanda vilivyopo nchini. Yeyote anayehitaji kutumia magogo ya Tanzania lazima awekeze viwanda nchini kwenye maeneo yenye malighafi hiyo.”Utatuzi wa Migogoro Serikali imeridhia hifadhi za misitu saba yenye ukubwa wa ekari 46,715 iliyoharibika na kupoteza sifa, itolewe kwa wanachi kwa ajili ya shughuli za makazi, kilimo na mifugo kuwaondolea kero za uhaba wa ardhi.Hatua hiyo ilikuja baada ya agizo la Rais John Magufuli alilotoa Januari 15 mwaka huu kwa mawaziri wa kisekta akitaka wawasilishe mapendekezo ya ufumbuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo wanayosimamia.Hivyo hifadhi za misitu 14 zimemegwa kwa ajili ya kilimo na mifugo wakati wakala ukiendelea kutatua migogoro kwa kushirikiana na wizara nyingine na wananchi wa maeneo yenye migogoro. Wakala umeendelea kuimarisha mipaka ya misitu ya hifadhi kupunguza migogoro kati ya wananchi na hifadhi za misitu.Katika mwaka 2018/2019, mipaka ya misitu 212 yenye urefu wa kilometa 1,989 ilisafishwa, maboya 2,507 na mabango 473 yaliwekwa. Kuhusu utatuzi wa migogoro ya mipaka baina ya vijiji na hifadhi, serikali imeandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 60 kwenye kanda za Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Kaskazini, Kati na Magharibi.
kitaifa
Na Upendo Mosha, Rombo MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wamemtuhumu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Magerth John, kwa kushindwa kufuata kanuni na  maadili ya utumishi wa umma na kusababisha kushindwa kutekeleza maazimio ya baraza la madiwani, jambo linalokwamisha shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo. Mbali na tuhuma hizo, pia mkurugenzi huyo anatuhumiwa kuwa na uhusiano mbaya na watendaji, huku akiwahamisha vituo vya kazi kwa kile kinachodaiwa kuwa na chuki binafsi. Akiwasilisha hoja binafsi ya utovu wa nidhamu wa mkurugenzi huyo katika kikao cha Baraza la Madiwani juzi, Diwani wa Kata ya Makiidi, Simon Kinabo, alisema tangu mkurugenzi huyo ateuliwe kuongoza halmashauri hiyo, amekuwa na utendaji mbovu unaolalamikiwa na watendaji, wananchi na madiwani.   Alisema utovu wa nidhamu umekuwa  kikwazo kwa watendaji, wananchi na madiwani, jambo linalochangia kuwapo na mpasuko mkubwa. “Muda sasa umepita tangu mkurugenzi aripoti hapa, amekuwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu na hili lilidhihirika alipopata ugeni wa mwananchi mmoja akihitaji huduma kwake, badala ya kumsikiliza na kumsaidia aliketi juu ya meza kwa dharau, huku akiongea na simu, ni jambo la ajabu sana,” alisema Kinabo.   Alisema amekuwa akiendesha halmashauri hiyo kwa mabavu na kushindwa kutoa ushirikiano kwa watendaji, huku wale walioonekana kutoa ushauri na kumpinga, waliandikiwa barua za uhamisho mara moja. “Kuna watendaji wetu wa halmashauri ambao wameonekana wakitoa ushauri na kumpinga kwa vituko anavyovifanya, wameandikiwa barua za uhamisho na ninaweza kuwataja watendaji hao kwa majina mbele ya baraza hili,” alisema. Kinabo alisema amekuwa akipuuza maagizo  mengi yanayotolewa na baraza la madiwani, jambo ambalo halikubaliki. Alisema mpaka sasa kuna maagizo mengi yamepuuzwa na kutokufanyiwa kazi kutokana na kuingiza masuala ya utendaji na siasa, ikiwa  ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma. Naye Diwani wa Kata ya Kyelamfua, Mokala Lubega, alisema mbali na tuhuma mbalimbali anazokabiliwa nazo, pia ameshindwa kusimamia vema vyanzo vya mapato kwa kutowalipa vibarua. Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Evaristy Silayo, alisema hoja binafsi iliyoletwa na diwani huyo ni ya msingi  na inapaswa kufanyiwa kazi na kujadiliwa ili kuinusuru halmashauri hiyo. “Kutokana na uzito wa hoja hiyo, ni lazima tutumie kanuni zetu zinazotuongoza, hatutaijadili hapa badala yake tutatafuta siku maalumu ya kumjadili, baraza litajigeuza kamati na kupata nafsi  ya kuijadili ili tufikie mwafaka kwa lengo la kuinusuru halmashauri yetu,” alisema Silayo. Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, mkurugenzi huyo aliwataka madiwani kuacha kuitisha kikao maalumu cha kumjadili, badala yake watumie kikao hicho hicho kumjadili kwa kigezo cha kubana matumizi.
kitaifa
Ni ukweli usiopingika kwamba kilimo nchini ndiyo uti wa mgongo wa uchumi na maendeleo yake.  Hiyo ni kwa kuzingatia kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa taifa hili wanategemea kilimo kwa ajili ya maisha yao ya kila siku. Vilevile, mazao ya kilimo ndiyo, kwa miaka nenda miaka rudi, yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa katika kuliingizia taifa fedha zikiwamo za kigeni. Pia kwa miaka mingi imekuwapo mipango na miradi mbalimbali yenye lengo la kuimarisha  na kukuza kilimo kwa kuweka mbinu kadha wa kadha zikiwamo za kuwasaidia wakulima moja kwa moja. Lakini pamoja na juhudi hizo, baadhi ya watendaji wamekuwa wakitumia fursa walizo nazo kufifisha maendeleo ya kilimo kwa kujinufaisha wenyewe. Ndiyo sababu tunaunga mkono agizo la Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan la kuiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha  wanaohusika na madeni ya pembejeo za kilimo kufikishwa katika Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru). Kwa mujibu wa Samia, uhakiki wa madeni ya wazabuni wa pembejeo uliofanywa na serikali umebaini kuwapo unyonyaji mkubwa kwa wakulima, hali ambayo inachangia kuwadhoofisha. Inadaiwa kuwa katika  baadhi ya maeneo uhakiki unaonyesha wakulima wametumia kiasi kikubwa cha pembejeo wakati si kweli. Kilichopo ni kwamba baadhi ya watendaji hula njama na wazabuni wa pembejeo na kuandika takwimu za uongo kuonyesha wakulima wa eneo fulani wametumia pembejeo za mamilioni ya fedha, wakati ni pembejeo hewa huku fedha zikiwa zimeingia mifukoni mwao! Udanganyifu huo na mwingine unaofanywa dhidi ya wakulima na taifa kwa ujumla ni hujuma kubwa kwa taifa kwa ujumla. Hayo yamekuwa yakifanyika, wakati mwingine kwa kuwarubuni wakulima au kutokana na wakulima kutokuwa na uelewa mzuri kuhusu mfumo wa kupatiwa pembejeo za kilimo. Yote hayo hufanywa kwa makusudi na watendaji wasiokuwa waaminifu kwa kushirikiana wazabuni wasiokuwa waaminifu. Wakulima wanakatishwa tamaa na wanashindwa kuinuka na kufikia maisha mazuri wakati taifa nalo linapoteza mamilioni ya fedha kwa sababu ya watu wachache wenye uchu wa utajiri wa haraka haraka. Ni hali ambayo inapaswa kurekebishwa haraka kwa manufaa na maendeleo ya taifa na watu wake. Vyombo  vya dola vinavyohusika, Takukuru, polisi na vingine vichukue hatua madhubuti na zisizotetereka kulikabili suala hilo mapema.
kitaifa
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani imesema, eneo hilo ni sehemu sahihi kuwekeza kwa kuwa ni salama, linapitika, na linafikika.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Fatuma Latu amesema Bagamoyo ni tulivu, ina barabara zinazopitika, kijiografia ni kiungo cha kwenda maeneo mbalimbali na ni jirani na jiji la Dar es Salaam.Dar es Salaam ni jiji kuu la biashara Tanzania, lina bandari, bandari kavu, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya usafiri wa ndani na safari za kwenda nje ya nchi.“Tunayo barabara kubwa kutoka Dar es Salaam kwenda mpaka Chalinze kwa maana ya Msata inaunga ya lami. Ni eneo ambalo linapitika, unaweza ukazalisha bidhaa na ikauzika kwenda Dar es Salaam na kwenda mikoani” amesema ofisini kwake mjini Bagamoyo.Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.Latu amesema barabara ya Bagamoyo kwenda Mlandizi imefanyiwa upembuzi yakinifu na itajengwa kwa kiwango cha lami.“Lakini pia kuna barabara inaunga pale Baobab kwenda Kibaha kwenye barabara ya Dar es Salaam- Morogoro na yenyewe tayari inatengenezwa kwa hiyo mnaweza mkaona ambavyo Bagamoyo ipo sehemu ambayo inafikika, inapitika kwahiyo biashara yoyote unaweza ukaifanya muda wowote” amesema.
uchumi
HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesema majeruhi wengi wa ajali wanaofanyiwa upasuaji wa vichwa ni wasiovaa kofi a ngumu (helmeti) pindi wanaposafi ri kwa kutumia pikipiki.Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo alisema jana kuwa, kutovaa helmeti kuna madhara makubwa kwani miongoni mwa waathirika hao ni waendesha pikipiki wenye kasumba ya mwendokasi na wasiotumia helmeti, pamoja na abiria wao. “Wengi ni vijana kati ya miaka 14 hadi 25 waliomaliza darasa la saba au kidato cha nne na hawa nao, wengi ni ambao hawana mafunzo ya uendeshaji pikipiki yaani anafundishwa leo na rafiki yake mtaani, kesho anaanza kuendesha na kubeba abiria,” alisema Chisseo.Katika maadhimisho ya hivi karibuni ya Wiki ya Kimataifa ya Usalama Barabarani, Mtandao wa Wadau kutoka Asasi za Ki- raia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera ihusuyo Usalama Barabarani nchini unasisitiza watunga sera na sheria kuifanyia marekebi- sho Sheria ya Usalama Barabarani ya Mwaka 1973 ili itamke kuwa ni lazima kwa dereva wa pikipiki au bajaji na abiria wake kuvaa kofia ngumu wawapo safarini.Aidha, katika chapisho lake la mapendekezo ya maboresho ya sheria ya usalama barabarani kwa mtazamo wa visababishi vya ajali, Mtandao huo unasema: “Sheria iweke pia kiwango cha ubora wa kofia ngumu ambacho kitatambulika na Shirika la Viwango vya taifa (TBS) kwa kulinganishwa na viwango vya Shirika la Viwango la Kimataifa.”Mratibu Mradi wa Usalama Barabarani wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Gladness Munuo, anasema utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2015 unaonesha kuwa, matumizi sahihi ya helmeti, hupunguza uwezekano wa vifo itokeapo ajali kwa asilimia 40 na kupunguza uwezekano wa majeraha makubwa kwa asilimia 70.Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano huyo wa KCMC, katika kipindi cha miezi sita iliyopita, hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wastani wa majeruhi 14 hadi 15 kwa wiki watokanao na ajali za pikipiki.“Katika wodi ya mifupa kunakofanyika pia upasuaji wa miguu, mikono au kichwa, kwa wiki tunakuwa na wastani wa majeruhi 15 hadi 30 ingawa idadi hiyo nayo inazidi kupungua, lakini wengi kati ya 6 hadi 7 ni wale wanaopata madhara makubwa katika vichwa wanapopata ajali wakiwa kwenye pikipiki kutokana na kutovaa helmeti,” alisema.Akaongeza: “Tatizo au kisababishi kikubwa cha hali hii ni wengi kutovaa helmeti sasa ikitokea ajali akiwa kwenye pikipiki, anagonga kichwa kwenye lami; au kama amevaa bila kufunga, ikitokea ajali, kofia inatoka kabla yeye hajafika chini, akifika anagonga kichwa moja kwa moja kwenye lami, jiwe au sehemu ngumu…”
kitaifa
WISCONSIN, MAREKANI PICHA  ya Babu aliye karibu kuaga dunia akinywa funda za mwisho za bia imewavutia watu wengi sana duniani. Mzee huyo ni Norbert Schemm, 87,wa Appleton, Wisconsin, alitaka kutumia muda wa mwisho alionao akiwa na wapendwa wake pembeni wakati akinywa bia. Pamoja na familia yake walizungumza, walicheka na kukumbuka matukio mbalimbali kabla ya kupiga picha ya pamoja ambayo mtoto wake aliituma kwenye kundi la Whats App la familia. Lakini saa chache baadae wakati Schemm alipofariki na mjukuu wake kutuma picha mtandaoni, familia nzima waliguswa sana na idadi ya watu wengi waliowafariji kwenye picha yake ya mwisho. Tayari ilikuwa ina maoni ya watu 4,000, na wengine 30,000 wakisambaza kwenye kurasa zao za Twitter na wengine 317,000 wakipendezwa na picha hiyo kwenye ukurasa wa Twitter pekee na kwenye mitandao mingine ya kijamii kama Reddit. Adam anasema: ”Babu yangu alikuwa na afya siku zote, lakini siku ya Jumapili juma lililopita alipokuwa hospitali madaktari walibaini kuwa ndio mwisho wa maisha yake. “Aliwaita wajukuu zake siku ya Jumatatu ili kutuambia. Tukapiga picha siku ya Jumanne usiku na kisha alipoteza maisha siku ya Jumatano kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo mpana”. ”Baba yangu alituambia babu alikuwa anataka bia na sasa nikitazama picha hii inanifariji. ”Ninaweza kusema babu yangu anatabasamu. Anafanya kile alichotaka kukifanya,” Adam anasema alisita kuweka picha kwenye mtandao wa kijamii mara ya kwanza kwasababu ya hali ya simanzi na uchungu wa mazingira ya picha hiyo, lakini aliamua kuendelea kwa sababu ulikuwa wakati mzuri sana. ”Inatusaidia katika machungu tuliyonayo. Inatufariji kuona wazee wetu na watoto wao wako pamoja, sote tuko pamoja katika wakati huu wa mwisho.” Ben Riggs, ni miongoni mwa watu walioguswa na picha hiyo, akaweka picha ya babu yake Leon Riggs, 86, akifurahia kitendo chake cha mwisho cha kuvuta sigara na kunywa bia. Ben ameiambia BBC kuwa aliiona picha hiyo kweye kurasa za Twitter ikamkumbusha babu yake kuhusu ombi lake la mwisho kabla ya kifo chake mwaka 2015. Ben alisema babu yake alikuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu, lakini mwishowe, yeye na baba yake walihisi ni muhimu kutimiza matamanio yake kabla ya kifo. Ben alisema jioni moja babu yake alifariki, kaka zake na baba yake walikutana kwa ajili ya kusherehekea maisha yake. Wakapiga picha nyingine ya familia. Ben Riggs alimpoteza baba na babu yake kwa kipindi cha saa 48, lakini alipata faraja kwa kuwa yeye na kaka zake walipata picha ya pamoja na baba yao. Ann Neumann, mwandishi wa kitabu cha ‘The Good Death, amesema: ”imewagusa wengi kwa sababu picha hutupa nafasi ya kufikiria kuhusu wapendwa wetu na kuungana na familia ya Schemm”. Amesema picha ambazo kila mtu angependa ni zile za kuwa na wale uwapendao katika siku yako ya mwisho. Kuna mamilioni ya hadithi kuhusu wazazi wanaopoteza maisha wakiwa hawana fahamu siku za mwisho za maisha yao. Kukosa nafasi ya kusema kwaheri, ni hofu ambayo binaadamu wengi wanayo. ”Kama kuna cha kujifunza kutokana na picha hii ni kushikamana na wale tunaowapenda, kunywa bia, shikana nao mikono na mshirikiane kwa hadithi mbalimbali. Kwa kuwa maisha yana mwisho”.
kimataifa
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM  KAMPUNI ya TBL Group imeeleza dhamira yake ya kuendelea kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu ikiwamo kuwajengea mazingira rafiki sehemu za kazi badala ya kuwabagua na kuwafanya wakose kujiamini na kujiona si sehemu ya jamii. Mkakati huo umeelezwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL Group, David Magesse, alipokuwa anaeleza sababu za kuanzishwa kwa mkakati huo. Alisema kampuni inao mtazamo wa kutoa ajira bila ya ubaguzi wa rangi, jinsia na ulemavu hivyo iko makini kuhakikisha wafanyakazi wake wote inaowapatia ajira wanafanya kazi katika mazingira bora na kupata haki zao zote sawa. “Kwa upande wa wafanyakazi wenye ulemavu tumewajengea mazingira rafiki ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri na tumekuwa tukishirikiana na taasisi ya CCBRT ambayo imekuwa ikitupatia miongozo inayotakiwa yakiwamo mafunzo ya ushirikishwaji wao katika majukumu ya kampuni bila kuwaacha nyuma.” Magesse alisema kampuni imeajiri watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali pamoja na kuwapatia fursa za maamuzi na kutoa mawazo yao kwa kujenga miundombinu rafiki kwao katika kupata huduma zinazostahili. Magesse alisema kampuni itaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi ya CCBRT ambayo pia itawasaidia wanapohitaji kutoa ajira kwenye nafasi za watu wenye ulemavu kuwapata wenye sifa zinazostahili kwa nafasi za taaluma mbalimbali zinazokuwepo. “Kwa ushauri wa wataalamu, kampuni imefikia viwango vya utekelezaji kanuni na miongozo ya kuwajengea watu wenye ulemavu mazingira mazuri sehemu za kazi kwa mujibu wa mwongozo wa Shirika la Kazi Duniani na sheria inayohusiana na huduma kwa watu wenye ulemavu ya mwaka 2010. Aidha, Magese alisisitiza kuwa katika muda wote ambao kampuni imewapatia ajira watu wenye ulemavu wamegundua kuwa wakijengewa mazingira bora sehemu za kazi wanafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu na ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwapatia fursa za kushiriki kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa. 
kitaifa
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliamsha shangwe za wananchi wa Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, mkoani Dodoma baada ya kuwasha umeme katika kijiji hicho. Naibu Waziri huyo, aliwasha umeme katika zahanati ya kijiji hicho pamoja na kisima cha maji ambapo kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa Backbone Transmission Investment Project (BTIP) (kv 400) ambao umesambaza umeme katika vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi kutoka Iringa hadi Shinyanga.Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Mgalu alisema kuwashwa kwa umeme katika kijiji hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano kufikisha umeme katika vijiji vyote nchini. Alisema, Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa vijiji takribani 2,018 vyenye umeme na kuanzia Januari 2016, vijiji vipya vilivyoongezeka ni takribani 5,000 hivyo hadi sasa vijiji 7,290 vina umeme kati ya Vijiji 12,268. Kuhusu usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayajapata umeme ingawa yamepitiwa na miundombinu alisema kuwa, kuna mradi wa ujazilizi, mzunguko wa pili unaolenga kuongeza wigo wa kuunganisha umeme katika vitongoji mbalimbali na Dodoma ni moja kati ya mikoa 9 itakayoguswa na mradi huo. Naibu Waziri pia amesisitiza wananchi kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo vitawawezesha kuondokana na gharama za wiring na kuwezesha kuunga wateja wengi katika mradi huo wa BTIP. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde (CCM) alishukuru serikali kwa kupeleka umeme katika kijiji hicho, hata hivyo aliomba umeme huo ufike katika maeneo muhimu kama vile shamba la umwagiliaji, nyumba za ibada, na vitongoji vya kijiji hicho.Aidha, aliipongeza serikali kwa kufanya kazi bila ubaguzi kwani idadi ya watu katika Kijiji hicho si kubwa ukiliganisha na vijiji vingine lakini serikali haikungalia idadi ya watu ili kufikisha umeme katika Kijiji hicho wala hadhi ya nyumba. Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chamwino, Baltazary Massawe alisema wilaya ya Chamwino in jumla ya vijiji 107 kati ya hivyo, vijiji 33 vimewekewa umeme kupitia miradi mbalimbali iliyopita kijijini hapo.Alisema vijiji vitakavyokidhi na umeme kupitia REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kwa wilaya ya Chamwino ni vijiji 32 na vijiji 11 kupitia mradi wa BTIP. Aidha wilaya ya Chamwino inahudumia sehemu ya jimbo la Dodoma katika kata ya Kikombo ambapo vijiji viwili vitanufaika kwa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na kujumuisha vijiji kuwa 45 kwa miradi inayoendelea kwenye wilaya ya Chamwino.Massawe alisema baada ya miradi hiyo kukamilika vijiji 82 kwa wilaya ya Chamwino vitakuwa vimenufaika na umeme.Alisema miradi ya umeme itawanufaisha wananchi katika mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia watoto na walimu katika shughuli za kielimu hasa kwa kusoma na kutumia vifaa vya Tehama.Pia upatikanaji wa maji kwa urahisi kwa kuwa nishati itasaidia kuyavuta kirahisi kutoka kwenye chanzo. Aidha huduma za afya zitaboreka kwani itasaidia kurahisisha mambo mengi ambayo yalikuwa hatafanyiki kwa kukosa huduma ya nishati ya umeme na kuamsha shughuli za kiuchumi.
kitaifa
Hatua hiyo itafanya shirika hilo la ndege kutoa huduma ipasavyo katika sekta ya anga na kukamata soko kwenye nchi za Afrika Mashariki, ambalo kwa sasa imeshikiliwa na nchi za Ethiopia, Kenya na Rwanda.Makamu wa Rais wa Mauzo katika Kampuni ya Ndege ya Latin Amerika, Afrika na Visiwa vya Caribbean, Van Rex Gallard alithitisha kuwa Tanzania imetoa oda ya ndege moja ya 787-8 Dreamliner, yenye thamani ya dola za Marekani milioni 224.6 na itaendeshwa na ATCL.Hivi karibuni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema wanatarajia kuanza Safari za Ulaya, Asia na Marekani katika kipindi kifupi na ndege hizo ni imara kufikia lengo hilo.Alisema Tanzania ilitia saini makubaliano na kampuni ya Bombardier Commercial Aircraft ya kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 Julai mwaka 2016 na miezi mitano baadaye walisaini kununua Boeing 787-8 Dreamliner. Matindi alisema Bombardier C300s, zitatumia kufungua safari za usafiri wa anga katika kanda sita za Kusini na Magharibi mwa Afrika, kwa lengo la kupata masoko hayo.“Tuna lengo la kukamata masoko ya Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe na baadaye kufika nchi za Afrika Magharibi za Ghana na Nigeria pamoja na kutumia ndege ya Dreamliner katika safari za kimataifa za China na India na baadaye kufuatiwa na kwenda bara za Ulaya katika awamu ya pili,” alisema.ATCL inatarajia kupata cheti kutoka taasisi ya kimataifa ya ukaguzi wa usalama na viwango kwa mashirika ya ndege duniani IOSA, kabla ya Juni mwaka huu, hali itakayowezesha kushirikiana kibiashara na watoa huduma wengine ili kuongeza mapato kupitia makubaliano ya hisa.Miaka miwili iliyopita, Tanzania ilianza mkakati wa kufufua shirika hilo la ndege la serikali kwa kuweka mikakati mbalimbali.Katika programu hiyo waliweka mikakati ya kununua ndege mpya sita kati ya mwaka 2016 hadi 2018, kulipa madeni na kuongeza mtaji na kukuza na kuendesha biashara kwa njia za kisasa.Kwa sasa, licha ya kuanza kusaka ofisi katika nchi mbalimbali, ATCL imetangaza ajira mpya 88 zikiwemo za wahudumu katika ndege.
uchumi
Na ELIYA MBONEA -ARUSHA KIKOSI cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, kimekusanya Sh 10.864,170,000 za faini kutoka kwenye makosa 362,136 kwa kipindi cha Januari 2017 hadi Machi 2019. Akitoa taarifa  ya kikosi hicho, RTO Joseph Bukombe, alimuomba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana, awaunge mkono kuhakikisha deni la Serikali Sh bilioni 13 zilizopo nje zinakusanywa. Bukombe alisema  kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu hakuna ongezeko la ajali za barabarani.  Akizungumzia wiki ya nenda kwa usalama, alisema, “mpaka sasa magari ya watu binafsi na ya biashara 17,000 na pikipiki 5,000 yamekaguliwa. Hatua hii itadumu kwa miezi mitatu baada ya hapo utakuwa ukaguzi wa lazima. “Hatua inafanyika chini ya kaulimbiu ya “Paza Sauti”, kila anayetumia chombo cha moto barabarani akiona hatari ya kusababisha mtu kujeruhiwa au kupata madhara anatakiwa kutoa taarifa. “Tunaamini kila mtu akipaza sauti kwa kusaidia muhusika alazimishwe kutii sheria hakutakuwa na madhara na hapo tutaokoa maisha ya watu,” alisema RTO Bukombe. Kuhusu hali ya usalama kwa January hadi Machi mwaka huu alisema   ajali 10 zilitokea ambako ajali za vifo zilikuwa saba, waliokufa watu tisa, ajali za majeruhi tatu, waliojeruhiwa watu 17. Alisema kwa Januari hadi Machi mwaka 2018 ajali zilikuwa 15 ambako ajali za vifo 11, waliokufa 12, ajali za majeruhi tatu, waliojeruhiwa 14 na ajali ya kawaida moja. Alisema kikosi hicho kimeongeza juhudi za kukamata makosa hatarishi   kukabiliana na ajali za barabarani, ikiwamo kuongeza doria kwa kutumia Speed Radar. “Tumejizatiti maeneo hatarishi kwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria hasa yenye miteremko mikali na makazi ya watu. “Lakini pia upimaji wa ulevi kwa madereva nazo zimeendelea kufanyika maeneo mbalimbali hasa kituo na kuwabaini madereva. “Ukiruhusu makosa madogo ya barabarani utakuwa unakaribisha makosa makubwa na madhara zaidi kwa watu,” alisema RTO Bukombe. Alitumia fursa hiyo kuwataka wanaodaiwa na Serikali kulipa madeni yao kwa sababu  yeyote anayedaiwa hatatoka salama mkoani humo.
kitaifa
NA CHRISTOPHER MSEKENA HAKUNA msanii duniani anayemfikia kwa utajiri rapa Shawn Carter ‘Jay Z’. Hakuna mwanamuziki wakike mwenye utajiri mkubwa kama alionao Robyn Fenty ‘Rihanna’ kwa mujibu wa Forbes. Jarida la Forbes linaloaminika duniani kwa kutoa orodha mbalimbali za watu maarufu na utajiri wanaoumiliki, limebainisha vyanzo vya mapato vinavyofanya wawili hao wawe na utajiri mkubwa zaidi tofauti na wasanii wenzao. Wameweka wazi kuwa Jay Z kwasasa ni rasmi amekuwa bilionea baada ya kufikisha utajiri wa dola za Marekani Bilioni 1 ambazo ni zaidi ya shilingi Trilioni 2 za Tanzania huku Rihanna akimiliki utajiri wa dola za Marekani milioni 600 sawa na shilingi Trilioni 1.3. Swaggaz, tunakupa mchanganuo rahisi wa vyanzo vya mapato vya Jigga na Rihanna kama ambavyo Forbes wamebainisha kwenye orodha zao, karibu ujifunze zaidi. JAY Z Mara kadhaa orodha ya utajiri imekuwa ikiongozwa na P Diddy, Jay Z na Dr Dre lakini safari hii ‘bae’ wa Beyonce ameshikilia namba moja na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufikisha utajiri wa dola bilioni 1. Vyanzo vyake vya mapato vimewekwa wazi. Jay Z ni mwanamuziki, mfanyabiashara na mwekezaji kwenye miradi mbalimbali katika tasnia ya muziki na ujasiliamali. Ikumbukwe kuwa Forbes hawatoi hesabu za fedha taslimu wanazomiliki wasanii bali wanahesabu thamani ya uwezekezaji aliofanya msanii husika, mapato ya kazi zake na vitega uchumi vingine. Kwa muktadha huo, Jay Z anapiga sana pesa kwenye uwekezaji wa shampeni yake inayoitwa Armand de Brignac inayouzwa shilingi 29,850 kwa chupa moja na kinywaji hicho humwiingizia dola za Marekani milioni 310 kwa mwaka. Rapa Jay Z, benki ana akiba inayokadiliwa kuwa ni dola za Marekani milioni 210 huku pombe yake kali inayoitwa D’Usse unayouzwa shilingi 91,800 na kuendelea kulingana na ukubwa wa chupa hivyo jumla imemwingizia dola milioni 100. Jay Z pia anatengeneza kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kupitia mtandao wake wa kusikiliza nyimbo (music streaming service) unaoitwa Tidal ambao ndani yake zinapatikana kazi za wasanii wakubwa duniani Kanye West, Coldplay, Beyonce, Nicki Minaj, Madonna, Usher na wengine huku ukichuana vikali na mtandao wa Spotify. Pia rapa huyu anamiliki lebo ya muziki ya Roc Nation iliyowahi na inayoendelea kufanya kazi na wasanii kama Dj Khaled, marehemu Nipsey Hussle, Shakira, Alicia Keys, Rihanna, Beyonce, Big Sean na wengine wengi. Lebo hiyo aliyoianzisha mwaka 2008, ina thamani ya dola za Marekani milioni 75 sawa na mapato yanayotokana na mauzo ya muziki hasa albamu zake ikiwamo ile ya 4:44. Hali kadharika sanaa ambazo amekuwa akizifanya sehemu mbalimbali ikiwamo mavazi ya Roca Wear ambazo thamani yake ni dola milioni 70. Hali kadharika, Jigga amefanya uwekezaji katika usafiri maarufu duniani wa Uber sambamba na kuwekeza kwenye ardhi kwa kujenga majumba ya kifahari kama vile Bel-Air Estate na East Hampton Mansion ambazo zina thamani  ya Dola milioni 70. JAY Z, BEYONCE WAJIPONGEZA Kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa kuwa Jay Z ndiye msanii wa kwanza kuwa bilionea, rapa huyo na mke wake Beyonce walikwenda kuburudika kwa mchezo wa mpira wa kikapu, usiku wa kuamkia juzi kwenye uwanja wa Courtside Oracle Arena katika fainali za ‘game’ 3 ya NBA kati ya Golden States Warriors na Torinto Raptors. Inadaiwa wawili hao walikaa viti vya mbele ambavyo kawaida huwa vinalipiwa shilingi milioni 190 lakini kwao viti hivyo vikauzwa kwa dola elfu 92 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200. RIHANNA  Unaweza ukashangaa kwanini Rihanna ametajwa kama mwanamuziki wakike mwenye utajiri mkubwa zaidi licha ya kutotoa  wimbo wowote toka alipoachia albamu yake ANTI mwaka 2016. Nje ya muziki Rihanna ni mjasiliamali na mwekezaji katika tasnia ya mitindo na urembo, amekuwa akiingia ubia na kampuni mbalimbali kubwa ambazo zimechangia kipato chake kuongezeka. Mrembo huyo kutoka visiwa vya Barbados, ameowaburuza wanamuziki wengine kama Madonna mwenye utajiri wa dola 570, Céline Dion mwenye dola 450 na Beyoncé mwenye utajiri wa dola 400. Vyanzo vikuu vya mapato kwa Rihanna ukiacha muziki ni bidhaa zake za urembo kama vile rangi za kucha na midomo zenye chapa Fenty Beauty, bidhaa iliyozinduliwa kwa kishindo mwezi Septemba, 2017 na kwa wastani mwaka jana ndani ya miezi 15 toka izinduliwe zikaingiza mapato ya dola za Marekani milioni 570. Pia Rihanna ni mbia wa kampuni ya Kifaransa, LVMH (Louis Vuitton Moet Hennessy), inayozalisha bidhaa za kifahari kama vile mvinyo, mavazi ya ngozi, saa za mkononi na manukato yenye chapa Fendi. RIHANNA AKODI KISIWA KUANDAA ALBAMU Mtandao wa Mirror umeripoti kuwa Rihanna, ambaye amekuwa akiishi nchini Uingereza tangu mwaka jana, amekodi kisiwa na studio za ‘State of the Art’ zilizopo visiwa vya Oseate,  ambacho kinagharibu Paundi 20,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 58 kwa siku moja lengo likiwa ni kupata utulivu wa kuandaa albamu yake ya tisa inayotajwa itaitwa R9.
burudani
Katika fainali iliyofanyika Dar es Salaam juzi, Kayumba aliibuka mshindi baada ya kumshinda mshiriki mwenzake, Nassib Fonabo, hiyo ikiwa ni baada ya mshiriki Frida Amani kutolewa katika hatua ya tatu bora.Mshindi huyo aliibuka mshindi baada ya kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Fonabo; na katika karata yake ya mwisho, aliimba wimbo wa Mama uliiombwa na Isha Mashauzi.Katika shindano hilo ambalo lilihudhuriwa na maelfu ya watu lilifanyika kwenye Ukumbi wa King Solomon, Kinondoni na kupambwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii Run Town wa Nigeria.Katika shindano hilo ambapo walioingia fainali walikuwa ni washiriki sita ambao ni washiriki wa mwaka huu ni Amani, Kayumba, Angel Kato, Fonabo, Jacqueline Kakenzi pamoja na Kelvin Gerson.Wote waliimba nyimbo nne nne kila mmoja kabla ya kuchujwa ambapo Kakenzi na Gerson walitolewa. Kisha walibaki wanne ambao ni Fonabo, Kato, Amani, Kayumba na kisha kutolewa tena Kato.Walibaki watatu na kisha alitolewa Amani ambaye ni mshiriki kutoka mkoani Arusha ambaye alikuwa anapenda zaidi kuimba nyimbo za kughani. Usiku huo ulipambwa na shoo za Yamoto Band, Christian Bella, Peter Msechu, Ben Pol, Kala Jeremiah na Run Town.
michezo
CAIRO, MISRI MLINDA mlango wa timu ya taifa ya Zimbabwe, George Chigova, ameweka wazi kuwa, kipigo walichokipata dhidi ya Misri katika mchezo wa ufunguzi wa Mataifa ya Afrika, hakikutokana na mgogoro wao na Chama cha soka (ZIFA). Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), huko nchini Misri kulikuwa na taarifa kwamba, timu ya Zimbabwe imegoma kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa posho zao kutoka kwa Chama cha soka nchini Zimbabwe. Mchezo huo wa ufunguzi ulimalizika kwa Zimbabwe kukubali kichapo cha bao 1-0, lililofungwa na Mahmoud Trezeguet, lakini Zimbabwe walionesha kiwango cha hali ya juu. “Tunajua kwamba, tulikuwa kwenye matatizo, lakini baada ya kumalizika kwa matatizo hayo wachezaji tuliambiana kuyasahau yaliyotokea na kuangalia nini tunatakiwa kukifanya kwenye mchezo huo. “Wote tulikuwa na furaha kubwa kushiriki mchezo huo wa kwanza, hivyo hatukuupoteza kwa sababu ya mgogoro wetu wa siku chache zilizopita kwa kuwa kila kitu kilikuwa kimekaa sawa. “Tunaamini kila chama cha soka kila matatizo yao na timu zao, hivyo kwa upande wetu tuliweza kuyamaliza, tunachotaka sasa ni kuwafanya watu wa Zimbabwe kujivunia uwepo wetu kwenye michuano hii,” alisema kipa huyo.
michezo
NA ALLY BADI- LINDI MAHAKAMA ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu kwenda jela miezi nane, Suleiman Mathew ambaye alikuwa mpinzani wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika Jimbo la Mtama. Mathew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Lindi na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali. Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina. Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha shaka. Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi sita. Alisema kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani. Baada ya kuwatia hatiani mahakama iliwapa nafasi washtakiwa ili waweze kujitetea ambapo waliomba  wapunguziwe adhabu. Akiwasilisha hoja za upande wa utetezi Wakili wa washtakiwa hao,  Deusdet Kamalamo aliiomba mahakama isiwape adhabu kali kwa madai kwamba wanafamilia inawategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kubwa kutaifanya ikose huduma zao. Baada ya utetezi huo, Wakili wa Serikali Juma Maige aliiomba mahakama hiyo iwape washtakiwa hao adhabu kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwao na wengine. Hakimu Mhina akitoa adhabu katika kesi hiyo namba 36/2016, chini ya kifungu cha 74 (1) na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, alisema mahakama inawapa adhabu, kila mshtakiwa  atatumikia kifungo cha miezi minane gerezani na kusema nafasi ipo wazi ya kukata rufaa iwapo wataona hawakuridhishwa na hukumu hiyo. Baada ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mathew alisikika akiguna na baadae aliketi sakafuni, huku katibu wake wa tawi, Ismail  ambaye alionekana kuchoka kutokana na hukumu hiyo akiwa amelowa kwa jasho. Mahakama hiyo pia iliwaachia huru washtakiwa wanne ambao ni wanachama waliokuwa wameshtakiwa pamoja na viongozi hao, baada ya ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa mashtaka kutokuwa na mashiko ya kuishawishi mahakama kuwatia hatiani. Washtakiwa hao ni Bashiru Rashid, Hassani Mchihima, Abdallah Masikini na Mohamedi Makolela ambao wote ni wakazi na wakulima wa Kata ya Nyangamala. Awali washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Aprili 3,  mwaka jana, maeneo ya Kata ya Nyangamala, mkoa Lindi, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali. Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Wakili wa upande wa utetezi,  Deusde Kamalamo alisema wanajiandaa kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo. “Tutakata rufaa kupinga uamuzi huu, leo naandaa barua ya kuomba nakala ya hukumu ili tuanze kuandaa rufaa ya wateja wangu,” alisema Wakili Kamalamo. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Methew alikuwa akipambana na Nape ndani ya CCM lakini alishindwa kufurukuta katika kura za maoni na baadae alijiengua na kujiunga na Chadema na kuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho. Katika hatua nyingine jana Diwani wa Kata ya Kyangasaga, wilayani Rorya, Christopher Kichinda maarufu ‘Protocol’ amehukumiwa kwenda jela miaka mitano. Akizungumzia hukumu hiyo Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche, alisema diwani huyo alikuwa anakabiliwa na kesi ya Katiba iliyokuwa inamkabili kuwa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya lakini alijitoa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa yaliyokuwa yanamkabili. “Ni kilio kingine kwa demokrasia ya nchi yetu na ufanisi kwa siasa za CCM,” alisema Heche. Mbali na viongozi hao wiki iliyopita Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ilimuhukumu Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (30), kifungo cha miezi sita kwa kufanya vurugu na kusababisha taharuki kwenye mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Dotto Ngimbwa awali alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa namba moja (Peter) na mwenzake Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi mosi, mwaka jana Kibaoni kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. MBOWE ALAANI Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumzia hatua ya Methew kuhukumiwa kwenda jela, alisema huo ni mkakati ulioandaliwa Serikali ya CCM kudhohofi sha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa. Hata hivyo, Mbowe aliwagiza viongozi wa chama hicho nchi zima kuandaa orodha ya kesi walizonazo ili kuziwasilisha jumuiya za kimataifa kuonyesha jinsi upinzani unavyokandamizwa na kupokonywa haki yao ya kufanya siasa. Alisema Methew amehukumiwa wakati tayari Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali akiwa ameshahukumiwa kwenda jela miezi sita.
kitaifa
USHIRIKA wa Wahitimu Wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUGECO) kwa kushirikiana na uongozi wa chuo hicho (SUA), umewezesha vijana 125 kwenda nchini Israel kwa ajili ya kujifunza teknolojia za kilimo, mifumo ya uzalishaji, masoko, ujasiriamali na kubadilisha fi kra na mtazamo.Mkurugenzi Mtendaji wa Sugeco, Revocatus Kimario alisema hayo hivi karibuni katika taarifa yake mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kufundisha vijana kujenga vitalu nyumba na ulimaji wa mbogamboga kibiashara kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba.Alisema jumla ya wataalamu 50 ambao ni wahandisi wa kilimo, maji na umwagiliaji wa vipando na udongo wa mbogamboga na matunda na wengine wa uchumi na biashara kilimo, walijengewa uwezo wa kufundishwa teknolojia ya kitalu nyumba. Hata hivyo Kimario alisema vijana hao walipelekwa nchini humo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kwa mwaka huu vijana 45, wapo nchini humo kujifunza kwa muda wa mwaka mmoja. Alisema wanaporudi huwafundisha vijana wenzao na wengine wamefanikiwa kujiunganisha na kuanzisha kampuni.Tayari vijana watatu wameweza kupata mkopo wa zaidi ya Sh milioni 200 kutoka Benki Maendeleo ya Kilimo na hivi sasa wanaendesha kilimo cha mbogamboga wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Alisema kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Sugeco imewafikia vijana 5,000 kuwahamasisha kuingia kwenye kilimo hususani kilimo biashara baada ya kufanyia kazi mambo ya msingi ikiwemo kubadili fikra na mitazamo yao.Aidha vijana hao baada ya kupewa stadi na ujuzi stahiki wa elimu ya ujasiriamali na jinsi ya kutunza fedha wameweza kufanya mambo mengi ya maendeleo na sasa baadhi yao wanaendesha miradi ya kuwaingizia kipato. Katika hatua nyingine, Kimario alisema kwa sasa vipo vikundi 15 vinavyowezeshwa na vinavyojihughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo wa kilimo cha vitalu nyumba.Naye Mtaalamu wa Lishe wa Sugeco, Jolenta Joseph ameeleza kuwa moja ya kazi zinazofanywa na wajasiriamali ni utengenezaji wa biskuti za viazi lishe, mikate na juisi yake. Alisema viazi lishe ni vizuri kwa afya kwa kuwa vina vitamini na madini na virutubishi vingine kwa wingi ambayo husaidia kuondoa utapiamlo na upungufu wa vitamizi A endapo vikitumiwa ipasavyo. Naye mjasiriamali aliyewezeshwa na Sugeco, Veronica Kavishe alisema alifundishwa jinsi ya kutengeneza juisi za aina mbalimbali za matunda na ya viazilishe na sasa biashara yake imekuwa na uhakika wa kumwingizia kipato, ambapo kwa siku anatengeneza juisi lita 200.
kitaifa
Wizara ya Katiba na Sheria imependekeza kurekebisha kifungu cha Sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu ili kumpa mamlaka Rais amteue kiongozi huyo. Kwa kuzingatia sheria ya sasa, Waziri ndiye mwenye mamlaka ya kumteua Kabidhi Wasii Mkuu.Mapendekezo ya Wizara ni sehemu ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali uliosomwa bungeni leo jijini Dodoma. Taratibu za kuupitisha muswada huo zimekamilika lakini imeshindikana kuupitisha kwa kuwa akidi ya wabunge haikutimia. Wabunge wamemaliza kuujadili muswada huo na unatarajiwa kupitishwa Jumatatu.Muswada huo unapendekeza kurekebisha kifungu cha pili cha sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu (Mamlaka na Utekelezaji wa Majukumu), Sura ya 27. Pendekezo hilo lina lengo la kuonanisha masharti ya sheria hiyo na masharti ya Sheria ya Wakala za Serikali , Sura ya 245 na pia kuanzisha nafasi ya Naibu Kabidhi Wasii Mkuu atakayekuwa Ofisa Masuhuli wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). wenye sehemu hiyo ya pili ya Muswada kuna pendekezo pia la kurekebisha kifungu cha nne cha sheria hiyo kwa kuweka masharti yatakayomwezesha Rais wa Tanzania amteue Kabidhi Wasii Mkuu."Sababu ya mapendekezo hayo ni kutokana na uzito wa majukumu na mamlaka ya Kabidhi Wasii Mkuu, hadhi ya ofisi yake na nafasi yake mahakamani kwa mujibu wa kifungu cha 4 (3) cha sheria hiyo. Muswada unaweka masharti kuhusu sifa za mtu anayestahili kuwa Kabidhi Wasii Mkuu na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu ili kutoa mwongozo kwa mamlaka ya uteuzi" amesema Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi wakati anawasilisha muswada huo. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 wa mwaka 2018 una lengo la kurekebisha sheria 13.
kitaifa
WAKATI wanariadha watatu wa Tanzania wakitarajia kupeperusha bendera ya taifa kesho katika mashindano ya Dunia, Katibu Mkuu wazamani wa Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui ameeleza sababu za Failuna Abdi (pichani) kushindwa kumaliza mbio katika mashindano hayo ya Dunia.Nyambui pia ni kocha wa kimataifa wa riadha, ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya taifa ya Brunei. Failuna alikimbia marathon kwa upande wa wanawake siku ya ufunguzi wa mashindano hayo, Septemba 27 Doha, Qatar, lakini alishindwa kumaliza sababu ya joto kali. Akizungumza kwa njia ya simu juzi kutoka Brunei, Nyambui alieleza sababu kadhaa zilizomfanya Failuna kujitoa katika mbio hizo kabla ya kumaliza kilometa 42, ikiwemo kutokuwa na kocha siku hiyo ya mbio na ugeni wake wa mashindano.Alisema kama mwanariadha huyo angekuwa na kocha, bila shaka angepata maelekezo kabla ya kuanza kwa mbio hizo na kusisitiza kunywa maji kabla na wakati wa mbio, lakini hilo halikufanyika.Alisema kuwa mwanariadha huyo alishindwa mbio tangu alipowasili Doha, kwani hakuwa na mtu wa kumpokea, hivyo alijikuta akikaa muda mrefu kiwanja cha ndege akisubiri kupokelewa hadi pale `alipookotwa’ na wasamalia wema. Pia Nyambui alisema kuwa hata siku ya mbio, mwanariadha hiyo hakuandaliwa maji maalumu, kama walivyofanya wengine, ambao walikuwa na makocha wao.Pia Nyambui alipinga vikali Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday kwenda Doha na badala yake alitaka nafasi hiyo angepewa kocha ili akajifunze kitu na kupata uzoefu wa mashindano ya kimataifa na kuja nchini kutoa funzo kwa wenzake na wanariadha anaowafundisha.Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday ambaye yuko Doha alisema kwa kushirikiana na wakala wa Failuna kutoka Uholanzi, walimuandalia mwanariadha huyo maji maalumu na alipata kila kitu kilichotakiwa.Alisema ukali wa joto la Doha ndilo lililomuangusha mwanariadha huyo, ambaye hiyo ni marathon yake ya tatu kushiriki na ni mara ya kwanza kushiriki marathon ya dunia.Kocha wa Failuna, Thomas John alisema jana kutoka Arusha kuwa kukosekana kwa kocha Doha, sio sababu za mwanariadha wake kushindwa, ila ni sababu ya kutokuwa na maandalizi mazuri, ambayo yalichangiwa na ukosefu wa fedha.Alikiri mwanariadha wake kutojiandaa vizuri na kusema kuwa kama RT ingekuwa na fedha, basi angemuandaa mwanariadha wake kisayansi zaidi ili aweze kukabiliana na joto hilo la Doha.
michezo
Miradi hii ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti mkoani Pwani kuungwa mkono na Watanzania wengi.Uzinduzi wa viwanja hivi vipya uliongozwa na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Martha Minga na Mkurugenzi Mkuu Bayport, John Mbaga na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu Bayport, John Mbaga alisema huduma zao zitakuwa njia rahisi kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo.“Viwanja hivi tunauza kwa mkopo na pesa taslimu, mkopo kwa wajasiriamali na watumishi wa kampuni binafsi, wanatakiwa kulipia malipo ya awali ya mita za mraba walizochagua, na Bayport itakamilisha malipo yaliyosalia na wateja hao kupatiwa nyaraka baada ya kukamilisha mkopo ambapo thamani ya viwanja ikianzia Sh 550,000,” alisema Mbaga.Mteja anatakiwa kulipa fedha zote za kiwanja kwenye akaunti ya Bayport, kukabidhi nakala za nyaraka za malipo kwenye ofisi za Bayport na kusubiri siku 90 ili akabidhiwe hati yake baada ya kukamilisha malipo yote.Naye Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile alisema amefurahishwa na huduma ya viwanja vya Bayport na jimbo lake kuwa sehemu ya mradi huo, jambo linaloiweka eneo hilo katika nafasi za juu.Huduma za viwanja katika maeneo ya Bagamoyo (Boko Timiza) zitauzwa kwa Sh 10,000 kwa mita moja ya mraba, Kibaha mita moja ya mraba itauzwa 9,000 na Chalinze mita moja ya mraba itauzwa kwa Sh 4,500.Mita moja ya mraba Tundi Songani, Kigamboni itanunuliwa kwa Sh 10,000 na Msakasa Kilwa mita ya mraba itauzwa 2,000 na Kiegea B mita moja ya mraba 3,500.
uchumi
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amesema kitendo cha baadhi ya wachezaji kujihusisha na mambo yasiyowahusu nje ya uwanja kimechangia kufanya vibaya na kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la FA. Ndoto za Simba kucheza Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani, ziliyeyuka juzi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kocha huyo raia wa Uganda amewatupia lawama wachezaji wake, akidai kuwa baadhi yao wanashinda kutwa nzima kwenye mitandao ya kijamii wakifanya mambo yaliyo nje ya utaratibu wa taaluma yao na kusababisha matatizo. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema hali hiyo inawafanya washindwe kutimiza majukumu yao uwanjani, kwani inafika wakati anampanga mchezaji akitarajia atafanya vizuri lakini matokeo yake wanamwangusha. “Wachezaji kama hawazingatii maadili ni vigumu timu kufanya vizuri, ndio maana jana (juzi) hatukufanya vyema kutokana na wengine kuwa majeruhi na baadhi kuchelewa mazoezi huku wakiomba ruhusa bila mpangilio,” alisema. Mayanja aliwataja wachezaji Hamis Kiiza na Jjuuko Murshid kuwa ni miongoni mwa waliochangia kupata matokeo mabaya, kutokana na kuchelewa  kujiunga mazoezini kwa wakati. Hata hivyo, kocha huyo alisema matokeo hayo si kipimo cha wao kufanya vibaya katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, bali yataongeza hamasa ya kufanya vizuri zaidi. Kwa kipigo cha juzi, Wekundu hao wa Msimbazi wameshindwa kuungana na mahasimu wao Yanga, Azam FC na Mwadui waliotangulia hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.
michezo
KIONGOZI wa zamani wa kundi haramu la Mungiki lililotikisa Jiji la Nairobi na mengine nchini hapa, Maina Njenga na baadhi ya washiriki wake, wamesema ni wakati mwafaka kwa Kenya kuwa na nafasi ya Waziri Mkuu kupitia kura ya maoni inayotakiwa kuitishwa na serikali. Njenga, akitoa dukuduku hilo kwa niaba ya wenzake, alisema kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa 2022, Kenya inatakiwa kupiga kura ya maoni ili kupitisha marekebisho ya Katiba na kuruhusu mfumo wa utawala wa waziri mkuu na manaibu wawili.Njenga ambaye ameachana na kundi la Mungiki baada ya kupigwa marufuku na serikali na kuingia katika ujenzi wa amani na mshikamano wa wananchi wa Kenya kupitia taasisi yake ya Amani Sasa Foundation. Alisema ataitumia taasisi hiyo pamoja na mambo mengine kuunga mkono maridhiano yaliyofikiwa Machi 9, mwaka huu kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga na kuunga mkono mageuzi yanayoendelea sasa hivi ya kiutawala kulingana na maridhiano hayo.Kabla ya Mungiki kupigwa marufuku na serikali ya Kenya, Njenga akiwa ni kiongozi wa kundi hilo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuungwa mkono na vijana wengi katika miji ya Nairobi, Mt Kenya na Nakuru. Kiongozi huyo alisema anaamini bado wafuasi wake wa enzi za Mungiki bado wapo naye ila kilichobadilika ni nadharia ya ukombozi kupitia fujo na mapigano ya kipindi hicho kubadilika na kuwa nadharia ya ukombozi kupitia amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wakenya wote. Katika pendekezo lake, Njenga anataka kuwe na viongozi watano wakuu katika nchi ambao ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Manaibu wake wawili.
kitaifa
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao  Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40)  na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele  ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa  kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020  maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
uchumi
JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI KAMATI ya Maadili (IC) ya Chama Tawala cha African National Congress (ANC), imependekeza kufukuzwa kwa Rais Jacob Zuma. Aidha kikao hicho kilichoitishwa kwa dharura kumjadili Zuma, kilitoa waraka maalumu kuhusu utendaji kazi wa kiongozi huyo. Waraka huo uliosainiwa na Mwenyekiti wa IC, Andrew Mlangeni, ulipangwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa ANC, Gwede Mantshe, ambaye ameombwa kuitisha mkutano wa dharura kujadili mwenendo wa Rais Zuma. Katika waraka huo, Mlangeni alisema kamati hiyo imevunjwa moyo kwa jinsi Rais Zuma alivyochukua uamuzi wa kulifanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri bila kushauriana na upande wowote. Vyanzo vya habari vinasema IC imepanga kukutana na Rais Zuma mwishoni mwa wiki kumshinikiza aachie ngazi. Hatua ya hivi karibuni ya Rais Zuma kumfuta kazi Waziri wa Fedha, Pravin Gordham, imezusha mzozo ndani ya ANC huku thamani ya fedha – Rand ikiendelea kuporomoka. Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa, alikosoa uamuzi huo akisema hakubaliani nao. Vyama vikuu vya upinzani kama Democratic Alliance (DA) na Economic Freedom Fighters Party (EFF), vimemwandikia barua Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Baleka Mbete vikimtaka aitishe kikao cha dharura cha Bunge kujadili suala hilo. Kikao cha awali kilichoitishwa na Bunge la Afika Kusini kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Zuma, kilishindwa kutokana na idadi kubwa ya wawakilishi wa ANC bungeni. Hata hivyo, huenda safari hii hali ikawa tofauti kutokana na kukithiri kwa kashfa za Rais Zuma na hali ya mpasuko inayoendelea kushika kasi ndani ya chama chake.
kimataifa
Na WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM KLABU ya Yanga, imewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea burudani zaidi katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara.  Ligi Kuu ambayo imesimama tangu Machi 17, mwaka huu, baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka maambukizi ya vizuri vya corona. Hivi karibuni Rais Dokta John Magufuli, alisema anafikiria kuruhusu ligi kuendelea, lakini kwa sharti la mechi kuchezwa bila mashabiki. Hadi ligi hiyo inasimama, baadhi ya timu zimecheza mechi 28, nyingine 29, huku Yanga pekee ikiwa imecheza michezo 27 na kukamata nafasi ya tatu, baada ya kukusanya pointi 51. Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, aliwataja mashabiki wao ‘kukaa mkao wa kula’, kwani kikosi chao kitarejea na makali zaidi. Alisema kuwa, kutokana na mazoezi wanayofanya wachezaji wao, anamini watacheza mpira wa burudani na ufundi sambamba na kushinda michezo. “Ninachopenda kuwaambia mashabiki wa Yanga, wakae mkao wa kupokea burudani, unajua kulikuwa hakuna mechi yeyote inayochezwa, kila mmoja ana hamu ya kuona timu yake inakuja vipi. “Sisi Yanga tunasema tunarejea kivingine, tutacheza mchezo mzuri, yaani ‘softball, tunataka kila mmoja afurahi, pia tunaingia uwanjani kupambana kutafuta pointi 30,”alisema. Alieleza kuwa, pamoja na kupigania nafasi mbili za juu, watapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania maarufu Kombe la Azam. “Wachezaji wetu tunawafuatilia, wazingatie program wanazopewa na mwalimu, pia wazingatie suala la afya katika kipindi hiki cha  ugonjwa wa corona,” alisema Nugaz. Kuhusu suala la usajili, alisema kila kitu kinaendelea kulingana na mahitaji ya mwalimu, wakati ukifika wataweka wazi wachezaji waliowasajili lakini kwa sasa  wanajipanga na mechi.
michezo
“KOFI Annan kwa njia mbalimbali alikuwa ni Umoja wa Mataifa. Alikuwa tayari kuhudumia watu kutoka kila sehemu ya dunia, na aliweza kutatua migogoro na hata kuwa sehemu ya kuunda dunia iliyo na amani,” ilisema taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.Ameandika hivyo baada ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan (80) kuaga dunia mapema jana wakati alipokuwa akipatiwa matibabu jijini Bern nchini Uswisi.Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa UN, Guterres alionesha kusikitishwa na taarifa za kifo cha mwanadiplomasia huyo mzaliwa wa Ghana huku akisema kuwa alipokuwa akimuona Annan, alikuwa anaona Umoja wa Mataifa.Guterres alisema, “Annan kwa njia mbalimbali alikuwa ni Umoja wa Mataifa. Alianza kazi kwenye nafasi tofauti tofauti mpaka kuuongoza umoja huo na kuufanya uheshimike na uwe na mipango endelevu.Akimzungumzia kwa namna alivyomsaidia, Katibu Mkuu huyo aliongeza, “Kama ilivyokuwa kwa wengine, nilipenda kumwita Annan mwalimu, lakini pia rafiki.Ninakumbuka kuwa alinipa heshima na kuniamini na kunipa majukumu kwenye Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi wakati huo yeye akiwa ndiye Katibu Mkuu... “…na hata baada ya kumaliza muda wake, alibaki kuwa mtu ambaye ningeweza kwenda kupata ushauri na msaada wa mawazo na tena najua kuwa si mimi pekee, lakini hata wengine wangeweza kwenda kumuona.”Aidha, alisema Annan alikuwa tayari kuhudumia watu kutoka kila sehemu mbalimbali ya dunia ikiwemo kutatua migogoro na hata kuwa sehemu ya kuunda dunia iliyo na amani.“Hiyo ndiyo alama aliyoiacha duniani,” aliongeza Guterres ambaye ni Katibu Mkuu wa pili wa UN baada ya Annan akitanguliwa na Ban Ki-Moon.Katibu Mkuu huyo alitoa pole kwa mke wake, Nane Annan pamoja na familia yake, lakini pia alitoa pole kwa wote waliofikwa na msiba wa mwanadiplomasia huyo aliyependa amani.Taarifa ya majonzi Taarifa rasmi iliyotoka mchana wa jana kupitia tovuti ya Mfuko wa Annan (Kofi Annan Foundation), ilisema “Amefariki akiwa amezungukwa na familia yake mkewe, Nane na watoto wake Ama, Kojo na Nina.“Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa akiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoka mwaka 1997 hadi 2007 na pia kuwa msuluhishi wa mizozo mbalimbali ya kisiasa duniani”.Taarifa hiyo iliongeza kuwa baada ya Annan kumaliza muda wake, alihudumu kama Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani ya mzozo wa nchi hiyo.Aliwafunda wengi Mbali na Katibu Mkuu Guterres kuwa miongoni mwa wale waliowahi kufanya kazi kwa kuaminiwa chini ya Annan, mwanasiasa mkongwe nchini, Profesa Anna Tibaijuka naye ni miongoni mwa waliopata fursa kuaminiwa katika nafasi za juu za umoja huo uliokuwa chini ya Annan.Profesa Tibaijuka alipozungumza na gazeti hili jana, alisema anasikitika kupata taarifa za kifo cha Annan aliyemtaja kama mwalimu wake na pia kiongozi shupavu, aliyemuamini na kumpa nafasi ya kiuongozi kwenye UN.Profesa huyo aliyeteuliwa kujiunga na ofisi kuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) mjini Geneva mwaka 1998, alisema alichojifunza kwa aliyemuibua (Annan) ni jinsi alivyokuwa akionesha jinsi gani Waafrika wanavyoweza kuongoza vizuri.“Kofi Annan alikuwa ni kiongozi shupavu, mpenda amani aliyependa haki iheshimiwe, lakini uongozi wake ulikuwa ni wa aina yake.“Alikuwa mpole na imara kwenye maamuzi na kwa nyakati tofauti alikuwa akiamini zaidi nguvu ya hoja na kufanya kazi kwa bidii, kitu ambacho kiliashiria uongozi uliotukuka,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Kofi Annan kuongoza Kituo cha Makazi Duniani (UN-Habitat).Profesa Tibaijuka ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Muleba Kusini mkoani Kagera (CCM), aliombwa na Annan kuongoza Kituo cha Makazi Duniani (UN-Habitat) ambapo alifanya hivyo kati ya mwaka 2006 mpaka 2010.Kofi Annan ni nani?Kofi Atta Annan na dada yake Efua Atta, walizaliwa kwenye mji wa Kumasi katika nchi ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Gold Coast, Aprili mwaka 1938. Majina ya pacha hao yalimaanisha kuwa walizaliwa Ijumaa huku majina yao ya kati yakimaanisha kuwa walikuwa ni pacha.Annan alikulia kwenye familia ya kitajiri - mababu zake walikuwa ni viongozi wa kitamaduni na baba yake alikuwa ni gavana wa mkoa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa ukoloni wa Uingereza Siku mbili tu kabla ya Kofi kufikisha miaka 19, Gold Coast ilipata Uhuru wake na kuitwa Ghana.Baada ya kusoma chuo kikuu, kwanza kwenye nchi iliyokuwa imepata uhuru ya Ghana, na baadaye huko Macalester College nchini Marekani, Annan alipata ajira yake ya kwanza kwenye Umoja wa Mataifa.Alianza kazi kama Ofisa wa Bajeti kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 1962 na ndani ya miongo minne akahudumu UN wakati aliipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Saba mwaka 1996, akiwa ni Mwafrika Mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo na mtu wa kwanza kutoka ndani ya UN yenyewe.Alihudumu kwa mihula miwili.Mpigania amani Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa ambaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.Muhula wa Annan kama Katibu Mkuu wa UN ulikumbwa na vita vya Iraq na janga la Virusi Vya Ukimwi.Katika salamu zake za rambirambi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ambaye mwaka 2007, Annan alijitosa kuongoza usuluhishi wa mgogoro wa uchaguzi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na baadaye kusaini mkataba wa amani, alimwita Annan “mtu ambaye alijitosa na kuiokoa nchi yetu isianguke.”Rais Vladimir Putin wa Urusi alisema kumbukumbu ya Annan “itabaki daima katika mioyo ya Warusi.”Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alisema “dunia siyo tu imepoteza mwanadiplomasia mahiri wa Afrika na mwenye kupenda masuala ya kibinadamu, lakini mlinzi wa amani na usalama wa dunia.”Akitangaza wiki ya maombolezo ya kitaifa, Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo alimwita Annan “mmoja wa Waghana wenye weledi.”Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema, “masikitiko kwa taarifa za kifo cha Kofi Annan. Kiongozi mahiri na mwanamageuzi wa UN, ametoa mchango mkubwa kuifanya dunia anayoiacha kuwa sehemu bora kuliko ile aliyozaliwa. Fikra na salamu zangu za rambirambi
kitaifa
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imesema inatarajia kuanzisha huduma ya vituo vya mafuta vinavyotembea (Mobile Pump Station) kwa kutumia magari maalumu yaliyotengenezwa kwa kazi hiyo.Akizungumza na HabariLeo jana, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Ewura, Titus Kaguo alisema kwa sasa wataalamu wanatengeneza matangi na namna ya kuyaweka kwenye vifaa vitakavyobeba matangi hayo. “Mshauri Mwelekezi ambaye ni Bico na UDSM (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) akimaliza ndiyo tutajua lini mradi huu utaanza na gharama zake,” alisema Kaguo.Alisema mradi huo unalenga kupambana na uuzaji wa mafuta katika chupa vijijini na nje ya miji. Kaguo alisema hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa nishati ya mafuta na kusisitiza kuwa nishati ya mafuta inatakiwa kuuzwa kwa utaratibu unaokubalika na kwa kuwa kujenga visima vikubwa ni gharama, wameona njia hiyo ni bora na itakuwa ni rahisi kuwafikia wateja wengi.Alisema katika maeneo mengi hapa nchini, wafanyabiashara wadogo wamekuwa wakisafirisha na kuuza mafuta kwa njia ambazo si sahihi na zinazohatarisha usalama wa vyombo vya watumiaji pamoja na maisha yao na kutolea mfano hasa maeneo ya vijijini ambako hakuna vituo vya mafuta.“Hata hivyo, Ewura tumejitahidi kukomesha tatizo la uchakachuaji wa mafuta ambalo lilikuwa limekithiri siku chache zilizopita, lakini sasa limekwisha baada ya kutumia njia ya vinasaba vya rangi pamoja na pia kwa kupitia uagizaji wa mafuta kwa pamoja katika meli moja,” alisema Kaguo. Alishauri watumiaji vya vyombo vya moto kuacha kujaza mafuta katika vyombo vyao wakati wa mchana kwa kuwa kiasi fulani cha mafuta hupotea kwa njia ya mvuke na kusababisha malalamiko ya kupunjwa mafuta na wahudumu au wamiliki wa vituo.
kitaifa
 TURIN, ITALIA  KWA mujibu wa taarifa kutoka ndani ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus, wamedai kuwa staa wao Cristiano Ronaldo alitakiwa kuripoti kikosini jana kwa ajili ya kujiunga na wachezaji wenzake.  Mchezaji huyo alikuwa nyumbani kwake nchini Ureno kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona tangu Machi mwaka huu, lakini uongozi wa timu yake umewataka wachezaji wote wa kigeni kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kumalizia msimu huu.  Ronaldo alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kigeni ambao waliruhusiwa kurudi kwao, hivyo jana mchezaji huyo alikuwa anasubiriwa kwenye kiwanja cha ndege.  Hata hivyo mchezaji huyo baada ya kuwasili nchini Italia atatakiwa kukaa karantini kwa wiki mbili kwa ajili ya kuangaliwa kama atakuwa na maambukizi yoyote ya virusi hivyo vya corona, hivyo Ronaldo ataungana na wachezaji wenzake katikati ya Mei.  Waziri mkuu nchini Italia, Giuseppe Conte, ameliwashia taa ya kijani shirikisho la soka nchini humo kuendelea na ratiba zao huku wakizitaka timu kuanza kufanya mazoezi Mei 4 mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na kumalizia msimu huu.  “Tunaamini ligi itaendelea kama kawaida endapo mambo yatakwenda vizuri, tunajua kila kitu kitakuwa sawa siku za hivi karibuni,” alisema waziri huyo.  Italia ni moja kati ya taifa ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na virusi vya corona tangu vilipogundulika Desemba mwaka jana huko nchini China.  Hadi sasa Italia ina jumla ya maambukizi ya watu 199,414, huku jumla ya watu 26,977 wakipoteza maisha na wengine 66,624 wakipona. Kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanazuia maambukizi mapya. 
michezo
Na Gurian Adolf-Sumbawanga WAKULIMA wa mpunga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, wameshauriwa kutumia mbegu mpya ya mpunga aina ya SARO 5 TXD-306 ili wanufaike na zao hilo. Hayo yalibainishwa na Ofisa Ufundi na Elimu wa Taasisi ya BRENT, Faustina Kalyalya anayetoa mafunzo ya kilimo bora cha mpunga kwa wakulima.   Akizungumza katika shamba darasa katika Kijiji cha Milepa wilayani humo, alisema taasisi hiyo ilianzishwa wilayani humo zaidi ya miaka mitano iliyopita ikiwa  na lengo la  kutoa elimu kwa wakulima katika suala zima la  kilimo bora sambamba na kuongeza  thamani katika mazao yao. Alisema wakulima wa mpunga wilayani humo bado wanalima kilimo cha kizamani na kwa kutumia mbegu za kizamani bila kufuata  taratibu  za kilimo bora, hali ambayo inawasababisha kutopata tija  katika kilimo wanacholima. Kalyalya alisema lengo kubwa la  kutoa elimu kwa wakulima hao ni kuona wanafanikiwa ambapo ni matarajio ya tasisi hiyo kuwa kila mkulima aweze kuvuna kwa kiwango cha gunia 40 za mpunga, hali ambayo itawawezesha kuona faida katika kilimo wanacholima. Naye Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Sumbawanga, Habona Kwileluya, alisema iwapo wakulima hao wakitumia mbegu ya mpunga aina  ya SARO 5 TXD-306 ambayo inaonekana kufanya vizuri katika bonde  hilo, watanufaika vizuri kwani asilimia kubwa ya wakazi wa bonde  hilo ni wakulima wa mahindi pamoja na mpunga.   Alisema ni vizuri wakulima wakafuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo waliopo katika maeneo yao, ikiwa  ni pamoja na kulima  kwa wakati na matumizi ya pembejeo za kilimo tofauti na hivyo wasitegemee muujiza wa kupata mafanikio katika kilimo.   Mmoja wa wakulima anayepata mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Brent, Isaya Katepa, alisema tatizo lililopo hususani katika mafunzo kwa vitendo ni wakulima kutotaka kwenda kushiriki katika shughuli za mashamba darasa wakidai kuwa wao wanalima mashamba yao binafsi kwa hiyo hawana muda wa kwenda kulima katika mashamba darasa ambayo yameandaliwa kwa ajili ya mafunzo. Katika msimu wa kilimo unaoisha hivi sasa, Brent imeanzisha mashamba darasa katika vijiji  vya Ng'ongo, Kaoze, Ilemba, Sakalilo na Milepa,
kitaifa
KIGALI, RWANDA MWANAMUZIKI maarufu nchini Rwanda, Ngabo Medard Jobert maarufu kama Meddy, amelazimika kusitisha ziara yake ya kimuziki katika nchi jirani ya Burundi kwa sababu za kiusalama. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa, RFI, imesema mwanamuziki huyo alitarajiwa kuwaburudisha wafuasi wa muziki wake jijini Bujumbura mwishoni mwa wiki hii, na sasa ziara hiyo kwa mujibu wa meneja wake, itafanyika wakati mwingine. Taarifa hiyo imeoneza kuwa uamuzi wa mwanamuziki huyo umechangiwa na hali iliyopo sasa ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili kuwa mbaya hivyo kuzua hofu  za kiusalama. Serikali ya Bujumbiura inawatuhumu viongozi wa Rwanda hususani Rais Paul Kagame mwenyewe kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kufanya kila wawezalo ili kumuondoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Madai ambayo Rwanda imetupilia mbali na kusisitiza kuwa tuhuma zinazotolewa na serikali ya Burundi ni mbinu za kutaka kujihusisha na mauaji ya kimbari dhidi ya wapinzani wake. Zaidi ya raia wa Burundi 250,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwezo Rwanda, kufuatia kuzuka kwa machafuko na mivutano ya kisiasa nchini Burundi. Machafuko nchini Burundi yalianza mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka 2015 kufuatia hatua ya Pierre Nkurunziza ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu. Licha ya kutekelezwa jitihada za kimataifa kwa minajii ya kuhitimisha mgogoro wa Burundi, lakini juhudi hizo hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda.
kimataifa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameitaja mikoa 11 iliyoanzisha mabaraza ya biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu, lakini utendaji wa mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.Ameitaja mikoa hiyo 11 ambayo mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, Shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya.Aidha, amebainisha kuwa mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Namba Moja wa Mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.Alizungumza hayo wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma. Aifafanua kuwa dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa serikali na sekta binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio mhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa, lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji,” alisema.
kitaifa
KAMISHNA Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Anna Makakala amepewa salamu za heshima kutoka kwa mataifa mbalimbali kwa kuindoa Tanzania kuwa uchochoro wa vitendo vya rushwa na kupitisha dawa za kulevya kwenda Ulaya.Nchi zilizotoa pongeza na kumpa heshima kwa kutambua mchango wa Kamishna Makakala ni China, Marekani, India, Ujerumani, Uingereza na Saudi Arabia. Salamu hizo za heshima zilitolewa Dra es Salaam juzi kwenye kongamano la viongozi wa dini lililoandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini na kushirikisha wajumbe 437 kutoka mikoa yote ya bara na visiwani.Aidha wajumbe kutoka mataifa hayo akiwemo Profesa Yi gen kutoka China, Dk Brooks Lasmax wa Ujerumani , Shehe Dk Syudih Muhmed wa Saudia Arabia, Askofu Owen kennedy kutoka Marekani, Mchumi George Frank kutoka Uingereza na Dk Surani Snjaly wa India walisema kwa nyakati tofauti kuwa mabadiliko chanya katika masuala ya uhamiaji sio tu yamesaidia kwa asilimia kubwa kupungua kwa biashara ya dawa za kulevya nchini Marekani na Ulaya lakini imeiletea heshima Tanzania kwa kutokuwa tena barabara ya kupitisha dawa za kulevya.Walidai kuwa siku za zamani wakiwa wageni waliokuwa wakipita mara kwa mara na kuingia Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA), maofisa uhamiaji walikuwa wanapokea mgeni kwa kumuuliza atampa dola ngapi kabla hata hajafanya ukaguzi na walikuwa wakipewa Dola za Marekani 100 mgeni hakaguliwi kabisa lakini sio sasa.Dk Surajy walimwagia sifa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa kuigeuza idara hiyo kuwa chombo cha heshima kwa nchi mbalimbali na kuongeza kuwa hivi sasa raia wa India wanatamani kuja Tanzania kujifunza njia rahisi ya kuondoa rushwa.
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na mawaziri na makatibu wakuu kwenye eneo la tanki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba badala ya Ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja. Alitoa agizo hilo jana mchana akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na naibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko kilometa 17 kutoka jijini Dodoma.“Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” alisisitiza. Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapa mrejesho mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo juzi alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara.“Nataka mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” alisema Waziri Mkuu. Aliwataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iende haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri.Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni Magereza,” alisema. Wakati huohuo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alimweleza Waziri Mkuu kuwa kuna wagongaji wa kokoto ambao wamepokea fedha, lakini wakaamua kufunga machimbo yao kwa sababu ya sikukuu. “Waziri wa Madini aongee nao hawa watu ili warejee na kufanya kazi kwa sababu baadhi yao wameshapokea fedha na mahitaji ya kokoto hapa ni makubwa na aliyebakia akifanya kazi ni Nyanza Road Works peke yake,” alisema.Naye Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imetoa transfoma tisa za kusaidia kupoza umeme, lakini ni wizara nne ambazo zimejitokeza na kulipia laini za transfoma hizo. “Wizara yetu tumetoa transfoma tisa za kusaidia umeme upatikane eneo la ujenzi. Niwaombe mawaziri waliopo, walipie service line tu ambazo gharama yake ni shilingi 921,000 ili wafungiwe transfoma na kazi iweze kufanyika mchana na usiku. Hadi sasa, tumeshapokea maombi kutoka wizara nne tu za Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Elimu na Nishati ili kazi imalizike ndani ya muda mfupi,” alisema Dk Kalemani.
kitaifa
NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM SERIKALI inatarajia kupeleka bungeni Muswada wa Sheria wa kushusha umri wa kuridhia vijana kupata huduma za Ukimwi bila ridhaa ya wazazi kutoka miaka 18 hadi 15 ili kupunguza wimbi la maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa vijana. Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Taifa ya Kuthibiti Ukimwi nchini (TACAIDS)), kubainisha kuwa kwa siku zaidi ya watu 200 hupata maambukizi mapya ya VVU, huku kati yao 80 wakiwa ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24. Kauli hiyo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile wakati akizindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za Ukimwi nchini. Dk. Ndugulile amesema tatizo la ugonjwa wa Ukimwi linabadilika kila mara hivyo kuchangia zaidi ya asilimia 40 ya vijana kuathiriwa huku asilimia 80 ya vijana hao wakiwa ni vijana wa kike. “Serikali tumeanza kuliona hilo na kuchukua hatua, hatua ya kwanza ni kushusha umri wa kuridhia kwani ni kweli vijana wanaanza kujamiiana wakiwa umri wadogo, takwimu zinaonesha kuanzia  wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 19, asilimia 27 ni wajawazito au wana watoto. “Kwa hali hii ya maambukizi tumeamua kupeleka muswada bungeni kushusha umri wa ridhaa hadi miaka 15. Ili sasa iweze kuruhusu kijana kuweza kupata huduma, kwa sababu kwa sasa inabidi apate ridhaa ya mzazi au mlezi,” amesema Dk. Ndugulile. Aidha, amesema wizara hiyo italeta mpango wa kuruhusu watu kujipima wenyewe ili kutoa motisha kwa akina baba kupima VVU. “Kama ilivyo kwa wanawake wanavyojipima ujauzito na kina baba watahamasika kujipima na naamini litawapa motisha,” amesema. Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dkt. Leonard Maboko amesema muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utasaidia vijana kupata huduma za Ukimwi kwa haraka bila ridhaa ya mzazi au mlezi kama ilivyo sasa. Amesema hadi sasa Tanzania inao watu milioni 1.5 wenye VVU ambao ni sawa na asilimia 4.7. “Lakini maambukizo mapya yamepungua kutoka 80,000 miaka mine iliyopita hadi 72,000. Katika kundi hili watanzania 6000 wanapata maambukizo mpaya kwa mwezi na kwa siku ni 200,” alisema. Aidha, amesema sababu za vijana kupata maambukizo zaidi ni kutoka kwenye utoto kwenda kwenye ujana. “Hawajapata elimu sawasawa hivyo inakuwa rahisi kwake kufanya maamuzi ambayo hana taarifa za kutosha. Lakini pia vijana wa kike kutaka kupata vitu kwa haraka. “Ndio maana tuna miradi ambayo inagusa kaya maskini kwa kuwasaidia kupata elimu ya ujasiriamali katika mikoa mitatu,” alisema. Kutokana na tatizo hilo Makamu wa Rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo alisema kwa mwaka huu katika kampeni hiyo ya kuchangia afua za Ukimwi wamelenga kukusanya Sh bilioni mbili. Hata hivyo, alisema hadi sasa tayari wamekusanya zaidi ya Sh bilioni 1.5 sawa na asilimia 67 ya lengo la kampeni hiyo ya mwaka huu ambayo sasa inatimiza miaka 17 tangu kuanzishwa kwake.Alisema tangu kuanzishwa kwa Kilimanjaro Challenge, zimekusanywa zaidi ya Sh bilioni 13 ambazo zimenufaisha asasi na taasisi mbalimbali 50 zinazoshughulikia masuala ya Ukimwi.
afya
SERIKALI imeeleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika wilaya ya Singida hali ambayo aligoma kushiriki uwashaji umeme katika baadhi ya vijiji.Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameagiza uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Singida kumsimamia kwa karibu mkandarasi, Eterne Consortium ya China.Mgalu ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuzindua uwashaji na usambazaji umeme , aliikamilisha katika vijiji vya Ibaga na Nkinto wilayani Mkalama lakini wilayani Singida, alisusa kuwasha umeme katika vijiji vya Idd Simba na Maghojoa .“Leo siwezi kuwasha umeme kwa mtu mmoja wakati wananchi wote hawa pia wanastahili kupata huduma kama hii, bali nitakagua tu. Sipendezewi kamwe na kasi ya utekelezaji wa mradi huu katika wilaya hii,” alisema Naibu Waziri akiwa kijiji cha Maghojoa.Alisisitiza, “Hapa mkoani na kwenye kanda kuna watu wanaopaswa kuona kazi hii ikifanyika kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa, lakini sivyo ilivyo. Hivi hadi aje waziri ndio kazi ifanyike? Hebu nyie watu wa Tanesco simamieni kasi ya utekelezaji wa mradi huu vinginevyo mtakuja niona mbaya mradi ukilegalega naondoka nanyi.”Aliagiza mamlaka zote zinazopeleka miradi vijijini kuhakikisha zinashirikiana na viongozi wa serikali za vijiji wananchi waone miradi hiyo ni yao hivyo washiriki kuisimamia na kuilinda kikamilifu.Aliwasihi wananchi kujiepusha na vitendo vya uhujumu wa miundombinu ya umeme ili kumnyima mkandarasi sababu ya kutoa visingizio vya kuchelewa kutekeleza miradi kwa wakati uliopangwa.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha alimweleza Naibu Waziri kuwa kasi ya utekelezaji mradi huo ulioanza Mei mwaka huu, ni ndogo hali inayofanya waamini kuwa mkandarasi huyo mpya hana tofauti na wa awali aliyenyang’anywa zabuni kutokana na kushindwa kufanya kazi hiyo ipasavyo.Akikabidhi mradi huo Desemba 21, mwaka jana katika Kijiji cha Mjughuda, wilayani humo, kwa mkandarasi mpya baada ya yule wa zamani kusitishiwa mkataba wake, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alimtaka kuhakikisha hakuna nyumba, shule, taasisi wala mitambo ya maji inayorukwa kwa sababu yoyote ile.
kitaifa
Addis Ababa, Ethiopia Kiongozi wa Jeshi la nchini Ethiopia, Jenerali Seare Monnen, ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema mkuu huyo na ofisa mwingine walipoteza maisha katika mji wa Amhara wakijaribu kuzuia mapinduzi dhidi ya utawala nchini humo. Mjini Ahmara kwenyewe, gavana wa mji huo Ambachew Mekonnen aliuawa pamoja na mshauri wake. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni. Waziri mkuu alikwenda kwenye kituo cha Televisheni akiwa na mavazi ya kijeshi kukemea mashambulizi hayo. Tangu uchaguzi wa mwaka jana, Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maofisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu. Marekani imewatahadharisha wafanyakazi wake mjini Addis Ababa kutotoka nje, ikisema ina taarifa kuhusu mashambulizi ya risasi siku ya Jumamosi. Jenerali Seare aliuawa sambamba na Jenerali mwingine, Gezai Abera, na mlinzi ambaye sasa anashikiliwa, ofisi ya habari ya waziri mkuu imeeleza. Mjini Amhara gavana aliuawa sambamba na mshauri wake mkuu Ezez Wasie, huku mwanasheria wa mji huo akijeruhiwa. Lake Ayalew ameteuliwa kuwa gavana mpya wa mji huo. Ofisi ya waziri mkuu imemshutumu mkuu wa usalama wa mji wa Amhara, Asaminew Tsige, kwa kupanga mapinduzi. Haijajulikana kama amekamatwa. “Jaribio la mapinduzi mjini Amhara ni kinyume cha katiba na chenye nia ya kuharibu amani ya eneo hilo,” ofisi hiyo ilieleza katika taarifa yake na kuongeza: “Tukio hili linapaswa kukemewa na raia wote wa Ethiopia na Serikali ina uwezo wa kupambana na kundi hili lenye silaha.” Wakazi wa makao makuu ya mji wa Amhara, Bahir Dar, waliripoti kusikia milio mikubwa ya risasi. Hiki ni kipindi kigumu kwa Ethiopia na waziri mkuu Abiy, ambaye anakabiliwa na mizozo ya wenyewe kwa wenyewe. Kiongozi wa kijeshi, Seare Mekonnen alitumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja baada ya kuteuliwa na waziri Abiy, ambaye alifanya mabadiliko kwenye idara ya usalama alipoingia madarakani mwezi Aprili mwaka jana. Ni wazi kuwa waziri mkuu anakabiliwa na upinzani kutoka ndani ya jeshi ambao wanapinga mtindo wake wa utawala. Kuuawa kwa gavana wa Amhara ambaye alikuwa mshirika muhimu kwenye mji huo pia ni pigo kubwa kwa waziri mkuu Abiy, mji ambao wenyewe unakabiliwa na changamoto za kiusalama na vurugu za baadhi ya makundi. Uchaguzi wa kwanza tangu bwana Abiy aingie madarakani unapaswa kufanyika mwakani lakini ni vigumu kuona namna gani hili jambo linafanikiwa kwenye nchi ambayo usalama wake ni mdogo. Hali ya kisiasa ni mbaya sana. Ardhi ya jamii ya Amhara ni mji wa pili wenye watu wengi na umeipa Ethiopia lugha ya taifa hilo, Amharic. Mapigano kati ya jamii ya Amhara na Gumuz iligharimu maisha ya watu mwezi uliopita mjini Amhara na mji jirani wa Benishangul Gumuz. Mapigano kati ya jamii hizo yalisababishwa na migogoro ya ardhi, takribani watu milioni tatu walikimbia makazi yao. Suala jingine ambalo waziri mkuu anapaswa kukabiliana nalo ni kutokuwepo kwa hali ya utulivu ndani ya jeshi.
kimataifa
MADRID, HISPANIA KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Hispania, Luis Enrique, ameahidi kufanya mambo makubwa, ikiwamo kukisuka upya kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Enrique, ambaye alikuwa kocha wa Barcelona, amechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa Hispania, Fernando Hierro, ambaye alifukuzwa baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Urusi. Hierro alikuwa kocha wa muda baada ya kocha aliyefanikiwa kuivusha timu hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, Julen Lopetegui, kufukuzwa siku chache baada ya kukubali kujiunga na klabu ya Real Madrid. Katika michuano hiyo nchini Urusi, Hispania ilishinda mchezo mmoja wa makundi dhidi ya Iran na baadaye kuondolewa na Urusi katika hatua ya 16 bora. “Hayatakuwa mapinduzi, haya ni mageuzi. Kwani unaweza kubadilisha mtindo wa kucheza bila kubadilisha kitu kingine, kama nilivyoonyesha nikiwa Barcelona. “Soka ni mageuzi endelevu na tuna wazo la kufanya hivyo. Tunaweza kucheza soka nzuri, kuwa na nguvu, kudhibiti mpira na kuwaumiza wapinzani wetu.Kuna vitu tunahitaji kuboresha, pia,” alisema Enrique. Enrique, ambaye aliwahi kuwa kocha wa Barcelona kati ya mwaka 2014 na 2017 na kushinda mataji mawili, likiwamo Ligi Kuu ya Hispania na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2015, pia aliongeza kuwa, atachagua wachezaji  wenye viwango na aina ya uchezaji wao, lakini si wenye majina makubwa. “Naona kama nachelewa kutangaza kikosi changu cha kwanza, kitawashangaza wengi, nina uhakika, kikosi cha awamu ya kwanza kitakuwa na wachezaji kama 70. “Wachezaji wengi miongoni mwao hawatakuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza na sitazungumza na mchezaji yeyote,” alisema. Miongoni mwa kazi yake ya kwanza kocha huyo itakuwa kumshawishi beki Gerard Pique kuacha mpango wake wa kustaafu soka la kimataifa, baada ya kuahidi kufanya hivyo wakati michuano ya Kombe la Dunia itakapomalizika. “Pique ni shughuli maalumu, kwani miaka miwili iliyopita alitangaza kujiuzulu. Napenda kuwa na wachezaji wote, akiwamo beki huyo, ameonyesha kuwa na kiwango kizuri, hata hivyo unatakiwa kuheshimu mawazo ya wengine,” alisema.
michezo
Mechi hiyo ni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake ambapo waamuzi wanatoka Ethiopia.Akizungumza na wachezaji hao kambini kwao Karume, Ilala jana, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alisema fedha hizo zimetoka kwa wadau mbalimbali wa soka.“Februari 12 nilikuja kuwatembelea hapa kambini, katika changamoto mlizoniambia zinawakabili ni upungufu wa fedha sasa nimetafuta fedha kutoka kwa watu mbalimbali nimepata Sh milioni 15,” alisema.“Katika hizo fedha kuna mdau mmoja ambaye hataki tumtangaze ametoa Sh milioni tatu, mwingine ni kampuni ya maziwa ya Asas imetoa Sh milioni mbili na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa Sh milioni 10,” alisema.Akizungumzia mchanganuo wa fedha hizo Wambura alisema endapo timu itashinda mechi ya keshokutwa kila mchezaji atapata Sh 300,000 na endapo itashinda mechi ya marudiano Zimbabwe kila mchezaji atapata kiasi kama hicho cha fedha.“Endapo mtashindwa kufunga basi fedha zitapewa uongozi na kufanyia shughuli nyingine,” alisema Anastazia na kuwataka wachezaji kushinda siku hiyo.Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema yanaendelea vizuri na kutaja viingilio katika mechi hiyo ni Sh 3,000 na Sh 2,000. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Cameroon baadaye mwaka huu.Twiga Stars ilishawahi kufuzu fainali hizo mwaka 2011 zilipofanyika Afrika Kusini.
michezo
Arodia Peter, Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendelo ya Jamii, imeishauri Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu (TCU) kuweka fedha za kujikimu za wanafunzi moja kwa moja kwenye akaunti zao binafsi ili kuepuka changamoto zinazojitokeza. Akisoma hotuba ya Kamati hiyo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, bungeni leo Aprili 29, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nkamia amesema wanafunzi wamekuwa wakichelewa kupata fedha za kujikimu kutokana na changamoto mbalimbali zinazokabili vyuo vyao na baadhi ya benki nchini. Amesema kutokana na baadhi ya vyuo kuwa na madeni ya mikopo benki, fedha za kujikimu za zimekuwa zikizuiwa na hivyo kusababisha hali ngumu kwa wanafunzi. Nkamia ambaye pia ni Mbunge wa Chemba,(CCM) amesema Kamati imeshauri serikali kuhakikisha inaboresha maslahi ya wahadhili na watumishi wa vyuo vikuu, hususani posho ya nyumba ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. “Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imebaini kuna changamoto ya wahadhili na watumishi wa vyuo vikuu hivyo kusababisha baadhi yao kuzuia matokeo ya mitihani ya wanafunzi, hivyo kamati inaona kuna hatari ya kutokea mgomo baridi,” ‘amesema Nkamia.
kitaifa
Manchester United wamekubali kulipa ada ya pauni milioni 55 kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Record) Hata hivyo madai hayo yamekanushwa huku vilavu hivyo vikiendelea kushauriana kuhusu usajili wa kiungo huyo. (Mail) Chelsea inapania kumuajiri kocha wa Derby Frank Lampard, kama maneja wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu kufikia mwisho wa wiki hii. (Standard) Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amekuwa akitafuta nyumba mjini Barcelona,licha ya tetesi kuibuka kuwa nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 anajiandaa kurejea Nou Camp. (Sport) Bayern Munich wanajiandaa kujiunga na Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Rodri, 22, kutoka Atletico Madrid. (AS – in Spanish) Kiungo wa kati wa Brazil Jorginho yuko tayari kuondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus mwaka mmoja baada ya kusajiliwa na Napoli kwa kama cha pauni milioni 50. (Mirror) Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kusajili beki wa England anaechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail) Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror) Arsenal inapania kusaini beki wa Celtic raia wa Uskochi Kieran Tierney, 22, msimu ujao. (Mail) Sporting Lisbon wanashauriana na Liverpool kuhusu usajili wa winga wa Ureno wa miaka 19, Rafael Camacho. (Standard) Norwich wanamatumaini ya kumnunua beki wa England Max Aarons, 19, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Manchester United. (Telegraph) West Ham wameifahamisha Manchester United na Manchester City kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota wa Kimataifa wa England anaecheza safu ya kati Declan Rice, 20, msimu huu wa joto. (Sky Sports) Arsenal wanajianda kuweka dau la kumnunua winga wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai, 18. (Football Insider) Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley. Kipa huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 33 ataingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa katika uwanja waTurf Moor mwezi ujao. (Guardian) Tetesi Bora Jumatano Paris St-German wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar mwenye umri wa miaka 27 msimu huu. (ESPN) Real Madrid huenda wakamjumuisha kiungo wa kati Mbrazil Casemiro, 27, kwa ofa yoyote ya kusaini Neymar kutoka PSG. (Marca) Manchester United wanataka Paul Pogba asiondoka katika klabu hiyo lakini akubali kuwa hali inaweza kubadilika waamue kumuuza nyota huyo wa Kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 . (Sky Sports) Huku hayo yakijiri Real Madrid, wameonywa na rais wao wa zamani, Ramon Calderon kutomsajili Pogba. (Sun) Manchester United watalazimika kulipa hadi pauni milioni 75 wakitaka kumsajili mlinzi Mfaransa Issa Diop,22 kutoka West Ham, baada ya Red Devils kukataa pendekezo la Hammer la kubadilishana wachezaji katika mkataba utakao mhusisha mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23. (Mirror) Everton wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, kutoka Barcelona kwa pauni milioni 22. (Mail) Ajenti wa Gareth Bale amepuuziliambali madai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid wa miaka 29 huenda akahamia Bayern Munich kwa mkopo. (Mirror)
michezo
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameutaka uongozi wa Kiwanda cha Kutengeneza Magunia ya Mkonge cha TPM (1998 LTD ) mkoani Morogoro, kutotekeleza mpango wake wa kusitisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa soko la bidhaa zao, kwa kuwa tayari serikali imeshaanza kuzitatua changamoto hizo.Waziri Kakunda amesema hayo juzi mjini Morogoro baada ya kukutana na uongozi wa kiwanda hicho na kusomewa taarifa na Maneja Mwandamizi wa MeTL anayeshughulikia uzalishaji wa magunia pamoja na mashamba ya Mkonge, Ndekirwa Nnyari, kuhusu changamoto za muda mrefu zinazokikabili kiwanda hicho.Kakunda amesema serikali inathamini mitaji inayowekezwa na wawekezaji katika viwanda na pia ina jukumu la kulinda mitaji yao isipote bure, kuwalinda watu wanaozalisha ajira zinazowanufaisha Watanzania wengi pamoja na kuiingizia mapato serikali.“Uongozi wa kiwanda andikeni barua niipate Jumatatu (leo) ikielezea changamoto zilizopo, maandiko haya yaandikwe kitaalamu,” amesema.Baada ya kufikishwa kwake atakutana na kamati ya uchumi na fedha ya Baraza la Mawaziri iweze kuona ni namna gani ya kusaidia kuzitatua changamoto za muda mrefu ikiwemo ya uingizwaji wa magunia ya jute kutoka nchi za barani Asia na kuuzwa kwa bei ya chini.Waziri Kakunda amesema yapo mahitaji makubwa ya ndani ya magunia kwa kiwango cha zaidi ya milioni 20 na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza uzalishaji mkubwa kwani uwezo wa kiwanda hicho ni kuzalisha magunia milioni 10 kwa mwaka.
uchumi
MADRID, HISPANIA WADAU na wapenzi wa soka nchini Uingeraza, watashindwa kuangalia mchezo wa El Clasico kati ya Barcelona ambao watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Real Madrid. Inadaiwa kwamba, mchezo huo wa kwanza kuikutanisha miamba hiyo msimu huu utapata nafasi ya kutazamwa moja kwa moja jumla ya nchi 100, lakini watu wa nchini Uingereza watakosa nafasi hiyo kutokana na muda ambao umepangwa mchezo huo kuchezwa. Mchezo huo umepangwa kupigwa saa 3:15 mchana, wakati sheria za soka nchini Uingereza zinadai kuwa ni ruksa kuonesha mchezo moja kwa moja kuanzia saa 2:45 na saa 5:15 kwa siku ya Jumamosi ambapo mchezo huo utapigwa. Kutokana na hali hiyo, Uingereza watashindwa kuutazama mchezo huo moja kwa moja (live) na badala yake watatazama matukio yatakayojiri katika mchezo mara baada ya kumalizika. Inasemekana kuwa Chama cha Soka nchini England (FA) na ligi kuu, waliwahi kukaa na kujadili juu ya sheria hiyo huku wakiwa na maana kwamba kuwafanya mashabiki nchini England wajitokeze kwa wingi viwanjani. Kwa hali hiyo mashabiki wa nchini Hispania, USA, China na mataifa mengine watafurahia mchezo huo kuutazama moja kwa moja. Inasemekana kuwa mwaka 2014, mashabiki ambao walikuwa wanaangalia soka kupitia Sky Sports, walishindwa kumuona mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez, katika dakika 15 za mwanzo kutokana na sheria hiyo kuwabana watu wa nchini Uingereza. Sheria hiyo ilipangwa tangu mwaka 1960, huku wakiwa na lengo la kukusanya mashabiki wengi viwanjani badala ya kuutazama mchezo katika televisheni. Sheria hiyo iliwekwa na mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Burnley, Bob Lord, ambapo alidai kuwa muda kama huo unawafanya mashabiki kubaki majumbani kuutazama mchezo badala ya kwenda uwanjani siku hiyo ya Jumamosi hivyo pato linakuwa dogo.
michezo
PATRICIA KIMELEMETA, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) leo linatarajia kuweka hadharani deni la Sh bilioni 121 inazowadaiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya Rais John Magufuli kuliagiza shirika hilo kuikatia umeme SMZ  baada ya kushindwa kulipa deni hilo   kwa ajili ya kusambaza umeme visiwani humo. Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa kuweka jiwe la msingi katika kituo cha kupooza umeme wa kilovoti 132 kilichopo Mtwara. Alikuwa  kwenye ziara ya siku nne ya mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, wiki iliyopita.   Ofisa Habari na Uhusiano wa Tanesco, Leyla Muhaji amesema  shirika  haliwezi kuficha suala hilo kwa sababu tayari Rais Magufuli amelizungumzia.  Alisema  uongozi wa shirika hilo umepanga kutoa mchanganuo wa deni hilo tangu lilipoanza hadi lilipofikia wananchi waweze kulielewa. “Hatuwezi kuficha deni la Zanzibar kwa sababu tayari Rais Magufuli ameliweka wazi. “Mimi na viongozi wangu tutajipanga tuweze kutoa mchanganuo wa deni lenyewe tangu lilipoanza hadi lilipofikia, kwa sasa tupo safarini lakini kesho(leo), tutakuwa ofisini,”alisema Muhaji. Alisema wataandaa taarifa hiyo ambayo itatolewa kwa waandishi wa habari waweze kuwahabarisha wananchi.   Rais Magufuli alisema   suala la umeme lisigeuzwe kuwa la siasa. Alisema wadaiwa sugu wa umeme wakatiwe umeme kwa vile  shirika hilo halipo kisiasa bali kwa utendaji, hivyo   wadaiwa sugu wote wanapaswa kulipa madeni hayo na   watakaoshindwa wakatiwe umeme hata kama ni Ikulu. Alisema Tanesco inapaswa kufuatilia madeni yake popote kwa sababu wakati mwingine fedha zinakuwa zinatolewa wizarani lakini wanaona umeme siyo muhimu.
kitaifa
Gurian Adolf -Sumbawanga WAKAZI 540 wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wamezikimbia nyumba zao baada ya Ziwa Tanganyika kujaa maji na kusababisha mafuriko katika vijiji viwili vilivyopo katika wilaya za Nkasi na Kalambo. Walikuwa wakiishi katika nyumba 108 zilizojengwa maeneo ambayo awali maji ya Ziwa Tanganyika yalikuwa yakifika kwenye vijiji vya Kipwa wilayani Kalambo na Kirando wilayani Nkasi ambapo kwa zaidi ya miaka 30 yalikauka na watu hao wakajenga makazi. Miundombinu mingine iliyofurika maji ni pamoja na mwalo wa samaki na gati katika Kijiji cha Kirando na gati jingine lililopo katika Kijiji cha Kipili wilayani Nkasi. Soko la kisasa la samaki lililopo katika Kata ya Kasanga wilayani Kalambo nalo limefurika maji na shughuli za kibiashara zimesimama. Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura, alisema mafuriko hayo yalikikumba Kijiji cha Kipwa miaka 23 iliyopita wakati wa mvua za El-nino za 2017/18. “Nyumba zote 90 za Kijiji cha Kipwa zimefurika maji baada ya Ziwa Tanganyika kujaa na kufika yalipokuwa awali, familia za watu 400 hazina makazi, wamepoteza kila kitu walichokuwa wakimiliki, taasisi mbili za umma ambazo majengo yake hayakuathirika ni shule ya msingi na zahanati tu,” alisema Julieth. Akifafanua zaidi aliongeza kuwa baadhi ya watu wamehifadhiwa katika vyumba vya madarasa ya shule ya msingi huku wengine wakiwa wamekimbilia kwenye maeneo ya miinuko pamoja na milimani. Hata hivyo amethibitisha kuwa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa na bado hasara halisi iliyosababishwa na mafuriko hayo haijafahamika hadi sasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya waathirika wa tukio hilo waliiomba Serikali kuwapatia msaada wa hali na mali ikiwemo makazi ya muda.
kitaifa
ELIZABETH HOMBO, Dar Na GUSTAPHU HAULE, Kibaha RAIS Dk. John Magufuli amesema ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shuleni. Amezitaka taasisi zinazotetea utaratibu wa wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, kufungua shule zao za wazazi lakini si kuilazimisha Serikali kufanya hivyo. Rais Magufuli ametoa agizo hilo   siku chache baada ya Taasisi ya HakiElimu kuitaka Serikali kuharakisha kupitia na kupitisha  miongozo  watoto wa kike waliojifungua warejee shuleni na kuendelea na masomo. Mbali na HakiElimu, pia wadau mbalimbali na baadhi ya wabunge wamekuwa wakitetea utaratibu wa wanafunzi wanaopata mimba kurudi shuleni wakitoa sababu mbalimbali za watoto wa kike kubeba mimba. Akizungumza jana akiwa katika ziara yake mkoani Pwani ambako pia alizindua viwanda saba, Rais alisema katu katika utawala wake hataruhusu utaratibu huo huku akizitaka taasisi binafsi zinazotetea wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni wafungue shule zao za wazazi. “Yaani anapata mimba amezaa mtoto iwe kwa makusudi,  kwa bahati mbaya au kwa raha yake, yaani aende shuleni ameshazaa! Si atawafundisha hawa wengine ambao hawajazaa! “Halafu akipata mimba tena ya pili anaenda nyumbani akizaa anarudi shuleni anapata wa tatu tena hivyo hivyo, yaani tusomeshe wazazi? “Nataka niwaambie na hizi Ngo’s na wote mnaonisikia ndani ya utawala wangu kama rais, hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni. “Nataka niwaeleze tukienda kwa mzaha wa namna hiyo na tukisikiliza hizi Ngo’s wanakotupeleka wanalimaliza taifa letu,” alisema Rais Dk Magufuli. Alisema Serikali yake ilitenga Sh bilioni 18 kwa ajili ya elimu bure  kwa sababu wapo watoto wa masikini ambao wanapata shida, lakini wanapokuwapo wachache wanaotetea hayo taifa litafika pabaya. Alisema hivi sasa ukifanywa uchunguzi watu ambao wanatetea hayo ndiyo hao hao ambao nao walipata mimba wakiwa shuleni. “Sasa narudia tena, hakuna mwenye mtoto katika elimu ya darasa la kwanza hadi sekondari kurudi shuleni kwa sababu amechagua maisha hayo ya mtoto akalee vizuri mtoto wake. “Lakini hata kama amepata mimba kwa bahati mbaya, yako mambo mengi ya kufanya ambayo yanaruhusu mtu aliyejifungua kufanya anaweza kwenda VETA, akajifunza kushona cherehani, akakopa kulima kilimo cha kisasa. “Labda ukazalie chuo kikuu huko wanaruhusiwa uwe mwaka wa kwanza, wa pili wewe zaa tu. “Lakini sekondari uzae halafu urudi tunapoteza maadili yetu, watazaa mno, itafika baada ya miaka kadhaa mtakuta darasa la kwanza wote wana watoto, wanawahi kwenda kunyonyesha kwa sababu mchezo huo ni mzuri na kila mmoja angependa aufanye,” alisema. Hata hivyo alivitaka vyombo vya dola kuhakikisha wale ambao wanawapa mimba wanafunzi sheria ifuatwe. “Nitoe wito kwa vyombo vya dola kwa sababu watakuja watu watasema, je wanaowapatia mimba itakuwaje? Sasa, je mimi niwabadilishe maumbile yao?   Wanaowapa mimba sheria ipo atakwenda kutumikia miaka 30. “Watu wa ajabu sana, hatuwezi kupeleka taifa hili katika maadili hayo. Kama wanaowatetea ni wazazi hawazuiliwi na hizi Ngo’s si wakafungue shule za wazazi kwa sababu wanakula tu fedha za bure za wafadhili lakini siyo waiamrishe Serikali kutekeleza hayo. “Nakupongeza Mama Salma Kikwete (Mbunge wa Kuteuliwa), ulisimama bungeni ukipinga haya endelea hivyo hivyo. “Sisi wote tuna watoto hata kama nina mtoto wangu wa kile apate mimba halafu arudi shuleni, wafanye halafu waone kama nitawarudisha shuleni. “Wametuletea watu kubakana wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake, wakati hata mbuzi au ng’ombe hafanyi huo mchezo… umeshawahi kuona mbuzi anakosea au ng’ombe?” alisema. PEMBEJEO HEWA Rais Dk. Magufuli alizungumzia suala la pembejeo hewa za kilimo ambako watu waliofariki dunia miaka zaidi ya 30 iliyopita wameandikiwa pembejeo kwenye vitabu. “Kuna watumishi hewa, vyeti hewa, wanafunzi hewa,   hivi sasa pia kuna pembejeo hewa. Wamepewa pembejeo na wameandikishwa wakati wamekufa zaidi ya miaka 30 sasa walikuwa wanatoka makaburini kuja kulima? Hata yanatokea Tanzania tu,” alisema. Aliwataka wakurugenzi wote nchini kabla ya Juni 30 mwaka huu, wawe wamekwenda kwenye kiwanda cha dawa za kuua mbu  kuchukua dawa hizo kwa ajili ya kuzisambaza. Katika hatua nyingine Rais Magufuli, alimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kurudisha serikalini viwanda vyote vinavyomilikiwa na wawekezaji walioshindwa kuviendeleza. Alisema kama wawekezaji hao watakuwa wabishi ni vema wakamatwe na ikiwezekana wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wawekezaji wengine ambao watakuwa wanamiliki wa viwanda bila kuviendeleza.
kitaifa
Na IBRAHIM YASSIN-NKASI MATUMAINI ya kupata mavuno mengi ya mahindi katika Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, yameanza kupotea baada ya wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavi jeshi kuvamia mashamba ya wakulima na kuyaharibu vibaya. Wadudu hao wamekuwa wakiharibu zaidi mazao ya mahindi kwa kula majani, kitoto cha mahindi na mbelewele kiasi cha mahindi hayo kushindwa kuzaa. Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya, Permin Matumizi, alisema wadudu hao wameingia wilayani Nkasi bila wakulima kugundua, wakifikiri kuwa ni wadudu aina ya zongoli na walishitushwa baada ya kuona wadudu hao hawafi kwa dawa za kawaida walizozoea kuwaulia wadudu hao. Alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa wakulima, wataalamu walibaini kuwa, wadudu hao ni viwavi jeshi ambao umbo lao ni kama la zongoli na kwa kitaalamu wanaitwa ‘maize stalkborer-heliothisspp’ na kuwa eneo lililoathirika zaidi ni katika vijiji vya Itekesya na Ntemba, vilivyoko katika Kata ya Kate. Alifafanua kuwa, wadudu hao ni hatari sana na zinahitajika juhudi za makusudi za kuhakikisha wanadhibitiwa mapema ili kuweza kuyanusuru mazao katika msimu huu wa kilimo wa 2017-18, ili baa la njaa lisije kutokea wilayani humo. Alisema mpaka sasa jitihada za Serikali zimefanyika kuhakikisha dawa za kuulia wadudu hao zinapatikana kwa wingi katika maduka yote ya pembejeo za kilimo na dawa sambamba na wakulima kushauriwa kuwatumia wataalamu wa kilimo katika kukabiliana na wadudu hao. Matumizi amewataka wakulima kushirikiana na wataalamu wa kilimo kufanya ukaguzi wa kina wa mashamba yote ili kuweza kubaini uwepo wa wadudu hao ili waweze kushirikiana katika kumaliza tatizo hilo.
kitaifa
Mtalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya faragha, Joe Cannataci ameomba jitihada za pamoja za kimataifa za kulinda na kuwawezesha watoto kukabiliana na mazingira ya mtandaoni. Tayari Cannataci ameanzisha mpango wa miaka miwili, ikiwa ni pamoja na mashauriano ya mtandaoni na ya umma, kukusanya mapendekezo yenye lengo la kuboresha ulinzi kwa ajili ya faragha ya mtandaoni kwa watoto kote duniani kwa kuweka msisitizo juu ya ulinzi na tabia sahihi mitandaoni.  Mapendekezo yatawasilishwa katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2021. Aidha, Cannataci amekaribisha maendeleo yaliyofikiwa Uingereza yakiwemo maelekezo ya serikali kuhusu mchakato wa kuanzisha kanuni mpya za ‘umri unaofaa’. Amesema kuwa, “nimeweka kanuni mpya ya umri unaofaa kama moja ya ajenda za mkutano ujao wa mwezi Septemba kuhusu kampuni kutumia taarifa binafsi. Ninataka kusikia kutoka kwa vinywa vyao wenyewe kampuni kama Google, Apple, Facebook, Microsoft, Amazon, Twitter na kadhalika ikiwa mapendekezo yanayotengenezwa yanaweza na yanatakiwa kuwekwa katika uhalisia kote duniani na ikiwa ni hivyo, iwe kwa namna gani na lini.”
kimataifa
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
uchumi
 MWAANDISHI WETU– DAR ES SALAAM  KAMPUNI ya ukopeshaji ya Letshego Holdings Ltd, imetenga Sh milioni 580 kusaidia nchi 11 zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona. Fedha hizo zitaelekezwa moja kwa moja katika akaunti ya mfuko wa taifa wa kila nchi, zikiwa na lengo la kuutokomeza ugonjwa ambao kwa sasa unaendelea kuua watu wengi duniani. Mtendaji Mkuu wa Letshego Tanzania Limited (Faidika), Baraka Munisi alisema pamoja na kampuni yao kushughulika na masuala ya ukopeshaji fedha, wameamua kuunga mkono kupiga vita maambukizi ya ugonjwa wa corona ambao umeathiri shughuli mbalimbali uchumi. Alisema Tanzania imepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 33 kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona, ambao ilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Alisema wamechukua hatua kubwa ya kuwasaidia wateja wake kutokana na changamoto zinazoendelea kutokea zilizosababishwa wa virusi vya corona. “Letshego imetoa malipo ya ahueni kwa wajasiriamali wote wadogo na wa kati na vile vile kutoa fursa kwa wateja wote kuomba kulipa mikopo kwa unafuu kutokana na kupungua kwa shughuli za kiuchumi katika masoko ya kanda yote.  Alisema ili kukabiliana na maambuziki ya virusi vya ugonjwa huo,wameamua kupunguza wafanyakazi wake wa masoko, badala yake imebaki nao wachache ili kuhamasisha mwongozo wa wataalam wa afya. Alisema kampuni yao, pia itahamasisha wateja wake kutumia mitandao yao ya kidigitali ili kupata taarifa za akaunti pamoja na kufanya maombi ya mkopo.  “Afya na ustawi wa wafanyakazi na wateja wetu inabaki kuwa kipaumbele chetu.  Tunawasaidia wateja jinsi ya kutumia teknolojia na uendeshaji kwa kutumia miundombinu yetu salama ya kidijiti.  Wateja wanahamasishwa kutumia mitandao ya kidijiti kama vile barua pepe, WhatsApp na kupiga simu kupitia huduma kwa wateja ambayo tumeongeza muda wa huduma kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku,” alisema. Alisisema itaendelea kushirikiana na Serikali na mamlaka za afya kuhamasisha miongozo rasmi ya afya, pia kuungana na ushauri wa kimataifa wa afya kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa.
afya
WANARIADHA kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamefanikiwa kushinda katika Mashindano ya wazi ya riadha ya kilomita 10’The Greath Health Arusha Run’ yaliyofanyika jana hapa.Wanaume waliokimbia kilomita 10 Faraja Lazaro aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dadika 28:56:77 akifuatiwa na Joseph Panga wote kutoka JWTZ kwa muda wa dakika 28:01:57 na nafasi ya tatu kushikiliwa na Mathayo Sombi kutoka Talent kwa muda wa dakika 29:26:66.Wanawake Cecilia Panga alimaliza kwa muda wa dakika 33:42:14 akifuatiwa na Iscah Cheruta kutoka Kenya kwa dakika 34:58:28, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Asha Salum kutoka JWTZ muda wa 35:02:43.Kocha Mkuu wa riadha katika JWTZ, Anthony Mwingereza amesema mafanikio yote ni chini ya usimamizi mahiri wa mazoezi kwa wanariadha hao na kusema hivi Sasa wanariadha hao wanajiandaa na Michezo ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika jijini Nairobi, Kenya mwezi ujao.Zaidi ya washiriki 800 kutoka ndani na nje ya mkoa Arusha walishiriki mbio hizo za kilomita 10, kilometa 2.5 kwa watoto na kilometa 5 kwa walemavu ikiwa ni mwaka wa tatu kufanyika zikilenga kuhamashisha cchezo wa riadha sambamba na upimaji afya kwa hiari .Katibu wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday alisema mbio zimeenda sawa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao ni viongozi ndani ya chama waliotaka kuzihujumu mbio zisifanyike lakini wamejulikana na watachukuliwa hatua kali iwe fundisho kwa wote wenye kukwamisha riadha.“Nampongeza mwandaaji wa mbio hizo Dokta Kylie Gyubi kwa kufanikisha kufanyika sambamba na kuimarisha afya chama kitaangalia ratiba ili mbio hizo zisigongane tarehe na mbio za Bagamoyo ,”amesema Gidabuday.Washindi mbalimbali walizawadiwa zawadi za fedha na medali ambapo mshindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume watakaokimbia kilomita 10 alijipatia shilingi 500,000, mshindi wa pili alipata 300,000, mshindi wa tatu alipata 100,000 na kuanzia mshindi wa nne hadi wa kumi atapata 50,000 kila mmoja.Zawadi kwa walemavu waliokimbia kilomita 5 mshindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume alijinyakulia shilingi 200,000, mshindi wa pili 150,000, mshindi wa tatu 100,000.Kwa upande wa watoto kilomita 2.5 mshindi atapata shilingi 100,000, mshindi wa pili 80,000, mshindi wa tatu 60,000 .
michezo
Ramadhan Hassan,Dodoma Mbunge wa Kaliua,Magdalena Sakaya (CUF) ameiomba Serikali kuipa mamlaka ya kusimamia sheria, Wakala wa Misitu (TFS) ili waweze kusimamia jambo la kukatwa miti hovyo . Akichangia leo Mei 24 bungeni wakati wa Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020,Sakaya amesema spidi ya ukataji miti nchini ni kubwa hivyo akaitaka Serikali kuipa Mamlaka,Wakala wa Misitu ili waweze kusimamia sheria. “Ukiangalia Spidi ya kukata mkaa inadhihiridha kwamba hali ya misitu yetu inaenda kuwa hatarini, Wakala wa Misitu wapewe Mamlaka, ukipewa Mamlaka unakuwa na uwezo wa kusimamia. “Miti inabakwa mbao zinazozalishwa hazijakomaa nataka nipate majibu kwanini mbao ambayo haijakomaa inaingizwa Sokoni.Nini mkakati wa Seriikali,”amehoji Sakaya. Aidha,Sakaya ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuliongezea bajeti Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)kwani lina majukumu mengi. “Serikali isipoangalia vivutio vyetu vitapotea Tanapa tunawapa majukumu makubwa wakati bajeti yake tumeipunguza kwa asilimia 18.Serikali ni lazima ikubali ipunguze tozo Tanapa imefanya kazi kubwa sana,kiukweli wanatakiwa kuongezewa bajeti tusipokuwa makini tunaenda kuiua Tanapa,”amesema Sakaya.
kitaifa
KIWANDA cha Bia Tanzania (TBL) kina mpango wa kujenga kiwanda chenye kuzalisha bidhaa hizo mkoani Dodoma na kutoa ajira kwa Watanzania 700 ujenzi wake ukitarajiwa kuwa umeanza ifikapo mwaka 2020.Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha lita milioni 6.4, kikitumia ardhi ya ekari 100 na gharama za uzalishaji zikikisiwa kufikia dola za Kimarekani milioni 100.Hata hivyo kiwanda hicho kinalalamikia uwepo wa mfumo uliowekwa na serikali (EST) wa kujua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda kama unaendana na kodi inayotolewa kwamba unaweza kushusha kiwango cha uzalishaji.Kadhalika serikali imesema inapokea kwa furaha kubwa dhana hiyo ya ujenzi wa kiwanda na kuahidi kutoa ushirikiano ili wasikwame lakini wakisisitiza viwanda kuzingatia uzalishaji wenye kutoa mchango katika patola Taifa.Akizungumza kiwandani hapo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Meneja Mkuu wa Konyagi, Davis Deogratius amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutanufaisha Watanzania walio wengi, kwa kupata ajira lakini pia kuzalisha bidhaa zitakazotumika kuzalisha vileo.Alisema wanafanya kazi kuzingatia sheria na taratibu za nchi ambapo ujenzi wa kiwanda hicho ni moja ya utekelezaji wa dhana ya uchumi wa viwanda, lakini pia wakilenga kuongeza maendeleo nchini.Kuhusu mfumo wa EST alisema wana wasiwasi utekelezwaji wake kwani TBL itaweka mtu wa kati ili kumlipa kwa ajili ya kufanya kazi ya kukagua kila bidhaa inayozalishwa katika kiwanda hicho ikiratibiwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stellah Manyanya alisema serikali inafurahia kuongezeka uzalishaji huku ikibainisha kuwa bia ya Tanzania inapendwa duniani.“Tumepokea kwa furaha kubwa suala la ujenzi wa kiwanda mkoani Dodoma, na hatutosita kutoa ushirikiano ili wasikwame, uzalishaji uendane na matakwa ya serikali ili kutoa mchango katika pato la taifa,” amesema.Hata hivyo amesema ipo haja ya kujiridhisha kuwa kiwango kinachozalishwa kama kinaendana na kodi inayolipwa ili ilingane na uhalisia.Kuhusu mfumo wa ETS, inayolalamikiwa na wadau, alisema serikali iliweka ili kujua bidhaa zinazozalishwa ili kodi ilingane, kama kuna dosari, lakini akiwataka kukutana na kujadiliana kuona ni namna gani kama kuna changamoto inaweza kuondolewa.Amesema iliwekwa kutokana na kwamba baadhi ya viwanda havikuwa wakweli kuhusu uzalishaji kwani ni lazima pande zote kunufaika na kile kinachozalishwa kinufanishe nchi na wawekezaji pia wanufaike.
kitaifa
Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM UONGOZI wa timu ya Simba, umesema upo tayari kukaa na Yanga meza moja kumaliza mgogoro uliopo baina yao na watani wao hao wa jadi juu ya beki wao, Hassan Ramadhani ‘Kessy’. Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juzi ilikaa kikao cha kuamua hatima ya mchezaji huyo na kutoa saa 72 kwa viongozi wa Yanga kumalizana na Simba. Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jana licha ya agizo hilo la kamati, Yanga wamekaa kimya jambo alilosema si la kistaarabu. “Sisi kama Simba hatuoni sababu ya kuendelea na malumbano haya na kumnyima  haki  Kessy, lakini wenzetu wanapaswa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa, sasa wamekataa kukaa meza moja tuyazungumze,” alisema. Kaburu aliongeza imekuwa kawaida kwa Yanga kuchukua wachezaji kutoka Simba, lakini kwa suala hili wanapaswa kujifunza kuwa wastaarabu na kwamba wangezungumza ili mambo yamalizike na mchezaji huyo awe huru. Akizungumza na MTANZANIA juu ya suala hilo Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema lipo juu ya kamati na kudai kuwa baada ya saa hizo kupita watatoa maamuzi. “Siwezi kusema tumezungumza au la, lakini kila kitu kitajulikana baada ya hizo saa 72, nasisitiza kuwa suala hili ni la kamati na si vinginevyo,” alisema katibu huyo. Yanga na Simba zimeingia kwenye mzozo juu ya usajili wa beki Kessy ambaye anadaiwa kusaini Yanga akiwa bado anatumikia adhabu ya kusimamishwa mechi tano na timu yake ya Simba. Kessy alipewa adhabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kugundulika kuwa na utovu wa nidhamu, adhabu ambayo inadaiwa  hakuimaliza na kuamua kusaini mkataba mpya na timu ya Yanga.
michezo
FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM BARAZA Kuu la Waslamu Tanzania (Bakwata) limepiga marufuku matukio ya muziki moto au maarufu kama magoma moto yanayorasimishwa na kaswida yanayotumiwa na Waislamu katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe kwa kuwa yanachafua taswira nzima ya dini hiyo. Marufuku hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir. Alisema jambo hilo limekiuka maadili ya Uislamu na liko nje ya dini hiyo. “Nachukua fursa hii kuwatangazia juu ya tukio ambalo limejitokeza la muziki moto ambao unarasmishwa na kaswida zinazotumika katika Uislamu ambazo zinatumika zaidi kwenye harusi… jambo hilo limekiuka maadili ya Uislamu na liko nje ya misingi ya Uislamu. “Tunawapiga marufuku na kuwazuilia wale wote wenye kupiga kaswida hizo na muziki huu unaorasimishwa na Uislamu kwa kuwa unachafua taswira nzima ya Uislamu, maadili na malezi mema kwa watoto wetu,” alisema Mufti. Kutokana na hali hiyo, aliwaagiza masheikh wote wa mikoa kuhakikisha wanakemea aina hiyo ya kaswida. “Masheikh wa mikoa, wilaya na kata, nawapa agizo la kuzuia na kukemea miziki hii ambayo inachafua maadili, wakemee katika nafasi walizonazo, ikiwa ni katika misikiti, hotuba zao na mihadhara mbalimbali wanayoifanya. “Pia nawaagiza maimamu na masheikh wa taasisi mbalimbali kukemea jambo hili na kuondosha hali hii. Mtume anasema ‘aonae jambo bovu basi aligeuze kwa mkono wake’ kila mmoja ana wajibu wa kulifanya jambo hili,” alisema Mufti. Alisema baraza limezuia jambo hilo na iwapo atatokea mtu akaamua kufanya kwa sura na kwa picha na kwa kuegemea katika Uislamu, atachukuliwa hatua kali za kisheria. Mufti aliwaasa kina mama kuwalea vijana katika malezi yaliyo bora pamoja na kupiga marufuku kuruhusu ngoma hizo kuja kwenye sherehe za watoto wao. “Ngoma moto hizo ambazo nimeonyeshwa na masheikh hazifai hata kidogo, siyo Uislamu, hatutaki kabisa kuona katika nchi yetu, ni mambo ya aibu, nchi yetu inahitaji watu wenye nidhamu, maadili, wasomi na viongozi wazuri wa hapo baadaye, hauwezi kupata viongozi kwa kuruhusu mambo ya namna hii yaendelee. “Mkoa unaoongoza kwa matukio haya sasa ni Dar es Salaam, tayari baadhi ya wahusika wameanza kutiwa nguvuni maeneo ya Kigamboni,” alisema Mufti. Alisema baraza hilo sasa litakuwa likiadhimisha Siku ya Bakwata (Bakwata Day) kila ifikapo Desemba 17 ya kila mwaka na mwaka huu, sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika viwanja vya Karimjee na kuwataka Watanzania wengi zaidi kujitokeza. Akizungumzia miaka 58 ya Uhuru, Mufti alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii huku akienzi juhudi kubwa zilizofanywa na waasisi wa taifa, ikiwamo kudumisha amani.
kitaifa
 WASHINGTON, MAREKANI IDADI ya wagonjwa waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani imepita 100,000 katika kipindi cha chini ya miezi minne. Taifa hilo limeandikisha vifo vingi zaidi ya taifa lolote lile huku watu milioni 1.69 wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo idadi ambayo ni asilimia 30 ya maambukizi yote duniani. Maambukizi ya kwanza nchini Marekani yaliripotiwa mjini Washington Januari 21, 2020. Kote duiniani kumekuwa na watu milioni 5.6 walioambukizwa virusi hivyo huku idadi ya vifo ikifikia 354,983 tangu mlipuko wa virusi hivyo kuzuka mjini Wuhan nchini China mwisho wa mwaka jana. Kufikia sasa idadi ya waliofariki nchini Marekani imefikia 100,276, kulingana na Chuo kikuu cha John Hopkins mjini Maryland ,ambacho kimekuwa kikifuatilia mlipuko huo. Muhariri wa BBC katika eneo la Marekani ya Kaskazini, Jon Sopel alisema kwamba idadi hiyo ni sawa na idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita vya Korea, Vitenam, Iraq na Afghanistan katika kipindi cha miaka 44 wakipigana. Hata hivyo, Marekani imeoredheshwa ya tisa duniani kwa kiwango cha watu wanaofariki nyuma ya Ubelgiji, Uingereza , Ufaransa na Ireland kulingana na chuo hicho. Majimbo 20 yaliripoti kuongezeka kwa kesi mpya kwa wiki iliokuwa inaisha siku ya Jumapili, kulingana na utafiti wa Reuters.
kimataifa
Yohana Paul – Mwanza MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewatahadharisha wahandisi wenye leseni zilizoisha muda wake kuwa hawatapata nafasi ya kufanya kazi ndani ya mkoa wake kuanzia Aprili. Alitoa tahadhari hiyo wiki iliyopita mkoani hapa, wakati akizungumuza na wahandisi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wakati wa kikao kilicholenga kutoa tathmini ya kazi za uhandisi nchini pamoja na nafasi ya wahandisi wazawa katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kitaifa. Mongella alisema kuanzia sasa wahandisi wote wanatakiwa kuwa na leseni halali, hivyo wote wenye leseni zilizoisha muda wanatakiwa kulipia. Alitoa nafasi hadi Machi 31, kila mmoja awe na leseni, kinyume na hapo atazungumza na wakuu wa wilaya wote wasifanye kazi nao. “Serikali tangu imeingia madarakani imetoa kipaumbele kwa wahandisi wazawa kwa kuwa inaamini ndio mnaweza kulifikisha taifa katika uchumi wa viwanda pasipo kikwazo chochote na bila hujuma. “Naomba mtambue ili mhandisi uweze kuaminika na kupewa kazi bila kutiliwa shaka, lazima uwe na leseni iliyohuishwa kwa maana ya ile ambayo inatambulika na mamlaka husika, hivyo nami kama kiongozi wa mkoa niwaambieni nitafanya kazi na wenye leseni zilizo ndani ya matumizi tu na si vinginevyo. “Binafsi napenda kufanya kazi na kila mhandisi aliyekidhi kigezo, sitegemei baada ya muda wa mwisho wa kuhuisha leseni nilioutoa kuisha, kuona mhandisi mwenye leseni iliyoisha muda anakuja kuomba kazi Mwanza, nawaambia hakuna mhandisi atafanya kazi. “Pia nakumbusha kazi ya uhandisi kama mnavyojua ni kazi ya kiapo, ndiyo maana leo pia kuna wenzenu wamekula kiapo, hii ni ishara kuwa kazi yenu inabeba roho za watu, inategemewa, jitahidini kufanya kazi kwa kuzingatia kiapo chenu ili kazi yenu iwe na manufaa kwa taifa lenu na si vinginevyo,” alisema Mongella. Msajili wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB), Patrick Barozi alisema hadi sasa kuna wahandisi waliosajiliwa 26,618 nchi nzima ambapo miongoni mwao, 2,925 ni wanawake sawa na asilimia 21. Alisema kazi ya uhandisi mbali na kuwa ni taaluma, pia ni kama dhamana kwa kuwa inahusisha kiapo. “Unapokuwa mhandisi unakuwa na nafasi kubwa ya kuisaidia nchi yako kwa kufanya kazi ama kwa kushauri jinsi ya ujenzi wa miradi mbalimbali. “Nawaomba wahandisi wote, ikiwamo hawa 40 waliokula kiapo leo, wafanye kazi kwa kuzingatia kiapo na kwa kutambua thamani ya taaluma ya uhandisi. “Kwani kuzingatia kiapo itasaidia kulinda maadili ya uhandisi na hii itaondoa changamoto ya wahandisi kufanya kazi bila mikataba, changamoto ambayo sisi wahandisi ni lazima tusimame pamoja kukemea. “Na niiombe Serikali yetu kuhakikisha wahandisi wanakuwa na mikataba wanapofanya kazi sehemu yeyote ili kuepusha sintofahamu ambazo hujitokeza.” alisema Barozi. Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania(MSCL), Erick Hamis aliwataka wahandisi wote hasa wale wanaohitimu vyuoni kuwa na uthubutu wa kufanya kazi.
kitaifa
Uamzi huo ulifanywa jana katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura, Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo, kumetokana na ukiukaji wa sheria na kanuni za biashara hiyo.Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na Ewura.Kampuni zilizofutiwa leseni ni Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.Mamlaka hiyo imeundwa chini ya sheria ya Ewura Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania. Mamlaka hiyo ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi katika sekta za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.
uchumi
AMSTERDAM, NETHERLANDS BEKI wa Ajax, Matthijs de Ligt, amethibitisha kuwa hakuna klabu ya ndoto yake iliyojitokeza hadi sasa licha ya kutakiwa na klabu nyingi barani Ulaya ikiwamo Barcelona na Man United. De Ligt (19), amekuwa akigombewa na klabu kubwa barani Ulaya zikihitaji kumsajili kwa ajili ya msimu ujao, lakini beki huyo anataka kuendelea kucheza Ajax msimu ujao. Mbali na klabu hizo, pia Juventus na Liverpool zimedaiwa kuifukuzia saini ya beki huyo ambaye alifanikiwa kuiongoza Ajax kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Licha ya De Ligt kutokuwa na haraka ya kufanya uamuzi kwa sasa, mkataba wake unamalizika mwaka 2021. De Ligt aliueleza mtandao wa NOS: “Sijafanya uamuzi wowote kwa sasa. “Mambo mengi yanaandikwa na kusemwa kuhusu mimi. Lakini hayajawahi kunifanya nichanganyikiwe. “Frenkie de Jong (ambaye amejiunga Barcelona) alishafanya uamuzi wake lakini mimi bado, huo ndio ukweli. “Unatakiwa kuangalia kile kilicho bora kwako kisha ndio ufanye uamuzi, nafahamu klabu nyingi zinanihitaji, ni jambo zuri.” De Ligt aliongeza: “Sina ndoto ya klabu nyingine tofauti na Ajax. Kila siku imekuwa ndoto yangu na kupata mafanikio nikiwa hapa. “Naangalia klabu bora kwa kazi yangu ambayo itakuwa sehemu sahihi kuendeleza kipaji changu. Lakini bado nina mkataba na Ajax, hivyo msimu ujao nitakuwa hapa.”
michezo
JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliezer Feleshi amesema wamejipanga kuboresha mahakama zote nchini kuanzia ngazi ya wilaya kutumia mfumo wa kielektroniki kwa kuweka taarifa zake zote mtandaoni.Jaji Kiongozi alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea banda la Mahakama katika viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) yanayoendelea.Alisema hivi sasa wameanza kusajili kesi kwa mfumo wa kielektroniki na pia majaji na mahakimu wa baadhi ya mahakama wameanza kuweka maamuzi ya kesi mbalimbali mtandaoni ili kurahisisha taarifa. Jaji Feleshi alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwapa fursa wananchi kusoma maamuzi ya kesi zote zinazotolewa hukumu kupitia njia ya mtandao badala ya kutumia muda mwingi kusafiri kwenda mahakamani kufuatilia.“Tumeanza kuboresha huduma za mahakama zetu ili kurahisisha huduma kwa wateja ambao ni wananchi, lakini pia kuokoa muda wao ili wajipange na kufanya kazi nyingine za maendeleo badala ya kufuatilia siku nzima kesi mahakamani,” alisema.Awali, Hakimu Mkazi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama, Victoria Nongwe alisema hatua hiyo ni mkakati wa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa mahakama. Akizungumzia mfumo huo, Hakimu Victoria alisema katika mfumo huo mawakili binafsi na wale wa serikali zaidi ya 632 wamepata akaunti tumizi ya kufungua kesi kwa njia hiyo na kwamba tangu kuzinduliwa kwake Februari mwaka huu, mashauri 1,111 yamewasilishwa.Akifafanua mashauri hayo, Hakumu Victoria alisema kati ya hayo mashauri 365 ya yameshasajiliwa mahakamani, 161 bado yapo kwa mawakili 223 yamerudishwa kwa marekebisho na mengine 66 yamekataliwa.“Mfumo huu ulianzishwa ikiwa ni mkakati wa mahakama wa kuboresha huduma zake na pia kupunguza malalamiko na kuweka mazingira bora ya utendaji kazi yenye kuepuka uwezekano wa kuwepo kwa vishawishi vya rushwa,” alisema.Alisema hivi sasa wakili aliyepata akaunti tumizi ya kufungua kesi mtandaoni anaweza kufungua kesi akiwa mahali popote, hivyo kurahisisha usajili wa kesi lakini pia iwapo kuna makosa katika usajili huo ombi hurudishwa kwa marekebisho. Kama halikubaliki pia wakili hupata taarifa ndani ya muda mfupi.
kitaifa
RAIS John Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na Majeshi mengine ya Ulinzi na Usalama nchini, kwa kazi nzuri ya kudumisha amani na usalama nchini, hasa katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.Alitoa pongezi hizo jijini hapa jana, baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba 118 za Askari Polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medeli East, katika siku yake ya pili ya ziara yake mkoani hapa. Alipongeza kwa kazi nzuri wanayofanya katika ulinzi wa usalama wa raia na mali zao, kwani hata matukio ya uhalifu nchini yamepungua katika kipindi hiki.Rais Magufuli aliwataka polisi waendelee kuchapa kazi za kulinda amani na utulivu nchini. Aliahidi kwamba changamoto zao zikiwemo za makazi, serikali itaendelea kuzifanyia kazi.“Kadiri fedha zinavyopatikana serikali itaendelea kuzitatua changamoto zinazowakabili polisi zikiwemo za makazi na nyingine,” alisema.Rais aliwataka waendelee kufanya kazi zao vizuri na waachane na vitendo vya kuwabambikizia watu kesi na vitendo vya kupokea rushwa, kwani vinachafua sifa nzuri ya jeshi hilo. Aliwataka maofisa wakubwa katika majeshi ya ulinzi na usalama, kuwajali, kuwaheshimu na kutowanyanyasa askari wadogo na wadogo nao kuwajali na kuwaheshimu askari wakubwa.Kutokana na kazi nzuri ya jeshi la polisi ya kulinda amani nchini, Rais Magufuli alilipa zawadi jeshi kwa kuwapa jengo la ghorofa nne la Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa), ili liwe makao makuu ya jeshi hilo. Jengo hilo ni la Wizara ya Maji, ambayo ililikabidhi kwa Ruwasa, ambayo tayari imeshalikarabati.Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kutolichukua jengo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma na kulifanya makao makuu. Badala yake, alieleza kuwa Polisi watumie jengo hilo la Ruwasa la ghorofa nne kama makao makuu, lakini pia Ruwasa iendelee kuwapo hapo katika majengo yake.Awali, akizungumza IGP Sirro alimuahidi Rais Magufuli kwamba wamejipanga vizuri katika kuwalinda raia na mali zao na kuhakikisha nchi inakuwa na amani. Sirro alisema tayari amehamia Dodoma na aliahidi kwamba atasimamia na kuhakikisha jengo la makao makuu ya jeshi hilo pamoja na nyumba ya IGP anasimamia na Desemba 31, mwaka huu ziwe zimekamilika.
kitaifa
Mwandishi wetu, Tanga WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shidakulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao. Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimukwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu kwa kukishirikiana namaafisa wa TRA mkoa wa Tanga. Maafisa hao waliwatembelea wafanyabiashara kwenye maduka yaoyaliyopo barabara za namba jijini Tanga kwa lengo la kuwaelimisha nakuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.Sambamba na hilo, maafisa hao pia waliweza kusikiliza kerozinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao kama mpango wa kutengeneza mazingira rafiki kati yao naTRA.Thabiti Salimu ambaye ni mfanyabiashara wa Ukwaju wa jumla na rejarejakatika eneo la barabara za namba amesema kuwa, atamshangaamfanyabiashara atayekwepa kulipa kodi hususani katika kipindi hikiambacho wameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kupitia kodi zao. “Rais Magufuli anatumia kodi zetu vizuri, tunaona utekelezaji wa miradimingi ya maendeleo hivyo lazima tuendelee kulipa kodi la sivyo kazi yautekelezaji wa miradi hii itakwama,” alisema Salimu. Naye Dina Mbenu, mfanyabiashara wa vipuli vya pikipiki amesema kuwa,ikiwa wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi watasababisha madhara yakiuchumi na kuathiri jitihada za serikali za kuboresha miundombinuikiwemo barabara. Amesema hatua ya maafisa wa TRA kuwatembelea kwenye maduka yaokwa lengo la kuwahamasisha kulipa kodi na kusikiliza kero na maoni yaoinawasaidia kutopoteza muda kwenye ofisi za TRA wakisubiri kuhudumiwa. Kwa upande wake Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Julius Mjenga amesemazoezi la kuwatembelea wafanyabiashara ni endelevu na kabla ya kufanyikaTanga, zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,Mbeya na Morogoro. Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutoa elimu ya kodi, kuwakumbushawafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kusikiliza maoni yao pamoja nachangamoto kwa ajili ya kuzitatua.Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure, aliwaombawafanyabiashara kuunga mkono zoezi linalofanywa na maafisa wa TRA lautoaji elimu ya kodi, kusikiliza maoni na changamoto zao kwa kuwa zoezi hilo linalenga kuboresha huduma kwa mlipakodi.“Niwaombe wafanyabiashara wote mkiwaona maafisa wanatembelea,msifunge maduka, wapokeeni na kuwapa ushirikiano kwa kuwa wanalengakuwaelimisha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenyebiashara zenu ambazo kwa pamoja tunaweza kuzitafutia ufumbuzi,”alisema Owure. Amesema zoezi hilo la utoaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiasharamkoani humo linatarajiwa kumalizika Juni 30, 2020 na kwamba lengo likiwani kutaka kuwafikia wafanyabiashara wengi mkoani hapo.
uchumi
Ngoma aliwaweka roho juu, mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatia habari kuwa, angesaini juzi kuichezea Simba kiasi cha Yanga kudaiwa ‘kumteka’ uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) aliporejea kutoka kwao.Habari zilizopatikana jana kutoka kwa Kaimu Msemaji wa Yanga, Anderson Chicharito zilisema Ngoma amesaini mkataba wa kuichezea Yanga wa miaka miwili lakini hakutaja dau lake.Hata hivyo, Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe amesaini Yanga huku vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vikiwa pia vimeripoti amefaulu majaribio na vipimo vya afya kuichezea Polkwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya soka ya nchi hiyo.Chicharito jana alisambaza picha ya Ngoma akionekana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika akisaini. Katika picha hiyo, Kiongozi Baraka Desdedit anashuhudia.Ngoma aliwaweka Yanga roho juu baada ya mchezaji mwingine wa Yanga, kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima wa Rwanda kudaiwa kusajiliwa Simba kwa dola 60,000 ingawa kakanusha.Wakati Yanga ikimnasa Ngoma, timu ya soka ya Majimaji FC imepanga kusajili wachezaji 11 wapya kuimarisha kikosi chake. Msemaji wa timu hiyo, Zakaria Mtigandi alisema tayari uongozi wao umeanza kufanya mazungumzo na wachezaji wanaotaka kuwasajili na mazungumzo yanaenda vizuri mpaka sasa.Alisema msimu huu wanahitaji wachezaji 25 badala ya 30 wa msimu uliopita watakaoweza kupambana kuipa timu mafanikio. Alisema wameacha wachezaji 16 na kubakiwa na 14 hivyo hao 11 watafanya kuwa na idadi ya wachezaji 25 wanaohitajika.Mtigandi aliongeza timu yao haina mpango wa kwenda nje kusaka wachezaji kwani wanaamini wanaweza kupata wachezaji ndani ya nchi na kuifanya timu kuwa ya ushindani. Alisema ili kunyakua wachezaji hao, wameunda kamati ya usajili inayofanya kazi usiku na mchana kupata wachezaji walio bora.Alisema kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Hersi Said akisaidiwa na Katibu Steven Ngonyani, na Kocha Kally Ongala. Imeandikwa na Mohammed Akida na Mohammed Mdose
michezo
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamekamata gari dogo la abiria, (Toyota Hiace) likiwa limebeba magunia ya mkaa yasiyo na vibali kutoka idara ya maliasili.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kulikamata gari hilo, Meneja wa Misitu Wilaya ya Igunga, Herry Mwangili amesema wakiwa doria wanazofanya kila siku walipata taarifa kutoka kwa wasiri wao kuwa kuna gari dogo la Hiace limebeba shehena ya magunia ya mkaa likitokea kata ya Itumba.Amesema baada ya taarifa hiyo waliweka doria katika barabara itokayo Igunga mjini kwenda kata za Nguvumoja, Lugubu na Itumba, ambapo saa 12 jioni walifanikiwa kuikamata gari hiyo na walipofanya ukaguzi walikuta dereva wa gari hilo, Donald Renald akiwa ametoa viti vya abiria na kuweka magunia 16 ya mkaa yote yakiwa hayana vibali.Alisema mmiliki wa gari hilo lenye namba za usajili T 85 AXX, Emmanuel Matemba alilipa faini ya Sh milioni moja huku mkaa wote ukitaifishwa na Wakala wa Huduma ya Misitu Igunga ambao baadaye utauzwa kwa wananchi baada ya kupewa kibali kutoka mkoani Tabora.Aidha, Mwangili alisema idara yake imefanikiwa kukamata pia baiskeli 25 zikiwa zimebeba magunia 30 ya mkaa yote yakiwa hayana vibali ambapo vyote vimehifadhiwa kwenye ofisi ya TFS Igunga. Dereva wa gari hiyo alipoulizwa juu ya tuhuma hiyo alikiri kubeba mkaa huo bila vibali kutoka Itumba hadi Igunga kwa bei ya Sh 62,000.“Baada ya kukosa abiria nilipata dili ya mkaa na ndio nikaona nibebe mkaa,” amesema Renald huku akidai wenye mkaa wote walikimbia baada ya mkaa huo kukamatwa.Kwa upande wake, mmiliki wa gari hilo, Matemba alisema gari yake hufanya safari zake Igunga - Nzega lakini alishangazwa baada ya kupigiwa simu kuwa gari limekamatwa na TFS likiwa na magunia 16 ya mkaa.
kitaifa
DAMASCUS, SYRIA RAIS Bashar al Assad, amesema Marekani inapaswa kujifunza kutokana na mzozo wa Irak na kuyaondoa majeshi yake kutoka Syria. Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Urusi Leo, Assad amesema Serikali yake imeanza kufungua milango kwa mazungumzo na waasi na ikishindikana watayakomboa maeneo yote kwa nguvu. Aliwataja kuwa ni pamoja na wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani, SDF wanaodhibiti theluthi moja ya Syria hasa maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Syria ambako majeshi ya Marekani yamepiga kambi. Rais huyo amesema mazungumzo ndiyo njia ya kwanza watakayotumia kuafikiana na kundi hilo la Kikurdi na iwapo hilo litashindikana, basi watalazimika kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na SDF kwa kutumia nguvu. Assad ametolea mfano wa Irak, akisema majeshi ya Marekani yaliivamia na kuingia humo bila ya kuwa na msingi wowote kisheria na sasa nchi hiyo imesalia kuwa katika mzozo. Alisema watu hawatakubali wageni kuingilia nchi za kanda hiyo ya Mashariki ya Kati. Alipoulizwa na kituo hicho kuhusu mtazamo wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa yeye ni ‘mnyama’, Assad alisema kile unachokisema kumhusu mtu mwingine ndivyo ulivyo. Trump alimwita Assad mnyama baada ya shambulizi linalodaiwa kuwa la silaha za sumu katika eneo la Douma Aprili, mwaka huu.
kimataifa
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KOCHA wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni, amesema hafikirii kuingia mkataba na klabu hiyo kabla ya kuwaandaa wachezaji na kupata kikosi bora cha kwanza kitakacholeta ushindani katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Kibadeni ambaye amewahi kuifundisha Simba na mshauri wa benchi la ufundi la timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa sasa, aliitwa kuinusuru timu hiyo na matokeo mabaya baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha mkuu, Felix Minziro. Akizungumza jana kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Kibadeni alisema bado ana kazi kubwa ya kuwasoma wachezaji akisaidiana na msaidizi wake ili kuandaa ‘first eleven’ itakayoleta ushindani Ligi Kuu. Alisema ni vigumu kufikiria suala la mkataba kwa kuwa sasa hana mpango huo na anachoangalia zaidi ni kuhakikisha timu hiyo inaondokana na matokeo mabaya na kupata pointi ambazo zitarejesha matumaini ya kubaki Ligi Kuu. “Suala la mkataba sijalipa kipaumbele wala kulifiria kwa sasa hadi nitakaporidhika na maendeleo mazuri ya timu kwa kupata pointi zaidi ya sita,” alisema. Alisema kwa kuanza kampeni zake za ushindi watahakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar kesho watakapowakaribisha Uwanja wa Karume, Dar es Salaam ili kuondokana na majanga ya kubaki mkiani mwa ligi hiyo wakiwa na pointi moja. “Kwa muda mfupi ambao nimeifundisha JKT Ruvu nimegundua kuna wachezaji wazuri ambao nitaweza kuwapa nafasi katika kikosi cha kwanza na kuanza safari ya ushindi kwenye mechi zinazofuata,” alisema. Tangu kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu, JKT Ruvu inakabiliwa na hali mbaya kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha ya kufungwa mechi sita na kupata sare moja baada ya kushuka dimbani mara saba.
michezo
DIWANI wa Kata ya Kilimani Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Neema Mwaluko (CCM) amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kata kwa kipindi cha miaka minne.Amesema ameweza kushughulikia tatizo la ardhi katika eneo la Chinyoyo, lililodumu kwa miaka 20. Kata ya Kilimani ambayo ni miongoni mwa kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ina mitaa minne na jumla ya wakazi 6,831. “Nimeshughulikia tatizo la ardhi kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, nimefanikiwa kutatua kero kubwa ya upimaji wa mtaa wa Chinyoyo iliyodumu takribani miaka 20, sasa mtaa umeshapimwa kwa njia ya maboresho kila mtu atabaki pale alipojenga tupo katika hatua ya mwisho ya maboresho kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa Jiji,” alisema. Pia, alisema katika uwezeshaji wananchi kiuchumi, amehamasisha na kutoa elimu ya namna bora ya kukuza biashara na kuziboresha, uundaji wa vikundi na jinsi ya upatikanaji wa mikopo inayotolewa na halmashauri. Alisema katika kipindi cha miaka minne, vikundi 43 viliundwa na kukaguliwa na kupatiwa usajili. Alisema vikundi 18 vilipatiwa mikopo ya halmashauri ya Sh 65,129,500. Alisema wamefanikiwa kutenga eneo la kujenga soko mtaa wa Chinyoyo, lenye ukubwa wa mita za mraba 5,518.Kwamba soko hilo litafanya mzunguko wa fedha kuwa mkubwa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali. Alisema kata hiyo ni miongoni mwa kata zinazopokea huduma ya kunusuru kaya maskini chini ya TASAF. Kuna jumla ya walengwa 113 na fedha walizopatiwa mpaka sasa ni Sh ilioni 89.4. Alisema mtaa wa Chinyoyo una walengwa 80, mtaa wa Nyerere walengwa 11, Imagi walengwa 11 na Kilimani walengwa 11.“Kupitia mradi wa Tasaf tumefanikiwa kuwapatia walengwa elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya uundaji wa vikundi vya uzalishaji mali ambapo hadi sasa vimekwishaundwa vikundi vine na vimesajiliwa.
kitaifa
RAIS John Magufuli ametoa wiki moja kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Viwanda na Biashara, kukamilisha taratibu za uwekezaji kwa Kampuni Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius, ambayo imecheleweshwa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari tangu mwaka 2017.Rais Magufuli alitoa maagizo hayo jana Ikulu Dar es Salaam, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Gansam Boodram aliyeongozana na Balozi wa Mauritius nchini, Jean Pierre Jhumun. Katika mazungumzo hayo, Boodram alieleza kuwa yupo tayari kulima ekari 25,000 za mashamba ya miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari na kwamba uwekezaji huo utawezesha kuzalishwa kwa tani 125,000 za sukari, ajira za kudumu 3,000 na ajira za muda 5,000.Lakini, alisema amekwama kuendelea kutokana na kusubiri majibu ya serikali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu upatikanaji wa eneo la uzalishaji wa miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.Rais Magufuli aliagiza ufanyike uchambuzi wa haraka katika maeneo ya Bonde la Mto Rufiji mkoani Pwani, eneo la shamba la Mkulazi mkoani Morogoro na eneo la Kibondo mkoani Kigoma ili mwekezaji huyo apatiwe na kuanza mara moja uwekezaji, kwa kuwa nchi inahitaji kuongeza uzalishaji wa sukari, utakaomaliza upungufu wa tani zaidi ya 100,000 ambazo kwa sasa zinaagizwa kutoka nje ya nchi.Rais Magufuli alimuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Edward Mhede kufuatilia makubaliano ya ushirikiano katika uvuvi kati ya Tanzania na Mauritius, ambayo hayajatiwa saini tangu mwaka 2017, licha ya wawekezaji wa Mauritius kuonesha nia ya kutaka kuwekeza katika uvuvi na viwanda vya samaki. Balozi Jhumun alimueleza Rais Magufuli kuwa Mauritius inao uzoefu mkubwa katika uvuvi na viwanda vya samaki.Alisema kwamba kwa kuitikia mwito wake wa kuhamasisha wawekezaji kuja hapa nchini, amefanikiwa kupata kampuni zilizo tayari kufanya uwekezaji huo baada ya makubaliano kati ya Tanzania na Mauritius kutiwa saini. Rais alizionya taasisi za serikali, kikiwemo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kutoharakisha taratibu za kuwawezesha wawekezaji kuwekeza.Alimhakikishia Balozi Jhumun kuwa atafuatilia, kuhakikisha uwekezaji wa kampuni ya SIT unafanyika. “Ndugu zangu watendaji wa serikali badilikeni, acheni kukwamisha wawekezaji, fanyeni maamuzi na kama yanawashinda toeni taarifa kwenye mamlaka za juu,” alisisitiza Rais Magufuli. Waziri wa Ardhi ni William Lukuvi na Waziri wa Viwanda na Biashara ni Joseph Kakunda.
kitaifa
MKOA wa Pwani umefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 147 kutokana na kodi mbalimbali katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu Tano.Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo wakati wa kikao cha mashauriano kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa huo.Ndikilo amesema kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2015 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa huo walikusanya kiasi cha Sh bilioni 64.9.“Fedha hizo za kodi zilitokana na kodi za Vat, income tax, paye ukiondoa kodi ya forodha nakushika nafasi ya 12 kati ya mikoa 30 ya kikodi nchini,” amesema Ndikilo.Amesema Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miaka minne iliyopita kwa kigezo cha ukusanyaji wa kodi ulikuwa chini sana na ulikuwa hautajwi lakini katika serikali hii mkoa umepiga hatua kubwa.“Tunaomba kupewa sehemu ya Ranchi ya Taifa Narco ukubwa wa ekari 6,000 kwenye eneo la Bandari Kavu ya Kwala Kibaha Vijijini ili kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuegesha magari, biashara, makazi, mahoteli na maghala, viwanda,” amesema Ndikilo.Aidha, alisema Narco wana eneo lenye ukubwa wa ekari 30,000 hivyo endapo watapata eneo hilo ili liwe la uwekezaji kwani ni karibu na Reli ya Kati, Reli ya Kisasa, Reli ya Tazara, sehemu ya kupokea umeme kutoka Bwawa la Nyerere Rufiji, jirani Bandari ya Dar es Salaam, chanzo cha maji ya Dawasa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Abdala Ndauka amesema changamoto mojawapo ni baadhi ya taasisi za zinazohusika na vibali kutumia nguvu badala ya kutoa elimu.Mfanyabiashara wa viwanda vya kokoto, Ally Murad alisema wanatumia gharama kubwa ya umeme wa jenereta wanaotumia kutokana na kutokuwa na umeme wa Tanesco hivyo wanaomba kupatiwa umeme.
kitaifa
    KHARTOUM, SUDAN RAIS wa Sudan, Omar el-Bashir, amekataa mwaliko kutoka utawala wa Saudia Arabia wa kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Kiislamu ambao Rais Donald Trump atakuwa mgeni rasmi. Bashir, ambaye alitoa sababu za kibinafsi, anasakwa kwa uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur na Marekani ilikuwa haikufurahia mwaliko wake katika mkutano huo. Sudan ilikuwa imesema kuwa inataka kuimarisha uhusiano wake na Marekani katika mkutano huo. Saudia ndilo taifa la kwanza la ziara ya kigeni ya Trump. Taarifa ya Ofisi ya Rais Bashir ilisema kuwa rais huyo aliomba msamaha kwa Mfalme Salma wa Saudia kwa kushindwa kuhudhuria mkutano huo wa Riyadh. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa juu ya uamuzi huo. Waziri wa masuala ya mataifa ya kigeni, Taha al-Hussein, atamwakilisha. Mwaka 2002 na 2010, mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita (ICC) ilitoa agizo la kukamatwa kwa Rais Bashir kwa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhaifu dhidi ya binadamu katika eneo la Darfur, ambapo takriban watu 300,000 waliuawa.
kimataifa
Msanii huyo ambaye aliteka nyoyo za waamini wengi alipotea miaka ya hivi karibuni baada ya kukumbwa na misukosuko ikiwemo kashfa mbalimbali za utapeli, mbali na kuzindua albamu yake atapamba tamasha hilo ambalo linawahusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.Mkurugenzi wa Msama Promosheni ambaye ndiye muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema:“Ni wazi ukimya wa Rose Muhando ulisababishwa na yeye mwenyewe kwa sababu kuna kipindi alikuwa ameendekeza tabia ya utapeli kwa mashabiki wake na baadhi ya mameneja.“Pia kulikuwa na kesi nyingi sana polisi zilikuwa zikimhusu, lakini kwa sasa amerudi tena kundini, alianguka kwa sasa amesimama tena, mashabiki wake wampokee ili aendelee kuwaburudisha mashabiki wake.“Natumaini hii ni habari njema kwa mashabiki wa injili kwa sababu nyimbo za Rose Muhando zimekuwa zinapendwa na kuchezwa na watu wa kila rika na kila dini kutokana na uzuri wake,” alisema Msama.Pia Msama alisema kuwa tamasha la mwaka huu kuna utofauti wa eneo la tukio kwa ajili ya Tamasha la Pasaka lakini ubora wa tamasha ni uleule na burudani ni ileile. Aprili 2 tamasha hilo la Pasaka litafanyika tena kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
michezo
KILO 300 za mbegu za korosho zimekabidhiwa kwa wananchi kata ya Miyombweni wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuzalisha miche 55,000 msimu ujao wa kilimo kwa kata hiyo pekee.Akikabidhi mbegu hizo jana, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune aliwataka wakazi wilayani hapa kuchangamkia kilimo cha zao hilo kwa kupanda miche kwenye mashamba yao, maeneo ya mipaka na pia majumbani.Mfune alisema korosho ni kati ya mazao yenye faida kubwa kwa sasa kwa mtu mmoja mmoja, kwa serikali na inaweza kuwa chanzo kizuri cha kukuza makusanyo ya halmashauri ikitunzwa. Aliwataka wakazi wa Wilaya ya Mbarali kupanda zao la korosho kwenye mashamba yao na maeneo yao ya makazi kujiongezea kipato.“Mikorosho ni kama miti ya kawaida, mbegu zimekuja za kutosha, muangalie maeneo yaliyo wazi muoteshe na nyumbani pia”, alisema.Alisema, baada ya miaka mitano, mtakuwa watu wengine kwani hilo ni zao jipya, kila mmoja ajaribu kujielimisha awe mkulima bora. Diwani wa Kata ya Miyombeni, Mustaulo Sanzala alisema wananchi ambao hawaamini kuhusu korosho wanaweza kwenda kujionea kwa wakulima ambao miti ya o imeanza kutoa matunda, na baada ya miaka mitano wataamini kupitia mikorosho iliyopandwa kipindi hiki.Diwani huyo alisema katika kulipa uzito wa kipekee zao la korosho, baadhi ya vijiji katika kata yake kikiwemo Mapogoro wamethubutu kugawa mashamba kwa wananchi walioonesha nia ya kulima zao hilo ili wapande kwa wingi.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbalari, Kivuma Msangi, Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya, Daniel Kamwela alisema hadi sasa wakulima 229 wamesajiliwa kwa uzalishaji wa zao la korosho na hekta 328 zimepandwa zao hilo kwa wilaya yote tangu kuanza kutolewa kwa hamasa.Awali kabla ya mkutano na wananchi Mkuu wa Wilaya alitembelea baadhi ya mashamba ya mikorosho ya wakulima Kata ya Miyombweni kukagua vitalu vya kuoteshea mbegu hiyo.Mwaka 2018/2019 halmashauri iliweza kununua kilo 300 za mbegu za korosho kugawa kwa wakulima, na mwaka 2019/2020 halmashauri imeweza kununua kilo 500 za mbegu za korosho zinazotegemea kuzalisha miche 70,000.
kitaifa
RAIS John Magufuli amemtumbua Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafi pa kutokana na kukosekana kwake katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Kijiji cha Chukuku kilichopo Masasi mkoani humo.Aidha, amewashukia viongozi wa Wilaya ya Nachingwea akiwamo Mkuu wa Wilaya hiyo, Rukia Muwango pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (DED), Bakari Bakari kwa kushindwa kutekeleza kwa wakati ujenzi wa soko na stendi la wilaya jambo lililowafanya wananchi kutangatanga.Aidha, amemjia juu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kwa kushindwa kusimamia maelekezo anayoyatoa kwa watendaji hao hali iliyosababisha miradi hiyo ya maendeleo kusimama huku mkuu wa wilaya hiyo akibainisha kuwa chanzo cha hatua hiyo ni migogoro iliyopo baina yao.Akiwa Chukuku, Rais Magufuli alimtumbua Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara baada ya kumuita mkuu huyo ili kumpa jukumu la kuwakamata viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) vya mkoa huo wanaodaiwa kutafuna kiasi cha Sh milioni 80 za wakulima hao mwaka 2017.Baada ya kupokea taarifa hizo kutoka kwa Diwani wa kata hiyo, Rais Magufuli alimuita Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Blasius Chatanda na kumuagiza kuhakikisha anawakamata viongozi hao na kisha alimuita Kamanda huyo wa Takukuru ambaye hata hivyo hakuonekana kuwepo katika mkutano huo. Kutokana na hatua hiyo, Rais Magufuli alimpigia simu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, na kumuagiza kumteua kamanda mwingine wa mkoa huyo na kumpeleka haraka mkoani Mtwara ili kwenda kushirikiana na RPC huyo kushughulikia suala hilo.Akiwa Nachingwea aliposimama na kuzungumza na wananchi akiwa njiani kwenda Masasi, ambako pamoja na mambo mengine alipokea kero mbalimbali za wananchi wa eneo hilo likiwamo soko na stendi, aliwashukia DC, DED pamoja na RC Zambi kwa kutosimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Awali wananchi hao wakiongozwa na mzee aliyetambulika kwa jina moja la Mkanjauka, walimweleza Rais juu ya kukwama kwa ujenzi wa soko na stendi, hivyo kushindwa kufanya shughuli zao za biashara na usafiri. Kutokana na malalamiko hayo, Rais Magufuli aliagiza apelekwe katika eneo la soko linalotajwa kutumia kiasi cha Sh milioni 71 kwa ajili ya ukarabati wake na kumshukia DED Bakari juu ya gharama halisi za ujenzi huo, hatua iliyowafurahisha wananchi hao na kumshangilia.Baada ya kutembelea soko hilo, Rais Magufuli alimuhoji mkurugenzi mtendaji huyo kuhusu kuchelewa kwa ujenzi wa soko hilo na stendi ikizingatiwa kuwa halmashauri hiyo inapokea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na zile zinazotokana na mapato yake ya ndani.DED huyo alisema wanakwama kwa sababu mapato ya ndani ni madogo, lakini akadai kuwa fedha nyingine zimekwenda kujenga wodi ya wazazi, jambo alilopingwa na Rais Magufuli akieleza kuwa anachofahamu fedha za ujenzi wa wodi hiyo zilitoka Hazina, suala lililothibitishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile.Aidha, Rais Magufuli alipomhoji mkuu wa wilaya hiyo kwa nini ameshindwa kusimamia ujenzi huo, aliyedai chanzo cha uchelewaji huo ni kutokuwepo kwa maelewano baina ya ofisi yake, Mkurugenzi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, maelezo yaliyomkera rais na kumuhoji inakuaje ashindwe wakati yeye ndiyo mwenyekiti wake.Kutokana na hali hiyo, aliwaagiza wote; RC Zambi, DC Muwango na DED Bakari kuhakikisha wanasimamia maagizo hayo vinginevyo wajiondoe wenyewe katika nafasi zao kabla hajawachukulia hatua pale itakapobainika kuwa wameshindwa kuyatekeleza.Akiwa Ndanda, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Blasius Byakanwa, kubaki hapo na kushughulikia suala la gharama kubwa za Hospitali Teule ya Ndanda ambayo serikali inagharamia dawa na mishahara. Kwa heshima ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, William Mkapa ambaye ni mwenyeji wa Masasa akitokea Kijiji cha Lupaso, amechangia Sh milioni 100 kwa Shule ya Sekondari ya Ndanda ambayo rais huyo mstaafu alisoma ili zifanyiwe ukarabati. Pia alitoa Sh milioni moja kwa wanafunzi kufanya sherehe.
kitaifa
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema hakuna migogoro ndani ya chama hicho kama inavyotafsiriwa na kutahadharisha wanachama wa chama hicho kuachana mara moja na matamko yasiyo na tija na kwamba atakayekiuka agizo lake atatumbuliwa.Bashiru aliyasema hayo jana wakati akifungua fremu za biashara za CCM zilizopo mkoani Dodoma ambapo amesema kwa kiwango chochote kile si sahihi kusema CCM kuna mgogoro na kwamba ni kuota ndoto za mchana kwani hakuna kitu kama hicho.“Kwa kiwango chochote kile kusema CCM kimenuka, msomi yeyote, mchambuzi yeyote, mwana historia yeyote, mwanasiasa yeyote makini, Mtanzania yeyote makini hawezi kuthubutu au kuota.“Chama hiki kwa historia yake, kwa itikadi yake, kwa safu yake ya uongozi, kwa mshikamano wake, kudhani kuwa eti kinameguka, ni ndoto na ndio maana natumia neno jepesi hao wanaodhani hivyo ni wapumbavu.“Mtu yeyote mwenye akili timamu hata kama ana chuki na wana CCM, anapaswa kufahamu kuwa chama chetu bado ni madhubuti, na uongozi wetu bado ni imara, na Mwenyekiti wetu (John Magufuli) bado ni jasiri, ana afya njema, akili yake ni madhubuti, ana nia njema ya kujenga taifa,” alisema Dk Bashiru.Kauli ya Dk Bashiru imekuja siku chache baada ya kuwepo kwa tetesi ya kuwepo kwa migogoro ndani ya chama hicho kwa kudaiwa kuwa kuna pande zimegawanyika na hivyo kuwa katika hatari ya kumeguka.Akizungumzia namna chama hicho kinavyojadili masuala yake ya ndani, Dk Bashiru alisema zipo taratibu za kukosoana kwa nidhamu ndani ya chama na kwamba hawapingi kukosolewa lakini iwe kwa nidhamu na si kejeli.“Na ole wake mwana CCM abainike anafanya malumbano ya kirejareja tutachukua hatua, kuna wakati watu wanaweza kutumia upuuzi unaoendelea kujifanya wao ndio makada kuliko wengine kutafuta kiki za kisiasa.“Wanaleta clip (kanda fupi za video) wanauza kwangu nitawafukuza, tuna kanuni na taratibu zetu, tuna miiko yetu, ole wake mwana CCM yeyote, kusaka kiki za kisiasa ili achaguliwe kwenye serikali za mtaa hapana atatimuliwa.”Alisema anaunga mkono tamko la vijana wa CCM Dodoma ambao walimpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na kwamba uchaguzi ujao watakuwa bega kwa bega kuhakikisha anapata kura za kishindo.“Nimekuja hapa pia kuwapongeza kwa azimio lenu la jana (juzi), na mimi niliyepata azimio hilo kuwa wote mpo nyuma ya Rais wetu, haitoshi kumpongeza Rais wetu, haitoshi kusema tunampenda, haitoshi kusema tupo pamoja, semeni matokeo ya kazi yake,” alisema na kuongeza;“Msipoteze muda kulumbana, kuweni wavumilivu, siasa za ushindani zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu lakini msiwe waoga, sisi uongozi mzima wa chama chetu, mimi ndio Katibu Mkuu, chama chetu ni imara kimuundo, kimfumo, kiitikadi, kifalsafa, kiuongozi. Wapuuzeni hao wapumbavu,” alisema bila kufafanua.Alisema viongozi wa CCM hawaogopi kukosolewa lakini hawapo tayari kudharauliwa, kutukanwa na kubezwa na kuitwa majina ya kejeli kwa watu ambao hawana shukrani, na kwamba hawajafunzwa hivyo.“Hatujazoea hivyo, ninachowaomba wana CCM jifunzeni kutoka kwa kiongozi wenu Rais Magufuli ambaye wakati wote hana muda wa malumbano, amekuwa akivumilia wanaomtusi wengine wenye umri wa watoto wake, amewavumilia na yupo tayari kuwasamehe pia, lakini kwa kufanya hivyo si kwamba ni muoga,” alisisitiza.Alisema kazi ya kujenga chama ni ya kufa kupona kwa wana CCM wote, kazi ya kutetea na kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ni kazi ya kufa na kupona kwa kila mwana CCM, kazi ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania ni kazi ya kufa na kupona kwa wana CCM wote, lakini pia kazi ya kulinda ushindi wa chama ni kazi ya kufa kupona ya wana CCM wote pia.“Mimi ni mwalimu wa Kiswahili, sasa kuna wakati mwingine ukichambua misamiati inayotumika kutangazia dunia kuwa CCM kuna mpasuko tena si wa kawaida ni wa mwaka, kwamba CCM imetumbuka na kutumbuliwa na kila aina ya kejeli kwa kweli wapuuzeni hao wapumbavu.“Mwalimu Nyerere alishatuasa tujisahihishe, kujisahihisha ni kujiimarisha, kujikosoa, tukosoane kwa adabu, nidhamu, tuache utoto.”Alisema CCM ni chama cha siasa, lakini tofauti na vyama vingine vyote Afrika, ni chama cha siasa cha ukombozi si chama cha siasa cha upuuzi, na kwamba anayechokozwa namba moja ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ni yeye na kwamba hachokozeki.“Na chini yangu kuna wakurugenzi wanaonisaidia, ngazi ya mkoa ni Katibu wa chama cha Mkoa, msichokozeke, ukichokozeka nitakuonya mara ya kwanza, ya pili ya tatu nakutumbua, kwa kuwa umebeba dhamana kubwa ya chama chetu, shughuli zote za chama ikiwemo kampeni za chama,” alionya.Bushiru alisisitiza hakuna ruhusa ya kupambana na malumbano, na badala yake waachane na hao wanaobwabwaja kitoto toto kwani watachoka wenyewe.“Ukitaka kujua mchezo wa kitoto wapinzani wameanza kuchangamkia maana wao wanacheza kindimu ndimu, sisi tupo viwango vya juu, ‘game’ yetu ni ya viwango vya kimataifa, ukiona wapinzani wamechangamkia porojo na upuuzi ndani ya CCM ujue hao walioanzisha upuuzi huo hawakitakii mema chama chetu.“Hawajui vizuri itikadi ya chama chetu na taratibu zake, mchezo wa kitoto waachie vyama vya upinzani…baada ya mchezo huo kutangazwa na kucheza wamechangamkia na kuchafuka matope na mavumbi hawana viatu, hiyo ligi iliyotangazwa si saizi yetu,” alisema.Aliwaeleza wana CCM kuwa Mwenyekiti Magufuli hana mpango wa kulegeza vyuma na badala yake kuwataka wavumilie tu watumbuliwe wapone na chama kipone na kuongeza; ‘nongwa kubwa hakuna sijui nini wala nini vyuma vimekaza kweli kweli.“Nikimpa Mhazini hapa kipaza sauti aseme kabla ya mfumo huu wa kubana wezi kuanzishwa na John Magufuli, akaunti ya chama ilikuwa na chini ya shilingi bilioni moja, mishahara ililipwa tarehe 40 hadi 50, na inalipwa kwa mkono.“Lakini sasa hivi kwenye akaunti kuna zaidi ya Sh bilioni 22, tunalipa mishahara kwa wakati, tunaendesha uchaguzi, tunaendesha gharama zote, tumenunua vifaa vyote na tunafanya uchaguzi hatujaomba sehemu yoyote, sasa mkisikia michwa inapiga kelele msishangae imelewa dawa,” alisema na kushangiliwa na wanachama wa chama hicho.Alisema ndani ya chama uongozi ni kunufaisha walio wengi, na kuwa hayo ndio makosa ya Rais Magufuli, na watu wenye kuhukumu ni wananchi, na kuwataka wanachama wa chama hicho kutopoteza muda kumsemea Rais.“Msipoteze muda kumsemea Rais Magufuli atajisemea yeye, vitendo vyake, misimamo yake itajisemea, sisi kazi yetu ni kuungana kwa pamoja kukihami chama chetu, chama hiki si cha Magufuli, maana nasikia kauli ya Mwenyekiti…Mwenyekiti peke yake, Mwenyekiti na chama chote na wananchi kwa ujumla,” alisema.
kitaifa
Asha Bani, Dar es Salaam Muungano wa Asasi za Kiraia zaidi ya 200 umekabidhi andiko lao kuhusu janga la virusi vya corona pamoja na mkakati wake wa utekelezaji. Akikabidhi andiko hilo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema kwa kuzingatia majukumu ya msingi ya Azaki kuna maeneo mapana ambayo wamepanga kushirikiana na serikali ni pamoja na uhamasishaji wa umma kuzuia maambukizi, mabadiliko ya kimfumo na sera. Mengine ni toaji wa huduma kama vile kuchangia vifaa tiba, elimu kwa umma vifaa vya usafi, utoaji wa misaada wa kisheria kwa waathirika, chakula, kisaikolojia, tafiti na tathmini za madhara. “Ufuatiliaji na uangalizi wa utoaji wa huduma za afya, kushauri na kusaidia pale penye changamoto zinazojitokeza pamoja na mikakati mingine,” ameelekeza Olengurumwa. Naye Naibu Waziri wa Afya, Dk. Ndugulile amesema changamoto za madaktari na wauguzi serikali inaendelea kutatua na kuhakikisha wanaagiza vifaa vya kutosha ili kujikinga na maradhi hayo. “Tunafahamu kuna changamoto mbalimbali za kawaida lakini serikali imejipanga kuhakikisha tunapambana nazo ingawa uhitaji wa vifaa hivyo ni mkubwa. “Changamoto ya vifaa kinga ni ya kidunia na si tu Tanzania na haikwepeki lakini sio sababu ya Watanzania kukosa huduma hospitalini kwa kuwa wahudumu hawana vifaa,” amesema.
kitaifa
WATU milioni 1.3 wanakufa kutokana na ajali za barabarani kila mwaka duniani, ambao ni sawa na watu 3,611 kila siku na kati yao asilimia 90 wanatoka katika nchi zinazoendelea Tanzania ikiwamo.Akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya usalama barabarani mkoani hapa jana, Mery Kessy, kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO alisema idadi hiyo ya vifo ni kubwa hivyo ni lazima juhudi zifanyike kuvipunguza.“Ndio maana WHO imeandaa mafunzo haya kwa ajili ya waandishi wa habari ili kuwapa utaalamu wa namna ya kuandika habari za usalama wa barabara ili kusaidia umma kujua athari za ajali hizo,” alisema.Kessy alisema takwimu hizo zinazotolewa na shirika hilo kila baada ya miaka miwili, zinaonesha kwamba, licha ya nchi zinazoendelea kuongoza kwa vifo na majeruhi wa ajali za barabarani, lakini ndizo zinazomiliki vyombo vichache vya usafiri kwa asilimia 10 tu.“Nchi zinazoendelea zinaongoza kwa kuua nguvu kazi kubwa kwani wengi wanaopoteza maisha ni watoto wa miaka mitano hadi 29 ambao ndio nguvu kazi inayotegemewa katika ujenzi wa uchumi wa nchi,” alisema.Alisema licha ya kupoteza nguvu kazi, lakini pia ajali hizo zinayatia hasara kubwa mataifa mengi, zikigharimu asilimia tatu ya Pato la Taifa (GDP). Naye mtaalamu kutoka Taasisi ha Helme Vaccune Tanzania, Alpherio Nchimbi, alisema kutokana na ajali kupoteza nguvukazi kubwa, Umoja wa Mataifa (UN) umeweka mkakati wa miaka 10 kuanzia mwaka 2011 hadi 2020.Alisema mkakati huo una lengo la kupunguza vifo na ajali barabarani, kuweka usimamizi wa usalama barabarani, usafiri salama, uendeshaji makini, vifaa salama vya barabarani, usalama wa watumiaji barabara na utoaji huduma baada ya kupata ajali.Alisema kwa hapa nchini kampeni za kupunguza ajali za barabarani zilifika bungeni na Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu, alichaguliwa kuwa balozi wa kampeni ya usalama barabarani pamoja na watu wengine 120.Akizungumza nafasi ya vyombo vya habari katika kupashana habari za usalama barabarani, Godwin Assenga, kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) alisema waandishi wanatakiwa kujiunga katika mitandao ya kijamii ambayo inatumiwa na vijana wengi duniani ili kutoa elimu hiyo.
kitaifa
TIMU nne zinazopeperusha bendera ya nchi kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Kombe la Shirikisho leo zinatarajiwa kuingia uwanjani kwenye michezo ya raundi ya pili ya marudio kwa hatua ya awali kuendeleza kampeni ya kusaka ushindi utakaowawezesha kusonga mbele.Timu nne zinazoiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo zinazotarajiwa kushuka viwanjani leo na kesho ni Yanga na Simba upande wa Ligi ya Mabingwa, na Azam FC na KMC upande wa Kombe la Shirikisho Afrika.Timu hizo zinaingia kwenye mechi hizo za marudiano baada ya michezo yao ya awali kwa asilimia kubwa kutawala sare isipokuwa Azam FC pekee, ambao walianza vibaya kwa kupoteza ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Fasili Ketema ya Ethiopia.Huku Simba wakiwa ugenini walitoka suluhu dhidi ya UD Songo ya nchini Msumbiji sawa na KMC waliotoka na matokeo kama hayo dhidi ya wenyeji wao As Kigali ya Rwanda, Yanga wakilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Township Rollers wakiwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Licha ya kwamba mchezo wa mpira huwa unadunda na kuleta matokeo ambayo hayakutarajiwa kwenye uwanja wa nyumbani, lakini wanapaswa kutumia nguvu ya mashabiki kwa kuanikiza kuwapa sapoti wachezaji kupata nguvu ya kupambana bila kuchoka ili kupata ushindi. Ukiachilia mbali mashabiki, kwa kipindi cha wiki moja kilichopita kila timu imefanya maboresho kwenye kikosi chake, ikiwemo kupata mechi za kirafiki kujiweka sawa kabla ya kuvaana na wapinzani wao.Timu zote hizo zina kila sababu ya kupambana kusaka ushindi bila kujali watakuwa kwenye uwanja wa ugenini au nyumbani kuhakikisha wanafanya vizuri kuendelea kulinda nafasi iliyopata nchini ya kuingiza klabu nne kwenye michuano hiyo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma tulipokuwa tunaingiza timu mbili. Makala haya yanakuletea tathmini fupi kwa kila mchezo na nini kila timu inapaswa kufanya kuhakikisha hairudii tena makosa yaliyopita ili kuiwezesha kupata ushindi katika mchezo wa wiki hii na kuondoka na ushindi.Simba v UD Songo SIMBA ambao ni mabingwa wa tetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanatarajiwa kushuka kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakabili wapinzani wao Songo kutoka nchini Msumbiji, hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa wababe hao kukutana, kwani kwenye mechi ya awali wawili hao walitoka suluhu mechi iliyopigwa ugenini kwenye mji wa Beira.Katika mchezo huo, Simba wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana historia waliyojijengea msimu uliopita kwa kufanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo kwa faida ya kutumia vema uwanja huo na nguvu ya mashabiki wa timu hiyo ambao wanajitokeza kwa wingi kuanikiza. Ingawa wapinzani wao hao wataingia kwenye mchezo huo wakiwa wamejipanga huku wakijua wazi Simba wakiwa nyumbani wanakuwa na nguvu ya kucheza.Kwa kutambua hilo, Simba wanahitaji kupata mabao ya mapema hali inyoweza kuwachanganya wapinzani wao na kutoka mchezoni faida ambayo inaweza kuwanufaisha na kuweza kupata ushindi wa mabao mengi kasha kutinga hatua inayofuata. Kwenye mechi iliyopita, Simba walionekana kukosa muunganiko mzuri kutoka sehemu ya katikati hadi sehemu ya kumalizia hali iliyochangia washambuliaji wa timu hiyo kama Meddie Kagere na John Bocco kukosa mipira ambayo ingeweza kuwa na manufaa na kuweza kupata ushindi ambao ungekuwa na faida kwa wekundu hao.Kupitia maandalizi waliyoyafanya kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, kikosi hicho kimeonekana kuimarika, jambo ambalo lilipongezwa na kocha wa kikosi hicho, Patrick Aussems aliyedai kwamba hayo ni maendeleo mazuri kuelekea kwenye mchezo huo wa narudiano kesho. Yanga v Township Rollers Yanga wapo ugenini nchini Botswana na leo jioni wanatarajiwa kushuka uwanjani kuwakabili wenyeji Township Rollers.Mchezo wa mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatazamiwa kuwa mgumu kwao kwa kuwa walipokuwa kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya awali walitoka sare ya kufungana bao 1-1, huku Rollers wakitangulia kupata bao kipindi cha kwanza na Yanga kusawazisha kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti. Pamoja na Yanga kuanzia nyumbani na nguvu ya mashabiki wao lakini walipambana vya kutosha kutafuta ushindi lakini wapinzani wao hao walionekana kuwa imara kwa kuzima mashambulizi yaliyokuwa yanaelekezwa langoni kwao.Ni mechi ya kufa na kupona kwa Yanga ambao wanahitaji ushindi wa mabao kuweza kujihakikishia kupata ushindi, jambo ambalo linawezekana kwao kwa kuwa kwa kipindi cha wiki moja iliyopita walienda kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ambako walipata michezo miwili ya kujiweka sawa kabla ya kukutana na wapinzani wao hao kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kupigwa leo kule Gaborone nchini Botswana.Kwenye mchezo uliopita Yanga walionekana kuwa na matatizo ya kikosi hicho kwa kukosa muunganiko na umakini wa kumalizia nafasi zilizopatikana hasa kwenye sehemu ya kumalizia kufunga. Naamini kupitia michezo ya majaribio waliyokwishapata kupitia kocha wa kikosi hicho Mwinyi Zahera wana uwezo mkubwa wa kupata matokeo kwa kuwa kipindi cha maandalizi hatakuwa amefanya maboresho ya kikosi hicho.Hiyo ni mara ya pili kwa Yanga kukutana na wapinzani wao hao, kwani mwaka juzi walikutana katika uwanja huo huo na matokeo yalikuwa sare ya kufungana bao 1-1, hali iliyowafanya wenyeji Township Rollers kufanikiwa kusonga mbele kwa faida ya ushindi walioupata ugenini. Azam Fc V Fasil Ketema Licha ya Ketema kufanikiwa kushinda ushindi kiduchu kwa bao 1-0 wakiwa kwao nchini Ethiopia, bado Azam wanapewa nafasi kubwa ya kuweza kupindua matokeo hayo na kuibuka na ushindi utakaowafanya kusonga mbele.Kwa kuwa walipokutana kwenye mechi hiyo ya awali, wawili hao walionekana kutokupishana kwenye kiwango cha kumiliki mchezo, hivyo Azam wana kila sababu ya kupindua matokeo hayo leo jioni kwenye Uwanja wao wa Azam Complex kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 kujihakikishia kusonga mbele. Hata historia yao bado Azam inawabeba wakiwa kwenye uwanja huo mara nyingi wanaibuka na ushindi kwenye kipindi chote ambacho timu hiyo ilikuwa inashiriki michuano hiyo ilikuwa na rekodi ya kutumia vema uwanja huo ambao ni machinjio yao.KMC v As Kigali KMC walitarajiwa jana kuingia kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakabili wapinzani wao As Kigali kutoka nchini Rwanda, hatua hiyo inakuja baada ya timu hiyo kuanza vyema ugenini kwa kutoka suluhu ugenini. Pamoja na kwamba KMC kukosa uzoefu kwenye michuano hiyo lakini bado walipewa nafasi kubwa ya kuweza kuwatibulia wapinzani wao hao kutoka Rwanda na hiyo inaleta taswira ya mechi ya awali iliyopigwa Kigali hadi mechi hiyo inakamilika wawili hao wakitoka suluhu.
michezo
Na FLORENCE SANAWA, TANDAHIMBA MKUU wa Wilaya ya Tandahimba, Sebastian Waryuba, ameshtushwa na taarifa ya hali ya hewa inayoonyesha kutakuwa na mvua chache mwaka huu. Kutokana na hali hiyo, amewaagiza madiwani wilayani hapa kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kulima mazao ya muda mfupi kwa ajili ya kukabiliana na njaa. Mkuu huyo wa wilaya alitoa maagizo hayo juzi wakati wa kikao cha baraza la madiwani. Kwa mujibu wa Waryuba, kitendo cha wakulima wilayani hapa kutegemea korosho kama zao la biashara, kinaweza kusababisha uhaba wa chakula utakaoathiri wananchi wengi. “Madiwani hakikisheni mnatoa elimu itakayowasaidia wananchi kupanda na kukuza mazao mengine yasiyokuwa ya biashara kama mihogo, mahindi na mtama. “Nasema hivyo kwa sababu taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa, inasema mvua zitakuwa chache ndiyo maana nasema taarifa hiyo inapaswa kufanyiwa kazi ili kuondoa tatizo la njaa linaloweza kuikumba halmashauri yetu kama hatua hazitachukuliwa haraka. “Ufikie wakati wakulima wasione aibu kupanda mihogo kwa sababu tumeshuhudia mashamba mengi ya korosho yakiwa na nafasi kubwa kati ya mkorosho na mkorosho. “Tutumie nafasi hizo kwa kupanda mazao tofauti sehemu ambazo kivuli hakitaweza kuathiri mazao hayo,” alisema Waryuba. Naye Diwani wa Kata ya Mchichira, Ashunga Ngope, alisema wakulima wengi wilayani humo wamekuwa na kawaida ya kulima korosho peke yake na kusahau kilimo cha mazao mchanganyiko. Kutokana na hali hiyo, aliwataka wakulima hao waanze kulima na mazao mengine ili waweze kukabiliana na njaa inayoweza kutokea wakati wowote. Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, Said Msomoka, alisema agizo hilo la mkuu wa wilaya lazima lifanyiwe kazi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu hiyo ili kuongeza uelewa katika kilimo.
kitaifa
SAKATA la Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, linazidi kuchukua sura mpya, baada ya suala hilo kuibuliwa upya bungeni.Polisi mkoani Dodoma wamepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo kupinga uamuzi wa Bunge.Jana Bunge lililazimika kufafanua upya suala la uwasilishwaji wa Ripoti ya CAG), likieleza kuwa serikali haijakiuka misingi ya kikatiba inayotaka ripoti hiyo iwasilishwe ndani ya siku saba baada ya kuanza kwa vikao vya Bunge baada ya kukabidhiwa kwa Rais.Kauli hiyo ya Bunge ilitolewa jana kutokana na muongozo ulioombwa na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), aliyedai kwa nini kwenye orodha ya shughuli za Bunge jana, hakukuwa na uwasilishwaji wa ripoti hiyo kama ambavyo Katiba inavyotaka. Akiomba muongozo huo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, Mnyika alisema:“Mapema leo (jana) asubuhi tumekabidhiwa orodha ya shughuli za leo ambayo pamoja na mambo mengine kulikuwa na hati ya kuwasilisha mezani.“Lakini Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba ya nchi Ibara ya 143 ibara ndogo ya 4 inasema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), atawasilisha kwa Rais kila taarifa itakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya pili,” amesema.Amesema baada ya Rais kupokea taarifa hiyo, atawaagiza watu wanaohusika wakaiwasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge, kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na iwasilishwe katika kikao hicho, kabla haijapita siku saba tangu siku iliyoanza kikao.“Endapo Rais hatochukua hatua ya kuwasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge CAG atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge au Naibu Spika, ikiwa kiti cha spika kipo wazi au ikiwa kwa sababu zozote spika hawezi kutekeleza shughuli zake, basi ataiwasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge,” alieleza..Alisema kwa sababu taarifa iliyotolewa na ofisi ya CAG inaonesha kwamba Machi 28 mwaka huu, Rais alipokea ripoti za ukaguzi kutoka kwa CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2018 na kikao cha kwanza cha Bunge kilianza Aprili 2, mwaka huu, bado taarifa hiyo haijawasilishwa ndani ya Bunge. Mnyika aliongeza:“Naomba muongozo wako ni kwa nini katika orodha ya shughuli za leo (jana) hakuna ripoti ya CAG kwenye hati zilizowasilishwa mezani. Ni tarehe ngapi hasa Rais ataagiza wanaohusika walete ripoti ya CAG bungeni kabla haijapita siku saba ambazo rais anatakiwa kwa mujibu wa Katiba kuwasilisha ripoti bungeni?”Kutokana na muongozo wa Mnyika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, aliomba muongozo akieleza kuwa Mnyika anataka kulipotosha Bunge.“Kwa mujibu wa utaratibu wa shughuli za Bunge katika mijadala inayoendelea leo (jana), Mnyika ameonesha kutafsiri Katiba, amejua kunukuu vifungu vya sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, lakini hakwenda mbali zaidi kusoma sheria zingine zinazoambatana na maagizo hayo ya kikatiba na sheria katika kufanya tafsiri za siku ambazo zimeandikwa kwenye katiba na sheria husika,” alisema.Alisema Mnyika anataka kuonesha kama serikali haitaki kuwajibika katika suala hilo.“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba muongozo wako linapotokea jambo kama hili, kiti chako kipo tayari kumtafsiria Mnyika, tafsiri ya sheria hizo ili asiendelee kulipotosha Bunge na akatuacha serikali tuendelee kujipanga kwa kuzingatia sheria na taratibu husika katika utekelezaji wa jambo hili,” alihitimisha.Akijibu muongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Chenge alisema Katiba lazima isomwe na sheria nyingine ili kutoa tafsiri.“Katiba kama ulivyoisoma lazima uisome na sheria nyingine. Na sheria moja inayotuongoza ni sheria ya tasfiri za maneno yote ambayo yametumika kwenye sheria, sura namba moja ndio inayoumika.Chenge aliongeza: “Kwa hiyo kwanza, jambo lenye halikutokea bungeni mapema leo (jana), kwenye Order Paper (orodha ya shughuli za Bunge) hakuna kitu kama hicho. Nakusihi sana (Mnyika) uende ukasome sheria ya tafsiri inapoeleza siku. Serikali haijaenda nje ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa Katiba. Tangu Bunge kuazimia kutofanya kazi na CAG Jumanne wiki iliyopita, kumeibuka sintofahamu ya namna ambavyo ripoti ya ukaguzi itakavyowasilishwa
kitaifa
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amepongeza utendaji kazi wa mgodi wa kuzalisha makaa ya mawe wa Kambas uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma na kuitaka migodi mingine nchini kuiga mfano kwenye uchimbaji madini kutoka kampuni hiyo.Biteko amesema hayo katika ziara yake katika mgodi huo uliopo kijiji cha Maniamba wilayani Songea, Ruvuma kukagua uchimbaji madini pamoja na kutatua changamoto zilizopo.Aliambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, maofisa Madini wa Songea, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya ya Songea.Baada ya kupokea taarifa ya uchimbaji madini katika mgodi huo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa mgodi huo, Yahya Yusuph Kambaulaya, Biteko aliupongeza mgodi huo kwa kuzalisha makaa ya mawe na kuuza ndani ya muda mfupi tangu imeanza uchimbaji Desemba mwaka jana.Aliutaka mgodi huo kuunganisha leseni zake 14 za madini ili kuwa na wachimbaji wa kati na wakubwa na kuzidi kuongeza mapato Serikalini.“Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 ni rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Ndani ya kipindi kifupi wameanza kuchimba kwa mafanikio makubwa, kutoa ajira kwa wazawa na kushiriki katika shughuli za huduma za jamii. Nazitaka kampuni za madini nchini kuiga mfano wa kampuni hii,” amesema Biteko.Amesema, anatarajia kuona mgodi wa Kambas unakua na kuitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ya Songea na Ofisa Madini wakiulea mgodi huo kwa kufuata sheria.Biteko alitaka halmashauri kutumia fedha za mapato ya mgodi huo kwa uwekezaji mbadala wa shule, vituo vya afya na barabara ili kuacha kumbukumbu nzuri katika vizazi vijavyo.Katika hatua nyingine, Biteko aliutaka mgodi wa Kambas kulipa kodi stahiki serikalini baada ya kuuza katika kituo cha mwisho badala ya mauzo ya hapo hapo mgodini (net back value).Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mdeme amempongeza Waziri Biteko kwa usimamizi makini wa sekta ya madini nchini akisema, ofisi yake ipo tayari kushirikiana na mwekezaji huyo pamoja na kutatua changamoto zitakazojitokeza.Akiwasilisha taarifa ya uzalishaji, Mtendaji Mkuu wa Mgodi wa Kuzalisha Makaa ya Mawe wa Kambas, Yahya Kambaulaya amesema, uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi huo umekuwa ukiongezeka siku hadi siku ambapo mpaka sasa wameshachimba tani 5,138.Amesema, tani hizo zilichimbwa kwa miezi mitatu, Desemba 2017, Mei, 2018 na Juni, 2018 na Januari hadi Aprili, 2018 uchimbaji makaa ya mawe ulisimama kutokana na mvua kubwa.Amesema, kuanzia Julai 2018 uzalishaji wa makaa ya mawe kwa siku ni tani 200 na malengo ya mgodi ni kuzalisha tani 600 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwezi mgodi utakuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya tani 18,000 hadi 21,000.Akielezea manufaa ya mgodi wa Kambas, Kambaulaya amesema mgodi umeweza kulipa serikalini kodi mbalimbali inayotokana na mauzo ya makaa ikiwa ni pamoja na mrabaha na ada ya ukaguzi Sh milioni 16, sh milioni 4.1 katika kijiji cha Maniamba za huduma za jamii.
uchumi
CHRISTOPHER MSEKENA LICHA ya kuonekana kuwa kwenye ndoa yenye furaha, staa wa Bongo Fleva na mjasiliamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, ameweka wazi ukatili mkubwa anaofanyiwa na mumewe, Ashrafu Sadiki maarufu kama Uchebe kwa miaka kadhaa sasa. Shilole ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga ukatili wanaofanyiwa wanawake kwenye ndoa zao, amewaomba radhi mashabiki kwa kutetea wengine huku yeye mwenyewe akichezea kichapo kila uchwao kutoka kwa Uchebe. Akizungumzia ukatili anaofanyiwa na mumewe, Shilole alisema Uchebe amekuwa akimpiga na kuondoka zake bila kujali anaendeleaje huku akibaki kuuguzwa na watu baki, ukatili uliofanya ndoa yao ikose uhai na furaha. “Watoto waniangalia kama baba na mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, sitaweza, Uchebe ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu kama vile utu wangu, mali zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja lakini  hilo halikuwahi kuzuia vipigo, dharau na usaliti,” alisema Shilole. Akizungumzia sababu za kupigwa vibaya na kuumizwa siku mbili zilizopita Shilole alisema: “Baada ya kutoka sabasaba kutafutia watoto wangu na kumtafutia yeye nilipigwa sana na sababu za kupigwa ni migogoro midogo ya kawaida ambayo ipo kwenye kila ndoa, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana tena namuheshimu sana lakini ‘solution’ aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini,” alisema. Aidha Shilole ambaye alifunga ndoa ya Uchebe, Desemba 7, 2017 jijini Dar es Salaam alitangaza kuvunja ndoa hiyo akisema: “Maisha yangu ni maisha ya watu kwa kiasi kikubwa, jamii inanitazama kama mfano, nimefika mwisho na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama mke wa Uchebe ila Mama aliyeamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake. Katika kutaka kuthibista hilo, MTANZANIA lilimtafuta Uchebe kwa namba yake inayoishia 83, simu iliita bil haikupokewa na baadaye haikupatikana kabisa mpaka tunaingia mitamboni. Tukio hilo ambalo Shilole ameamua kulitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram, limewaibua mastaa kibao kama vile Flaviana Matata, Nay wa Mitego, Lulu Diva, Jacqueline Wolper, Riyama Ally, Linex, Rose Ndauka, Ben Pol, Aunt Ezekiel, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Nandy, Kajala, Marioo, Rosa Ree, Aika, Batuli na wengineo wengi waliompa pole na kupinga ukatili huo.
afya
Vincent Bossua alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea klabu hiyo yenye masikani yake katika makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani akichukua nafasi ya Joseph Zuttah kutoka Ghana ambaye alisitishwa mkataba wake.Pluijm alisema kuwa Bossua yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kinachoshiriki mashindano ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika na uwezo wake utasaidia Yanga zaidi kwenye mashindano ya kimataifa.“Ni beki mwenye uzoefu mkubwa sana, ana nguvu, na anatumia akili pia, ni mzuri katika kukaba lakini pia kuanzisha mashambulizi, lakini pia ni mzuri kwa mipira ya juu,” alisema Pluijm.Alisema kwamba kuongezeka kwa Bossua kutaifanya Yanga kuwa na mabeki wanne wa kati na kuwataja kuwa ni nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub’Cannavaro’, Kelvin Yondani na Mbuyu Twite ambaye pia anaweza kucheza nafasi hiyo.“Yondani na Cannavaro wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu sana, kama binadamu nao huchoka wakati mwingine, sasa Bossua ataleta changamoto mpya na zaidi atawafanya kupata muda wa kupumzika,”alijinasibu Pluijm.Mbali na Bossua Yanga pia ilimsajili Thabani Kamusoko ambaye ni kiungo mkabaji kutoka klabu ya Platnum ya Zimbabwe.
michezo
ADAM MKWEPU NA MITANDAO KOCHA wa vinara wa Ligi Kuu England, Leicester City, Claudio Ranieri, ana mtihani mgumu leo pale timu yake itakapoikabili Everton kwenye moja ya michezo ya Ligi Kuu England. Ushindi wa Leicester City utakua zawadi tosha kwa mashabiki wake kuelekea Sikukuu ya Krismasi kwani watakua wamejihakikishia timu yao kukaa kileleni mwa ligi wakati wa sherehe hizo. Leicester City inajitupa uwanjani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi, Chelsea, mchezo ambao ulipelekea kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, kufungashiwa virago. Washambuliaji, Riyad Mahrez pamoja na Jamie Vardy, wameonekana kuwa na mvuto wa kipekee pamoja na kumpa imani kocha wao baada ya Vardy kufunga mabao 15 huku akitabiriwa kufunga zaidi ya mabao 18 msimu huu. Wasiwasi upo juu ya klabu ya Everton kama inaweza kuiondoa Leicester City kileleni kabla ya Krismasi na hii ni endapo ama Arsenal au Manchester City wakishinda michezo yao. Kocha wa Everton, Javier Martinez, anakiri kwamba ikiwa kama klabu inaongozwa na bajeti ndogo inaweza kusababisha matokeo ya mshangao kwa wapenda soka. Martinez alidai Leicester City inastahili kuwa nafasi waliyonayo sasa kutokana na kujipanga vema baada ya kugundua mapungufu yao kabla ya kuingia ligi kuu. Ranieri anatamani wachezaji wake kufanya jitihada za kutafuta ushindi katika mechi hiyo kwa kuwa anafahamu si rahisi kuifunga timu hiyo. Everton haikufungwa katika mechi nane ilizocheza katika michuano yote lakini wameweza kupata pointi tatu katika michezo miwili ya mwisho kati ya sita walizocheza. Kumbukumbu zinaonesha kwamba klabu ya Leicester City inakuwa katika wakati mgumu inapokutana na Everton kwasababu kati ya mechi 20 walizowahi kucheza, walifanikiwa kushinda moja tu. Ingawa katika kumbukumbu hizo timu hiyo haikuwahi kufungwa katika michezo 11 waliyocheza nyumbani ambayo walifanikiwa kushinda saba kati ya hizo. Martinez alithibitisha mlinzi wa klabu hiyo, John Stones, atacheza mechi hiyo baada ya kukosa mchezo dhidi ya Norwich City kutokana na kuwa majeruhi. Southampton vs Tottenham Baada ya klabu zote kuambulia kichapo wiki iliyopita, hivyo matumaini yao yamekuwa katika mchezo huu ambao utawafanya kurudisha hari ya mchezo. Spurs chini ya Mauricio Pochettino ilifungwa 2-1 na Newcastle United na ni dhahiri wamepania kushinda mchezo wa leo ili kutinga ‘top four’. Southampton nao pia wamekuwa wakipata matokeo mabovu katika mechi za hivi karibuni na timu hiyo inayofundishwa na Ronald Koeman haina budi kushinda kufufua matumaini yao kucheza michuano ya Ulaya.
michezo
  Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MGANGA wa Tiba asilia, Ashura Mkasanga (33), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma akituhumiwa kumuua Mariamu Saidi (17), mkazi wa Mkoa wa Kigoma kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kisha kukichoma moto. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema mwili wa marehemu ulikutwa kwa mganga huyo katika Kitongoji cha Chang’ombe, Kijiji cha Chamwino Ikulu wilayani Chamwino. Alisema mwili huo ulikutwa ukiwa umekatwa shingo kwa kutenganishwa na kiwiliwili na kichwa kikiwa kimechomwa moto na kubaki fuvu lisiloweza kutambulika sura yake. Kamanda huyo alisema baadhi ya sehemu za mwili wa marehemu ambazo ni mkono wa kushoto, shingo, kifua na sehemu za siri ziliunguzwa kwa moto. “Mnamo tarehe 8 mwezi huu majira ya saa nne usiku katika Kitongoji cha Chang’ombe, Kijiji cha Chamwino Ikulu, mtu mmoja mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mariamu Saidi (17), mkazi wa Kigoma aliuawa kwa kukatwa shingo yake,” alisema. Kamanda Mambosasa alisema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa mganga huyo asiye na kibali cha kuendesha shughuli za tiba asili, analaza wagonjwa nyumbani kwake, kufanya matambiko na kupiga ramli chonganishi. Alisema wamewakamata watu 11 wakiwamo wasaidizi wa mganga huyo ambao ni Victor Daniel (24) na mume wa mganga huyo, Noel Mazengo(30)
kitaifa
NAIROBI, KENYA RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameomba radhi kwa kutojiandaa na mwitikio mkubwa wa wapiga kura uliolazimisha kufutwa kwa uchaguzi wa mchujo wa chama chake nchi nzima. Kenyatta alisema chama cha Jubilee kitafanya uchaguzi mpya wa mchujo leo na kesho. “Viongozi hawakutarajia mwitikio mkubwa wa watu kujitokeza kupiga kura na kusababisha upungufu wa karatasi za kura,” alisema. Hilo lilisababisha vurugu kote nchini wakati wagombea walipowatuhumu wenzao kwa uchakachuaji. Kenyatta alitarajia mwitikio wa asilimia 25 lakini uliotokea ulikuwa wa zaidi ya asilimia 70. “Kura za mchujo kwa kawaida hazivuti mwitikio mkubwa wa wapiga kura kama tulioshuhudia Ijumaa iliyopita na hapo inaonesha hatukuwa tumejiandaa vyema," alisema. Kati ya kaunti 21, ambazo kura za mchujo zilikuwa zifanyike, ni chache zilizoweza kuendesha. Mchakato huo unafanyika kupata wagombea wa chama watakaochuana na wenzao pinzani wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti, ambapo pia rais mpya atachaguliwa. Mwongo uliopita, watu zaidi ya 1,300 walikufa katika machafuko yaliyotokana na uchaguzi wenye utata, lakini wa karibuni uliofanyika mwaka 2013 ulikuwa wa amani.
kimataifa