content
stringlengths 1k
24.2k
| category
stringclasses 6
values |
---|---|
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema mgawanyo wa ajira mpya za walimu utazingatia vipaumbele vya maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu hasa maeneo ya vijiji ambayo yana changamoto ya miundo mbinu ya barabara na mahitaji mengine ya kijamii.Waziri Ndalichako amesema hayo akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi wa wilaya na walimu wa shule ya sekondari Janda wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma na kusema kuwa maeneo yenye upungufu mkubwa ndiyo kipaumbele kwa sasa katika mgawanyo wa walimu ili kuleta uwiano wa kitaaluma kwa nchi nzima.Kutokana na hilo alitoa agizo kwa maofisa elimu nchi nzima kuhakikisha wanatuma taarifa zao za mahitaji na upungufu wa walimu hadi kufikia Machi 15 mwaka huu na baada ya muda huo hakuna taarifa ya upungufu wa walimu itakayopokelewa kwake.Waziri Ndalichako amesema, wakati serikali inatekeleza mpango wa elimu bila malipo, uboreshaji wa miundombinu ya shule kupitia mpango wa lipa kwa matokeo lakini pia inaliangalia suala la taaluma kwa kuhakikisha kunakuwepo na walimu wa kutosha katika shule zote nchini na itaendelea kuajiri walimu wapya kila wakati kulingana na upatikanaji wa fedha serikalini.Katika hatua nyingine, waziri huyo wa elimu alieleza kusikitishwa na ufaulu duni wa wanafunzi wa kike mkoani Kigoma na kutaka wadau kuungana kuhakikisha wanasimamia kwa karibu mkakati wa kuinua ufaulu wa wanafunzi wa kike mkoani humo.Akiwa mkoani humo, Waziri Ndalichako alisema amepokea taarifa za wilaya kuhusu hali ya elimu mkoani humo ambapo taarifa za ufaulu kwa wanafunzi wa kike zimekuwa za kusikitisha zikionesha wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakikatisha masomo na kushindwa kuwa na nafasi ya kutosha kuendelea na masomo ya juu.Sambamba na hilo, ametoa mwito kwa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii na kuweka dhamira ya dhati katika masomo yao, jambo ambalo litawafanya wafanye vizuri kwenye masomo yao na kuwa viongozi wa baadaye ili kutoa mchango wao kwa taifa.Hata hivyo, Waziri Ndalichako alikataa kukubaliana na changamoto za uduni wa miundo mbinu ya shule na kusema kwamba mbona wanaofaulu pia wanatoka kwenye shule hizo hizo ambazo wanafunzi wengine wanalalamikia.Katika hatua nyingine, waziri huyo wa elimu alisema serikali imetoa kiasi cha Sh bilioni moja kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule za sekondari wilayani Buhigwe kupitia mpango wa Lipa kwa Matokeo (EP4R) huku akiahidi kutoa kiasi cha Sh milioni 100 kwa shule ya sekondari ya Janda na compyuta moja.Awali akitoa taarifa kwa waziri huyo, Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe, Marycelina Mbehoma alisema kuwa kumekuwa na ufaulu duni wa wanafunzi wa kike katika wilaya hiyo sababu kubwa, ikiwa ni kupewa majukumu ya kuwa walezi wa familia na hivyo kudondoka kimasomo.Mbehoma alisema kuwa hali hiyo inafanya wanafunzi kuingia kwenye mtego wa ujauzito au kuacha masomo ambapo halmashauri imeanza kutekeleza mkakati wa kimkoa wa kuinua ufaulu wa wanafunzi wa kike ujulikanao kama wanafunzi wa kike wanaweza wapewe nafasi. | kitaifa |
Anna
Potinus – Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, amewajia juu wanasiasa wanaoingilia masuala ya uchambuzi wa zabuni ambapo amewataka kuachana na tabia hiyo na kuipa nafasi serikali kfanya kazi yake. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 29, wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 katika ziwa Victoria litakalojengwa kwa muda wa miezi 48. “Huu mkataba wa Kigongo-Busisi nikiwaambia yaliyotekea ni maajabu, sasa hivi inakua ni tabia tenda ikishatangazwa watu wanaanza kujipanga kumwambia mkandarasi ili wapate hela hiyo ni tabia chafu tena wengine ni viongozi kama mimi na bahati nzuri hawaji kwangu kwasababu wataambulia matusi,” amesema. “Tenda zikishatangazwa kuna watu wanaanza kujiendekeza, mimi ninasema
hata angekuwa ni mtoto wangu ukiniletea hilo siku hiyo na nyumbani kwangu
unahama, sasa niwaombe wale ambao walizoea kule tulikotoka kila tenda
ikitangazwa wanaanza kupitapita waache serikali ifanye kazi yake ili wakikosea
taratibu zipo tuwafunge,” amesema. “Wengine ninawaheshimu lakini
wanataka kuingilia masuala ya uchambuzi wa tenda, jamani sio kazi ya wanasiasa
tuachie serikali ifanye kazi yake, huyu Mfugale anapambana na mengi wengine
hawana aibu wanampigia simu, wanamuandikia barua na wengine wanamshtaki kwenye Taasisi
za serikali, hatuendi hivyo uliza kwanza unachotaka kufanya,” amesema. Aidha amesema daraja hilo la Kigongo-Busisi linalotarajia kugharimu bilioni
592, litaunganisha vema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa usafiri wa
ardhini na hivyo kupunguza muda wa kusafiri na kuleta tija katika kufanya
biashara miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. | kitaifa |
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) limekaribisha mradi wa utafiti wa kisomi, kabla ya uchimbaji wa urana (uranium) utakaohusisha Tanzania, Malawi, Namibia na Zambia.Akifungua jana mkutano wa siku moja wa wasomi na wadau wengine wa mazingira jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka, alisifu mradi huo kwa maelezo kwamba utafanya tafiti za kisomi, ambazo zitatoa mwelekeo thabiti wa kutunza mazingira ya Tanzania katika uchimbaji wa madini ya urana. "Huu ni mradi mzuri kwa sababu tafiti za kisomi zitasaidia kutupa upeo wa kulinda mazingira ya nchi yetu na nchi tatu zilizomo katika mradi huu," Dk Gwamaka. Alisema kuwa tafiti za kisomi ni muhimu na itaongeza uelewa miongoni mwa washiriki.Dk Gwamaka alisema kama wadau watakubaliana basi uchimbaji wa urana, utakuwa na manufaa kwa nchi zote husika na hasa kwa kuwa urani inatoa mchango mkubwa katika kuzalisha umeme. Warsha ya aina hiyo inafanyika pia katika nchi za Malawi, Namibia na Zambia, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuwa na uchimbaji, uchakataji, usafirishaji na matumizi salama ya urana.Wajumbe walitoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wizara ya Madini na NEMC, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, zinazojishughulisha na madini pamoja na mazingira. Nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma, ndicho kinachoratibu na kukusanya taarifa zitakazotoa majibu iwapo ni busara na ni namna gani urani ichimbwe hapa Tanzania au vinginevyo.Washiriki katika warsha hiyo walijadili changamoto zinazojitokeza katika uchimbaji wa madini, hasa urani kwa sababu urani ni madini yenye madhara makubwa kwa viumbe na mazingira na hasa kama uchimbaji unafanywa kabla ya utafiti wa kutosha. Mkuu wa Kitivo cha Sayansi Mazingira na Teknolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Meserecordias Lema alisema washirika walipata nafasi ya kujadili namna bora ya kuboresha sheria ili ziendane na sheria za nchi husika."Warsha hii ililenga kutafuta njia bora ya kufanyia maboresho ya sheria katika uchimbaji wa urani kusudi mataifa yote manne yawe na mfumo wa sheria mmoja ili kuondokana na madhara ya urani katika nyanja mbalimbali," Dk Lema alisisitiza. Alisema wajumbe walijikita katika ulinzi na usalama kwenye uchimbaji, uchakataji na usafirishaji na matumizi salama ya urani. | kitaifa |
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo, ambalo limebeba kauli mbiu ya ‘Mrembo na Mazingira Safi’ alisema yeye kama waziri mwenye dhamana atayaangalia mashindano hayo kwa umakini mkubwa.“Watanzania mrudishe tena imani yenu kwa mashindano haya na kuhakikisha yanafanyika kwani madhumuni ni kuibua vipaji na kutengeneza ajira mbalimbali,” alisema Nnape.Aidha, Nape aliwataka wasimamizi wa mashindano hayo yanayoandaliwa na Kampuni ya Lino International Agency chini ya Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga kuhakikisha wanayasimamia mashindano hayo na kuzingatia madhumuni yake.Amewataka waandaaji wa mashindano hayo kusahau matatizo waliyopitia kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mashindano hayo na serikali ipo tayari kuwaunga mkono katika kufanikisha mashindano hayo.Mkurugenzi wa Lino International Agency na Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema wameamua kufanya mabadiliko makubwa katika kamati hiyo na kuteua wajumbe wapya 10 wa kuiongoza.Lundenga aliwataja wajumbe hao kuwa ni Lucas Ruta ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Mohamed Bawaziri, Shah Ramadhan, Ham Hashim, Almish Hazal ambaye ni mwanasaikolojia, Charles Hamka ambaye ni Mhazini wa Kamati, Mary Emmanuel, Msemaji wa Kamati Fance Nkuhi, Ojambi Masaburi pamoja na Deo Kaptein.Uzinduzi huo ulisindikizwa na burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa Kizazi kipya Linah Sanga na kundi la Wanne Star. | michezo |
LONDON, Uingereza KWA kutumia gazeti la the Telegraph, Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson amesema kuna masuala ”zaidi tunapaswa kufanya” kupambana na ubaguzi wa rangi. Kutokana na hali hiyo, Johnson ametangaza tume mpya kutazama ”aina zote za hali ya kutokuwepo kwa usawa.” Johnson alisema ” hakuna mtu yeyote anayejali kuhusu nchi hii anayeweza kupuuza maandamano ya kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi yaliyojitokeza baada ya kifo cha George Floyd. Lakini mbunge wa chama cha Labour, David Lammy alisema kuwa ni wakati wa kuchukua hatua sasa na si tathimini nyingine. Alisema Uingereza isijaribu ”kuandika upya historia ya zamani” kwa kuondoa alama za kihistoria. Urithi wa Uingereza uachwe ”kwa amani” aliongeza. Johnson alikemea ”Magenge ya watu wa mrengo wa kuliza” waliohusika kwenye maandamano ya vurugu siku ya Jumamosi , yaliyosababisha zaidi ya watu 100 kukamatwa jijini London, baada ya maelfu kukusanyika wakisema wanazilinda sanamu. Hatua hiyo ilikuja baada ya sanamu moja kwenye viwanja vya bunge kuandikwa maneno kwa rangi ” alikuwa mbaguzi” mwishoni mwa juma lililopita mjini Bristol, waandamanaji dhidi ya ubaguzi wa rangi waliangusha sanamu ya mfanyabiashara wa utumwa Edward Colston. Maelfu ya watu wameandamana nchini Uingereza kama sehemu ya maandamano ya Black Lives Matter, baada ya kifo cha Floyd mjini Minneapolis mwezi uliopita. Alisema anaunda tume kutazama hali ya kutokuwa na usawa kwa kuwa ”haina maana tu kusema kuwa tumefanikiwa kupambana na ubaguzi wa rangi”. Aliandika: ”Kuna mengi ya kufanya na tutayafanya. Ni wakati kwa tume kutathimini suala ya usawa katika ajira, afya, elimu na maeneo mengine.” Maswali kuhusu kutokuepo kwa usawa katika sekta ya afya, yamekuwa yakijitokeza wakati wa janga la virusi vya corona, baada ya takwimu kuonesha kuwa watu wa jamii ya wachache wamekua wakipoteza maisha zaidi kutokana na virusi vya corona. Waziri kivuli wa Sheria, David Lammy alisema idadi kadhaa ya malalamiko kuhusu ubaguzi wa rangi yametolewa, kama vile ripoti yake mwenyewe kuhusu wanavyotendewa watu weusi, raia wa Asia na watu wa jamii ya walio wachache ”Unaweza kuelewa kwanini mara nyingine Uingereza tunataka takwimu, data, lakini hatutaki kuchukua hatua,” aliiambia BBC Radio 4. ”Watu weusi hawatafuti visingizio kama Boris anavyoashiria, wanaandamana hasa kwa sababu muda wa tathimini umekwisha na sasa ni muda wa kuchukua hatua.” Waziri huyo kivuli ametoa wito kwa bunge na mapendekezo ya tathimini zilizofanyika awali kufanyiwa kazi. Simon Woolley, mwanzilishi wa operesheni ya Black Vote na mwenyekiti wa chombo kinachotazama masuala ya usawa , amesema ” ametiwa moyo” na tangazo kuhusu kuundwa kwa tume. | kimataifa |
KADRI siku zinavyoenda, teknolojia inazidi kukua. Wataalamu wa sayansi nao wanazidi kubuni vitu mbalimbali vinavyo0saidia kurahisisha maisha katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya.Betri ya moyo ambayo kitabibu huitwa ‘pacemaker’ ni miongoni mwa vifaa ambavyo vimebuniwa ili kumsaidia mtu ambaye moyo wake unashindwa kuzalisha umeme wa kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili.Taarifa zilizopo zinabainisha kuwa, binadamu wa kwanza kunufaika na tiba hiyo, aliwekewa kifaa hicho mwaka 1960 ilikimsaidie kusukuma damu katika moyo ulioshindwa kusukuma damu kwa kutumia umeme wa asili.Tangu kuanzishwa kwa huduma za upandikizaji wa betri ya moyo kwenye mwili wa binadamu, watu zaidi ya milioni tatu dunianihuwekewa kifaa hicho kila mwaka. Miongoni mwa watu maarufu waliopandikizwa mashine hiyo ya moyo kifua ni kocha aliyewahi kuifundisha klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza, Sir Alex Ferguson aliyewekewa kifaa hicho mwaka 2003.Huu ni mwaka wa 17 Ferguson akiishi na kifaa hicho mwilini. Mwingine ni wanamuziki maarufu, Sir Elton John aliyewekewa kifaa hicho mwaka 1999. Huyu alikuwa kwenye safari ya kwenda kwenye sherehe ya David Beckam.Alipofika uwanja wa ndege, alijisikia vibaya na baada ya kufanyiwa vipimo, iligundulika kuwa mapigo yake ya moyo hayafanyi kazi vizuri hivyo, alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa hicho.Aidha, yupo Dick Chen, aliyekuwa Naibu Rais wa Marekani, katika uongozi wa Rais George Bush. Hata hivyo, licha ya kifaa hicho kuwa mkombozi kwa watu wenye matatizo ya umeme wa moyo, inaelezwa kuwa, baadhi ya wagonjwa wanaowekewa kifaa hicho hupata sonona na baadhi yao huishia kujiua.Hayo yalibainika katika utafiti uliofanywa na jopo la madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikina na Kitengo cha Magonjwa ya Akili katika Hosptiali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kupitishwa rasmi Novemba 29 mwaka jana.Akizungumzia utafiti huo, Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dk Pedro Pallangyo anasema wagonjwa wenye shida ya moyo wanawekewa kifaa hicho maalum (pacemaker) ili kuwasaidia moyo kupiga mapigo yanayokidhi mahitaji yao.“Hata hivyo, siyo wagonjwa wote ambao wakiwekewa wanapokea vifaa hivi kama ipasavyo kiakili; tafiti zimeonesha baadhi ya wagonjwa hupata hofu, sonona na wengine hata kujiua baada ya kuwekewa vifaa hicho,” anasema Dk Pallangyo.Anasema kwa wengi walioripotiwa kupata changamoto hiyo, imetokana na kujawa na hofu kubwa akimtolea mfano mzee wa miaka 83 aliyefikishwa hospitali hapo na kutibiwa kwa kuwekewa kifaa hicho, lakini baadae alikutwa amefariki kifo ambacho hakikueleweka.“Katika utafiti wetu, ‘case study’ yetu ilikuwa ni mzee wa miaka 83 ambaye alitokea Nyanda za Juu Kusini na kuletwa JKCI kwa uchunguzi zaidi,” anasema Pallagyo Anasema mzee huyo alifikishwa katika taasisi hiyo akiwa na maumivu kifuani na mwilini na pia alikuwa amepoteza fahamu kwa takribani miezi sita.Kwa mujibu wa Dk Pallangyo, historia yam zee huyo ilionesha alikuwa na matatizo hayo ya moyo kwa miaka tisa. Hata hivyo, walifanikiwa kumtibu na matarajio ya kumrudishia uhai yalikuwa makubwa, lakini mgonjwa alifariki baadaye kwa sababu ambazo hazikujulikana. Kutokana na hali hiyo Pallagyo anasema wagonjwa wanaowekewa betri ya moyo wanahitaji pia uchunguzi zaidi wa kisaikolojia ili kugundua matatizo ambayo hayajabainika.“Ni muhimu kufanya uchunguzi wa aina hii mapema na kuchukua hatua kwa wakati ili kuleta matokeo chanya katika matibabu,” anasema Anaongeza: “Mpaka sasa duniani kote watu watatu wameripotiwa kujiua baada ya kuwekewa betri na wawili kabla ya huyu wetu mzee wa Nyanda za Juu Kusini waliripotiwa kuwa na matatizo ya akili,” alisisitiza.Dk Pallagyo anasema chapisho hilo la JKCI kuhusu utafitiu ni la kwanza duniani kuhusisha mtu ambae hana historia ya magonjwa ya akili kujiua baada ya kuwekewa betri.“Kilichomuua mgonjwa siyo kifaa alichowekewa, bali ni mabadiliko ya kisaikolojia aliyopata mgonjwa baada ya kuwekewa kifaa,” anasisitiza na kuongeza “Fundisho hapa ni kwa watoa huduma na ndugu wa mgonjwa kuwa makini kugundua na kutoa msaada wa haraka kabla hayajatokea kama haya tuliyochapisha.”SONONA NI NINISonona ni mwitikio wa kihisia ambao hutokea kwa mtu baada ya kushuhudia tukio na kumsababishia maumivu makali. Chama Cha Tiba ya Magonjwa ya Akili cha Marekani (PTSD) kinaelezea kuwa matukio hayo humletea mtu hisia za hofu, mashaka, wasiwasi, kujitenga, kilio na mshituko na mwingine kuogopa kuwaona watu fulani au kutembelea maeneo ambayo matukio hayo yametokea.Aidha, sonona humfanya mtu kuwa mpweke, mwenye hofu, mashaka na asipopata matibabu anaweza kupata ugonjwa wa akili. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), sonona imeathiri watu takribani 300 milioni ambapo kila mwaka husababisha matukio karibu 800,000 ya watu kujiua duniani.MOYOHii ni ogani ya mwili inayoendesha mzunguko wa damu mwilini. Kazi yake kuu ni kusukuma damu kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.UMEME WA MOYOUmeme wa moyo ni mfumo wa kipekee, huweza kutolewa katika kiwango maalumu kinachowezesha misuli ya moyo yenye mpangilio sawa na yenye ufanisi. Mifumo hii inapokwenda isivyotakiwa, husababisha mgonjwa kuwekewa betri ya moyo ili kusaidia uzalishaji wa umeme katika moyo wake na hivyo, kutatua tatizo la mapigo yasiyo ya kawaida. Mashine hii ndiyo inamfanya kuendelea kuishi pasipo kupata mapigo ya moyo yasiyo ya kwaida. Mashine hii ndiyo mbadala wa kituo cha uzalishaji umeme wa moyo ili kuwezesha kuwapo kwa mapigo ya moyo yasiyo na hitilafu.Hitilifu yoyote katika mfumo wa umeme wa moyo na misuli ya chemba za moyo inayoletwa na magonjwa mbalimbali ya moyo, huweza kuathiri mwenendo wa mapigo ya moyo.SABABU ZA HITILAFUSababu kubwa ya kutokea hitilafu ya mapigo ya moyo inatajwa kuwa ni kuingiliwa mfumo mzima wa usambaaji wa umeme wa moyo. Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja magonjwa ya misuli ya moyo, matatizo ya kuzaliwa, shinikizo la damu, homa, matumizi ya tumbaku, ulevi wa kupindukia, historia ya kupata shambulizi la moyo na kuwahi kufanyiwa upasuaji wa moyo.Mambo mengine yanayoweza kuchangia ni pamoja na utumiaji wa vinywaji vyenye caffein, matibabu ya dawa ikiwamo kwinini na dawa ya pumu; mfano Aminophiline na kutowiana kwa chumvi na maji mwilini. Kadhalika, utumiaji wa dawa za kulevya na matatizo ya tezi inayozalisha homoni zinazochangia ukuaji mwili. Mara nyingine chanzo cha tatizo kinaweza kisigundulike moja kwa moja.Uwepo wa hitilafu ya mapigo ya moyo unaweza kusababisha mapigo ya moyo kuwa na kasi ya juu, kuwa na kasi ndogo au mapigo ya moyo kwenda pasipo mpangilio mzuri. Moyo huwa na misuli ambayo huwa na kazi ya kujikunja na kukunjuka ili kusukuma damu mwilini. Kila pigo moja la moyo huzalisha mtiririko wa haraka wa mapigo makuu mawili ya misuli ya chemba za moyo.Kwa kawaida, moyo una chemba nne, juu ziko mbili na chini mbili, chemba hizi zina misuli ambayo hutoa mapigo kwa ajili ya kusukuma damu. Pigo la kwanza la moyo hutokea katika chemba za juu; atria, wakati pigo la pili kusukuma damu hutokea katika chemba za chini ya moyo zijulikanazo kama ventriko.Chemba za juu hupokea damu inayoingia katika moyo na kuisukuma katika chemba za chini ambazo hupokea damu hiyo na kuisukuma kutoka ndani ya moyo kwenda katika mapafu na sehemu nyingine mwilini. Kwa kawaida mapigo ya moyo hudhibitiwa na nguvu ya msukumo wa umeme.Katika hali ya kawaida, nguvu msukumo wenye umeme hutolewa na kitu kilichopo kiasili katika moyo kijulikanacho kama ‘sinus node’. Kipo upande wa kulia wa moyo, chemba ya juu. Sinus node ni sawa na mashine ya pacemaker ambayo mwanadamu ametengenezewa kutatua hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo. Tatizo linapopata matibabu ya uhakika, ni mara chache linaweza kuhatarisha maisha. Hata madhara yake pamoja na kuwa ni makali, lakini yanazuilika kwa matibabu. Vipimo muhimu ambavyo hufanyika ni pamoja na kipimo cha ECG na ECHO vinavyobaini matatizo mbalimbali ya moyo.Mashine hii hupendekezwa na madaktari wa moyo kuwekewa mtu mwenye tatizo la kutoa mapigo ya moyo yenye kasi ndogo. Kwa kawaida, kasi ya mapigo kwa mtu aliyetulia ni kati ya 60-100 kwa dakika. Vilevile, inapendekezwa kutumika kwa mgonjwa mwenye kizuizi cha mpitisho wa umeme wa moyo. Hili ni tatizo linalotokana na kuingiliwa utiririkaji wa umeme inaposambaa au umeme kuwa mdogo.KUJIKINGAIli kuzuia matatizo hayo, inashauriwa kuepukana na mambo hatarishi yanayochangia kutokea kwa magonjwa ya moyo ikiwamo udhibiti wa uzito wa mwili, matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe kupita kiasi na matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, zingatia kula vyakula visivyo na mafuta mengi, tumia kwa wingi mboga za majani, matunda na epuka nafaka zilizokobolewa.Kumbuka pia kufanya mazoezi mara kwa mara. Inashauriwa kufanya uchunguzi wa afya ya moyo mara kwa mara, angalau mara moja ndani ya miezi sita ili kubaini matatizo ya moyo mapema kabla hayajaleta madhara. | kitaifa |
Ushindi huo wa Simba unaiwezesha timu hiyo kufikisha pointi 44, inaendelea kuwa nyuma ya Azam FC yenye pointi 45, lakini Wana lambalamba hao wamebaki na michezo miwili mkononi wakati wekundu wa Msimbazi wamebaki na mechi moja.Hata hivyo, pamoja na ushindi huo Simba bado ina nafasi finyu ya kumaliza ya pili kwani ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha pointi 47 huku ikiombea Azam ifungwe mechi zote.Kwa mara ya mwisho Simba ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara katika msimu wa 2011/12 na tangu wakati huo haijawahi kutwaa ubingwa huo.Azam FC inahitaji pointi tatu tu ili itemize pointi 48, ambazo haziwezi kufikiwa na Simba wala timu nyingine yoyote na hivyo kuifanya kumaliza ya pili nyuma ya Yanga iliyotwaa ubingwa mapema.Katika mchezo huo, Simba ndio ilikuwa ya kwanza kufunga bao katika dakika ya 49 kupitia kwa Ibrahim Ajibu baada ya kupata pasi ya Ramadhani Singano `Messi’.Azam FC nao walisawazisha katika dakika ya 62 mfungaji akiwa ni Mudathir Yahaya aliyeingia kipindi cha pili baada ya kupata pasi ya Kipre Tchetche.Dakika ya 75 Singano anaifungia Simba bao la pili akipiga mpira kutoka nje ya 18 baada ya kipa wa Azam FC kutoka nje ya goli. Azam FC waliongeza nguvu baada ya kumtoa Kavumbagu na kumuingiza John Boko, lakini mabadiliko hayo hayakuisaidia timu hiyo kwani jahazi lake lilizama.Mshambuliaji Mganda wa Simba Emmanuel Okwi nusura afunge bao katika dakika ya 68 baada ya kupiga shuti lililopanguliwa kifundi na kipa wa Azam FC Aishi Manula.Kutoka Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani wenyeji Coastal Union walichanua na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United. Matokeo hayo yameifanya Coastal Union kufikisha pointi 31 ikiwa katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo.Huko kwenye uwanja wa Manungu Turiani, wenyeji Mtibwa Sugar walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting.Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Mzamiru Yassin katika dakika ya 55 na Ame Ally katika dakika ya 65. Ushindi huo unaifanya Mtibwa iliyopo katika nafasi ya saba kwenye msimamo kufikisha pointi 31. | michezo |
MAHAKAMA ya Mwanzo Nunge, Manispaa ya Morogoro, imewahukumu kwenda jela miezi sita na kazi ngumu watu 22 baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya ngono na uzururaji.Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama hiyo, Emelia Mwambagi na wengi waliohukumiwa ni wasichana ambao waliangua vilio huku wakiomba kusamehewa. Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa kwa zaidi ya saa tano kabla ya kutolewa hukumu, ilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya washtakiwa hao maarufu kama ‘Dada poa na Kaka poa’ baada ya kukamatwa usiku wa Agosti 16, mwaka huu katika eneo la Kahumba mjini hapa.Hakimu Mwambagi alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa washtakiwa hao na wengine wanaotumia miili yao kujidhalilisha na kuwadhalilisha wazazi, ndugu na jamaa kwenye maeneo wanayotoka. Alisema washtakiwa wote waliokamatwa ni vijana wenye uwezo wa kufanya kazi za halali za kuwaingizia kipato, lakini wamekuwa wakizurura na wengine wakitumia vibaya miili yao kujidhalilisha.Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mwambagi, aliwaachia huru washtakiwa sita kutokana na kuridhishwa na utetezi wao na vielelezo walivyoviwasilisha mahakamani hapo kuwa hawahusiki na tuhuma hiyo. Katika utetezi wao, washtakiwa hao walidai walikamatwa kwenye nyumba za kulala wageni walipokwenda kujipumzisha baada ya kutoka safari, huku wengine wakidai kukamatwa katika maeneo yao ya kazi ikiwamo ya mama na baba lishe. | kitaifa |
Rais wa zamani wa Peru Alan García, amefariki dunia baada ya kujipiga risasi kabla ya kukamatwa na polisi waliokuwa wamewasili nyumbani kwake kwa ajili ya kumkamata juu ya mashtaka ya rushwa. Kifo cha García kimethibitishwa na Rais wa sasa wa Peru, Martín Vizcarra. Kabla
ya tukio hilo, maofisa wa polisi walikuwa wametumwa kumkamata Garcia nyumbani
kwake kwa madai hayo ya rushwa. Kwa
upande wa Waziri wa Mambo ya Ndani Carlos Morán aliwaambia waandishi wa habari
kuwa polisi walipofika, García aliomba kwenda kuoiga simu na kuingia ndani ya
chumba na kujifungia kwa ndani. Anasema
dakika chache baadaye, walisikia mlio wa risasi ukitokea katika chumba
alichokuwamo Garcia. Polisi
walilazimika kufungua mlango kwa nguvu na kumkuta García ameketi kwenye akiwa na jeraha la
risasi kwenye kichwa chake. Katibu
wa García, Ricardo Pinedo, alisema rais huyo wa zamani alikuwa na silaha nne au
tano nyumbani mwake, zawadi alizopata kutoka kwa wanajeshi, na kwamba alikuwa
ametumia mojawapo ya hizo silaha kujiua mwenyewe. Kupita
mtandao wa Twitter, Rais Vizcarra amesema “alishtushwa” na kifo cha rais
wa zamani na kutoa salam za pole kwa familia yake. García
alishtakiwa kwa kuchukua rushwa kutoka kampuni ya ujenzi wa Brazil Odebrecht,
shtaka ambalo awali aliwahi kulikana. García
aliwahi kuwa rais wa tangu 1985 hadi 1990 na kuongoza tena kuanzia 2006 hadi
2011. | kimataifa |
PATRICIA KIMELEMETA, IDARA ya Uhamiaji imekamata mitambo ya kughushi nyaraka mbalimbali za idara hiyo pamoja na mashine za kielektroniki (EFDs). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Usimamizi wa Mipaka, Samwel Magweiga alisema nyaraka hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kuikosesha serikali mapato stahiki. “Tumewakamata watu watano ambao walikuwa wakijifanya ni mawakala wa idara yetu na walikuwa wakiwatapeli wananchi kwa kujifanya ni maofisa wa idara ya uhamiaji wakati ni mapateli. “Mpaka sasa upelelezi umekamilika na kwamba wakati wowote tutawafikisha mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Magweiga. Alisema watu hao wamekuwa wakitumia mitambo mbalimbali ya kughushi zinazofanywa na idara hiyo huku wakijua kuwa wanachokifanya ni kinyume cha sheria. Licha ya mitambo hiyo, watu hao wamekutwa na nyaraka zinazoonyesha shughuli za serikali zikiwamo miradi ya maendeleo pamoja na mashine za kielektroniki (EFDs) zinazotumika kukusanya fedha za Serikali. Kutokana na hali hiyo, idara hiyo imepiga marufuku watu wote wanaojifanya mawakala wa idara hiyo na kufanya kazi zinazofanana na uhamiaji kinyume cha sheria na kuonya kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani. Alisema, wananchi wanaotaka huduma kutoka idara hiyo wanapaswa kufika kwenye ofisi za uhamiaji popote zilizopo ili waweze kuhudumiwa kwa mujibu wa sheria. Aliongeza kwamba ili kuepusha utapeli huo, wananchi wanapaswa kushirikiana na idara hiyo kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya watu wanaojifanya mawakala ili waweze kutafutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo. Alisema mpaka sasa idara hiyo imepata taarifa ya kuwepo kwa magenge ya wahalifu wanaotumia jina la idara hiyo kwa ajili ya kuwatapeli wananchi. | kitaifa |
Aveline kitomary Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
Aminieli Aligaeshi amesema hospitali hiyo kwa kushirikia na Taasisi ya Mifupa
(MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), inachukua tahadhari ya virusi vya corona
kwa kuhakikisha kila mmoja ananawa mikono kabla ya kuingia ndani ya hospitali
hiyo. Aligaeshi amesema hatua nyingine iliyochukuliwa ni kupunguza idadi ya
ndugu jamaa na marafiki ambao wanaenda kuona wagonjwa ambapo kwa sasa ni ndugu
wawili tu wataruhusiwa kumuona mgonjwa. “Tunawataka wafanyakazi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia
eneo la Muhimbili kunawa mikono kwa kutumia maji yenye dawa yaliyowekwa katika
maeneo mbalimbli ya taasisi hizo kabla na baada ya kuingia ndani ya Hospitali,
wodini na sehemu za kutolea huduma. “Tumeunda kikosi kazi kinachoratibu zoezi zima la tahadhari dhidi
ya Corona ambacho kinatoa mafunzo kwa wafanyakazi wote wa taasisi hizo,
wanafunzi, mafunzo kwa wakufunzi (ToT) watakaosaidia kuelimisha umma kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya. “Uongozi wa Taasisi hizi umekubaliana kwa kauli moja kuwa kuanzia sasa
wataruhusiwa ndugu wawili tu kwa kila mgonjwa mmoja wakati wa asubuhi na jioni
ambapo mchana ni mtu mmoja tu atakayeruhusiwa kupeleka chakula kwa mgonjwa ili
kupunguza msongamano mkubwa uliopo eneo la Muhimbili,” amesema Aligaeshi. Hata hivyo amewaomba wananchi kuwaunga mkono ili kuongeza tahadhari
zaidi. | afya |
['Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba kikosi chake chenye wachezaji wa umri mdogo kinaimarika kila uchao ikilinganishwa na vile walivyoanza msimu. ', 'United imeshinda mara moja katika mechi zake tano za ligi ya Uingereza na ilihitaji penalti kuishinda klabu ya daraja la kwanza ya Rochdale katika michuano ya Carabao siku ya Jumatano. ', "''Sijasema kwamba itakuwa rahisi msimu huu'' , alisema mkufunzi huyo wa Man United. ", "''Kutakuwa na changamoto. Tunaposhindwa mechi lazima tujiamini na kile tunachofanya''. ", 'Kikosi hicho cha Solkjaer ambacho kilishindwa 2-0 na West Ham wikendi iliopita , kitachuana na Arsenal katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatatu usiku. ', "''Utamaduni upo, hatuna tatizo na jinsi wachezaji wanachukulia kila mechi, na viwango'' , aliongezea. ", "''Unaweza kuona dhidi ya Astana na Rochdale, wanataka kucheza vizuri na mara nyengine wanaharakisha mashambulizi yao''.", 'Siku ya Jumanne, klabu hiyo ilitangaza mapato yaliovunja rekodi ya £627m. ', 'Baada ya kuifunga Chelsea magoli manne sufuri chini ya usimamizi wa Solskjaer klabu hiyo sasa ipo nafasi ya nane katika ligi na inawafuata viongozi Liverpool kwa pointi 10 baada ya mechi sita.', "''Mechi yoyote katika ligi ya Premia inaweza tukashinda na pia tunaweza kupoteza'', alisema Solskjaer. ", "Mara nyengine unasimama uwanjani ukiwa na furaha kwa kushinda mechi , mara nyengine umekasirika kwa kuwa umepoteza. Lazima tuonyesha picha nzuri''. ", "''Unaweza kuona jinsi tulivyoimarika katika safu ya ulinzi hapo ndipo tunapowekeza huku Aaron Bissaka na Harry Maguire wakiweka ulinzi wa kutosha. Hatufungwi magoli mengi''.", "''Tukisonga mbele, hiyo ndio safu iliokumbwa na majeraha chungu nzima. Paul Pogba, Anthony Martial, Marcus Rashford - tumekuwa na bahati mbaya. Haisaidii unapopoteza wachezaji - vijana hawa wanahitaji kupata mfumo wa kucheza''.", 'Solskjaer aliwashukuru mashabiki, ambao kikosi chao kilimaliza katika nafasi tatu za kwanza katika ligi ya Premia mara moja katika kipindi cha misimu sita iliopita na kutoa wito kwa mashabiki kuendelea kuisaidia timu hiyo ', 'Kijana Mason Greenwood alifunga kwa mara pili akiichezea United dhidi ya Rochdale katikati ya wiki kufuatia kukosekana kwa mshambuliaji Marcus Rashford na Martial.', 'Solskjaer alisema kwamba hawatawashiriikisha wachezaji wawili waliojeruhiwa dhidi ya Arsenal huku Paul Pogba akiwa katika mbio za kuwa tayari Jumatatu kufuatia jeraha la kifundo cha mguu.', 'Licha ya ukosefu, Solskjaer ana wasiwasi kumchezesha Green wood , 17 katika safu ya mashambulizi. ', "''Amethibitisha kwamba unapompata katika eneo hatari ni hatari sana'' , alisema Solskjaer. ", "''Kitu kilichonifurahisha kumuhusu ni kwamba hawezi kuharibu nafasi za kufunga, hivyobasi sina wasiwasi kumuhusu hata kidogo. Hatahivyo tumemzuia hatuwezi kumrusha katika safu ya mbele kila mara licha ya kwamba amethibitisha kwamba yuko tayari kila mara kucheza mbele''.", 'Wakati huohuo Luke Shaw amerudi katika mazoezi alisema Solskjaer na atarudi kabla ya likizo ya kimataifa mnamo mwezi Oktoba.'] | michezo |
Na CHRISTOPHER MSEKENA
YUMO kwenye orodha ya watangazaji wa burudani wanaofanya vizuri kwa sasa kupitia kipindi chake cha Papaso kikiwa na msisimko unaowavuta wasikilizaji wengi wasikilize TBC FM kila siku za wiki saa 1- 4 usiku, huyu ni D’ Jaro Arungu maarufu kama Baba Mzazi.
D’ Jaro Arungu ni mzaliwa wa Rorya mkoani Mara akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia yao, ni baba wa watoto watatu licha ya kwamba bado hajaoa.
Swaggaz limekutana na mtangazaji huyu na kupiga naye stori mbili tatu kuhusu maisha na mwenendo wa tasnia ya burudani kwa kuwa yeye ni mmoja wa wadau wenye ushawishi wa aina yake.
Swaggaz: Shabiki wa Papaso anataka kufahamu D’ Jaro ni nani, ametokea wapi na historia yako kwa kifupi.
D’Jaro Arungu: Safari yangu ilianzia Times FM nikiwa kama ripota wa habari za michezo kwa kujitolea baadaye nikaenda Kiss FM, Mwanza ila nilikaa kwa wiki mbili tu kwa sababu meneja wa vipindi aliniambia sina kipaji cha utangazaji ambapo hata aliyekuwa meneja wa vipindi wa Times FM aliwahi kunisimamisha licha ya kuwa nilikuwa najitolea.
Sikukata tamaa, nikakutana na Abdallah Mwaipaya wa Radio One, akaniambia niende PRT Radio (TBC FM kwa sasa), kwa kipindi hicho walikuwa na uhaba wa watangazaji, nilisita kwa sababu nilijiona sina vigezo kwa kuwa nilikuwa ndiyo nimemaliza kidato cha nne na kuchaguliwa kidato cha tano Benjamini Mkapa Sekondari ingawa sikumaliza kidato cha sita kwa sababu za kifamilia ambapo baba aliachishwa kazi akarudi kijijini na mama pamoja na wadogo zangu.
Mimi nikabaki Dar kuhangaika na maisha bila kusaidiwa na ndugu hata mmoja zaidi ya marafiki na watu baki.
Swaggaz: Ilikuwaje ulipofika kwenye usahili TBC FM?
D’Jaro Arungu: Usahili ulikuwa na watu wengi sana wenye elimu zao na ilikuwa inafanywa kwa awamu, mkiwa 100 mnachukuliwa watatu, baadaye kwa mtindo huohuo huo tukapatikana watu tisa.
Namkumbuka Jerry Muro, Gabriel Zakaria, Jamila Isdory na wengine na kati ya hao tukapita, mimi, Jerry Muro na yule dada.
Nawashukuru sana TBC kwa kuwa waliona kipaji changu na hawakunibania kama nilivyokuwa nabaniwa huko kwingine, ndiyo maana leo hii wengi wananitaka tena kwa dau kubwa ila nimekuwa mgumu kuhama TBC, naipenda kwa moyo wangu wote.
Swaggaz: Umefanya kazi na mastaa wengi, staa gani aliwahi kukuudhi katika kazi zako?
D’Jaro Arungu: Waliniudhi kipindi naanza kutangaza, ukiwaita kwa interview wana-promise then siku ya siku hawaji. Baadhi yao ni Profesa Jay, Juma Nature, Linex, Ali Kiba, Banana Zoro, MB Dog nk.
Niliwasamehe maana nilijua ipo siku watanitafuta wao, ila heshima sana kwa AY toka enzi hizo hadi sasa hakuwahi kukosa kipindi kama una interview naye na sasa wao ndiyo wanaomba waje tena foleni ni kubwa.
Swaggaz: Staa gani wa kike Bongo anakuvutia na je unatazama filamu za Kibongo na unawashauri nini wasanii?
D’Jaro Arungu: Kwanza sitazami kabisa filamu hivyo sina cha kuwashauri na mrembo anayenivutia ni Jokate Mwegelo.
Swaggaz: Umewahi kukutana na malalamiko ya wasanii kudai unawabania?
D’Jaro Arungu: Kwangu mimi hawajawahi kusema nawabania, wengi wamepita mkononi mwangu kama kina Diamond, Nay wa Mitego, 20%, marehemu Omary Omary na Dogo Mfaume, Timbulo, Best Naso, Chief Maker na wengine wengi na wanathamini mchango wangu.
Swaggaz: Watu gani ni muhimu kwenye safari yako ya utangazaji?
D’Jaro Arungu: Napenda nimshukuru mtangazaji wa Uhuru FM, Sigori Paul. Yeye na Paul James ‘PJ’ ndiyo walinipigania Times FM hadi nikaanza kuripoti habari za michezo kwa kujitolea ingawa nilipigwa chini baadaye.
Lakini leo hii ripoti za Ipsos zinaonyesha Baba Mzazi D’jaro Arungu ndiyo mtangazaji wa redio anayependwa zaidi na hata Tuzo za Watu zilionyesha hivyo ndiyo maana nilishinda na hivi majuzi tuzo za Tanzania Instagram Awards nilishinda kipengele cha ‘Best Male Presenter’.
Swaggaz: Una ushauri gani kwa vijana ambao wanakata tamaa wakikutana na magumu kwenye maisha?
D’Jaro Arungu: Nawaasa kutokukata tamaa mapema, leo hii nisingekuwa hapa na nimejiendeleza kusoma mpaka sasa nipo Chuo Kikuu cha Tumaini, namaliza mwakani mwezi Oktoba, Shahada ya Mawasiliano ya Umma. | burudani |
Kauli ya Mtangazaji wa Radio Clouds FM, Gardner G Habash kuhusiana na mtoto wake imezua mjada katika mitandao ya kijamii. Wengi wamemponda kuwa kauli hiyo haina maadili mazuri kwa mtoto huku wengine wakiona ni sahihi kwa kile alichokieleza. Baadhi ya magroup ya WhatsApp mjadala huo ulipamba moto kwa kile alichokieleza kuhusiana na mwanae huku wengine wakisambaza picha ambayo inaonyesha mwanae amemlalia. Gardner alisema anatamani mwanaye Karen awe na mahusiano na mtu mkubwa mwenye umri kama wake ‘Sugar dad’ ili amtunze. Alidai kuwa watu wa umri wa mtoto wake hawawezi kumuelewa wala kumsaidia chochote kwani wao wenyewe wanatafuta maisha. “Alafu umpe mzigo kama huu ataweza kulipa bill zake,” alieleza Gardner Baadhi ya mashabiki walichangia mjadala huo huku wengine wakimponda na wengine kumuambia ndio maana alitungiwa wimbo. Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, alisema kabila nyingi za Tanzania inaonyesha mtoto wa kile ni kitega uchumi cha mahari. “Unazani kuvaa shati, suruale, soksi na viatu alivyo design beberu humbadilisha mtu Mindset? Ndio hao waliotolewa bush lakini bush halijawatoka kichwani. Anauza mtoto wa kike kama nyama ya buchani,” aliandika Fatma. Baba Mpumbavu, Baba asiye na hekima Wala akili Ni Kama shimo la taka, daima hutoa harufu mbaya https://t.co/3fX19oaOx4 — Aneth Stanley (@AnethStanley) January 6, 2020 Kabila nyingi za #TZ zinaona watoto wa kike ni kitega UCHUMI cha Mahari. Unadhani kuvaa shati, suruali, soksi na viatu alivyo Design Beberu humbadilisha mtu MINDSET? Ndio hao walietolewa BUSH lakini BUSH halijatoka KICHWANI. Anauza mtoto wa kike kama nyama BUCHANI! Mxxx https://t.co/eE0wZxDaHt — fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) January 6, 2020 | burudani |
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema kikosi chake kilistahili kupata ushindi kwa sababu walicheza vizuri kuliko Yanga.Yanga na Simba walikutana Uwanja wa Taifa juzi katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wake mahiri, Meddie Kagere.Kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo zenye upinzani mkali kwenye soka la Tanzania, zilitoka sare ya bila ya kufungana.Aussems alisema baada ya mechi hiyo kuwa kikosi chake kilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na walistahili kupata ushindi walioupata.“Tulicheza soka la kuvutia kwa dakika zote za mchezo na ushindi wetu unaongeza morali kwa kikosi changu na kuendelea kujitengenezea mazingira mazuri kwenye michezo inayokuja,” amesema Aussems.Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kupoteza mchezo huo wa juzi kulisababishwa na wachezaji wake kukosa ubunifu wa kujua kama wapinzani wao wanamiliki mchezo na wafanyeje kuwadhibiti.“Nimekubali matokeo, Simba walistahili kushinda kwa kuwa walicheza vizuri katika kipindi chote cha mchezo na kwa upande wetu wachezaji walikosa umakini na ubunifu ni wakati gani tucheze kupata matokeo,” amesema Zahera.Ushindi huo umewafanya wekundu hao wa Msimbazi, Simba kurejea kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 39 baada ya kucheza michezo 16 .Huku Yanga wakiendelea kushika usukani kwa hazina ya pointi 58 baada ya kucheza michezo 24, licha ya kupoteza mchezo huo uliotawaliwa na Simba mwanzo mwisho.Huo ni mchezo wa pili kupoteza kwa vinara hao kwani mchezo wa awali walipoteza ugenini dhidi ya Stand United kwa bao 1-0 katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. | michezo |
MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM BAADA ya kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kibabe kwa kuichapa AS Vita mabao 2-1, Simba leo itajua itavaana na nani katika hatua hiyo. Saa chache kutoka sasa, droo ya robo fainali itapangwa, ambapo Simba itajua inavaana na nani kati ya vigogo watatu wa soka la Afrika ambao ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC), Wydad Casablanca ya Morocco au mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Esperance ya Tunisia. Simba ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D, nyuma ya Al Ahly ya Misri, hivyo kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Wekundu hao wa Msimbazi watakutana na moja ya timu hizo zilizoongoza makundi ya A, B na C. Kanuni za michuano hiyo zinaeleza wazi kuwa timu zote zilizomaliza nafasi ya pili zitawekwa katika chungu kimoja na zile zilizomaliza kinara zikiwekwa pia chungu kimoja. Kwa maana hiyo, Simba itakutana na moja kati ya timu kutoka Uarabuni, ambako kuna timu mbili za Wydad Casablanca na Esperance au DRC kuumana na TP Mazembe. Wydad Casablanca ilimaliza kinara wa kundi A, ikiwa na pointi 10 baada ya michezo sita, Esperance ilimaliza kinara wa kundi B, na pointi zake 14, huku TP Mazembe ikiwa mbabe wa kundi C ikiwa na pointi 11. Katika hatua hiyo ya robo fainali, Simba itaanzia nyumbani baada ya kumaliza nafasi ya pili, hivyo kinara wa kundi atapata faida ya kuanzia ugenini. Simba itaanzia kwenye uwanja wa nyumbani, ambapo imekuwa ikifanya vizuri kwa michezo yote dhidi ya wapinzani wao hatua ya kwanza na 16 bora. Timu hiyo ilianzia hatua ya awali ya michuano hiyo kwa kuvaana na Mbabane Swallows ya Eswatini, huku Simba wakianzia kwenye uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. Wekundu hao wa Msimbazi waliendeleza rekodi zao nzuri nyumbani katika mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza ya michuano dhidi ya Nkana Red Devils na kushinda kwa mabao 3-1 na kutinga hatua ya makundi. Katika hatua ya makundi, Simba ilikuwa miongoni mwa timu zilizonufaika na matumizi mazuri ya uwanja wa nyumbani kwa kuvuna pointi tisa, zilizowapeleka robo fainali ya michuano hiyo. Katika hatua hiyo, Simba ilianza kwa kuicharaza JS Saoura mabao 3-0, ikaichapa Al Ahly bao 1-0, kabla ya kufunga hesabu kwa kuiondoa AS Vita kwa mabao 2-1. Kuelekea hatua hiyo ya robo fainali, Mtanzania linakuletea takwimu za timu hizo tatu ambazo moja kati hizo itakutana na Simba. Wydad Casablanca Timu hiyo ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika walilolitwaa msimu uliopita baada ya kuilaza AS Vita kwa jumla ya mabao 4-3 katika michezo miwili ya fainali iliyochezwa nyumbani na ugenini. Wydad ilianza kwa kuchapwa mabao 3-1 katika fainali ya kwanza iliyochezwa jijini Kinshasa, kabla ya kupindua meza kwa kushinda mabao 3-0 nyumbani na kutawazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo. Wababe hao wa Morocco walianzia raundi ya kwanza ya michuano hii kwa kuvaana na Jaaraf ya Senegal, ambapo ilianza kushinda mabao 2-0 nyumbani, kabla ya kupoteza mchezo wa marudiano ugenini kwa mabao 3-1, lakini ilitinga hatua ya makundi kutokana na faida ya bao la ugenini. Timu hiyo ilipangwa kundi A pamoja na timu za Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, ASEC Mimosa ya Ivory Coast na Lobi Stars ya Nigeria. Wydad ilizindua kampeni zake za hatua ya makundi kwa kuvaana na ASEC na kushinda kwa mabao 5-2 nyumbani, ikichapwa mabao 2-1 na Mamelodi ugenini katika mchezo wa pili, ikaifunga Lobi Stars bao 1-0 nyumbani, kabla ya kulazimishwa suluhu na Lobi Stars katika mchezo wa marudiano. Ikakubali kichapo cha mabao 2-0 na ASEC ugenini, kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mamelodi bao 1-0 nyumbani. Katika michezo yake nane ya michuano hiyo, timu hiyo haijashinda mchezo ugenini katika mechi zake nne, imepoteza tatu na kutoka sare moja, ambapo hadi sasa imefunga mabao 10 na kufungwa mabao nane. ESPERANCE Timu hiyo ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambayo waliitwa msimu uliopita baada ya kuichapa Al Ahly ya Misri katika michezo ya fainali ya nyumbani na ugenini. Eperance ilianza kwa kuchapwa mabao 3-1 katika mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa Misri, kabla ya kushinda mabao 3-0 katika fainali ya pili na kutwaa taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3. Timu hiyo ilianzia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya michuano hii ambapo walipangwa kundi B na timu za Horoya ya Guinea, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na FC Platinum ya Zimbabwe. Wababe hao wa Tunisia walizindua kampenizi zao kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Horoya ugenini, ikaichapa FC Platinum mabao 2-0 nyumbani, ikilazimisha suluhu na Orlando Pirates ugenini. Katika mkondo wa pili, timu hiyo ilianza kwa kuichapa mabao 2-0 Orlando katika mchezo wa marudiano nyumbani, ikiitandika mabao 2-0 Horoya nyumbani kabla ya kumaliza kwa kuilaza FC Platinum mabao 2-1 ugenini. Licha ya kumaliza kama timu iliyokusanya pointi nyingi katika hatua ya makundi, lakini timu hiyo imeshinda michezo mitatu ya nyumbani, mmoja ugenini na kutoka sare miwili, ikifunga mabao tisa na kuruhusu mabao mawili tu. TP MAZEMBE Wababe hao wa zamani wa michuano hiyo, walianzia raundi ya kwanza kwa kucheza na Zesco United ya Zambia, ambapo mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0 nyumbani, kabla ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini na kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1. Timu hiyo ilipangwa katika kundi C na timu za Costantine ya Algeria, Club African ya Tunisa na Ismailia ya Misri. Mazembe ilizindua kampeni zake kwa kuichapa Ismaily mabao 2-0 nyumbani, ikichapwa mabao 3-0 ugenini na Constatine, ikahitimisha michezo ya mkondo wa kwanza kwa kuifumua Club African mabao 8-0. Ilianza mkondo wa pili kwa kurudiana na Club African na kulazimisha suluhu, ikitoka sare ya bao 1-1 na Ismailia ugenini, kabla ya kumaliza kwa kuilaza Constantine mabao 2-0 nyumbani. Katika michezo hiyo minane, Mazembe imeshinda mechi nne nyumbani na moja ugenini, huku pia ikipoteza mchezo mmoja ugenini na kutoka sare miwili. Hizo ni timu ambazo moja wapo itakutana na Simba SC baada ya kuchezeshwa droo leo huko Cairo nchini Misri. | michezo |
KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi anahofi a huenda timu yake ikapokea dhahama ya mabao kutoka kwa Simba kesho baada ya kikosi chake kukosa muda wa mapumziko kutokana na safari ndefu ya kutoka Mwanza.Mbeya City imetoka kucheza dhidi ya Alliance juzi Mwanza na kutoka suluhu, ambapo jana walianza safari ya kwenda Dar es Salaam kwa njia ya barabara na wanatarajiwa kufika leo kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.Akizungumza na gazeti hili jana Mwambusi alisema hawatakuwa na muda wa kupumzika kujiandaa na mchezo wa Simba, lakini hawana jinsi kwani ratiba iliyopo ilipangwa pasipokuangalia miundombinu ya nchi.“Tunatarajia kuingia Jumamosi kwa sababu tunasafiri na basi, tutafika tukiwa tumechoka na hatuna muda wa kupumzika, ndivyo ratiba ilivyopangwa haijaangalia kabisa miundombinu yetu,” alisema.Mwambusi alisema kuna haja kubwa Bodi ya Ligi kuangalia ratiba na kuzipa nafasi timu zinazotoka kucheza mikoa ya mbali na kwenda kwingine, zipewe nafasi angalau siku mbili ili zipate muda wa kusafiri na kupumzika tayari kwa mchezo unaofuata.Alisema mchezo huo huenda ukawa ni miongoni mwa michezo migumu kwao ikizingatia na ubora wa timu wanayokwenda kukutana nayo, lakini kingine akisema wenyeji wao wametoka kupoteza mchezo uliopita.Simba imetoka kupoteza dhidi ya Mwadui katika mchezo wa ligi uliochezwa hivi karibuni mkoani Shinyanga na wekundu hao walichapwa bao 1-0. Alisema wanawaheshimu wekundu hao ila watahakikisha wanapambana kwa jinsi walivyojiandaa kupata matokeo mazuri.Mbeya City imecheza jumla ya michezo nane na kati ya hiyo imeshinda mmoja, sare tano na kupoteza michezo miwili ikishika nafasi ya 16. | michezo |
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John Magufuli amesema, kama kuna kiongozi serikalini hataki kufuatwa fuatwa na watendaji wa chama hicho aondoke.Ametoa msimamo huo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na viongozi wa chama hicho na jumuiya zake ngazi ya wilaya na mkoa kwenye mikoa yote 32.Ameagiza viongozi hao wahakikishe miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwamba atasikitika sana ikitekelezwa chini ya kiwango wakati viongozi hao wapo.“Msikae kimya mnapoona miradi ya Serikali inadorora. Waelezezi viongozi wa Serikali kwenye wilaya na mikoa husika na mkiona hatua hazichukuliwi mjulisheni hata Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Ninyi ndio watawala. Tulizunguka kufanya kampeni ili tutawale…jeuri ya kutawala ni kutawala kweli, anayekuja pale ni mtumishi, wewe ni mtawala ilimradi tu usivuke nje ya mipaka ya sheria za nchi” amesema Dk Magufuli.Amesema chama lazima kiangalie matokeo ya utekelezaji wa miradi na kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM lazima lazima viongozi wote walioteuliwa watambue kuwa wanatekeleza Ilani ya chama hicho.“Wala pasitokee kiongozi yeyote ndani ya Serikali anayesema chama kinanifuata fuata. Lazima chama kikufuate fuate, kama hutaki kufuatwa fuatwa na chama ondoka upishe tuweke watu wengine. Chama ndio waajiri, chama wanataka kuangalia Ilani ya Uchaguzi inatekelezwaje”amesema Magufuli.Amewataka viongozi hao wa chama waitetee Serikali na kutangaza mafanikio na kwamba kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano. | kitaifa |
NEW YORK-MAREKANI AJALI iliyotokana na utaratibu wa matengenezo ya kawaida
imetajwa kuwa chanzo cha watumiaji wa mitandao ya WhatsApp, Facebook na
Istagram juzi kushindwa kutuma wala kupokea picha, video na mafaili mengine. Jana kampuni inayomiliki mitandao hiyo ya Facebook ililazimika
kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo ikisema sasa tatizo hilo limetatuliwa na
mitandao hiyo imerudi kwa asilimia 100. Juzi baada ya tatizo hilo kutokea kulikuwa na maneno na
hisia nyingi, kwamba huenda mitandao hiyo imedukuliwa. Shirika la Kijasusi la Marekani la CIA lilipata wakati
mgumu na hata kuamua kujibu shutuma zilizoelekezwa kwake kupitia mtandao wa
Twitter. “Ndio, nasi pia tumeathirika na mtandao wa Instagram
kuwa chini, hapana sisi hatujasababisha,
La hatuwezi kurekebisha shida yako, je umejaribu kuzima na kuwasha tena?
” CIA waliandika kujibu maswali ya watu waliokuwa wakiwashutumu kupitia
Twitter. Msemaji wa Facebook, ambaye pia alizungumza kwa niaba ya
Instagram na WhatsApp, alifafanua kuwa; “Matengenezo ya kawaida ya kila siku kwa bahati mbaya
yalisababisha hitilafu kwa watumiaji
kushindwa kupakua au kutuma picha na
video”. Kwa mujibu wa DownDetector, ambao ni wafuatiliaji
wa huduma za mitandao, maelfu ya watumiaji wa WhatsApp, Instagram na Facebook
waliripoti shida hiyo juzi baada ya kutokea hitilafu. Facebook pamoja na kusema wamerejea kwa asilimia 100 walikiri shida hiyo kuathiri watu katika
maeneo mengi duniani. Jumatano DownDetector waliripoti kuwa shida hiyo ilianza
karibu saa 6: 00 nchana na iliathiri Facebook pamoja na huduma za Instagram na WhatsApp. “Tumekwishatatua shida iliyotokea na tumerudi kwa
asilimia 100 kwa kila mtu,” iliandika kampuni hiyo katika ukurasa wake wa Twitter
saa 6:00 jana usiku, na kuongeza kuwa wanaomba radhi kwa usumbufu wowote
uliojitokeza. Juzi hiyo hiyo, Twitter nao walisema walikuwa wanapitia
hali kama ile ile iliyowakuta watumiaji wa WhatsApp, Istagram na Facebook. “ Tuna shida na DM. tunafanyia kazi na tutawajulisha mara moja
tukiishatatua. Tunaomba radhi kw usumbufu wowote” ulisomeka ujumbe wa Twitter siku hiyo hiyo ya Jumatano. Kwa mujibu wa DownDetector, maelefu ya watumiaji duniani
kote waliripoti shida hiyo huku Ulaya na Amerika ya Kaskazini ikiwa ndiyo
iliyoathirika zaidi. Si tu kwa mtumiaji mmoja mmoja, biashara na kampuni pia
ziliathirika na tatizo hilo. Mapema mwaka huu tatizo kama hilo lililodumu kwa saa 24
liliikumba Facebook huku sababu ikitajwa kuwa ni mabadiliko ya kwenye ‘server’.
Tatizo hilo ambalo lilitokea
Machi 13 , mwaka huu linaaminika kuwa baya zaidi kuwahi kuikumba kampuni hiyo
kubwa ya intaneti inayowafikia watu wanaokadiriwa bilioni 2.7. | kimataifa |
NA MAREGES NYAMAKA ZIMECHEZWA mechi nne hadi sasa msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara na tayari timu kongwe; Simba na Yanga, hazionekani katika nafasi mbili za juu katika msimamo wa ligi. Simba ipo nafasi ya nne ikiwa imejikusanyia pointi nane sawa na Yanga ambao wanatofautiana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Mtibwa Sugar ambao wikiendi iliyopita walipoteza asilimia 100 ya ushindi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting, bado wapo kileleni mwa ligi hiyo na pointi 10. Wakata miwa hao kutoka Turiani, Morogoro wamewazidi Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 10 pia kwa wingi wa mabao ya kufunga. Nafasi ya tatu inashikiliwa na timu iliyopanda daraja na inajivunia idadi kubwa ya wadhamini, Singida United, yenye pointi tisa baada ya michezo minne. Azam FC na Mtibwa Sugar wote wameshinda michezo mitatu na kutoka sare moja kiasi cha kuonekana tishio kwa Yanga na Simba wenye mashabiki lukuki. Mtibwa Sugar ambao wananolewa na kocha mzawa, Zuberi Katwila, wameonyesha utofauti ambao unaweza kusema wameziumbua timu zilizotumia usajili mkubwa ikiwamo Simba inayojigamba kutumia zaidi ya bilioni moja. Ikumbukwe Mtibwa Sugar haijafanya usajili wa kutisha au wa wachezaji wenye majina makubwa kama ilivyo utamaduni wao misimu yote licha ya kuondokewa na wachezaji wao tegemeo kama vile, Salim Mbonde, Said Mohamed na Ally Shomari, ambao wote walitua Simba, lakini imeendelea kucheza soka la kuvutia na kupata matokeo bora. Licha ya wadau wa soka kuendelea kuichukulia kama ni ya kawaida yao kuongoza ligi kwa muda, lakini hawa hawa ndio waliofanya vibaya msimu uliopita wakiwa na kocha wao huyo huyo ambapo takribani mechi saba walitoka sare. Kwa upande wa Azam FC chini ya kocha wao, Aristica Cioaba raia wa Romania, ambaye muda wote wa mchezo anasimama kutoa maelekezo kwa wachezaji huku akionyesha ukali, haikupewa nafasi na wadau wengi ya kuanza vyema ligi. Hatua hiyo ilitokana na kuondokewa na wachezaji wake tegemeo akiwemo nahodha John Bocco, kipa Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni (wote Simba) na Gadiel Michael aliyetua Yanga wakiwa kama chaguo la kwanza, lakini imekuwa tofauti kabisa. Takwimu zinaonyesha Wanalambalamba hawa ni timu pekee ambayo haijaruhusu wavu wao kuguswa ambapo langoni anasimama Mghana, Razak Abalora, aliyesajiliwa dakika za mwisho. Abalora tayari anaanza kuizoea ligi. Safu ya ushambuliaji ya Azam FC inaongozwa na Mbaraka Yusuph aliyejiunga na timu hiyo akitokea Kagera Sugar na sasa ndiye aliyechukua mikoba ya Bocco ambapo tayari amefunga mabao mawili kati ya matatu waliyofunga katika michezo yote minne. Viungo wamekuwa mhimili muhimu kwa timu hiyo kupata matokea kutokana na kocha huyo kuchezesha viungo watano kwa wakati mmoja ambao ni Himid Mao, Stephan Kingue, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo na Bruce Kangwa. Huku Mtibwa Sugar wakionekana kuanza vizuri msimu huu, Kagera Sugar imekuwa na matokeo ya kusuasua na kuzua mshangao mkubwa kwa wadau wa soka kulingana na ubora waliomaliza nao msimu uliopita. Wanankurunkumbi hao wanaonolewa na kocha bora wa msimu uliopita, Mecky Mexime, aliyekiongoza kikosi hicho kumaliza nafasi ya tatu hadi sasa hakijaonja ladha ya ushindi na wanaburuza mkia wakiwa na pointi moja. | michezo |
NAIROBI, KENYA
MKALI wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kwa jina la Jaguar, ameamua kumrudia Mungu wake mara baada ya kuona ugumu kwenye kampeni za kuwania ubunge kupitia chama chake.
Wiki iliyopita msanii huyo alitajwa kuwa amepita katika kura za maoni dhidi ya mpinzani wake, Maina Kamanda, lakini baadaye taarifa ikatoka kwamba kulikuwa na makosa hivyo matokeo yalibadilishwa na Maina akatangazwa mshindi huku akimwacha Jaguar akibaki kulalamika.
Kutokana na hali hiyo, Jaguar alionekana akidondosha machozi mbele ya wananchi kwa kuwa aliamini tayari amemaliza kila kitu, lakini watu hao walimshauri amuunge mkono mshindi na wafanye kazi pamoja.
Hali hiyo imemfanya msanii huyo amrudie Mungu wake kwa kufanya maombi ya mara kwa mara huku akikutana na wachungaji mbalimbali akiwamo Margaret Kenyatta.
“Ninaamini Mungu ndio kila kitu kwangu, hata kama kuna mchezo unachezeka, ila ninaamini malipo yake yako hapa hapa, kikubwa ninachokifanya ni kumshitakia Mungu wangu,” alisema Jaguar. | burudani |
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa, amewatema katika kikosi hicho nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Simon Msuva wa Yanga huku akiwaita Mwinyi Kazimoto wa Simba na kipa Shaban Cado wa Mwadui FC. Jana kocha huyo alitangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaoivaa Chad Machi 13, mwaka huu mjini Djamena katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwakani. Mkwasa pia amemtema winga, Mrisho Ngassa, anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini na kuwarejesha Jonas Mkude wa Simba na beki Erasto Nyoni wa Azam FC. Wachezaji wengine walioitwa Stars ni makipa Aishi Manula (Azam ), Ally Mustapha (Yanga) na mabeki, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani kutoka Yanga, Shomari Kapombe, David Mwantika (Azam) na Mohamed Hussein (Simba). Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Ismail Juma (JKU), Said Ndemla (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar) na Deus Kaseke (Yanga). Washambuliaji walioitwa ni nahodha, Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam), Elias Maguli (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Ajib (Simba). Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba wachezaji walioitwa kujiweka fiti kwenye mazoezi wanayofanya ndani ya klabu zao kwani hakutakuwa na muda wa kufanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa ugenini. “Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mechi za kimataifa za Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika zitachezwa kati ya Machi 18 na 20, hivyo wachezaji wote watakuwa na majukumu katika timu zao na muda wa kufanya mazoezi ya pamoja hautakuwepo. “Ndio maana nasisitiza kwa wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe na kujiweka fiti wanapokuja kwenye safari ya kwenda Chad,” alisema. | michezo |
Na PENDO FUNDISHA-MBEYA
WATENDAJI wa vijiji, kata na wataalamu wa halmashauri, wametakiwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za uhamishaji wa makao makuu ya ofisi za Serikali, ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima kwa wananchi.
Hayo yameelezwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ilembo Inyara, Shisieta na Insonso, vilivyopo wilayani Mbeya.
Katika mazungumzo yake, Makalla alisema alilazimika kuyasema hayo baada ya kuibuka kwa mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji cha Ilembo Inyara na Shisieta, wanaogombania eneo la kujenga ofisi za kata.
Alisema kwamba, ofisi za Serikali hazihamishwi kiholela bali ni lazima zifuate utaratibu hasa zile zinazohamisha makao makuu ya mji kutoka kijiji fulani kwenda kijiji kingine.
“Suala hili limetajwa hata katika Katiba ya nchi na wote lazima tuheshimu Katiba yetu kwani si ya CCM wala Chadema bali ni Katiba ya Tanzania.
“Katiba ya nchi yetu imeeleza madhumuni ya kuweko kwa Serikali za Mitaa na lengo lake ni kupeleka madaraka kwa wananchi na kutoa haki ya kupanga mipango na shughuli za maendeleo.
“Lakini ukiangalia mchakato uliofanyika wa kuhamisha ofisi ya mtendaji kata kutoka Kijiji cha Ilembo Inyara kwenda Shisieta, unaona umeghubikwa na changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.
“Pamoja na hayo, nawaomba wananchi wa vijiji hvi, kamati za maendeleo za kata na baraza la madiwani, kutoa mapendekezo yenu pamoja na wataalamu wa halmashauri waangalie jiografia ya mahala pa kuweka ofisi hizo na si kukurupuka,” alisema Makalla.
Pamoja na hayo, aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kwamba Serikali ya Mkoa wa Mbeya na wilaya, zitaratibu zoezi hilo la uhamishaji wa ofisi ya kata ili haki itendeke na watu wa pande zote waridhike. | kitaifa |
Na SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM HIVI karibuni, nyota wa kikapu Tanzania, Hasheem Thabeet alizua gumzo kwa wadau mbalimbali wa mchezo huo, baada ya kuanika hadharani usajili wake na moja ya timu zinazoshiriki Ligi ya Kuu ya Kikapu nchini Japan, Yokohama B-Corsairs. Nyota huyo aliyezaliwa Februari 16 mwaka 1987, amewahi kuzichezea timu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBA nchini Marekani kama vile, Houston Rockets, Oklahoma City Thunder, Memphis Grizzlies na zingine kabla ya kushuka kiwango na kushiriki Ligi ndogo (Development League) ya nchini humo. Alfred Ngalaliji ni mkufunzi wa mpira wa kikapu ngazi ya Taifa hapa nchini, anazungumza na SPOTIKIKI, juu usajili wa mchezaji huyo na mambo mbalimbali yanayohusu muelekeo wake nchini Japan. Spotikiki: Una tetesi zozote juu ya nyota wa Tanzania Hasheem Thabeet kumwaga wino kwenye moja ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Kikapu nchini Japan? Ngalaliji: Sinaushahidi wa kutosha, ingawa nimeona picha zake zikiashiria kitu kama hicho. Spotikiki: Vipi kama ukijihakikishia amemwaga wino kwa ajili ya kuitumikia Yokohama B-Corsairs inayoshiriki ligi hiyo? Ngalaliji: Kwake yeye litakuwa jambo jema ila kwa sisi tunayemtazama na kumfuatilia, sidhani kama atakuwa amefanya maamuzi sahihi katika kukuza na kuendeleza kikapu chake. Spotikiki: Unakitu chochote cha kuzungumzia maisha ya nyota huyo kipindi yupo NBA na kuondoka kwake? Ngalaliji: Unajua wakati akiwa NBA alicheza msimu mmoja tu na ule uliofuata hakuwa na mafanikio yoyote ndani ya klabu, hivyo watawala wa timu ikabidi wamrudishe kwenye ligi ndogo (D-League) ili acheze kwa kiwango, ndipo wampandiishe daraja sambamba na kuingia naye mkataba. Spotikiki: Kutokana na uzoefu pamoja na ukongwe ulionao kwenye mpira wa kikapu, unadhani kwanini hakufanya vema ligi ndogo ili apande NBA? Ngalaliji: Asikuambie mtu, ligi ndogo siku zote inakuwa ngumu kwasababu kila mchezaji anahitaji kuonyesha kiwango chake ili apande daraja, pamoja na Thabeet kuwahi kukodisha wakufunzi wamsimamie mazoezi, lakini bado kiwango chake hakikuonekana. Spotikiki: Wakati Thabeet anaichezea timu ya Grand Rapids inayoshiriki ligi ndogo, kupitia mashindano maalumu ya kusaka vipaji ‘Summer League’ aliripotiwa kufanya tukio la kuvunja viti ndani ya chumba cha kubadilishia nguo, unafikiri hiyo ni miongoni mwa sababu zilizomnyima ulaji timu za NBA? Ngalaliji: Unajua unapokuwa mchezaji mkubwa mwenye jina kama yeye, lazima jopo la watu likufuatilie, sitaki kuhukumu kwa kile kilichomtokea Grand Rapids, isipokuwa inawezekana hiyo nayo ikawa sababu kwa wenye timu zao. Spotikiki: Yanasemwa mengi kutoka midomoni mwa wadau wa kikapu nchini juu ya mchezo huo kupotea kabisa, kwenye ulimwengu wa kikapu, baada ya kujichimbia Japan, kwako wewe unalitizama hilo kwa jicho gani? Ngalaliji: Waswahili wanamsemo wao usemao kuwa ‘Lisemwalo lipo kama halipo basi laja’, mimi naona tumpe muda kila mmoja wetu atajionea. Spotikiki: Upi wito wako kwa nyota huyo? Ngalaliji: Aendelee kujituma, hata uko aliko sasa kuna wachezaji wengi wenye viwango na kila mmoja atahitaji kuonyesha uwezo wake ili afike mbali. Spotikiki: Ushauri wako kwa wachezaji wa mchezo huo hapa nyumbani ni nini? Ngalaliji: Vijana watulize akili kwa kucheza mpira wa kikapu kwa kuzingatia sheria na kanuni ili wafikie malengo, mbali na hilo niwatake wale ambao wamefanikiwa kusajiliwa na timu mbalimbali barani Afrika kuzitumia vema nafasi hizo ili waitangaze Tanzania. | michezo |
NA WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM TIMU ya Yanga imeendelea kuwapa raha mashabiki wake, baada jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo, lilifungwa dakika ya 40 kwa kichwa na mshambuliaji David Molinga. Molinga sasa amefikisha idadi ya mabao saba aliyoifungia Yanga msimu huu. Kinara wa mabao mpaka sasa ni mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ambaye amefunga mara 12. Kwa ushindi wa jana dhidi ya Shooting, Yanga imelipa kisasi baada ya kulazwa bao 1-0 na wanajeshi hao wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kati ya timu hizo uliochezwa pia kwenye uwanja huo. Pia ushindi wa jana uliifanya Yanga kufikisha pointi 37 na kusalia nafasi ya tatu, baada ya kucheza michezo 18, ikishinda 11, sare nne na kupoteza mara tatu, ikiwa nyuma ya vinara Simba iliyoko kileleni na pointi zake 50, kupitia michezo 20 iliyoshuka dimbani, ikishinda 16, sare mbili na kupoteza mbili. Nafasi ya pili ipo Azam yenye pointi 41, baada ya kushuka dimbani mara 20, ikishinda michezo 12, sare tano na kupoteza mara tatu. Mchezo ulianza kwa Yanga kuutawala mchezo na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Shooting. Dakika ya 15, pasi safi ya Papy Tshishimbi ilimkuta Molinga, lakini mpira wa kichwa alioupiga kwa ufundi ulipanguliwa na kipa wa Shooting, Mohamed Makaka. Dakika ya 25, mkwaju wa Benard Morrison ulipanguliwa na Makaka. Wakati wote huu, Shooting ilionekana kukosa mbinu sahihi za kuipenya safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya beki kisiki, Lamine Moro. Dakika ya 32, Tshishimbi alipokea pasi safi ya Haruna Niyonzima, lakini mkwaju wake dhaifu ulidakwa na Makaka. Dakika ya 37, mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo huo, Rafael Ilambi wa Morogoro, baada ya kumfanyia madhambi Shaaban Kisiga wa Shooting. Dakika ya 39, mshambuliaji Fully Maganga alikaribia kuifungia Shooting, lakini mpira wake wa kichwa ulidakwa na kipa wa Yanga, Metacha Mnata. Mkakati wa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael ulizaa matunda dakika ya 40 baada ya pasi nzuri ya Nchimbi kumkuta Molinga ambaye aliunganisha wavuni mpira kwa kichwa na kuwapa Wanajangwani hao bao la uongozi. Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipokamilika. Kipindi cha pili, Shooting ilionekana kuamka na kuutawala mchezo. Dakika ya 57, Kocha Mkuu wa Shooting, Salum Mayanga, alimtoa William Patrick na kumwingiza Shaaban Msala. Dakika ya 62, Graham Naftari aligongesha mwamba wa juu wa Yanga kabla ya mpira kurudi uwanjani. Dakika ya 68, Tshishimbi alilimwa kadi ya njano kwa kumchezea madhambi Maganga. Dakika ya 69, Eymael alimtoa Molinga na kumwingiza Yikpe Gislain. Dakika ya 79, Baraka Mtui wa Shooting alilimwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Morrison. Dakika ya 80, Yikpe alishindwa kutumia vema pasi ya Nchimbi kuifungia Yanga bao la pili, baada ya kupiga shuti dhaifu lililodakwa na Makaka. Dakika ya 81, Eymael alimtoa Morrison na kumwingiza Deus Kaseke. Pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na kila upande, dakika 90 zilikamilika kwa Yanga kutakata kwa bao 1-0. Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa jana, Azam ilishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mbao na Alliance zikatoka sare ya bao 1-1, Coastal Union ikaitandika Polisi Tanzania mabao 2-1. Mwadui ikatoka sare ya mabao 2-2 na Singida United, Mbeya City ikaishinda Prisons bao 1-0, Kagera Sugar ilatoka suluhu na Biashara United, wakati Lipuli ikaitungua Mtibwa Sugar bao 1-0. | michezo |
ZURICH, USWISI RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),Gianni Infantino, amependekeza kuongezwa kwa timu za mataifa 16 kutoka 32 zinazoshiriki michuano ya Kombe la Dunia. Idadi hiyo itafanya kuwapo kwa timu 48 ambazo ni zaidi ya ahadi yake ya awali alioitoa katika kampeni za urais wa Fifa ambapo alitaka michuano hiyo kushirikisha jumla ya timu 40. Kwa mujibu wa Infantino (46), anaeleza kuwa mataifa 16 yataondolewa katika mzunguko wa kwanza na kubakia mataifa 32 yatakayoshiriki hatua ya makundi ikifuatiwa na hatua zaidi ya mtoano. Infantino alisema uamuzi wa kupanua michuano hiyo mikubwa duniani inatarajia kufanyika Januari mwakani. “Tupo mbioni kutafuta njia sahihi ya kuboresha michuano hii na kabla ya kufika katika uamuzi, kwanza tutafanya mdahalo mwezi huu wa kujadili hoja hii. Infantino alisema kwa sasa timu 32 kutoka katika mataifa mbalimbali zitashiriki katika hatua za awali za mtoano na washindi kujiunga na timu 16 washindi wa hatua ya makundi. “Kwa sasa tunaendelea na utaratibu wa kawaida wa Kombe la Dunia kwa kuwa na timu za mataifa 32, lakini hapo baadaye tunatarajia kuwa na timu 48. “Wazo la Fifa ni kuendeleza soka katika mataifa yote, dunia ni kubwa hivyo tunataka kufanya mashindano haya yawe zaidi na yalivyokuwa hapo awali,” alisema Infantino ambaye alichukua nafasi ya Rais wa Fifa wa zamani, Sepp Blatter, Januari 26, mwaka huu. Infantino aliongeza kuwa wazo hilo litapanua mashindano hayo kwa kuwa yatashirikisha mataifa ambayo hayakupata nafasi hapo awali. Katika wazo hilo jipya, inadaiwa huenda ikatokea England kucheza dhidi ya Iceland katika mzunguko wa kwanza kama England hawakufuzu moja kwa moja. | michezo |
MWANDISHI
WETU-DAR ES
SALAAM RAIS Dk. John Magufuli ameagiza Wizara ya Fedha na
Mipango kutoa Sh Bilioni 40 kwa ajili ya kumalizia madeni yote ya wakulima wa
korosho yaliyobaki baada ya Serikali kununua korosho za wakulima katika msimu
wa mwaka 2018/19. Rais
Magufuli alitoa maagizo hayo jana, Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na
viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi za Serikali ambazo zinahusika
katika uzalishaji na mauzo ya zao la Korosho mkutano ambao pia ulihudhuriwa na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Rais
magufuli pia pamoja na kuagiza Wizara ya Fedha na Mipango itoe fedha hizo pia
aliagiza Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha fedha hizo zinawafikia
wakulima leo na sio vinginevyo, na pia kuhakikisha wanalipwa wakulima
wanaostahili kupata malipo hayo. Aidha, rais
alieleza kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa Wizara ya Kilimo na viongozi
wa Mikoa na Wilaya ambao katika maeneo yao kumetokea wizi mkubwa wa fedha za
wakulima kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) hali iliyosababisha
wakulima wengi kuishi maisha duni. “Nataka
mfanye kazi, hakuna mtu wa kuwanyanyasa, nendeni mkashughulikie kero za
wakulima, mna vyombo vya ulinzi na usalama nendeni mkavisimamie, kinyume na
hapo nitakuona hutoshi kwenye nafasi hiyo,” alisema Rais Magufuli. katika hatua
nyingine, Rais Magufuli alisikitishwa kuona viongozi wa Wizara, Mikoa na Wilaya
hawajachukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaowaibia wakulima hadi alipoamua
kumtuma Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, ambaye kwa muda mfupi amebaini kuwepo
wizi wa shilingi Bilioni 1.23 na tayari amefanikisha kurejeshwa kwa shilingi
Milioni 375 katika Mkoa wa Lindi pekee. Aliwataka
viongozi wa Wizara ya Kilimo, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kubadilika na
kuhakikisha haki za wakulima zinalindwa ipasavyo kwa kurejesha fedha zilizoibwa
na kuzuia mianya yote ya wizi. “Na kuhusu
minada ya korosho,nataka utaratibu uliowekwa wa kufungua mnada kuanzia saa 2:00
asubuhi hadi saa 10:00 Jioni na kisha kufungua masanduku yenye zabuni kwa uwazi
mara baada ya saa 10 jioni uheshimiwe, ili kuepusha njama za upangaji wa bei,”
alisema Raios Magufuli. upande wao,
Viongozi wa Mikoa na Wilaya wamemuahidi, Rais Magufuli kuwa wanakwenda
kusimamia maelekezo yake na kuhakikisha haki za wakulima zinalindwa. | kitaifa |
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inawashikilia vigogo watatu wa Taasisi ya Mikopo ya Pride Tanzania, huku ikimtaka Mkurugenzi Mtendaji wake, Rashid Malima kuripoti haraka kwa mahojiano kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh bilioni 1.8.Malima imeelezwa kuwa amekimbilia nchini Marekani, baada ya taasisi hiyo kufa kutokana na ukata wa fedha huku kigogo huyo wa Pride Tanzania akidaiwa kutafuna kiasi hicho cha fedha.Aidha, Takukuru inamsaka aliyekuwa mtumishi wa Chuo Kikuu cha Elimu (DUCE), Josephata Mseti Machiwa, kwa tuhuma za kutafuna fedha za mikopo ya wanafunzi ambao zilipaswa kulipia ada.Akizungumza jana Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema walipata taarifa kutoka kwa wananchi wema wakidai kutafunwa kwa fedha za Pride hivyo walikuwa wanatafutwa muda mrefu kwa masuala mbali mbali ya rushwa na ubadhirifu.“Taasisi ya Pride Tanzania ilikuwa inajihusisha na mikopo midogo kwa wananchi hasa wakina mama na kuanzisha shughuli zao za uchumi,” alisema Brigedia Jenerali Mbungo na kuongeza: “Mamlaka iliyosajili ilikuwa imeundwa mahususi kwa ajili ya wananchi wenye kipato kidogo shughuli za uvuvi, kilimo, biashara na ilisajiliwa rasmi mwaka 1999 na kupata ruzuku kutoka Norad (shirika la misaada ya kimaendeleo la Norway) yenye dola za Marekani milioni nne.“Ilianza vizuri na ilisaidia kutoa mikopo kwa wananchi, lakini ghafla matatizo yalitokea ya ubadhirifu, rushwa zilisababisha taasisi hii kufungwa, kwa sasa haipo.” “Tulipata taarifa kutoka kwa wananchi wema, tukawasaka wote waliohusika na wizi wa fedha, tumefanikiwa kuwapata viongozi watatu; Alfred Kasonka alikuwa Meneja wa Fedha, Abdallah Kitwara na Paska Sima alikuwa mtunza fedha, bado tunaendelea na mahojiano nao na wanatupa ushirikiano vizuri,” aliongeza.Aidha, alisema Takukuru inamsaka Mkurugenzi Mtendaji wa Pride, Rashid Malima ambaye amekuwa akiongoza taasisi hiyo kama Mkurugenzi Mtendaji tangu mwaka 1993 hadi 2018 alipotimkia nchini Marekani.“Rashid Malima (65), ni mtu mzima, lakini kakimbia nchi yake kwa ubadhirifu, tunamtaka aje apambane na tuhuma zake, wananchi waliopo Marekani wakimuona wamwambie arudi nyumbani haraka na kuweka sawa rekodi yake kwa serikali,” alisisitiza bosi huyo wa Takukuru.“Nyaraka tunazozishikilia tumebaini Malima aliweza kuiba kiasi cha shilingi bilioni 1.8, hizi ni taarifa tulizozikamata inaweza kuwa zaidi, bado tunafanya uchunguzi kujua kiasi sahihi.“Pia wapo ambao tumewakamata tunaendelea kuwahoji Alfred Kasonka (Meneja wa Fedha), Abdallah Kitwara na Paska Sima (Mtunza Fedha),” alisisitiza Brigedia Jenerali Mbungo na kufafanua kuwa taasisi hiyo haimuonei mtu na kwamba mpaka mtu anaitwa tayari wameshajiridhisha vya kutosha.Hatua hiyo ya Takukuru imekuja ikiwa tayari Pride imefungwa mapema mwaka huu baada ya kuripotiwa kufilisika huku ikishindwa kutoa mikopo kwa wateja wake na kulipa stahiki za wafanyakazi pamoja na michango ya pensheni na kodi ya serikali. | kitaifa |
MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imemwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Imni Patterson, kujieleza juu ya taarifa wanazozitoa kwenye mitandao yao ya kijamii ikiwamo maambukizi ya corona nchini. Taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jana, ilisema lengo la kumwita balozi huyo ni kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Itakumbukwa Juni mwaka jana wizara hiyo pia ilimwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini, kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ambayo ubalozi huo, uliitoa juu ya angalizo la kiusalama la uwezekano wa kutokea kwa shambulio la kigaidi. Wito huo ulitokana na taarifa ya ubalozi huo juu ya angalizo la kiusalama kuhusu shambulio la kigaidi katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo eneo la Masaki. Jana taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema Dk Patterson aliitwa na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge, kwenye Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ibuge alieleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19. “Akitolea mfano Katibu Mkuu amezitaja taarifa zilizotolewa na Ubalozi huo Mei 13 mwaka huu Mei 25 kwenye ukurasa wa Twitter wa Ubalozi huo. Alisema taarifa hizo zote zilionekana kukusudiwa kutoa tahadhari kwa raia wa Marekani waliopo nchini na wanaotarajia kuja Tanzania kuwa jiji la Dar es Salaam siyo salama kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wagojwa wa COVID-19. “Tahadhari hizo pia zimeendelea kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam (bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo ambalo siyo kweli na linauwezekano wa kusababisha taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi ilhali hali halisi sivyo ndivyo inavyodaiwa,” ilisema taarifa ya wizara. Ilisema Ibuge alimjulisha Dk Patterson kuhusu umuhimu wa Ubalozi kutoa taarifa zilizothibitishwa kwa sababu Serikali haina kizuizi cha aina yoyote kwa mabalozi kutafuta na kupata taarifa sahihi na zenye ukweli. Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ibuge alimshukuru Kaimu Balozi huyo kwa ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Marekani katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama na maeneo mengine ya maendeleo. | kitaifa |
Derick Milton, Busega Mkuu wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera amesemakuwa wilaya hiyo imeandaa tamasha kubwa la kukuza na kuendeleza Utalii uliopo na Kanda ya Ziwa kwa ujumla litakalofanyika kwa siku nne kuanzia Desemba 29 hadi Januari Mosi mwaka huu. Mwera amesema kuwa tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Itongo Lamadi, ambapo linatarajia kushirikisha zaidi ya watalii na wajasiriamali 300. Amesema katika ufunguzi wa tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utalii , Constantine Kanyasu, huku siku ya kilele mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk. Raphael Chegeni. Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 37, Mkuu huyo wa Wilaya amesema lengo la tamasha hilo ni kutangaza Utalii wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Mji wa Lamadi pamoja na utamaduni wa mkoa wa Simiyu na Mara. “Wilaya ya Busega tumekuwa tukipakana na hifadhi bora nchini ya Serengeti, lakini bado hatujaweza kuitumia katika kutangaza Utamaduni wetu, wananchi wa mji wa Lamadi kuitumia kufanya biashara, tuliona tuanzishe tamasha hili kuweza kujitangaza lakini pia wananchi wa Lamadi waweze kufanya biashara kupitia ujasiriamali wao wa kisanaa,” amesema Mwera. Aidha amesema kuwa watalii kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti watakuwepo kuweza kuangalia utamaduni wa wasukuma, wasanii wa Sanaa mbalimbali za ususi, uchoraji na kuchonga huku akitangaza uwepo wa Utalii wa baiskeli, kutembelea Serengeti na Utalii wa Boti ziwa Victoria. Mkuu huyo wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote wa Wilaya hiyo na kanda ya ziwa wenye ubunifu mbalimbali kujitokeza na kutangaza bidhaa zao kwani hakutakuwa na kiingilio. | kitaifa |
Akizungumza na wakuu wa idara zilizo chini ya wizara hiyo na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Waziri Nagu alisema kwa kuwa wajasiriamali Watanzania wataweza kubuni, kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo ipasavyo hatua ambayo kwa namna yoyote itawaletea maendeleo.Katika hotuba yake hiyo, Waziri Nagu alieleza mafanikio katika maeneo yanayohusu Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji ambapo kwa upande wa Sekta Binafsi alisema kuna mafanikio makubwa yamepatikana kupitia Mradi wa Kukuza Ushindani wa Sekta Binafsi hasa katika Mpango wa Fanikiwa Kibiashara na Mpango wa Ruzuku ya Kuchangia.“Mpango wa Fanikiwa Kibiashara unatekelezwa na Serikali kwa ushirikiano na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na unajumuisha Programu mbili za Kuendeleza biashara na Mashindano ya mipango ya biashara,” alisema.Alisema chini ya Programu ya Mashindano ya Mipango ya Biashara, wajasiriamali 4,500 waliwezeshwa kwa kupewa mafunzo ya ujasiriamali na mipango yao ya biashara kushindanishwa ambapo kati yao wajasiriamali 2,780 walishinda na kupewa ruzuku ya mbegu mtaji ambapo Sh bilioni 9.9 zilitolewa ili kukuza na kuboresha biashara zao na kuongeza ajira.Kuhusu Mpango wa Ruzuku ya Kuchangia mafanikio makubwa yalikuwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Biashara ambao ulilenga kusaidia Vyuo vya Elimu ya Juu kubuni kozi mpya za kuongeza ujuzi na ufanisi kazini, programu ambayo imewezesha kampuni 1,728 kusajiliwa ambapo kati yake 786 zilipata Sh bilioni 7.8 kama ruzuku ya kuanzisha na kuendeleza miradi.Waziri alisema pia kuwa ili kuisimamia vizuri Sekta Binafsi, Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Sekta Binafsi ya mwaka 2013 imeandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Sekta Binafsi na kwamba kazi ya kukusanya maoni ya wadau mbalimbali inaendelea.Kuhusu Uwekezaji, Waziri Nagu alisema mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini kwa kuandaa na kutekeleza sera na sheria zinazovutia uwekezaji, kuwekwa kwa vivutio vya kodi na visivyo vya kodi ili kuhamasisha na kuvutia uwekezaji.“Serikali imekamilisha maandalizi ya Sera ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPP) ya mwaka 2009, Sheria ya PPP ya mwaka 2010 na Kanuni za PPP za mwaka 2011,” alisema Waziri Nagu.Kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi, Dk Nagu alisema mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuwajengea wananchi uwezo wa stadi za kubuni, kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi na biashara kwa njia ya utoaji wa elimu na mafunzo ya ujasiriamali.Alisema mafanikio mengine ni jitihada za kuhamasisha utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa umma na kuwajengea wadau kama vile Vyama vya Akiba na Mikopo (Saccos) na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zinazojishughulisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi uwezo wa kutoa mikopo, mafunzo na vitendea kazi kwa wajasiriamali wadogo. | uchumi |
Esther Mbussi, Mwanza Wafanyabiashara, wadau wa bandari na wasafirishaji wa shehena za mizigo kutoka nchi mbalimbali, wameshauriwa kutumia Bandari ya Mwanza kutokana na bandari hiyo kuwa ya gharama nafuu na kutumia muda mfupi kuliko zote. Kaimu Meneja wa Bandari ya Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya, amesema hatua hiyo ni kwa sababu Bandari ya Mwanza Kusini ndiyo inawaunganisha na Bandari zote za Ziwa Victoria. “Tuna gati za kisasa, vitendea kazi vya kutosha na sisi ndiyo wenye bei nafuu kuliko wote na tunatumia muda mfupi. “WFP ni mteja wetu mkubwa ambapo wanatumia Bandari ya Isaka kusafirisha chakula mara kwa mara kwenda Sudan Kusini, lakini pia Rwanda, Burundi na Uganda nao ni wadau wetu wakubwa,” amesema. Lwesya pia amesema kumekuwapo na mikakati mbalimbali ili kuendana na mahitaji ya wateja na soko lililopo ikiwamo kuendelea na wateja waliopo, kutafuta wateja wapya na kurudisha walioondoka kwenye soko na kuzidisha wateja wakubwa. Ametaja mikakati mingine ni kurasimisha bandari binafsi, ununuzi wa vifaa vipya kwa ajili ya ubebaji wa mizigo na kuajiri wafanyakazi wapya ili kuimarisha utendaji. | kitaifa |
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameshtushwa na kitendo cha mfanyabiashara wa Kata ya Mpwapwa wilayani Sumbawanga, Julius Mwanisawa kujimilikisha ardhi yote ya kitongoji cha Memya.Ardhi hiyo ina milima yenye misitu ya hifadhi na vyanzo vya maji. Mfanyabiashara huyo amezuia wakazi wa eneo hilo kuiendeleza ardhi ya eneo hilo.Kitongoji cha Memya kipo katika kata ya Mpwapwa hakina shule ya msingi wala zahanati huku ujenzi wake ukisuasua kutokana na mgogoro wa ardhi uliopo baina ya wakazi wa kitongoji hicho na Mwanisawa.Licha ya kuwa mgogoro huo umefikishwa katika Mahakama ya Ardhi mkoani Rukwa bado Wangabo alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfany Haule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Nyangi Msemakweli kufuatilia kesi ya mgogoro huo.Amewataka viongozi hao wapate taarifa na kujua sababu za Mwanisawa kujimilikisha ardhi yote ya kitongoji cha Memya vikiwemo vyanzo vya maji na hifadhi ya misitu. Alitoa agizo hilo alipotembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vinavyojengwa na wakazi wa kitongoji cha Memya.Naye diwani wa Mpwapwa, Abel Mambachika alimueleza Wangabo kuwa Mwanisawa amewazuia wananchi kufyatua matofali kwa kuwa ardhi yote ni mali yake.Aidha Wangabo aliwaagiza viongozi wa Kata ya Mpwapwa akiwemo diwani wake, Mambachika wahakikishe mipaka ya kitongoji hicho na maeneo yatapojengwa taasisi za umma ikiwemo shule na zahanati yanatambuliwa na kupimwa ili kusiwepo migogoro.Ofisa Ardhi, Sekretarieti ya mkoa wa Rukwa, Kelvin Mahundi aliwaeleza wakazi wa kitongoji hicho kuwa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kisheria kujimilikisha vyanzo vya maji vikiwemo visima na milima. | kitaifa |
NEW YORK, MAREKANI RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amemwita mwenzake wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni Goliati mkubwa ambaye anatishia kuzifuta nchi nyingine duniani, wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini New York. Mugabe amemshauri Trump kuzima tarumbeta lake mara moja, huku akiweka kumbukumbu kuwa aliwahi kutishiwa kuondolewa madarakani na Rais huyo mwenye utata aliyeingia madarakani mapema Januari 20, mwaka huu, akichukua nafasi ya Rais mstaafu, Barrack Obama. Katika kipindi cha kampeni za kuwania urais wa Marekani, Trump alidokeza kuwa wapo viongozi wanatakiwa kung’olewa madarakani, akiwamo Robert Mugabe, huku akisisitiza kuwa, Bara la Afrika linapaswa kutawaliwa tena na wakoloni. Akizungumza mkutanoni hapo, Mugabe alisema: “Wengine (sisi) tulijisikia fedheha sana, tulitishwa na hotuba ya Trump”. Katika mkutano huo wa Rais wa Zimbabwe, Mugabe alimwambia Trump kuwa ni wakati wa “kupiga tarumbeta” lake kupigania amani. Hotuba ya Mugabe ilikuja baada ya Trump, aliyesimama mkutano hapo, kuzilaumu kwa nguvu nchi za Korea Kaskazini, Iran na Venezuela. Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, alionekana kuchapa usingizi wakati Trump akitoa hotuba yake mapema wiki hii. Picha zinaonyesha kuwa, wakati Trump akitoa hotuba yake, yeye (Mugabe) alikuwa ameegesha kichwa chake kwenye kiti alichokalia pamoja na kufumba macho yake. Aidha, inaonekana kuwa amesikiliza vya kutosha hotuba ya Trump ambayo imemkosoa, hali ambayo imechochea yeye kumwita rais huyo wa Marekani kuwa Goliati anayezungumzwa kwenye kitabu cha Wakristo cha Biblia. Goliati anaelezewa kwenye kitabu hicho kuwa alidhamiria kuiangamiza Israel, kabla ya kukumbana na baadaye kuuawa na Daudi. “Huku ni kurudi kwa Goliati wa dhahabu, je, tupo tayari kumpokea Goliati huyu anayetishia ustawi wa nchi nyingine? Naomba niseme hiki kwa Rais wa Marekani, Trump, tafadhali piga tarumbeta lako la kuthamini umoja, amani, ushirikiano, mshikamano, majadiliano, ambayo tunayo kwa kipindi chote,” alisema Mugabe. Kiongozi huyo, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa sera za uvamizi za nchi za magharibi, ametumia hotuba yake kusema kuwa amelishinda dubwana la ubeberu. | kimataifa |
CHUMVI inayozalishwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi, imepata soko kubwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na ubora wake.Na kutokana na uhakika wa soko uliochangia pia kuongezeka kwa uzalishaji wa chumvi katika mkoa huo, bidhaa hiyo sasa inashika nafasi ya nne katika kuingiza mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, ikitanguliwa na sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji.Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi, Jomaary Satura wakati akielezea Fursa za Biashara na Uwekezaji zinazopatikana katika Manispaa hiyo ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa.Amesema soko kubwa la chumvi ya Lindi lilikuwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini kama vile Ruvuma, Mbeya, Iringa na Njombe, lakini kutokana na kuongezeka kwa ubora na uzalishaji, chumvi hiyo sasa inauzwa Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).Halmashauri ya Manispaa ya Lindi inapakana na Bahari ya Hindi kuanzia eneo la Mto Mkavu mpaka Mkwaya ambalo ni eneo lenye urefu wa kilomita 112 ambalo ni la Manispaa linalotumika kuzalisha chumvi.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, Manispaa ya Lindi pekee ina mashamba ya chumvi zaidi ya 144. Sehemu kubwa ya chumvi inayozalishwa katika kiwanda cha chumvi cha Neel Salt cha Mkuranga, Pwani inatoka katika Manispaa ya Lindi.Chumvi pia inazalishwa kwa wingi katika wilaya ya Kilwa ambayo pia inategemea masoko ya ndani na nje ya nchi hasa nchi za ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai anasema chumvi itokayo Kilwa inalisha soko la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.Mmiliki wa mashamba ya chumvi wilayani Kilwa, Saidi Ali Timamy, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mshindo Salt, anasema mbali na masoko ya ndani ya nchi, chumvi yake imepata masoko katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kama vile Rwanda na Burundi.Anaamini katika siku za baadaye, chumvi hiyo itapata masoko zaidi katika mataifa ya Uganda na DRC kwa kuwa tayari bidhaa hiyo imeshapata soko la kuaminika katika nchi jirani za Rwanda na Burundi.Tamimy amesema uzalishaji wa chumvi katika mashamba yake umeongezeka baada ya kununua mashine ya kusaga bidhaa hiyo.Amesema kila shamba lina mabirika 20 yanayozalisha viroba 30,000 vya kilo hamsini.Kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, chumvi hiyo ili iweze kutumiwa na wanadamu lazima iwekwe madini joto. Tamimy alisema anafuata taratibu hizo kwa kila mzigo wa chumvi itokayo katika shamba lake. | uchumi |
MKUTANO wa wadau wa maji kutathmini changamoto kubwa ya kukauka na kuchafuliwa kwa vyanzo vya maji nchini, unatarajia kuanza mjini Kigoma leo.Katika mkutano huo Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (pichani) anatarajiwa kuongoza viongozi wa wizara hiyo na wataalamu kutoka bodi za mabonde tisa ya maji nchini. Mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika mkoani Kigoma ukihusisha wadau 250, wakiwamo wadau wa maendeleo wanaochangia na kufadhili miradi ya maji nchini, utajikita kupitia taarifa za hali ya rasilimali za maji nchini na kutoka na maazimio ya nini kifanyike kunusuru hali hiyo.Ofisa wa Bodi ya Maji ya bonde la ziwa Tanganyika, Chobariko Rubwabwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya rasilimali za maji ambazo haziendani na utunzaji na uhifadhi wa vyanzo hivyo. Alieleza kuwa kutokana na changamoto hizo hali inaweza kuwa mbaya siku zijazo na kuathiri upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.“Mkutano utapokea na kujadili taarifa za bodi za mabonde ya maji nchini, utafanya mapitio ya tathmini ya Sera na Sheria kuona namna ambavyo wataweka mkakati wa kuzitumia katika kulinda vyanzo vya maji na kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali za maji nchini,” alisema Rubwabwa. Rubwabwa alisema kuwa changamoto ya uchafu wa vyanzo vya maji kwenye mito na maziwa kwa sasa ni kubwa hasa maeneo yenye viwanda kutokana na kemikali kuingizwa kwenye vyanzo hivyo hali inayochangia uchafuzi mkubwa wa vyanzo vya maji nchini.Akieleza kuhusu athari za uchafuzi huo kwa bonde la ziwa Tanganyika Rubwabwa alisema kuwa kwa sasa uchafuzi siyo mkubwa kama mikoa mingine lakini alikiri kuwa athari za tabia nchi kutokana na shughuli za kibinadamu zimekuwa na athari kubwa kwenye bonde hilo. Alifafanua kuwa tafiti zinaonesha kukauka wa ziwa Sagala na Nyamagoma kama hatua za dharula hazitachukuliwa.“Wataalamu wote wa wizara watakuwa hapa wakiongozwa na Waziri wa maji, viongozi na wataalamu wote kutoka bodi za mabonde tisa ya maji nchini lakini pia tumeyaalika mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo ambao wanaochangia na kufadhili miradi ya maji nchini,” alisema Rubwabwa.Ofisa huyo wa bodi ya maji ya bonde la ziwa Tanganyika alisema kuwa mkutano utafanya tathmini ya utendaji wa bodi za mabonde hayo, kufanya tathmini ya tafiti zinazofanywa katika matumizi ya maeneo ya mabonde, utoaji vibali wa matumizi ya maji na uundwaji wa bodi za watumiaji wa maji kwenye miradi mbalimbali ya maji iliyoanzishwa nchini.Akizungumzia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mkoa Kigoma kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira Ofisa Kilimo Sekretarieti ya mkoa Kigoma, Joseph Rubuye alisema kuwa hali hiyo imechangia uvamizi wa vyanzo vya maji na kusababisha wakulima kukimbilia kulima ndani ya mabonde hayo kwenye mito na maziwa. | kitaifa |
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa watatu wanaodaiwa kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mkazi wa Bunju A, Kinondoni, Robson Orotho kwa madai ya kutolipa faini ya usafi, watafikishwa mahakamani haraka.Kamanda Muliro amesema, watuhumiwa hao ambao ni askari mgambo wa Kinondoni, watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria haraka kwa sababu tukio walilofanya liko wazi na lina ushahidi.“Sisi kazi yetu ni kupepeleza na kupeleka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali. Jumatatu tutapeleka asubuhi na tuna imani siku hiyo hiyo wataandikiwa hati ya mashtaka na kupelekwa mahakamani,” amesema Muliro.Juzi Kamanda Muliro alitoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa hao kutokana na video, iliyorushwa mitandao mbalimbali ya kijamii, ikiwaonesha askari hao wakimshambulia kwa rungu Orotho.Askari hao walimshambulia Orotho kwa madai ya kutolipa faini ya usafi kiasi cha Sh 50,000. Muliro aliwakumbusha wananchi na vyombo vyote vya umma na binafsi kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za nchi na kuacha kuchukua sheria mikononi pale wanapokuwa wakidai haki zao. | kitaifa |
Na Safina Sarwatt WATUMISHI wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuwa na utayari wa dawa na vifaa tiba katika jengo maalumu la maradhi ya mlipuko, ili liweze kutoa huduma stahiki kama atatokea mgonjwa mwenye virusi vya corona. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati alipokagua jengo maalumu la maradhi ya mlipuko na kuzungumza na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo. Alisema tayari serikali imeshakamilisha kila kitu kinachohitajika hivyo hawana budi kujipanga ili kutoa huduma stahiki endapo atapatikana mtu mwenye virusi hivyo kwenye eneo hilo. Dk Ndungulile alisema hadi hivi sasa hakuna kisa cha mtu yoyote nchini mwenye virusi hivyo lakini Serikali inajipanga kuhakikisha itakabiliana navyo endapo vitafika nchini. “Kwakuwa jengo hilo ni la dharura hata watumishi watakao toa huduma wanatakiwa kukaa mkao wa dharura wakati wote kwasababu ugonjwa hauna muda maalumu, ifahamike kwamba dereva wa gari la wagonjwa ni nani, anayesimamia utunzaji dawa ni nani, gari ipi itakayo tumika ili kuondoa sitofahamu pindi itakapotokea, “alisema. Dk Ndungulile alisema haitakuwa vyema Serikali kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kutoa huduma za magonjwa ya dharura na mgonjwa akitokea ashindwe kutibiwa. Tume ya Afya ya China jana ilisema kulikuwa vifo vipya 143, hivyo idadi ya waliofariki dunia kutokana na virusi hivyo mpaka sasa ni 1,523. Kati ya vifo hivyo vipya, vinne viliripotiwa katika mji wa Hubei. Pia watu wengine 2,641 wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo na kufanya idadi ya waathirika wa janga hilo mpaka sasa kufikia 66,492. Mbali hayo pia aliipongeza hospitali hiyo kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa Serikali wa GEPG kutoka sh millioni 1 hadi milioni 8 kwa siku. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mawenzi, Dk. Jumanne Karia alisema hivi sasa wanajipanga na timu yake katika kuhakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa sambamba na kuongeza ukusanyaji wa mapato. “Hospitali imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza ukusanyaji wa mapato, ambapo kwasasa hospitali kwa siku inakusanya milioni 8 na bima ya afya milion 180 kwa mwezi, “alisema. | afya |
UANZISHWAJI wa Akaunti Jumuifu ya Hazina imesaidia katika kudhibiti matumizi ya fedha za umma, ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za kulipa mishahara watumishi wa umma.Hayo yamebainishwa jana na Kamishna Msaidizi wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Charles Mwamwaja alipokuwa akijibu maswali ya wabunge wakati wa semina iliyojumisha wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na ile ya Hesabu za Serikali (PAC).Katika swali lake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia alitaka kujua kama mfumo huo wa Akaunti Jumuifu ya Hazina ina manufaa yoyote hasa kutokana na halmashauri kushindwa kutumia fedha katika mwezi wa kwanza wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2018/19kutokana na mfumo huo kushindwa kufanya kazi."Tulipoanza kutekeleza bajeti ya mwaka 2018/19 kwa mwezi mzima halmashauri zimeshindwa kutumia fedha, ingawa zile za mishahara zilikuwa zinapatikana, sasa nataka kujua kama mfumo huo una manufaa?"Dk Mwamwaja alisema pamoja na changamoto za upya wa mfumo huo, ila umekuwa na faida kubwa na kutolea mfano kuwa baada ya kuisha mwaka wa fedha 2017/18 kulikuwa na matokeo chanya ya kuwapo kwa fedha ambazo zimevuka mwaka.Alisema pia kupitia mfumo huo, serikali imekuwa inaweza kufuatilia mapato na matumizi ya kila halmashauri hapa nchini jambo ambalo limeisaidia serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za umma."Hata kwenye suala la ulipaji mshahara, mbali na udhibiti wa watumishi hewa na wale wenye vyeti feki, bado gharama za kulipa mishahara ya watumishi wa umma imepungua kwa kiasi kikubwa," alisema.Katika swali lingine Nkamia alihoji ni kwa nini bajeti za mashirika na taasisi za umma ambazo zimekuwa zikitoa gawio kwa serikali lakini bajeti zake hazionekani kwenye bajeti kuu ya serikali kama ilivyo nchi za Kenya na kwingineko.Dk Mwamwaja amesema ni kweli kuwa kwa sasa bajeti za taasisi na mashiriki ya umma hazioneshani kwenye bajeti kuu ya serikali na kuongeza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha siku zijazo bajeti hizo zinakuwa wazi kwa umma na bunge."Ukiangalia kwenye Sheria ya Bajeti inazungumzia kwa uwazi suala la kuingiza bajeti za mashirika na taasisi za umma kwenye bajeti kuu na huko ndiko tunakoelekea kuwa taarifa za kina za bajeti ya mashirika na taasisi za umma ziwe wazi ili wabunge waweze kushauri," alisema.Aidha, Dk Mwamwaja alisema changamoto kubwa ya madeni ya serikali inatokana na kutokuwa na uwiano wa mapato na matumizi na kuwa kwa sasa serikali imejipanga kushughulika na suala hilo kwa taasisi kutekeleza bajeti zao kulingana na fedha walizopangiwa.Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Bernadeta Mushashu (CCM) alihoji ni kwa nini madeni ya serikali yanalimbikizwa?Aidha, akichangia Mbunge wa Iramba Mashariki, Alan Kiula (CCM) alisema kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa kwa serikali na Bunge hasa kutokana na bajeti inayowasilishwa kutokuwa na taswira ya uhalisia na kuhimiza haja ya kuishirikisha sekta binafsi katika suala zima la mapato. | kitaifa |
SERIKALI imesema uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kuzuia Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri (DEDs) kusimamia uchaguzi, hayawezi kuathiri uchaguzi wowote wa marudio wala uchaguzi zijazo.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi (pichani) alisema tayari wametoa taarifa ya nia ya kukata rufaa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kupinga uamuzi uliotolewa Ijumaa iliyopita na jopo la majaji watatu.Amesema amekuwa akiulizwa kuhusu athari za uamuzi huo kuhusu uchaguzi ujao na chaguzi ndogo za marudio hivyo hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani nafasi ya kukata rufaa ipo.Profesa Kilangi amesema, mpaka sasa hawajapata nakala ya uamuzi huo ili waweze kujiridhisha ni kitu gani hasa mahakama hiyo imeelekeza. Pia alisema kuwa kwa misingi ya sheria pale serikali inapotoa taarifa ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani, inaifanya hukumu hiyo isitekelezeke.“Kwa mujibu wa kifungu cha 14 (3) cha Sheria ya Utekelezaji wa haki na wajibu inasema serikali kwa maana ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa Wakili Mkuu wa Serikali akishatoa taarifa ya nia ya kukata rufaa basi hiyo taarifa moja kwa moja inazuia utekelezaji wa hukumu ile,” alifafanua Profesa Kilangi.Alisisitiza kuwa ibara ya 30 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeeleza mambo yanayoweza kufanyika katika mazingira kama haya na katika sheria kifungu cha 13 pia kimeeleza.Akizungumzia sababu za kukata rufaa, Profesa Kilangi alisema wanakata rufaa kupinga ubatilishwaji wa kifungu cha 7 (1) na kifungu cha 7(3) ambavyo mahakama ilisema kuwa vinakinzana na Katiba ya mwaka 1977.Katika vifungu hivyo vya sheria ya uchaguzi ambavyo vinatamka kuwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa na Halmashauri anaweza kusimamia uchaguzi na kifungu cha 7(3) kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kuteua wasimamizi wa uchaguzi miongoni mwa watumishi wa umma pale inapoona inafaa.Alisema kuwa baadhi ya vifungu ambavyo mwanachama wa Chadema, Bob Wangwe alivipinga mahakamani iliona havina ukinzani na badala yake ni halali kuendelea kutumika kama vile kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambacho kinamtambua Mkurugenzi wa Uchaguzi anateuliwa na Rais kutoka katika utumishi wa umma na kifungu cha 7 (2). | kitaifa |
MAHAKAMA ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imepanga kuwa na Jukwaa la pamoja kujadili masuala ya msingi ya biashara kukuza uchumi.Akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma mapema wiki hii, Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte alishukuru pendekezo la kuwa na jukwaa hilo na kusema litasaidia zaidi kukuza uchumi wa taifa.“Jukwaa hili ambalo tumependekeza kufanyika mara nne kwa mwaka litasaidia TPSF na Mahakama ya Tanzania kujadili changamoto kwani kuna Mashauri ya Kibiashara ambayo yakimalizwa mapema biashara zitaendelea na hatimaye uchumi utakua,” alisema Shamte.Mbali na Jukwaa, Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF na Wajumbe wa Bodi wa Taasisi hiyo ambao walimtembelea Jaji Mkuu kujitambulisha, aligusia pia juu ya ucheleweshaji wa baadhi ya Mashauri ya Kibiashara Mahakamani.“Napongeza Mahakama kuendelea kuboresha huduma zake na kugusia baadhi ya mashauri ya biashara yanayochukua muda mrefu, Tunaomba Jaji Mkuu uangalie jambo hili kipekee,” alisema.Ujumbe huo uligusia kuboresha na kukuza sekta ya biashara na uwekezaji nchini ambayo Mahakama ina mchango katika kufanikisha hili. Jaji Mkuu wa Tanzania, Juma aliwahakikishia wajumbe kasi ya maboresho ambayo Mahakama inafanya ikiwemo matumizi ya TEHAMA.“Mahakama ya Tanzania ina baadhi ya mifumo inayofanya kazi, Mfumo wa Utunzaji Takwimu Kielektroniki (JSDS), ‘e-filling’ na kadhalika,. Tunahitaji ushirikiano na wadau kuhakikisha Mahakama inatoa haki,” alisema Jaji Mkuu.Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania ipo tayari kuipitisha TPSF kuhusu mifumo hiyo kuona jinsi gani inafanya kazi kwa maslahi yao. Jaji Mkuu alibainisha mikakati ya mahakama kukabili mlundikano wa mashauri katika ngazi za mahakama akitoa wito kwa mawakili na wadau kufanya kazi kwa weledi na kutoa haki.Alisema mahakama za mwanzo zimejiwekea miesi sita kumaliza kesi, za Wilaya/ Mkoa kesi zisizidi mwaka mmoja na Mahakama ya Rufani na ile ya Mahakama Kuu zisizidi miaka miwili. | kitaifa |
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imejiweka katika nafasi nzuri ya kukata tiketi ya kushiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani inayotarajiwa kufanyika Cameroon.Stars ilifufua matumaini hayo baada ya kuwachapa Cape Verde mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumanne ya wiki hii ambapo mabao hayo yalifungwa na Simon Msuva na Mbwana Samatta.Kabla ya mchezo huo, Stars walikuwa na pointi mbili wakiburuza mkia wa Kundi L ambalo lilikuwa linaongozwa na Uganda waliokuwa na pointi saba, Cape Verde nne, Lesotho mbili ambao walikuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga, huku kila timu ikiwa imeshacheza mechi tatu.Siku tatu kabla ya mchezo huo ambao Stars walionesha kiwango kikubwa cha hali ya juu, walipokea kichapo cha kikatili cha mabao 3-0 walipokuwa ugenini Praia, Cape Verde.Kocha wa Stars, raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike, anasema haikuwa rahisi mpaka kuifanya timu hiyo kuwa na ari kubwa ya kupambana katika mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi iliyopita kwa mabao mengi.Anasema kuwa kazi hiyo hakuifanya peke yake bali benchi zima la ufundi, wachezaji, serikali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na wadau wote wa soka, kila mmoja alifanya kazi yake kikamilifu kuelekea mchezo huo ambao ulikuwa unahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri.Amunike anasema: “Tulivyorudi kutoka Cape Verde ambapo tulifungwa 3-0 ulikuwa ni muda mgumu kwetu lakini tukakaa pamoja na kujaribu kujipa moyo tukiamini kuwa tunaweza hivyo tusife moyo, kikubwa kilichonifurahisha nipale nilipoona wamefanya kile ambacho tulikuwa tunakizungumza na kukifanyia kazi,” anasema.“Cape Verde ina wachezaji wazuri ambao baadhi yao wanacheza Ufaransa na wengine Ureno, ukiwaangalia uwezo wao uwanjani utagundua kabisa sio watu wa mchezomchezo, wanajua jinsi ya kumiliki mpira na kuutafuta pale wanapoupoteza. ”Kocha huyo ambaye aliichezea FC Barcelona enzi zake, anasema kwa muda mfupi aliokaa nchini, amegundua kuwa nchi hii ina rundo la wachezaji wazuri ila hawakuwa wakitumika vizuri.“Katika mpira silaha kubwa ni kukiamini kikosi chako kinapokwenda kwenye mapambano, nimegundua kuwa Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kuwa na wachezaji wengi wazuri wanaojitambua, nimefurahishwa na jinsi wachezaji wangu kucheza kwa kujituma.Amunike anajua fika kiu ya watanzania ipo katika kuiona Stars inashiriki Afcon mwakani baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1980, lakini anaweka wazi kuwa jambo hilo linahitaji uvumilivu na sio kama litakuja ghafla kama wengi wanavyodhani.“Napenda kila mmoja atambue kuwa kila safari ina changamoto zake huwezi kwenda safari bila kukutana na vikwazo njiani, hivyo tunavyosema kuwa tunakwenda Cameroon tujue tutakutana na vitu vingi ambavyo vitatukatisha tamaa ila kitu kikubwa ambacho ni muhimu ni kujituma zaidi, kuanzia mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla, tunajua kama tutafanya hivi tunaweza kusonga mbele.“Nimefurahishwa na watanzania kwa kile walichokifanya katika mchezo huu, nawashukuru mashabiki wote kwa kuja uwanjani, najua inakuwa ngumu kuamini kuwa tutashinda baada ya kufungwa 3-0 lakini watu wengi walikuja na kutushangilia mwanzo mwisho…“Mbali na mashabiki pia napenda kuvishukuru vyombo vya habari kwa kazi mliyoifanya, ushauri wangu ni kuwa tuzidi kuwa pamoja, tusipoteze imani na timu yetu inabidi tuje uwanjani na tuwe tunawatia moyo wachezaji wetu nawashukuruni sana tuendelee kupambana pamoja naamini tunaweza kupata tiketi ya kwenda Cameroon.”Baada ya ushindi katika mchezo huo Stars imefikisha pointi tano na kubadili msimamo wa kundi ambapo Uganda ambao waliwafunga Lesotho wamekaa kileleni wakiwa na pointi 10, Stars wakapanda kutoka mkiani hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi tano, Cape Verde wakashushwa mpaka nafasi ya tatu na pointi zao nne na Lesotho wanashika mkia wakiwa na pointi 2 , hilo limemfanya Amunike ajawe na furaha isiyo kifani.“Kikubwa kilichonifurahisha tulikuwa mkiani mwa kundi lakini ghafla tumekuwa wa pili, kila kitu kinawezekana kama tukiwa pamoja kwa kushirikiana, sina wasiwasi kabisa naamini kwa sasa tutaendelea kuwa pamoja na timu yetmu hii.“Siku zote kila mtu huwa na ndoto ya kufanya kitu fulani ila inatakiwa uwe na mipango madhubuti, ukiangalia tupo kwenye kundi lenye nchi nne na kila mmoja anatamani kwenda Cameroon, sio jambo rahisi kihivyo kujiaminisha kuwa sisi tutaenda,” anasema.Ratiba inaonesha kuwa Novemba 19, Stars itakuwa ugenini kucheza na Lesotho ambao kama watashinda watajisafishia zaidi njia. Mara tu dakika 90 za mchezo dhidi ya Cape Verde kumalizika tayari Amunike ameshahamishia akili zake zote katika mchezo huo ujao ambapo anasema: “Mchezo wetu ujao ni dhidi ya Lesotho siwezi kutabiri kitatokea nini lakini nataka kuhakikisha hatufanyi makosa ambayo yatatugharimu, nitaiandaa timu ya kupambana nao na kuwashinda.” Naam, ni kweli Tanzania ipo kwenye nafasi nzuri, ingawa si rahisi kihivyo, bado tunahitaji kujipanga ili kufanikisha hilo. | kitaifa |
BADI MCHOMOLO MIONGONI mwa vitu ambavyo vimechangia kwa mabingwa
wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid kushindwa kufanya vizuri
msimu huu ni kutokana na kuondoka kwa kocha wao Zinedine Zidane. Zidane aliondoka ikiwa ni siku chache baada ya kuipa
timu hiyo ubingwa wa tatu mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kuwafunga Liverpool mabao 3-1, hivyo nafasi yake ikachukuliwa na Santiago
Solari, ambaye alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya Hispania kwa wakati huo. Solari halishindwa kuwatumia wachezaji hao ambao
waliandika historia ya kubeba taji hilo kubwa kwa misimu mitatu mfululizo, hakuna
kikubwa ambacho alikiongeza, ila inaonekana kwamba halishindwa kuwatumia
wachezaji hao. Hiyo ilikuwa moja ya sababu, lakini sababu nyingine
ni kuondoka kwa aliyekuwa mshambuliaji wao hatari Cristiano Ronaldo. Ronaldo alikuwa mmoja kati ya wachezaji wenye
mchango mkubwa wa mafanikio ya timu tangu alipojiunga mwaka 2009. Baada ya kuisaidia Real Madrid kuchukua taji hilo la
Ligi ya Mabingwa mwaka jana, mchezaji huyo aliondoka na kujiunga na klabu ya
Juventus ambayo anaitumikia kwa sasa. Kuondoka kwa wawili hao kukaacha pengo kubwa ambapo
hadi sasa linaonekana kuwa wazi. Madrid wamejikuta wakiondolewa kwenye michuano
hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora dhidi ya Ajax ikiwa ni
mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22. Hata hivyo, kwenye michuano ya Ligi Kuu Hispania timu
hiyo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi huku Atletico Madrid
wakishika nafasi ya pili na nafasi ya kwanza ikiendelea kushikiriwa na mabingwa
watetezi Barcelona. SPOTIKIKI imekufanyia uchambuzi wa kina ambao Zidane
anaamini anaweza kurudisha heshima ya timu hiyo kutokana na mambo sita. Kupewa
huru Hii ni moja kati ya pointi ambayo Zidane aliomba
kutoka kwa rais wa timu hiyo Florentina Perez. Wakati wanazungumza juu ya
kumrudisha kuwa kocha mkuu kitu cha kwanza alichokiomba ni kupewa uhuru wa
kufanya kazi yake. Kumekuwa na madai kwamba, baadhi ya makocha wamekuwa
wakiingiliwa kwenye majukumu yake ya kazi hasa pale anapofanya maamuzi ya
kuwachukulia hatua wachezaji. Hivyo Zidane anaamini akipewa uhuru wa kazi,
atahakikisha anarudisha heshima ya timu hiyo ambayo ilianza kupotea tangu
kuondoka kwake. Kuuza
wachezaji Kocha huyo mpya anaamini katika kikosi cha timu hiyo
kuna wachezaji ambao hawafai kuitumikia timu, hivyo akisema wachezaji hao
wauzwe basi kitendo hicho kifanyike. Hata kama hakitofanyika, basi akiamua kumuacha
benchi kusitokee na mtu yeyote kumpigia kelele kwa nini mchezaji fulani
anaachwa benchi. Uwepo
wa Marcelo na Isco Hawa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa
kutakiwa kuondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu. Marcelo anahusishwa kutaka kumfuata rafiki ya
Cristiano Ronaldo katika klabu ya Juventus, wiki kadhaa zilizopita beki huyo wa
pembeni aliweka wazi kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba ana kila sababu ya
kuondoka na anavutiwa kujiunga na Juventus. Hata hivyo, inasemekana kuwa Ronaldo anachochea mchezaji
huyo kutua katika klabu hiyo ya Bibi Kizee wa Turin. Kwa upande mwingine Isco ni mmoja kati ya wachezaji
ambao walikuwa na nafasi kubwa chini ya Zidane misimu iliopita, lakini baada ya
kuondoka mchezaji huyo amekua akikosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza
chini ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Solari. Kutokana na hali hiyo Isco aliweka wazi kuwa, haoni
sababu ya kuendelea kuwa mchezaji wa timu hiyo, hivyo ni wakati wa kuondoka
huku Manchester City ikiwa chini ya kocha wake Pep Guardiola ikiwa na lengo la
kuinasa saini ya mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu. Lakini ujio wa Zidane ndani ya Madrid, unaweza
kurudisha furaha za wachezaji hao kwa kuwa ameomba kuwazuia kuondoka kwao. Neymar
hasisajiliwe Rais Perez amekuwa akisikika kua na nia ya kutaka
kumsajili Neymar raia wa nchini Brazil ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu
ya PSG. Neymar anahusishwa kutaka kurudi nchini Hispania
ikiwa pamoja na klabu yake ya zamani ya Barcelona, lakini Zidane amedai kwamba hakuna
sababu ya Madrid kumsajili mchezaji huyo. James
Rodriguez Huyu ni nyota wa Real Madrid ambaye kwa sasa
anakipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa mkopo, kumekuwa na taarifa kwamba
kutokana na kiwango anachokionesha mchezaji huyo Madrid wanataka kumrudisha. Lakini Zidane amedai hayupo kwenye mipango yake,
hivyo ni bora akaachwa aendelea kuitumikia Bayern Munich kwa mkopo au kuuzwa
moja kwa moja. Usajili
wa Mbappe Rais Perez alikuwa kwenye mipango ya kuboresha
kikosi hicho kwa kuwasajili nyota wa PSG, Neymar na Kylian Mbappe mara baada ya
kumalizika kwa msimu huu, lakini Zidane amedai Madrid wapambane kuhakikisha
wanaipata saini ya Mbappe. Kwa kufanya hivyo, kocha huyo amewahakikishia heshima
ya Real Madrid itarudi kama ilivyo misimu iliopita. Wapo ambao wameshangaa kuona Zidane akirudi Madrid, wanaamini
maamuzi hayo yanaweza kuja kushusha heshima yake kutokana na kile alichokifanya
akiwa na timu hiyo kwa miaka ya nyuma, bora angeacha historia aliyoiweka Madrid
na kwenda kujiunga na klabu zingine. | michezo |
LONDON, ENGLAND BAADA ya Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kumshambulia Arsene Wenger kwamba ni kocha ambaye yupo katika wakati mgumu wa kufukuzwa na klabu yake, naye Wenger amemjibu kocha huyo kwa kusema anajivunia kuwa na jina kubwa katika chama cha soka nchini England. Hata hivyo, Mourinho alimshambulia kocha huyo kwa kudai kuwa anapenda kuwalalamikia waamuzi wakati anapopoteza mchezo. Wenger alionekana kumtupia lawama mwamuzi Mike Dean ambaye alichezesha mchezo wa wapinzani hao wiki moja iliyopita, huku Arsenal ikikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Chelsea. Lakini Wenger amesema hana wasiwasi kwa kuwa ana jina kubwa na amekuwa kwenye soka kwa miaka zaidi ya 30, hivyo ana uzoefu mkubwa. “Najivunia kuwa nafanya kazi yangu vizuri na timu kwa ajili ya mashabiki wetu, nina uzoefu mkubwa katika soka kwa kuwa nimekuwa kwenye mchezo huu kwa miaka 30 sasa na najua umuhimu wa soka,” alisema Wenger. Hata hivyo, kocha huyo anaamini kuwa klabu yake ina nafasi kubwa ya kuweza kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kutokana na ushindi walioupata mwishoni mwa wiki wa mabao 5-2 dhidi ya Leicester City, huku Manchester City ambao walikuwa wanaongoza katika msimamo wa Ligi wakipokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Tottenham na kuwapisha Manchester United kileleni. “Manchester City wamepoteza mchezo wao wa kwanza ambapo kwa upande wetu unatupatia nafasi ya kusogea juu, michuano ni migumu lakini tunaamini tutafanya vizuri,” aliongeza Wenger. | michezo |
Shirikisho la Masumbwi duniani (WBO) limetaka bingwa wa mkanda wa uzito wa juu wa shirikisho hilo Muingereza Anthony Joshua kupambana dhidi ya Oleksandr Usyk ili kutetea mkanda huo la si hivyo aurejeshe mezani mkanda huo Joshua ambaye hajamaliza hata wiki tangu kurejesha mkanda huo kiunoni kwake toka kwa Andy Ruiz Jr itamlazimu kutii agizo hilo la WBO kwani kuna dalili kubwa za kupoteza sifa za kumiliki mkanda huo Mambo ni magumu kwa Joshua kwani hata mkanda mwingine anao umiliki wa IBF pia ameamuliwa kurejesha mezani au kupambana Kubrat Puven ambaye ana haki za kuomba kupewa mkanda huo iwapo Joshua anshindwa kuzichapa naye Shirikisho la mchezo huo dunia limetaka Joshua na timu yake kuhakikisha wanatoa maamuzi ndani ya siku 30 baada ya kupata barua hiyo la sivyo atanyanganywa mkanda huo ghali zaidi Kwa mujibu wa barua hiyo Joshua ana siku 180 tu za kujianda na kupambana na Usyk ambaye amepambana mapambano saba ya professional akiwa ameshinda mapambano matatu kwa K.O kwa manne kwa pointi | michezo |
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM BENKI ya I&M Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, lakini inang’ara kwa kutoa bidhaa na huduma za kipekee ambazo zinakidhi mahitaji yote ya mteja katika soko. I&M Tanzania ilitambulisha akaunti mpya ya wanawake ya Tunaweza inayotoa suluhisho kwa wanawake wa ngazi zote kuanzia mmoja mmoja, wajasiriamali hadi kikundi au taasisi. Akaunti hiyo inajitofautisha kwa kutoa huduma bila malipo yoyote, haina makato ya kila mwezi na viwango vyake vya riba vinavutia kwenye akiba. Akizungumza leo jijini Dar es Salaa, katika maonyesho hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M, Anitha Pallangyo, alisema kuwa bidhaa hiyo mpya imeunganishwa kwenye mtandao wa benki wa kidijitali ili kuwapa wateja huduma bora na endelevu wakati wowote wanapohitaji. Alisema I&M Tanzania ni sehemu ya I&M Holdings Kenya iliyoanzishwa mwaka 1974 kama kampuni ya huduma za kifedha kabla baadaye kubadilishwa kuwa benki ya biashara. “Mwaka huu inasherehekea miaka kumi ya huduma zetu katika soko la Tanzania. Tunafurahi kuendelea kuhudumia wateja wetu na wateja wapya, pia tunashukuru wateja wetu na washikadau wote walioshiriki katikakuiletea benki mafanikio makubwa kwa kipindi chote cha miaka kumi kwenye soko.” “Tunatoa huduma kadhaa za kifedha ikiwa ni pamoja na akaunti ya akiba, current akaunti kwa madhumuni ya biashara, mikopo ya biashara, huduma za kubadili fedha, uhamishaji fedha kitaifa na kimataifa, huduma za kidijitali ambazo hutoa fursa kwa mteja kupata huduma za benki kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *150*32# au kupitia iClick- huduma ya benki kwa njia ya mtandao inayopatikana bila kikomo kwa saa 24,” alisema Anitha Meneja Masoko na Mawasiliano huyo wa benki hiyo, alisema kuwa pia benki yao wanatoa unafuu na urahisi wa kupata mikopo na huduma nyingine kadhaa ambazo ziliwafanya watu waliotembelea banda lake kwenye maonyesho ya Sabasaba lililopo ukumbi wa Karume, upande wa kulia wa lango la kuingilia kuhamasika na kutaka kujua zaidi kuhusu benki hiyo. “I&M inafungua milango kwa Watanzania wote kwenda kujiunga na benki inayojali mahitaji yao, iliyo tayari kuwapa huduma za kipekee za kifedha kupitia wafanyakazi wake wenye uzoefu zaidi katika kutoa huduma bora kwa wateja. “Mbali na kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba, benki hiyo inatoa huduma zake bora kupitia mtandao wa matawi yake yaliyoko maeneo ya Maktaba, Indira Gandhi, Nyerere, Kariakoo, Oysterbay pamoja na mikoani ikiwa ni pamoja na Moshi, Arusha na Mwanza,” alisema Timu ya wafanyakazi wa mauzo na idara ya masoko wa benki hiyo kutoka matawi yake ya Dar es Salaam inayoongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M, Anitha Pallangyo na Ofisa Masoko na Mawasiliano, Debora Mwakyoma wapo kwenye maonyesho hayo ili kuwapa wageni na wale ambao wanataka kuwekeza katika benki inayoaminika na salama ikiwa na huduma za ATM zinazopatikana kwa saa 24. | uchumi |
Na CHRISTIAN BWAYA FARIDA amekuwa akisifika kuwa ni mtoto mwenye nidhamu kwa wazazi wake. Mara zote ana usikivu, utii na heshima kwa watu. Hadi anamaliza darasa la saba, hakuwahi kupishana kwa vyovyote na wazazi wake. Mambo yalianza kubadilika alipofika kidato cha pili. Siku moja wakati muda wa kwenda kanisani umefika, hakuonekana kuwa na haraka tofauti na kawaida yake. “Unafanya nini muda wote mbona kama huna haraka?” aliuliza mama yake kwa hasira. “Najiandaa mama,” alijibu huku akiendelea kutengeneza nyusi zake. “Muda umeisha mwanangu tunachelewa,” baba aliamua kuingilia kati. Ukweli ni kwamba Farida hakuwa na nia ya kwenda kanisani akiambatana na wazazi wake. Alichokosa ni ujasiri wa kulisema hili wazi wazi kwa wazazi wake. Baada ya dakika 10 za kusubiri, baba alikumbushia kwa hasira: “Farida tunakusubiri.” “Basi tangulieni baba. Nitakuja mwenyewe!” Hicho ndicho alichokuwa anakitaka. Hakupenda kuambatana na wazazi wake. Katika umri wake wa miaka 14, Farida ameanza kujenga umbali na familia yake. Wazazi wake wanapozungumza naye, haonekani kufuatilia wanachokisema. Zamani, kwa mfano, alikuwa mchangamfu katika mazungumzo. Siku hizi ameanza kuwa mkimya hasa anapokuwa nyumbani. Hata hivyo, anapokuwa shuleni akiwa na marafiki zake, Farida ni mwongeaji mzuri. Kwanini basi Farida anakuwa mkimya anapokuwa nyumbani? Ukweli ni kwamba, Farida ana mambo mengi moyoni mwake kwa kuwa ni kijana chipukizi. Matamanio ya kujihakikishia hadhi sawa na mtu mzima yanamfanya ahisi wazazi wake hawamwelewi. Wanaposisitiza kwenda naye kanisani, hiyo kwake ni sawa na kumchukulia kama mtoto asiyeweza kujisimamia. Ingawa anahitaji uhuru zaidi, wazazi wake wana wasiwasi. Wanajua hatari ya uhuru huo na wanaamini bado ni mtoto anayehitaji uangalizi wa karibu. Wakifanya hivyo, Farida anahisi ‘kufuatwa fuatwa.’ Katika mazingira kama haya, wazazi wanahitaji kuangalia namna ya kumfanya Farida ajisikie kuwa na uhuru kiasi hata kama bado watakuwa wanamfuatilia bila yeye kujua. Uhuru wa wastani utamfanya aamini wazazi wake wanatambua hadhi mpya aliyonayo. Katika umri alionao, Farida anatamani kutumia muda mrefu akiwa na marafiki zake zaidi kuliko familia yake. Mtandao mpya wa marafiki mbali na familia yake unamsaidia kutengeneza haiba yake akiwa mtu mzima. Hali hii, hata hivyo, inawatia hofu wazazi. Wazazi, kwa kutambua hatari ya uhuru, wanatamani kumdhibiti zaidi. Kadiri wanavyojaribu kumdhibiti, wanashangaa tatizo jingine linajitokeza. Umbali na tofauti za mara kwa mara zinaendelea kuongezeka. Badala ya kumdhibiti, hali inayoweza kumfanya ajihisi bado mtoto, inashauriwa kujenga ukaribu wa mawasiliano yanayotambua uhuru wake. Mitazamo mipya inayo hitalifiana na wazazi, ni hali inayotarajiwa kwa kijana chipukizi kama Farida. Hali hii mara nyingi hutengeneza mashindano yasiyo ya wazi kati ya mzazi na kijana wake. Kinachoshindaniwa, mara nyingi ni mamlaka. Mzazi anahisi mamlaka yake yanadharauliwa na mtoto anayejifanya mjuaji, na mtoto naye anajihisi bado anaonekana mtoto asiye na sauti. Mashindano haya ya kichini chini yanaweza kupanda ngazi na kugeuka kuwa ukosefu wa nidhamu. Mtoto anamwona mzazi wake kama mkoloni aliyepitwa na wakati na mzazi naye anamwona kijana chipukizi kama mtoto asiyejua maisha ni kitu gani. Katika mazingira kama haya, kupambana naye inaweza isiwe njia mwafaka. Kadiri unavyopambana naye, ndivyo unavyojenga ukuta wa mawasiliano baina yenu. Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Kwa unasihi wasiliana naye kwa 0754 870 815. | afya |
Tangu wiki iliyopita, Simba imekuwa kwenye maandalizi ya kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu katika mchezo huo utakaopigwa Aprili 3, mwaka huu mkoani Njombe ili kuzidi kujiweka sawa katika kuwania ubingwa msimu huu.Lechantre amefunguka akisema baada ya kuisuka timu yake kwenye kupambana kucheza kwa mbinu tofauti katika mechi inayohitaji matokeo na siyo pointi kama ilivyokuwa kwa Al Masry ya Misri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, sasa amebadili mipango na amewaeleza wachezaji wake nini cha kufanya ili kumaliza mchezo mapema dhidi ya Njombe.Amefafanua zaidi kuwa katika mechi hiyo hakuna cha ziada cha kufanya zaidi ya kushambulia na kucheza kwa kuwaandama wapinzani wao mwanzo mwisho ili kuhakikisha wanaanza vyema kuondoka na pointi tatu katika mechi hiyo kati ya 30 zilizosalia kabla ya kumalizika kwa ligi msimu huu.“Maandalizi yamekuwa mazuri na tumekuwa na mbinu za tofauti kuelekea katika mechi hiyo maana hii ni tofauti na ile ya Al Masry.Kule wachezaji walibadilika kutokana na mechi ilihitaji matokeo zaidi na si pointi tatu, lakini huku tunahitaji zaidi pointi.“Kwa hiyo lazima tubadilike kutokana na mazingira, maana mechi ya Njombe muhimu zaidi ni pointi, hivyo tutaingia kwa lengo la kushambulia kwa muda wote langoni mwa wapinzani na kufanya kila linalowezekana kutokana na tulivyojiandaa kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu," alisema kocha huyo Mfaransa. | michezo |
VIHIGA, KENYA MREMBO kutoka Homa Bay, Rebella Omollo, ameshinda tuzo ya Miss Utalii 2016 nchini Kenya katika kinyang’anyiro cha warembo 44 waliotoka maeneo mbalimbali nchini humo. Rebella aliibuka mshindi usiku wa kuamkia jana huko Vihiga, ukumbi wa Kidudu nchini Kenya. Shindano hilo lilionekana kuwa na ushindani wa hali ya juu hasa kwa warembo sita waliokuwa wakiwania nafasi tatu za juu lakini Rebella alionekana kufanikiwa kuwashawishi majaji kutokana na uwezo wake wa kujieleza pamoja na tabasamu lake la kuvutia. “Tunakubali kwamba hakuna mtu ambaye anakubali kukaa kwenye nchi ambayo haina amani. Kenya ina makabila 42 pamoja na tamaduni 42 lakini wote tunaonekana kuwa pamoja kama Wakenya. “Tuna amani ya kutosha, hii ni nchi ambayo unaweza ukaishi na wala usione tofauti yoyote. Tunapenda kutumia neno ‘Hakuna matata Kenya’. Tunawakaribisha wageni wote duniani kwa ajili ya kuishi na sisi, kufanya ziara na mambo mengine mengi. “Napenda kuwashauri Wakenya wenzangu kuipenda nchi yetu kufanya uwekezaji katika biashara, bila sisi wenyewe hakuna atakayekuja kufanya hivyo,” alisema Rebella. | burudani |
SERIKALI ya Tanzania imesema itaendelea kufanya kazi kwa karibu na kuimarisha uhusiano wake wa muda mrefu na wa kihistoria na Serikali ya Poland kwa faida ya nchi zote mbili.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwingi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya Uhuru wa Poland zilizofanyika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam juzi.Balozi Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, alisema Tanzania na Poland zinajivunia ushirikiano mzuri walionao tangu wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939-1945.Alisema wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, maelfu ya wananchi wa Poland walipewa hifadhi ya ukimbizi Tanzania Bara wakati huo ikijulikana kama Himaya ya Uingereza Tanganyika (Britain’s Tanganyika Territory).“Kulikuwa na kambi sita katika Tanganyika ambapo kambi kubwa ilikuwa kwenye Kijiji cha Tengeru mkoani Arusha na kambi zingine ndogo zilikuwa maeneo mbali mbali ikiwemo mkoani Kigoma, Kidugala na Ifunda (Iringa), Kondoa (Dodoma) pamoja na Morogoro,” alieleza Balozi Mwinyi.Kwa mujibu wa Balozi Mwinyi, wananchi hao wa Poland wakiwa nchini Tanzania, waliamua kujiendeleza kimaisha ikiwemo kujishughulisha na kilimo, biashara ndogondogo, kujenga kliniki, hospitali, makanisa na shule.Baada ya kwisha kwa vita hivyo, imeelezwa kuwa wengi wa wananchi hao wa Poland waliamua kurudi nchini mwao, lakini wengine waliamua kubaki Tengeru mpaka sasa. Kutokana na histori hiyo, Balozi Mwinyi alisema Poland imeendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa Tanzania katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu.“Nchi zetu hizi mbili zinashirikiana kwenye kilimo, biashara, uwekezaji, elimu hususan kupitia udhamini wa masomo kwa Watanzania kusoma nchini Poland pamoja na sekta ya maji,” alieleza Balozi Mwinyi.Aliongeza kuwa Serikali ya Poland imesaidia katika uunganishwaji wa matrekta ya URSUS nchini kwenye Kiwanda cha TAMCO kilichopo Kibaha mkoani Pwani. Alisema Poland pia inatoa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania namna ya kuunganisha na kutengeneza matrekta hayo.Mbali na mradi huo wa matrekta, alisema Serikali ya Poland pia inasaidia katika ujenzi na ukarabati wa maghala ya kuhifadhia nafaka kwenye mikoa minane ya Rukwa, Katavi, Manyara, Ruvuma, Dodoma, Shinyanga, Njombe na Songwe.Alisema maghala hayo yatakapokamilika, yataongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani za ujazo 251,000 za sasa hadi kufikia tani za ujazo 501,000. Kwa mujibu wa Balozi Mwinyi, Tanzania imeendelea kuvutia watalii kutoka Poland kwa kuwa kila mwaka watalii 12,000 hufika Kisiwani Zanzibar. Alisema idadi hiyo imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka miwili kwa kuwa mwaka 2016 watalii waliofika Kisiwani humo kutoka Poland walikuwa 7,000 tu.Kwa kuwa malengo ya Tanzania ni kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025, alisema ni muhimu kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi na kutoa wito kwa kampuni za Poland kuja kuwekeza nchini.Kwa upande wake, Balozi wa Poland nchini, Krzysztof Buzalski alisema anafurahi kuona ushirikiano wao na Tanzania unazidi kuimarika wakati ambao taifa lao linatimiza miaka 100 ya uhuru wake.Balozi Buzalski alisema Tanzania na Poland zinahitaji kushirikiana kwa dhati kwa kuwa ndiyo njia pekee ya nchi hizo kunufaika na fursa walizonazo kama vile teknolojia, bidhaa, kilimo na utalii.“Kama ulivyo msemo wa Kiswahili kwamba ‘Mvumilivu hula mbivu’, hivyo tunahitaji kuwekeza muda wetu, nguvu zetu na juhudi zetu ili tuweze kufanikisha haya,” alieleza Balozi Buzalski. | kitaifa |
Yanga juzi iliifunga Mwadui FC ya Shinyanga mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC iliifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 Uwanja wa Manungu, Turiani.Azam imemaliza mechi zake za viporo, ambapo imecheza mechi 24 ikiwa na pointi 55 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga iliyocheza mechi 23 ikiwa na pointi 56.Yanga itamaliza mechi yake ya viporo Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba ndiyo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 24.Kocha Mayanja alisema ushindi wa Yanga na Azam umezidisha ugumu kwenye ligi na sasa hawana budi kuongeza jitihada kushinda mechi zao.“Hakuna kupumzika, lazima kichwa kiume kujua tutafanya vipi kuwa mabingwa, ligi imezidi kuwa ngumu,” alisema.Taji la ubingwa wa ligi ndilo pekee lililobaki kwa Simba kulipigania baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Kombe la FA) mwanzoni mwa wiki hii.Simba inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili kuikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mechi yenye ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hiyo ya Mwanza kutoa upinzani mara kwa mara inapokutana na Simba.“Mechi yetu na Coastal ni ngumu, na matokeo ya wapinzani wetu yamefanya iwe ngumu zaidi, kwani sasa ni lazima tushinde kama tunataka kuendelea kwenye mbio za ubingwa,” alisema Mayanja. | michezo |
UCHAGUZI mdogo wa Jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida lililokuwa likiongozwa na Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, utafanyika Julai 31, mwaka huu.Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage, alisema jana kuwa NEC tayari imetoa Ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge, Jimbo la Singida Mashariki baada ya Spika, Job Ndugai kuitaarifu tume hiyo uwepo wa nafasi ya wazi ya ubunge katika jimbo hilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Singida.Juni 29, mwaka huu, Spika wa Bunge, Ndugai alitangaza Lissu kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa Spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba mfululizo ya Bunge bila ruhusa ya Spika.Hata hivyo indaiwa Lissu yuko Ubelgiji kwa matibabu.Jaji Kaijage alisema amezingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa uchagu huo mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki.Kwa mujibu wa Jaji Kaijage, fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Julai 13 hadi Julai 18, mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika Julai 18, mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Julai 19 hadi Julai 30, mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni Julai 31, mwaka huu.Kaijage alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya NEC wakati wa kipindi cha uchaguzi huu mdogo.Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu alipopigiwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa Dodoma katika vikao vya Bunge lakini baada ya matibabu Nairobi nchini Kenya na Brussels nchini Ubelgiji, amekuwa akionekana akifanya ziara katika nchi kadhaa za Ulaya na marekani na kuishutumu Serikali ya Tanzania. | kitaifa |
Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, asili yake na wazazi wake kisiasa ni Chama cha ASP na hajawahi kufikiria kuunga mkono upinzani kama ambavyo Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anavyompakazia na kumchafua kisiasa. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, kutokana na matamshi ya Maalim Seif akiwa ziarani Mkoa wa Mjini Magharibi na kudai kuwa Samia anaunga mkono upinzani. Shaka alisema si jambo la kutarajiwa kwa Maalim Seif ajivike joho la uzushi na uongo na kutoa madai yasiyokuwa na mashiko. Alisema madai yake kuwa Makunduchi si eneo la ASP na kwa asili ni upinzani si kweli, kwa sababu katika uchaguzi wa mwisho mwaka 1963, Sheikh Idris Abdul Wakil wa ASP, alimshinda Sheikh Ameir Tajo wa ZPP katika kiti cha uwakilishi katika Bunge la Legco. “Samia ni mzaliwa wa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na aliwahi kuwa mwakilishi wa jimbo hilo katika Baraza la Wawakilishi, Zanzibar. Maalim Seif amejaribu kupandikiza chuki na kuwagawa Wazanzibari lakini ameshindwa. Ametaka urais tangu mwaka 1984 hadi 2015 ameukosa,” alisema. Shaka alisema anaelewa Maalim Seif anawachukia wananchi wa Makunduchi kutokana na kuwania urais na Mzee Wakil akamshinda, akamvua cheo cha Waziri Kiongozi kisha Serikali yake ikamuweka kuzuizini kwa muda wa miaka mitatu. “Anatapatapa na kutaka kueneza siasa za mgawanyiko ili akubalike Makunduchi. Wananchi wa Mkoa wa Kusini hawajasahau dhihaka ya kuitwa ng’ombe kwa ushabiki wa Maalim Seif aliyemchafua hayati Mzee Wakil,” alisema. Pia alimtaka asimpakazie Samia kuwa anataka kuwania urais wa Zanzibar mwaka 2020 wakati sasa hivi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Alifukuzwa mwaka 1987 kwa jaribio la kuipasua CCM. Mwalimu Julius Nyerere alimbeba Maalim Seif, lakini aliambiwa huyo ni mzito humuwezi akabisha, mwishowe alimfukuza,” alisema. Shaka alisema hata Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe, alipoaswa na aliyekuwa Waziri Kiongozi, Ramadhani Haji Faki, asimteue alibisha na matokeo yake Maalim Seif alimgeuka na kusababisha akavuliwa nyadhifa zote mwaka 1984. “Maalim Seif ni mgeni Zanzibar hata uraia wake bado una utata, aliwahi kutakiwa ashiriki mdahalo wa asili yake akaukimbia, hatutaki kusema ila tukisema na kutaja historia yake atakimbia, asijilinganishe na Mama Samia ni zao la ASP na atafia CCM hata yeye ni CUF upepo, lakini ni CCM masilahi ndiyo maana tangu alipofukuzwa hajarudisha kadi yetu,” alisema. | kitaifa |
PATRICIA KIMELEMETA na JOHANNES RESPICHIUS MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu, amekaa mahabusu kwa takribani dakika 45, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumtia hatiani kwa kosa la kutumia bangi na kuhukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh milioni mbili. Wema, ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006, jana alikaa kwenye mahabusu ya mahakama hiyo wakati akisubiri taratibu za kulipwa kwa faini aliyotozwa. Baada ya ndugu zake kulipa faini, msaani huyo alitoka mahabusu saa 7 mchana na kuondoka kwenye viwanja vya mahakama hiyo. Awali akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwaachia huru washtakiwa wengine wawili waliokuwa wanashtakiwa pamoja na Wema. Washtakiwa hao, ambao ni wafanyakazi wake, ni Matilda Abass na Angelina Msigwa. Hakimu Simba akisoma hukumu hiyo, iliyochukua takribani dakika 40, alisema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano, huku upande wa washtakiwa katika kesi hiyo walijitetea wenyewe. Alisema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa pande zote mbili, mahakama hiyo imejiridhisha pasi na shaka kuwa mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo, Wema Sepetu, anatumia dawa za kulevya aina ya bangi. Alisema, awali wakati anasikiliza ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka, mashahidi hao walitoa vielelezo vya kuonyesha kuwa, Wema anatumia dawa hizo. Alisema shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, ambaye ni Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu, Elias Mulima, alisema alipokea sampuli za vielelezo viwili, kimoja cha misokoto inayodhaniwa ni ya bangi na kingine ni mkojo uliohifadhiwa kwenye kikontena. Alisema misokoto hiyo inadaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema, baada ya kufanyiwa uchunguzi na askari polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi (Central). Alisema mkemia huyo baada ya kupewa vielelezo hivyo, alivifanyia vipimo kwa wakati tofauti, ambapo kilichodhaniwa kuwa ni bangi alikichanganya na dawa maalumu ambayo ilionyesha kuwa kweli ni bangi na baadaye kufanya kipimo cha pili kupitia mitambo maalumu na majibu yalikuwa hivyo hivyo. Alisema shahidi huyo alipokea sampuli nyingine ya mkojo wa Wema, ambaye alipelekwa ofisini kwake akiwa chini ya ulinzi wa Inspekta Willy na askari mwanamke, aliyefahamika kwa jina moja la Marry. Alisema mara baada ya kumfanyia vipimo, majibu yalionyesha kuwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya bangi ambazo zilikaa kwenye mkojo huo kwa siku 28. Alisema shahidi wa pili, Inspekta Willy, aliieleza mahakama hiyo kuwa, waliongozana na WP Mary kupeleka vielelezo hivyo kwa Mkemia ili viweze kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara. Alisema, shahidi wa tatu, WP Mary, aliieleza mahakama hiyo kuwa, siku ya tukio aliambiwa aongozane na Wema kwenda nyumbani kwake, Ununio, kwa ajili ya kufanya upekuzi. Alisema tukio hilo lilitokea baada ya Wema kutajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kutumia dawa za kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP). Alisema wakiwa njiani, alimuuliza mtuhumiwa (Wema) kama anatuma dawa za kulevya, mtuhumiwa huyo alikiri na kudai kuwa, anatumia kama starehe. Alisema shahidi wa nne katika kesi hiyo, Mjumbe wa nyumba 10, Stephen Ndonde, alidai mahakamani hapo kuwa, siku ya tukio aliitwa kushuhudia upekuzi nyumbani kwa Wema. Alisema, shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa wakati upekuzi unaendelea, walikuta kipisi cha msokoto katika chumba cha kuvaa nguo cha msanii huyo na chumba cha mfanyakazi wake walikuta kipisi kingine. Hakimu Simba alisema shahidi wa tano, Koplo wa Polisi, Robert, aliieleza mahakama kuwa, alipokea maagizo kutoka kwa bosi wake ya kupeleka vielelezo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ikiwamo msokoto mmoja na vipisi viwili vya dawa za kulevya idhaniwayo kuwa bangi. Alisema walitoa ushahidi wao mahakamani hapo, ambako Wema alikana kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na alisema hakuna mtu anayeweza kuingia chumbani kwake. Pia alisema wakati wa upekuzi, polisi walikuta msokoto wa bangi. Hakimu Simba alisema wakati polisi wanafika nyumbani kwa Wema kufanya upekuzi huo, wafanyakazi wake, Matilda na Angelina, walikuwa wameketi barazani. Mara baada ya kusema hayo, mahakama hiyo ilimtia hatiani Wema kwa mashtaka ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na kuwaachia huru wafanyakazi wake, Matilda na Angelina. Upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili Constantine Kikula, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa wa kwanza, Wema, ili iwe fundisho kwa wengine kwa sababu ni msanii na kioo cha jamii, lakini alikuwa anaweza kutumia dawa za kulevya, jambo ambalo linaweza kusababisha kuwashawishi wasanii wengine kufanya hivyo. Wakili wa Utetezi, Albert Msando, aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshtakiwa kwa sababu ni kosa la kwanza, hivyo anaweza kubadilika na kuwashawishi wananchi wasiweze kutumia dawa hizo. Mara baada ya kujitokeza kwa malumbano hayo ya kisheria, Hakimu Simba alimhukumu Wema kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh milioni mbili, kila kosa anatakiwa kutoa faini ya Sh milioni moja. Alitoa onyo kali kwa msanii huyo kujirekebisha na kuacha kabisa kutumia dawa hizo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya. Hata hivyo, msanii hiyo alikidhi masharti ya hukumu hiyo na kuachiwa huru. | burudani |
Aveline Kitomary, Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo amethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya corona ambaye ni mwanamume aliyekuwa akitibiwa katika kituo cha matitabu ya wagonjwa wa corona kilichopo nje ya hospitali ya Mloganzila. Waziri Ummy amesema mgonjwa aliyepoteza maisha ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa akipatiwa matibabu katika kituo hicho. “Nasikitika kutangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid -19 hapa nchini kilichotokea alfajiri ya leo tarehe Machi 31, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Mloganzila Dar es salaam. “Marehemu ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine, tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na tunatoa pole kwa ndugu hasa wa marehemu,” amesema Waziri Ummy. Hadi sasa jumla ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19 nchini ni 19, aliyepona ni mmoja na aliyefariki dunia ni mmoja. | afya |
Taifa Stars ambayo iliweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja jijini Addis Ababa, jana iliendelea na ratiba yake ya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ikifanya mazoezi yake asubuhi tu.Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij alisema anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake ilifanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.Nooij alisema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.Akizungumzia mechi dhidi ya Misri keshokutwa, Nooij alisema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri.“Nafahamu tunaenda kucheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo,” alisema Mholanzi huyo akizungumzia mechi hiyo ya kwanza ya Kundi G ambalo pia lina timu za Nigeria na Chad.Aidha, Nooij alisema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Afcon.Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa, hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.Taifa Stars inatarajia kuondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia saa tano usiku na kufika Cairo saa nane usiku, kisha kuunganisha safari ya kwenda Alexandria ambako mchezo huo utafanyika.Mchezo kati ya Misri dhidi ya Tanzania utachezwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab kuanzia saa moja jioni kwa saa za Misri sawa na saa mbili kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.Waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchini Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa (mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma (mwamuzi msaidizi wa kwanza) na Wolday Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili). | michezo |
Na Christian Bwaya, UMEWAHI kuzungumza kitu cha kawaida lakini ukashangaa mtu anasirika? Unafikiri ni kwa nini mtu akasirike kwa jambo dogo ambalo pengine lilisemwa kwa nia njema? Kuna sababu nyingi. Mojawapo ni namna unavyowasiliana naye. Vile unavyoweka ujumbe wako inaweza kufanya ama usieleweke au ueleweke tofauti na vile ulivyotarajia. Mara nyingi tunafikiri tunajua kuwasiliana kwa sababu tu tunawafahamu wale tunaozungumza nao na tunajua wanataka kusema nini. Hata hivyo, wataalamu wa mawasiliano wanasema tunapowasiliana na watu tunaofikiri tunawafahamu vizuri, hatuwasiliani vizuri kama tunavyowasiliana na watu tusiowafahamu. Unapozungumza na mtu unayemfahamu, ni rahisi kujiaminisha unajua anachotaka kukisema. Hufanyi jitihada za maana kumwelewa na kumsikiliza kwa sababu tayari akili yako inakuaminisha unajua atasema nini. Lakini tunapozungumza na mtu usiyemjua ni rahisi kuwa makini zaidi hasa kama unamheshimu. Kuelewa kinachosemwa Maisha yetu ni mtiririko wa mawasiliano. Mke na mume wanahitaji kujifunza namna ya kuwasiliana vyema. Wazazi wanahitahitaji kujua namna ya kuwasiliana vyema na watoto wao. Mawasiliano yakifanyika vizuri, huboresha uhusiano wa watu kwa sababu mwenye ujumbe anajisikia kueleweka na mpokeaji naye anajisikia kueleweka. Hata hivyo, si kila mawasiliano yanaweza kujenga uhusiano. Uhusiano haujengwi kwa uwezo wa kueleza mtazamo wako kwa namna ambayo yule anayekusikiliza anaweza kukuelewa. Uhusiano hujengwa na uwezo wako wa kumsikiliza mwenzako na kumpa nafasi ya kufafanua anachokitaka. Kwa kuzingatia umuhimu huo, makala haya yanasaili mbinu tatu zinazoweza kukusaidia kuwasiliana vizuri zaidi na mwenzako. Heshimu hisia za mwenzako Hatua ya kwanza ya kuwasiliana na mwenzako ni kujali hisia zake. Binadamu ni kiumbe anayeheshimu hisia zake. Ukigusa hisia zake, iwe kwa kumkwaza au kumfurahisha, atachukulia kwa uzito. Hisia hazisahauliki. Usipoweza kugusa hisia za mtu hutaweza kuwasiliana naye ipasavyo. Ili uweze kugusa hisia za mtu lazima uondoe kiambaza kinachoweza kukutenganisha naye. Kiambaza kimoja wapo ni kujiona una hadhi kuliko yeye. Unapojiona ‘uko juu’ unaharibu. Jifunze kujiona mtu wa kawaida anayejali utu wa mtu zaidi kuliko hadhi na madaraka. Unapoweza kufanya hivyo, unagusa hisia za mwenzako na kwa vyovyote atakusikiliza. Sikiliza zaidi Mara nyingi tunapozungumza tunatamani kusikilizwa. Tunaamini sisi ndio watu wenye taarifa na uelewa sahihi kuliko wanaotusikiliza. Ukishaamini una haki ya kusikilizwa, hata katika mazingira unayoonesha kusikiliza, kimsingi unakuwa ukingoja zamu yako ya kuongea. Unafikiria utasema nini baada ya hapo. Tatizo ni kuwa kadri unavyotamani kusikilizwa ndivyo unavyomfanya anayepaswa kukusikiliza ajione hathaminiki. Kutokuthaminika humfanya ajenge umbali wa kihisia na hivyo kukosa ari ya kukusikiliza. Jenga mazoea ya kusikiliza watu kwa makini. Hapa hatuzungumzii kusikiliza kinachosemwa pekee, bali namna gani kinasemwa, kitu gani hakisemwi wazi na kipi kimejificha. Fuatilia mazungumzo Kumfanya mtu ajisikie anaheshimiwa na kusikilizwa ni sehemu muhimu ya mawasiliano. Unahitaji kujifunza kuonyesha unafuatilia mazungumzo. Kwanza, epuka kumkatisha mtu anapoongea au kumalizia sentensi yake. Mtu anapoona unaingilia maneno yake anahisi tayari unaamini unajua anachotaka kusema. Pia, itikia anachokisema mwenzako kumtia moyo kuwa unajali na kufuatilia mazungumzo yake. Itikia kwa kutikisa kichwa, kumwangalia machoni, maneno kama ‘mmh-mh!’ Muhimu ni kuwa unapozungumza na mtu mpe mrejesho. Rudia anachokisema kwa maneno yako na uliza maswali hapa na pale. Kwa kufanya hivyo, utamfanya aone unajali. Mwandishi ni Mhadhiri wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi. Blogu: http://bwaya.blogspot.com, 0754870815. | kitaifa |
NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema licha ya kutofanya usajili katika kikosi chake hadi sasa katika usajili wa dirisha dogo, mwendo wao utakuwa ni ule ule kama walioanza nao Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Katika msimamo wa ligi hiyo hadi sasa Mtibwa Sugar imecheza mechi tisa ambapo imeshinda mechi saba, sare moja na kupoteza mmoja. Kwa matokeo hayo, Mtibwa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 22 nyuma ya Yanga waliopo nafasi ya pili kwa pointi 23 na Azam wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 25. Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mexime ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, alisema licha ya kutokuwepo na mabadiliko makubwa katika kikosi chake bado kitaendelea kutembeza dozi kwa kila timu watakayokutana nayo. “Tulivyoanza ndivyo tutakavyomaliza kwani lengo letu ni kuona msimu huu Mtibwa inamaliza katika nafasi tatu za juu baada ya kushindwa kuyafikia malengo hayo kwenye kipindi kirefu kilichopita. Mtibwa Sugar leo itakuwa ugenini katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuwakabili wenyeji wao, Mbeya City. | michezo |
CHRISTINA GAULUHANGA Na AVELLINE KITOMARY-DAR ES SALAAM SERIKALI imesema wagonjwa wa homa ya dengue wanazidi kuongezeka na
hadi sasa wamefikia 1,901 huku Kata ya Ilala, Dar es Salaam ikiongoza kwakuwa
na wagonjwa 235. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mganga Mkuu wa
Serikali, Profesa Muhammad Kambi, alisema tangu watoe taarifa katika kipindi
cha siku tisa, wamepata wagonjwa wapya 674. Profesa Kambi alisema ni vyema wananchi wakachukua tahadhari kwa sababu
hawana uhakika kama mafuta ya nazi na majani ya mpapai yanatibu ugonjwa huo
kama ambavyo wengi wanaaminishana kwa sasa. Alisema wamekuwa na wastani wa wagonjwa 75 kwa kila siku ikiwa ni
tofauti na Aprili ambapo kuliwa na wastani wa wagonjwa 32. “Ongezeko hili linasababishwa na uelewa kuhusu ugonjwa huu kwa
wananchi, sasa hivi wengi wenye dalili wanajitokeza kupima katika vituo vya
afya na tunaendelea kufanya tathimini kama kweli mafuta ya nazi na majani ya
mpapai yanatibu,” alisema Profesa Kambi. Alisema tangu kuanza kwa ugonjwa huo Januari, jumla ya watu 1,901
wamethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo ama kati yao 1,809 wanatoka Dar
es Salaam. Profesa Kambi alisema 89 walitoka Tanga huku Singida, Kilimanjaro na Pwani walitoka mmoja mmoja. “Hakuna vifo vilivyotokea hadi sasa tangu tamko lilipotolewa Mei
10 mjini Dodoma,” alisema. DALILI ZA UGONJWA Profesa Kambi alizitaja dalili za dengue kuwa ni kupata vipele vidogovidogo,
kuvilia damu kwenye ngozi na kutoka damu sehemu za fizi, ndomoni, puani, macho
na kwenye njia ya haja kubwa. Alisema hadi sasa Serikali inapima ugonjwa huo bure katika vituo
mbalimbali vya afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Amana, Temeke,
Mwananyamala, Sinza, Vijibweni, Mnazi Mmoja, Lugalo, Mbagala, FFU Ukonga na vituo vya Bombo na Horohoro mkoani Tanga. “Serikali imeagiza vipimo vingine vya kupima wagonjwa 30,000 ambavyo vitasambazwa Dar es Salaam na maeneo
mengine,” alisema Profesa Kambi. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas Ndungile, alisema hadi sasa vituo
vya kupima ugonjwa huo kwa Dar es Salaam na Tanga vimeongezeka kutoka saba vya
awali hadi kufikia 19. Alisema alili za dengue huanza kujitokeza kati ya siku tatu hadi 14
tangu mtu alipoambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Dk. Ndungile alisema hadi sasa kuna kata 20 katika Mkoa wa Dar es
Salaam ambazo zimeripotiwa kuwa na wagonjwa zaidi ya 25. Alisema kata hizo zinaongozwa na Ilala ambayo ina wagonjwa 235, Upanga 87, Kisutu 86, Mbezi 78, Tegeta 27 na
nyinginezo. Aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na
kuua mazalia ya mbu. | kitaifa |
RUFAA ya kupinga kufutiwa dhamana iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, itaanza kunguruma katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.Mbowe na Matiko walikata rufaa hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwafutia dhamana Novemba 23, mwaka jana. Hatua ya rufaa hiyo kuendelea na usikilizwaji ni baada ya Mahakama ya Rufaa, kutupilia mbali rufani ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), aliyepinga mahakama hiyo kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu ina upungufu kisheria, ikiwemo kukosekana kwa haki ya kusikilizwa na rufaa kutoambatanishwa na mwenendo wa kesi hiyo.Rufaa hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika, ambaye kabla ya DPP kukata rufaa hivyo, kutoipa mamlaka mahakama hiyo kuendelea na usikilizwaji, alisikiliza mapingamizi ya pande zote mbili. Mbowe na Matiko wanawakilishwa na Wakili Peter Kibatala walikata rufaa kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kwa kuwasilisha hoja nne.Wakata rufaa hao wanadai mahakama haijawapa nafasi wadhamini ya kujieleza kwa mujibu wa sheria. Pia walidai mahakama imekosea kuwafutia dhamana kwa sababu Novemba 12, 2018 Mbowe na Matiko, walifika mahakamani bila kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi. Wanadai masharti ya dhamana waliyopewa washitakiwa ni kinyume cha sheria. Novemba 27, mwaka jana, Jaji Rumanyika aliona kuwa rufaa hiyo imepelekwa mahakamani hapo chini ya hati ya dharura, hivyo aliagiza mwenendo wa shauri upelekwe mahakamani hapo pamoja na wahusika wapande zote wafike ikiwemo upande wa mashitaka.Hata hivyo, Novemba 28, mwaka huo, upande wa mashitaka na wa utetezi walifika mahakamani hapo na mapingamizi ya pande zote yalisikilizwa. Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo kwa sababu tatu, ikiwemo warufani kushindwa kukata rufaa kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa, kwani taarifa ya kusudio la kukata rufaa imekosekana.Baada ya Jaji Rumanyika kusikiliza mapingamizi hayo, alikubaliana na hoja za upande wa serikali za kupewa mwenendo wa shauri hilo wa kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Kisutu uliochapishwa, ambao unasomeka vizuri na sio kama ule waliopewa awali.Pia alikubaliana na hoja ya pingamizi ya upande wa serikali kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana, zinakiuka matakwa ya sheria, kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa ya kupinga masharti hayo ya dhamana, yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka jana.Hata hivyo, baada ya mahakama kupanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo, upande wa mashitaka ulidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, kupinga maamuzi yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka. | kitaifa |
Na Mwandishi Wetu USAFIRI wa Uber ni wa gharama nafuu na salama zaidi ukilinganisha na usafiri mwingine hapa nchini. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi wanne. Gharama zake huanzia Sh 3,000 na kuendelea kulingana na mahali unakokwenda, watu wengi wanaufurahia kwa kuwa hata inapotokea wamesahau kitu ndani ya gari hukipata kikiwa salama. Ili biashara iweze kukua zaidi, ushirikiano ni jambo muhimu. Kwa sababu hii, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo na Uber wameamua kuingia makubaliano ya kibiashara ili kuwaondolea usumbufu wateja wao. Ushirikiano huu wa kimkakati ulisainiwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, ukilenga kuwasaidia watumiaji wa Uber kufanya malipo ya safari zao kupitia Tigopesa, moja kati ya mifumo maarufu ya malipo ya kidigitali nchini. Gharama za kuita taxi pia hazitakuwapo kwa watumiaji wa Tigo, hili ni jambo la kupongeza zaidi. Ushirikiano huu unahakikisha miamala ya malipo isiyo na usumbufu kwa watumiaji wa Uber ambao hawana kadi za malipo za bank (Credit au Debit card), ambao pia wanahitaji urahisi wa miamala isiyo ya fedha taslimu. Wateja zaidi ya milioni sita wanaotumia huduma ya Tigopesa tayari wanalipa bili za huduma mbalimbali na nyinginezo kwa kutumia Tigopesa. Watakuwa pia na fursa ya kupata Uber kwa haraka na kwa usalama zaidi, usafiri wa uhakika pamoja na huduma nyinginezo.
Ushirikiano huu wa kwanza wa aiana yake kwa Uber Afrika Mashariki, ni hatua kubwa ya safari ya Tanzania kuelekea mapinduzi ya kidigitali na ni maono ya Tigo ya kuwa na maisha ya kidigitali yenye werevu na yanayounganisha huduma mbalimbali ambayo wakati wote imekuwa ndio kauli mbiu ya Tigo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari anasema ushirikiano kati ya Uber na Tigo utaleta huduma mpya kwa wateja wao pamoja na Uber jijini Da es Salaam. “Tunapongeza athari nzuri za mabadiliko katika teknolojia ya simu nchini. Ushirikiano wetu na Uber utahamasisha kutumia mitindo mipya ya kipekee ya maisha ya kidigitali katika soko hili linalokua kwa kasi, ikiwa inapanua utumiaji wa Uber na Tigo kwa mamililoni ya Watanzania,” anasema Karikari.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanawakaribia kwa kasi wenzao wa Jiji la Nairobi, nchini Kenya katika kuingia katika biashara ya Taxi inayoshamiri. Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, Uber imekua na kufikisha magari 3000 jijini Da es Salaam kukiwa na uwezekano wa kupanuka kuelekea katika maeneo mengine ya Tanzania. Meneja wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado anasema ushirikiano huu unadhihirisha nia ya dhati ya kampuni kuwahudumia wasafiri, madereva kwa upana zaidi kupitia mbinu halisi za hapa nchini. “Ushirikiano huu unawakilisha msingi muhimu kwa ajili ya sisi kufanya mapinduzi ya usafiri wa taxi hapo baadae,” anasema Amado. Naye Meneja wa Uber nchini, Alfred Msemo anasema madereva na watumiaji wa Uber watavuna matunda ya biashara yatokanayo na ushirikiano huu. “Tunashauku kuhusu ushirikiano wetu na Tigo nchini Tanzania, ambao utasaidia watumiaji wote wa Uber na madereva wenye line za Tigo kutumia App ya Uber katika simu zao bure bila malipo yoyote. “Uber ni App ya Smartphone ambayo husaidia kuwatoa watu kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa kubofya kitufe. “Wito na maono ya Uber ni kutoa huduma ya usafiri ambayo ni salama, ya uhakika na yenye gharama nafuu kwa kila mtu, kila mahali. Ushirikiano huu utahamasisha maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam ambao ni wateja wa Tigo kutumia App ya Uber kuzunguka sehemu mbalimbali hapa jijini,” anasema Msemo. Kampuni hizi mbili zitakuwa zikifanya kazi kwa pamoja katika bidhaa na promosheni ambazo zinalenga kuongeza thamani kwa wateja wapya na waliopo. Tigo na Uber nchini Tanzania watatangaza ofa za kusisimua hivi karibuni kuwasaidia wateja kuwasiliana na Uber jijini Dar es Salaam ambako huduma za usafiri huo zinapatikana kwa sasa. | afya |
Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kilitegemea mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Aliko Dangote, atakuwa mtu wa mwisho kulalamikia sera za uwekezaji kutokana na upendeleo aliopewa hapa nchini. Mbali na hilo, TIC imesema taarifa zilizotolewa na Mwandishi wa Financial Time (FT), John Aglionby, kuhusu Tanzania kuwa na mazingira hatarishi kwa wawekezaji si sahii na inalenga kupotosha ukweli juu ya hali halisi. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe alisema maelezo hayo ambayo ilielezwa kuwa ni ya tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote, yamelenga kupotosha sera za uwekezaji na kuwaogopesha wawekezaji ambao wameendelea kuiamini Tanzania na kuwekeza mitaji mikubwa. “Tunatarajia Dangote awe mtu wa mwisho kulaumu, kwani Serikali imejitahidi kumwekea mazingira bora ya uwekezaji hasa pale Rais alivyoshugulikia suala lake la kupata gesi kwenye kiwanda chake, pia kuruhusiwa kuchimba mwenyewe makaa ya mawe kama hatua ya kuondoa mzunguko mkubwa uliokuwapo. “Isitoshe Dangote mwenyewe wakati akihojiwa kwenye kituo kimoja nchini Uingereza alisema yeye hakumtuhumu Rais Dk. John Magufuli, bali alizungumzia hali ya uwekezaji katika nchi za Afrika ziweze kuboresha mazingira na sera za uwekezaji kila wakati hivyo maelezo yaliyotolewa na mwandishi huyo si ya Dangote,” alisema. Mwambe alisema TIC haiamini kama Dangote anaweza kuwa msemaji wa sekta ya madini hasa ukilinganisha uwekezaji wake ni kwenye sekta ya viwanda hususani saruji na serikali imekuwa mstari wa mbele kusikiliza na kufanyia kazi maoni ya mfanyabiashara huyo. Alisema kwa sasa hivi Tanzania ipo katika vita ya kiuchumi hivyo mabadiliko ambayo yanaendelea kufanywa na Serikali wapo baadhi ya watu huko duniani hawayataki hususan kwenye sekta ya madini. Aidha alisema makala hiyo inajionyesha wazi kuwa mwandishi hafahamu vizuri sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 ambayo inatambua umiliki binafsi wa mali na kuzuia uwezekano wa kutaifisha mali hizo bila sababu za msingi wa kisheria. Alisema katika kuboresha mazingira ya uwekezaji wanaendelea kufanya marekebisho ya sera pamoja na sheria ili ziweze kuwa na manufaa kwa wote na kwamba Kiuto kimeendelea kupokea wawekezaji kutoka nchini mbalimbali na Tanzania imekaribishwa baadhi ya nchi kwenda kukutana na wawekezaji. “Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji ndio maana kituo cha uwekezaji kimeendelea kuwa kikitingwa (buzy) kupokea wawekezaji mbalimbali hivyo nashang’aa hizi taarifa zinatoka wapi. “Kwenye ripoti ya (IMC) inaonyesha Tanzania katika vipimo vya kimataifa kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji imepanda nafasi saba hadi kufikia 144,” alisema Mwambe. Alisema changamoto ambazo zipo kama vile miundombinu na umeme, serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaboresha ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni BRELA, mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge, ujenzi na ukarabati wa barabara. | kitaifa |
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Emmanuel Amunike amekiri kikosi chake kucheza vibaya kwenye mechi yake dhidi ya Cape Verde iliyochezwa Praia juzi na kufungwa mabao 3-0.Stars ikihitaji ushindi kujiweka vizuri katika michuano hiyo ya kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika ‘Afcon’ 2019 iliwaacha watanzania mdomo wazi baada ya kufungwa idadi hiyo ya mabao na kupoteza matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.Baada ya suluhu na Uganda katika mechi iliyopita, na kwa namna kikosi kilivyocheza Kampala siku hiyo , matumaini ya wengi ilikuwa kupata matokeo mazuri juzi, jambo ambalo lilikuwa tofauti.Akizungumza baada ya mechi hiyo, Amunike alikiri kikosi chake kucheza vibaya tangu kipindi cha kwanza na kuruhusu mabao mawili ya haraka haraka.Stars ilifungwa mabao mawili ndani ya dakika 23 na kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 na kisha wenyeji wao kufunga bao la tatu katika kipindi cha pili.“Tulicheza vibaya tangu kipindi cha kwanza na kuruhusu mabao mawili ya haraka haraka, lakini nafasi bado tunayo tutarekebisha makosa katika mechi ya marudiano,” amesema Amunike.Stars ilitarajiwa kurejea nchini jana na keshokutwa itakuwa na mechi ya marudiano dhidi ya Cape Verde kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Stars sasa imecheza mechi tatu katika kundi L linaloongozwa na Uganda ambapo imetoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.Stars inawania kufuzu fainali za Afcon kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ilipofanyika Lagos, Nigeria ambapo Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza na ya mwisho. | michezo |
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ameagiza kusimamishwa kazi maofisa wawili wa juu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), ili kupisha uchunguzi baada ya nchi kukumbwa na katikakatika umeme ndani ya miezi miwili.Dk Kalemani alitoa maelekezo hayo juzi jioni jijini hapa baada ya kukutana na viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Tanesco. Alitoa siku saba kuanzia Jumamosi kwa bodi hiyo kuunda tume itakayochunguza suala hilo.“Bodi lazima ichukue hatua kuhakikisha kinachosemwa gridi kutoka, gridi haitoki na kusababisha nchi nzima au sehemu ya nchi kukosa umeme. Lazima mchukue hatua za makusudi kuhakikisha hilo halijitokezi tena.“Maelekezo yangu kwa menejimenti kupitia Mwenyekiti wa Bodi, unda timu mahususi kuanzia leo (juzi) ya kuchunguza na kufuatilia jambo hili kwa kuhusisha tasnia na taasisi mbalimbali sio Tanesco peke yake. Ndani ya siku saba nipate matokeo ya nini chanzo cha tatizo hilo ili lisijirudie kabisa,” aliagiza Waziri.“Jambo linapotokea ina maana kuna uzembe katika usimamizi, au kutofuatilia maelekezo ya serikali, au kunaweza kuwa na hujuma kwa baadhi ya watumishi wasiokuwa wazalendo.“Kwa hiyo kuanzia leo (juzi), Bodi ichukue hatua mahususi za kiutawala dhidi ya Naibu Mkurugenzi wa generation na Naibu Mkurugenzi wa transmission, ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao,” alisema.“Haya yanatokana na uzembe au kutochukua hatua au kutowawajibisha watu wa chini yao, jambo hili limejitokeza mara nyingi. Haiwezekani nchi ibaki kwenye giza nusu saa, maana yake usalama wa nchi haupo, haiwezekani viwanda visimame ndani ya nusu saa maana yake uzalishaji unasimama na kodi ya serikali inapotea, hawa watu waanze kuchunguzwa mara moja na wote wanaohusika,” alisisitiza Waziri Kalemani.Dk Kalemani alisema ametaarifiwa kuwa nchi ilikabiliwa na tatizo la kukatikatika umeme kati ya Novemba 28 na 30 na Desemba 4 na 14 kutokana na kutokea hitilafu gridi ya taifa na kusisitiza hiyo ni hatari kwa usalama wa nchi. Alisema maofisa hao wa juu wa Tanesco wanapaswa kueleza ni kwa nini nchi imepatwa na tatizo la kukatikakatika umeme mara nne ndani ya miezi mwili wakati nchi inazalisha ziada ya umeme megawati 252 gridi ya Taifa.Waziri aliagiza bodi hiyo kuhakikisha maeneo ya mijini ambayo hayajaunganishiwa huduma ya umeme na yanasubiri kuunganishwa yapelekewe ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.“Yako maeneo ya mijini ambayo hayahitaji kuunganishwa umeme na yamekaa bila kuunganishiwa muda mrefu huku yako ndani ya mipango ya shirika na fedha imeshatoka kila mkoa. Tunataka kuona ndani ya miezi mitatu wamefikishiwa huduma hiyo.Na hii ni kazi yako mwenyekiti wa bodi, toa maelekezo kwenye menejimenti yako,” aliagiza Waziri. Pia aliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kuhakikisha ifikapo Desemba 30, mwaka huu, iwe imewaunganishia umeme wateja wote nchi nzima ambao wameshalipia gharama za kuunganisha umeme na hawajapewa huduma.“Kuna wateja ambao wameshalipia gharama za kuunganishiwa umeme, miezi miwili, mmoja, mitatu na hawajaunganishwa. Naagiza wateja wa aina hii nchi nzima wawe wameunganishiwa umeme hadi Desemba 30 mwaka huu,” alisema. | kitaifa |
KESHO mchana, Tanzania itaandika historia nyingine katika sekta ya usafi ri wa anga nchini baada ya ndege yake mpya ya tano kuwasili nchini.Ndege hiyo mpya aina ya Airbus 220-300 imekabidhiwa juzi mjini Montreal nchini Canada kwa timu ya wataalamu na watendaji kutoka Tanzania na leo alfajiri wameondoka kurejea nchini ambako watafika kesho mchana. Akizungumza na gazeti hili kwa simu akiwa nchini Canada, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi ambaye ni miongoni mwa timu iliyokwenda kukabidhiwa ndege hiyo, alisema baada ya ndege kufanyiwa majaribio yote wataalamu waliikagua na kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa.“Tunashukuru ndege yetu ni nzuri na mpya, imekaguliwa na kufanyiwa majaribio iko vizuri na kesho (leo) alfajiri tunaondoka kurudi nyumbani tutafika keshokutwa (kesho) mchana,” alisema Matindi. Alisema ndege hiyo ni moja kati ya ndege mpya mbili aina zilizonunuliwa na serikali kutoka Kampuni ya Airbus nchini Canada ikiwa ni juhudi za kufufua sekta ya usafiri wa anga na kuinua uchumi sambamba na kuongeza idadi ya watalii wanaokuwa mojakwa moja nchini.Matindi alisema ndege ya pili iko kwenye hatua za mwisho za uundwaji wake na itakapokamilika, itaanza majaribio ya kuruka na kisha timu ya ukaguzi itakwenda nchini humo kufanya ukaguzi kabla ya kukabidhiwa. “Ndege mpya mbili tulizokuwa tunatarajia kuzipokea hivi karibuni, moja tumeshakabidhiwa na hiyo nyingine iko kwenye hatua za mwisho za uundwaji na iko timu ya ukaguzi itaenda na itatoa ripoti yao,” alisema Matindi.Akizungumzia ndege hizo ambazo awali zilipaswa kuwa tayari na kuwasili nchini Novemba mwaka huu, Matindi alisema walipokea maombi kutoka kwa watengenezaji wa ndege hizo, Kampuni ya Airbus Canada ya kusogeza mbele tarehe ya kuzikabidhi ili kumalizia mambo madogo ya matengenezo yaliyosalia. “Ni kweli awali tulikuwa tuzipokee ndege hizo Novemba mwaka huu, lakini watengenezaji walituomba kusogeza mbele muda wa kukabidhiwa na ni kitu cha kawaida, na tumeshaipokea moja na kesho watanzania wataiona tukifika, ”alisema Matindi.Ndege hizo mbili kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 132, daraja la kwanza 12 na daraja la kawaida abiria 120. Awali, ndege hizo zilijulikana kwa jina la Bombardier C Series, na Julai mwaka huu, Kampuni ya Airbus iliingia mkataba wa ununuzi na kuzibadilisha jina na kuziita A220-300. Kwa ununuzi wa ndege hizo aina ya A 220-300 Tanzania inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika, kununua ndege hizo zenye kasi, za kisasa, zenye nafasi sambamba na kutumia mafuta kidogo.Aidha, ununuzi wa ndege hizo mbili unaifanya nchi hadi sasa kuwa na jumla ya ndege mpya sita ambazo ni Bombardier Q 400 tatu, Boeing 787-8 Dreamliner moja, A220-300 mbili ambapo moja ndiyo hiyo inayowasili kesho. Jumanne wiki hii, akizungumza na waandishi wa habari nchini, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema ndege hizo mbili mpya moja itatua nchini Desemba 23 na nyingine itatua Januari mwakani.Kamwelwe alisema rubani na wahudumu wa ndege walishakwenda nchini humo kuipokea na kama ratiba haitabadilika ndege hiyo itawasili kesho na kusema itaongeza safari za ndege na kuifanya nchi kukua kiuchumi. Akizungumzia ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo nayo imenunuliwa na kuwasili nchini mwaka huu, Matindi alisema hivi sasa inaendelea na safari za ndani ambayo ni ruti ya Mwanza kila siku jioni na wakati wowote kuanzia sasa watafanya uzinduzi wa safari za nje ambako watazindua ruti ya kwanza kwenda Mumbai nchini India.“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) ambayo kwetu kwa sasa tumeshafikia mwisho,” alisema bosi huyo wa ATCL. Hata hivyo, ATCL kupitia kwenye mtandao wao yapata mwezi ya nne sasa, imekuwa ikitangaza bei za safari za ruti hiyo ya kwenda India katika Jjiji la Mumbai, ambapo wamesema bei ya kuanzia itakuwa dola 286 kwa daraja la kawaida na daraja la kwanza ni kuanzia dola 455.ATC wakati huo mwaka 1977, ilikuwa na ndege tisa, lakini kutokana na usimamizi mbaya ilishindwa kuendelea kutoa huduma za usafiri ipasavyo na mwaka 1994 iliunganishwa nguvu na Kampuni ya Ndege ya Uganda na ile ya Afrika Kusini, zikafanya kazi kwa miaka sita hadi mwaka 2000 ilipotangaza kupata hasara ya Sh bilioni 50. | kitaifa |
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), linatarajia kumuaga kocha wa timu ya Taifa ya soka ya wanawake ‘Twiga Stars’, Nasra Abdallah, huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na Muethiopia, Asrat Abate ambaye anatarajia kutua nchini kesho au Jumamosi. Abate atarithi mikoba ya Nasra aliyefeli kuing’arisha Twiga, ambayo mapema mwaka huu ilitolewa na Zimbabwe katika mechi za kusaka tiketi ya kushiriki katika fainali ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake, zinazotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Cameroon. MTANZANIA ilipata habari kutoka nchini Ethiopia, zikidai kuwa tayari TFF ilifanya mawasiliano na Abate kumueleza nia ya kumtaka aje kuifundisha timu hiyo iwe na mafanikio. “Shirikisho la Tanzania ‘TFF’ linawania kumchukua kocha wetu anaitwa Asrat Abate, alikuwa anafundisha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 na 20, ni mzuri atawasaidia tayari taarifa zimeenea kwetu,” kilisema chanzo hicho nchini Ethiopia. MTANZANIA baada ya taarifa hizo lilifanya mawasiliano na ofisa mmoja wa ngazi za juu ndani ya shirikisho, ambaye alikiri kuwepo kwa habari hizo ila kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kuwa sio msemaji. “Ni kweli aisee, ila umenishtua mmepataje taarifa hizi, kocha anatarajia kuingia nchini Ijumaa au Jumamosi,” alisema kwa kifupi mtoa taarifa huyo. Nasra alirithi mikoba ya Rogasian Kaijage, ambaye aliamua kubwaga manyanga, awali timu hiyo ilikua inafundishwa na Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa anafundisha Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’. | michezo |
HATIMAYE ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere ya Watanzania kupata umeme kutoka Maporomoko ya Rufi ji inatimia, kwa leo Rais John Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bwawa.Rais Magufuli ambaye aliwasili Kisaki mkoani Morogoro jana, tayari kwa kazi hiyo anayoifanya leo, pia ametoboa siri ya kutumia usafiri wa treni kuja kuzindua mradi huo. Aidha, ametoa onyo la mwisho kwa viongozi wa Mkoa wa Morogoro kukomesha uhalifu unaofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima.Rais Magufuli alisafiri kwa treni ya Tazara jana asubuhi kutoka Dar es Salaam hadi Kisaki mkoani Morogoro, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufua umeme wa maji katika mto Rufiji. Uwekaji huo wa jiwe la msingi la mradi huo utakaofua megawati 2,115 utafanyika leo katika Pori la Akiba la Selous wilayani Rufiji mkoani Pwani. “Nimeamua kuja kwa treni makusudi.Nimetaka kutua hapa Kisaki kwa sababu ni mji unaokua kwa kasi sana,” alisema Rais Magufuli alipozungumza na mamia ya wananchi wa Kisaki alipofika jana mchana akiambatana na mkewe Mama Janeth.Aliwaambia wananchi hao kwamba kwa kujengwa mradi huo mkubwa wa umeme, Kisaki ichangamkie fursa za kujenga hoteli na nyumba za kulala wageni watakaokwenda Rufiji kuona utalii utakaotokana na mradi huo. “Chapeni kazi mfaidike na mradi huu. Mkienda kufanya kazi kule msiibe vifaa. Huu ni mwanzo tu wa mafanikio makubwa. Hapa mji wenu utabadilika sana,” alisema Rais Magufuli.Aliwageukia viongozi wa Mkoa wa Morogoro na kuwataka kukomesha matatizo ya wafugaji ambao wanavamia mashamba ya wakulima. “Natoa onyo la mwisho mkomeshe matatizo ya wafugaji.Nilikuja hapa na Rais wa Awamu ya Nne miaka minne sasa imepita. Tatizo halijaisha. Nataka mkomeshe hili tatizo. Likiendelea nitajua hamtoshi kuendelea kuwa viongozi,” Rais Magufuli alimwambia Mkuu wa Mkoa, Dk Stephen Kebwe na watendaji wake.Alisema wapo viongozi wanaohongwa wakiwamo polisi, hivyo akawataka wakikamata mifugo ipigwe mnada pamoja na kuwa na mahakama zinazotembea ili kuendesha mashitaka kwa wahalifu.Katika kuchangia maendeleo, Rais Magufuli alitoa Sh milioni 400 za kujenga kituo cha afya Kisaki. Pia aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi ambazo zimepatikana Sh milioni 39.Ameagiza ujenzi huo uanze kesho na kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, utadumu kwa miezi mitatu. Katika uwekaji jiwe la msingi la mradi wa kufua umeme wa maji wa Rufiji, maandalizi yake yamekamilika.Viongozi mbalimbali wa serikali, mabalozi na wananchi takribani 2,000 watahudhuria sherehe za leo wilayani Rufiji. Mradi huo unaojengwa na mkandarasi Kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy zote za Misri, una gharama ya Sh trilioni 6.5 za Watanzania wenyewe. Utakamilika Juni 2022. | kitaifa |
Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa shtaka la utekaji. Waliofikishwa mahakamani ni Happyness Gimonge
(22), mkazi wa Kivule na James Shayo (23), msanii na mkazi wa
Kitunda. Wakili wa Serikali Abudi Yusuph, alidai mbele ya
Hakimu Frank Moshi kuwa Mei 6, eneo la Kimara Bonyokwa, Wilaya ya Ubungo,
washtakiwa walimteka Angle Mwita na kumwambia mama yake Christina Massa atume
Sh milioni 52 ili kumpata mtoto wake. Hata hivyo, washtakiwa kwa pamoja walikana
kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa kesi bado
haujakamilika. Hakimu Moshi alisema shtaka hilo linadhaminika
endapo washtakiwa watakuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria,
watakaotoa bondi ya Sh milioni 5 kwa kila mmoja. Washtakiwa walishindwa kukidhi masharti ya
dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yao itakaposomwa tena Juni 10, mwaka
huu. Wakati huo huo, mahakama hiyo imempandisha
kizimbani Alex Elieza (27), mkazi wa Temeke kwa shtaka la wizi. Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu Mkazi
Karoline Kiliwa, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Neema Moshi, alidai Novemba 23,
2018 eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa kama mwajiriwa wa Kampuni
ya Bevco Distribution Ltd, aliiba Sh milioni 30 na gari lenye namba za usajili
MC 377 BFZ aina ya Mahindra mali ya mwajiri wake. Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande
wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe
ya kutajwa tena. Hakimu Kiliwa alisema dhamana iko wazi kwa
mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka hati ya mali isiyohamishika
yenye thamani ya kiasi cha Sh milioni 30. Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti
ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa Juni 10, mwaka
huu. | kitaifa |
ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM KATIBU Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amesema kutokana na
mwenendo wa siasa ulivyo nchini, huenda wanasiasa wakasababisha idadi ya wapigakura
ikashuka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaokuja. Akizungumza na wanahabari katika kipindi cha ‘Tujadiliane’
kinachoendeshwa na UTPC jana jjini Dodoma, Dk. Bashiru alisema iwapo siasa
hazitapewa taswira nzuri, upo uwezekano wa idadi ya wapigakura kushuka tofauti
na ilivyozoeleka. Alisema Tanzania imekuwa katika rekodi nzuri ya watu
wanaojitokeza kupiga kura ambao wamekuwa wakifikia zaidi ya asilimia 70 ya
waliojiandikisha, lakini uchaguzi wa hivi karibuni unaonesha kuna mabadiliko
kwa idadi hiyo. “Ukiangalia rekodi, kadiri tunavyochafua siasa zikawa za
uongo uongo na mbwembwe, matokeo yake idadi ya wapigakura inashuka. Hatujawahi
kukosa chini ya asilimia 70 ya waliojiandikisha ambao wanajitokeza kupiga kura,
tuna rekodi nzuri ya kitaifa, lakini ukiangalia mwelekeo idadi inashuka, hali ambayo
siyo nzuri,” alisema. Dk. Bashiru alikuwa akizungumzia namna CCM inavyojipanga
kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba
mwaka huu na namna anavyoona mwelekeo wa kisiasa katika utaratibu wa usimamizi
wa kura za maoni na upigaji kura. Alisema ni vyema wanasiasa wajenge utamaduni wa kuhamasisha
umma na kuonyesha kuwa kura ni sehemu ya kuleta mabadiliko, hivyo kujua umuhimu
wao kushiriki katika upiaji kura. Suala jingine alisema ni kwa wanasiasa kuacha ulaghai
wakati wa kampeni na waahidi mambo ambayo wana uhakika watayatekeleza kwa kuwa
ahadi hewa pia ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wapigakura. Dk. Bashiru alisema ni vyema pia wanasiasa watambue kuwa
hali ya siasa ya sasa si rahisi kama ilivyokuwa miaka iliyopita kwa kuwa idadi
ya vijana ni kubwa na uelewa wa watu umeongezeka, hivyo suala ambalo hataki
kuona likitokea ni la wananchi kukata tamaa ya uchaguzi kwa sababu ya matendo
ya wanasiasa. Alisema uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa una thamani
kubwa kuliko nyingine kwa sababu viongozi watakaochaguliwa ndio walio karibu
kabisa na wananchi na ndio wanaotatua matatizo yao ya kila siku. | kitaifa |
Rais John Magufuli na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamezindua jengo la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kutoa mwito kwa Waafrika kuziheshimu na kuzitekeleza kivitendo fikra za Mwalimu Nyerere katika kuendeleza bara la Afrika na Waafrika.Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisema kuwa fikra za Mwalimu Nyerere zin- azidi kuishi katika maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla, kutokana na uwezo wake wa kuona mbali. Alisema fikra hizo haijainufaisha Tanzania peke yake, isipokuwa pia zimelinufaisha bara zima la Afrika. Alitoa mifano ya nchi za Uganda, Malawi, Zambia, Namibia, Afrika Kusini, Msumbiji na nyingine nyingi zilizonufaikana na kazi, weledi na fikra za maendeleo za Mwalimu Nyerere. Rais Magufuli aliuelezea umati huo kuwa katika kudhihirisha Mwalimu Nyerere ameshiriki maendeleo ya Uganda, jana akiwa Ikulu Magogoni Dar es Salaam, Museveni alimuonesha Rais Magufuli chumba alichowahi kulala katika Ikulu hiyo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Alisema, “Najua hata huyu Rais Museveni watoto wake watatu wamezaliwa hapa nchini ambapo mmoja kazaliwa Muhimbili, mwing- ine Ocean Road na mwingine Oysterbay, sasa muone kuwa huyu ni kama mtanzania tu wa hapahapa ;na wapo wengine wengi ambao nao wamenufaika na hekima za Mwalimu Nyerere”. Aliwataka Watanzania kuwa wazalendo katika kuzungumzia mema ya Mwalimu Nyerere na kuwapongeza Watanzania na watu wa mataifa ya nje, wanaounga mkono harakati za kimaendeleo za Mwalimu. Katika mazungumzo yake, Rais Museveni alishukuru mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuikomboa Uganda dhidi ya utawala wa Iddi Amini. Alitaka Mwalimu Nyerere aheshimiwe, kwa kuyaenzi mazuri ambayo amekuwa akiyafanya kwa jamii za kiafrika. Alisema, Tanzania ilikuwa ni kitovu cha mapambano dhidi ya udhalimu na ilifanikiwa kukwepa mipango kadhaa ya hujuma kumuua Mwalimu Nyerere ikilinganishwa na waasisi wengine wa miaka hiyo. | kitaifa |
KOCHA Msaidizi wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Simba, Masoud Djuma amesema anatamani kukutana na Gor Mahia kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Juni 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Simba ilipoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya Gor Mahia, katika mchezo wa fainali wa michuano ya SportPesa Super Cup, iliyoshirikisha timu nane iliyofanyika hivi karibuni mjini Nakuru, Kenya. Akizungumza na gazeti hili jana, Djuma alisema kitu cha msingi anachokifanya kwa sasa ni kurekebisha mapungufu aliyoyaona kupitia kwenye michuano hiyo ili wacheze fainali za Kagame kama walivyokusudia.“Lengo langu kubwa ni kucheza fainali na Gor Mahia ili kulipa kisasi kwa sababu walitufunga kwenye fainali ya SportPesa kule kwao Kenya, tulikuwa na mapungufu lakini tupo kwenye maandalizi kabambe ya kuhakikisha tunabakiza taji Tanzania,” alisema Djuma. Kocha huyo alisema amewaita wachezaji wake wote kuingia kambini ili kuanza maandalizi ya michuano hiyo ambayo pia alisema ataitumia kama kipimo cha kuwajaribu wachezaji wake waliosajiliwa kwa msimu ujao.Alisema anatambua kuwa msimu ujao wa ligi watakuwa na changamoto kubwa ya kutetea taji lao kutokana na mafanikio waliyopata msimu uliopita hivyo wanalazimika kujenga kikosi imara kitakachopambana kupata matokeo bila kuhofia timu yoyote ndani na nje ya nchi. Simba ndiyo bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ya Kombe la Kagame, ikilitwaa mara sita na kuzipiku timu nyingine kubwa zikiwemo watani zao wa jadi Yanga ambao wamelibeba mara tano. Yanga haitashiriki michuano ya mwaka huu baada ya kujitoa kwa madai ya kujiandaa na michuano ya kimataifa. | michezo |
Na Waandishi Wetu-Dar/Zanzibar
WAKATI Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, ikiendelea na vikao vyake Dar es Salaam, wafuasi zaidi ya 100 wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad wamekuwa wakikesha kulinda ofisi za Makao Makuu Zanzibar.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Profesa Lipumba kutangaza uteuzi wa wakurugenzi wa upande wa Zanzibar na kuahidi kwenda kuwakabidhi ofisi wiki hii Visiwani humo.
Kutokana na hali hiyo, MTANZANIA imeshuhudia kundi la wanachama hao wa CUF Zanzibar wanaomuunga mkono Maalim Seif wakilinda ofisi za chama hicho zilizopo Mtendeni na Vuga kwa lengo la kuwazuia wakurugenzi hao.
Hatua hiyo imekuja baada ya Maalim Seif kuwataka wafuasi wake juzi mjini Unguja kwamba wawe tayari kulinda ofisi za chama hicho na kupinga uteuzi wa wakurugenzi hao, huku wakiwaita ni feki.
Alisema hila zinazofanywa na Profesa Lipumba ni za makusudi, huku akisema jambo la muhimu ni kuhakikisha wanachama na viongozi wote wasiokubaliana naye wanaungana ili kuhakikisha kuwa hakuna uovu ama ukiukwaji wa sheria utakaofanywa ndani ya chama hicho.
“Ni lazima tulinde chama pamoja na viongozi wake na si vinginevyo, CCM wamekuwa wakifanya kila aina ya majaribu dhidi ya CUF kwa lengo la kumpotezea muda Maalim Seif, ila sisi kama wanachama katu hatukubali.
“Tutasimama imara kulinda kila aina ya mali na hata viongozi, lakini si kuwaruhusu hao wanaoitwa wakurugenzi wa Bwana Yule (Lipumba) kuingia hapa. Ninarudia tena, kama wakithubutu kuingiza hata pua habari yao wataipata,” alisema Masoud Salim Faki ambaye ni mwanachama wa CUF.
MTANZANIA ilimtafuta Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya, ambaye alisema kuwa kauli ya Katibu Mkuu wake Maalim Seif ni ya kujihami na yenye hofu dhidi ya jambo fulani.
“CUF ni taasisi na ina ofisi mbili, moja ipo Zanzibar Mtendeni na Dar es Salaam Buguruni na Katiba inaeleza kuwa kiongozi yeyote wa chama ana haki ya kufanya kazi katika eneo lolote.
“Tunazo taarifa kuwa amechukua vijana kutoka shamba kama 100 ambao tangu jana (juzi) wamekuwa wakilinda ofisi ya Vuga na Mtendeni jambo ambalo anawapotezea muda tu hawa vijana,” alisema Sakaya.
Kutokana na hali hiyo, alisema wao wameendelea na vikao vya kawaida vya kuimarisha chama kuanzia juzi na jana ambapo wakurugenzi wote wanaotambulika kwa mujibu wa Katiba wamehudhuria.
Alisema ofisi za chama haziwezi kuwa kama mali au kampuni ya mtu binafsi kwani siku zote wenye mali zote huwa ni wanachama na si vinginevyo.
“Wakurugenzi walioteuliwa wataendelea na majukumu yao kwa upande wa Zanzibar na hata Bara maana hufanya kazi siku zote kwa pamoja na eneo lolote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoelekezwa kwa mujibu wa Katiba ya CUF,” alisema Sakaya.
Wiki iliyopita, Profesa Lipumba alitangaza uteuzi wa wakurugenzi wapya na manaibu wao ambao ni Nassor Seif (Mipango na Uchaguzi), Mbunge wa zamani wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Kurugenzi ya Mambo ya Nje), Haroub Mohamedi Shamis (Naibu Fedha na Uchumi), Masoud Ali Said (Naibu Habari na Uenezi) na Thiney Juma Muhamed akiteuliwa kuwa Kamanda wa Blue Guard Tanzania. | kitaifa |
Na JANETH MUSHI-ARUSHA SERIKALI imeombwa kuwapatia wafanyabiashara wa nyama kibali cha kusafirisha ngozi nje ya nchi ili kuweza kunufaika kiuchumi na kuliingizia Taifa mapato zaidi. Ombi hilo lilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Nyama jijini Arusha, Alex Lasiki, alipokuwa akizungumza katika hafla ya chama hicho kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. Alisema Serikali imeruhusu kuuzwa mifugo nje ya nchi ambapo wakati mwingine wanalazimika kuuza mifugo hiyo bei ya chini, huku wanunuzi kutoka nchi jirani ya Kenya wakinufaika zaidi kutokana na kupata malighafi zaidi ikiwemo ngozi na pembe. “Tunaiomba Serikali ituruhusu kusafirisha ngozi na malighafi nyingine zinazotokana na mifugo kwani itatusaidia kukuza mitaji yetu kama wafanyabiashara, lakini pia italiongezea Taifa kipato,” alisema. Mwenyekiti huyo alitaja changamoto kubwa inayowakabili kuwa ni pamoja na kuwepo kwa wimbi kubwa la mabucha feki yasiyokidhi viwango na wengi wao kutokuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo na kuiomba Serikali kufanya msako wa kuwabaini watu hao wanaokiuka masharti ya biashara hiyo. Naye Diwani wa Kata ya Olorieni, Zakaria Mollel (Chadema) ambaye pia ni mfanyabiashara wa nyama, alisema kumekuwapo na urasimu mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara wanaosafirisha ng’ombe hao kwenda nchi jirani ya Kenya kutokana na wao kutolipa kodi na hivyo kuiingizia hasara Serikali. Kutokana na changamoto hiyo, Mollel alisema ni vizuri Serikali ikaweka mnada katika mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga ili kuliingizia mapato Taifa na kuhakikisha wale wote wanaosafirisha mifugo kuwa na leseni na hatimaye kuweza kulipa kodi. Kwa upande wake Ofisa Biashara kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha, Godfrey Edward, alikitaka chama hicho kuanzisha uongozi wao katika kila kata ili waweze kudhibiti uanzishwaji holela wa mabucha yasiyozingatia afya ya walaji. | kitaifa |
MWANAFUNZI Mtanzania Felister Rushubiza, ameibuka ‘kidedea’ kwa kuongoza kitaifa katika matokeo ya kumaliza Elimu ya Juu ya Sekondari, yaani 2018 Grade 12 Ordinary Level Top Ten nchini Namibia.Felister (18) ni mtoto wa pili, kati ya watoto wanne, wa familia ya Joseph Rushubiza inayoishi nchini humo kwa takribani miaka 20 sasa.Felister amepata matokeo hayo, baada ya kuhitimu elimu darasa la 12 katika Shule ya Sekondari ya ‘St. Boniface College’.Kwa taratibu za kielimu za nchini humo, mwanafunzi huanza darasa la kwanza hadi la saba kwa elimu ya msingi na baadaye husoma darasa la nane hadi la 10 elimu ya sekondari. Kisha humalizia darasa la 11 na 12 kwa mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari.Akizungumza na gazeti hili kutoka Jiji la Windhoek, Namibia, Felister alisema matokeo hayo yametokana na jitihada zake katika masomo na kumuomba sana Mungu kila wakati, akiwa na malengo ya kuja kuwa mbunifu na msanifu wa majengo. “Muda wote nilikuwa nilielekeza akili yangu katika masomo na kumuomba Mungu hasa nilipokuwa ‘Grade’ 12, nilifanya hivyo nikiamini kuwa ndio msingi wa mafanikio” alisema Felister. Kwa upande wake, baba mzazi wa Felister, Joseph Rushubiza, alisema anafurahishwa na matokeo hayo. Alisema ingawa alitarajia mtoto wake kufanya vizuri, hakutarajia kama angeweza kufanya vizuri, kiasi cha kuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa. “Niliamini angefanya vizuri kwa kuwa shule aliyohitimu ambayo pia alisoma ‘grade’ ya nane hadi kumi, ilikuwa ikitoa matokeo mazuri kwa kipindi kirefu, na alipofaulu kuingia ‘grade’ ya kumi na moja na kumi na mbili alikuwa akishika nafasi ya pili katika mitihani ya kawaida ya darasani,” alisema Rushubiza. Alisema Felister amefanikiwa kuwa wa kwanza kitaifa, baada ya kufanya vizuri wa wastani wa alama’ A’ katika masomo sita, kati ya saba, huku moja akipata wastani wa alama ‘C’, hatua iliyomwezesha kuibuka kinara dhidi ya wenzake. Kwa matokeo hayo Felister alipata ufaulu wa wastani 86.79 huku mshindi wa pili akiwa ni Remigius Manuwere, aliyepata ufaulu wa asilimia 85.18. Mshindi wa tatu alikuwa Ndeiweda Ndaameki, aliyepata ufaulu wa asilimia 83.88. Alisema utaratibu unaotumika nchini humo, unamtaka mwanafunzi kufaulu masomo sita katika jumla ya masomo saba, anayokutana nayo katika mtihani wa mwisho. “Ni jambo la furaha kwetu kama wazazi kuona mtoto wetu amefanya vizuri katika matokeo yake na zaidi tunaipongeza Serikali ya nchini hapa kwa kutambua umuhimu wa matokeo hayo na kujitokeza kuwapongeza watoto wote waliofanya vizuri akiwemo binti yetu,” aliongeza Rushubiza. Alisema Serikali ya Namibia ikiongozwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, iliandaa sherehe maalumu na kuwapongeza wanafunzi 10 waliofanya vizuri akiwemo Felister, ambaye anasema matokeo yake yamezidi kuleta chachu kwa wadogo wake wawili wa kiume ndani ya familia hiyo. Alisema kufanya vizuri kwa Felister, ambaye alizaliwa nchini humo, pia kumetokana na hamasa ya matokeo mazuri ya dada yake, ambaye kwa sasa anasomea masomo ya udaktari wa meno nchini Norway. Aidha alisema wakati huu ambao binti yake huyo anajiandaa kujiunga na elimu ya chuo kikuu, mara atakapomaliza elimu mipango yake ni kuwa Mhandisi na Msanifu wa Majengo, fani aliyosema kuwa imekuwa ikipendwa na binti huyo kwa kipindi kirefu. Baba mzazi wa Felister ni mtaalamu wa dawa (Mfamasia), wakati mama yake ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa Umeme, kwa sasa ni mjasiriamali wa shughuli mbalimbali. | kitaifa |
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imetangaza kuanza operesheni maalumu nchi nzima ili kukagua maeneo yanayotolewa huduma za chakula hasa katika mikusanyiko ya watu na sherehe mbalimbali ili kubaini kama zinakidhi taratibu za kiafya lengo likiwa ni kulinda afya za wananchi. Inaelezwa, kwa mujibu wa takwimu, watu milioni 600 dunia huugua kwa nyakati mbalimbali kutokana na kula chakula ambacho si salama na watu zaidi ya 420,000 hufariki dunia.Kwa Afrika, watu milioni 91 huugua na watu 137,000 hufariki kwa chakula kisicho salama hususani kwenye mikusanyiko ya watu. Akizungumza katika mkutano wa watoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko ya watu jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo alisema operesheni hiyo itahusisha pia chama cha watoa huduma ya chakula katika sherehe, misiba na mikusanyiko ambao hawazingatii sheria. Alisema operesheni hiyo itaangalia huduma hiyo kuanzia utayarishaji, usafirishaji pamoja na kuangalia wafanyakazi wanaoandaa huduma hiyo ya vyakula kama wanakidhi vigezo na taratibu zilizowekwa.“Wananchi wamekuwa katika hatari za kiafya kutoka na watoa huduma ya Chakula wasiozingatia sheria, hivyo ni muhimu vyakula hivyo kuwa salama ili kulinda afya ya jamii...naamini mkutano huu uliolenga kujadili uzingatiaji wa sheria katika utoaji wa huduma hiyo utaleta matokeo chanya,” alisema Kijo. Alisema chakula ni muhimu katika hafla nyingi, hivyo wameona upo umuhimu wa kukutana na wadau hao na kuwaelimisha umuhimu wa kufuata kanuni kabla ya kuchukua hatua.Alisema wamebaini kuna changamoto nyingi katika utoaji huduma hiyo na kutozingatia sheria na kusababisha madhara kwa jamii. “Maeneo mengi yanayoandaliwa chakula hayakidhi kanuni za afya, unakuta wafanyakazi hawajielewi anatoka kujisaidia kucha chafu, anafuta uchafu kwenye nguo anakanda au kumenya chakula... wanasafirisha chakula katika mazingira mabovu, ndoo hadi za chooni zinahifadhiwa chakula,” alieleza.Aliongeza kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa mwaka 2015, watu milioni 600 huugua kwa kula chakula ambacho si salama, na 420,000 hufariki dunia na tatizo hilo ni kubwa Afrika ambako watu milioni 91 huugua na 137,000 hufariki kwa kula chakula kisicho salama mikusanyiko ya watu. “Kutokana na hali hiyo, tutahakikisha tunasimamia sheria na kufungia watoa huduma wanaohatarisha maisha ya wananchi... zaidi ya watoa huduma 637 wamesajili na asilimia 37 kutoka jijini Dar es Salaam na idadi hiyo ni ndogo kwa kuwa kundi la wafanyabiashara hao wengi hawajasajiliwa,” alifafanua. Mkurugenzi wa Love Catering Service, Michael Lee alisema sheria hizo zikisimamiwa na Serikali ipasavyo, zitasaidia watu wasio na taaluma kuheshimu kazi hiyo ambayo kwa sasa imedharaulika. | kitaifa |
VITA dhidi ya biashara ya bidhaa za magendo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki bado ni mbichi na juhudi za kutokomeza janga hilo zinahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo.Hayo yalisemwa na maofisa wa mpakani katika mpaka wa Uganda na Kenya kwenye Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Busia, ambako bidhaa za magendo zimekuwa zikipitishwa katika njia za panya bila kupitia kituoni hapo.Biashara hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa ni kinywaji aina ya bia, inatajwa kuipa serikali ya Kenya hasara kubwa ya mapato, kwani zimekuwa zikipitishwa bila kulipiwa ushuru kwa mujibu wa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Biashara hiyo ya magendo imewanogea mpaka wamiliki wa sehemu za kuuzia bia na sehemu nyingine za starehe ambao wanaagiza bidhaa hiyo kupitia njia za vichochoroni kutokana na haina gharama kubwa na inawapa faida kubwa.Mfano chupa moja ya bia yenye ujazo wa nusu lita nchini Uganda inauzwa kwa shilingi za Kenya 80 lakini ikifika nchini Kenya inauzwa kwa shilingi za Kenya 200 na katika Kituo cha Busia na Malaba inauzwa kwa Sh 100.Serikali ya Kenya inajipanga kuboresha sheria na ulinzi wa mipakani ili kuzuia biashara hiyo haramu ambayo imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo. | kitaifa |
WIZARA sita zitashirikiana kufanya sensa ya kilimo na mifugo Novemba, mwaka huu, Tanzania Bara na Visiwani. Akizungumza katika semina ya siku mbili ya wahariri na waandishi kutoka mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, jijini hapa jana, Mtakwimu Mwandamizi kutoka Idara ya Takwimu za Kilimo, Samweli Kawa alisema hiyo ni muhimu kupima kiwango cha umasikini nchini. Pamoja na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, wizara nyingine zitakazoshiriki katika sensa hiyo ya kilimo na mifugo ni Wizara ya Kilimo, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar (OCGS). Alisema sensa hiyo itahusisha mazao yote makubwa ya kilimo yakiwemo ya chakula, biashara na mazao ya bustani, mifugo aina zote, wafugaji wa samaki, nyuki na shughuli za jamii nchini. Alisema wakulima wadogo waliochaguliwa ni wenye mashamba ya mita za mraba 25 na mifugo kuanzia ng’ombe mmoja, mbuzi 50 na kuku 100 na kingine katika kaya na familia hizo. Kawa alisema sensa hiyo ni ya sampuli, itahusisha wakulima wakubwa na wadogo, wakulima wakubwa mashamba yatapitiwa na madogo yatachukuliwa machache kwa niaba ya mengine.Alisema takwimu za sensa hiyo pamoja na kutumika katika mipango ya serikali, zitatumika vyuoni kutoa mafunzo, uzalishaji na ufugaji; ufugaji wa samaki na nyuki na wadau. Alisema sensa hiyo itakuwa ya tano tangu kuanza, nyingine zilifanyika mwaka 1971/1972, 1993/1994, 2003/2004, 2007/2008 na hii ya mwaka huu 2018/2019 itakuwa ya tano.Alisema maandalizi yamefanyika kwa kuorodhesha kaya zitakazohusika, Tanzania Bara na Zanzibar, sampuli za kaya, na majaribio tayari ya madodoso yameshafanyika katika mikoa sita Bara na miwili Kaskazini Unguja na Kusini Pemba Visiwani. Alivitaka vyombo vya habari kuwa mabalozi kwa kuelimisha umma kushiriki na kutoa ripoti ya taarifa mbalimbali kuhusu sensa hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa. Mtakwimu Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa alisema mafunzo hayo ya wahariri na waandishi yanalenga kuwajengea uwezo wa kuandika kwa usahihi takwimu zinazotolewa na ofisi hiyo.Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Daniel Andrew alisema mabadiliko ya sheria NBS tangu ile ya mwaka 1995 hadi ya 2019 yanalenga kupanua wigo wa upatikanaji wa takwimu hizo.Mwanasheria kiongozi wa NBS, Oscar Mangula alisema mabadiliko ya sheria mwaka 2019, yameruhusu taasisi kutolazimika kuripoti NBS wakati zinaenda kufanya utafiti nchini. | kitaifa |
Kiongozi huyo amethibitisha mpango huo uko katika hatua za mwisho na kwamba, The Gunners watatoa ofa kwa makocha wa Uganda kwa kuwekeza katika vifaa vya mazoezi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki."Tulikwenda London mwezi uliopita Januari 16 na kufanya vikao vitatu na uongozi wa Arsenal FC wenye lengo la kujenga urafiki nao,” Onyik aliiambia Xinhua."Tulikubaliana kwamba watafundisha baadhi ya makocha wetu, wataipa Uganda Cranes nafasi ya kufanya mazoezi uwanja wa Emirates London, kujenga kituo cha soka na pia timu yao itutembelee mwakani Juni na kucheza baadhi ya mechi”.Chanzo hicho cha habari kutoka China kilisema Waziri wa Michezo, Charles Bakkabulindi, amethibitisha kwamba maelezo zaidi na kuhusu mkandarasi atakayejenga kituo hicho vitakuwa wazi Machi."Kuwa na kituo kikubwa na kizuri Uganda kutasaidia maendeleo ya soka nchini,” alisema Bakkabulindi."Makocha wetu kufundishwa kutawasaidia kuendeleza mchezo huo nchini,” alisema."Mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na wenye soko na hiyo inaelezea kwanini tumefikiria kuwa na urafiki na timu hiyo kubwa”. | michezo |
WAANDISHI WETU-MOROGORO/DAR MJI wa Morogoro umeendelea kuwa katika hali ya utulivu huku ukimya
ukitawala katika eneo ilipotokea ajali ya lori la mafuta ambalo lilipuka moto
na kusababisha vifo vya watu 75 hadi sasa. MTANZANIA ilitembelea katika eneo la ajali Msamvu Mtaa wa Itigi,
ambalo lipo jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi Mkoa wa Morogoro ambapo baadhi ya
watu wanaofanya shughuli zao ikiwamo biashara, wamesema kuwa upweke umetawala
huku idadi kubwa ya vijana ambao walikuwa wakionekana katika eneo hilo kufariki
dunia kwa ajali hiyo. Dereva Bodaboda Kijiwe cha Maraha, Daimon Chibigasi alisema eneo
ilipotokea ajali hiyo ndipo kijiwe chao
cha kazi, lakini siku ya tukio wengi walichelewa kufika huku kundi kubwa la
watu waliopoteza maisha walikuwa ni wapiga debe, pamoja na wapita njia. Alisema wakati ajali hiyo inatokea yeye alikuwa upande wake wa pili
wa barabara ambapo walishuhudia idadi kubwa la wapiga debe, wapita njia
wakikimbilia kwenye eneo hilo la tukio ambapo wengine walikuwa wakipiga picha
kwa kutumia simu zao. “Mateja (watumia dawa za
kulevya) ndio waliokuwa wengi na wapita njia, maana wengi hatuwaoni mtaani, ule
wingi wao ambao tumeuzoea mtaani haupo na zile pilikapilika za kuitia abiria hapa
kwenye tuta umepungua sana, kwa kweli hali imepooza tofauti na awali. “Ofisi yetu imeungua, hapa ndio kijiwe chetu, sisi mafundi pikipiki
na muuza mitumba ambaye alikuwa anatundika nguo zake kwenye miti hii
iliyoungua, kwa sasa inabidi tupaki huku pembeni,” alisema Chibigasi Naye Rajabu Idd maarufu Jaji, alisema ugumu wa maisha hususani kwa
vijana ni sababu ya kufanya kitu chochote bila kuangalia madhara yake. “Kinachosababisha ni ugumu
wetu wa maisha, mtu kalala na njaa halafu asikie kuna sehemu kuna riziki,
hawezi kuiacha eti kwa hofu inaweza kutokea hatari, muda ule mtu unafurahia
kutuliza njaa uliyonayo,” alisema Idd. Aidha, alisema mpaka sasa waendesha bodaboda wawili katika kijiwe chao ndio walipatwa na
maafa hayo huku akieleza kwamba kundi kubwa la waliopoteza maisha ni wapiga
debe. “Wapiga debe wengi hatuna historia zao na wengi hawajulikani
wanakoishi, lakini wamepungua sana, hata ukishusha abiria sasa hivi huwaoni, mwanzo
walikuwa wengi mpaka wanagombania abiria, wengine walikuwa wanatafuta abiria
kwa ajili ya gari za IT na magari binafsi,” alisema MNARA KUJENGWA Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Morogoro
kujenga mnara wa kumbukumbu katika eneo
iliyozikwa miili ya watu 61 katika eneo la Kola ambapo hadi sasa waliopoteza
maisha katika ajali hiyo wamefikia 75. Hayo aliyasema jana mjini hapa katika eneo la mazishi ya miili ya
watu 61 katika eneo la Kola mjini hapa, ambapo alisema kuwa ni vema ukajengwa
mnara huo wa kumbukumbu na ambao pia aliagiza uzungushiwe uzio. Pamoja na hali hiyo Majaliwa amewataka viongozi wizara ya afya kwa kushirikiana
na serikali Mkoa wa Morogoro kuendelea kusimamia kazi hiyo hadi hali ya utulivu
itakaporejea. “Viongozi muendelee kutoa
ushirikiana na familia ya
majeruhi na wafia kwa kipindi
chote ili kuhakikisha zoezi linakwisha
pasipo sintofahamu kuhusu miili ya marehemu
hawa,” alisema Majaliwa MIILI 61 YAZIKWA Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, alisema kuwa
hadi sasa tayari miili ya watu 61 imeshazikwa katika makaburi ya Kola na
mingine tisa iko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa
ya Mkoa wa Morogoro. WALIOFARIKI
WAFIKIA 75 Idadi ya vifo vya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo
imeongezeka na kufikia 75 baada ya majeruhi wengine wanne waliokuwa wakipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhibili (MNH) kufariki dunia jana. Akizungumzia na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari
Mkuu wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, aliwataja waliofariki kuwa ni pamoja na
Jackson Shao(25), Kulwa Dominic (28), Isamail Mwanga (28) na Muhidin Mtingwa (42). Aligeisha alisema hadi sasa ni majeruhi 39 pekee wanaoendelea
kupatiwa matibabu hospitalini kati ya 46, waliofikishwa katika hospitali baada
ya wengine watatu kufariki dunia juzi. “Mpaka sasa kuna vifo saba ambapo watatu walipoteza maisha jana
(juzi) wakati wanasafirishwa na leo (jana) wameongezeka wanne, tumebakiwa na majeruhi 39 kati ya wale
46 walioletwa Muhimbili. “Kuna majeruhi wengine hawana ndugu tunaomba kama una ndugu yako hapa
ujitokeze na hawa waliofariki ndugu zao
wajitokeze pia ili waweze kuchukua miili ya ndugu zao ambayo imehifadhiwa hapa
hospitalini. “Kama hospitali tunaendelea kufanya kila tunachoweza katika
kuwahudumia majeruhi hawa, dawa tunazo na wataalamu wapo muda wote
kuwahudumia,” alisema Aligaeshi. Aligaesha aliwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili
kuwasaidia majeruhi hao kutokana na uhitaji mkubwa wa damu katika matibabu yao. MBATIA ATOA NENO Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameishauri
Serikali kushirikiana na hospitali binafsi ili kuhakikisha majeruhi hao
wanapatiwa matibabu katika mazingira rafiki kutokana na hali waliyonayo. Mbatia aliwaambia waandishi Dar es Salaam jana kuwa licha ya Serikali
kuahidi kugharamia matibabu ya majeruhi hao, ni vema pia ikashirikiana na
hospitali hizo ili kuwezesha kupatikana kwa wodi kubwa na zenye viyoyozi
tofauti na sasa ambapo wamewekwa katika chumba kidogo kinachotumia feni za
kawaida. Mbatia alisema Serikali na wadau wengine hawapaswi kuangalia suala la
gharama badala yake wafikirie mateso wanayoyapata majeruhi hao ambao baadhi yao
wameungua kwa zaidi ya asilimia 95 ya miili yao. “Nitoe rai kwa Serikali na hili liwapendeze Watanzania wengine pale
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kile chumba walichowekwa kwa kweli ile wodi ni
ndogo kuwaweka wote kwa pamoja. Lakini niliwasiliana na wataalamu mbalimbali wa
tiba wa ndani na nje ya nchi, watu walioungua miili yao kwa asilimia 95 au
zaidi wanahitaji kuwa kwenye hali ya joto stahiki. “Wanatakiwa wawe kwanza kwenye eneo kubwa la kutosha na wawe kwenye
viyoyozi waweze kutunzwa na kuhudumiwa vizuri, joto walilonalo pale linaendelea
kuwatesa,”alisema Mbatia. Mbatia alisema hospitali binafsi kama vile Regency, TMJ, Aga Khan,
Bugando, KCMC na hospitali nyingine za aina hiyo nchini, zinaweza kuchukua japo
wagonjwa wawali au watatu kila moja ili
kuipunguzia mzigo Muhimbili na kwamba hatua hiyo itawezesha baadhi ya watu
wenye uwezo kujitokeza kuwalipia gaharama za matibabu baadhi ya majeruhi. HABARI HII
IMEANDALIWA NA ASHURA KAZINJA, RAMADHAN LIBENANGA (MORO), AVELINE KITOMARY, LEONARD
MANG’OHA NA NEEMA SIGALIYE (Tudarco) | kitaifa |
Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM
CHAMA Cha wafugaji Tanzania (CWT), kimeiomba Serikali kuwaruhusu kuingiza mifugo yao katika hifadhi za taifa kwa dharura ili kuinusuru kutokana na ukame unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Wafugaji hao walisema hali ya ukame imekuwa tishio na tayari wamepoteza mifugo mingi inayokufa kwa njaa baada ya majani kukauka kutokana na kukosa mvua kwa muda mrefu.
Sambamba na hilo, pia wamealaani matukio ya kuuawa kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini, likiwamo lililotokea hivi karibuni wilayani Arumeru mkoani Arusha ambako watu wanne wamepoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi za moto na askari wa Suma JKT.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa CWT, Magembe Makoye, alisema Serikali ilichukulie suala la ukame kuwa ni dharura na hivyo iwaruhusu kuingiza mifugo ili kupata chakula katika hifadhi hizo na baada ya ukame kupungua mifugo hiyo irudishwe maeneo yake ya awali.
“Tunaiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na ile ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuangalia namna ya kuwasaidia wafugaji ili kunusuru mifugo yao ambayo ndiyo uchumi wao na taifa kwa ujumla.
“Katika hili, tunashauri wafugaji waruhusiwe kuingiza mifugo hiyo japo mara mbili kwa wiki, wakati wakisubiri mvua kunyesha,” alisema Makoye.
Kuhusu mauaji, Makoye alisema kuwa ni ya ukandamizaji dhidi ya wafugaji.
“Upo utaratibu wa kisheria wa kuwaondoa wafugaji katika maeneo yasiyo rasmi, lakini si kwa kuwapiga risasi na kuwaua,” alisema Makoye.
Aidha Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Francis Nzuki, alisema kuwaua wafugaji na hata makundi mengine ni uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo hawatalifumbia macho.
Katika hatua nyingine, Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), umeikumbusha Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi Katiba mpya kama ilivyokubaliwa katika mkutano wa haki za binadamu uliofanyika Geneva, Uswisi.
Katika mkutano huo uliohusisha pia asasi za kiraia na THBUB, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengulumwa, alisema Tanzania iliridhia mapendekezo 133, likiwamo la kutengeneza Katiba mpya ya wananchi. | kitaifa |
GENEVA, USWISI NCHI wanachama wa mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kupata ulemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani. Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO, kuna nia ya kuhakikisha kunakuwepo mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka. Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote. WHO kwa sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha. Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa ambazo ilikua gharama kupatikana kwenye nchi zilizo masikini hasa kusini mwa jangwa la Sahara. Hali ya umaskini na kutokuwa na vituo vya afya vinavyokidhi mahitaji kumesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakitafuta tiba ya kienyeji ambayo husababisha madhara zaidi. Lakini mpango huu mpya utalenga kuwafundisha watoa huduma wa afya jinsi ya kushughulikia mtu aliyeumwa na nyoka na elimu ya huduma ya kwanza kwa jamii iliyo hatarini. Kila mwaka zaidi ya watu 100,000 hufa duniani kutokana na kuumwa na nyoka asilimia 20 wakitoka barani Afrika. Karibu watu nusu milioni wana ulemavu wa kutokuona, kukatwa viungo na ulemavu mwingine kutokana na mashambulizi ya nyoka. | kimataifa |
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kongwa imemhukumu kwenda jela miaka sita Ofisa Tabibu wa wilaya hiyo, Martine Ndahani kwa tuhuma za kumshawishi mwananchi ampe rushwa ya Sh 100, 000 ili mgonjwa wake awekewe damu. Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kisasila Malangwa baada ya kuridhishwa na mashahidi tisa waliojitokeza kutoa ushahidi. Upande wa mtuhumiwa ulikuwa na mashahidi watatu waliojitokeza kutoa ushahidi ambao haukuiridhisha mahakama. Baada ya kusikikiza ushahidi wa pande zote, Hakimu Malangwa alimhukunu kwenda jela miaka sita au kulipa faini ya Sh 500,000 kwa kila kosa alilosomewa. Kesi hiyo ilikuwa chini ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma, Moshi Kaaya. Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema baada ya kufanya uchunguzi walimkamata mtuhumiwa huyo ambaye ni tabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa na kumfungulia mashtaka ambayo hukumu imetolewa. Kibwengo alisema wananchi wanapaswa kushirikiana na Takukuru kutoa taarifa pale wanapoona kuna viashiria vya rushwa. Wakati huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Kondoa imemhukumu kwenda jela miaka minne, Jeremia Magawa aliyekuwa msimamizi wa miradi ya Kampuni ya FM Engineering iliyokuwa inasambaza umeme wa REA katika Kijiji cha Kiteo wilayani Kondoa. Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mateso Masao baada ya kusikikiza ushahidi wa pande zote. Mahakama ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo alichukua jumla ya Sh 120, 000 kwa wananchi wawili ili awawekee nguzo za umeme karibu na nyumba. Hata hivyo hakufanikiwa baada ya kunaswa na mtego wa Takukuru na kufikishwa mahakamani. Kesi hiyo ilikuwa chini ya mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Haule. | kitaifa |
Tunu Nassor – Dar es Salaam CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ubungo kimewazi wazi mikakati
yake ikiwamo kuhakikisha wanarudisha majimbo ya Ubungo na Kibamba pamoja na kata
zote 14 katika Uchaguzi Mkuu utajaofanyika Oktoba mwaka huu ili yawe katika
himaya yao. Akizungumza katika semina elekezi kwa wenyeviti na wajumbe wa
serikali za mitaa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja alisema
wameanza kujipanga kuanzia ngazi ya shina kwa kufanya vikao na viongozi wote. Alisema wanafanya semina za viongozi mara kwa mara kuhakikisha kila
mmoja anatekeleza majukumu kwa nafasi yake. “Mikakati iliyopo ni kuhakikisha tunapata ushindi mkubwa katika
nafasi ya urais, kurudisha majimbo yote mawili na kupata viti vyote 14 vya
udiwani,” alisema Mgonja. Alisema wamefanya ziara katika matawi 136 kuhakiki uhai wa chama
ikiwa ni pamoja na kuondoa migogoro midogo baina ya wanachama ambayo huenda
ingewatenga katika kipindi cha uchaguzi. “Katika ziara hiyo tumeangalia pia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ya CCM na kupokea kero mbalimbali za
wananchi,” alisema Mgonja. Aliongeza kuwa wanashukuru kupata msingi wa kuwa na wenyeviti wa
serikali za mitaa 90 pamoja na wajumbe 450 wanaotokana na chama hicho. “Tayari tuna msingi wa mkubwa wa ushindi kutoka kwa wenyeviti na
wajumbe wa serikali za mitaa ambapo sasa mitaa yote wanatokana na CCM,” alisema
Akizungumzia semina hiyo, Mgonja alisema viongozi hao wa mitaa
wanatambulika na katiba ya nchi na katiba na sera ya CCM . “Mtanatakiwa kusoma Ilani kwa kuwa kuna maelekezo kwenu
yatakayowaongoza katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi,” alisema Mgonja. Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya hiyo, Chifu Sylvester Yaredi
alisema semina hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuboresha weledi na ufanisi wa
viongozi hao. Alisema katika semina hiyo wamewajengea uaelewa katika suala la
mahusiano mema kati yao na chama pamoja na maadili ya uongozi. “Tunatarajia baada ya mafunzo haya ufanisi katika utendaji kazi
utaongezaka mara dufu baada ya kujua
mipaka yao ya kazi,” alisema Yaredi. Alisema wamejifunza miiko , wajibu na kipi wafanye na wasivyotakiwa
kuviofanya wakati wa kutekeleza majukumu yao. | kitaifa |
Busungu ambaye aling’ara hivi karibuni katika mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers, alionekana kufanya vizuri baada ya kuifungia Yanga mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa siku hiyo.Akizungumza na gazeti hili, Busungu alisema anatarajia kuonesha uwezo na kujituma katika michuano ya kimataifa na ligi, ikiwezekana kuwa mfungaji bora.“Mashabiki wa Yanga wategemee mambo mengi mazuri kutoka kwangu, watafurahi kwa kuwa nimejipanga kupigana sio tu katika tu kujionesha bali kuisaidia timu,” alisema mshambuliaji huyo.Mchezaji huyo aliyejiunga na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika katika timu yake ya Mgambo Shooting, alisema kitu kitakachomwezesha kufanya makubwa ni kuendelea kuonesha nidhamu ndani ya uwanja na nje.Alisema bila kuonesha nidhamu na kujituma itakuwa ni ngumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kila mtu kupambana ili kubaki katika kikosi hicho.“Mimi kazi yangu ni kuonesha uwezo wangu uwanjani, kuhusu kama nitapangwa kikosi cha kwanza anayejua ni kocha, lakini naahidi kufanya vizuri katika michezo ijayo,” alisema. | michezo |
Na Eliya Mbonea, Arusha Wakati afya ya MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji wa mfupa kwenye mguu wa kulia jana, familia yake imelalamikia suala upelelezi wa tukio la kujeruhiwa kwake. Akizungumza mjini hapa juu kuhusu hali ya Lissu, Msemaji wa familia ya Lissu, Wakili Alute Mughwai, amesema hali ya ndugu yao inaendelea na vizuri na wanamshukuru Mungu kwa kila hatua anayopitia katika matibabu lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote waliyopewa kuhusu uchunguzi wa tukio hilo. “Hakuna taarifa tuliyopewa kama ndugu licha ya kuziomba mamlaka ziombe msaada wa kiupelelezi kutoka nje, lakini tulijibiwa polisi wanaweza kufanya uchunguzi japo hadi sasa hakuna kinachoendelea, wasiwasi wetu ni kwamba polisi hawana utayari wa kuchunguza tukio hili ndiyo sababu wamekuwa kimya,” amesema. Kutokana na hali hiyo, Wakili Mughwai amelikumbusha Jeshi la Polisi na mamlaka husika kuhakikisha wanafanya upelelezi wa tukio hilo ikiwamo kuwakamata wahusika. “Mungu aliye pamoja nasi tunaamini atafunua njia nyingine nasi tuchukue hatua zitakazofuata baada ya kukaa na kushauriana na mgonjwa. Hii tutaifanya pale tutakapoona masuala yamegonga mwamba,” amesema Wakili Mughwai. Kuhusu mawasiliano na Ofisi ya Bunge kuchangia matibabu ya Lissu ambaye ana haki ya kupatiwa matibabu kutoka kwenye ofisi hiyo, Wakili Mughwai amesema hadi sasa wana zaidi ya mwezi mmoja na siku 15 bila kuwa na mawasiliano na ofisi ya Bunge. “Familia ilipokea barua ya Bunge Februari Mosi, mwaka huu ikitutaarifu kupokea barua yetu ya Januari kuhusu kuhamishwa kwa Lissu kwenda Ubelgiji kutoka Hospitali ya Nairobi alikolazwa tangu apigwe risasi na kututaarufu kwamba wamewasiliana na Wizara ya Afya iliyotoa madaktari watatu kwenda Nairobi kwa ajili ya kumuona Lissu lakini hawakuweza kumuona kwani tayari alishapelekwa Ubelgiji,” amesema. Lissu alijeruhiwa kwa risasi Septemba 7, mwaka jana nyumbani kwake mkoani Dodoma kisha kusafirishwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi. | kitaifa |
MIOYO ilivunjika wakati mataifa yote matano ya Afrika, Senegal, Nigeria, Misri, Morocco na Tunisia – kutolewa katika hatua ya kwanza ya mashindano ya Kombe la dunia, lakini baadhi ya mashabiki wanasema hawajapoteza matumaini. “Angalau bado tuna timu ya taifa ya Ufaransa, “ watu wengi walitania katika mitandao ya kijamii.Hata Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron naye aliingia katika utani, pale alipowaambia Wanigeria juzi kuwa sasa Super Eagles wametolewa katikamashindano ya Kombe la Dunia, inabidi waishangilie Ufaransa. Ni kweli, timu ya taifa ya Ufaransa ina wachezaji 14 katika kikosi chake, ambao wanaweza kuchezea nchi za Afrika.Wachezaji wawili wa Ufaransa wenye undugu wamefanya hivyo. Kaka yake Paul Pogba, Florentin, anachezea Guinea, wakati kaka yake Steve Mandanda, Parfait, yeye anachezea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wote awali walikuwa wakiichezea timu za taifa za vijana za Ufaransa kabla ya kuamua kuzichezea timu, ambako wazazi wao wanakotoka. Nyota wa sasa wa Ufaransa katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia, mwenye umri wa miaka 19, Kylian Mbappé, alizaliwa na baba Mcameroon na mama Mfaransa.Wakati huohuo, Ubelgiji ina wachezaji nane wenye asili ya Afrika, ambapo mmoja kati ya wazazi wao ama baba au mama au wote wanatoka katika bara hilo, Katika kikosi hicho kuna wachezaji kama akina Kompany, Fellaini, Lukaku, Dembélé, Boyata, Batshuayi, Chadli na Tielemans. SHERIA ZA FIFA Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) liliweka sheria na taratibu za mchezaji kuweza kuchezea taifa jingine: Wacheza soka ambao wanacheza mashindano ya kishindani ya kimataifa katika timu moja hawawezi kuhamia katika timu ya taifa jingine. Lakini sheria hii ilirahisishwa na kuwawezesha wanasoka kubadili utaifa kutoka katika timu ya vijana hadi ileya wakubwa.Mechi za kirafiki hazizuii, hivyo Diego Costa aliweza kuhamia Hispania baada ya kucheza mechiza kirafiki za kimatifa akiwa na timu ya taifa ya Brazil, kama alivyofanya mchezaji wa Ubelgiji Nacer Chadli baada ya kuichezea mchezo wakirafiki timu ya taifa ya Morocco. Wachezaji ambao hawana uhusiano wa kidamu na nchi, waliruhusiwa tu kuwakilisha nchi hiyo ikiwa tu watakuwa wameishi na kucheza soka katika nchi hiyo kwa miaka mitano. Lakini hilo ni tofauti kabisa na wakimbizi, ambao wanaweza kuichezea nchi wanayoishi kama wakimbizi bila ya kuishi pale kwa miaka mitano. SWEDEN NA KENYA Pia waliondoka katika mashindano ni pamoja na England, Sweden, Uruguay, Brazil, Urusi na Croatia.Wachezaji wenye wazazi wa Afrika katika kikosi cha England ni Delle Alli – ambaye baba yake anatokea Nigeria na mchezaji mwenzake Danny Welbeck ambaye alizaliwa Manchester na wazazi wa Ghana. Msweden, John Guidetti aliishi Kenya kwa miaka mitatu akiwa mtoto, akionesha kipaji chake akiwa na timu ya watoto ya Nairobi iliyoshiriki Lig Ndogo. Mashabiki wa Kenya walifurahia kubadilishana picha katika mitandao ya kijamii ya chipukiuzi Guidetti. “Bado nina uhusiano mkubwa na Kenya na kila wakati ninarudi nchini humo na kupata mapokezi makubwa, “alisema Guidetti akikaririwa na gazeti la Standard.Kocha wazamani wa Guidetti, Chris Amimo, aliliambia gazeti hilo kuwa Guidetti “wakati wote amekuwa akipangwa katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Kenya. Anapenda kucheza. “Baba yake anafanyakazi katika shule ya Sweden, ambayo iko jirani kabisa na uwanja wa Ligi Ndogo, “alionsema. Wakati Guidetti ambaye anaangukia katika sheria hizo za Fifa, mchezaji mwenzake wa Sweden Martin Olsson alizaliwa na mama Mkenya na kinadharia ana nafasi ya kuchagua moja kati ya nchi hizo. “Wachezaji wengi wa kulipwa ambao wamethibitishwa kucheza soka la kiamtaifa, wanacheza Ulaya…” “Ni kweli sita kati ya wachezaji 23 katika kikosi cha Morocco waliocheza fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia, walizaliwa katika nchi hiyo.” | michezo |
NA JESSCA NANGAWE DILI la kiungo mahiri wa Simba, Said Ndemla, kwenda kucheza soka la kulipwa Sweden limefikia hatua nzuri, ambapo anatarajia kusafiri nchini humo wiki ijayo. Tayari klabu ya Simba imempa baraka zote kiungo huyo kwaajili ya kwenda kujaribu bahati yake katika klabu ya AFC Eskilistuna, inayomhitaji. Akizungumza na MTANZANIA, meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu zitakazomruhusu mchezaji wake kuingia Sweden. “Suala la Ndemla lipo kwenye hatua za mwisho, kinachosubiriwa ni hati yake ya kusafiria ambayo wakati wowote itatoka, tunaamini siku yoyote kuanzia Jumatatu anaweza kuondoka,” alisema Kisongo. Ndemla alikuwa anahitajika katika klabu hiyo tangu mwishoni mwa msimu uliopita, lakini uongozi wa Simba uliweka ngumu baada ya kudai bado ulikuwa unahitaji mchango wake katika kikosi cha Msimbazi. Endapo kiungo huyo atafuzu majaribio yake, ataungana na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu, aliyejiunga na timu hiyo mapema Januari, mwaka huu. | michezo |
MWAFUNZI, Zawadi Pindua (15) aliyekuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Mwimbi iliyoko wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa amekufa baada kutoa mimba ili aendelee na masomo baada ya muhula wa masomo kuanza Januari mwaka huu.Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Justine Masonje amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwanaume aliyempa ujauzito na kumsaidia mwanafunzi huyo kutoa mimba iliyomsababishia umauti amekamatwa .Alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji ha Tunyi kilichopo katika kata ya Mambwe Nkoswe wilayani Kalambo Januari 13 mwaka huu saa tisa mchana nyumbani kwa mwanaume anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.Kamanda Masonje alieleza kuwa Ofisa wa Kijiji cha Tunyi Hassan Lupasa aligundua mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa nyumbani kwa mtuhumiwa na aliongoza msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa .“Marehemu na mtuhumiwa waliondoka kijijini Mwimbi Januari 22, mwaka huu na kwenda kujificha katika kijiji cha jirani cha Tunyi ambapo mtuhumiwa alimsaidia mwanafunzi huyo kutoa mimba ili shule zikifunguliwa Januari mwaka huu arudi shule na kuendelea na masomo yake,” alieleza.Kamanda Masonje aliongeza kusema kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali wa shauri lake kukamilika | kitaifa |
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amepokea Ripoti Maalumu kutoka kwa Kamati Tendaji ya Madini ya Ujenzi na Madini ya Viwandani kuhusu changamoto zilizopo katika uchimbaji wa madini na masoko ya kuuzia madini hayo.Kikao hicho kilichoongozwa na Biteko, kilifanyika juzi jijini hapa kikiwa ni mwendelezo wa vikao vya kamati hiyo vilivyoanza Novemba 14, mwaka huu, vikilenga kujadili changamoto wanazozipitia wachimbaji katika shughuli za uzalishaji wa madini hayo.Biteko aliwataka viongozi wa kamati ya madini ya ujenzi na kamati ya madini ya viwandani, kufanya kazi kwa ushirikiano ili wafanikiwe na kuwaahidi kuzifanyia kazi changamoto zao.“FEMATA wamefanikiwa katika shughuli zao si kwa sababu wana akili sana ila wanashirikiana kwenye maamuzi yao, na mimi pia nashirikiana kwa karibu sana na Rais wenu wa Femata, John Bina, migawanyiko itawafanya msifanikiwe,” alisema Biteko.Aidha, alimpongeza Rais wa Wachimbaji Wadogo, John Bina kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuliongoza Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) na kuwataka wachimbaji wa madini kote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali katika sekta ya madini.“Kazi ya kusimamia rasilimali ya madini sio ya wizara peke yake ila ni kazi ya wananchi wote wakiwemo FEMATA, wachimbaji wenyewe na wadau wote wa madini,”alisisitiza Biteko.Aliongeza kuwa serikali inawathamini wachimbaji na wanachopaswa kuelewa ni kwamba sekta inazo changamoto nyingi na haziwezi kuisha kwa siku moja na kusema, “mimi binafsi ukiniuliza ninatamani nione wachimbaji wanafurahi, nione watu wote kwenye sekta wanafurahi.”Pia, Biteko alisema ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inaonesha usafirishaji wa madini nje ya nchi umepanda kwa asilimia 48 kutoka Oktoba 2018 hadi Oktoba 2019, hiyo ikionesha wachimbaji wamekubali. | kitaifa |
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake licha ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa juzi dhidi ya TP Mazembe ya Congo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mchezo huo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na hivyo Simba kuwa na kibarua kigumu cha kufanya katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Lubumbashi wikiendi hii.Huo ni mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kushindwa kupata ushindi wa pointi tatu kwenye uwanja huo, baada ya kushinda mechi zake zote za awali na zile za makundi za michuano hiyo, walizocheza kwenye uwanja huo.Matokeo hayo ni furaha kwa Mazembe ambao wanarekodi nzuri ya kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani hali inayowaweka Simba kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje na hatma yao ya kuendelea au kutoendelea kubaki Lubumbashi, Congo katika mchezo wa marudiano.Akizungumza baada ya kukamilika kwa mchezo huo Aussems alisema wachezaji wa timu hiyo walicheza vizuri na kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa, huku akijipa matumaini kuwa timu yake bado ina nafasi ya kufanya vizuri.“Licha ya kutoka suluhu nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu, walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kutumia, kufanya makosa kwa mchezaji ni kawaida kwenye mchezo hata sisi makocha wakati mwingine tunafanya makosa nitaongea nao na kulifanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano,” alisema Aussems.Kwa upande wake kocha wa TP Mazembe ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Mihayo Kazembe alisema wamepata ushindani mkubwa kutoka Simba hali ambayo hawakutegemae kulingana na rekodi zao za michezo ya nyuma waliyocheza na Simba.Simba ilifungwa mara mbili, nyumbani na ugenini katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2011.Alisema ushindani ulikuwa mkubwa kila timu ilicheza vizuri walitengeneza nafasi za kupata mabao, lakini walikosa umakini wa kuzitumia vizuri nafasi hizo. | michezo |
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu. | uchumi |
Iyoooooo! Spika Job Ndugai na kundi la wabunge 35 wa Bunge la Tanzania pamoja na Piere wamerejea nchini siku ya jana kutoka Misri walipokwenda kuipa hamasa #TaifaStars inayoshiriki #AFCON2019. Spika na wabunge hao pia walikuwa na ratiba ya kuzungukia maeneo mbalimbali ya kihistoria na kiuchumi pamoja na uwekezaji katika michezo yaliyoko nchini Misri. Pierre na baadhi ya wabunge wajamhuri ya muungano wa Tanzania walienda nchini Misri kuishangilia timu ya Taifa iliyokua inacheza mechi yake ya kwanza na Senegal kwenye michuano hiyo baada ya miaka 39. Siku ya juzi Tanzania ilichakazwa magoli 2 kwa bila na timu ya Senegal katika michuano hiyo ya Afcon inayoendelea nchini Misri. Kipigo hicho kimewachangaya na kuwagawa baadhi ya wadu wa soka nchini na hasira zao wakaamua kuzielekeza kwa kikosi hicho cha ushangiliaji . Wanadai kuwa ilitokana na laana ya kumpleka mtu kama Piere mzee wa Liquid aliyejipatia umaarufu kwa ulevi na kudai kuwa next time tuwapeleke watu kama mapadre na masheikh . | michezo |
Na GUSTAPHU HAULE, PWANI JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani, Kitengo cha Usalama Barabarani, limekusanya Sh milioni 52 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyotokea katika kipindi cha Novemba na Desemba, mwaka huu. Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Salum Morimori, alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari mjini Kibaha. Morimori, alisema kuwa Novemba mwaka huu walianza kufanya operesheni maalumu ya kukamata madereva wanaokiuka sheria za barabarani na kufanikiwa kukusanya Sh milioni 51 zilizotokana na faini kwa makosa 1,738 yaliyokamatwa.
Aidha, alisema katika kipindi cha Desemba operesheni hiyo ilifanyika katika maeneo ya Chalinze na kufanikiwa kukamata magari 44 ambayo kati ya hayo madereva saba wamefikishwa mahakamani na wengine kulipa faini ya Sh milioni 1.1. Morimori, alisema kuwa makosa yanayokamatwa ni pamoja na mwendokasi, ulevi kwa madereva, kupita magari ya mbele sehemu isiyoruhusiwa, ubovu wa magari pamoja na madareva kukosa leseni. “Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani kimejipanga kudhibiti ajali za barabarani kwa kufanya operesheni maalumu, hususani katika kuhakikisha kipindi cha sikukuu kinapita bila ajali,” alisema Morimori. Aliwataka madereva kutii sheria bila shuruti kwa kuzingatia sheria za barabarani na kwamba yeyote atakayekamatwa akiwa amelewa pombe hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. | kitaifa |
RAIS Dk. John Magufuli amesema anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu ya kuongezwa kipindi cha urais kutoka miaka mitano hadi saba kwa kuwa ni kinyume na Katiba ya nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza Ikulu, Dar es Salaam jana alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, aliwataka wananchi kupuuza mjadala huo. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa katika mkutano huo Magufuli alimwelekeza Polepole kuwajulisha wanachama wa CCM na Watanzania kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha urais. “Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadala huo kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama na ni kinyume na Katiba ya CCM na Katiba ya nchi,” alisema Polepole. Polepole alisema Magufuli aliwataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi, badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM iliyonadiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Pia alisema Magufuli hana mpango wowote na hatarajii kuongeza kipindi cha urais wakati wote wa uongozi wake. Kauli ya Magufuli inajibu hoja za baadhi ya viongozi, wakiwamo wabunge ambao mara kadhaa walikaririwa wakitaka kuongezwa kwa ukomo wa urais na ubunge hadi kufikia miaka saba ili kumpatia rais na wabunge muda wa kutekeleza majukumu yao. Hoja ya kuongeza ukomo wa urais ilianza kuibuliwa Septemba 12, mwaka jana na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), alipowasilisha kusudio lake la muswada binafsi wa mabadiliko ya Katiba unaohusu kuongeza ukomo wa Bunge. Nkamia aliwasilisha kusudio hilo kwa mujibu wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016, kupitia barua yake aliyoisaini Septemba 12, mwaka jana iliyokuwa ikipendekeza kuongeza muda wa Bunge kutoka miaka mitano hadi saba na kupunguza muda wa uongozi wa vijiji kutoka miaka mitano hadi minne. Hata hivyo, kupitia ujumbe mfupi aliouandika katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp, Nkamia, aliamua kuondoa kusudio hilo baada ya kile alichodai kuwa ni majadiliano na maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa CCM. Mbali na andiko hilo, mwaka jana MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Nkamia kupitia simu yake ya mkononi na kumuuliza kama ana sababu nyingine zaidi ya alizozitaja kupitia ujumbe huo mfupi na lini atakuwa tayari kuwasilisha tena muswada huo. Katika majibu yake, alisema: “Naomba ibaki hivyo hivyo kama ilivyo katika meseji sina cha kuongeza, kuhusu ni lini nitapeleka tena, nayo subiri kwa sababu nimesema nimesitisha kwa muda, maana yake nitawasilisha tena nitakapokuwa tayari.” Hoja ya Nkamia ilipingwa na wanasiasa wakongwe, akiwamo Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa na wasomi mbalimbali. Akizungumza na Kituo cha Televisheni cha Azam, Septemba, mwaka jana, Msekwa, alisema CCM haiwezi kukubaliana na maoni ya kuongeza muda wa kiongozi yeyote kutoka kipindi cha miaka mitano kilichopo kwa mujibu wa Katiba ya sasa. Pia alisema kwa uzoefu wake bungeni, anaona kuna tafakari nyingi zilizofanywa kabla ya taifa kuamua kipindi cha utawala kuwa miaka mitano na si vinginevyo. Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alipozungumza Septemba, mwaka jana na MTANZANIA Jumapili, alimpinga Nkamia, huku akisema lengo lake lilikuwa ni kujipendekeza kwa Magufuli ili ampe uwaziri. Mbali na Nkamia, mwingine aliyetoa hoja ya kuongeza muda wa ukomo wa nafasi ya rais, ni Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, aliyetaka Magufuli aongezewe miaka mingine 10 ya kuongoza ili atawale kwa miaka 20. Maji Marefu alitoa kauli hiyo Agosti, mwaka jana wakati Magufuli alipokuwa akizundua kituo kipya cha mabasi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mbali na hao, pia hoja hiyo iliibuka Desemba, mwaka jana kwenye mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambako wajumbe walitoa ushauri wa kuongeza ukomo wa urais na kuwa miaka saba na kujibiwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd, kuwa suala hilo linajadilika. Balozi Seif alidai kuwa suala hilo haliwezi kuathiri Katiba ya Tanzania. Wakati hao wakitoa hoja ya kuongeza muda wa ukomo wa urais, Septemba 18, mwaka jana, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), alisema anakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ili kupunguza muda wa viongozi kukaa madarakani kutoka miaka mitano na iwe minne kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na uamuzi zaidi wa kuendesha nchi yao. | kitaifa |
Na ASHA BANI SERIKALI imetangaza kushusha bei ya dawa na vifaa tiba hapa nchini, baada ya kuanza kufanya ununuzi wa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi bila kutumia mawakala. Punguzo hilo limehusisha mikataba na wazalishaji 73, kati yao 10 ni wazalishaji wa ndani na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inaagiza dawa, vifaa vya maabara na vitendanishi kutoka nchi 20 tu. Akitangaza mabadiliko hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema kushuka kwa dawa hizo ni agizo la Rais Dk. John Magufuli. “Hatua ya kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kama tulivyoeleza hapo awali imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kununua dawa kwa asilimia 15 hadi 80. “Mabadiliko haya ya bei, yaani unafuu huo wa bei kiuhalisia umeanza kuonekana tangu Julai Mosi, mwaka huu ambapo wazalishaji wanaleta dawa MSD. Kupungua kwa bei kutaviwezesha vituo vya afya na hospitali kununua dawa zaidi kwa bei nafuu,” alisema Ummy. Alizitaja baadhi ya nchi walizotoa vibali kwa wazalishaji 46 ni Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Falme za Kirabu, Bangladeshi, India, Tanzania na Kenya. Alisema aina 178 za dawa zinatoka kwa wazalishaji hao, huku vifaa tiba, jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba kutoka katika nchi ya Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania. Alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni chanjo ya homa ya ini iliyouzwa kwa Sh 22,000 kwa sasa itauzwa Sh 5,300, dawa ya sindano ya diclofenac kwa ajili ya maumivu vichupa 10 vya dozi, awali ilikuwa ni Sh 2,000, sasa itauzwa kwa Sh 800. Pia alisema shuka moja iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh 22,000, sasa itauzwa kwa Sh 11,000, mipira ya kuvaa mikononi inayokaa 50 kwa boksi itakuwa ikiuzwa Sh 18,200 kutoka Sh 19,200 na dawa ya kupambana na maambukizi ya bakteria yenye vidonge 15 itauzwa Sh 4,000 kutoka Sh 9,800. Pia amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha bei ya dawa zinashushwa kama watakavyoelekezwa na MSD. Alizitaka halmashauri, vituo, hospitali kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa na wizara hiyo iliyopo katika kitabu cha MSD. Alisema watakuwa wanabandika mabango kama wanavyofanya Ewura na ikitokea muuzaji hajatekeleza hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu, alisema watajitahidi kuhakikisha dawa zinapatikana kwa asilimia 100, huku akimwomba Ummy kuhakikisha halmashauri na hospitali zinawasilisha mahitaji yao kwa wakati. “Tunaomba ushirikiano wa wadau wote, tumejipanga kuhakikisha tunavuka malengo kusambaza dawa kutoka asilimia 81 ya sasa hadi 100,” alisema. Pia alisema MSD itahakikisha dawa zinapatikana kwa wakati, hivyo ni muhimu wananchi kutoa ushirikiano. | kitaifa |
FAMILIA ya Naomi Marijani, mwanamke anayedaiwa kuuawa na mumewe Khamis Luongo kisha kuchomwa moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, imesema bado haina imani kama ndugu yao huyo kuteketezwa kwa moto wa mkaa.Kauli yao hiyo imekuja baada ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kigamboni, Thobias Walelo kubainisha kuwa Naomi ameuawa na mumewe huyo ambaye baada ya tukio hilo alichimba shimo na kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia mkaa magunia mawili.Walelo alisema, Jeshi la Polisi lilimhoji Luongo aliyekiri kutekeleza mauaji hayo na kuwa aliuchomea mwili nyumbani kwake Gezaulole Kigamboni, hatua iliyowafanya wataalamu kutoka Jeshi la Polisi kufuatilia mabaki ya mwili wa marehemu Kigamboni ili kuchukua mabaki ya mwili kwa uchunguzi ili kubaini ukweli kama mabaki hayo ni mwili wa Naomi.Jana gazeti hili liliwasili nyumbani kwa dada wa marehemu, Salma Marijani aishiye, Mbweni- Ubungo, Dar es Salaam na kuzungumza na Msemaji wa familia Wiseman Marijani ambaye alibainisha kuwa hawana imani kama ndugu yao amechomwa moto kweli. Hata hivyo alisema kuwa familia itaendelea kusubiri majibu ya Polisi. Alisema mtuhumiwa huyo amedanganya wanafamilia kuwa ndugu yao amesafiri nje ya nchi baada ya kupata mwanaume mwingine huku akijua fika kuwa amemuua. | kitaifa |
FRANCIS Kimanzi amepata pigo la kwanza kama kocha wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, baada ya timu yake kufungwa na Msumbiji katika mchezo wa kimataifa wa kirafi ki juzi.Bao la kipindi cha pili lililofungwa na Canhembe Amancio lilitosha kuwawezesha wageni kupata ushindi wao wa kwanza katika majaribio manne katika mchezo huo dhidi ya Harambee Stars na kuwanyima Wakenya nafasi ya kutamba nyumbani.Kipigo hicho kimekuja siku moja baada ya mwanariadha wa Kenya wa marathon, Eliud Kipchoge kuweka historia katika mbio hizo Vienna, Australia Jumamosi. Kipchoge amekuwa binadamu wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili baada ya kutumia saa 1: 59:40 wakati wa mbio hizo zilizojulikana kama INEOS 1:59 nchini Australia.Kipchoge, ambaye alikuwa akisaidiwa na wanariadha 41, ameingia katika kitabu cha kumbukumbu cha Guinness kwa kukimbia marathon chini ya saa mbili. Jumapili, Wakenya walisheherekea mafanikio mengine baada ya Brigid Kosgei kuvunja rekodi ya dunia kwa wanawake kwa zaidi ya dakika moja katika Chicago marathon.Kosgei alitimua mbio kirahisi na kuweka rekodi hiyo ya dunia kwa kutumia saa 2:14: 04, akipunguza dakika moja na sekunde 21 kutoka ile ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na Muingereza Paula Radcliff aliyoiweka mwaka 2003.Kwingineko, Kenya imefuzu kwa mara ya pili mfululizo kucheza Michezo ya Olimpiki licha ya kufungwa katika fainali katika mashindano ya wanawake ya rugby ya Afrika yaliyofanyika huko Monastir. | michezo |
Na Mwandishi Wetu-Morogoro UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, hafahamu wala hajui dhana ya demokrasia ya vyama vingi, jambo linalomfanya kiongozi huyo kila siku kuilaumu Serikali. Kauli hiyo ya UVCCM, imekuja siku chache baada ya Sumaye kudai kwamba watawala wa Serikali wa sasa wanaiogopa Katiba Mpya na kugeuka kuwaandama wapinzani kwenye mfumo wa vyama vingi. Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza na vijana wa CCM Mvomero wakati akielekea mkoani Dodoma ambapo alisema hatua hiyo ya Sumaye ya kudai kuna mfumo mgumu wa demokrasia haileti mantiki kwa sasa. Alisema msingi wa kuruhusiwa vyama vingi nchini si kukwamisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii au kuwafanya wananchi kila siku wakusanyike viwanjani kusikiliza mikutano ya hadhara bila kutilia maanani uzalishaji mali viwandani, mashambani na maofisini. “Vijana wenzangu hata ligi ya soka au mashindano ya kutafuta warembo yana msimu na vipindi vyake, timu haziwezi kushiriki michuamo mwaka mzima bila wachezaji na waamuzi kupumzika, domokrasia ya wapi ambayo haina vipindi vya kampeni. “…uchaguzi au watu kutakiwa kufanya kazi za maendeleo acheni kusikiliza poroja za wanasiasa waliochoka vijana chapeni kazi sasa ili kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Shaka . Alisema UVCCM imeshangazwa na matamshi ya Sumaye anayedai kuwa serikali ya awamu ya tano inakandamiza misingi ya demokrasia kwasababu tu imevitaka vyama kuendesha shughuli za kisiasa kwenye mikutano ya ndani ili kuwapa nafasi wananchi kujituma na kuzalisha. Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema hata kanuni na fomula za masomo ya hesabu, kemia na baiolojia hazilingani katika kupata majawabu halisia hivyo akataka ifahamike demokrasia nayo ina vipindi vya kampeni , mikutano ya hadhara, uandikishaji, upiga kura, kuhesabu na kutangazwa matokeo . “UVCCM tunamfahamu Sumaye toka akiwa Naibu Waziri wa Kilimo hadi Waziri Mkuu, hana rekodi nzuri ya kiutendaji ilioleta tija, mafanikio au ufanisi katika maeneo aliyoyaongoza, yaonyesha ni mshabiki wa hadithi kuliko kufanya kazi,” alisema. Kutokana na hali hiyo alimtaka mwanasiasa huyo kufuta ndoto na fikra siku moja itatokea CCM kudondoka madarakani kisha yeye au mshirika wake Edward Lowassa mmoja kati yao awe urais wa Tanzania. “Tanzania imechoka kuwa ombaomba wa kila msaada toka kwa wahisani na washirika wa maendeleo, Serikali ya CCM imezinduma usingizini na kujitambua, haitaruhusu upuuzi usio na manufaa ili ionekane demokrasaa maana yake ni mikutano ya hadhara bila uzalishaji mali,” alisema | kitaifa |
WANAFUNZI wanaopata mimba katika shule za msingi na sekondari Singida imepungua kwa asilimia 66.66 kutoka mimba 54 mwaka jana hadi mimba 18, Novemba 30 mwaka huu.Ofisa Elimu Sekretarieti ya Mkoa wa Singida (REO), Nelasi Mulungu alieleza kuwa kati ya idadi hiyo, wasichana wa shule za sekondari ni 15, watatu waliobaki ni kutoka shule za msingi.Akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Singida (RCC) mjini hapa juzi, Mulungu alisema wanafunzi waliopata mimba wamepungua kufuatia ushirikiano mzuri baina ya wazazi, jamii, walimu na wanafunzi.“Natoa mwito kwa jamii kuendelea kushirikiana na serikali ili kutokomeza tatizo hilo. Naomba wasichana wanaosoma kujitambua na kujiona wana thamani kubwa kuchangia maarifa kwa maendeleo ya familia zao na taifa,” alisema.Alitaka kila halmashauri ya wilaya kujenga hosteli za wasichana za kutosha ili kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa, maabara na nyumba za walimu ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu bora.Kuhusu upungufu wa walimu, Mulungu alisema mahitaji bado makubwa na serikali itakabili changamoto kadri fedha zinavyopatikana ili kuhakikisha elimu nchini inakuwa bora zaidi. | kitaifa |
NEEMA imeanza kuwaangukia wakulima wa mahindi mkoani Ruvuma, baada ya serikali kuamua kupandisha bei ya kununulia mahindi kutoka Sh 470 hadi 600 kwa kilo. Hatua hiyo imelenga kuwapatia soko la uhakika na kuwakomboa na umaskini. Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea, Ramadhan Nondo alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake mjini Songea. Nondo alisema serikali imeipa Kanda ya Songea mgao wa kununua tani 25,000 za mahindi na imepeleka Sh bilioni moja kwa awamu ya kwanza. Hadi kufikia mwishoni mwa wiki, imeshanunua tani 900.45 huku kazi ya ununuzi ikiendelea.Alisema, msimu ulipofunguliwa walianza kununua mahindi kwa bei ya Sh 470. Lakini, kadri siku zilivyokwenda na kuwepo kwa ushindani kutoka kwa wafanyabiashara wengine, bei ilizidi kushuka na serikali kulazimika kuongeza bei kama hatua ya kuwavu tia wakulima. Hata hivyo, alieleza kuwa licha ya kupandisha bei, bado mwitikio ulikuwa mdogo. Ndipo, serikali kupitia NFRA tangu Septemba Mosi mwaka huu, iliongeza bei ya Sh 520 maeneo ya vijijini na Sh 600 kwenye kituo kikuu kilichopo Ruhuwiko Songea mjini, kama njia itakayoshawishi wakulima kupeleka mahindi kwa NFRA.Kwa mujibu wa Nondo, upatikanaji wa mahindi mwaka huu umekuwa wa kusuasua. Hali hiyo inatokana na mahitaji kuwa makubwa, ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wanunuzi walikuwa wachache.Hali hiyo imesababisha mahindi kugombewa, hasa baada ya kuja kwa wafanyabiashara kutoka nchi jirani za Zimbabwe na Malawi.Nondo alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, wanatarajia kukutana na vikundi vya wakulima na kuwashawishi kuuza mahindi yao kwa NFRA.Aliwahimiza kuchangamkia fursa ya bei kubwa, inayotolewa na serikali. Aidha, Nondo alisema serikali imetoa mafunzo kwa wakulima wa mahindi wa wilaya zote zinazolima zao hilo mkoa Ruvumani kuhusu umuhimu wa kilimo cha kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima wa mahindi waliipongeza serikali kuongeza bei ya mahindi. Walisema hatua hiyo itasaidia kuboresha maisha yao na kumaliza tatizo la umaskini.Ali Mapunda na Ambrose Ngonyani walisema ni faraja kuona serikali imeanza kutambua mchango na juhudi kubwa zinazofanywa na wakulima, kwani kwa muda mrefu bei ya mahindi haijawahi kufikia Sh 600. | kitaifa |